Nyinyi nyote mna furaha kupokea tuzo mbele ya Mungu na kuwa walengwa wa fadhili Zake machoni Pake. Haya ni matakwa ya kila mtu baada ya yeye kuanza kuwa na imani kwa Mungu, kwani mwanadamu kwa moyo wake wote hujitahidi kupata mambo yaliyo juu na hakuna aliye tayari kubaki nyuma ya wengine. Hii ndiyo njia ya mwanadamu. Kwa sababu hii hasa, wengi kati yenu wanajaribu daima kujipendekeza kwa Mungu mbinguni, lakini kwa kweli, uaminifu wenu na uwazi kwa Mungu ni wa kiasi kidogo sana ukilinganishwa na uaminifu na uwazi wenu kwenu wenyewe. Mbona Nasema hivi? Kwa sababu Sikiri uaminifu wenu kwa Mungu kabisa, na zaidi Nakana kuwepo kwa Mungu aliye ndani ya mioyo yenu. Hiyo ni kusema, Mungu mnayemwabudu, Mungu asiye dhahiri mnayempenda, hayupo kabisa. Kinachonifanya niseme haya kwa uhakika ni kwamba mko mbali sana na Mungu wa kweli. Uaminifu mnaomiliki unatokana na kuwepo kwa sanamu mioyoni mwenu, na kunihusu Mimi, Mungu anayeonekana kama asiye mkubwa wala mdogo machoni penu, mnachofanya ni kunikiri kwa maneno tu. Ninaposema juu ya umbali wenu mkubwa kutoka kwa Mungu, Ninamaanisha jinsi mlivyo mbali sana na Mungu wa kweli, ilhali Mungu asiye dhahiri Anaonekana kuwa karibu. Nisemapo “asiye mkubwa,” inamaanisha jinsi Mungu mnayemwamini siku ya leo anaonekana tu kuwa mwanadamu asiye na uwezo mkubwa; mwanadamu asiye wa fahari sana. Na Nisemapo, “asiye mdogo,” inamaanisha kuwa ingawa mwanadamu huyu hawezi kuita upepo na kuamuru mvua, hata hivyo Anaweza kumwita Roho wa Mungu kufanya kazi inayotingisha mbingu na dunia, hivyo kumchanganya mwanadamu kabisa. Kwa nje, nyote mnaonekana kuwa watiifu sana kwa huyu Kristo aliye duniani, lakini kwa kiini hamna imani Kwake wala kumpenda. Ninachomaanisha ni kwamba yule mliye na imani kwake kwa kweli ni yule Mungu asiye dhahiri katika hisia zenu, na yule kweli mnayempenda ni Mungu mnayemtamani usiku na mchana, lakini bado hamjamwona kamwe kibinafsi. Na kuhusu huyu Kristo, imani yenu ni sehemu tu, na upendo wenu Kwake si kitu. Imani inamaanisha imani na kusadiki; upendo unamaanisha kusujudu na kusifu ndani ya mioyo yenu, bila kuondoka. Lakini imani yenu na upendo wenu kwa Kristo wa siku ya leo vimepunguka chini ya hili. Ikujapo kwa imani, mna imani Kwake jinsi gani? Ikujapo kwa upendo, mnampenda jinsi gani? Hamjui kabisa kuhusu tabia Yake, sembuse kiini Chake, hivyo ni jinsi gani kwamba mna imani Kwake? Uko wapi uhalisi wa imani yenu Kwake? Mnampenda jinsi gani? Uko wapi uhalisi wa upendo wenu Kwake?
Wengi wamenifuata bila kusita hadi leo, na katika miaka hii michache, nyote mmepitia uchovu mwingi. Nimefahamu vizuri tabia ya asili na mazoea ya kila mmoja wenu, na imekuwa vigumu sana kuingiliana nanyi. Cha kusikitisha ni kwamba ingawa nina maarifa nyingi kuwahusu, hamna ufahamu hata kidogo kunihusu. Sio ajabu wengine wanasema mlidanganywa na mwanadamu katika wakati wa mkanganyiko. Hakika, hamwelewi chochote kuhusu tabia Yangu, na hata zaidi hamwezi kufahamu yaliyo akilini Mwangu. Sasa ninyi kunielewa visivyo kunaongezeka haraka, na imani yenu Kwangu inabaki ile imani iliyokanganyika. Badala ya kusema kwamba mna imani na Mimi, ingekuwa bora kusema kwamba nyote mnajaribu kujipendekeza Kwangu na kunibembeleza. Nia zenu ni rahisi sana—yeyote anayeweza kunituza, nitamfuata, na yeyote anayeweza kuniwezesha kutoroka majanga makubwa, nitaamini kwake, awe Mungu ama Mungu fulani yeyote. Hakuna kati ya haya yanayonihusu. Kuna wanadamu wengi kama hao kati yenu, na hali hii ni nzito sana. Ikiwa siku moja, majaribio yatafanywa kuona ni wangapi kati yenu wanamwamini Kristo kwa sababu mna umaizi kuhusu kiini Chake, basi Nahofia kwamba hakuna mmoja wenu atakuwa na uwezo kufanya Ninavyotaka. Hivyo haitakuwa hoja kwa kila mmoja wenu kuzingatia swali hili: Mungu mliye na imani na Yeye ni tofauti sana na Mimi, na kwa hivyo, nini basi ni kiini cha imani yenu kwa Mungu? Kadri mnavyozidi kuamini katika mnayedai kuwa Mungu wenu, ndivyo mnavyozidi kupotea mbali sana nami. Basi, ni nini msingi wa suala hili? Nina uhakika hakuna mmoja wenu amewahi kufikiria suala hili, lakini mmefikiria uzito wake? Mmewaza kuhusu matokeo ya kuendelea na imani ya namna hii?
Sasa, matatizo yaliyowekwa mbele yenu ni mengi, na hakuna mmoja wenu aliye na uhodari wa kuleta ufumbuzi. Iwapo haya yataendelea, basi walio katika hatari ya kupoteza ni nyinyi wenyewe pekee. Nitawasaidia kuyatambua matatizo, lakini itabakia kwenu kupata ufumbuzi.
Nawathamini sana wale wasio na shaka kuhusu wengine na pia nawapenda sana wale wanaokubali ukweli kwa urahisi; kwa aina hizi mbili za wanadamu Ninaonyesha utunzaji mkubwa, kwani machoni Pangu wao ni waaminifu. Kama una udanganyifu mwingi, basi utakuwa na moyo wenye hadhari na mawazo ya shaka juu ya mambo yote na wanadamu wote. Kwa sababu hii, imani yako Kwangu inajengwa kwa msingi wa shaka. Imani kama hii ni moja ambayo kamwe Sitaitambua. Bila imani ya kweli, basi utakuwa mbali hata zaidi na upendo wa kweli. Na ikiwa unaweza kumshuku Mungu na kumkisia utakavyo, basi wewe bila shaka ni mdanganyifu zaidi kati ya wanadamu wengine. Mnakisia iwapo Mungu anaweza kuwa kama mwanadamu: mwenye dhambi isiyosameheka, mwenye tabia ndogondogo, anayependelea na asiye na mantiki, aliyekosa hisia ya haki, mwenye mbinu ovu, mdanganyifu na mjanja, na pia anayefurahishwa na uovu na giza, na kadhalika. Si sababu ambayo mwanadamu ana mawazo kama haya kwamba hana hata ufahamu mdogo wa Mungu? Imani kama hii ni sawa na dhambi! Zaidi ya hayo, kuna hata wale wanaoamini kwamba Sifurahishwi na yeyote isipokuwa wale wanaojirairai na kujipendekeza, na kwamba wale wasio na ujuzi huu hawatakaribishwa na watapoteza nafasi yao katika nyumba ya Mungu. Je, haya ndiyo maarifa ambayo mmepata kwa miaka hii yote mingi? Ni haya ndiyo mliyoyapata? Na ufahamu wenu kunihusu hauko kwa kutoelewa kama huku tu; mbaya hata zaidi ni kukufuru kwenu Roho wa Mungu na kuitukana Mbingu. Hii ndiyo maana Ninasema kwamba imani kama yenu itawasababisha tu kupotea mbali na Mimi na kukuwa na upinzani mkubwa dhidi Yangu. Kwa miaka mingi ya kazi, mmeona ukweli mwingi, lakini mnajua kile masikio Yangu yamesikia? Ni wangapi kati yenu walio tayari kukubali ukweli? Nyote mnaamini kwamba mko tayari kulipa gharama ya ukweli, lakini ni wangapi walioteseka kweli kwa ajili ya ukweli? Yote yaliyo ndani ya mioyo yenu ni uovu, na hivyo mnaamini kwamba yeyote, bila kujali ni nani, ni mjanja na asiye mwaminifu. Hata mnaamini kwamba Mungu mwenye mwili angekuwa bila moyo wa ukarimu na upendo wema kama tu binadamu wa kawaida. Zaidi ya hayo, mnaamini kwamba tabia ya adabu na asili yenye huruma na ukarimu ziko kwa Mungu wa mbinguni pekee. Na mnaamini kwamba mtakatifu kama huyu hayuko, na kwamba giza na uovu tu ndio unaotawala duniani, ilhali Mungu ni kitu ambacho mwanadamu huwekea matumaini yake ya mazuri na mema, na mtu maarufu aliyebuniwa na mwanadamu. Ndani ya akili zenu, Mungu aliye mbinguni ni mnyoofu sana, mwenye haki, na mkubwa, anayestahili ibada na upendezewaji, lakini Mungu huyu aliye duniani ni mbadala tu na chombo cha Mungu aliye mbinguni. Mnaamini Mungu huyu hawezi kuwa sawa na Mungu wa mbinguni, na hata zaidi hawezi kutajwa kwa pumzi moja na Yeye. Ifikapo kwa ukubwa na heshima ya Mungu, ni mali ya utukufu wa Mungu aliye mbinguni, lakini ifikapo kwa tabia na upotovu wa mwanadamu, vinahusishwa na Mungu aliye duniani. Mungu aliye mbinguni daima ni mkuu, ilhali Mungu wa duniani daima ni asiye na maana, mdhaifu na asiyejimudu. Mungu aliye mbinguni haathiriwi na hisia, kwa haki tu, ilhali Mungu aliye duniani ana motisha za kibinafsi tu na Hana haki na mantiki yoyote. Mungu aliye mbinguni hana udanganyifu hata kidogo na daima ni mwaminifu, ilhali Mungu wa duniani daima ana upande mdanganyifu. Mungu aliye mbinguni anampenda sana mwanadamu, ilhali Mungu wa duniani anamjali mwanadamu isivyotosha, hata kumpuuza kabisa. Ufahamu huu usio sahihi umewekwa kwa muda mrefu kwa mioyo yenu na unaweza pia kuendelezwa mbele katika siku za usoni. Mnachukulia matendo yote ya Kristo kwa msimamo wa wadhalimu na kuhukumu kazi Yake yote na utambulisho Wake na kiini Chake kwa mtazamo wa waovu. Mmefanya kosa kubwa sana na kufanya kile ambacho hakijawahi kufanywa na wale kabla yenu. Yaani, mnamtumikia tu Mungu mkuu aliye mbinguni na taji juu ya kichwa Chake na hammshughulikii kamwe Mungu mnayemchukulia kuwa asiye na maana kabisa kiasi cha kutoonekana kwenu. Hii siyo dhambi yenu? Huu sio mfano halisi wa kosa lenu dhidi ya tabia ya Mungu? Mnamwabudu sana Mungu aliye mbinguni. Mnapenda sana sura zilizo kuu na kuheshimu wanaojulikana kwa ajili ya umbuji wao. Mnaamrishwa kwa furaha na Mungu Anayejaza mikono yenu na utajiri, na mnatamani sana Mungu Anayeweza kutimiza tamaa zenu zote. Yule tu msiyemwabudu ni Mungu huyu asiye mkuu; Chombo chenu tu cha chuki ni ushirikiano na huyu Mungu ambaye hakuna mwanadamu anayeweza kumchukulia kuwa mkuu. Kitu pekee ambacho hamko tayari kufanya ni kumtumikia huyu Mungu ambaye hajawahi kuwapa senti hata moja, na Yule tu msiyemtamani ni huyu Mungu asiyependeza. Mungu kama huyu hawezi kuwawezesha kupanua upeo wenu wa macho, kuhisi kana kwamba mmepata hazina, sembuse kutimiza mnachotaka. Mbona, basi, mnamfuata? Je, mmefikiria kuhusu maswali kama haya? Kile ufanyacho hakimkosei huyu Kristo tu; cha muhimu hata zaidi, kinakosea Mungu aliye mbinguni. Nadhani kwamba, haya siyo madhumuni ya imani yenu kwa Mungu!
Mnatamani sana kwa Mungu kufurahishwa nanyi, lakini bado mko mbali sana na Mungu. Tatizo ni nini hapa? Mnakubali tu maneno Yake, lakini sio ushughulikiaji na upogoaji Wake; hata zaidi hamwezi kukubali mpangilio Wake wote, kuwa na imani kamilifu Kwake. Tatizo, basi, ni gani hapa? Kimsingi, imani yenu ni kaka tupu la yai lisiloweza kutoa kifaranga. Kwani imani yenu haijawaletea ukweli ama kuwapa maisha, na badala imewaletea hisia danganyifu ya tumaini na msaada. Madhumuni ya imani yenu kwa Mungu ni kwa ajili ya tumaini hili na msaada huu badala ya ukweli na maisha. Kwa hivyo, Nasema kwamba mkondo wa imani yenu kwa Mungu si mwingine bali ni kujaribu kujipendekeza kwa Mungu kupitia utumwa na kutokuwa na aibu, na hauwezi kuchukuliwa kuwa imani ya kweli hata kidogo. Kifaranga anaweza kujitokezaje kwa imani kama hii? Kwa maneno mengine, ni tunda lipi ambalo imani kama hii inaweza kuzalisha? Azma ya imani yenu kwa Mungu ni kutimiza nia zenu kupitia kumtumia Mungu. Huu sio ukweli zaidi unaoonyesha kosa lenu dhidi ya tabia ya Mungu? Mnaamini kuwepo kwa Mungu aliye mbinguni lakini mnakataa yule Mungu aliye duniani. Hata hivyo, Sikubaliani na maoni yenu. Nawapongeza tu wale wanadamu wanaosimama imara na kumtumikia Mungu wa duniani, kamwe sio wale wasiomkiri Kristo aliye duniani. Bila kujali jinsi wanadamu kama hawa walivyo waaminifu kwa Mungu aliye mbinguni, mwishowe, hawatauepuka mkono Wangu unaoadhibu waovu. Wanadamu kama hawa ni waovu; ni wale waovu wanaompinga Mungu na hawajawahi kumtii Kristo kwa furaha. Bila shaka, idadi yao inajumuisha wale wote wasiomjua na, zaidi, wasiomkiri Kristo. Unaamini kwamba unaweza kutenda utakavyo kwa Kristo alimradi wewe ni mwaminifu kwa Mungu aliye mbinguni? Makosa! Kutomjua Kristo kwako ni kutomjua Mungu aliye mbinguni. Bila kujali uaminifu wako kwa Mungu aliye mbinguni, ni maneno matupu tu na kujifanya, kwani Mungu aliye duniani si muhimu tu kwa mwanadamu kupokea ukweli na ufahamu mkubwa zaidi, lakini hata zaidi ni muhimu kwa lawama ya mwanadamu na baadaye kwa kuushika ukweli kuwaadhibu waovu. Umeelewa matokeo yenye faida na yanayodhuru hapa? Umepata kuyapitia? Ningependa siku moja hivi karibuni ninyi muelewe ukweli huu: Kumjua Mungu, mnapaswa kumjua sio tu Mungu wa mbinguni lakini, hata muhimu zaidi, Mungu aliye duniani. Msiyachanganye yaliyo kipaumbele ama kuruhusu yaliyo ya pili kuchukua nafasi ya yaliyo ya msingi. Ni kwa njia hii tu ndiyo unaweza kujenga uhusiano mzuri na Mungu, kuwa karibu na Mungu, na kupeleka moyo wako karibu na Yeye. Kama umekuwa wa imani kwa miaka nyingi na kushirikiana na Mimi kwa muda mrefu, lakini bado unabaki mbali na Mimi, basi Nasema kwamba ni lazima iwe kuwa mara nyingi unaikosea tabia ya Mungu, na mwisho wako utakuwa mgumu sana kufikiria. Kama miaka mingi ya ushirikiano na Mimi haijakubadilisha kuwa mwanadamu aliye na ubinadamu na ukweli, ila badala yake imeingiza njia zako ovu ndani ya asili yako, na huna maono maradufu ya uwongo kuhusu fahari kuliko awali pekee lakini kutonielewa kwako kumeongezeka pia, kiasi kwamba unakuja kunichukulia kuwa rafiki yako mdogo wa kando, basi Nasema kwamba mateso yako si ya juujuu tena, lakini yamepenya ndani kwa mifupa yako. Yote yaliyosalia ni wewe kusubiri matayarisho ya mazishi yako kufanywa. Huhitaji kunisihi basi Niwe Mungu wako, kwani umetenda dhambi inayostahili kifo, dhambi isiyosameheka. Hata kama Ningeweza kuwa na huruma nawe, Mungu aliye mbinguni Atasisitiza kuchukua maisha yako, kwani kosa lako dhidi ya tabia ya Mungu si shida ya kawaida, lakini lile lililo kubwa sana kiasili. Wakati utakapofika, usinilaumu kwa sababu ya kutokujulisha mbeleni. Yote yanarudia haya: Wakati unashirikiana na Kristo—Mungu aliye duniani—kama mwanadamu wa kawaida, yaani, unapoamini kwamba Mungu huyu si chochote ila ni mwanadamu, ni hapo basi ndipo utaangamia. Hili ndilo onyo Langu la pekee kwenu nyinyi nyote.
kutoka
katika Neno Laonekana katika Mwili
Chanzo:
Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni