Smiley face

Jumamosi, 30 Novemba 2019

Zawadi ya Kupendeza Zaidi Ambayo Mungu Amenipa

Maisha ya kanisa
Yixin Jiji la Shijiazhuang, Mkoa wa Hebei
Kabla, ningewasikia mara kwa mara ndugu zangu wa kiume na wa kike wakisema, “Kila kitu ambacho Mungu hufanya ni kwa ajili ya matokeo mazuri; ndiyo yote wanayohitaji watu.” Nilikubali hili na kukubaliana nalo, lakini sikuwa na ufahamu wowote kupitia uzoefu wangu mwenyewe. Baadaye nilipata ufahamu kiasi kwa njia ya mazingira ambayo Mungu aliniumbia.

Ijumaa, 29 Novemba 2019

Ni Muhimu Sana Kutii Kazi ya Roho Mtakatifu

Umwombe Mungu
Xiaowei Mji wa Shanghai
Wakati fulani kitambo, hata kama daima nilipata msukumo kiasi na fadhila wakati dada mmoja aliyeshiriki nami alishiriki nuru aliyokuwa amepata wakati alipokula na kunywa neno la Mungu, pia kila wakati nilikuwa na hisia ya muda mrefu kuwa alikuwa anajionyesha. Ningejiuliza, “Nikimjibu sasa hivi, sitakuwa nikimtia moyo? Kwa namna hiyo, sitaonekana basi kuwa duni kuliko yeye?” Matokeo yake yakawa, nilikataa kutaja maoni yangu mwenyewe katika ushirika au kutoa maoni kuhusu mawazo yoyote aliyoshirikisha. Wakati mmoja, dada yangu, alipopata utambuzi fulani kutoka kwa kula na kunywa fungu fulani la neno la Mungu, alihisi kuwa kulikuwa na kasoro fulani na hali yetu na kuniuliza kama ningekuwa radhi kuwasiliana naye kuhusu fungu hilo la neno la Mungu. Mara tu alipouliza, mawazo haya yote na hisia za chuki zilitanda juujuu: “Unataka tu kujishuhudia mwenyewe, kuwa na wasikilizaji wa kuhubiria. Kwa nini niwasiliane na wewe?” Hata nilifika kiwango cha kuhepa mkutano ili isinibidi kumsikiliza. Baada ya muda, nilihisi uzito mkubwa moyoni mwangu, nilijua kitu fulani kilikuwa kibaya na hali yangu, lakini sikuweza kufikiria njia nzuri ya kutatua mgogoro wangu wa ndani. Kile nilichoweza kufanya tu ni kujishughulisha kikamilifu katika wajibu wangu, kula na kunywa neno la Mungu, na kuimba nyimbo za injili ili kujizuia kutokana na hisia hizi hasi. Hata hivyo, kila mara nililazimika kukabiliana na hali ya sasa, uharibifu huo huo ungeinuka katika moyo wangu—mambo yalikuwa yanazidi kuwa mabaya, sio mazuri—na sikuwa na dokezo la nini kufanya kuhusu hayo.

Alhamisi, 28 Novemba 2019

Kutumia Neno la Mungu Kama Kioo

Kumwabudu Mungu
Wu Xia Mji wa Linyi , Mkoa wa Shandong
Baada ya kuikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho na kula na kunywa neno la Mungu, ilikuwa dhahiri kwangu kwamba ni muhimu sana kwamba mimi nijifahamu. Kwa hiyo, nilipokuwa nikila na kunywa neno la Mungu, nilihakikisha nimejithibitisha tena dhidi ya neno ambalo Mungu humfichua mwanadamu. Katika hali nyingi, niliweza kutambua kasoro zangu na upungufu. Nilihisi kwamba ningekuja kujifahamu kweli. Hata hivyo, ilikuwa ni kwa njia ya ufunuo kutoka kwa Mungu tu nilipoweza kuona kwamba kwa hakika sikujifahamu kulingana na neno la Mungu.

