Smiley face
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mwendelezo-wa-Neno-Laonekana-katika-Mwili. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mwendelezo-wa-Neno-Laonekana-katika-Mwili. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 13 Januari 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)(Sehemu ya Nne)


Mahitaji ya Mungu kwa Wanadamu


1. Utambulisho na Hadhi ya Mungu Mwenyewe
Mwenyezi Mungu alisema, Tumefikia mwisho wa mada ya "Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote," vilevile na ile ya "Mungu ni wa kipekee Mungu Mwenyewe." Baada ya kufanya hivyo, tunahitaji kufanya muhtasari. Muhtasari wa aina gani? Unaomhusu Mungu Mwenyewe. Kwa kuwa ni kumhusu Mungu Mwenyewe, basi lazima ugusie kila kipengele cha Mungu, vilevile aina ya imani ya watu kwa Mungu. Na kwa hiyo, kwanza lazima Niwaulize: Baada ya kusikia mahubiri, Mungu ni nani katika jicho la mawazo yako? (Muumbaji). Mungu katika jicho la mawazo yako ndiye Muumbaji.

Ijumaa, 12 Januari 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)(Sehemu ya Tatu)

1. Jinsi Mungu Anatawala na Kuongoza Ulimwengu wa Kiroho


3) Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Wanaomfuata Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Baada ya hayo, hebu tuzungumzie mzunguko wa uhai na mauti wa wale wanaomfuata Mungu. Hili linawahusu, hivyo kuweni makini. Kwanza, fikiria kuhusu ni makundi gani ambamo watu wanaomwamini Mungu wanaweza kugawika. Kuna mawili: wateule wa Mungu na watendaji-huduma.

Alhamisi, 11 Januari 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)(Sehemu ya Pili)

1. Jinsi Mungu Anatawala na Kuongoza Ulimwengu wa Kiroho

1) Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Wasioamini
Mwenyezi Mungu alisema, Hebu tuanze na mzunguko wa uhai na mauti wa wasioamini. Baada ya watu kufa, wanachukuliwa na msimamizi kutoka ulimwengu wa kiroho. Na ni kitu gani chao kinachukuliwa? Sio miili yao, bali ni roho zao. Roho zao zikichukuliwa, wanawasili katika sehemu ambayo ni ofisi ya ulimwengu wa kiroho, sehemu ambayo hasa hupokea roho za watu ambao wamekufa. (Kumbuka: sehemu ya kwanza wanapokwenda baada ya mtu yeyote kufa ni pageni kwa roho.)

Jumatano, 10 Januari 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)(Sehemu ya Kwanza)


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)


Mwenyezi Mungu alisema, Leo, tunafanya ushirika juu ya mada maalum. Kwa kila mmoja wenu, kuna vitu viwili vikuu tu ambavyo mnapaswa kujua, kuvipitia na kuvielewa—na vitu hivi viwili ni vipi? Cha kwanza ni kuingia binafsi kwa watu katika maisha, na cha pili kinahusu kumjua Mungu. Leo Nawapa uchaguzi: Chagua kimoja. Mngependa kusikia kuhusu mada inayouhusu uzoefu wa maisha ya kibinafsi ya watu, au mngependa kusikia inayohusu kumjua Mungu Mwenyewe?

Jumanne, 9 Januari 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)(Sehemu ya Tatu)


2. Mungu anaweka Uwiano Kati ya Vitu Vyote ili Kumpatia Binadamu Mazingira Imara kwa ajili ya Kuendelea Kuishi


Tumemaliza kusema juu ya jinsi ambavyo Mungu anatawala sheria za vitu vyote vilevile jinsi ambavyo Anawakimu na kuwalea binadamu wote kupitia sheria Zake kwa ajili ya viumbe vyote ndani ya sheria hizo. Hiki ni kipengele kimoja. Kinachofuata, tutazungumza juu ya kipengele kingine, ambacho ni njia moja ambayo Mungu ana udhibiti wa kila kitu. Hivi ndivyo, baada ya kuumba vitu vyote, Akaweka uwiano wa uhusiano kati yao. Hii pia ni mada kubwa sana kwenu.

Jumatatu, 8 Januari 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)(Sehemu ya Pili)



Ikiwa viumbe vyote vingepoteza sheria zao, visingeishi tena; ikiwa sheria za viumbe vyote zingekuwa zimepotea, basi viumbe hai miongoni mwa viumbe vyote visingeweza kuendelea. Binadamu pia wangepoteza mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo wanayategemea kwa ajili ya kuendelea kuishi. Ikiwa binadamu wamepoteza hiyo yote, wasingewea kuendelea kuishi na kuongezeka kizazi baada ya kizazi. Sababu ya binadamu kuendelea kuishi mpaka sasa ni kwa sababu Mungu amewapatia binadamu viumbe vyote kuwalea, kuwalea binadamu kwa namna tofauti.

Jumapili, 7 Januari 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)(Sehemu ya Kwanza)


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)


Kwa kipindi hiki chote, tumezungumza juu ya mambo mengi yanayohusiana na kumjua Mungu na hivi karibuni tulizungumza kuhusu kitu fulani muhimu sana juu ya mada hii: Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote. Wakati uliopita tulizungumza juu ya vipengele vichache vya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyatengeneza kwa ajili ya binadamu, vilevile Mungu kuandaa kila aina ya riziki ya lazima kwa ajili ya watu katika maisha yao.

Jumamosi, 6 Januari 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)(Sehemu ya Nne)

2. Chakula cha Kila Siku na Kinywaji Ambavyo Mungu Anawatayarishia Wanadamu

Mwenyezi Mungu alisema, Niambie; Kuna chochote ambacho Mungu hufanya, bila kujali iwapo kitu hicho ni kikubwa au kidogo, kisicho na thamani au maana? Kila kitu Afanyacho kina thamani na maana. Tujadili hili kutoka kwa swali ambalo watu mara nyingi hulizungumzia: Ni kipi kilitangulia, kuku au yai? Je, utajibuje hili? Kuku alitangulia, hilo ni hakika! Kwa nini kuku alitangulia? Kwa nini yai halingetangulia? Je, kuku haanguliwi kutoka kwa yai? Mayai huangua kuku, kuku huatamiza mayai.

Ijumaa, 5 Januari 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)(Sehemu ya Tatu)


2. Chakula cha Kila Siku na Kinywaji Ambavyo Mungu Anawatayarishia Wanadamu

Tulikuwa tumezungumza sasa hivi kuhusu sehemu ya mazingira ya jumla, yaani, hali zilizo muhimu kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu ambazo Mungu aliwatayarishia wanadamu tangu Alipoumba ulimwengu. Tumezungumza sasa hivi kuhusu vitu vitano, na vitu hivi vitano ndivyo mazingira ya jumla. Tunachoenda kuzungumzia baada ya hapo kinahusiana kwa karibu na kila maisha ya wanadamu katika mwili. Ni hali muhimu inayolingana zaidi na inayokubaliana zaidi na maisha ya mtu katika mwili. Kitu hiki ni chakula.

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)(Sehemu ya Pili)


(3) Sauti
Mwenyezi Mungu alisema, Kitu cha tatu ni sauti. Hiki pia ni kitu ambacho mazingira ya kuishi ya kawaida ya wanadamu yanatakiwa kuwa nacho. Sauti iliumbika Mungu alipoumba vitu vote. Mungu aliishughulikia vizuri sana wakati huo. Hiki ni kitu muhimu sana kwa Mungu na pia kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu. Kama Mungu hangeshughulikia suala la sauti vizuri, ingekuwa kizuizi kikubwa kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu. Hiyo ni kusema kwamba ingekuwa na athari yenye maana sana kwa mwili na maisha ya mwanadamu, kiasi kwamba wanadamu hawangeweza kuendelea kuishi katika mazingira kama hayo.

Alhamisi, 4 Januari 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)(Sehemu ya Kwanza)


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)


Mwenyezi Mungu alisema, Tuendelee na mada ya mawasiliano ya wakati uliopita. Je, mnaweza kukumbuka ni mada gani tuliwasiliana wakati uliopita? (Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.) Je, “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote” ni mada mnayohisi ikiwa mbali sana nanyi? Mtu fulani anaweza kuniambia wazo kuu la mada hii tuliyowasiliana wakati uliopita? (Kupitia kwa uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, ninaona kwamba Mungu hulea vitu vyote na hulea wanadamu.

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII (II) Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote(Sehemu ya Tatu)


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)

Mwenyezi Mungu alisema, Baada ya kujadili kwa kina hadi sasa, mnahisi kwamba mna uelewa wa juujuu wa maana ya kidokezo cha kirai “Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote”? (Ndiyo.) Nilijua kwamba Nilipojadili mada hii watu wengi wangefikiri kwa haraka juu ya jinsi Mungu ni kweli na namna ambavyo neno Lake linatukimu, lakini wangeifikiria tu katika kiwango hiki. Baadhi hata wangehisi kwamba Mungu kukimu maisha ya binadamu, kutoa chakula na kinywaji cha kila siku na mahitaji yote ya kila siku haihesabiki kama kumkimu mwanadamu. Je, baadhi ya watu hawahisi namna hii?

Jumatano, 3 Januari 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII (II) Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote(Sehemu ya Pili )


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote 
(I)

Mwenyezi Mungu alisema, Leo Nitashiriki nawe mada mpya. Mada itakuwa ni nini? Kichwa cha mada kitakuwa "Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote." Je, hii siyo mada kubwa kidogo kuweza kuijadili? Je, inaonekana kama kitu ambacho kidogo hakiwezi kufikika? Mungu kuwa chanzo cha uhai kwa vitu vyote inaweza kuonekana ni mada ambayo watu wanahisi kutohusika nayo, lakini wote wanaomfuata Mungu wanapaswa kuielewa.

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII | Mhutasari wa Mamlaka ya Mungu, Tabia ya Haki ya Mungu, na Utakatifu wa Mungu

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII | Mhutasari wa Mamlaka ya Mungu, Tabia ya Haki ya Mungu, na Utakatifu wa Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Mnapomaliza maombi yenu, je, mioyo yenu inahisi utulivu katika uwepo wa Mungu? (Ndiyo.) Ikiwa moyo wa mtu unaweza kutulizwa, ataweza kusikia na kuelewa neno la Mungu na ataweza kusikia na kuuelewa ukweli. Ikiwa moyo wako hauwezi kutulizwa, ikiwa moyo wako siku zote unayoyoma, au siku zote unafikiria juu ya mambo mengine, utaathiri kuja kwako pamoja kusikia neno la Mungu. Sasa, ni kitu gani cha msingi tunachokijadili wakati huu? Hebu sote turudi nyuma kidogo katika hoja kuu. Kuhusiana na kumjua Mungu Mwenyewe, yule wa kipekee, sehemu ya kwanza tuliyoijadili ni ipi? (Mamlaka ya Mungu.)

Jumamosi, 30 Desemba 2017

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)(Sehemu ya Nne)



Mwenyezi Mungu alisema, Hebu turudi kuzungumza kuhusu mbinu ambazo Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu. Tumeongea karibuni kuhusu mbinu mbalimbali ambazo Mungu anafanya kazi kwa mwanadamu ambazo kila mmoja wenu mnaweza kupitia nyinyi wenyewe, kwa hivyo sitatoa maelezo zaidi. Lakini katika mioyo yenu pengine mmechanganyikiwa kuhusu mbinu ambazo Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu, ama kwa kiwango cha chini zaidi ana upungufu wa maelezo, kwa hivyo itawafaidi kumzungumzia.

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)(Sehemu ya Tatu)



Mwenyezi Mungu alisema, Najua kwamba sasa watu wengi wananitarajia kusema ni nini hasa utakatifu wa Mungu, lakini Ninapozungumza kuhusu utakatifu wa Mungu Nitaongea kwanza kuhusu matendo ambayo Mungu anafanya. Nyinyi nyote mnapaswa kusikiza kwa makini, kisha nitawauliza utakatifu wa Mungu ni nini hasa. Sitawaeleza moja kwa moja, lakini badala yake nitawaacha mjaribu kuutambua, kuwapa nafasi ya kuutambua. Mnafikiri nini kuhusu mbinu hii? (Ni nzuri.) Kwa hivyo sikizeni kwa makini.

Ijumaa, 29 Desemba 2017

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)(Sehemu ya Pili)



Tumetoka tu kuongea kuhusu jinsi Shetani hutumia maarifa kumpotosha mwanadamu, basi kinachofuata wacha tushiriki kuhusu jinsi Shetani hutumia sayansi kumpotosha mwanadamu. Kwanza, kwa kutumia sayansi kumpotosha mwanadamu, Shetani hutumia jina la sayansi kuridhisha kutaka kujua kwa mwanadamu, kuridhisha hamu ya mwanadamu [a] kutafiti sayansi na kuchunguza siri. Pia, katika jina la sayansi, Shetani huridhisha haja ya mwili na mahitaji ya mwanadmu kuendelea kuinua ubora wao wa maisha. Shetani hivyo, katika jina hili, hutumia njia ya sayansi kumpotosha mwanadamu.

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)(Sehemu ya Kwanza)



Mwenyezi Mungu alisema, Mnahisi vipi baada ya kusema sala zenu? (Tunafurahia na kuguswa sana.) Wacha tuanze ushirika wetu. Tulishiriki mada ipi wakati uliopita? (Utakatifu wa Mungu.) Na ni kipengele kipi cha Mungu Mwenyewe kinahusisha utakatifu wa Mungu? Je, kinahusisha kiini cha Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo ni nini hasa mada inayohusiana na kiini cha Mungu? Je, ni utakatifu wa Mungu? (Ndiyo.) Utakatifu wa Mungu: hiki ni kiini cha kipekee cha Mungu. Ni nini ilikuwa dhamira kuu tuliyoshiriki wakati uliopita? (Kutambua uovu wa Shetani.) Na ni yapi tuliyoyashiriki wakati uliopita kuhusu uovu wa Shetani? Mnaweza kukumbuka?

Jumanne, 26 Desemba 2017

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu (II)(Sehemu ya Nne)



E. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Mienendo ya Kijamii Kumpotosha Mwanadamu
Mwenyezi Mungu alisema, Je, mienendo ya kijamii ni kitu kipya? (La.) Hivyo ilianza lini? Mtu anaweza kusema kwamba mienendo ya kijamii ilianza wakati Shetani alipoanza kuwapotosha watu? (Ndiyo.) Mienendo ya kijamii inajumuisha nini? (Mtindo wa mavazi na vipodozi.) Hiki ni kitu ambacho watu mara nyingi wanakutana nacho. Mtindo wa mavazi, mtindo wa kisasa na mienendo, hiki ni kipengele kidogo. Kuna kingine zaidi? Je, misemo maarufu ambayo watu wanapenda kusema inahesabika pia? Je, pia mitindo ya maisha ambayo watu wanataka inahesabika?

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu (II)(Sehemu ya Tatu)


    Mwenyezi Mungu alisema, Kuhusu utakatifu wa Mungu, hata kama inaweza kuwa mada inayojulikana, katika majadiliano inaweza kuwa dhahania kiasi kwa watu wengine, na maudhui yake yanaweza kuwa ya kina sana. Zamani, watu hawakushughulika sana na mada ya utakatifu wa Mungu, kwa hivyo hawaielewi. Lakini msijali, Nitawasaidia kuelewa maana ya utakatifu wa Mungu. Naona kwamba ni vigumu kidogo kwenu kupokea, wacha tuseme hili kwanza: Iwapo unataka kujua mtu, angalia tu kile anachofanya na matokeo ya vitendo vyake, na utaweza kuona kiini cha mtu huyo. Kwa hivyo hebu tushiriki kuhusu utakatifu wa Mungu kutoka kwa mtazamo huu kwanza.