Smiley face

Jumatano, 4 Oktoba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kufanya Matendo Mema ya Kutosha Ili Uandae Mwisho Wako wa Safari

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
 Unapaswa Kufanya Matendo Mema ya Kutosha Ili Uandae Mwisho Wako wa Safari


Nimefanya kazi nyingi miongoni mwenu na, ni wazi kwamba, Nimezungumza vizuri pia. Hata hivyo, Nahisi kwamba maneno na kazi Yangu havijatimiza lengo la kazi Yangu ya siku za mwisho. Maana, katika siku za mwisho, kazi Yangu si kwa ajili ya mtu au watu fulani bali ni kwa manufaa ya kufafanua tabia Yangu asilia. Hata hivyo, kutokana na sababu nyingi—pengine ukosefu wa muda au shughuli nyingi za kazi—tabia Yangu haijamwezesha binadamu kunijua hata kidogo.  Kwa hivyo, Ninasonga mbele na katika mpango Wangu mpya, kazi Yangu ya mwisho, kufungua ukurasa mpya ili wale ambao wataniona watajipiga kifuani na kuulilia uwepo Wangu bila kukoma. Kwani Ninaleta mwisho wa mwanadamu duniani, na baada ya hapo, Nitaweka wazi tabia Yangu kwa mwanadamu ili wanijuao na wasionijua “watayalisha macho yao” na kuona kwamba kweli, nimekuja kwa wanadamu, duniani mahali ambapo vitu vyote vinazidi kuongezeka. Huu ni mpango Wangu, “kukiri” Kwangu kwa pekee tangu Nimuumbe mwanadamu. Matilaba yangu ni kuona mnafuatilia kwa moyo wenu wote kila Ninachokifanya, maana kiboko Changu kinamkaribia mwanadamu tena, karibu na wale wote wanaonipinga.
Pamoja na mbingu, Ninaanza kazi ambayo ni lazima Niifanye. Kwa hivyo Mimi husafiri kati ya misururu ya watu na kupita kati ya mbingu na ardhi. Hakuna mtu anayetambua mienendo Yangu au kuitambua maneno Yangu. Kwa hivyo, mpango Wangu bado unaendelea kwa urahisi. Ni vile tu hisia zenu zimekuwa ngumu kiasi kwamba hamjui hatua za kazi Yangu hata kidogo. Hata hivyo, siku moja, mtakuja kutambua kusudio Langu. Leo hii, Ninaishi miongoni mwenu na Ninasumbuka pamoja nanyi. Kwa muda mrefu, Nimeelewa mtazamo alio nao mwanadamu juu Yangu. Nisingependa kutangaza wazi, wala kutoa mifano zaidi ya kile kinachoniumiza ili kuwaaibisha. Ombi Langu la pekee ni kwamba myaweke moyoni yale yote mliyoyafanya kwa ajili ya hukumu siku tutakapokutana tena. Nisingependa kumshutumu yeyote miongoni mwenu kwa njia isiyo ya kweli, kwa sababu Nimekuwa Nikifanya mambo kwa njia ya haki, bila upendeleo, na yenye heshima. Bila shaka Ningependa kwamba nyinyi pia ni waadilifu na hamtafanya lolote lililo kinyume na mbingu na ardhi na dhamiri yenu. Haya pekee ndiyo Ninayowauliza. Wengi wanasumbuka na hawana amani kwa sababu wametenda maovu mabaya, na wengi wanaona aibu kwamba hawajawahi tenda lolote zuri. Tena wapo wengi ambao hawatahayari kutokana na dhambi zao na badala yake, wanakuwa wabaya zaidi, huku wakizitoa sura zao mbaya—ambazo zilikuwa bado hazijaonyeshwa kikamilifu—ili kujaribu silika Yangu. Huwa sijali au sitilii maanani matendo ya mtu yeyote mmoja. Badala yake, Mimi hufanya kazi Ninayopaswa kufanya, kujifunza maarifa, kuzunguka katika nchi au kufanya lile ambalo lilanipendeza. Katika wakati muhimu, Mimi hurejelea kazi Yangu miongoni mwa wanadamu kama Nilivyopanga, bila kuchelewa hata kidogo, na hili hufanywa kwa urahisi na kwa makini. Hata hivyo, kuna watu ambao wanawekwa pembeni katika kila hatua ya kazi Yangu, kwa sababu Ninadharau hali yao ya kujipendekeza na hali ya kujifanya wanyenyekevu. Wale wanaonichukia hakika watatelekezwa, iwe ni kwa kupenda au kwa kutopenda. Kwa ufupi, Ninataka wale wote Ninaowadharau kuwa mbali Nami. Ni dhahiri kwamba, sitawahurumia wale waovu ambao wamebaki katika makao Yangu. Kwa kuwa siku ya adhabu ya mwanadamu inakaribia, sina wasiwasi wa kuzitupa nje zile nyoyo zote zinazostahili dharau, kwa kuwa Nina mpango Wangu Mwenyewe.
Huu ndio wakati Ninapoamua mwisho wa kila mtu, wala si hatua ya kuanza kumshughulikia mwanadamu. Mimi huandika maneno na matendo yote ya kila mtu katika kitabu Changu, na vilevile njia walizozifuata wakiwa wafuasi Wangu, sifa zao asilia, na utendakazi wao wa mwisho. Kwa njia hii, hakuna mtu yeyote atakayeepuka mkono Wangu na kila mmoja atakuwa wa aina yake kama Nilivyowaweka. Ninaamua mwisho wa kila mwanadamu si kwa kuzingatia umri, ukubwa, kiwango cha mateso au kwa kiwango cha chini sana, kiwango cha huzuni bali ni kwa kuangalia kama ana ukweli ndani yake. Hakuna chaguo lingine ila hili tu. Ni sharti mjue kwamba wale wote ambao hawatimizi mapenzi ya Mungu wataadhibiwa. Huu ndio ukweli usiobadilika. Kwa hivyo, wale wote wanaoadhibiwa wanaadhibiwa kwa ajili ya haki ya Mungu na malipo kwa vitendo vyao viovu. Sijafanya mabadiliko yoyote katika mpango Wangu tangu kuuanzisha. Ni vile tu, kwa binadamu, wale ambao kwao Mimi huelekeza maneno Yangu wamepungua kwa idadi, kadhalika wale Ninaowakubali kwa dhati. Hata hivyo, Ninasisitiza kwamba mpango Wangu haujawahi kubadilika; badala yake, ni imani na upendo wa mwanadamu ambao hubadilika daima, kufifia daima, kiasi kwamba upo uwezekano wa kila mwanadamu kubadilika kutoka kujipendekeza Kwangu hadi kufikia hali ya kunidharau au hata kunitoa maishani mwake kabisa. Mtazamo Wangu kwenu hautakuwa baridi wala moto hadi pale Nitakapochukizwa sana na hatimaye kuwaadhibu. Hata hivyo, katika siku ya adhabu, bado Nitawaona lakini nyinyi hamtaweza kuniona. Tayari Ninahisi kuwa maisha miongoni mwenu ni ya kuchosha na kuchusha, kwa hivyo ni wazi kuwa, Nimechagua mazingira tofauti Yangu kuishi ili Niepuke maneno yenu mabovu na tabia zenu mbaya ili muache kunitweza na kunifanya mjinga. Kabla Sijawaacha, Ninawasihi mjiepushe kufanya yale ambayo hayaambatani na kweli. Badala yake, mnafaa kufanya yale yote ambayo yanawapendeza watu wote na yana manufaa kwa binadamu wote na pia kwa mwisho wa safari yenu wenyewe, la sivyo, yule atakayeteseka katika maafa hatakuwa mwingine ila wewe.
Huruma Zangu ni kwa wale wanaonipenda Mimi na kujinyima wenyewe. Na adhabu inayoletwa kwa waovu ni thibitisho la tabia Yangu ya haki na zaidi sana, ushuhuda wa hasira Yangu. Msiba utakapokuja, njaa na baa litawakumba wale wanaopinga Mimi na watalia kwa uchungu. Wale wote ambao wametenda aina zote za dhambi katika miaka mingi kama wafuasi Wangu hawatakuwa bila hatia; daima, wao pia wataishi katika hali ya taharuki na woga kukiwepo na msiba ambao haujawahi kushuhudiwa katika enzi zote zilizopita. Na wafuasi Wangu wote ambao hawakuwa wakimtii mwingine yeyote yule ila mimi watafurahi na kushangilia ukuu Wangu. Watakuwa na uridhisho usio na kifani na kuishi kwa raha ambayo sijawahi mpa mwanadamu. Kwa sababu Ninathamini matendo mema ya mwanadamu na kuchukia maovu yao. Tangu Nilipoanza kumwongoza mwanadamu, Nimekuwa Nikitamani kupata kikundi cha wanadamu ambao wanafikiria kama Mimi. Na sijawahi kuwasahau wale ambao hawana fikira sawa na Zangu; Nimewachukia sana moyoni Mwangu, Nikisubiri tu nafasi kutoa adhabu kwa hao waovu na kufurahia hilo. Siku Yangu tayari imefika na siwezi kusubiri zaidi!
Kazi Yangu ya mwisho si kumwadhibu mwanadamu tu bali pia kupanga hatima ya mwanadamu. Aidha, kazi Yangu ni kupokea shukrani kutoka kwa kila mtu kwa yale yote ambayo Nimefanya. Ninataka kila mtu aone kwamba yale yote niliyofanya ni sahihi na ni dhihirisho la tabia Yangu; si kwa uwezo wa mwanadamu, wala nguvu za asili, ambao ulimleta mwanadamu. Kinyume na hili, mimi Ndiye ambaye Ninalisha kila kiumbe miongoni mwa vitu vyote. Bila uwepo Wangu, mwanadamu anaweza tu kuangamia na kusumbuka kutokana na mashambulizi ya misiba. Hamna yeyote atakayeona uzuri wa jua na mwezi au dunia ya kijani kibichi; mwanadamu atakumbana tu na usiku wenye baridi na bonde lisiloepukika la uvuli wa mauti. Mimi tu Ndiye wokovu wa pekee wa mwanadamu. Mimi tu ndiye tumaini la pekee mwanadamu na zaidi ya hayo; Mimi tu Ndiye mwamba wa uwepo wa mwanadamu. Bila Mimi, mwanadamu atasimama mara moja. Bila mimi, mwanadamu atakumbana na msiba mkuu huku akikanyagwa na mapepo, hata kama hamna anayenisikiliza. Nimefanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na yeyote yule ila mimi Nikiwa na matumaini kwamba mwanadamu atanilipa kwa kutenda mema. Ingawa wachache wanaweza kunilipa, bado Nahitimisha safari Yangu duniani na Nianze kazi ambayo itatokea baada ya hapa, kwa sababu safari Yangu miongoni mwa wanadamu kwa miaka hii mingi imekuwa na matokeo mazuri, na Nimefurahishwa sana. Sijali sana kuhusu idadi ya watu ila kuhusu matendo yao mazuri. Kwa hali yoyote ile, Ninatumaini kwamba mtatenda mema huku mkijitayarisha kuuona mwisho wa safari yenu. Huu ndio wakati Nitakaporidhika; la sivyo, hakuna yeyote miongoni mwenu atayeepuka maafa. Maafa haya yatatekelezwa Nami na ni wazi kwamba Mimi ndiye Niliyeyapanga. Ikiwa hamtaweza kutenda kwa Wema mbele Yangu, hamtaweza kuyaepuka maafa. Wakati wa majonzi, vitendo vyenu havikuwa vinafaa kabisa, kwa sababu imani na upendo wenu vilikuwa tupu, na ulionyesha tu woga au hali yenu ya uthabiti. Kwa mintarafu hii, Nitafanya hukumu ya mazuri au mabaya. Shaka Yangu inaendelea kuhusu vitendo na tabia zenu ambazo Nitatumia kufanya uamuzi kuhusu hatima yenu. Hata hivyo, ni sharti Niseme wazi kwamba sitawahurumia wale ambao hawakuwa waaminifu Kwangu kabisa wakati wa majonzi, kwa sababu huruma Yangu ina mipaka. Zaidi ya hayo, Simpendi yeyote yule ambaye amewahi kunisaliti Mimi, wala Nisingependa kujihusisha na wale ambao hawawajali wenzao. Bila kujali ni nani, hii ndiyo tabia Yangu. Ni lazima Niwaambie hili: Wowote watakaouhuzunisha moyo Wangu hataweza kupokea huruma Yangu tena, na wowote ambao wamekuwa waaminifu watadumu moyoni Mwangu milele.
kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili 
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni