Tunadharau wale wote walio kinyume na Bwana Yesu; wote wataishia kuangamizwa. Nani aliwaambia wasiamini kwamba Bwana Yesu ni Mwokozi? Bila shaka, kuna nyakati ambapo tunaiga Bwana Yesu katika kuwa na huruma kwa watu wa dunia, kwa kuwa hawaelewi, na ni sahihi kwamba tuwe wavumilivu na kuwasamehe. Kila kitu tufanyacho ni kwa mujibu wa maneno ya Biblia, kwani kila kitu ambacho hakifuatani na
Biblia ni chenye kufuata imani tofauti na ni uzushi, Imani ya aina hii imekita mizizi katika akili ya kila mmoja wetu. Bwana wetu yumo katika Biblia, na tusipoondoka kwenye Biblia basi hatutaondoka kwa Bwana; tukitii kanuni hii, tutapata wokovu. Sisi huhimizana, kila akisaidia mwingine, na kila wakati tunapokusanyika pamoja ni matumaini yetu kwamba kila kitu tunachosema na kutenda kinaambatana na matakwa ya Bwana na kuwa kitabaliwa na Bwana. Licha ya uhasama mkali ulioko kwenye mazingira yetu, mioyo yetu imejaa furaha. Tunapowaza kuhusu baraka hizi tunazoweza kupata kwa urahisi, je, kuna kitu ambacho hatuwezi kukitenga kando? Je, kuna kitu ambacho hatuko tayari kuachana nacho? Yote haya hayapingwi, na haya yote yako chini ya macho angalifu ya Mungu. Sisi, walio wachache wa maskini ambao tumeinuliwa kutoka jaani, ni sawa tu na wafuasi wote wa Bwana Yesu wa kawaida tukiota kuhusu kunyakuliwa, na kubarikiwa, na kutawala mataifa yote. Upotovu wetu umeanikwa peupe machoni pa Mungu, na tamaa zetu na uchoyo zimehukumiwa machoni pa Mungu. Hata hivyo, yote haya hutokea bila ajabu kabisa, na tena yenye mantiki sana, na hakuna hata mmoja kati yetu ambaye hushangaa kama hamu zetu ni za haki, sembuse yeyote kati yetu ambaye anashuku usahihi wa yote yale ambayo sisi hushikilia. Nani anayeweza kujua mapenzi ya Mungu? Njia hii hasa ni gani ambayo binadamu hutembelea, hatujui jinsi ya kutafuta, au kuchunguza, sembuse kujishughulisha nayo. Kwa maana sisi hujali tu kuhusu kama tutaweza kunyakuliwa, kama tunaweza kubarikiwa, kama kuna pahali tumetengewa katika ufalme wa mbinguni, na kama sisi tutaweza kupata mgawo wa maji ya mto wa uzima na matunda ya mti wa uzima. Je, si ni kwa ajili ya kupata vitu hivi ndiyo tunamwamini Bwana na kuwa wafuasi Wake? Dhambi zetu zimesamehewa, tumetubu dhambi zetu, tumekunywa kikombe cha mvinyo ambao ni mchungu, na tumeuweka msalaba migongoni mwetu. Nani anayeweza kusema kuwa Bwana hatafurahi kukubali gharama ambayo tumelipia? Nani anayeweza kusema kuwa hatujatayarisha mafuta yanayotosha? Hatungependa kuwa wale mabikira wapumbavu, ama mmoja wa wale ambao wameachwa. Aidha, tunaomba mara kwa mara, tukimwomba Bwana atuepushe kutokana na kudanganywa na Kristo wa uongo, kwa maana imeandikwa kwenye Biblia: “Basi iwapo mtu yeyote atawaambia, Tazameni, Kristo yuko huku, au yuko pale; msiamini hili. Kwa kuwa wataibuka makristo wasio wa kweli, na manabii wasio wa kweli, nao wataonyesha ishara kubwa na vioja; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi” (Mathayo 24:23-24). Sisi sote tumeweka mistari hii ya Biblia kwenye kumbukumbu, tunaijua vyema sana, na tunaiona kama hazina ya thamani, kama hati ya muamana ambayo inaamua ikiwa tunaweza kuokolewa au kunyakuliwa …Mungu amenyamaza, na kamwe hawajawahi kujionyesha kwetu, ilhali kazi Yake haijawahi kusimama. Yeye huangalia dunia nzima, na huamuru vitu vyote, na kuona maneno yote na matendo yote ya mwanadamu. Yeye huendesha usimamizi Wake kwa hatua zilizopimwa na kulingana na mpango Wake kwa kimya, na bila madhara ya kutia shauku, ilhali nyayo Zake hukaribia, moja baada ya nyingine, daima hukaribia binadamu, na kiti Chake cha hukumu kimeenezwa katika ulimwengu kwa kasi ya umeme, na baada yake kiti Chake cha enzi mara moja hushuka kati yetu. Ni tukio la adhimu jinsi gani hilo, tukio hilo ni mandhari ya adhimu na yenye taadhima! Kama njiwa, na kama simba anayenguruma, Roho huja kati yetu. Yeye ni hekima, Yeye ni haki na uadhama, na Yeye huja kwa ukimya kati yetu, akiwa na mamlaka na akiwa amejawa na upendo na huruma. Hakuna mtu anayefahamu kuwasili Kwake, hakuna mtu anayekaribisha kuwasili kwake, na zaidi ya hayo, hakuna mwanadamu ambaye anajua chote ambacho yuko karibu kufanya. Maisha ya mwanadamu yanaendelea kama awali moyo wake hauna tofauti, na siku zinapita kama kawaida. Mungu huishi kati yetu, mwanadamu kama watu wengine, kama mmoja wa wafuasi wasio na maana kabisa na kama muumini wa kawaida. Ana shughuli Zake Mwenyewe, malengo Yake mwenyewe, na zaidi ya hayo, Ana uungu usiomilikiwa na binadamu wa kawaida. Hakuna mtu ambaye ameona kuwepo kwa uungu Wake, na hakuna mtu ambaye ametambua tofauti ya kiini Chake na kile cha binadamu. Sisi huishi pamoja Naye, bila mipaka au kuogopa, kwa kuwa katika macho yetu, Yeye ni muumini asiye wa maana tu. Yeye huona matukio yetu yote, na fikra na mawazo yetu yote yanawekwa wazi mbele Yake. Hakuna mtu ambaye huwaza chochote kuhusu kazi Yake na isitoshe, hakuna aliye na shuku hata kidogo kuhusu kitambulisho Chake. Chote tunachofanya ni kuendelea na shughuli zetu, kana kwamba Yeye hahusiani nasi …
Kwa bahati, Roho Mtakatifu huonyesha kifungu cha maneno “kupitia” Kwake, na hata ingawa inaonekana ni jambo lisilotarajiwa sana, tunalitambua hata hivyo kama tamko kutoka kwaa Mungu, na tunaukubali kwa urahisi kutoka kwa Mungu. Hii ni kwa sababu, bila kujali ni nani anayeonyesha maneno haya, ilimradi yanatoka kwa Roho Mtakatifu tunapaswa kuyakubali, na hatufai kuyakana. Tamko linalofuata linaweza kuja kupitia mimi, au wewe, ama kupitia yeye. Yeyote yule, yote ni neema ya Mungu. Ilhali bila kujali mtu huyo ni nani, hatufai kumwabudu mtu huyu, kwa kuwa bila kujali chochote, mtu huyu hawezi kuwa Mungu, wala hatuwezi kwa njia yoyote ile kumchagua mtu wa kawaida kama huyu kuwa ndiye Mungu wetu. Mungu wetu ni mkubwa na mwenye kuheshimika sana; mtu asiye na maana kama huyu anawezaje kusimama katika nafasi Yake? Zaidi ya hayo, tunamsubiri Mungu aje na kuturudisha kwa ufalme wa mbinguni, na kwa hivyo mwanadamu asiye na umuhimu hivyo anawezaje kuwa na sifa zinazostahili kufanya kazi ngumu na muhimu kama hiyo? Bwana akirudi tena, ni lazima iwe juu ya wingu jeupe, ambalo halaiki ya watu wanaweza kuliona. Huo utakuwa wa adhimu namna gani! Itawezekanaje kwamba Anaweza kujificha kwa siri kati ya kundi la watu wa kawaida?
Na bado ni huyu mtu wa kawaida, aliyefichika kati ya watu, ndiye anayefanya kazi hii mpya ya kutuokoa. Yeye hatupi maelezo yoyote, wala Hatuambii kwa nini amerudi, lakini Yeye anafanya tu kazi anayotarajia kufanya kwa hatua zilizopimwa, na kwa mujibu wa mpango Wake. Maneno Yake na matamshi Yake yanazidi kuja kwa wingi. Kuanzia kufariji, kuonya, kukumbusha, na kupeana onyo mpaka kukaripia na kufundisha nidhamu; kuanzia kutumia sauti ya upole na laini mpaka kutumia maneno makali na ya adhimu—lakini hakuna inayompa mwanadamu huruma na kumtia hofu. Kila kitu Anachosema kinatufikia kwetu na kulenga siri zilizofichwa ndani yetu, maneno Yake huchoma mioyo yetu, huchoma nafsi zetu, na hutuacha tukiwa tumejaa aibu isiyovumilika, tusijue pa kujificha. Tunaanza kutafakari iwapo Mungu Aliye katika roho ya huyu mtu kweli anatupenda, na nini hasa Anafanya. Labda tunaweza tu kunyakuliwa baada ya kuvumilia mateso haya? Vichwani mwetu tunafanya hesabu … kuhusu hatima inayokuja na kuhusu majaliwa yetu ya baadaye. Bado, kama awali, hakuna hata mmoja wetu anayeamini kwamba Mungu amechukua mwili tayari ili kutenda kazi kati yetu. Japokuwa Ametuandama kwa muda mrefu sana, ingawa tayari Yeye amesema maneno mengi uso kwa uso nasi, bado tunabaki bila hiari ya kumkubali mtu aliye wa kawaida kiasi hicho awe Mungu wa mustakabali wetu, na bado hatuna nia ya kumwaminisha mtu huyu asiye na maana udhibiti wa mustakabali na majaliwa yetu. Kutoka Kwake, tunafurahia ugavi usioisha wa maji ya uhai, na kupitia Kwake tunaishi uso kwa uso na Mungu. Lakini tunashukuru tu kwa neema ya Bwana Yesu aliye mbinguni, na hatujawahi kamwe kupa umakini hisia za huyu mtu wa kawaida mwenye kumilikiwa na uungu. Bado, kama awali Yeye kwa unyenyekevu, hufanya kazi Yake akiwa amefichwa ndani ya mwili, akipeana maonyesho a moyo Wake wa ndani zaidi, kana kwamba hafahamu kukataliwa Kwake na binadamu, kana kwamba yeye milele husamehe utoto na ujinga wa mwanadamu, na milele huvumilia mtazamo wa mwanadamu Kwake usioheshimu.
Pasipo sisi kujua, huyu mtu asiye muhimu ametuelekeza katika hatua moja baada ya nyingine ya kazi ya Mungu. Sisi hupitia majaribu tele, kuvumilia kurudi kusikohesabika, na tunajaribiwa na kifo. Tunapata kujua kuhusu tabia ya Mungu ya haki na uadhama, kufurahia, pia, upendo na huruma Zake, tunakuja kufahamu nguvu za Mungu ambazo ni kubwa na hekima Yake, tunashuhudia uzuri wa Mungu, na kutazama hamu Yake ya kumwokoa mwanadamu. Kwa maneno ya huyu mtu wa kawaida, tunakuja kujua tabia na kiini cha Mungu, kufahamu mapenzi ya Mungu, kujua asili ya mwanadamu na kiini cha mwanadamu, na tunapata kuona njia ya wokovu na ukamilifu. Maneno Yake hutufanya sisi “tufe,” na tena hutufanya “kuzaliwa upya”; maneno Yake hutufariji, na ilhali pia hutuacha tukiwa tumejawa na hatia na hisia ya kuwa wadeni; maneno Yake hutuletea furaha na amani, lakini pia maumivu makubwa sana. Wakati mwingine sisi ni kama wanakondoo wa kuchinjwa mikononi Mwake; wakati mwingine sisi ni kama kipenzi cha roho Yake na kufurahia upendo Wake wenye upole; wakati mwingine sisi ni kama adui Yake, na chini ya macho Yake tunageuzwa majivu na ghadhabu Yake. Sisi ni jamii ya wanadamu waliookolewa Naye, sisi ni funza machoni Pake, na sisi ni wanakondoo waliopotea ambao, usiku na mchana, Yeye hunuia kuwapata. Yeye ni mwenye huruma kwetu, hutudharau, Yeye hutuinua, Yeye hutufariji na kutuhimiza, Yeye hutuongoza, yeye hututia nuru, yeye huturudi na kutufundisha nidhamu, na Yeye hata hutulaani. Usiku na mchana, Yeye hakomi kamwe kuwa na wasiwasi nasi na hutulinda na kututunza usiku na mchana, Asiwache upande wetu kamwe, bali humwaga damu ya moyo Wake kwa ajili yetu na hulipia gharama yoyote kwa ajili yetu. Miongoni mwa matamshi ya mwili huu mdogo na wa kawaida wa nyama, tumefurahia ukamilifu wa Mungu na kuona hatima ambayo Mungu ametupa. Licha ya haya, majivuno bado yanazua rabsha mioyoni mwetu, na sisi bado hatuna nia ya kukubali kikamilifu mtu kama huyu kama Mungu wetu. Ingawa Yeye ametupa mana nyingi sana, nyingi sana ya kufurahia, hamna kati ya haya ambalo linaweza kuchukua nafasi ya Bwana katika mioyo yetu. Tunaheshimu utambulisho maalum na hadhi ya huyu mwanadamu kwa kusita sana. Bora hafungui mdomo Wake kututaka tukiri kwamba Yeye ni Mungu, sisi kamwe hatuwezi kukata kauli wenyewe na kukiri Yeye ni Mungu ambaye yuko karibu kuja na ilhali amekuwa akifanya kazi kati yetu kwa muda mrefu sana.
Mungu huendelea na matamshi Yake, akitumia mbinu mbalimbali na mitazamo kutuonya kuhusu kile tunachofaa kufanya na wakati uo huo akipea moyo Wake sauti Maneno Yake hubeba nguvu ya maisha, hutuonyesha njia tunayopasa kutembea, na yanatuwezesha kujua ukweli ni nini. Tunaanza kuvutiwa na maneno Yake, tunaanza kuzingatia sauti Yake na jinsi Anavyoongea, na bila hiari tunaanza kuvutiwa na hisia za ndani kabisa za mwanadamu huyu asiye wa ajabu. Yeye hutema damu ya moyo Wake kwa niaba yetu, hupoteza usingizi na hamu ya chakula kwa ajili yetu, analia kwa ajili yetu, anashusha pumzi kwa ajili yetu, anaugua magonjwa akigumia kwa ajili yetu, anadhalilishwa kwa ajili ya wokovu na hatima yetu, na uasi wetu na kufa ganzi kwetu kunatoa machozi na damu kutoka kwa moyo Wake. Njia hii ya kuwa na kumiliki si ya mtu wa kawaida, wala haiwezi kumilikiwa au kufikiwa na mtu yeyote aliyepotoka. Anaonyesha uvumilivu na subira isiyomilikiwa na mtu wa kawaida, na upendo Wake si kitu ambacho kiumbe chochote kimepewa. Hakuna mtu mbali na Yeye anayeweza kujua mawazo yetu yote, au kufahamu asili yetu na kiini chetu kwa dhahiri na ukamilifu, ama kuhukumu uasi na upotovu wa binadamu, ama kusema nasi na kufanya kazi kati yetu kama hivi kwa niaba ya Mungu aliye mbinguni. Hakuna mtu isipokuwa Yeye ambaye amepewa mamlaka, hekima, na heshima ya Mungu; tabia ya Mungu na kile Mungu Anacho na alicho yanatoka, kwa ukamilifu wao, ndani Yake. Hakuna mtu mbali na Yeye ambaye anaweza kutuonyesha njia na kutuletea mwangaza. Hakuna yeyote ila Yeye anayeweza kutufichulia siri ambazo Mungu hajatufunulia tangu uumbaji hadi leo. Hamna yeyote isipokuwa Yeye ambaye anaweza kutuokoa kutokana na utumwa wa Shetani na tabia yetu potovu. Yeye humwakilisha Mungu. Yeye huonyesha moyo wa ndani zaidi wa Mungu, ushawishi wa Mungu, na maneno ya hukumu ya Mungu kwa wanadamu wote. Ameanzisha enzi mpya, nyakati mpya, na kuleta mbingu na nchi mpya na kazi mpya, na ametuletea matumaini, akimaliza maisha ambayo tuliishi katika hali isiyo dhahiri, na kuwezesha nafsi yetu nzima kuona njia ya wokovu kwa udhahiri kamili. Ameshinda ubinadamu wetu wote, na kupata mioyo yetu. Tangu wakati huo na kuendelea, akili zetu zimepata ufahamu, na nafsi zetu huonekana kufufuka: Huyu mwanadamu wa kawaida asiyekuwa na umuhimu, ambaye huishi kati yetu na ambaye amekataliwa na sisi zamani—Je, huyu si ni Bwana Yesu, ambaye daima huwa kwa mawazo yetu, tukiwa tumeamka au kuota, na ambaye tunamtamani usiku na mchana? Ni Yeye! Ni Yeye kweli! Yeye ni Mungu wetu! Yeye ndiye ukweli, njia, na uzima! Yeye ametuwezesha kuishi tena na kuona nuru, na amekomesha mioyo yetu kuhangaika. Tumerudi nyumbani mwa Mungu, tumerejea mbele ya kiti Chake cha enzi, tuko uso kwa uso pamoja na Yeye, tumeshuhudia uso Wake, na tumeona njia iliyo mbele. Wakati huu, mioyo yetu imeshindwa kabisa na Yeye; hatuna shaka kuhusu Yeye ni nani tena, hatupingi tena kazi Yake na neno Lake, na tunasujudu, mbele Yake. Hakuna tunachotaka zaidi yakufuata nyayo za Mungu maishani mwetu mwote, na kufanywa wakamilifu naye, na kulipa fadhila Yake, na kulipa upendo Wake kwetu, na kutii matayarisho na mipangilio Yake, na kushirikiana na kazi Yake, na kufanya kila kitu tunachoweza ili kukamilisha kile Anachotuaminia.
Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni