
Xiaocao Mji wa Changzhi, Mkoa wa Shanxi
Siku moja, niliona kifungu hiki kifuatacho cha neno la Mungu kwa maandishi “Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu”: “Katika kipindi kile alichomfuata Yesu, Petro alitazama na kutia moyoni kila kitu kuhusu maisha Yake: Matendo Yake, maneno Yake, mwendo Wake na maonyesho Yake. … Tangu wakati huo akiwa na Yesu, Petro alitambua pia kwamba hulka Yake ilikuwa tofauti na ile ya binadamu wa kawaida. Siku zote alikuwa na mwenendo dhabiti na hakuwahi kuwa na haraka, hakupigia chuku wala kupuuza chochote, na aliyaishi maisha Yake kwa njia iliyokuwa ya kawaida na ya kuvutia. Katika mazungumzo, Yesu alikuwa mwenye madaha na uzuri, mwenye uwazi na mchangamfu ilhali pia mtulivu, na Hakuwahi kupoteza heshima Yake katika utekelezaji wa kazi Yake. Petro aliona kwamba Yesu wakati mwingine alikuwa mnyamavu, ilhali nyakati nyingine alizungumza kwa mfululizo. Wakati mwingine Alikuwa na furaha sana kiasi cha kwamba aligeuka na kuwa mwepesi na mchangamfu kama njiwa, na ilhali nyakati nyingine Alihuzunika sana kiasi cha kwamba hakuzungumza kamwe, ni kana kwamba alikuwa mama aliyeathirika na hali ya hewa. Nyakati nyingine Alijawa na hasira, kama askari jasiri anayefyatuka kuwaua adui, na wakati mwingine hata kama simba anayenguruma. Nyakati nyingine Alicheka; nyakati nyingine aliomba na kulia. Haijalishi ni vipi Yesu alivyotenda, Petro alizidi kuwa na upendo na heshima isiyokuwa na mipaka Kwake. Kicheko cha Yesu kilimjaza kwa furaha, huzuni Yake ikamtia simanzi, hasira Yake ikamtetemesha, huku huruma Zake, msamaha na ukali vyote vikamfanya kuja kumpenda Yesu kwa kweli, na akaweza kumcha na kumtamani kwa kweli. Bila shaka, Petro alikuja kutambua haya yote kwa utaratibu baada ya kuishi kando yake Yesu kwa miaka michache” (Neno Laonekana katika Mwili).