Smiley face

Jumatatu, 13 Novemba 2017

Sura ya 13. Maana ya Utendaji wa Watu Kuamua Matokeo Yao



1. Hakuna Ambaye Angeokolewa iwapo Mungu Angeangalia Tu Maonyesho ya Asili ya Watu
Mwenyezi Mungu alisema: Kwa sasa, utendaji wa watu unaamua matokeo yao, lakini huu utendaji ni upi? Je, unaujua? Nyinyi mnaweza kufikiri kwamba hili linarejelea tabia ya watu iliyopotoka ikijionyesha kazini mwao, lakini halimaanishi lile. Utendaji huu unanena kuhusu ikiwa unaweza kuweka ukweli kwenye vitendo au la na ikiwa unaweza kusalia mwaminifu na kujizatiti unapotenda wajibu wako au la, na vilevile mtazamo wako wa kumwamini Mungu, msimamo wako kwa Mungu, uamuzi wako wa kuteseka kwa ajili ya ugumu, mtazamo wako kwa kukubali hukumu na kupogolewa, kiwango chako cha mabadiliko na idadi ya dhambi kubwa. 

Sura ya 12. Mapenzi ya Mungu ni Kuwaokoa Watu kwa Kiwango Kikubwa Sana Kinachowezekana



1. Usijishughulishe na Ikiwa Umejaaliwa na Mungu, bali Ujishughulishe na Ufuatiliaji Wako
Mwenyezi Mungu alisema: Watu wengi hawaelewi mapenzi ya Mungu; wanafikiri kuwa kila mtu ambaye ameamuliwa na Mungu ataokolewa bila kuepuka na wanafikiri kuwa kila mtu asiyeamuliwa na Mungu hataokolewa hata wakiyafanya mambo vyema zaidi. Wanafikiri kwamba Mungu hataamua matokeo ya watu kulingana na utendaji na tabia yao. Iwapo unafikiri hivi, basi unamwelewa Mungu visivyo kabisa. 

Jumapili, 12 Novemba 2017

Sura ya 11. Kutatua Asili na Kutenda Ukweli


1. Uhusiano Kati ya Ubinadamu na Uwezo wa Kutenda Ukweli
Mwenyezi Mungu alisema: Watu husema kuwa kutenda ukweli ni vigumu kabisa. Basi mbona watu wengine wanaweza kutenda ukweli? Watu wengine husema ni kwa sababu kwa asili wanaipokea kazi ya Roho Mtakatifu ikifanya kazi juu yao, na pia kwa sababu ni wazuri kiasili. Hoja hii ina kiwango fulani cha mantiki. Watu wengine ni wazuri kiasili; wana uwezo wa kutenda ukweli. 

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I(Sehemu ya Kwanza )



Mwenyezi Mungu alisema: Leo tunawasiliana kuhusu mada muhimu. Hii ni mada ambayo imezungumziwa tangu kuanza kwa kazi ya Mungu mpaka sasa, na inayo umuhimu mkuu kwa kila mtu. Kwa maneno mengine, hili ni suala ambalo kila mmoja atakutana nalo kwenye mchakato wote wa kusadiki kwake katika Mungu na suala ambalo lazima lizungumziwe. Ni suala muhimu, lisiloepukika ambalo mwanadamu hawezi kujitenganisha nalo. 

Jumamosi, 11 Novemba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Moja

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Kanisa la Mwenyezi Mungu  Tamko la Ishirini na Moja

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Moja


Mwenyezi Mungu alisema: Mwanadamu huanguka katikati ya mwanga Wangu, na anasimama imara kwa sababu ya wokovu Wangu. Niletapo wokovu ulimwenguni kote, mwanadamu hujaribu kutafuta njia za kuingia miongoni mwa mtiririko wa marejesho Yangu, ilhali kuna watu wengi ambao huoshwa wasijulukane waliko na gharika hii ya urejesho; kuna watu wengi ambao wamezama na kumezwa na mafuriko haya na kuna watu wengi pia ambao husimama imara huku kukiwa na mafuriko, ambao hawajawahi kupoteza hisia zao za mwelekeo, na ambao wamefuata mafuriko mpaka sasa. 

Sura ya 10. Wale Wanaopenda Ukweli Wana Njia ya Kufuata



1. Kama hali ya Watu Ni Ya Kawaida Inategemea na Kama Wanapenda Ukweli au La
Mwenyezi Mungu alisema: Watu wengi wameibua suala lifuatalo: Baada ya ushirika wa juu, wanahisi wazi kabisa, wanakuwa na nguvu zaidi, na hawana hisia hasi—lakini hali kama hiyo inabaki tu kwa karibu siku kumi, ambapo baadaye hawawezi kudumisha hali ya kawaida. Suala ni nini? Je mmewahi kujiuliza kinachosababisha hili? Mbona hali zenu ni nzuri sana katika siku hizo takriban kumi za kwanza? Wengine wanasema kuwa hili ni tokeo la kutolenga ukweli. 

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Tamko la Kumi Na Sita

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Kanisa la Mwenyezi Mungu|Tamko La Kumi Na Sita

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Tamko La Kumi Na Sita

Mwenyezi Mungu alisema: Kuna mengi Mimi natamani kumwambia mwanadamu, mambo mengi sana ambayo lazima Nimwambie. Lakini uwezo wa mwanadamu wa kukubali una upungufu mwingi: Hana uwezo wa kuyaelewa kabisa maneno Yangu kulingana na kile Ninachokitoa, na anaelewa kipengele kimoja tu lakini haelewi vingine. Lakini Simmalizi mwanadamu kwa ajili ya ukosefu wa nguvu wake, wala Siudhiki na udhaifu wake. 

Ijumaa, 10 Novemba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Kanisa la Mwenyezi Mungu  Tamko la Ishirini

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini


Mwenyezi Mungu alisema: Utajiri wa jumba Langu ni bila idadi na usioeleweka, lakini mwanadamu hajawahi kuja Kwangu kuufurahia. Hana uwezo wa kuufurahia mwenyewe, wala wa kujilinda mwenyewe kwa kutumia juhudi zake mwenyewe; badala yake, yeye daima huweka imani yake kwa wengine. Kati ya wale wote Ninaowatazamia, hakuna mtu aliyewahi kunitafuta kwa makusudi na moja kwa moja. Wao wote huja mbele Zangu kwa kushawishiwa na wengine, wakiwafuata watu wengi, na hawana nia ya kulipa gharama au kutumia muda kustawisha maisha yao.