Smiley face
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mafarisayo. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mafarisayo. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 14 Novemba 2019

Kutambua Kuwa Niliitembea Njia ya Mafarisayo

Umwombe Mungu
Wuxin Mji wa Taiyuan, Mkoa wa Shanxi
Kitu ambacho tumezungumzia mara kwa mara katika ushirikiano wa awali ni njia ambazo zilitembewa na Petro na Paulo. Inasemekana kwamba Petro alizingatia kujijua mwenyewe na kumjua Mungu, na alikuwa mtu ambaye Mungu alimpenda, ilhali Paulo alizingatia tu kazi yake, sifa na hadhi yake, na alikuwa mtu ambaye Mungu alimdharau. Daima nimekuwa na hofu ya kuitembea njia ya Paulo, ambayo ndiyo sababu mimi kwa kawaida mara nyingi husoma maneno ya Mungu kuhusu uzoefu wa Petro ili kuona jinsi alivyopata kumjua Mungu. Baada ya kuishi hivi kwa muda, nilihisi kwamba nilikwishakuwa mtiifu zaidi kuliko hapo awali, hamu yangu ya sifa na hadhi ilikuwa imedidimia, na kwamba nilikuwa nimepata kujijua kidogo. Wakati huu, niliamini kwamba ingawa sikuwa kabisa kwa njia ya Petro, inaweza kusemwa kuwa nilikuwa nimegusa ukingo wake, na angalau ilimaanisha sikuwa naelekea kwa njia ya Paulo. Hata hivyo, ningeaibishwa na ufichuzi wa neno la Mungu.

Jumatano, 23 Oktoba 2019

Kwa Nini Nimetembea Njia ya Mafarisayo

Mafarisayo
Suxing Mkoa wa Shanxi
Mimi ni mtu mwenye kiburi na majivuno, na cheo kimekuwa udhaifu wangu. Kwa miaka mingi katika imani yangu, nimefungwa na sifa na cheo na sijaweza kujiweka huru kutoka kwazo. Mara kwa mara nimepandishwa cheo na kubadilishwa na mtu mwingine; nimekuwa na vizuizi vingi katika cheo changu na nimekumbwa na matuta mengi njiani. Baada ya miaka mingi ya kushughulikiwa na kusafishwa, nilihisi kwamba sikuwa nachukulia cheo changu kwa uzito. Sikutaka kuwa kama nilivyokuwa katika nyakati zilizopita nikifikiri kwamba mradi nilikuwa kiongozi ningeweza kukamilishwa na Mungu na kwamba iwapo sikuwa kiongozi, basi sikuwa na matumaini. Nilielewa kwamba pasipo kujali jukumu ambalo nilikuwa natimiza, nilihitaji tu kutafuta ukweli na ningefanywa kamili na Mungu; kufuatilia sifa na cheo ni njia ya yule anayempinga Kristo. Sasa ninahisi kwamba pasipo kujali jukumu ambalo ninatimiza, naweza kubali kutokuwa na cheo. Ni sheria ya mbingu na dunia kwamba uumbaji utimize wajibu wake. Haijalishi pale unapowekwa, unapaswa kukubali mipango ya Mungu. Wakati upotovu wa umaarufu na cheo unafichuliwa, unaweza kutatuliwa kwa kuutafuta ukweli. Haijalishi ninachokabiliwa nacho wakati ninatimiza wajibu wangu, mradi ninauelewa ukweli nitakuwa tayari kulipia gharama. Kwa kuzingatia haya, nilifikiri kuwa nilikuwa tayari nimetembea njia ya kutafuta ukweli. Nilifikiri kwamba nimepata tena utu na mantiki. Mungu hupekua moyo na kuchunguza akili. Alijua kwamba nilikuwa mwenye najisi katika kutafuta kwangu ukweli, na kwamba sikuwa kweli natembea njia ya kuutafuta ukweli. Mungu alijua mbinu ya kutumia ili kunitakasa na kuniokoa.

Alhamisi, 17 Oktoba 2019

Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Je, ungependa kumwona Yesu? Je, ungependa kuishi na Yesu? Je, ungependa kuyasikia maneno yaliyonenwa na Yesu? Iwapo ni hivyo, basi utakaribishaje kurudi kwa Yesu? Je, uko tayari kabisa? Utakaribisha kurudi kwa Yesu kwa namna gani? Nafikiri kuwa kila ndugu anayemfuata Yesu angependa kumpa Yesu makaribisho mazuri. Lakini Je, mmewazia hili: Mtamjua Yesu kweli Atakaporejea? Je, mtaelewa kweli kila kitu Atakachosema? Je, mtakubali kweli, bila masharti, kila kazi ambayo Anafanya? Wale wote ambao wamesoma Biblia wanajua kuhusu kurudi kwa Yesu, na wale wote ambao wamesoma Biblia wanangoja kwa makini kuja Kwake. Nyote mmetazamia kufika kwa wakati huo, na uaminifu wenu ni wa kusifika, imani yenu kweli ni ya kuleta wivu, lakini mnatambua kuwa mmefanya kosa kuu? Yesu Atarejea kwa namna gani? Mnaamini kuwa Yesu Atarudi juu ya wingu jeupe, lakini Nawauliza: Wingu hili jeupe linaashiria nini? Na kwa kuwa wafuasi wengi wa Yesu wanangoja kurejea Kwake, Atashuka miongoni mwa watu wapi? Iwapo ninyi ni wa kwanza kati ya wale ambao Yesu Atawashukia, Je, wengine hawataona jambo hili kama lisilo la haki sana? Najua kuwa nyinyi mna ukweli mkubwa na utiifu kwa Yesu, lakini mmewahi kukutana na Yesu? Mnajua tabia Yake? Mmewahi kuishi na Yeye? Mnaelewa kiasi gani kumhusu kwa kweli? Wengine watasema kuwa maneno haya yanawaweka katika tatizo gumu. Watasema, “Nimesoma Biblia kuanzia mwanzo hadi mwisho mara nyingi sana. Nitakosaje kumwelewa Yesu? Usijali kuhusu tabia ya Yesu—najua hata rangi ya nguo Alizopenda kuvaa. Je, haushushi hadhi yangu ukisema simwelewi?” Napendekeza kuwa usiyapinge masuala haya; ni heri utulie na kufanya ushirika juu ya maswali yafuatayo: Kwanza, unajua uhalisi ni nini, na nadharia ni nini? Pili, unajua dhana ni nini, na ukweli ni nini? Tatu, unajua kile kinachowazwa na kile kilicho halisi?

Jumanne, 15 Oktoba 2019

1. Kumjua Mungu ni nini hasa? Kuwa kwa ufahamu wa Biblia na nadharia ya teolojia unaweza kuchukuliwa kama kumjua Mungu?

X. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kipengele cha Ukweli Kuhusu Jinsi ya Kumjua Mungu

1. Kumjua Mungu ni nini hasa? Kuwa kwa ufahamu wa Biblia na nadharia ya teolojia unaweza kuchukuliwa kama kumjua Mungu?

Maneno Husika ya Mungu:
Kumjua Mungu kunamaanisha nini? Kunamaanisha kwamba mwanadamu anajua shangwe, hasira, huzuni na furaha ya Mungu; huku ndiko kumjua Mungu. Unasema kwamba umemwona Mungu, ilhali huelewi shangwe, hasira, huzuni, na furaha ya Mungu, huelewi tabia Yake, wala huelewi haki Yake. Huna ufahamu wa rehema Zake, na hujui Anachokipenda ama Anachokichukia.Huu si ufahamu wa Mungu. Ikiwa unamjua, unamwelewa, na unaweza kuelewa mapenzi Yake kiasi, basi unaweza kumwamini kwa kweli, kumtii kwa kweli, kumpenda kwa kweli, na kumwabudu Yeye kwa kweli. Ikiwa huelewi mambo haya, basi unafuata tu, mtu fulani anayefuata tu na kufuata umati. Hiyo haiwezi kuitwa kutii kwa kweli au ibada ya kweli. Je! Ibada ya kweli inafanyika vipi? Hakuna wowote wanaomjua Mungu na kumwona Mungu kwa kweli ambao hawamwabudu Yeye, ambao hawamheshimu. Wote lazima wasujudu na kumwabudu Yeye. Kwa sasa, wakati wa kazi ya Mungu mwenye mwili, kadri watu wanavyokuwa na ufahamu zaidi wa asili ya uungu wa Mungu, wa tabia Yake na kile Anacho na alicho, ndivyo wanavyovithamini zaidi na kumcha Yeye. Kwa kawaida, ufahamu mdogo unamaanisha kutokuwa makini zaidi, na kwamba Mungu anachukuliwa kama mwanadamu. Ikiwa watu wanamjua Mungu na kumwona kweli, watatetemeka kwa hofu. Kwa nini Yohana alisema, “Yeye anayekuja baada ya mimi ni mwenye nguvu kuniliko, ambaye mimi si wa kufaa kubeba viatu vyake”? Ijapokuwa ufahamu wa ndani ya moyo wake haukuwa wa kina kirefu sana, lakini alijua kwamba Mungu ni wa ajabu. Ni watu wangapi wanaoweza kumcha Mungu sasa? Bila kuijua tabia Yake, mtu anawezaje kumheshimu? Ikiwa watu hawajui kiini cha Kristo na hawaelewi tabia ya Mungu, hawawezi kumwabudu Mungu wa vitendo kwa kweli. Ikiwa watu wanaona tu kuonekana kwa nje kwa kawaida kwa Kristo na hawajui asili Yake, ni rahisi kwa wao kumchukulia Kristo kama mtu wa kawaida. Huenda wakachukua mtazamo usio wa heshima Kwake, wanaweza kumdanganya, kumkataa, kutomtii, na kutoa hukumu Kwake. Wanaweza kujiona kuwa sahihi na kuchukulia neno Lake na kazi Yake kama yasiyo na maana, wahodhi mawazo kumhusu Mungu, na kumshutumu na kumkufuru. Ili kutatua masuala haya mtu lazima ajue kiini cha Kristo, uungu wa Kristo. Hiki ndicho kipengele kikuu cha kumjua Mungu; ni kile waumini wote wanapaswa kutimiza.