Jumatano, 27 Novemba 2019

Sitapumbazwa Tena na Nia Njema

Kumwabudu Mungu
Meng Yu Mji wa Pingdingshan, Mkoa wa Henan
Wakati mmoja nilipokuwa nikitimiza wajibu wangu, niliona kuwa ndugu fulani alikuwa akijaribu kuwafurahisha dada zake, maonyesho ya hali mbovu ya tabia yake machoni mwangu. Niliamua kutafuta fursa ya kumkumbusha haya mambo. Siku zilipita na nikaona utendaji wake wa wajibu ulikuwa wenye matokeo machache mazuri—ushahidi wa maoni yangu ya awali kumhusu. Kwa hiyo niliamua kuzungumza naye uso kwa uso. Hata hivyo, tulipogusia suala hili, alikataa kwa ukali maoni yangu yote na akajibu kwa ukali kwamba nilikuwa mwenye kukosoa sana. “Kwa miaka hii yote,” alisema, “wakati wowote unapowasiliana nami, unanikemea kwa mtazamo wa kudharau, na leo unasema kwa namna hiyo ya kudharau....” Mazungumzo hayo yakageuka kuwa mabaya zaidi kuliko yasiyozaa matunda—yalivunjika kwa kutokubaliana kabisa. Majibizo yake yaliniongoza kwa uamuzi mchungu, nikifikiri: “Niliwasiliana ili nisaidie, sio kukuaibisha kwa kufichua upungufu wako. Badala ya kusikiliza, ulinitafutia makosa na kunishutumu kuwa mwenye mtazamo wa kudharau. Sawa! Mimi nitakuacha uwe. Hata hivyo, nia zangu zilikuwa njema, na kukatalia kwako kunaonyesha tu kuwa hutafuti ukweli.” Tangu wakati huo, daima nimejichukulia kama yule ambaye alikuwa sahihi, wakati nikifikiri ndugu huyo ndiye aliyekuwa na makosa peke yake. Hata hivyo, hivi karibuni nilipata ufahamu kujihusu kwa njia ya kushughulikia watu, vitu na mambo ambavyo Mungu ameweka karibu nami.

Jumanne, 26 Novemba 2019

Ni Kwa Kuuelewa Ukweli tu Ndio Mtu Anaweza Kuwa na Utambuzi

Umwombe Mungu
Yi Ran Mji wa Laiwu , Mkoa wa Shandong
Wakati fulani awali, kwa sababu yangu kutoelewa kanuni iliyotumiwa na kanisa ya masahihisho ya wafanyakazi wa kanisa, wakati kanisa lilibadilisha kiongozi, dhana iliibuka ndani yangu. Kutoka kwa kile nilichoweza kuona, dada aliyebadilishwa alikuwa mzuri sana kwa kupokea na kushirikiana ukweli, na aliweza kuwa wazi juu ya maonyesho yake ya upotovu. Kwa hiyo sikuweza kujua asilani jinsi mtu fulani aliyetafuta ukweli sana angeweza kubadilishwa. Inawezekana kwamba yeye alizungumza juu ya maonyesho yake mwenyewe ya upotovu sana, na hivyo kiongozi wake kwa makosa alimchukua kuwa mtu asiyefuatilia ukweli, na kumbadilisha? Kama hili ndilo lililotokea kweli, basi si fursa ya mafunzo kwa mtu ambaye alikuwa anafuta ukweli imeangamizwa?

Jumatatu, 25 Novemba 2019

Watu Wasio na Hila Sio Lazima Wawe Waaminifu

Utambuzi wa Maisha
Cheng Mingjie Jiji la Xi’an, Mkoa wa Shaanxi
Mimi hujiona kuwa mtu wa aina ya kuwa wazi na mchangamfu. Mimi huzungumza na watu kwa njia ya waziwazi; chochote ninachotaka kusema, mimi husema—mimi sio aina ya mtu wa kuzungukazunguka. Katika kuingiliana kwangu na watu mimi huwa ni mwaminifu na wazi kiasi. Mara kwa mara, mimi hudanganywa na kudhihakiwa kwa sababu ya kuwaamini wengine kwa urahisi. Ilikuwa tu baada ya kuanza kwenda kanisani nilipopata mahali ambapo ningepaita pangu. Nilijiwazia mwenyewe: “Katika siku za nyuma kutokuwa na hila kwangu kumenifanya mwenye kuweza kudhuriwa na udanganyifu wa wengine; lakini katika kanisa Mungu anataka watu waaminifu, kwa hivyo mimi si lazima niwe na wasiwasi tena juu ya kuwa maasumu.” Nilihisi faraja hasa niliposikia kwamba Mungu anawapenda wale waaminifu na sahili, na kwamba ni waaminifu tu watakaopata wokovu wa Mungu. Nilipoona jinsi ndugu zangu wa kiume na wa kike walivyokuwa na majonzi walipoanza kutambua asili yao ya udanganyifu lakini hawakuweza kuibadilisha, nilihisi kufarijika hata zaidi kwamba, kuwa mwaminifu na waziwazi, isingenibidi kupitia majonzi kama hayo. Siku moja, hata hivyo, baada ya kupokea ufunuo kutoka kwa Mungu, hatimaye niligundua kwamba sikuwa mtu mwaminifu niliyedhani nilikuwa.

