Smiley face

Jumanne, 4 Desemba 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ni Lazima Wale Wanaofaa Kufanywa Wakamilifu Wapitie Usafishaji

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ni Lazima Wale Wanaofaa Kukamilishwa Wapitie Usafishaji

Kama unamwamini Mungu, ni lazima umtii Mungu, uweke ukweli katika vitendo na utimize wajibu wako wote. Zaidi ya hayo, ni lazima uelewe mambo unayopaswa kupitia. Ikiwa unapitia tu kushughulikiwa, kufundishwa nidhamu na hukumukama wewe unaweza tu kumfurahia Mungu, lakini huwezi kuhisi wakati Mungu anakufundisha nidhamu au kukushughulikia, hili halikubaliki. Labda katika wakati huu wa usafishaji unaweza kushikilia msimamo wako. Hii bado haitoshi; ni lazima uendelee mbele. Funzo la kumpenda Mungu halina mwisho, na hakuna kamwe kikomo kwake. Watu huona kuamini katika Mungu kama jambo rahisi mno, lakini mara tu wanapopata uzoefu kiasi wa vitendo, wao hutambua kwamba imani katika Mungu si rahisi kama watu wanavyofikiria. Wakati Mungu anafanya kazi ili kumsafisha mwanadamu, mwanadamu huteseka, upendo wake kwa Mungu unakuwa mkubwa zaidi, na nguvu za Mungu zaidi zinafichuliwa kwake. Kadiri usafishaji wa mwanadamu ulivyo wa kiwango cha chini, ndivyo upendo wake kwa Mungu ulivyo wa kiwango cha chini, na ndivyo nguvu za Mungu zinafichuliwa kwake kwa kiwango cha chini. Kadiri usafishaji wake na uchungu wake ulivyo mkubwa na zaidi yalivyo mateso yake, ndivyo upendo wake wa kweli kwa Mungu utakavyokuwa, ndivyo imani yake kwa Mungu itakavyokuwa ya kweli, na ndivyo maarifa yake ya Mungu yatakuwa ya kina. Katika uzoefu wako utaona kwamba wale ambao wanakabiliwa na usafishaji mkubwa na uchungu, na kushughulikiwa sana na kufundishwa nidhamu, wana upendo mkubwa kwa Mungu, na maarifa ya kina na elekevu ya Mungu. Wale ambao hawajapitia kushughulikiwa wanayo maarifa ya juu juu tu, na wanaweza tu kusema: “Mungu ni mzuri sana, Yeye huwapa watu neema ili waweze kumfurahia Yeye.” Kama watu wamepitia kushughulikiwa na kufundishwa nidhamu, basi hao wanaweza kuyazungumza maarifa ya kweli ya Mungu. Hivyo kazi ya Mungu katika mwanadamu ilivyo ya ajabu zaidi, ndivyo ilivyo ya thamani zaidi na ni muhimu zaidi. Kadiri inavyokosa kupenyeza kwako zaidi na kadiri isivyolingana na mawazo yako, ndivyo kazi ya Mungu inavyoweza kukushinda, kukupata, na kukufanya mkamilifu. Umuhimu wa kazi ya Mungu ni mkubwa sana! Kama Hangemsafisha mwanadamu kwa njia hii, kama Hangefanya kazi kulingana na njia hii, basi kazi ya Mungu haingekuwa na ufanisi na ingekuwa isiyo na maana. Hii ndiyo sababu ya umuhimu wa ajabu wa uteuzi Wake wa kundi la watu katika siku za mwisho. Hapo awali ilisemwa kuwa Mungu angelichagua na kulipata kundi hili. Kadiri ilivyo kuu kazi Anayofanya ndani yenu, ndivyo ulivyo mkubwa na safi upendo wenu. Kadiri kazi ya Mungu ilivyo kuu zaidi, ndivyo mwanadamu anavyoweza kuonja hekima Yake na ndivyo maarifa ya mwanadamu Kwake yalivyo ya kina zaidi. Katika siku za mwisho, miaka 6,000 ya mpango wa Mungu wa usimamizi itafika kikomo. Je, inawezekana ifike mwisho hivyo tu, kwa urahisi hivyo? Baada ya Yeye kuwashinda wanadamu, je, kazi Yake itakuwa imefika mwisho? Je, inaweza kuwa rahisi vile? Watu hufikiria kwamba ni rahisi sana, lakini kile ambacho Mungu anafanya si rahisi vile. Bila kujali ni sehemu gani ya kazi ya Mungu, yote ni isiyoeleweka kwa mwanadamu. Ikiwa ungeweza kuifahamu, basi kazi ya Mungu ingekuwa isiyo na maana au thamani. Kazi inayofanywa na Mungu ni isiyoeleweka; inakinzana pakubwa na mawazo yako, na kadiri isivyopatana na mawazo yako, ndivyo inavyoonyesha zaidi kwamba kazi ya Mungu ni ya maana; ingekuwa inalingana na mawazo yako, basi ingekuwa isiyo maana. Leo, unahisi kwamba kazi ya Mungu ni ya ajabu mno, na kadiri ilivyo ya ajabu, ndivyo unahisi kwamba Mungu ni asiyeeleweka, na kuona jinsi matendo ya Mungu yalivyo makubwa. Kama Angefanya tu kazi fulani ya juu juu ya kutimiza wajibu kumshinda mwanadamu na Aachie hapo, basi mwanadamu hangeweza kuona umuhimu wa kazi ya Mungu. Ingawa unapokea usafishaji kidogo sasa, ni wa faida kubwa sana kwa ukuaji wa maisha yako—na hivyo ugumu wa aina hii ni wenye umuhimu mkubwa sana kwako. Leo, unapokea usafishaji kidogo, lakini baadaye utaweza kwa kweli kuyaona matendo ya Mungu, na hatimaye utasema: “Matendo ya Mungu ni ya ajabu mno!” Haya ndiyo yatakuwa maneno moyoni mwako. Baada ya kupitia usafishaji wa Mungu kwa muda (majaribu ya[a] watenda huduma na wakati wa kuadibu), baadhi ya watu hatimaye walisema: “Kuamini katika Mungu ni kugumu kweli kweli!” “Kugumu” huku kunaonyesha kwamba matendo ya Mungu ni yasiyoeleweka, kuwa kazi ya Mungu ni yenye umuhimu na thamani kubwa, na ni yenye kustahili sana kuthaminiwa na mwanadamu. Ikiwa, baada ya Mimi kufanya kazi nyingi hivi, hukuwa na maarifa hata kidogo, basi kazi Yangu ingeweza kuwa na thamani bado? Itakufanya useme: “Huduma kwa Mungu ni ngumu kweli, matendo ya Mungu ni ya ajabu mno, Mungu kweli ni mwenye hekima! Yeye ni mwenye kupendeza kweli!” Kama, baada ya kupitia kipindi cha uzoefu, una uwezo wa kusema maneno kama haya, basi hii inathibitisha kuwa umepata kazi ya Mungu ndani yako. Siku moja, wakati uko nje ya nchi kueneza injili na mtu akuulize: “Imani yako katika Mungu iko vipi?” Utaweza kusema: “Matendo ya Mungu ni ya ajabu kweli!” Baada ya kukuona ukisema hivyo, watahisi kwamba kuna kitu ndani yako na kwamba matendo ya Mungu kweli ni yasiyoeleweka. Huku kweli ni kutoa ushahidi. Utasema kuwa kazi ya Mungu imejaa hekima, na kazi Yake ndani yako imekushawishi kwa kweli na kuushinda moyo wako. Wewe daima utampenda kwa maana Yeye anastahili zaidi upendo wa wanadamu! Kama unaweza kuzungumza kwa vitu hivi, unaweza kuigusa mioyo ya watu. Haya yote ni kutoa ushahidi. Kama unaweza kuwa shahidi wa ajabu, kuwagusa watu hadi watoe machozi, hiyo inaonyesha kwamba kwa kweli wewe ni mmoja anayempenda Mungu. Hii ni kwa sababu unaweza kutenda kama shahidi wa upendo kwa Mungu na matendo ya Mungu yanaweza kuonyeshwa kupitia kwako. Na kwa njia ya kujieleza kwako, watu wengine wanaweza kutafuta Matendo Yake, wapate uzoefu wa Mungu, na wao wataweza kusimama imara katika kila mazingira wanayojikuta katika. Ni kutoa ushahidi kwa njia hii ndio kutoa ushahidi kwa dhati, na hili hasa ndilo linalohitajika kutoka kwako sasa. Unafaa kusema kwamba matendo ya Mungu ni muhimu sana na yanastahili kuthaminiwa na watu, kwamba Mungu ni wa thamani mno na Yuko kwa wingi, Hawezi tu kusema, lakini hata zaidi Anaweza kusafisha mioyo ya watu, kuwaletea starehe, na Anaweza kuwapata, kuwashinda, na kuwakamilisha. Kutoka katika kupitia kwako utaona kwamba Mungu ni mwenye kupendwa sana. Hivyo unampenda Mungu kiasi gani sasa? Je, unaweza kweli kusema mambo haya kutoka moyoni mwako? Wakati unaweza kuonyesha maneno haya kutoka kwenye kina cha moyo wako utaweza kuwa na ushuhuda. Mara tu uzoefu wako unapofikia kiwango hiki utakuwa na uwezo wa kuwa shahidi wa Mungu, na utakuwa umefuzu kwa ajili yake. Kama huwezi kufika kiwango hiki katika uzoefu wako, basi wewe bado utakuwa mbali sana. Ni jambo la kawaida kwa watu kuwa na udhaifu katika usafishaji, lakini baada ya usafishaji unapaswa kuweza kusema: “Mungu ni mwenye hekima sana katika kazi Yake!” Kama wewe kweli unaweza kuelewa utambuzi wa utendaji wa hili, ni wa thamani, na uzoefu wako ni wa thamani.

Je, ni nini unachofuatilia sasa? Unachopaswa kuwa ukifuatilia ni kama wewe una uwezo wa kuonyesha matendo ya Mungu, kama unaweza kuwa onyesho na udhihirisho wa Mungu, na kama wewe unastahili kutumiwa na Yeye. Ni kiasi gani cha kazi ambacho Mungu hakika amefanya kwako? Ni kiasi gani ambacho umeona, ni kiasi gani ambacho umegusa? Umepitia kiasi gani, na kuonja kiasi gani? Kama Mungu amekujaribu, kukushughulikia, au kukuadhibu—haijalishi chochote, matendo Yake na kazi Yake vimetekelezwa juu yako, lakini kama muumini katika Mungu, kama mtu ambaye ana nia ya kufuatilia kukamilishwa na Yeye, je, una uwezo wa kuonyesha matendo ya Mungu kwa njia ya uzoefu wako mwenyewe wa utendaji? Je, unaweza kuishi kwa kumdhihirisha Mungu kupitia kwa hili? Je, unaweza kuwakimu wengine kupitia uzoefu wako mwenyewe wa utendaji, na kugharimika mwenyewe kwa ajili ya kazi ya Mungu? Ili kuwa na ushuhuda kwa ajili ya matendo ya Mungu lazima uweze kueleza matendo Yake ni nini, na hili linafanywa kupitia uzoefu wako, maarifa, na mateso ambayo umevumilia. Je, wewe ni mtu ambaye huwa na ushuhuda kwa ajili ya matendo ya Mungu? Je, una matamanio haya? Kama unaweza kuwa na ushuhuda kwa ajili ya jina Lake, na hata zaidi, matendo Yake, pamoja na kuishi kwa kudhihirisha sura ambayo Yeye anataka kutoka kwa watu Wake, basi wewe ni shahidi wa Mungu. Je, unashuhudia kwa ajili ya Mungu vipi kwa hakika? Kutafuta na kuwa na hamu sana ya kuishi kwa kumdhihirisha Mungu, kuonyesha matendo ya Mungu kupitia kwa maneno yako, kuwaruhusu watu kujua na kuona matendo Yake—kama kweli unatafuta yote haya, Mungu atakukamilisha. Ikiwa yote unayotafuta ni kukamilishwa na Mungu na kubarikiwa mwishoni kabisa, basi mtazamo wa imani yako katika Mungu si safi. Unapaswa kuwa ukifuatilia jinsi ya kuona matendo ya Mungu katika maisha ya kweli, jinsi ya kumridhisha Yeye wakati anafichua mapenzi Yake kwako, kutafuta jinsi ya kutoa ushuhuda kwa maajabu Yake na hekima, na jinsi ya kuonyesha nidhamu na ushughulikiaji Wake kwako. Haya yote ni mambo unayopaswa kuwa ukijaribu kuelewa sasa. Kama upendo wako kwa Mungu ni ili tu uweze kushiriki katika utukufu wa Mungu baada ya Yeye kukukamilisha, bado hautoshi na hauwezi kukidhi mahitaji ya Mungu. Unahitaji kuwa na uwezo wa kuwa na ushuhuda kwa matendo ya Mungu, kutosheleza mahitaji Yake, na kuwa na uzoefu wa kazi ambayo Amefanya kwa watu kwa njia ya utendaji. Iwe ni maumivu, machozi, au huzuni, lazima uyapitie yote kwa vitendo. Haya yote ni ili uweze kuwa shahidi wa Mungu. Je, ni chini ya utawala wa nini hasa sasa ndiyo unateseka na kutafuta ukamilifu? Je, ni kuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu? Je, ni kwa ajili ya baraka za mwili au kwa ajili ya matarajio ya baadaye? Dhamira zako zote, motisha, na malengo ya kibinafsi ya kufuatilia lazima yarekebishwe na hayawezi kuongozwa na mapenzi yako mwenyewe. Kama mtu mmoja anatafuta ukamilifu kupokea baraka na kutawala katika madaraka, wakati yule mwingine anafuatilia ukamilifu kumridhisha Mungu, kwa ajili ya kuwa shahidi wa matendo ya Mungu kwa kweli, je, ni ipi kati ya njia hizi mbili za ufuatiliaji ndiyo ungechagua? Ukichagua ya kwanza, basi bado uko mbali sana na viwango vya Mungu. Nilisema kabla ili kuruhusu matendo Yangu kujulikana wazi katika ulimwengu wote na kwamba Ningetawala kama Mfalme katika ulimwengu. Kwa upande mwingine, kilichoaminiwa kwenu ni kwenda kutoa ushuhuda kwa matendo ya Mungu, si kwa ajili yenu kuwa wafalme na kuonekana ulimwenguni wote. Acha ulimwengu wote ujazwe na matendo ya Mungu. Acha kila mtu ayaone na ayakiri. Hili linasemwa kuhusiana na Mungu Mwenyewe, na kile ambacho wanadamu wanapaswa kufanya ni kutoa ushuhuda kwa ajili ya Mungu. Je, unajua kiasi gani kuhusu Mungu sasa? Je, unaweza kutoa ushuhuda kwa Mungu kiasi gani? Je, ni lengo gani la Mungu kumkamilisha mwanadamu? Mara baada ya kuelewa mapenzi ya Mungu, je, unapaswa kuonyeshaje kujali kuelekea mapenzi Yake? Kama uko tayari kukamilishwa na uko tayari kutoa ushuhuda kwa matendo ya Mungu kulingana na kile unachoishi kwa kudhihirisha, kama una hii nguvu ya msukumo, basi hakuna lililo gumu sana. Wanachohitaji watu sasa ni kujiamini. Kama una hii nguvu ya msukumo, basi ni rahisi kuachilia chochote chenye uhasi, cha kukaa tu, uvivu na mawazo ya mwili, falsafa za maisha, tabia ya uasi, hisia, na mengineyo. 

Wakati wanapitia majaribu, ni kawaida kwa watu kuwa dhaifu, au kuwa na uhasi ndani yao, au kukosa uwazi juu ya mapenzi ya Mungu au njia yao ya kutenda. Lakini katika hali yoyote, lazima uwe na imani katika kazi ya Mungu, na usimkane Mungu, kama Ayubu. Ingawa Ayubu alikuwa dhaifu na aliilaani siku yake ya kuzaliwa, yeye hakukana kwamba vitu vyote katika maisha ya binadamu vilikuwa vimetolewa na Yehova, na kwamba Yehova pia Ndiye anayevichukua vyote. Haijalishi jinsi alivyojaribiwa, alidumisha imani hii. Haijalishi ni aina gani ya usafishaji unayopitia katika uzoefu wako wa maneno ya Mungu, Mungu anahitaji imani ya binadamu. Kwa njia hii, kinachofanywa kamili ni imani ya watu na matarajio. Wakati huwezi kuyagusa au kuyaona, ni katika hali hii ndiyo imani yako inahitajika. Imani ya watu inahitajika kwa wakati ambao kitu hakiwezi kuonekana kwa macho tu, na imani yako inahitajika wakati huwezi kuziachilia dhana zako mwenyewe. Ukiwa huna uwazi kuhusu kazi ya Mungu, kinachotakiwa ni imani yako na kwamba uchukue msimamo imara na kuwa shahidi. Wakati Ayubu alifikia hatua hii, Mungu alimwonekania na kuzungumza naye. Yaani, ni kutoka ndani ya imani yako tu ndipo utaweza kumwona Mungu, na wakati una imani Mungu atakukamilisha. Bila imani, Hawezi kufanya hivyo. Mungu ataweka juu yako chochote ulicho na matumaini ya kupata. Kama huna imani, huwezi kukamilishwa na hutakuwa na uwezo wa kuona matendo ya Mungu, na zaidi huwezi kuona kudura Yake. Wakati una imani na unaweza kugusa matendo Yake katika uzoefu wako wa utendaji, Mungu atakuonekania, na Atakupa nuru na kuongoza kutoka ndani. Bila hiyo imani, Mungu hataweza kufanya hivyo. Kama umepoteza matumaini katika Mungu, utawezaje kupata uzoefu Wake? Kwa hiyo, ni wakati tu una imani na huweki mashaka kumhusu Mungu, ni wakati una imani ya kweli Kwake tu bila kujali Anachokifanya ndipo Atakuangazia na kukupa nuru katika mapito yako, na ni hapo tu ndipo utaweza kuona matendo Yake. Mambo haya yote yanafanikishwa kupitia katika imani, na imani inafanikishwa tu kupitia usafishaji—imani haiwezi kukua bila kuwepo kwa usafishaji. Je, imani inarejelea nini? Imani ni kusadiki kwa kweli na moyo wa dhati ambao wanadamu wanapaswa kumiliki wakati wao hawawezi kuona au kugusa kitu, wakati kazi ya Mungu haiambatani na dhana za binadamu, wakati inazidi uwezo wa binadamu. Hii ndiyo imani Ninayozungumzia. Watu wanahitaji imani katika nyakati za shida na usafishaji, na pamoja na imani huja usafishaji. Hivi havichanguliki. Haijalishi jinsi Mungu anavyofanya kazi au ni aina gani ya mazingira uliyomo, utaweza kufuatilia maisha, kuendeleza kazi ya Mungu ndani yako, na kuufuatilia ukweli. Utakuwa na uelewa wa matendo ya Mungu na utakuwa na utaweza kutenda kulingana na ukweli. Hii ni imani yako ya kweli, na hii inaonyesha kuwa hujapoteza tumaini kwa Mungu. Bado utaufuatilia ukweli katika usafishaji, utaweza kumpenda Mungu kwa kweli na wala hutakuwa na mashaka Kwake. Haijalishi Anachofanya, bado utatenda ukweli kumridhisha Yeye, na utaweza kwa undani kutafuta mapenzi Yake na kujali mapenzi Yake. Ni hii tu ndiyo imani ya kweli katika Mungu. Awali, wakati Mungu alisema kwamba ungetawala kama mfalme, ulimpenda, na wakati Alijionyesha hadharani kwako, ulimfuata. Lakini sasa Mungu amejificha, huwezi kumwona, na shida zimekujia. Kwa wakati huu, je, unapoteza matumaini katika Mungu? Hivyo wakati wote ni lazima ufuatilie maisha na kutafuta kuridhisha mapenzi ya Mungu. Hii inaitwa imani ya kweli, na ni aina ya upendo ulio wa kweli na mzuri zaidi.

Ilikuwa kwamba watu wote wangefanya maazimio yao mbele ya Mungu na kusema: “Haijalishi asiyempenda Mungu, ni lazima mimi nimpende.” Lakini sasa, unakabiliwa na usafishaji. Si sambamba na dhana zako, hivyo unapoteza imani katika Mungu. Je, huu ni upendo wa kweli? Umesoma mara nyingi kuhusu matendo ya Ayubu—Je, umesahau kuyahusu? Upendo wa kweli unaweza tu kukua kutoka ndani ya imani. Unakuza upendo wa kweli kwa Mungu kupitia usafishaji wako, katika uzoefu wako halisi wewe hujali mapenzi ya Mungu kwa njia ya imani yako, na kwa njia ya imani yako unautelekeza mwili wako mwenyewe na kuyafuatilia maisha—hili ndilo watu wanapaswa kufanya. Ukifanya hivi utaweza kuona matendo ya Mungu, lakini ukikosa imani hutaweza, na hutaweza kupata uzoefu wa kazi Yake. Iwapo unataka kutumika na kukamilishwa na Mungu, ni lazima umiliki kila kitu: uwe tayari kuteseka, imani, uvumilivu, utiifu na pia uwezo wa kupitia kazi ya Mungu, kupata kufahamu mapenzi Yake na kujali huzuni Yake. Kumkamilisha mtu si rahisi, na kila kisa cha usafishaji unachopitia kinahitaji imani na upendo wako. Kama unataka kukamilishwa na Mungu, kwenda mitaani tu hakutoshi, na kugharimika mwenyewe kwa ajili ya Mungu pekee hakutoshi pia. Ni lazima umiliki mambo mengi ili uweze kuwa mtu ambaye anakamilishwa na Mungu. Unapokabiliwa na mateso ni lazima uweze kutozingatia mwili na usilalamike dhidi ya Mungu. Wakati Mungu anajificha kutoka kwako, ni lazima uweze kuwa na imani ya kumfuata Yeye, kudumisha upendo wako wa awali bila kuuruhusu ufifie au kutoweka. Haijalishi anachofanya Mungu, ni lazima utii mpango Wake, na kuwa na nia zaidi ya kuulaani mwili wako mwenyewe kuliko kulalamika dhidi Yake. Wakati unakabiliwa na majaribu lazima umridhishe Mungu licha ya kutotaka kuacha kitu chochote unachopenda, au kilio cha uchungu. Ni hili tu linaloweza kuitwa upendo wa kweli na imani. Haijalishi kimo chako halisi ni kipi, ni lazima kwanza umiliki nia ya kupitia ugumu pamoja na imani ya kweli, na ni lazima uwe na nia ya kuutelekeza mwili. Unapaswa kuwa tayari binafsi kuvumilia ugumu na kupata hasara kwa maslahi yako binafsi ili kuridhisha mapenzi ya Mungu. Lazima pia uwe na moyo wa kujuta mwenyewe, kwamba hukuweza kumridhisha Mungu katika siku za nyuma, na kuwa na uwezo wa kujuta mwenyewe sasa. Kusiwe na hata kimoja kati ya hivi kinachokosa na Mungu atakukamilisha wewe kupitia vitu hivi. Ikiwa huna hali hizi, huwezi kufanywa mkamilifu.

Sasa, watu wote wameona kuwa mtu anayemtumikia Mungu lazima asijue jinsi ya kuteseka kwa ajili yake tu, lakini hata zaidi, anapaswa kuelewa kwamba kuamini katika Mungu ni kwa ajili ya kutafuta kumpenda. Mungu kukutumia wewe si kwa ajili ya kukusafisha wewe tu au kukufanya uteseke, lakini ni kukufanya ujue matendo Yake, kujua umuhimu halisi wa maisha ya binadamu, na hasa kukufanya ujue kwamba kumtumikia Mungu si kazi rahisi. Kupata uzoefu wa Mungu hakuhusu kufurahia neema Yake, lakini zaidi kuhusu kuteseka kwa sababu ya upendo wako Kwake. Kwa kuwa unafurahia neema ya Mungu, lazima pia ufurahie kuadibu Kwake—lazima upitie haya mambo yote. Unaweza kupata uzoefu wa nuru ya Mungu ndani yako, na unaweza pia kupitia ushughulikiaji Wake kwako na hukumu Yake. Kwa njia hiyo, unakuwa na uzoefu wa pande zote. Mungu amefanya kazi ya hukumu kwako, na Yeye pia amefanya kazi ya kuadibu kwako. Neno la Mungu limekushughulikia, lakini pia limekupa nuru, limekuangazia. Wakati unataka kukimbia, mkono wa Mungu bado unakuvuta kwa nguvu. Hizi kazi zote ni kukufahamisha kwamba kila kitu kuhusu mwanadamu kinadhibitiwa na Mungu. Unaweza kufikiri kuamini katika Mungu ni kuhusu mateso, au kufanya mambo mengi kwa ajili Yake, au kwa ajili ya amani ya mwili wako, au ni kwa ajili ya kila jambo kwenda vyema kwako, kwa ajili ya kila jambo kuwa la kustarehesha—lakini hakuna kati ya haya ambayo ni madhumuni ambayo watu wanapaswa kuwa nayo kwa ajili ya kuamini katika Mungu. Kama hayo ndiyo unayoamini, basi mtazamo wako si sahihi na huwezi kukamilishwa kabisa. Matendo ya Mungu, tabia ya Mungu ya haki, hekima Yake, maneno Yake, na maajabu Yake na kutoeleweka kwa kina Kwake yote ni mambo ambayo watu wanapaswa kuelewa. Tumia uelewa huu kuachana na maombi ya kibinafsi na pia matumaini ya mtu binafsi na dhana zilizo moyoni mwako. Ni kwa kuondoa haya tu ndiyo unaweza kukidhi masharti yanayotakiwa na Mungu. Ni kwa njia hii tu ndio unaweza kuwa na uzima na kumridhisha Mungu. Kumwamini Mungu ni kwa ajili ya kumridhisha Yeye na kuishi kwa kudhihirisha tabia ambayo Yeye anahitaji, ili matendo na utukufu Wake viweze kudhihirishwa kupitia kundi hili la watu wasiostahili. Huo ndio mtazamo sahihi wa kuamini katika Mungu, na pia lengo unalopaswa kutafuta. Unapaswa kuwa na mtazamo sahihi wa kuamini katika Mungu na kutafuta kupata maneno ya Mungu. Unahitaji kula na kunywa maneno ya Mungu, na kuwa na uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha ukweli, na hasa kuona matendo Yake ya utendaji, kuona matendo Yake ya ajabu kotekote katika ulimwengu mzima, pamoja na kazi ya vitendo Yeye hufanya katika mwili. Kwa njia ya uzoefu wao halisi, watu wanaweza kufahamu ni jinsi gani hasa Mungu hufanya kazi Yake kwao na mapenzi Yake kwao ni yapi. Haya yote ni ili kuondoa tabia yao potovu ya kishetani. Jiondolee uchafu na udhalimu ndani yako, ondoa nia zako mbaya, na unaweza kuendeleza imani ya kweli katika Mungu. Kwa kuwa tu na imani ya kweli ndiyo unaweza kweli kumpenda Mungu. Unaweza tu kweli kumpenda Mungu kwa msingi wa imani yako Kwake. Je, unaweza kufanikisha kumpenda Mungu bila kumwamini? Kwa kuwa unaamini katika Mungu, huwezi kukanganyika kuhusu jambo hilo. Baadhi ya watu hujawa na nguvu mara tu wanapoona kwamba imani katika Mungu itawaletea baraka, lakini hupoteza nguvu zote mara tu wanapoona wanafaa kupitia kusafishwa. Je, huko ni kuamini katika Mungu? Mwishowe, imani katika Mungu inahusu utiifu kamili na mzima mbele Yake. Unaamini katika Mungu lakini bado una madai Kwake, una mawazo mengi ya kidini ambayo huwezi kuyapuuza, maslahi ya kibinafsi huwezi kuacha, na bado unatafuta baraka za mwili na unataka Mungu auokoe mwili wako, kuiokoa nafsi yako—haya yote ni maonyesho ya watu wenye mtazamo usio sahihi. Hata kama watu wenye imani za kidini wana imani katika Mungu, hawatafuti mabadiliko ya tabia, hawafuatilii maarifa ya Mungu, na wanatafuta tu maslahi ya miili yao. Wengi kati yenu wana imani ambazo ni za kikundi cha kusadiki kidini. Hiyo siyo imani ya kweli katika Mungu. Kuamini katika Mungu lazima watu wamiliki moyo wa kuteseka kwa ajili Yake na radhi ya kujitoa wenyewe. Isipokuwa wakikidhi haya masharti mawili haihesabiki kama imani katika Mungu, na hawatakuwa na uwezo wa kufikia mabadiliko ya tabia. Ni watu tu wanaotafuta ukweli kwa kweli, wanaotafuta maarifa ya Mungu, na kufuatilia maisha ndio wale ambao kweli wanaamini katika Mungu.

Wakati majaribio yanakuja juu yako, utaiunganishaje kazi ya Mungu kukabiliana nayo? Je, utakuwa hasi au utaelewa usafishaji wa Mungu wa wanadamu kutoka kwa kipengele chema? Utapata faida gani kutoka kwa usafishaji wako? Je, upendo wako kwa Mungu utakua? Wakati uko chini ya usafishaji, utaweza kuunganisha majaribu ya Ayubu na kuichukulia kazi ya Mungu ndani yako kwa uzito? Je, utaweza kuona jinsi Mungu anawapima wanadamu kwa njia ya majaribio ya Ayubu? Ni aina gani ya mvuto ambao majaribu ya Ayubu yanaweza kuleta kwako? Je, utakuwa tayari kuwa shahidi kwa Mungu katikati ya usafishaji wako, au utataka kuuridhisha mwili katika mazingira ya starehe? Mtazamo wako kuhusu imani kwa Mungu ni upi kwa kweli? Je, kweli ni kwa ajili Yake, na si kwa ajili ya mwili? Je, kweli una lengo la kutafuta kwako? Je, uko tayari kupitia usafishaji ili ufanywe mkamilifu na Mungu, au badala yake ungeona heri kuadibiwa na kulaaniwa na Mungu? Je, hakika unaonaje jambo la kuwa na ushuhuda wa Mungu? Watu wanapaswa kufanya nini katika mazingira fulani ili kwa kweli wawe shahidi wa Mungu? Kwa kuwa Mungu wa utendaji ameonyesha sana kazi ya hakika ndani yako, kwa nini siku zote una mawazo ya kuondoka? Je, imani yako katika Mungu ni kwa ajili ya Mungu? Kwa wengi wenu, ni kwa ajili mipango ya binafsi na harakati za faida binafsi. Watu wachache sana wanaamini katika Mungu kwa ajili ya Mungu—je, huu sio ukaidi?

Kazi ya usafishaji kimsingi ni ya kukamilisha imani ya watu na mwishowe kufikia hali ambapo unataka kuondoka lakini huwezi, ambapo baadhi ya watu wanaondolewa hata kipande cha matumaini lakini bado wanayo imani yao, ambapo watu hawana tena tumaini katika siku za zao za usoni, na kwa wakati huu tu ndio usafishaji wa Mungu utatamatika. Binadamu bado hawajafikia hatua ya kuelea kati ya maisha na kifo—hawajaonja mauti, hivyo usafishaji haupo katika mwisho. Hata wale ambao walikuwa katika hatua ya watenda huduma hawakuwa wamesafishwa kabisa, lakini Ayubu alikuwa amesafishwa, bila kitu cha kutegemea. Watu lazima wapitie usafishaji mpaka ile hatua ambayo hawana matumaini na kitu cha kutegemea—ni hapo tu ndipo huo utakuwa usafishaji. Wakati wa watenda huduma, moyo wako daima ulikuwa umetulia mbele ya Mungu. Bila kujali Alichofanya na bila kujali mapenzi Yake kwa ajili yako yalikuwa nini, wewe daima ulitii mipango Yake na mwishoni mwa barabara, ulielewa kila kitu. Kupitia majaribu ya Ayubu pia ni kupitia majaribu ya Petro. Wakati Ayubu alijaribiwa yeye alikuwa shahidi, na mwishowe Yehova alidhihirishwa kwake. Ni baada tu ya kuwa shahidi ndipo alistahili kuona uso wa Mungu. Kwa nini inasemwa: “Mimi najificha kutoka nchi ya uchafu lakini Najionyesha kwa ufalme mtakatifu”? Hiyo ina maana kwamba wakati tu uko mtakatifu na kuwa shahidi ndipo unaweza kuwa na hadhi ya kuuona uso wa Mungu. Kama huwezi kuwa shahidi kwa ajili Yake, hauna hadhi ya kuuona uso Wake. Ukijiondoa au kulalamika dhidi ya Mungu ukikabiliwa na usafishaji, kushindwa kuwa shahidi Wake na kuwa kichekesho cha Shetani, hutapata sura ya Mungu. Kama wewe ni kama Ayubu, ambaye katikati ya majaribu aliulaani mwili wake na wala hakulalamika dhidi ya Mungu, na aliweza kuuchukia mwili wake bila kulalamika au kutenda dhambi kwa njia ya maneno yake, huko ni kuwa shahidi. Unapopitia usafishaji kwa kiasi fulani na bado unaweza kuwa kama Ayubu, mtiifu kabisa mbele ya Mungu na bila mahitaji mengine Kwake au dhana zako mwenyewe, basi Mungu atakuonekania. Sasa Mungu hakuonekanii kwa sababu una nyingi za dhana zako mwenyewe, maoni yako binafsi, mawazo ya ubinafsi, mahitaji ya binafsi na maslahi ya kimwili, na wewe hustahili kuuona uso Wake. Ukimwona Mungu, utampima kwa njia ya dhana yako mwenyewe—basi ni wewe unayemsulubisha. Kama mambo mengi yanakuja kwako ambayo si sambamba na dhana zako lakini unaweza kuyaweka kando na kujua matendo ya Mungu kutoka kwa mambo haya, na katikati ya usafishaji unadhihirisha moyo wako wa upendo kwa Mungu, huku ni kuwa shahidi. Kama nyumba yako ina amani, unafurahia starehe za mwili, hakuna mtu anayekutesa, na ndugu na dada zako katika kanisa wanakutii, je, unaweza kuonyesha moyo wako wa upendo kwa Mungu? Je, hili linaweza kukusafisha? Ni kwa kupitia katika usafishaji tu ndiyo upendo wako kwa Mungu unaweza kuonyeshwa, na ni kwa mambo yasiyo sambamba na dhana yako kutokea tu ndiyo unaweza kufanywa mkamilifu. Ni kupitia mambo mengi hasi, matatizo mengi ndipo Mungu anakukamilisha. Ni kupitia kwa matendo mengi ya Shetani, shutuma, na udhihirisho wake kwa watu wengi kwamba Mungu anakuruhusu upate ujuzi, hivyo kukufanya uwe mkamilifu.

Ukigusa matendo ya Mungu katika uzoefu wako halisi, Yeye atakuonekania, na kukupa nuru na kukuongoza kutoka ndani. Kama wewe huwezi kutii maneno Yake, Hataweza kufanya hivyo. Kama huna imani, kama umepoteza matumaini katika Mungu, utawezaje kupata uzoefu? Kama una imani ya kweli ndani Yake na huna tashwishi, ukifungua moyo wako Kwake, Atakukamilisha. Atakupa nuru katika hali yako ya vitendo na katika maisha yako. Katika maisha ya watu ya utendaji, wana matatizo mengi ya kibinafsi, na zaidi ya hayo, hawawezi kuona wazi kiasi cha kazi ya Mungu, hivyo hii inahitaji imani. Imani huja tu kupitia kwa usafishaji—haiwezi kuendelea bila ya kusafishwa. Kama una dhana ambazo huwezi kuachilia na unakuza mashaka kwa Mungu, utazama chini katika usafishaji, na katika nyakati hizi unachohitaji zaidi ni imani.

Uzoefu wako mwingi wa kushindwa, udhaifu, na nyakati za uhasi vinaweza kusemekana kuwa majaribio ya Mungu kwako. Hii ni kwa sababu kila kitu hutoka kwa Mungu, mambo yote na matukio yako katika mikono Yake. Kama unashindwa au kama wewe ni dhaifu na unajikwaa yote yako kwa Mungu na vipo katika mfumbato Wake. Kutoka kwa upande wa Mungu, haya ni majaribio yako, na kama huwezi kutambua hivyo, yatageuka majaribu. Kuna aina mbili za hali ambazo watu wanapaswa kutambua: Moja inatoka kwa Roho Mtakatifu, na nyingine huenda inatoka kutoka kwa Shetani. Hali moja ni kwamba Roho Mtakatifu anakuangazia na Anakuruhusu upate kujijua mwenyewe, kuchukia na kujuta mwenyewe na kuweza kuwa na upendo wa kweli kwa Mungu, kuweka moyo wako katika kumridhisha Yeye. Hali nyingine ni kwamba unajijua mwenyewe, lakini wewe ni hasi na dhaifu. Inaweza kusemwa kuwa huo ni usafishaji wa Mungu. Inaweza pia kusemwa kuwa ni majaribu ya Shetani. Ukitambua kuwa huu ni wokovu wa Mungu kwako na kuwa wewe ni mdeni Wake mkubwa, na kama kuanzia sasa utajaribu kulipa deni Lake na usianguke tena katika upotovu kama huo, kama utaweka juhudi katika kula na kunywa maneno Yake, na kama siku zote unajichukua kama anayekosa, na kuwa na moyo wa hamu, basi haya ni majaribu ya Mungu. Baada ya mateso kumalizika na wewe kwa mara nyingine tena unasonga mbele, Mungu bado atakuongoza, atakuangazia, atakupa nuru, na kukustawisha. Lakini kama hulitambui na wewe ni hasi, kujiachilia tu kukata tamaa, kama unafikiri hivi, basi jaribio la Shetani limekufikia. Wakati Ayubu alipitia majaribio, Mungu na Shetani walikuwa wanawekeana dau, na Mungu alimruhusu Shetani amtese Ayubu, kumjaribu. Hata ingawa ilikuwa ni Mungu aliyekuwa anamjaribu Ayubu, hakika alikuwa ni Shetani ndiye aliyemjia. Kwa Shetani, ilikuwa ni kumjaribu Ayubu, lakini Ayubu alikuwa upande wa Mungu na kama haingekuwa vile, angeanguka katika majaribu. Mara baada ya watu kuanguka katika majaribu wao huanguka katika hatari. Kupitia usafishaji inaweza kusemwa kuwa jaribio kutoka kwa Mungu, lakini kama hauko katika hali nzuri inaweza kusemwa kuwa majaribu kutoka kwa Shetani. Kama hauko na uwazi juu ya maono, Shetani atakushutumu na kukuchanganya. Kabla ya kujua, utaanguka katika majaribu.

Kama hupitii kazi ya Mungu kamwe hutaweza kufanywa mkamilifu. Katika mapito yako, lazima pia uingie katika maelezo madogo—unawezaje kukuza dhana zako na nia nyingi sana? Ni matendo ya aina gani yanayofaa uliyo nayo kwa haya? Kama unaweza kupitia kazi ya Mungu, hii ina maana kwamba una kimo. Kama unaonekana tu kuwa na nguvu, hiki si kimo halisi na wewe huwezi kuchukua msimamo kabisa. Ni wakati tu mnaweza kupata uzoefu wa kazi ya Mungu na kutafakari kazi ya Mungu wakati wowote, mahali popote, mnaweza kumwacha mchungaji, muishi kivyenu kwa kumtegemea Mungu, na mnaweza kuona matendo halisi ya Mungu, ni hapo tu ndipo mapenzi ya Mungu yatatimizwa. Sasa hivi, watu wengi hawajui jinsi ya kulipitia. Wanapokumbana na suala hawajui jinsi ya kulishughulikia, hawawezi kuipitia kazi ya Mungu, na hawezi kuishi maisha ya kiroho. Lazima uchukue maneno ya Mungu na kuyafanya ndani ya maisha yako ya utendaji.

Wakati mwingine Anakupa aina fulani ya hisia—unapoteza starehe yako ya ndani, unapoteza uwepo wa Mungu, na wewe unakuwa katika giza. Hii ni aina ya usafishaji. Wakati wowote unapofanya kitu kinaenda mrama au kugonga ukuta. Hii ni nidhamu ya Mungu. Unaweza kufanya kitu na usiwe na hisia yoyote dhahiri kukihusu, na wengine hawajui pia, lakini Mungu anajua. Yeye hatakuacha, na Atakufundisha nidhamu. Kazi ya Roho Mtakatifu ni yenye kina sana. Kwa makini sana Anatazama kila neno na tendo la watu, kila tendo na mwendo wao, na kila wazo lao na fikira ili watu waweze kupata ufahamu wa ndani wa vitu hivi. Unafanya kitu mara moja na kinaenda mrama, unakifanya tena na bado kinaenda mrama, na hatua kwa hatua utapata kuelewa kazi ya Roho Mtakatifu. Kupitia mara nyingi za kufundishwa nidhamu, utajua cha kufanya ili kuwa sambamba na mapenzi ya Mungu na kile kisichoambatana na mapenzi Yake. Mwishowe, utakuwa na majibu sahihi kwa uongozi wa Roho Mtakatifu ndani yako. Wakati mwingine utakuwa muasi na utakemewa na Mungu kutoka ndani. Haya yote hutoka kwa nidhamu ya Mungu. Kama humthamini Mungu, kama unaidharau kazi Yake, Hatashughulika nawe hata kidogo. Kadiri unavyomchukua Mungu kwa makini, ndivyo Atakavyokupa nuru zaidi. Sasa hivi, kuna baadhi ya watu katika kanisa ambao wana imani iliyovurugwa na yenye kuchanganyikiwa, na wao hufanya mambo mengi yasiyofaa bila nidhamu, na hivyo kazi ya Roho Mtakatifu haiwezi kuonekana wazi ndani yao. Baadhi ya watu hupigana, hupata fedha, na kufanya biashara bila nidhamu yoyote, na mtu wa aina hiyo yuko katika hatari zaidi. Siyo tu kwamba sasa hawana kazi ya Roho Mtakatifu, lakini katika siku zijazo wao watakuwa wagumu kukamilisha. Kuna watu wengi ambao kwao kazi ya Roho Mtakatifu haiwezi kuonekana, ambao nidhamu ya Mungu haiwezi kuonekana kwao. Wao ni wale ambao hawako wazi juu ya mapenzi ya Mungu na ni wasiojua kazi Yake. Wale ambao wanaweza kusimama imara katikati ya usafishaji, wanaofuata Mungu bila kujali Anachofanya, na angalau wanaweza kutoondoka, au kutimiza 0.1% ya kile ambacho Petro alitimiza wanafanya vyema, lakini hawana thamani kwa ajili ya matumizi. Watu wengi huelewa mambo haraka, wana upendo wa kweli kwa Mungu, na wanaweza kuzidi kiwango cha Petro. Mungu hufanya aina hii ya kazi, na mtu wa aina hii anaweza kupata nidhamu na nuru Yake na kwa haraka kutupa mbali chochote ambacho si sambamba na mapenzi ya Mungu. Mtu wa aina hii ni kama dhahabu—ni mtu wa aina hii tu ndiye mwenye thamani! Kama Mungu amefanya aina nyingi za kazi lakini bado uko kama mchanga, kama jiwe, basi huna thamani!

Kazi ya Mungu katika nchi ya joka kubwa jekundu ni ya ajabu na isiyoeleweka. Yeye ataondoa baadhi ya watu kwa sababu kuna kila aina ya watu katika kanisa—kuna watu ambao hutumia fedha za kanisa, wale ambao wanawadanganya wengine, na zaidi. Kama hujui kwa uwazi kazi ya Mungu utakuwa hasi; hii ni kwa sababu kazi ya Mungu inaweza tu kuonekana katika watu wachache. Wakati huo itakuwa wazi ni nani ambao wanampenda Mungu kwa kweli na wasiompenda. Wale ambao kweli wanampenda Mungu wana kazi ya Roho Mtakatifu, wale ambao hawampendi kwa kweli watafichuliwa kupitia kazi Yake, hatua moja kwa wakati. Watakuwa walengwa wa kuondolewa. Watu hawa watafichuliwa katika kipindi cha kazi ya ushindi—hawana thamani ya kufanywa wakamilifu. Na wale ambao wamekamilishwa wamepatwa na Mungu katika ukamilifu wao wote, na wana uwezo wa kumpenda Mungu kama vile Petro. Wale ambao wameshindwa hawana upendo wa hiari, lakini wana upendo usioonyesha hisia, na wao wanalazimika kumpenda Mungu. Upendo wa hiari unakuzwa kwa njia ya uelewa uliopatikana kupitia uzoefu wa vitendo. Upendo huu unachukua moyo wa mtu na unamfanya kujitolea kwa Mungu kwa hiari; maneno ya Mungu yanakuwa msingi wao na wanaweza kuteseka kwa ajili ya Mungu. Bila shaka haya ni mambo yanayomilikiwa na mtu ambaye amekamilishwa na Mungu. Kama unataka tu kushindwa, basi huwezi kuwa na ushuhuda kwa Mungu; kama Mungu angetimiza tu lengo Lake la wokovu kwa njia ya kuwashinda watu, basi hatua ya watenda huduma ingekuwa inatosha. Hata hivyo, kuwashinda watu si lengo la mwisho la Mungu—lengo Lake la mwisho ni kuwakamilisha watu. Hivyo badala ya kusema kwamba hatua hii ni kazi ni ya kuwashinda watu, sema kuwa ni kazi ya kukamilisha na kuondoa. Baadhi ya watu hawajashindwa kabisa, na katika harakati ya kuwashinda, kundi la watu watafanywa wakamilifu. Vipande hivi viwili vya kazi vinafanywa kwa pamoja. Watu hawajaondoka kwa muda mrefu sana kama huu wa kazi; ukweli huu unaonyesha kuwa lengo la ushindi limekuwa na mafanikio—huu ni ukweli wa kushindwa. Usafishaji si kwa ajili ya kushindwa, lakini ni kwa ajili ya kukamilishwa. Bila usafishaji, watu hawangeweza kukamilishwa. Hivyo usafishaji ni wa thamani! Leo kundi moja la watu linakamilishwa, kundi moja la watu linapatwa. Baraka kumi zilizotajwa hapo awali zote zililengwa kwa wale ambao wamekamilishwa. Kila kitu kuhusu kubadilisha sura zao duniani kunalenga wale ambao wamekamilishwa. Wale ambao hawajakamilishwa hawezi kufanikisha hili.

Tanbihi:

a. Maandishi asilia yanaacha “majaribu ya.”

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Soma Zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Asili ya Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni