Smiley face
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo ulinzi-wa-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo ulinzi-wa-Mungu. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 27 Desemba 2019

Baraka Kwa Sababu ya Ugonjwa—Insha Juu ya Upendo wa Mungu


Maisha ya kanisa
Dujuan Japani
Nilizaliwa katika familia fukara katika kijiji cha mashambani. Tangu niwe mtoto, niliishi maisha magumu na nilidharauliwa na wengine. Wakati mwingine sikujua hata kama ningepata chakula changu cha kufuatia, sembuse kumbwe na vitu vya watoto kuchezea. Kwa kuwa familia yangu ilikuwa fukara, nilipokuwa mdogo, ningevaa nguo zilizokuwa zikivaliwa na dadangu mkubwa awali. Nguo zake mara nyingi zilikuwa kubwa sana kwangu. Kama matokeo, nilipoenda shuleni, watoto wengine wangenicheka na hawangecheza na mimi. Utoto wangu ulikuwa mchungu sana. Kuanzia wakati huo kuendelea, ningejiambia kwa siri: Mara nitakapokuwa mtu mzima, nitakuwa mtu wa sifa na kupata pesa nyingi. Sitaruhusu wengine kunidharau tena. Kwa sababu familia yangu haikuwa na fedha, nililazimika kuacha shule kabla ya shule ya upili. Nilienda mji wa jimbo ili kufanya kazi katika kiwanda cha dawa. Ili kupata pesa zaidi, mara nyingi ningefanya kazi hadi saa tatu au nne usiku. Hata hivyo, fedha nilizopata hazikuwa za kutosha kufikia malengo yangu. Baadaye, niliposikia kwamba dada yangu alikuwa na uwezo wa kupata katika siku tano pesa nilizopata kwa mwezi kutokana na kuuza mboga, niliacha kazi yangu katika kiwanda cha dawa na nilikwenda kuuza mboga. Baada ya muda, nilipata kwamba ningeweza kupata hata pesa nyingi zaidi kwa kuuza matunda, kwa hiyo niliamua kuanza biashara kuuza matunda. Baada ya kuolewa na mume wangu, tulianzisha biashara ya mkahawa. Nilidhani kuwa kwa vile sasa nilikuwa na mkahawa, ningeweza kupata hata pesa zaidi. Mara nilipoweza kupata kiasi kikubwa cha mapato, kwa kawaida, ningeweza kushinda pendo na staha ya wengine. Watu wengine wangeanza kuniheshimu na wakati huo huo, ningeweza kuishi maisha bora zaidi. Hata hivyo, baada ya kuendesha biashara hiyo kwa kipindi cha muda, niligundua kuwa kwa hakika sikuwa natengeneza fedha nyingi. Nilianza kupata wasiwasi. Ni lini ningeweza kuishi maisha ambayo wengine wangependa?

Alhamisi, 17 Oktoba 2019

Kutanafusi kwa Mwenye Uweza

Kutanafusi kwa Mwenye Uweza

Kutanafusi kwa Mwenye Uweza

Kunayo siri kubwa moyoni mwako, ambayo hujawahi kuifahamu kamwe, kwa sababu umekuwa ukiishi katika ulimwengu bila mwanga. Moyo wako na roho yako vimepokonywa na yule mwovu. Macho yako yamezuiwa kwa giza yasione, na huwezi kuliona jua angani wala nyota ikimetameta wakati wa usiku. Masikio yako yamezibwa na maneno ya udanganyifu, na husikii sauti ya Yehova ingurumayo kama radi, wala sauti ya maji yakitiririka kutoka katika kiti cha enzi. Umepoteza kila kitu ambacho kilipaswa kuwa chako kwa haki, kila kitu ambacho Mwenye uweza alikupa. Umeingia katika bahari ya mateso isiyokuwa na mwisho, bila nguvu ya kukuokoa, bila matumaini ya kurudi ukiwa hai, na yote unayofanya ni kupambana na kusonga kila siku.… Tokea wakati huo, hungeweza kuepuka kuteswa na yule mwovu, uliwekwa mbali na baraka za mwenye Uweza, mbali na kukimu kwa mwenye Uweza, unatembea katika njia ambayo huwezi kurejea nyuma tena. Kuitwa mara milioni hakuwezi kusisimua moyo wako na roho yako. Unalala fofofo mikononi mwa yule mwovu, ambaye amekushawishi katika ulimwengu usio na mipaka, bila mwelekeo na bila alama za barabarani. Tokea hapo, umepoteza hali yako ya asili ya kutokuwa na hatia na utakatifu wako, na kuanza kujificha kutokana na utunzaji wa mwenye Uweza. Ndani ya moyo wako, yule mwovu anakuelekeza katika kila jambo na anakuwa uhai wako. Humwogopi tena, kumwepuka, au kumshuku; badala yake, unamchukulia kama Mungu aliye moyoni mwako. Unaanza kumtunza na kumwabudu, na nyinyi wawili mnakuwa msiotengana kama mwili na kivuli chake, kila akitoa nafsi yake kwa mwingine katika uzima na mauti. Hujui lolote kabisa kuhusu mahali ulikotoka, kwa nini ulizaliwa, au kwa nini utakufa. Unamtazama Mwenye uweza kama mgeni; hujui mwanzo Wake, sembuse yale yote ambayo Amekutendea. Kila kitu kitokacho Kwake kimekuwa cha kuchukiza kwako. Huvitunzi wala kujua thamani yavyo. Unatembea kando na yule mwovu, kuanzia siku ile ulipoanza Mwenye uweza alianza kukukimu. Wewe na yule mwovu mmepitia maelfu ya miaka ya dhoruba na tufani pamoja, na pamoja naye, mnampinga Mungu ambaye alikuwa chanzo cha uhai wako. Hujui lolote kuhusu kutubu, sembuse kwamba umefikia ukingo wa kuangamia. Unasahau kwamba yule mwovu amekujaribu na kukutesa; umesahau asili yako. Kwa njia hii, yule mwovu amekuwa akikuharibu, hatua baada ya hatua, hata mpaka leo. Moyo wako na roho yako vimekufa ganzi na vimeoza. Umeacha kulalamika juu ya maudhi ya dunia ya wanadamu, na huamini tena kwamba dunia si ya haki. Bado hujali sana kama Mwenye uweza yupo. Hii ni kwa sababu ulimchukulia yule mwovu kuwa baba yako wa kweli kitambo, na huwezi tena kutengana naye. Hii ndiyo siri iliyo moyoni mwako.

Jumapili, 23 Desemba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Bila Ya Wokovu wa Mungu, Singeweza Kuwa Hapa Leo

Bila Ya Wokovu wa Mungu, Singeweza Kuwa Hapa Leo

Zhang Jin, Beijing
Agosti 16, 2012

Mimi ni dada mzee mwenye miguu miwili yenye kasoro. Hata wakati hali ya hewa ni nzuri nje, nina shida kutembea, lakini wakati maji ya mafuriko yalipokuwa karibu kunimeza, Mungu aliniruhusu kutoroka hatari kimiujiza.