Smiley face
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo neno-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo neno-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 29 Machi 2019

Neno la Mungu | Sura ya 30

Amkeni, ndugu! Amkeni, kina dada! Siku Yangu haitakawishwa; wakati ni uhai, na kuushika wakati ni kuokoa uhai! Wakati hauko mbali sana! Mkifanya mitihani ya kuingia katika chuo kikuu na msipite, mnaweza kujaribu tena na mubukue kwa ajili ya mtihani. Hata hivyo, siku Yangu haitakuwa na ucheleweshaji kama huo. Kumbuka! Kumbuka! Ninakuhimiza kwa maneno haya mazuri. Mwisho wa dunia unafunguka mbele ya macho yenu wenyewe, majanga makubwa yanakaribia upesi; Je, maisha yenu ni muhimu au kulala, kula, kunywa, na kuvaa kwenu ndivyo muhimu? Wakati umekuja wa ninyi kufikiria kwa makini mambo haya. Msiwe wenye shaka tena na msiogope kuwa na uhakika!

Ijumaa, 1 Machi 2019

Neno la Mungu | Sura ya 25

Mwenyezi Mungu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani, Mungu wetu Anatawala! Mwenyezi Mungu anaweka miguu Yake kwenye Mlima wa Mizeituni. Uzuri ulioje! Sikiliza! Sisi walinzi tunapaza sauti zetu: tunaimba kwa pamoja kwa sauti zetu, kwa kuwa Mungu amerudi Sayuni. Tunaona kwa macho yetu wenyewe ukiwa wa Yerusalemu. Furahieni na kuimba kwa sauti kwa pamoja, kwa kuwa Mungu ametufariji na Ameukomboa Yerusalemu. Mungu ameweka wazi mkono Wake mtakatifu machoni pa mataifa yote, mtu halisi wa Mungu amejitokeza! Miisho yote ya dunia imeona wokovu wa Mungu wetu.

Jumatano, 2 Januari 2019

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 9

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 9


Nataka kukukumbusha kwamba huwezi kuwa na wasiwasi hata kidogo juu ya neno Langu na kutokujali kwa aina yoyote hakukubaliki. Unapaswa kulisikiliza na kulitii na kutenda mambo kulingana na nia Zangu. Daima lazima uwe macho na kamwe usiwe na tabia ambayo ni ya kiburi na ya kujidai, na lazima kila wakati unitegemee Mimi ili kutupilia mbali tabia ya zamani ya asili ambayo hukaa ndani yako. Unapaswa daima kuwa na uwezo wa kudumisha hali ya kawaida mbele Yangu, na uwe na tabia thabiti Kuwaza kwako lazima kuwe kwa busara na wazi na hakupaswi kuyumbishwa au kudhibitiwa na mtu yeyote, tukio, au kitu.