Smiley face
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo ukamilifu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo ukamilifu. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 20 Januari 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Wale Waliokamilishwa Pekee Ndio Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Wale Waliofanywa Kuwa Watimilifu Ndio Tu Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Wale Waliokamilishwa Pekee Ndio Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana

Kwa kweli, kazi inayofanywa sasa ni kuwafanya watu kumtoroka Shetani, kutoroka babu zao wa kale. Hukumu zote kwa neno zinalenga kufichua tabia potovu ya binadamu na kuwawezesha watu kuelewa kiini cha maisha. Hukumu hizi zote zilizorudiwa zinapenyeza mioyo ya watu. Kila hukumu inaathiri kwa njia ya moja kwa moja hatima yao na inalenga kujeruhi mioyo yao ili waweze kuachilia yale mambo hayo yote na hivyo basi kuja kujua maisha, kuujua ulimwengu huu mchafu, na pia kujua hekima ya Mungu na uweza Wake na kujua mwanadamu huyu aliyepotoshwa na Shetani.