Smiley face
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kazi-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kazi-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 14 Oktoba 2019

Neno la Mwenyezi Mungu|Maonyo Matatu

Kazi ya Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu

Neno la Mwenyezi Mungu|Maonyo Matatu

Kama muumini wa Mungu, hamfai kuwa watiifu kwa yeyote mwingine isipokuwa Yeye katika mambo yote na mjilinganishe na moyo Wake katika mambo yote. Hata hivyo, ingawa wote huelewa mafundisho haya, ukweli huu wa kimsingi ulio wazi kabisa kwa binadamu hauwezi kuonekana kuwa kujumuishwa kwao kikamilifu, kutokana na ugumu wao, kama vile hali yao ya kutojua, upuzi, au ufisadi. Kwa hivyo, kabla mwisho wenu haujaamuliwa, Ninafaa kuwaambia kwanza baadhi ya mambo, ambayo ni yenye umuhimu mkubwa sana kwenu.

Jumamosi, 12 Oktoba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako

Kazi ya Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako

Nimefanya kazi nyingi miongoni mwenu na, ni wazi kwamba, Nimezungumza vizuri pia. Hata hivyo, Nahisi kwamba maneno na kazi Yangu havijatimiza lengo la kazi Yangu ya siku za mwisho. Maana, katika siku za mwisho, kazi Yangu si kwa ajili ya mtu au watu fulani bali ni kwa manufaa ya kufafanua tabia Yangu asilia. Hata hivyo, kutokana na sababu nyingi—pengine ukosefu wa muda au shughuli nyingi za kazi—tabia Yangu haijamwezesha binadamu kunijua hata kidogo.

Ijumaa, 11 Oktoba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Kazi ya Mungu,neno la Mungu,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Njia ya maisha si kitu ambacho kinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, wala hakipatikani kwa urahisi na wote. Hiyo ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote.

Alhamisi, 10 Oktoba 2019

Neno la Mwenyezi Mungu|Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu



Neno la Mwenyezi Mungu|Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu

Enzi ya zama ishaenda, na enzi mpya imefika. Mwaka baada ya mwaka na siku baada ya siku, Mungu amefanya kazi nyingi. Alikuja duniani, kisha Akaondoka. Mzunguko kama huu umeendelea kwa vizazi vingi. Siku ya leo, Mungu anaendelea kama mbeleni kufanya kazi Anayopaswa kufanya, kazi ambayo bado Hajaikamilisha, kwani hadi leo, bado Hajaingia mapumzikoni. Kutoka wakati wa uumbaji hadi leo, Mungu amefanya kazi nyingi, lakini ulijua kwamba kazi anayoifanya Mungu leo ni nyingi kuliko awali na kipimo ni kikubwa zaidi? Hii ndiyo maana Nasema Mungu amefanya jambo kubwa miongoni mwa wanadamu.

Jumatano, 9 Oktoba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi.

Jumatatu, 7 Oktoba 2019

Neno la Mwenyezi Mungu|Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?

Kazi ya Mungu,Neno la Mungu,Mwenyezi Mungu

Neno la Mwenyezi Mungu|Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?

Huenda ikawa safari yako ya imani katika Mungu imekuwa ndefu zaidi ya mwaka mmoja au miwili, na labda kwa maisha yako umestahimili ugumu mwingi miaka hii yote; au labda haujapitia ugumu na badala yake umepokea neema nyingi. Kuna uwezekano pia kuwa hujapitia ugumu wala kupokea neema, na badala yake umeishi maisha ya kawaida tu. Hiyo haijalishi, kwani wewe bado u mfuasi wa Mungu, kwa hivyo tushikiriane kuhusu mada ya kumfuata Mungu. Lakini, lazima Niwakumbushe wote wanaoyasoma maneno haya kwamba neno la Mungu huelekezwa kwa wale wanaomtambua na wale wanaomfuata Mungu, na sio kwa watu wote wa ulimwengu, wakiwemo wale wasiomtambua Mungu.

Jumapili, 6 Oktoba 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo


Neno la Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

Nimefanya kazi kubwa miongoni mwa binadamu, na maneno ambayo Nimeeleza wakati huu yamekuwa mengi. Maneno haya ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, na yalikuwa yanaeleza ili binadamu aweze kulingana na Mimi. Ilhali Nimewapokea watu wachache tu duniani ambao wanalingana na Mimi, na hivyo Nimesema kwamba binadamu hathamini maneno Yangu, kwa kuwa binadamu halingani na Mimi. Kwa njia hii, kazi ambayo Naifanya sio tu kwa ajili ya mwanadamu aweze kuniabudu; muhimu zaidi, ni kwa ajili ya mwanadamu aweze kulingana na Mimi.

Jumamosi, 5 Oktoba 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa

Kazi ya Mungu,Sauti ya Mungu,Umeme wa Mashariki

Neno la Mwenyezi Mungu | Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa

    Nimewatafuta wengi duniani wawe wafuasi Wangu. Kati yao ni wale wanaohudumu kama makuhani, wanaoongoza, wanaojumuisha wana, wanaojumuisha watu, na wale wanaotoa huduma. Ninawagawa katika makundi haya tofauti kwa msingi wa uaminifu wanaonionyesha. Wakati wanadamu wote wameainishwa kulingana na aina, yaani, asili ya kila aina ya mwanadamu inapowekwa wazi, basi Nitamhesabu kila mwanadamu miongoni mwa aina yake kamili na kuweka kila aina katika nafasi yake kamili ili Nikamilishe lengo Langu la ukombozi wa mwanadamu.

Ijumaa, 4 Oktoba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu


Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu

Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na wote hutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu. Kabla ya nyinyi kumwona Yesu, yaani, kabla ya nyinyi kumwona Mungu Aliye kwenye mwili, mnaweza kuwa na mawazo mengi, kwa mfano, kuhusu sura ya Yesu, njia Yake ya kuzungumza, njia Yake ya maisha, na kadhalika. Hata hivyo, wakati mmemwona hasa, mawazo yenu yatabadilika haraka. Ni kwa nini? Je, mnataka kujua? Hata ingawa fikira za mwanadamu hakika haziwezi kupuuzwa, haikubaliki hata zaidi kwa mwanadamu kubadilisha kiini cha Kristo.

Alhamisi, 3 Oktoba 2019

Matamshi ya Kristo | Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Je, ungependa kumwona Yesu? Je, ungependa kuishi na Yesu? Je, ungependa kuyasikia maneno yaliyonenwa na Yesu? Iwapo ni hivyo, basi utakaribishaje kurudi kwa Yesu? Je, uko tayari kabisa? Utakaribisha kurudi kwa Yesu kwa namna gani? Nafikiri kuwa kila ndugu anayemfuata Yesu angependa kumpa Yesu makaribisho mazuri. Lakini Je, mmewaza iwapo mtamjua Yesu kweli Atakaporejea? Je, mtaelewa kweli kila kitu Atakachosema? Je, mtakubali kweli, bila masharti, kila kazi ambayo Anafanya? Wale wote ambao wamesoma Biblia wanajua kuhusu kurudi kwa Yesu, na wale wote ambao wamesoma Biblia wanangoja kwa makini kuja Kwake. 

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Pili)

kazi ya Mungu,Neno la Mungu,ukweli

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Pili)

Punde tu Shetani anaposhindwa, hivyo ni kusema, punde tu mwanadamu anaposhindwa kabisa, mwanadamu ataelewa kwamba kazi yake yote ni kwa ajili ya wokovu, na kuwa mbinu ya wokovu huu ni kurejesha kutoka kwa mikono ya Shetani. Miaka 6,000 ya kazi ya Mungu ya usimamizi imegawanywa katika awamu tatu: Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Awamu hizi zote tatu za kazi ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, ambayo ni kusema, ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu ambaye ameharibiwa na Shetani kwa kiasi kikubwa. Wakati huo huo, hata hivyo, pia ni ili kwamba Mungu afanye vita na Shetani.

Jumanne, 1 Oktoba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Kwanza)

Neno la Mungu,kazi ya Mungu,Kumjua Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu(Sehemu ya Kwanza)

Mwanadamu anaelewa sehemu ndogo ya kazi ya leo na kazi ya baadaye, lakini hafahamu hatima ambapo mwanadamu ataingia. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutekeleza wajibu wa kiumbe: Mwanadamu anapaswa kumfuata Mungu kwa lolote afanyalo, na mnapaswa muendelee mbele kwa njia yoyote ambayo Nitawaambia. Wewe huna mbinu ya kufanya mipango yako mwenyewe, na huna uwezo wa kujitawala mwenyewe; yote ni lazima yaachwe kwa rehema za Mungu, na kila kitu kinadhibitiwa na mikono Yake. 

Jumatatu, 30 Septemba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni

Kupata Mwili,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni

    Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu. Kwa hivyo, chemichemi Yake ni ile ya Mungu Mwenyewe; Dutu hii haitapinga kazi Yake Mwenyewe, na Yeye hangeweza kufanya kitu chochote kinachoharibu kazi Yake Mwenyewe, wala milele Yeye kutamka maneno yoyote ambayo yanakwenda kinyume na mapenzi Yake Mwenyewe.

Jumapili, 29 Septemba 2019

Matamshi ya Kristo| Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Pili)

Wakati kazi ya Mungu inafikia hatua fulani, na usimamizi Wake kufikia hatua fulani, wale wanaoutafuta moyo Wake wote huwa na uwezo wa kutimiza matakwa yake. Mungu humwekea mwanadamu matakwa kulingana na viwango Vyake mwenyewe, na kulingana na kile ambacho mwanadamu anaweza kufanikisha. Akiwa anazungumzia usimamizi Wake, Yeye humwonyesha njia mwanadamu , na kumpa mwanadamu namna ya kudumu. Usimamizi wa Mungu na vitendo vya mwanadamu vipo katika hatua sawia kikazi, na yote yanafanyika kwa wakati mmoja. Mazungumzo kuhusu usimamizi wa Mungu yanagusia mabadiliko katika tabia ya mwanadamu, na yanazungumzia kuhusu yale yafaayo kufanywa na mwanadamu, na mabadiliko katika tabia ya mwanadamu, hugusia kazi ya Mungu; hakuna wakati ambao haya mawili yanaweza kutenganishwa.

Jumamosi, 28 Septemba 2019

Matamshi ya Kristo|Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza)

Kazi ya Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu haitengani na mwanadamu, kwa kuwa mwanadamu ni chombo cha kazi hii na kiumbe wa pekee aliyeumbwa na Mungu anayeweza kutoa ushuhuda kwa Mungu. Maisha ya mwanadamu na shughuli zake zote havitengani na Mungu, na vyote vinaongozwa na mkono wa Mungu, na inaweza kusemwa kuwa hakuna mtu anayeweza kuishi bila Mungu. Hakuna anayeweza kupinga hili, kwani ndio ukweli. Kila Akifanyacho Mungu ni kwa faida ya mwanadamu, na kinalenga hila za Shetani. Kila anachokihitaji mwanadamu kinatoka kwa Mungu, na Mungu ndiye chanzo cha maisha ya mwanadamu.

Ijumaa, 27 Septemba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Kupata Mwili,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Mungu mwenye mwili wa kwanza Aliishi duniani kwa miaka thelathini na tatu na nusu, lakini Alitekeleza huduma Yake kwa miaka mitatu na nusu pekee ya hiyo miaka yote. Kipindi Alichofanya kazi na kabla Aanze kazi Yake, Alikuwa na ubinadamu wa kawaida. Aliishi na ubinadamu Wake wa kawaida kwa miaka thelathini na tatu na nusu. Katika miaka yote mitatu na nusu ya mwisho Alijifichua kuwa Mungu mwenye mwili. Kabla Aanze kutekeleza kazi ya huduma Yake, Alikuwa na ubinadamu wa kawaida, bila kuonyesha ishara ya uungu Wake, na ni baada tu ya kuanza rasmi kutekeleza huduma Yake ndipo uungu Wake uliwekwa wazi.

Alhamisi, 26 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu | Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Pili)

Kazi Yake katika mwili ni ya umuhimu mkubwa, ambao umezungumzwa kuhusiana na kazi, na Yule ambaye hatimaye anahitimisha kazi ni Mungu mwenye mwili, na sio Roho. Baadhi ya watu wanaamini kwamba Mungu wakati fulani anaweza kuja duniani na kumtokea mwanadamu, ambapo atawahukumu wanadamu wote, akimjaribu mmoja baada ya mwingine bila mtu yeyote kupitwa. Wale wanaofikiri kwa namna hii hawafahamu hatua hii ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Mungu hamhukumu mwanadamu mmoja baada ya mwingine, na hamjaribu mwanadamu mmoja baada ya mwingine; kufanya hivyo sio kazi ya hukumu.

Jumatano, 25 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu | Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Kwanza)

Kupata Mwili,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Mungu alifanyika mwili kwa sababu lengo la kazi Yake si roho ya Shetani, au kitu chochote kisicho cha mwili, ila mwanadamu, ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa na Shetani. Ni kwa sababu hii kabisa kwamba mwili wa mwanadamu umeharibiwa ndio maana Mungu akamfanya mwanadamu mwenye mwili kuwa mlengwa wa kazi Yake; aidha, kwa sababu mwanadamu ni mhusika wa uharibifu, Amemfanya mwanadamu kuwa mlengwa wa kazi Yake katika hatua zote za kazi Yake ya wokovu. Mwanadamu ni kiumbe anayekufa, ni wa mwili na damu, na Mungu ndiye tu Anayeweza kumwokoa mwanadamu. Kwa namna hii, Mungu ni lazima Awe mwili ambao una tabia zinazofanana na mwanadamu ili Aweze kufanya kazi Yake, ili kwamba kazi Yake iweze kupata matokeo mazuri zaidi.

Jumanne, 24 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu | Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Pili)


Kazi ya Mungu Mwenyewe ni maono ambayo mwanadamu lazima afahamu, kwa kuwa kazi ya Mungu haiwezi kutekelezwa na mwanadamu, wala haimilikiwi na mwanadamu. Hatua tatu za kazi ndizo ukamilifu wa usimamizi wa Mungu, na hakuna ono kuu kuliko hili linalopaswa kufahamika kwa mwanadamu. Kama mwanadamu hafahamu maono haya makuu, basi si rahisi kumjua Mungu, na si rahisi kujua mapenzi ya Mungu, na, zaidi ya hayo, njia ambayo mwanadamu anapitia inazidi kuwa ngumu. Bila maono, mwanadamu hangeweza kufika umbali huu.

Jumatatu, 23 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu|Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Kwanza)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu.