Smiley face

Ijumaa, 15 Februari 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I)” Sehemu ya Kwanza



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I)” Sehemu ya Kwanza


Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.

Maudhui ya video hii:
Kwenye Siku ya Kwanza, Mchana na Usiku wa Mwanadamu Vinazaliwa na Kujitokeza Waziwazi kwa Msaada wa Mamlaka ya Mungu
Kwenye Siku ya Pili, Mamlaka ya Mungu Yalipangilia Maji, na Kufanya Mbingu, na Anga za Mbinu za Kimsingi Zaidi za Kuishi kwa Binadamu Kuonekana
Kwenye Siku ya Tatu, Matamshi ya Mungu Yazaa Ardhi na Bahari, na Mamlaka ya Mungu Yasababisha Ulimwengu Kujaa Maisha

 Soma Zaidi: 

Mwenyezi Mungu anasema,“Maisha ya Muumba ni yale yasiyo ya kawaida, fikira Zake ni zile zisizo za kawaida, na mamlaka Yake ni yale yasiyokuwa ya kawaida, na kwa hivyo, wakati matamshi Yake yalipotamkwa, yale matokeo ya mwisho yalikuwa “na ikawa hivyo.” Ni wazi kwamba, Mungu hahitaji kufanya kazi kwa mikono Yake wakati Anapofanya matendo; Anatumia tu fikira Zake kutoa amri, na matamshi Yake ili kuagizia, na kwa njia hii mambo yanatimizwa. Kwenye siku hii, Mungu aliyakusanya maji katika mahali pamoja, na Akaiacha ardhi kavu kujitokeza, baada ya hapo Mungu aliifanya nyasi kuota kutoka kwenye ardhi, na papo hapo palimea mimea ya msimu iliyozaa mbegu, na miti ya kuzaa matunda, na Mungu akaainisha kila mojawapo kulingana na aina, na kusababisha kila mmea kuwa na mbegu yake. Haya yote yaliwezekana kulingana na fikira za Mungu na amri za matamshi ya Mungu, na kila mmea ulijitokeza, mmoja baada ya mwingine, kwenye ulimwengu huu mpya.

Wakati Alikuwa aanze kazi Yake, Mungu tayari alikuwa na picha ya kile Alichonuia kutimiza katika akili Zake na wakati ambapo Mungu alianza kutimiza mambo haya, na ndio wakati ambao pia Mungu alikifungua kinywa Chake kuongea kuhusu maudhui ya picha hii, mabadiliko katika viumbe vyote yalianza kufanyika kutokana na mamlaka na nguvu za Mungu. Bila ya kujali namna Mungu alivyofanya, au Alivyoonyesha mamlaka Yake, kila kitu kilitimizwa hatua kwa hatua kulingana na mpango wa Mungu na kwa sababu ya matamshi ya Mungu, na mabadiliko ya hatua kwa hatua yalifanyika kati ya mbingu na ardhi kutokana na matamshi na mamlaka ya Mungu. Mabadiliko na matukio haya yote yalionyesha mamlaka ya Muumba, na nguvu za maisha ya Muumba zisizo za kawaida na zenye ukubwa. Fikira Zake si mawazo mepesi, au picha tupu, lakini mamlaka yanayomiliki nishati kuu na ile isiyo ya kawaida, na ndio nguvu zinazosababisha viumbe vyote kubadilika, kufufuka, kupata nguvu upya, na kuangamia. Na kwa sababu ya haya, viumbe vyote hufanya kazi kwa sababu ya fikira Zake, na, wakati uo huo, yote haya yanatimizwa kwa sababu ya matamshi kutoka kinywa Chake….

Kabla ya viumbe vyote kujitokeza, kwenye akili za Mungu mpango wa Mungu ulikuwa umeundwa kitambo, na ulimwengu mpya ulikuwa umetimizwa kitambo. Ingawaje kwenye siku ya tatu mimea aina yote ilijitokeza ardhini, Mungu hakuwa na sababu yoyote ya kusitisha hatua za uumbaji Wake kwa ulimwengu huu, Alinuia kuendelea kunena matamshi Yake, kuendelea kutimiza uumbaji wa kila kiumbe kipya. Angenena, angetoa amri Zake, na angeonyesha mamlaka Yake na kuendeleza nguvu Zake, na Alitayarisha kila kitu Alichokuwa amepanga ili kutayarishia viumbe vyote na mwanadamu ambaye Alinuia kuumba….”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni