Smiley face
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo uaminifu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo uaminifu. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 13 Januari 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)(Sehemu ya Nne)


Mahitaji ya Mungu kwa Wanadamu


1. Utambulisho na Hadhi ya Mungu Mwenyewe
Mwenyezi Mungu alisema, Tumefikia mwisho wa mada ya "Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote," vilevile na ile ya "Mungu ni wa kipekee Mungu Mwenyewe." Baada ya kufanya hivyo, tunahitaji kufanya muhtasari. Muhtasari wa aina gani? Unaomhusu Mungu Mwenyewe. Kwa kuwa ni kumhusu Mungu Mwenyewe, basi lazima ugusie kila kipengele cha Mungu, vilevile aina ya imani ya watu kwa Mungu. Na kwa hiyo, kwanza lazima Niwaulize: Baada ya kusikia mahubiri, Mungu ni nani katika jicho la mawazo yako? (Muumbaji). Mungu katika jicho la mawazo yako ndiye Muumbaji.

Alhamisi, 16 Novemba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Nne

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Tamko la Ishirini na Nne

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Nne


Mwenyezi Mungu alisema: Kuadibu kwangu kunawajia watu wote, lakini pia kunakaa mbali na watu wote. Maisha yote ya kila mtu yamejaa upendo na pia chuki Kwangu, na hakuna mtu ambaye amewahi kunijua na kwa hivyo mtazamo wa mwanadamu Kwangu ni wa sitasita, na hauna uwezo wa kuwa kawaida. Lakini Nimekuwa Nikimlea na kumchunga mwanadamu na ni kwa sababu ya upumbavu wake ndiyo maana hana uwezo wa kuona matendo Yangu yote na kuelewa nia Zangu. Mimi Ndiye Ninayeongoza katika mataifa yote, na ndiye Mkubwa Zaidi kwa watu wote; kwa ufupi ni kwamba mwanadamu hanijui Mimi.