Smiley face
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ushuhuda-wa-Kuipitia-Hukumu-ya-Kristo. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ushuhuda-wa-Kuipitia-Hukumu-ya-Kristo. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 26 Januari 2019

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Kutumia Neno la Mungu Kama Kioo

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Kutumia Neno la Mungu Kama Kioo


Wu Xia    Mji wa Linyi , Mkoa wa Shandong

Baada ya kuikubali kazi hii na kula na kunywa neno la Mungu, ilikuwa dhahiri kwangu kwamba ni muhimu sana kwamba mimi nijifahamu. Kwa hiyo, nilipokuwa nikila na kunywa neno la Mungu, nilihakikisha nimejithibitisha tena dhidi ya neno ambalo Mungu humfichua mwanadamu. Katika hali nyingi, niliweza kutambua kasoro zangu na upungufu. Nilihisi kwamba ningekuja kujifahamu kweli. Hata hivyo, ilikuwa ni kwa njia ya ufunuo kutoka kwa Mungu tu nilipoweza kuona kwamba kwa hakika sikujifahamu kulingana na neno la Mungu.

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Mapambano ya Kufa na Kupona

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Mapambano ya Kufa na Kupona


Chang Moyang Mjini Zhengzhou, Mkoani Henan

"Unapoutelekeza mwili, bila shaka kutakuwa na mapambano ndani. Shetani anataka ufuate dhana za mwili, kulinda maslahi ya mwili. Hata hivyo, neno la Mungu bado linakupa nuru na kukuangaza ndani, linakupa msukumo kwa ndani na kufanya kazi kutoka ndani. Katika hatua hii, ni juu yako kama unamfuata Mungu, au Shetani. Kila wakati ambapo ukweli unatendwa na kila wakati ambapo watu wanapofanya mazoezi ya kumpenda Mungu, kuna pambano kubwa.

Alhamisi, 24 Januari 2019

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Si Rahisi Kwako kwa Hakika Kujijua Mwenyewe

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Si Rahisi Kwako kwa Hakika Kujijua Mwenyewe


Zhang Rui     Mji wa Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang

Nilikuwa mtu mdanganyifu. Katika neno la Mungu tunaweza kuona kwamba watu wadanganyifu hawataokolewa na Mungu; ni watu wanyofu tu watakaopata sifa Zake. Kwa hiyo, nilitaka kuwa mtu mnyofu, kwa utambuzi kufanya mazoezi ya kuzungumza kwa usahihi, kuwa bila upendeleo na wa busara, na kutafuta ukweli kutoka kwa mambo ya hakika wakati wa kutoa taarifa juu ya masuala. Katika kazi yangu, kama iwe ni kosa au upungufu, mimi nililielezea kwa undani kwa kiongozi. Pia kwa utambuzi niliuchangua na kuufichua upotovu wangu mwenyewe. Kila wakati nilipoweka hili katika matendo, nilihisi kuwa nilikuwa nimepitia mabadiliko fulani na nilipata ladha kidogo ya kuwa mtu mnyofu.

Jumapili, 20 Januari 2019

Ushuhuda wa Wakristo|Katikati ya Maafa Niliiona Tabia ya Haki ya Mungu

Ushuhuda wa Wakristo|Katikati ya Maafa Niliiona Tabia ya Haki ya Mungu


Li Jing, Beijing

7 Agosti, mwaka wa 2012

Siku hiyo, ilianza kunyesha asubuhi. Nilikwenda kwa mkutano nyumbani mwa ndugu mmoja, wakati mvua ilipoendelea kuongezeka zaidi na zaidi kwa uzito. Kufikia alasiri ilikuwa ikinyesha kana kwamba ilitoka mbinguni moja kwa moja. Wakati tulipomaliza mkutano wetu, mvua ilikuwa imeingia katika ua wa ndugu yangu, lakini kwa sababu nilikuwa na wasiwasi juu ya familia yangu, nilijitahidi kwenda nyumbani. Nusu ya barabara huko, baadhi ya watu waliokimbia hatari waliniambia, "Je, si wewe unatoroka, bado unakwenda nyumbani?" Nilipofika nyumbani, mtoto wangu aliniuliza, "Je, mafuriko hayakukuzoa?" Ni hapo tu nilipojua kwamba sikuwa na Mungu moyoni mwangu.

Jumamosi, 19 Januari 2019

Ushuhuda wa Wakristo|Moto Ulioshtua Taifa katika Wilaya ya Ji, Mji wa Tianjin

Ushuhuda wa Wakristo|Moto Ulioshtua Taifa katika Wilaya ya Ji, Mji wa Tianjin


Chen Yao, Tianjin

Jengo la Laide lilikuwa mojawapo ya vituo vikubwa zaidi vya ununuzi katika wilaya ya Ji. Juni 30, mwaka wa 2012 ilikuwa ni Jumamosi, na Laide lilikuwa na ukuzaji wa bidhaa, hivyo kulikuwa na idadi kubwa ya wateja. Wakati fulani baada ya saa tisa alasiri hiyo, jengo likashika moto ghafla. Mkuu wa jengo, akiogopa kuwa wateja katika machafuko haya wangechukua vitu au kutolipa, alifunga na kuweka vizuizi kwa lango kuu kwenye ghorofa ya kwanza, na kuwafukuza wateja hadi ghorofa ya pili na ya tatu. Kitu ambacho hakikutarajiwa ni kwamba moto ulikuwa mkali zaidi na zaidi, hatimaye ukifika kiwango cha kutodhibitika kabisa.

Jumatatu, 24 Desemba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tabia ya Mungu ni Haki na, Hata Zaidi, Upendo

Tabia ya Mungu ni Haki na, Hata Zaidi, Upendo

Fang Xin, Beijing
Agosti 15, mwaka wa 2012
 Tangu mwaka wa 2007, nilipoikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, ingawa nimeonekana juu juu kuwa na kazi nyingi sana kutekeleza majukumu yangu, sijaupa moyo wangu kwa Mungu, na mara nyingi nimehisi kufungwa kiasi cha msongo wa pumzi na masuala madogo ya familia.

Jumapili, 23 Desemba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Bila Ya Wokovu wa Mungu, Singeweza Kuwa Hapa Leo

Bila Ya Wokovu wa Mungu, Singeweza Kuwa Hapa Leo

Zhang Jin, Beijing
Agosti 16, 2012

Mimi ni dada mzee mwenye miguu miwili yenye kasoro. Hata wakati hali ya hewa ni nzuri nje, nina shida kutembea, lakini wakati maji ya mafuriko yalipokuwa karibu kunimeza, Mungu aliniruhusu kutoroka hatari kimiujiza.

Alhamisi, 20 Desemba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kupenya Ukungu ili Kuona Mwanga

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kupenya Ukungu ili Kuona Mwanga


Faith China

Mimi ni mfanyakazi wa kawaida. Mwishoni mwa Novemba, 2013, mfanyakazi mwenza aliona kwamba mke wangu na mimi tungefanya kelele nyingi sana juu ya vitu vidogo, kwamba kila siku tulikuwa na wasiwasi na huzuni, hivyo alipitisha kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku mwisho kwetu. Kutoka kwa neno la Mwenyezi Mungu, tumejifunza kwamba mbingu na dunia na vitu vyote viliumbwa na Mungu, na kwamba uhai wa mtu amekirimiwa na Mungu. Tumeelewa pia ukweli wa fumbo la mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita, fumbo la kupata mwili, hatua tatu za Mungu za kazi katika kuwaokoa wanadamu, umuhimu wa kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho, na tondoti zingine.

Jumatatu, 17 Desemba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Baraka Kwa Sababu ya Ugonjwa —Insha Juu ya Upendo wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Baraka Kwa Sababu ya Ugonjwa —Insha Juu ya Upendo wa Mungu 


Dujuan Japani

Nilizaliwa katika familia fukara katika kijiji cha mashambani. Tangu niwe mtoto, niliishi maisha magumu na nilidharauliwa na wengine. Wakati mwingine sikujua hata kama ningepata chakula changu cha kufuatia, sembuse kumbwe na vitu vya watoto kuchezea. Kwa kuwa familia yangu ilikuwa fukara, nilipokuwa mdogo, ningevaa nguo zilizokuwa zikivaliwa na dadangu mkubwa awali. Nguo zake mara nyingi zilikuwa kubwa sana kwangu. Kama matokeo, nilipoenda shuleni, watoto wengine wangenicheka na hawangecheza na mimi. Utoto wangu ulikuwa mchungu sana. Kuanzia wakati huo kuendelea, ningejiambia kwa siri: Mara nitakapokuwa mtu mzima, nitakuwa mtu wa sifa na kupata pesa nyingi.

Jumapili, 16 Desemba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kutembea Katika Njia Ng’avu ya Maisha

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Njia Ng’avu ya Maisha

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kutembea Katika Njia Ng’avu ya Maisha


Xie Li, Marekani

Zamani nilikuwa mtu ambaye angefuata mitindo ya dunia, nilitaka kujiachilia kwa maisha ya anasa, na nilijali tu kuhusu anasa za mwili. Mara nyingi ningeenda na rafiki zangu kwa KTV usiku mzima, ningeenda matembezi kwa motokaa katikati ya usiku, ningeenda kuvua samaki katika bahari, na kusafiri pande zote nikitafuta vyakula vizuri. Ningeona wengine walionizunguka, na wao wote pia walikuwa wanajizatiti kula vizuri, kuvaa vitu vizuri, na kufurahia vitu vizuri.

Jumatatu, 19 Novemba 2018

Umeme wa Mashariki | Huku Ni Kuweka Ukweli Katika Vitendo

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ukweli

Fan Xing    Mji wa Zhumadian, Mkoa wa Henan

    Katika siku za nyuma, nilikuwa nimeunganishwa na dada mmoja kufanya kazi kwa wajibu fulani. Kwa sababu nilikuwa na majisifu na mwenye kiburi na sikutafuta ukweli, nilikuwa na mawazo kiasi ya kabla kuhusu dada huyu ambayo niliweka moyoni mwangu daima na sikuzungumza waziwazi naye. Tulipotengana, sikuwa nimeingia katika ukweli wa uhusiano wa kufanya kazi wenye kuridhisha.

Ijumaa, 16 Novemba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Siri Niliyoishikilia kwa Kina Ndani ya Moyo Wangu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kristo

Wuzhi    Mji wa Linyi, Mkoa wa Shandong

Katika majira ya kuchipua ya mwaka wa 2006, nilinyang’anywa cheo changu kama kiongozi na nikarudishwa nilikotoka kwa sababu nilifikiriwa kuwa “bwana ndiyo” sana. Niliporejea mara ya kwanza, nilitumbukia ndani ya kikalibu cha mateso na maumivu makubwa.

Jumanne, 13 Novemba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kuna Furaha Kubwa Katika Uaminifu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Gan’en    Mji wa Hefei, Mkoa wa Anhui

Katika maisha yangu, siku zote nimeongozwa na msemo, “Mtu hapaswi kuwa na moyo wa kuwadhuru wengine, lakini lazima awe macho ili asidhuriwe” katika uingiliano wa kijamii. Kamwe huwa siwaridhii wengine imani yangu kwa urahisi.

Alhamisi, 8 Novemba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mwenyezi Mungu Amenipa Fursa ya Pili Katika Maisha

 Ndugu wawili wa kawaida, Beijing

Agosti 15, 2012

Julai 21, mwaka wa 2012 ilikuwa siku isiyosahaulika sana kwangu, pamoja na kuwa siku muhimu zaidi ya maisha yangu.
Siku hiyo, mvua kubwa ilikuwa ikinyesha katika Wilaya ya Fangshan jijini Beijing—ilikuwa kubwa kuliko yoyote iliyowahi kuonekana pale katika miaka sitini na mmoja.

Ijumaa, 12 Oktoba 2018

Umeme wa Mashariki | Kutupa mbali Jozi La Shetani Kunakomboa

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Masharik, ukweli

Momo     Mji wa Hefei, Mkoa wa Anhui

    Kabla ya kumwamini Mungu, bila kujali chochote nilichokuwa nikifanya, sikuwahi kutaka kubaki nyuma. Nilikuwa tayari kukubali shida yoyote ili mradi ingemaanisha ningeinuka juu ya kila mtu mwingine zaidi. Baada ya kumkubali Mungu, mtazamo wangu uliendelea kuwa sawa, kwa sababu niliamini kikamilifu msemo, “Hakuna maumivu, hakuna faida,” na kuona mtazamo wangu kama ushahidi wa msukumo wangu.

Ijumaa, 28 Septemba 2018

Umeme wa Mashariki | Kwaheri kwa Zile Siku za Kushindana na Majaliwa


Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mungu




Yixin


Kijiji cha kishamba kilichojikokota kimaendeleo, wazazi wangu waliochoka kwa sababu ya kazi zao, maisha ya shida za kifedha … kumbukumbu hizi za huzuni zilitia alama kwa mawazo yangu machanga, zilikuwa ni hisia yangu ya kwanza ya “majaliwa.” Baada ya kuanza kwenda shule, mara ya kwanza nilipomsikia mwalimu wangu akisema kwamba “Unadhibiti majaliwa yako katika mikono yako mwenyewe,” niliweka maneno haya imara mawazoni mwangu.

Alhamisi, 27 Septemba 2018

Umeme wa Mashariki | Mama wa "Vijijini" Akutana na Binti Mkwe wa "Mjini"


Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mungu

Liu Jie, Hunan
Maoni Tofauti, Migongano Ya Siku Zote

Mimi ni mke wa kawaida, mke mzuri na mama mwenye upendo, mimi huwatunza vizuri mume wangu na watoto wangu, mimi hufanya kazi kwa bidii na mwekevu katika kuendesha nyumba yangu, na sijawahi kamwe kutumia fedha zangu bila hadhari. Lakini kitu kisichofikirika kilinifika.

Jumatano, 26 Septemba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mabadiliko ya Mtu Aliyeanguka


Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Yesu

Tong Xin    Mkoa wa Fujian

Nilizaliwa vijijini. Nilitoka kwa nasaba ya wakulima wanyenyekevu na zaidi ya hayo familia yetu ilikuwa na watu wachache, kwa hiyo mara nyingi tulikuwa tunadhulumiwa. Nilipokuwa na umri wa miaka 13, kulikuwa na mtoto aliyepigwa na mtu fulani kutoka nje ya kijiji chetu.

Jumatatu, 10 Septemba 2018

Umeme wa Mashariki | Maneno ya Mungu Huniongoza Kujifunza Jinsi ya Kuwafundisha Wanangu (I)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mungu, Umeme wa Mashariki

Maneno ya Mungu Huniongoza Kujifunza Jinsi ya Kuwafundisha Wanangu (I)

Xiaoxue, Malesia

Nina wana wawili wa kiume na wameachana na mwaka mmoja. Ili kuwalea kuwa watu waliostaarabika, wenye tabia nzuri, watu wema ambao wataweza watajijengea jina katika jamii na kufanikiwa, walipokuwa na umri wa miaka miwili, nilijadiliana na mume wangu juu ya kuwatafutia shule nzuri ya chekechea. Baada ya ziara kadhaa, maulizo na kulinganisha, tulichagua shule ya chekechea ya Kiingereza kwa sababu waliweka umuhimu juu ya ubora wa tabia au akili na uwezo wa watoto, ambao ulifanana na mtazamo wangu juu ya kufundisha watoto. Ingawa ada za masomo zilikuwa za juu kiasi, alimradi watoto waliweza kuendeleza vizuri na kupata elimu bora, lilikuwa la thamani kutumia pesa zaidi kidogo.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Maneno ya Mungu Huniongoza Kujifunza Jinsi ya Kufundisha Watoto Wangu (II)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kristo

Maneno ya Mungu Huniongoza Kujifunza Jinsi ya Kufundisha Watoto Wangu (II)

Xiaoxue, Malesia

Siku moja baada ya mlo mkuu wa siku, nilimfundisha mwanangu mvulana mkubwa jinsi ya kusoma Kichina—maneno rahisi tu, “Mbinguni, dunia, watu, na, dunia, baba, mama….” Nilimfundisha mara chache hasa, lakini bado hakuweza kuandika. Angeandika neno la kwanza na kisha kusahau lililofuata. Hasira ndani yangu ilipanda, na kunyakua rula iliyokuwa juu ya meza na kumgonga mara kadhaa. Nilimpigia kelele kwa sauti kubwa: “Wewe ni mpumbavu jinsi gani! Huwezi hata kujifunza maneno haya machache!” Mwanangu mkubwa alipigwa mpaka akalia, “waa, waa” na kutoroka na kukimbia kusimama pembeni.