Smiley face

Jumamosi, 25 Novemba 2017

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III(Sehemu ya Pili )


Mwenyezi Mungu alisema: Tumezungumza tu kuhusu kazi yote ambayo Mungu amekamilisha, misururu ya mambo Aliyoyafanya kwa mara ya kwanza. Kila mojawapo ya mambo haya yanahusiana na mpango wa Mungu wa usimamizi na mapenzi ya Mungu. Yanahusiana pia na tabia binafsi ya Mungu na kiini Chake. Kama tunataka kuelewa bora zaidi kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho, hatuwezi kukoma katika Agano la Kale au katika Enzi ya Sheria, lakini tunahitaji kusonga mbele pamoja na hatua ambazo Mungu alichukua katika kazi Yake. Hivyo basi, Mungu alipotamatisha Enzi ya Sheria na kuanza Enzi ya Neema, hatua zetu binafsi zimefika katika Enzi ya Neema—enzi iliyojaa neema na ukombozi. Katika enzi hii, Mungu tena Alifanya kitu cha muhimu sana kwa mara ya kwanza. Kazi katika enzi hii mpya kwa Mungu na hata kwa mwanadamu ilikuwa sehemu mpya ya kuanzia. Sehemu hii mpya ya kuanzia ilikuwa tena kazi mpya ambayo Mungu alifanya kwa mara ya kwanza. Kazi hii mpya ilikuwa kitu ambacho hakikuwahi kutokea awali ambacho Mungu alitekeleza na hakikufikirika na binadamu na viumbe vyote. Ni kitu ambacho kwa sasa kinajulikana kwa watu wote—hii ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza Mungu aligeuka kuwa binadamu, mara ya kwanza Alianza kazi mpya kwa umbo la binadamu, Akiwa na utambulisho wa mwanamume. Kazi hii mpya ilionyesha kwamba Mungu alikuwa Amekamilisha kazi Yake katika Enzi ya Sheria, kwamba Asingefanya au kusema tena chochote chini ya sheria. Wala Asingewahi tena kuzungumza au kufanya chochote kwa mfano wa sheria au kulingana na kanuni au masharti ya sheria. Yaani, kazi Yake yote inayotokana na sheria ilisitishwa milele na isingeendelezwa, kwa sababu Mungu alitaka kuanza kazi mpya na kufanya mambo mapya, na mpango Wake kwa mara nyingine tena ulikuwa na sehemu mpya ya kuanzia. Hivyo basi, Mungu lazima Angemwongoza binadamu hadi katika enzi inayofuata.

Kama hii ilikuwa habari ya shangwe au ya kisirani kwa binadamu ilitegemea kiini chao kilikuwa kipi. Inaweza kusemekana kwamba hizi hazikuwa habari za shangwe, lakini zilikuwa habari za kisirani kwa baadhi ya watu, kwa sababu Mungu alipoanza kazi Yake mpya, watu hao ambao walifuata tu sheria na masharti, ambao walifuata tu kanuni lakini hawakumcha Mungu wangeegemea upande wa kutumia kazi nzee ya Mungu ili kuishutumu kazi Yake mpya. Kwa watu hawa, hizi zilikuwa habari za kisirani; lakini kwa kila mtu aliyekuwa hana hatia na aliyekuwa wazi, aliyekuwa mwenye ukweli kwa Mungu na aliyekuwa radhi kupokea ukombozi Wake, Mungu kuwa mwili kwa mara ya kwanza zilikuwa habari zenye shangwe sana. Kwani tangu kuwepo na binadamu, hii ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza Mungu kuonekana na kuishi miongoni mwa wanadamu katika umbo ambalo halikuwa Roho; badala yake, Alizaliwa na mwanadamu na kuishi miongoni mwa watu kama Mwana wa Adamu, na kufanya kazi katikati yao. Hii “mara ya kwanza” ilizivunja dhana za watu na pia ilikuwa zaidi ya kufikiria kote. Aidha, wafuasi wote wa Mungu walipata manufaa ya kushikika na kuonekana. Mungu hakuikomesha tu enzi nzee, lakini pia Alikomesha mbinu Zake za kale za kufanya kazi pamoja na mitindo ya kufanya kazi. Hakuruhusu tena wajumbe Wake kuwasilisha mapenzi Yake, na hakufichika tena katika mawingu na hakuonekana tena au kuongea kwa binadamu kupitia kwa ishara za amri kwa radi. Tofauti na chochote kile cha awali, kupitia kwa mbinu ambayo haikufirika kwa binadamu ambayo pia ilikuwa ngumu kwa wao kuelewa na kukubali—kupata mwili—Aligeuka na kuwa Mwana wa Adamu ili kuendeleza kazi ya enzi hiyo. Hatua hii iliwashangaza binadamu, na ikawa pia isiyo na utulivu kwao, kwa sababu Mungu kwa mara nyingine alikuwa ameanza kazi mpya ambayo Hakuwahi kufanya tena. Leo, tutaangalia ni kazi gani mpya ambayo Mungu alikamilisha katika enzi mpya, na katika haya yote ya kazi mpya, tabia ya Mungu nayo ilikuwa vipi, na nini Alicho nacho na kile Alicho ambayo tunaweza kuelewa?

Yafuatayo ni maneno yaliyorekodiwa katika Agano Jipya la Biblia.
1. Mat 12:1 Wakati huo katika siku ya Sabato Yesu alipitia mashamba ya nafaka; na wanafunzi wake walihisi njaa, nao wakaanza kung’oa masuke ya nafaka na kuyala.

2. Mat 12:6-8 Lakini nasema kwenu, Kwamba mahali humu yumo aliye mkubwa kuliliko hekalu. Lakini iwapo mngejua maana ya hili, Naitaka rehema, na siyo sadaka, msingewashutumu wale wasio na hatia. Kwa sababu Mwana wa Adamu ni Bwana hata wa siku ya Sabato.

Hebu kwanza tuangalie dondoo hii: “Wakati huo katika siku ya Sabato Yesu alipitia mashamba ya nafaka; na wanafunzi wake walihisi njaa, nao wakaanza kung’oa masuke ya nafaka na kuyala.”

Kwa nini tumeichagua dondoo hii? Dondoo hii ina uhusiano upi na tabia ya Mungu? Katika maandiko haya kitu cha kwanza tunachojua ni kwamba ilikuwa ni siku ya Sabato, lakini Bwana Yesu alipita kule nje na kuwaongoza wanafunzi Wake katika mashamba ya nafaka. Lakini zaidi “cha kufedhehesha” ni kwamba waliweza hata “wakaanza kung’oa masuke ya nafaka na kuyala.” Katika Enzi ya Sheria, sheria za Yehova Mungu zilikuwa kwamba watu wasingeweza kuenda vivi hivi tu au kushiriki katika shughuli katika siku ya Sabato—kulikuwa na mambo mengi ambayo hayangefanywa siku ya Sabato. Hatua hii ya Bwana Yesu ilikuwa ya kuchanganya hasa kwa wale waliokuwa wameishi chini ya sheria kwa muda mrefu, na iliweza hata kuchochea upinzani mkubwa. Kuhusiana na mchanganyiko wao na namna walivyouzungumzia kile ambacho Bwana Yesu alifanya, tutaweka hilo pembeni kwa sasa na kuzungumzia kwanza kwa nini Bwana Yesu alichagua kufanya hivi katika siku ya Sabato, kwa siku zote, na kile Alichotaka kuwasilisha kwa watu waliokuwa wakiishi katika enzi ya kale kupitia katika hatua hii. Huu ndio uhusiano kati ya dondoo hii na tabia ya Mungu ambayo Ningependa kuzungumzia.

Bwana Yesu alipokuja, Alitumia vitendo Vyake utendanji kuweza kuwasiliana na watu: Mungu alikuwa ameiondoa Enzi ya Sheria na alikuwa ameanza kazi mpya, na kazi hii mpya haikuhitaji uadhimisho wa Sabato; wakati Mungu alipotoka katika mipaka ya siku ya Sabato, hicho kilikuwa tu kionjo cha mapema cha kazi Yake mpya, na kwa kweli kazi Yake kubwa ilikuwa ikiendelea kujitokeza. Bwana Yesu aliopanza kazi Yake, tayari Alikuwa ameacha nyuma zile pingu za Enzi ya Sheria, na alikuwa ametupilia mbali zile taratibu na kanuni zilizokuwa za enzi hiyo. Ndani yake hakuwa na dalili za chochote kuhusiana na sheria; Alikuwa ameitupa nje mzima mzima na hakuifuata tena, na Hakuhitaji tena mwanadamu kuifuata. Kwa hivyo hapa unaona kwamba Bwana Yesu alipita katika mashamba siku ya Sabato; Bwana hakupumzika lakini, alikuwa akipita kule nje akifanya kazi. Hatua hii Yake ilikuwa ya kushtua kwa dhana za watu na iliweza kuwawasilishia ujumbe kwamba Hakuishi tena chini ya sheria na kwamba Alikuwa ameacha ile mipaka ya Sabato na kujitokeza mbele ya mwanadamu na katikati yao katika taswira mpya, huku akiwa na njia mpya ya kufanya kazi. Hatua hii Yake iliwaambia watu kwamba Alikuwa ameleta pamoja naye kazi mpya iliyoanza kwa kwenda nje ya sheria na kwenda nje ya Sabato. Wakati Mungu alitekeleza kazi Yake mpya, Hakushikilia tena ya kale, na Hakujali tena kuhusu taratibu za Enzi ya Sheria. Wala Hakuathirika na kazi Yake mwenyewe katika enzi ya awali, lakini Alifanya kazi kwa kawaida katika siku ya Sabato na wakati wanafunzi Wake waliona njaa, waliweza kuvunja masuke na wakala. Haya yote yalikuwa kawaida sana machoni mwa Mungu. Mungu angeweza kuwa na mwanzo mpya kwa nyingi za kazi Anazotaka kufanya na mambo Anayotaka kusema. Punde Anapokuwa na mwanzo mpya, Hataji kazi Yake ya awali tena wala kuiendeleza. Kwani Mungu anazo kanuni Zake katika kazi Yake. Anapotaka kuanzisha kazi mpya, ndipo Anapotaka kumleta mwanadamu katika awamu mpya ya kazi Yake, na wakati kazi Yake imeingia katika awamu ya juu zaidi. Kama watu wanaendelea kutenda kulingana na misemo au taratibu za kale au kuendelea kushikilia kabisa kwazo, Hatakumbuka au kulisifu jambo hili. Hii ni kwa sababu tayari Ameileta kazi mpya, na ameingia katika awamu mpya ya kazi Yake. Anapoanzisha kazi mpya, Anaonekana kwa mwanadamu akiwa na taswira mpya kabisa, kutoka katika mtazamo mpya kabisa, na kwa njia mpya kabisa ili watu waweze kuona dhana zile tofauti za tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho. Hii ni mojawapo ya malengo Yake katika kazi Yake mpya. Mungu hashikilii ya kale au kutumia njia isiyotumika na wengi; Anapofanya kazi na kuongea sio njia ya kutilia mipaka kama vile watu wanavyofikiria. Ndani ya Mungu, vyote ni huru na vimekombolewa, na hakuna hali ya kukinga, hakuna vizuizi—kile Anachomletea mwanadamu vyote ni uhuru na ukombozi. Yeye ni Mungu aliye hai, Mungu ambaye kwa kweli, na kwa hakika yupo. Yeye si kikaragosi au sanamu ya udongo, na Yeye ni tofauti kabisa na sanamu ambazo watu huhifadhi na kuabudu. Yeye yuko hai na mwenye nguvu na kile ambacho maneno Yake na kazi Yake humletea binadamu vyote ni uzima na nuru, uhuru na ukombozi wote, kwa sababu Yeye anashikilia ukweli, uzima, na njia—Yeye hajazuiliwa na chochote katika kazi yoyote Yake. Bila kujali watu wanavyosema na namna wanavyoona au kukadiria kazi Yake mpya, Ataitekeleza kazi Yake bila kusita. Hatakuwa na wasiwasi kuhusu dhana zozote za yeyote au kazi na maneno Yake kuelekezewa vidole, au hata upinzani wao mkubwa katika kazi Yake mpya. Hakuna yeyote miongoni mwa viumbe vyote anayeweza kutumia akili ya binadamu, au kufikiria kwa binadamu, maarifa au maadili ya binadamu kupima au kufasili kile ambacho Mungu anafanya, kutia fedheha, au kutatiza au kukwamiza kazi Yake. Hakuna kizuizi chochote katika kazi Yake na kile Anachokifanya, na haitawekewa kizuizi chochote na binadamu yeyote, kitu chochote, au kifaa chochote, na haitakatizwa na nguvu zozote za kikatili. Katika kazi Yake mpya, Yeye ni Mfalme anayeshinda daima, na nguvu zozote za kikatili na uvumi wote na hoja za uwongo zote kutoka kwa mwanadamu zimekanyagiwa chini ya kibao Chake cha kuwekea miguu. Haijalishi ni hatua gani mpya ya kazi Yake ambayo Anatekeleza, lazima iendelezwe na ipanuliwe katika mwanadamu, na lazima itekelezwe bila kuzuiliwa kote ulimwenguni mpaka pale ambapo kazi Yake kubwa imekamilika. Huu ndio uweza na hekima ya Mungu, na mamlaka na nguvu Zake. Hivyo basi, Bwana Yesu angeweza kwenda kule nje waziwazi na kufanya kazi katika siku ya Sabato kwa sababu ndani ya moyo Wake hakukuwa na sheria zozote, na hakukuwa na maarifa au kanuni zozote zilizotokana na binadamu. Kile Alichokuwa nacho kilikuwa ni kazi mpya ya Mungu na njia Yake, na kazi Yake ndio iliyokuwa njia ya kumweka huru mwanadamu, kumwachilia, kumruhusu kuwepo katika nuru na kumruhusu kuishi. Na wale wanaoabudu sanamu au miungu ya uwongo wanaishi kila siku wakiwa wamefungwa na Shetani, wakiwa wamezuiliwa na aina zote za sheria na mila—leo kitu kimoja hakiruhusiwi, kesho kingine—hakuna uhuru katika maisha yao. Wao ni sawa na wafungwa katika pingu wasio na shangwe ya kuzungumzia. “Kuzuiliwa” linawakilisha nini? Linawakilisha shurutisho, utumwa na uovu. Punde tu mtu anapoabudu sanamu, anaabudu mungu wa uwongo, akimwabudu roho wa uovu. Kuzuiliwa kunaenda sambamba na hilo. Huwezi kula hiki au kile, leo huwezi kwenda nje, kesho huwezi kuwasha jiko lako, siku inayofuata huwezi kuhamia katika nyumba mpya, siku fulani lazima zichaguliwe kwa minajili ya harusi na mazishi, na hata za wakati wa kujifungua mtoto. Haya yote yanaitwa nini? Haya yanaitwa kuzuiliwa; ni utumwa wa mwanadamu, na ndizo pingu za maisha za Shetani na roho wa maovu wanaowadhibiti, na wanaozuilia mioyo yao na mili yao. Je, kuzuiliwa huku kunapatikana kwa Mungu? Tunapozungumzia utakatifu wa Mungu, unafaa kwanza kufikira haya: Kwa Mungu hakuna vizuizi. Mungu anazo kanuni katika maneno na kazi Yake, lakini hakuna kuzuiliwa, kwa sababu Mungu Mwenyewe ndiye ukweli, njia na uzima.

Sasa hebu tuangalie dondoo ifuatayo: “Lakini nasema kwenu, Kwamba mahali humu yumo aliye mkubwa kuliliko hekalu. Lakini iwapo mngejua maana ya hili, Naitaka rehema, na siyo sadaka, msingewashutumu wale wasio na hatia. Kwa sababu Mwana wa Adamu ni Bwana hata wa siku ya sabato” (Mat 12:6-8). “Hekalu” hapa linamaanisha nini? Kwa ufupi, “hekalu” linaashiria jengo refu la kupendeza, na katika Enzi ya Sheria, hekalu lilikuwa ni pahali pa makuhani kumwabudu Mungu. Bwana Yesu aliposema “mahali humu yumo aliye mkubwa kuliliko hekalu,” “mmoja” ilikuwa ikirejelea nani? Ni wazi, “mmoja” ni Bwana Yesu katika mwili kwa sababu Yeye tu ndiye aliyekuwa mkuu kuliko hekalu. Na maneno hayo yaliwaambia watu nini? Yaliwaambia watu watoke hekaluni—Mungu alikuwa tayari ameshatoka nje na hakuwa tena akifanyia kazi ndani yake, hivyo basi watu wanafaa kutafuta nyayo za Mungu nje ya hekalu na kufuata nyayo Zake katika kazi Yake mpya. Usuli wa Bwana Yesu kusema haya ilikuwa kwamba chini ya sheria, watu walikuwa wameiona hekalu kama kitu kilichokuwa kikuu zaidi kuliko Mungu Mwenyewe. Yaani, watu waliliabudu hekalu badala ya kumwabudu Mungu, hivyo basi Bwana Yesu akawaonya kutoabudu sanamu, lakini kumwabudu Mungu kwa sababu Yeye ndiye mwenye mamlaka ya juu zaidi. Hivyo basi, alisema: “Naitaka rehema, na siyo sadaka.” Ni wazi kwamba katika macho ya Bwana Yesu, watu wengi sana katika sheria hawakumwabudu tena Yehova Mungu, lakini walikuwa tu wakipitia mchakato wa kutoa sadaka na Bwana Yesu aliamua kwamba mchakato huu ulikuwa ibada ya sanamu. Waabudu sanamu hawa waliliona hekalu kama kitu kikuu, cha juu zaidi kuliko Mungu. Ndani ya mioyo yao kulikuwa tu na hekalu, wala si Mungu, na kama wangelipoteza hekalu, wangepoteza mahali pao pa kukaa. Bila ya hekalu hawakuwa na mahali popote pa kuabudu na wasingeweza kutoa sadaka zao. Mahali pao pa kukaa kama palivyojulikana ndipo walipofanyia shughuli zao kwa jina la kumwabudu Yehova Mungu, na hivyo basi wakaruhusiwa kuishi katika hekalu na kutekeleza shughuli zao binafsi. Ule utoaji sadaka wao kama ulivyojulikana ulikuwa tu kutekeleza shughuli zao za kibinafsi za aibu wakisingizia kwamba walikuwa wanaendesha ibada yao katika hekalu. Hii ndiyo iliyokuwa sababu iliyowafanya watu wakati huo kuliona hekalu kuwa kuu kuliko Mungu. Kwa sababu walilitumia hekalu kama maficho, na sadaka kama kisingizio cha kuwadanganya watu na kumdanganya Mungu, Bwana Yesu alisema haya ili kuwaonya watu. Mkitumia maneno haya kwa wakati wa sasa, yangali bado halali na yenye umuhimu sawa. Ingawa watu wa leo wameweza kupitia kazi tofauti za Mungu kuliko watu wa Enzi ya Sheria walivyowahi kupitia, kiini cha asili yao ni kile kile. Katika muktadha wa kazi leo, watu bado watafanya aina sawa ya mambo kama yale ya “hekalu kuwa kuu kuliko Mungu”. Kwa mfano, watu huona kutimiza wajibu wao kama kazi yao; wanaona kutoa ushuhuda kwa Mungu na kupigana na joka kubwa jekundu kama harakati ya kisiasa ya kulinda haki za kibanadamu, kwa ajili ya demokrasia na uhuru; wao hugeuza wajibu wao ili kutumia weledi wao kuwa ajira, lakini wanachukulia kumcha Mungu na kujiepusha na maovu tu kama kipande cha kanuni ya kidini ya kufuatwa; na kadhalika. Je, maonyesho haya kwa upande wa binadamu hasa hayako sawa na “hekalu ni kuu kumliko Mungu”? Isipokuwa tu kwamba miaka elfu mbili iliyopita, watu walikuwa wakiendeleza shughuli zao za kibinafsi katika hekalu linaloshikika, lakini leo, watu wanaendeleza shughuli zao za kibinafsi katika mahekalu yasiyogusika. Wale watu wanaothamini masharti huona masharti kuwa kuu zaidi kuliko Mungu, wale watu wanaopenda hadhi huona hadhi kuu zaidi kuliko Mungu, wale watu wanaopenda ajira zao huziona ajira hizo kuwa kuu zaidi kuliko Mungu na kadhalika—maonyesho yao yote yananifanya Mimi kusema: “Watu humsifu Mungu kuwa ndiye mkuu zaidi kupitia kwa maneno yao, lakini kwa macho yao kila kitu ni kikuu zaidi kuliko Mungu.” Hii ni kwa sababu punde tu watu wanapopata fursa katika njia yao ya kumfuata Mungu ili kuonyesha vipaji vyao, au kuendelea na shughuli zao binafsi za kibiashara au ajira yao binafsi, wanakuwa mbali na Mungu na kufanya kwa bidii ajira wanayoipenda. Kuhusiana na kile ambacho Mungu amewaaminia, na mapenzi Yake, mambo hayo yote yametupiliwa mbali kitambo. Katika hali hii, ni nini tofauti baina ya watu hawa na wale wanaoendesha biashara zao katika hekalu miaka elfu mbili iliyopita?

Kisha, hebu tuangalie sentensi ya mwisho katika dondoo hii ya maandiko: “Kwa sababu Mwana wa Adamu ni Bwana hata wa siku ya Sabato.” Je, kunao upande wa utendaji kwa sentensi hii? Je, unaweza kuona upande wa utendaji kwa sentensi hii? Kila kitu anachosema Mungu kinatoka moyoni Mwake, kwa hivyo kwa nini Alisema hivi? Unaielewa vipi sentensi hii? Unaweza kuelewa maana ya sentensi hii sasa, lakini wakati huo si watu wengi walikuwa wanaielewa kwa sababu binadamu alikuwa tu ametoka katika Enzi ya Sheria. Kwao, kutoka katika Sabato lilikuwa jambo gumu sana kufanya, sembuse kuelewa Sabato ya kweli ilikuwa nini.

Sentensi “Mwana wa Adamu ni Bwana hata wa siku ya Sabato.” inawaambia watu kwamba kila kitu cha Mungu ni visivyo vya mwili, na ingawa Mungu anaweza kukupa mahitaji yako yote ya kimwili, punde tu mahitaji yako yote ya mwili yametimizwa, utoshelevu unaotokana na mambo haya unaweza kuchukua nafasi ya ufuatiliaji wako wa ukweli? Kwa kweli hiyo haiwezekani! Tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho ambayo tumeweza kushiriki pamoja ni kweli. Haiwezi kupimwa kupitia kwa gharama ya juu ya vifaa vya kimwili wala thamani yake kupimwa kwa pesa, kwa sababu si kifaa cha anasa, na kinatoa mahitaji ya moyo wa kila mmoja. Kwa kila mmoja, thamani ya ukweli huu usioshikika inafaa kuwa kubwa zaidi kuliko thamani ya vitu vyovyote vya anasa unavyofikiria kuwa ni vizuri, sivyo? Kauli hii ni kitu mnachohitaji kukiwazia. Hoja kuu ya kile nilichosema ni kwamba kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho na kila kitu cha Mungu ndivyo vitu muhimu zaidi kwa kila mtu na haviwezi kubadilishwa na kifaa chochote cha anasa. Nitakupa mfano: Ukiwa na njaa, unahitaji chakula. Chakula hiki kinaweza kuwa kizuri kwa kiasi fulani au kinaweza kuwa kimekosa kitu fulani kwa kiasi fulani, lakini mradi tu umekula ukashiba, hisia ile mbaya ya kuwa na njaa haitakuwepo tena—itakuwa imeondoka. Unaweza kuketi pale kwa amani, na mwili wako utakuwa umepumzika. Njaa ya watu inaweza kutatuliwa kwa chakula, lakini ukiwa unamfuata Mungu na kuhisi kwamba huna ufahamu wowote Wake, unawezaje kutatua utupu huu katika moyo wako? Hali hii inaweza kusuluhishwa kwa chakula? Au unapomfuata Mungu na huelewi mapenzi Yake, ni nini unachoweza kutumia ili kufidia ile njaa katika moyo wako? Katika mchakato wa uzoefu wako wa wokovu kupitia kwa Mungu, wakati ukifuatilia mabadiliko katika tabia yako, kama huelewi mapenzi Yake au hujui ukweli ni nini, kama huelewi tabia ya Mungu, huhisi wasiwasi sana? Huhisi njaa na kiu kuu katika moyo wako? Je, hizi hisia hazikuzuii dhidi ya kuhisi pumziko katika moyo wako? Hivyo basi unaweza kufidia vipi njaa hiyo katika moyo wako—kunayo njia ya kutatua suala hilo? Baadhi ya watu huenda kufanya ununuzi, baadhi hupata rafiki wa kuwaambia yaliyo moyoni, baadhi hulala mpaka watosheke, wengine husoma zaidi maneno ya Mungu, au wakatia bidii zaidi na kutumia jitihada nyingi zaidi kukamilisha wajibu wao. Je, mambo haya yanaweza kutatua ugumu wako halisi? Nyinyi nyote mnaelewa kikamilifu aina hizi za mazoea. Unapohisi kuwa huna nguvu, unapohisi tamanio kubwa la kupata nuru kutoka kwa Mungu ili kukuruhusu kujua uhalisi wa ukweli na mapenzi Yake, ni nini unachohitaji kingi zaidi? Kile unachohitaji si mlo kamili, na wala si maneno machache mema. Zaidi ya hayo, si lile tulizo na kutosheka kwa muda kwa mwili—kile unachohitaji ni Mungu kuweza kukueleza moja kwa moja, kwa wazi kile unachofaa kufanya na namna unavyofaa kukifanya, kuweza kukuonyesha wazi ukweli ni nini. Baada ya kuelewa haya, hata kama ni sehemu ndogo tu, huhisi kuwa umetosheka zaidi katika moyo wako kuliko vile ambavyo ungekuwa umekula mlo mzuri? Wakati moyo wako umetosheka, huo moyo wako, nafsi yako nzima, havipati pumziko la kweli? Kutokana na mfano huu na uchambuzi, je, mnaelewa sasa ni kwa nini Nilitaka kusemezana na nyinyi kuhusu sentensi hii, “Mwana wa Adamu ni Bwana hata wa siku ya Sabato”? Maana yake ni kwamba kile kinachotoka kwa Mungu, kile Alicho nacho na kile Alicho, na kila kitu Chake vyote ni vikuu zaidi kuliko kitu kingine chochote, kikiwemo kile kitu au yule mtu ambaye uliwahi kuamini kuwa unamthamini zaidi. Hivyo ni kusema, kama mtu hawezi kupata maneno kutoka katika kinywa cha Mungu au kama haelewi mapenzi Yake, hawezi kupata pumziko. Katika yale mtakayopitia katika siku zako za usoni, mtaelewa ni kwa nini Nilitaka nyinyi kuona dondoo hii leo—hii ni muhimu sana. Kila kitu ambacho Mungu anafanya ni ukweli na maisha. Ukweli kwa mwanadamu ni kitu ambacho hawawezi kukosa katika maisha yao, kitu ambacho hawawezi kuishi bila; unaweza pia kusema kwamba ndicho kitu kikuu zaidi. Ingawa huwezi kukiangalia au kukigusa, umuhimu wake kwako hauwezi kupuuzwa; ndicho kitu cha pekee kinachoweza kukuletea pumziko moyoni mwako.

Je, ufahamu wenu wa ukweli umefungamana na hali yenu ya kibinafsi? Katika maisha halisi, lazima kwanza ufikirie ukweli upi unahusiana na watu, vitu, na vifaa ambavyo umekumbana navyo; ni miongoni mwa ukweli huu ndimo unaweza kupata mapenzi ya Mungu na kuunganisha kile ulichokumbana nacho na mapenzi Yake. Kama hujui ni vipengele vipi vya ukweli vinavyohusiana na mambo uliyokumbana nayo lakini unaenda kwa njia ya moja kwa moja kutafuta mapenzi ya Mungu, mtazamo huu hauna mwelekeo kwa kiasi fulani na hauwezi kufanikisha matokeo. Kama unataka kutafuta ukweli na kuelewa mapenzi ya Mungu, kwanza unahitaji kuangalia ni mambo ya aina gani ambayo umekumbana nayo, ni vipengele vipi vya ukweli ambavyo mambo hayo yanauhusiano navyo, na kisha uutafute ukweli katika neno la Mungu ambalo linahusiana na kile ulichopitia. Kisha utafute njia ya matendo sahihi kwako katika ukweli huo; kwa njia hii unaweza kupata ufahamu usio wa moja kwa moja kuhusu mapenzi ya Mungu. Kutafuta na kutenda ukweli si kutumia kanuni au kufuata fomyula bila kufikiria. Ukweli si wa kifomyula, wala si sheria. Haujakufa—ni maisha, ni kitu kilicho na uhai, na ni kanuni ambayo lazima kiumbe kifuate na kanuni ambayo lazima mwanadamu awe nayo katika maisha yake. Hiki ni kitu ambacho lazima uelewe zaidi kutoka kwa uzoefu. Haijalishi ni katika awamu gani ambayo umeifikia katika uzoefu wako, huwezi kutenganishwa na neno la Mungu au ukweli, na kile unachoelewa kuhusu tabia ya Mungu na kile unachojua kuhusu kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho ni vitu ambavyo vimeonyeshwa vyote katika maneno ya Mungu; vimeungana kabisa na ule ukweli. Tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho vyenyewe ni ukweli; ukweli ni dhihirisho halisi la tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho. Unafanya kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho kuwa thabiti na kukionyesha waziwazi; unakuonyesha moja kwa moja kile ambacho Mungu anapenda, kile ambacho Hapendi, kile Anachokutaka ufanye na kile ambacho Hakuruhusu ufanye, ni watu wapi Anaowadharau na ni watu wapi Anaowafurahia. Katika ule ukweli ambao Mungu anaonyesha watu wanaweza kuona furaha, hasira, huzuni, na shangwe Yake, pamoja na kiini Chake—huu ndio ufichuzi wa tabia Yake. Mbali na kujua kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho, na kuelewa tabia Yake kutoka katika neno Lake, kile kilicho muhimu zaidi ni haja ya kufikia ufahamu huu kupitia kwa uzoefu wa kimatendo. Kama mtu atajiondoa katika maisha halisi ili kumjua Mungu, hataweza kutimiza hayo. Hata kama kuna watu wanaoweza kupata ufahamu fulani kutoka katika neno la Mungu, ufahamu huo umewekewa mipaka ya nadharia na maneno, na kuna tofauti na vile ambavyo Mungu alivyo kwa kweli.

Kile tunachozungumzia sasa kimo ndani ya ule upana wa hadithi zilizorekodiwa katika Biblia. Kupitia katika hadithi hizi, na kupitia uchambuzi wa mambo haya yaliyofanyika, watu wanaweza kuelewa tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho ambayo Ameonyesha, na kuwaruhusu kujua kila kipengele cha Mungu kwa upana zaidi, kwa kina zaidi, kikamilifu, na kwa undani zaidi. Hivyo basi, njia pekee ya kujua kila kipengele cha Mungu ni kupitia hadithi hizi? La, siyo! Kwani kile Mungu anachosema na kazi Anayofanya katika Enzi ya Ufalme kinaweza kuwasaidia watu kwa njia bora zaidi kujua tabia Yake, na kuijua kikamilifu. Hata hivyo, Nafikiri ni rahisi zaidi kujua tabia ya Mungu na kuelewa kile Alicho nacho na kile Alicho kupitia baadhi ya mifano au hadithi zilizorekodiwa katika Biblia ambazo watu wamezoeana nazo. Nikichukua maneno ya hukumu na kuadibu na ukweli ambao Mungu anaonyesha leo ili kukufanya umjua Yeye neno kwa neno, utahisi kwamba haipendezi inachosha mno, na baadhi ya watu hata watahisi kwamba maneno ya Mungu yanaonekana kuwa yanafuata fomyula fulani. Lakini tukichukulia hadithi hizi za Biblia kama mifano ya kuwasaidia watu kujua tabia ya Mungu, basi haitaonekana kuwa ya kuchosha. Unaweza kusema kwamba katika mkondo wa kuonyesha mifano hii, maelezo ya kile kilichokuwa moyoni mwa Mungu wakati huo—hali Yake ya moyo au hisia Zake za moyoni, au fikira na mawazo Yake—vimesimuliwa kwa watu katika lugha za kibinadamu, na lengo la haya yote ni kuwaruhusu kushukuru, kuhisi kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho na kujua kwamba si fomula. Si hadithi ya kale, au kitu ambacho watu hawawezi kuona wala kugusa. Ni kitu ambacho kwa kweli kipo ambacho watu wanaweza kuhisi, na kufahamu. Hili ndilo lengo la msingi. Unaweza kusema kwamba watu wanaoishi katika enzi hii wamebarikiwa. Wanaweza kuzitumia hadithi za Biblia kupata ufahamu mpana zaidi wa kazi za awali za Mungu; wanaweza kuiona tabia Yake kupitia katika kazi ambayo Amefanya. Na wanaweza kuelewa mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu kupitia kwa tabia hizi ambazo Ameonyesha, kuelewa maonyesho yale thabiti ya utakatifu Wake na utunzaji Wake kwa binadamu ili kuweza kufikia maelezo zaidi na maarifa ya kina zaidi kuhusu tabia ya Mungu. Naamini kwamba nyinyi nyote mnaweza kuhisi haya yote!

Ndani ya upana wa kazi ambayo Bwana Yesu alikamilisha katika Enzi ya Neema, unaweza kuona kipengele kingine cha kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho. Kilionyeshwa kupitia kwa mwili Wake, na kikawezeshwa kwa watu kuiona na kufahamu zaidi kupitia kwa ubinadamu Wake. Ndani ya Mwana wa Adamu, watu waliweza kuona namna ambavyo Mungu katika mwili alivyoishi kwa kudhihirisha ubinadamu Wake, na wakaona uungu wa Mungu ulioonyeshwa kupitia kwa mwili. Aina hizi mbili za maonyesho ziliwaruhusu watu kuweza kumwona Mungu aliye halisi sana, na kuwaruhusu kuwa na dhana tofauti ya Mungu. Hata hivyo, katika kipindi cha muda kati ya uumbaji wa ulimwengu na mwisho wa Enzi ya Sheria, yaani, kabla ya Enzi ya Neema, kile kilichoonekana, kilichosikizwa, na kupitiwa na watu kilikuwa tu kipengele kitakatifu cha Mungu. Kilikuwa kile ambacho Mungu alifanya na kusema katika himaya ile isiyoshikika, na mambo ambayo Aliyaonyesha kutoka katika nafsi Yake halisi ambayo yasingeweza kuonekana au kuguswa. Mara nyingi, mambo haya yaliwafanya watu kuhisi kwamba Mungu alikuwa mkubwa sana, na kwamba wasingeweza kusonga karibu na Yeye. Picha ambayo Mungu kwa kawaida aliwapa watu ilikuwa kwamba Alionekana akipotea, na watu walihisi hata kwamba kila mojawapo ya fikira na mawazo Yake yalikuwa yenye mafumbo mno na yasiyoeleweka mno kiasi kwamba hakukuwa na njia ya kuyafikia, isitoshe hata kujaribu kuelewa na kuyashukuru. Kwa watu, kila kitu kuhusu Mungu kilikuwa cha mbali—mbali mno kiasi kwamba watu wasingeweza kukiona, wasingeweza kukigusa. Ilionekana Alikuwa juu katika mbingu, na ilionekana kwamba Hakukuwepo kamwe. Hivyo basi kwa watu, kuelewa moyo na akili ya Mungu au kufikiria Kwake kokote kusingeweza kutimizika, na hata kufikika. Ingawa Mungu alitenda kazi fulani thabiti katika Enzi ya Sheria, na Akaweza kutoa pia maneno fulani na kuonyesha tabia fulani mahususi ili kuwaruhusu watu kushukuru na kuona maarifa halisi fulani kumhusu, bado hatimaye, hilo lilikuwa ni maonyesho ya Mungu kuhusu Alicho nacho na kile Alicho katika ulimwengu usioshikika, na kile watu walielewa, kile walichojua kilikuwa bado kile cha kipengele takatifu kuhusu kile Alicho nacho na kile Alicho. Mwanadamu asingeweza kupata dhana thabiti kutoka kwa[a] kile Alicho nacho na kile Alicho, na ile picha waliyokuwa nayo kuhusu Mungu ilikuwa bado ndani ya mawanda ya “Roho iliyo ngumu kukaribia, inayoonekana na kupotea.” Kwa sababu Mungu hakutumia kifaa mahususi au taswira katika ulimwengu wa kimwili kuonekana kwa watu, bado wasingeweza kumfafanua Yeye kwa kutumia lugha ya kibinadamu. Katika mioyo na akili za watu, siku zote walitaka kutumia lugha yao binafsi ili kuanzisha kiwango kwa ajili ya Mungu, kumfanya Agusike na kumfanya Awe binadamu, kama vile Alikuwa mrefu kiasi gani, Alikuwa mkubwa kiasi gani, Alifanana vipi, Anapenda nini hasa na hulka Yake mahususi ni gani. Kwa kweli, moyoni Mwake Mungu alijua kwamba watu walifikiria hivyo. Alikuwa wazi sana kuhusu mahitaji ya watu, na bila shaka Alijua pia kile Alichofaa kufanya, hivyo basi Alitenda kazi Yake kwa njia tofauti na Enzi ya Neema. Njia hii ilikuwa takatifu na vilevile iliyostaarabishwa. Katika kipindi cha Muda ambacho Bwana Yesu alikuwa akifanya kazi, watu wangeweza kuona kwamba Mungu alikuwa na maonyesho mengi ya kibinadamu. Kwa mfano, Aliweza kucheza, Aliweza kuhudhuria harusi, Aliweza kuwasiliana kwa karibu na watu, kuongea na wao, na kujadili mambo pamoja nao. Aidha, Bwana Yesu aliweza pia kukamilisha kazi nyingi zilizowakilisha uungu Wake, na bila shaka kazi Yake yote ilikuwa ni maonyesho na ufichuzi wa tabia ya Mungu. Katika kipindi hiki, wakati uungu wa Mungu ulitambuliwa kupitia kwa mwili wa kawaida ambao watu wangeweza kuona na kugusa, hawakuhisi tena kwamba Alikuwa akionekana na kutoweka, na kwamba wangeweza kumkaribia. Kinyume cha mambo ni kwamba, wangejaribu kuelewa mapenzi ya Mungu au kuuelewa uungu Wake kupitia kila hatua, maneno, na kazi ya Mwana wa Adamu. Mwana wa Adamu mwenye mwili alionyesha uungu wa Mungu kupitia kwa ubinadamu Wake na kuwasilisha mapenzi ya Mungu kwa binadamu. Na kupitia maonyesho ya mapenzi na tabia ya Mungu, Aliwafichulia watu yule Mungu asiyeweza kuonekana au kuguswa katika ulimwengu wa kiroho. Kile watu walichoona kilikuwa Mungu Mwenyewe, anayeshikika na aliye na mwili na mifupa. Hivyo basi Mwana wa Adamu mwenye mwili Alifanya mambo kama vile utambulisho binafsi wa Mungu, hadhi, taswira, tabia, na kile Alicho nacho na kile Alicho kuwa thabiti na kupewa picha ya binadamu. Ingawa sura ya nje ya Mwana wa Adamu ilikuwa na upungufu fulani kuhusiana na taswira ya Mungu, kiini Chake na kile Alicho nacho na kile Alicho yote hayo yaliweza kwa kikamilifu kuwakilisha utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu—kulikuwa tu na tofauti fulani katika jinsi ya maonyesho. Bila kujali kama ni ubinadamu wa Mwana wa Mungu au uungu Wake, hatuwezi kukana kwamba Aliwakilisha utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu mwenyewe. Katika kipindi hiki cha muda, hata hivyo, Mungu alifanya kazi kupitia mwili, Akaongea kutoka kwa mtazamo wa mwili, na kusimama mbele ya mwanadamu kwa utambulisho na hadhi ya Mwana wa Adamu, na hili liliwapa watu fursa ya kukumbana na kupitia maneno na kazi ya kweli ya Mungu miongoni mwa binadamu. Iliweza pia kuwaruhusu watu kuwa na utambuzi wa uungu Wake na ukubwa Wake katikati ya unyenyekevu, vilevile na kupata ufahamu wa mwanzo na ufafanuzi wa mwanzo wa uhalali na uhalisi wa Mungu. Hata ingawa kazi iliyokamilishwa na Bwana Yesu, njia Zake za kufanya kazi, na mitazamo ambayo kutoka kwayo Aliongea ilitofautiana na ile ya nafsi halisi ya Mungu katika ulimwengu wa kiroho, kila kitu kumhusu kilimwakilisha kwa kweli Mungu Mwenyewe ambaye binadamu walikuwa hawajawahi kumwona awali—hili haliwezi kukataliwa! Hivi ni kusema, haijalishi ni kwa umbo gani ambalo Mungu huonekana, haijalishi huongea kutoka katika mtazamo upi, au Yeye hukabiliana na binadamu kupitia kwa taswira gani, Mungu hawakilishi chochote isipokuwa Yeye Mwenyewe. Hawezi kumwakilisha binadamu yeyote—Hawezi kumwakilisha binadamu yeyote aliyepotoka. Mungu ni Mungu Mwenyewe, na hili haliwezi kukataliwa.
Julai 23, 2014
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni