Smiley face

Jumanne, 26 Juni 2018

"Njia ya Kwenda katika Ufalme wa Mbinguni ni Yenye Hatari" (4) - Kwa Nini Binadamu Humwasi Mungu?


Miaka elfu mbili iliyopita, Mungu alipopata mwili kama Bwana Yesu na kuja miongoni mwa wanadamu kuwakomboa binadamu Alikataliwa katika enzi ya giza, hatimaye kusulubiwa msalabani na binadamu waovu wenye upotovu. Bwana Yesu alitabiri kwamba Angekuja tena katika siku za mwisho, Akisema: "Kwa kuwa kama vile umeme, umulikavyo toka upande mmoja chini ya mbingu, na kumulika upande mwingine chini ya mbingu; ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu katika siku yake. Lakini kwanza, ni lazima apate mateso mengi, na kukataliwa na kizazi hiki.” (Luka 17:24-25). Kwa nini Bwana Yesu atakapokuja tena katika siku za mwisho “Atakataliwa na kizazi hiki”? Mungu alipoonekana mara mbili katika mwili kufanya kazi Yake kwa nini alikumbwa na uasi na shutuma kali na binadamu wapotovu? Je, unajua sababu katika hili? Video hii fupi itakufichulia jibu.
Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, ni Bwana Yesu aliyerudi. Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu linajitokeza kwa sababu ya kuonekana kwa kazi ya Mungu na iliyojumuishwa na wale wote waliomkubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya dhati ya siku za mwisho na walishindwa na kuokolewa na neno la Mungu. Kondoo za Mungu husikia sauti ya Mungu. Kwa sababu ya kuonekana kwa maneno ya Kristo wa siku za mwisho, watu zaidi na zaidi ambao wana kiu ya kutafuta ukweli wameshindwa na neno la Mungu na kurudi kwa Mwenyezi Mungu. Wamepata maji ya kunywa na kulishwa na neno la Mungu na kufurahia kazi na mwongozo wa Roho Mtakatifu, wakithibitisha kwa hakika kwamba Mwenyezi Mungu ndiye kurudi kwa Mkombozi ambaye tumemtarajia kwa miaka mingi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni