Gangqiang ni Mkristo. Aliona namna upendo wa Bwana na huruma Yake kwa binadamu vilivyo vikubwa, na akaamua mara nyingi kwamba angempenda Bwana, kumridhisha Bwana, kutekeleza neno la Bwana, na kuwa na mwenendo wake binafsi kama mtu anayesifiwa na Bwana. Lakini alipotoa athari ya kimatendo kwa neno la Bwana, aligundua kwamba kwake yeye mwenyewe kulikuwa na mambo mengi potovu na ya uasi-ubinafsi, kiburi, udanganifu, na ulaghai na kadhalika.
Tabia hizi potovu zilikuwa zinamrudisha nyuma, na hakuwa na nguvu kamwe za kuyatekeleza maneno ya Bwana. Kwa sababu hii, alikuwa na mfadhaiko kabisa, na mara nyingi alimwita Bwana kwa usadizi. Gangqiang baadaye alienda Marekani kufanya kazi na huko akafahamiana na Dada Zhao wa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Kupitia kwa mawasiliano ya Dada Zhao na kushuhudia kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, na kwa kuyasoma baadhi ya maneno ya Mwenyezi Mungu, Gangqiang alipata kujua kwamba Bwana Yesu alikuwa tayari Amerudi, na kwamba Alikuwa ametekeleza kazi ya kuhukumu na kutakasa binadamu, Akimwelekeza binadamu katika njia ya kuitatua asili yake yenye dhambi. Moyo wa Gangqiang ulikuwa umepata nuru, na alikubali kwa furaha kazi ya Mungu ya siku za mwisho, na akaja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Kwa kulisoma neno la Mwenyezi Mungu, aliuelewa ukweli fulani, na maisha yake ya huzuni yaliangazwa na maneno ya Mungu …
Kanisa la Mwenyezi Mungu lilikuja kuwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu.
NYUMBANI
Usomaji wa Maneno ya Mwenyezi Mungu
Filamu za Injili
Kwaya za Injili
Maisha ya Kanisa—Mfululizo wa Maonyesho Mbalimbali
Video za Nyimbo na Ngoma
Msururu wa MV za Ufalme
Video za Nyimbo za Dini
Filamu za Maisha ya Kanisa
Filamu za Uzoefu wa Mateso
Kufunua Mfululizo wa Video za Ukweli
Sehemu za Filamu
Aina za Dondoo za Video
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni