Smiley face
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Njia-ya-Uzima-wa-Milele. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Njia-ya-Uzima-wa-Milele. Onyesha machapisho yote

Jumapili, 20 Oktoba 2019

Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu Pekee

Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu Pekee

Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu Pekee

Kila mtu anahisi kuwa usimamizi wa Mungu ni wa ajabu, kwa sababu watu wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu hauna uhusiano wowote na mwanadamu. Wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu ni kazi ya Mungu pekee, shughuli za Mungu, na hivyo wanadamu hawajali kuhusu usimamizi wa Mungu. Kwa njia hii, kuokolewa kwa wanadamu kumekuwa kusiko yakini na kusiko dhahiri, na kumebaki tu maneno matupu. Hata kama mwanadamu anamfuata Mungu ili aokolewe na aingie katika hatima inayopendeza, mwanadamu hajishughulishi na jinsi ambavyo Mungu Hutekeleza kazi Yake. Mwanadamu hashughulishwi na Anachokipanga Mungu na anachopaswa kufanya ili aokolewe.Huzuni iliyoje! Kuokolewa kwa mwanadamu hakuwezi kutenganishwa na usimamizi wa Mungu, aidha hakuwezi kutenganishwa na mipango ya Mungu. Na bado mwanadamu hafikirii chochote kuhusu usimamizi wa Mungu, na hivyo anaendelea kujitenga mbali na Mungu. Kutokana na hayo, idadi ya watu wanaomfuata Mungu inaendelea kuongezeka bila kujua mambo yanayohusiana na kuokolewa kwa mwanadamu kama vile uumbaji ni nini, kuamini kwa Mungu ni nini, jinsi ya kumwabudu Mungu, na kadhalika. Kufikia sasa, basi, lazima tuzungumze kuhusu usimamizi wa Mungu, ndiposa kila mfuasi ajue wazi umuhimu wa kumfuata Mungu na kumwamini. Watakuwa na uwezo wa kuchagua njia watakayoifuata ipasavyo, badala ya kumfuata Mungu tu ili kupata baraka, au kuepukana na majanga, au kuwa na mafanikio.

Jumatano, 22 Agosti 2018

Swahili Gospel Movie Clip "Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" (8) - Jinsi ya Kupata Njia ya Uzima wa Milele



Kwa maelfu ya miaka waumini wa Bwana wametaka kupata uzima wa milele, lakini hakuna mtu ambaye ameweza kutimiza matamanio haya. Sasa, umechanganyikiwa kuhusu kama kweli kuna njia ya uzima wa milele au la au umechanganyikiwa juu ya jinsi unavyoweza kufuatilia hili kwa njia ambayo utapata njia ya uzima wa milele? Hii video fupi itakuambia jinsi ya kupata njia ya uzima wa milele.

Jumatatu, 20 Agosti 2018

Swahili Gospel Movie Clip "Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" (6) - Tofauti Kati ya Njia ya Toba na Njia ya Uzima wa Milele



Bwana Yesu na Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja. Bwana Yesu hufanya kazi ya ukombozi, Yeye anahubiri njia ya toba. Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho anafanya kazi ya hukumu ya kuwatakasa wanadamu, Yeye huleta njia ya uzima wa milele. Sasa, kama unataka kujua tofauti kati ya njia ya toba na njia ya uzima wa milele, tafadhali angalia hii video fupi.

Jumapili, 19 Agosti 2018

Swahili Gospel Movie Clip "Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" (5) - Ni Nani Anayempa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele?



Bwana Yesu alisema, "Lakini yeyote atakayekunywa maji yale nitakayompa hatahisi kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji yakibubujika katika uzima wa milele" (Yohana 4:14). Bwana Yesu ndiye chanzo cha maji hai ya uzima, Yeye ndiye njia ya uzima wa milele, lakini, kama ilivyoshudiwa na Umeme wa Mashariki, ni Kristo wa siku za mwisho pekee—Mwenyezi Mungu anaweza kuwapa watu njia ya uzima wa milele.

Jumamosi, 27 Januari 2018

Dondoo ya Filamu ya Bwana Wangu Ni Nani – Kristo ndiye Chanzo cha Uhai na Vile Vile Bwana wa Biblia



Biblia imejaa maneno ya Mungu na vile vile uzoefu na ushuhuda kutoka kwa mwanadamu ambao unaweza kutupa uhai na ni yenye manufaa sana kwetu. Bwana Yesu alisema, “Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima: Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, bado ataishi: Na yeyote aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele.” (Yohana 11:25-26). Lakini kwa nini, baada ya miaka 2,000, hakuna kati ya wale walio na imani katika Bwana ambao wamesoma Biblia wamewahi kupata uzima wa milele? Inaweza kuwa kwamba Biblia haina njia ya uzima wa milele? Inaweza kuwa kwamba wakati Bwana Yesu alitekeleza kazi Yake ya ukombozi kwamba Hakuwapa binadamu njia ya uzima wa milele? Tunapaswa kufanya nini ili kuweza kupata njia ya uzima wa milele?