Jumapili, 24 Novemba 2019

Kwa Nini Sijabadilika Baada ya Miaka Mingi ya Imani

Kutafakari kwa Kikristo
Jinru Mji wa Nanyang, Mkoa wa Henan
Wakati ndugu wa kiume au wa kike alipoonyesha dosari zangu au hakusikiza kauli yangu ama sikuhisi kushawishika au nilibishana nao. Nilijutia vitendo vyangu baadaye, lakini nilipokabiliwa na mambo haya, sikuweza kujizuia mwenyewe kuifichua tabia yangu potovu. Nilisumbuliwa na hili kwa kina, na nikafikiri: Kwa nini maneno ya wengine yanaweza kuniaibisha hadi kukasirika? Na kwa nini sijabadilika hata kidogo licha ya miaka minane ya kumfuata Mungu? Nilikuwa na wasiwasi na tena na tena nilitafuta kutoka kwa Mungu, nikimuuliza kunipa nuru ili niweze kujua chanzo cha mbona tabia yangu potovu haikuwa imebadilika

Jumamosi, 23 Novemba 2019

Kupata Ahueni kwa Njia ya Kumwamini Mungu

Zenye Kupumzisha
Zhuanbian Mji wa Shanghai
Ingawa nilikuwa nikimfuata Mungu kwa miaka mingi, nilikuwa karibu sijafanya maendeleo yoyote na kuingia kwangu katika maisha, na hii ilinifanya nihisi kuwa na wasiwasi sana. Hasa wakati niliposikia rekodi ya mahubiri juu ya kuingia kwa maisha, na kusikia mtu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu akizungumza na ndugu wa kiume na wa, nilihisi nikiwa nimejawa na wasiwasi nikimsikia akisema jambo kama hili, “Nyinyi sasa mnamwamini Mungu na mmeonja uzuri wa ukimbizaji wa ukweli. Nyinyi mmeanza kuingia kwa njia sahihi na mmejaa imani katika ukimbizaji wenu wa wokovu.” Nikawaza, “Watu hawa wamemwamini Mungu kwa muda mfupi sana lakini wameingia tayari na wamejaa imani sana kuhusu kuokolewa. Na bado niko hapa nikiwa nimemwamini Mungu hadi sasa na bado sijaipata ukweli na tabia yangu katika maisha haijapitia mabadiliko yoyote kamwe, bila kujali kuwa nilikuwa nimeingia kwa njia sahihi. Ni rahisi kuongelea kufikia wokovu kuliko kukuweka katika vitendo!” Niliwaza jinsi hao wa hapo juu walifanya ushirika kwamba ukweli ungeweza kutatua upotovu wote wa wanadamu, lakini sikuwa nimepitia jambo hili kamwe. Hata nilihisi kwamba ukweli ungeweza kutatua upotovu wa watu wengine lakini sio wangu mwenyewe, kwa hiyo nilipoteza imani katika ukimbizaji wangu wa ukweli na wa wokovu. Ingawa nilikuwa na ufahamu kwamba hali yangu mwenyewe haikuwa sahihi, hapakuwa na njia yoyote ambayo ningeweza kuiepuka, hivyo ningeweza tu kumlilia Mungu kwa msaada. Baadaye, maneno Yake yalinipatia nuru, yakinifanya nione ni kwa nini nilikuwa nimemwamini Mungu kwa miaka mingi hivyo na bado sikuwa nimeendelea katika maisha, na kwa nini hali yangu haikuwa imepitia mabadiliko yoyote. Mungu pia aliniweka kwa njia ya kutenda na kuingia katika ukweli.