Smiley face

Jumamosi, 15 Septemba 2018

Wimbo wa Maneno ya Mungu | Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,Mungu, Mungu




  • Wimbo wa Maneno ya Mungu
  • Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote
  • I
  • Kutoka unapoingia katika dunia hii ukilia,
  • unaanza kutenda wajibu wako.
  • Katika mpango na utaratibu wa Mungu,
  • unachukua nafasi yako,
  • na unaanza safari ya maisha.
  • Vyovyote vilivyo msingi wako
  • ama safari iliyo mbele yako,
  • hakuna anayeweza kuepuka utaratibu
  • na mpango ambao Mbingu imeweka,
  • na hakuna aliye na amri juu ya hatima yake,
  • kwani ni Yule tu anayetawala juu ya vitu vyote
  • ndiye ana uwezo wa kazi kama hii.
  • II
  • Tangu siku ambayo mwanadamu alikuja kuwepo
  • Mungu amekuwa imara katika kazi Yake,
  • Akisimamia ulimwengu huu na kuelekeza
  • mabadiliko na kusonga kwa vitu vyote.
  • Kama vitu vyote,
  • mwanadamu kwa kimya na bila kujua anapokea
  • uboreshaji wa utamu,
  • mvua na umande kutoka kwa Mungu.
  • Kama vitu vyote,
  • mwanadamu bila kujua anaishi chini
  • ya utaratibu wa mkono wa Mungu.
  • III
  • Moyo na roho ya mwanadamu
  • viko mkononi mwa Mungu,
  • na maisha yote ya mwanadamu yanatazamwa
  • machoni mwa Mungu.
  • Bila kujali kama unaamini katika hili ua la,
  • chochote na vitu vyote,
  • viishivyo au vilivyokufa,
  • vitageuka, vibadilike, vifanywe upya, na kupotea
  • kulingana na fikira za Mungu.
  • Hivi ndivyo Mungu hutawala juu ya vitu vyote.
  •  
  • kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
  •           Sikiliza zaidi: Nyimbo za Neno la Mungu 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni