Smiley face
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kumbukumbu-za-Maongezi-ya-Kristo. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kumbukumbu-za-Maongezi-ya-Kristo. Onyesha machapisho yote

Jumapili, 4 Februari 2018

Sura ya 45. Watu Waliochanganyikiwa Hawawezi Kuokolewa


Mwenyezi Mungu alisema, Imesemwa “Yeye afuataye hadi mwisho ataokolewa,” lakini hili ni rahisi kuweka katika vitendo? Sio, na watu wengine hawawezi kufuata hadi mwisho. Pengine watakapokabiliwa na wakati wa majaribu, ama uchungu, ama jaribio, basi wanaweza kuanguka, na kutoweza kusonga mbele tena. Mambo ambayo hufanyika kila siku, yawe ni makubwa ama madogo, yanaweza kutikisa uthabiti wako, kuumiliki moyo wako, kuzuilia uwezo wako wa kufanya jukumu lako, ama kudhibiti kuendelea kwako mbele—vitu hivi vyote vinahitaji kuchukuliwa kwa uzito, lazima vichunguzwe kwa makini ili kuutafuta ukweli, na ni vitu vyote ambavyo vinafanyika katika ulimwengu wa uzoefu.

Jumatano, 31 Januari 2018

Sura ya 38. Yeye Ambaye Hukosa Ukweli Hawezi Kuwaongoza Wengine


Mwenyezi Mungu alisema, Je, kweli mnaelewa kuhusu mabadiliko katika tabia ya mtu? Mabadiliko katika tabia yanamaanisha nini? Je, mnaweza kutambua mabadiliko katika tabia? Ni hali zipi zinaweza kufikiriwa kuwa mabadiliko katika tabia ya maisha ya mtu, na ni hali zipi ambazo ni mabadiliko tu katika tabia ya nje? Tofauti ni ipi kati ya mabadiliko katika tabia ya mtu ya nje na mabadiliko katika maisha ya mtu ya ndani?

Jumatatu, 29 Januari 2018

Sura ya 36. Kujijua Mwenyewe Hasa Ni Kujua Asili ya Binadamu


La muhimu katika kufikia badiliko la tabia ni kujua asili ya mtu mwenyewe, na hili ni lazima litoke kwa ufunuo na Mungu. Ni katika neno la Mungu tu ambapo mtu anaweza kujua asili yake ya kutia kinyaa, afahamu katika asili yake mwenyewe sumu mbalimbali za Shetani, atambue kuwa yeye ni mjinga na mpumbavu, na atambue dalili dhaifu na hasi katika asili yake mwenyewe. Mara haya yanapojulikana kikamilifu, na unaweza kwa hakika kunyima mwili, daima kutekeleza neno la Mungu, na kuwa na mapenzi ya kujiwasilisha kikamilifu kwa Roho Mtakatifu na kwa neno la Mungu, basi umeianza njia ya Petro.

Jumapili, 28 Januari 2018

Sura ya 32. Ni Watu wa Aina Gani Watakaoadhibiwa


Mwenyezi Mungu alisema, Kukufuru na kashfa dhidi ya Mungu ni dhambi ambayo haitasamehewa kwa enzi hii na enzi ijayo na wale wanaofanya dhambi hii hawatazaliwa upya kamwe. Hili linamaanisha kwamba tabia ya Mungu haiwezi kuvumilia kosa la wanadamu. Watu wengine wanaweza kusema maneno yasiyofaa au maneno mabaya wakati hawaelewi, au wanapodanganywa, kuwekewa vikwazo, kudhibitiwa, au kukandamizwa na wengine. Lakini wanapokubali njia ya ukweli katika siku zijazo watajawa na majuto. 

Ijumaa, 26 Januari 2018

Sura ya 94. Wale Ambao Hawawezi Kuishi Mbele Ya Mungu Daima Ni Wasioamini


Mwenyezi Mungu alisema, Nguzo inapopandishwa kidogo, mnaweza kupiga hatua kidogo. Si jambo baya kuwa na mahitaji ya juu kutoka kwenu na wala si jambo baya kuwauliza maswali magumu. Lengo ni kuwafanya muwe na ufahamu zaidi juu ya elimu na maarifa ya kawaida ya kipengele cha weledi cha wajibu wenu.[a] Huenda labda nyinyi bado hulalamika katika nyoyo zenu, mkisema: "Tumejifunza mambo mengi mazuri lakini Mungu huwa hayataji kamwe au kuturuhusu kuyatumia. 

Jumapili, 14 Januari 2018

Sura ya 92. Njia ya Utendaji katika Kusuluhisha Ukaidi


Mtu huwa na tatizo lipi anapopenda kupeana visingizio? Ni nini kiini chake? Yeye ni mkaidi. Watu wakaidi hawakubali ukweli kwa urahisi; sio watiifu, na wanaposikia neno moja ambalo haliambatani na dhana, mitazamo, wanayopenda, hisia au mihemko yao wenyewe, basi hawalikubali; husema, “Sijali iwapo liko sahihi au ni mbaya, ni nani aliyelinena, lilinenwa katika muktadha gani, au iwapo linahusiana na majukumu na wajibu wangu; siyajali mambo haya.

Jumatatu, 1 Januari 2018

Sura ya 91. Kupitia Aina Tofauti Za Mazingira Kuna Manufaa Kwa ukuaji Wa Maisha Ya Binadamu

Ni vyema kupitia mazingira ya aina tofauti. Mungu hakupangii mazingira haya bila sababu. Yeye hakuongozi popote pale bila makusudi, bali Yeye huandaa mazingira fulani spesheli kwa kila mmoja—mazingira ya kifamilia, mazingira ya kimaisha, mazingira uliyokulia, namazingira unatekeleza majukumu yako punde utakapo mwamini. Yeye hutayarisha hali au mazingira fulani spesheli kwako wewe kuzipitia. 

Jumapili, 31 Desemba 2017

Sura ya 88. Kulipa Gharama ili Kupata Ukweli ni Muhimu Sana


Mwenyezi Mungu alisema, Sio rahisi kwa vijana kuendeleza kazi; wengi wao hawadumishi mwendo. Ni lazima moyo wako uwe mtulivu, lazima uweze kudumisha mwendo na uwe tayari kutumia muda kwake. Wengine hujiburudisha au kuwachezea wengine, lakini wewe unasema, "Siwezi, sina wakati. Biashara yangu ina shughuli sana. Nendeni mkajiburudishe. Ni lazima niipange biashara yangu.” Unaweza tu kufaulu kwa kushughulika na kujitolea kwa biashara yako. Kwa kweli, hukosi nguvu sasa, wala hukosi ujuzi wa kitaalamu.

Alhamisi, 28 Desemba 2017

Sura ya 62. Ili Kuwa Mwaminifu, Unapaswa Kujiweka Wazi kwa


Mwenyezi Mungu alisema, Wengine Je, mna uzoefu wowote wa kuwa waaminifu? (Ni vigumu kuwa mwaminifu). Na mbona ni vigumu? (Ninapotafakari juu yangu kila siku, nagundua kuwa najua vyema kujifanya, na kwamba nimesema mengi ambayo si sahihi. Wakati mwingine, maneneo yangu yatakuwa na hisia na motisha, wakati mwingine, nitaunda ujanja fulani ili kutimiza malengo yangu, nikisema ukweli nusu ambao haulingani na mambo ya hakika; maneno mengine, pia, yatakuwa hayapasi kabisa, na ya kubuniwa.)

Sura ya 59. Namna ya Kumridhisha Mungu katikati ya Majaribu


Mwenyezi Mungu alisema, Ninaibua maswali machache kwa tafakari yenu: Tangu mara ya mwisho tuliposema kwamba kutakuwa na miaka saba mingine ya majaribu makubwa, iwe ni kwa dhiki au majanga, je, mmegundua kusudi la Mungu kupitia kwa hayo? Ni asili gani ya binadamu mnaweza kuona katika mijibizo na mitazamo ya watu kwa miaka hii saba ya majaribu? Hili litachanganuliwa vipi? Fikirieni hilo. Ninazungumzia asili ya binadamu katika kila ushirika, kufikia chanzo, kuchanganua asili ya binadamu, na kuchanganua kiini. Ni juu yenu basi kuwasiliana ufahamu wenu kuhusu hizi mada.

Jumamosi, 16 Desemba 2017

Sura ya 58. Upendo wa Kweli wa Mungu kwa Wanadamu


Mwenyezi Mungu alisema, Katika kukifahamu kiini cha Kristo, kipengele kimoja ni kuwa na uwezo wa kutofautisha kati ya kupata mwili Kwake na binadamu; aidha, watu ambao wanafahamu kiini cha Kristo wana uwezo zaidi kuwa hakika kuhusu Mungu kuwa mwili na uwezo zaidi wa kuamini kuwa Yeye kweli Yupo, kuwa Yeye si nabii, mtume, wala mwenye kufunua, na hasa si mtu mdogo aliyetumwa hapa na Mungu; bali Yeye ni mwenye mwili, Yeye ni Kristo, Naye ni Mungu Mwenyewe. Hata kama mwili ulikuwa sehemu miongoni mwa watu, Alikuwa mtu wa kawaida na kiini cha Uungu.

Ijumaa, 15 Desemba 2017

Sura ya 56. Je, Unauelewa Upendo wa Mungu kwa Binadamu?

 

Mwenyezi Mungu alisema, Upendo wa Mungu, ambaye alikuwa mwili, unajidhihirisha wapi kwa binadamu? Baada ya kupitia uzoefu wa kazi hatua kwa hatua, mnaweza kuona kwamba Mungu anapozungumza katika kila hatua ya kazi, anatumia ruwaza fulani, anazungumza unabii fulani, na anaonyesha ukweli fulani na tabia ya Mungu, na watu wote wana mijibizo. Mijibizo yao ni nini? Hawajinyenyekeshi kwa Mungu, hususan hawachukui hatua ya kutafuta ukweli, au hawapo radhi kukubali kazi ya Mungu.

Alhamisi, 14 Desemba 2017

Sura ya 55. Usieleze Kile Mungu Alicho Nacho na Kile Alicho


Mwenyezi Mungu alisema, Kazi na matamshi ya Mungu ya miaka michache iliyopita yote yamerekodiwa kimsingi katika kitabu, Neno Laonekana katika Mwili. Baadhi ya maneno katika kitabu hiki ni ya kinabii na yanatabiri vile enzi za baadaye zitakavyokuwa. Unabii kwa kweli ni mfumo wa jumla, na zaidi ya nusu ya kitabu kinajadili kuingia kwa mwanadamu kwa maisha, kinaweka wazi utu, na kinazungumzia kuhusu kumwelewa Mungu na tabia Yake.

Jumatano, 13 Desemba 2017

Sura ya 54. Watu Ambao Daima Wana Mahitaji kwa Mungu Ndio wa Mwisho Kuwa Tayari Kusikia Hoja


Mwenyezi Mungu alisema, Kama utajielewa, ni lazima uielewe hali yako ya kweli; jambo muhimu zaidi katika kuielewa hali yako mwenyewe ni kuwa na ufahamu juu ya fikira zako na mawazo yako. Katika kila kipindi cha muda, fikira za watu zimekuwa zikidhibitiwa na jambo moja kubwa; ikiwa unaweza kuzielewa fikira zako, unaweza kukielewa kitu kilicho nyuma yazo. Hakuna mtu anayeweza kuzidhibiti fikira na mawazo yake. Je, fikira na mawazo haya hutoka wapi? Je, ni nini kiini cha matilaba haya? Je, fikira hizi na mawazo haya huzalishwaje? Je, zinadhibitiwa na nini?

Jumapili, 10 Desemba 2017

Sura ya 53. Kuelewa Visawe na Tofauti katika Asili ya Binadamu

 

Mwenyezi Mungu alisema, Je, mnaona kwa dhahiri njia ya imani yenu kwa Mungu na njia yenu ya kufuata ukweli? Imani katika Mungu kweli ni nini? Je, mmetosheka baada ya kupitia shida kidogo? Watu wengine hufikiri kwamba baada ya kupitia hukumu na kuadibiwa, kupogolewa na ushughulikiwaji au baada ya kufichua hali yao ya kweli, wamemaliza na matokeo yao yameonekana. Wengi wa watu hawawezi kuona suala hili kwa dhahiri, na wao wote husimamishwa hapo, bila kujua jinsi ya kuitembea njia iliyo mbele. 

Sura ya 52. Dalili za Udanganyifu Ndani ya Mwanadamu na Asili ya Mwanadamu Ambazo Humsaliti Mungu


Mwenyezi Mungu alisema, Ugumu ambao watu wanaweza kuukabili kwa urahisi katika uzoefu wao, vitu ambavyo vinawasababisha watu kuanguka kwa urahisi, na pahali ambapo udhaifu wa jaala wa kila mtu upo yote ni masuala ambayo lazima mtu awe na ujuzi nayo. Kwa nini unaanguka, unamwacha Mungu na kupoteza imani ya kuendelea na ukimbiziaji wako wa ukweli unapokabiliana na mambo fulani? Kwa sasa, kila mtu yumo hatarini mwa mambo haya. 

Jumamosi, 9 Desemba 2017

Sura ya 51. Je Unajua Ukweli Hakika Ni Nini?


Mwenyezi Mungu alisema, Ninyi nyote mara nyingi mmepata uzoefu wa hali ya kuwa katika mkutano, na kuhisi kana kwamba huna chochote cha kuhubiri kuhusu—hatimaye unajilazimisha na unasema kitu cha juu juu. Unajua vizuri kuwa maneno haya ya juu juu ni kanuni, lakini unahubiri kuyahusu hata hivyo, na mwishowe unahisi kuwa huna shauku, na watu chini yako wanasikiliza na wanahisi kuwa yanachosha sana—je hilo halijafanyika? 

Sura ya 49. Unapaswa Kuutumia Ukweli Kumaliza Hali Yako Hasi



Mwenyezi Mungu alisema, Watu wengi wana hali hizi ambazo tumejadiliana hapo awali, hata ingawa si wazi kama hapo awali. Hii ni kwa sababu watu hawakuwa na ufahamu wowote wa ukweli wakati huo, na hawakuelewa chochote. Siku hizi, unasikiliza zaidi, na kwa kiwango cha chini kabisa, nyote mnaelewa baadhi ya mafundisho. Hata hivyo, una hali fulani zilizojikita ndani ambazo hazijafunuliwa. Una uwezo wa kuuona upotovu kwa wazi ambao mara nyingi hufunuliwa na kuwa na ufahamu mara tu unapofunuliwa; unajua asili ya malengo yako yaliyofunuliwa, maneno, na vitendo.

Ijumaa, 8 Desemba 2017

Sura ya 46. Ni Kwa Kuujua Uweza wa Mungu Pekee Ndipo Unaweza Kuwa na Imani ya Kweli


Mwenyezi Mungu alisema, Wengi wa watu hawaelewi kazi ya Mungu na si rahisi kuelewa kipengele hiki. Kitu cha kwanza ambacho lazima ujue ni kwamba kunawakati ulioteuliwa wa kazi yote ya Mungu na bila shaka si kama ilivyodhaniwa na watu. Mwanadamu hawezi kamwe kuelewa kazi ambayo Mungu ataifanya ama wakati Ataifanya. Anafanya sasa kile kinachostahili kufanywa sasa na hiki ni kitu ambacho hakuna anayeweza kukiharibu; Anafanya baadaye kile kinachostahili kufanywa baadaye, na hachelewi hata kwa sekunde moja, na hakuna anayeweza kuharibu jambo hilo pia.

Sura ya 48. Ni kwa Kuzielewa Hali Zako tu Ndipo Utakapoweza Kutembea Katika Njia Sawa



Ndani ya mwanadamu mara nyingi zipo baadhi ya hali mbaya. Miongoni mwao ni baadhi ya hali ambazo zinaweza kuwaathiri watu au kuwadhibiti. Kunazo baadhi ya hali ambazo zinaweza hata kumfanya mtu kuiacha njia ya kweli na kuelekea katika njia mbovu. Kile mwanadamu anachokitafuta, kile wanachozingatia na njia wanayochagua kuifuata—haya yote yanahusiana na hali zao za ndani. Hata zaidi ni udhaifu wa mwanadamu au nguvu inayohuhusiana moja kwa moja na hali zao za ndani.