Smiley face

Jumapili, 9 Desemba 2018

Wimbo Mpya wa Dini | "Kazi ya Mungu Inaendelea Kuboreshwa" | Have You Followed God's Footsteps?


Wimbo Mpya wa Dini | "Kazi ya Mungu Inaendelea Kuboreshwa" | Have You Followed God's Footsteps?


Kazi ya Mungu inaendelea kuwa bora;

ingawa kusudi linabaki bila kubadilika,

mbinu ya kazi Yake inabadilika daima,

na hivyo pia wale wanaomfuata.

Kadiri ambavyo Mungu anafanya kazi zaidi,

ndivyo anavyozidi mwanadamu kumjua, kikamilifu,

ndivyo tabia ya mwanadamu inavyozidi kubadilika

pamoja na kazi Yake ifaavyo.

Kazi ya Mungu inaendelea kuboreshwa;

Kazi Yake kamwe sio nzee na ni mpya daima.

Yeye kamwe harudii kazi ya zamani,

kazi ambayo haijafanywa awali tu ndiyo Atakayoifanya.


Mungu hadumishi kazi ile ile;

inabadilika kila mara na ni mpya daima.

Ni sawa na Mungu kunena maneno mapya

na kufanya kazi mpya kila siku kwako.

Hii ni kazi ambayo Mungu anafanya;

umuhimu upo katika "ajabu," na "mpya."

"Mungu habadiliki na Yeye atakuwa Mungu daima."

Huu ni msemo ambao hakika ni ukweli.

Kazi ya Mungu inaendelea kuboreshwa;

Kazi Yake kamwe sio nzee na ni mpya daima.

Yeye kamwe harudii kazi ya zamani,

kazi ambayo haijafanywa awali tu ndiyo Atakayoifanya.


Lakini kwa kuwa kazi ya Mungu hubadilika kila mara,

kwa wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu,

na wanadamu wapumbavu wasiojua ukweli,

Wao huishia kuwa wapinzani wa Mungu.

Kiini cha Mungu hakitabadilika kamwe;

Mungu ni Mungu kila mara na kamwe sio Shetani.

Lakini hii haimaanishi kuwa kazi Yake haibadiliki,

na ipo daima kama kiini Chake.

Unasema kuwa Mungu habadiliki kamwe,

lakini utaeleza vipi "sio nzee kamwe, mpya daima"?

Kazi ya Mungu inakua na kubadilika,

Anaonyesha mapenzi Yake na kufanya yajulikane kwa mwanadamu pia.

Kazi ya Mungu inaendelea kuboreshwa;

Kazi Yake kamwe sio nzee na ni mpya daima.

Yeye kamwe harudii kazi ya zamani,

kazi ambayo haijafanywa awali tu ndiyo Atakayoifanya.


kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

        

Sikiliza zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni