Smiley face
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Roho-Mtakatifu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Roho-Mtakatifu. Onyesha machapisho yote

Jumanne, 15 Oktoba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Kunayo mambo mengi ambayo Ninatumai mtaweza kufikia. Hata hivyo, matendo yenu na maisha yenu yote hayawezi kutimiza kwa ujumla mahitaji Yangu, kwa hiyo lazima Nilenge suala moja kwa moja na kuwafafanulia moyo na akili Zangu. Tukichukulia kwamba uwezo wenu wa utambuzi na ufahamu wenu vyote ni duni sana, karibu mmekosa kabisa kujua tabia na dutu Yangu, na hivyo ni suala la dharura kwangu Mimi kuwafahamisha kuhusu haya. Haijalishi hapo awali ulielewa kiwango kipi au kama uko radhi kuelewa masuala haya, lazima bado Niyaelezee kwenu kwa undani.

Jumatatu, 14 Oktoba 2019

Neno la Mwenyezi Mungu|Maonyo Matatu

Kazi ya Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu

Neno la Mwenyezi Mungu|Maonyo Matatu

Kama muumini wa Mungu, hamfai kuwa watiifu kwa yeyote mwingine isipokuwa Yeye katika mambo yote na mjilinganishe na moyo Wake katika mambo yote. Hata hivyo, ingawa wote huelewa mafundisho haya, ukweli huu wa kimsingi ulio wazi kabisa kwa binadamu hauwezi kuonekana kuwa kujumuishwa kwao kikamilifu, kutokana na ugumu wao, kama vile hali yao ya kutojua, upuzi, au ufisadi. Kwa hivyo, kabla mwisho wenu haujaamuliwa, Ninafaa kuwaambia kwanza baadhi ya mambo, ambayo ni yenye umuhimu mkubwa sana kwenu.

Jumapili, 13 Oktoba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Wewe U Mwaminifu kwa Nani?

kazi ya Mungu,Sauti ya Mungu,kumjua Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Wewe U Mwaminifu kwa Nani?

Kila siku mnayoiishi sasa ni ya maana sana na muhimu sana kwa hatima yenu na majaliwa yenu, kwa hivyo mnapaswa kufurahia kila mlicho nacho na kila dakika inayopita. Mnapaswa kutumia muda wenu vizuri ili muweze kujinufaisha, ili msije kuishi maisha haya bure. Pengine mnajihisi kukanganyikiwa mnaojiuliza ni kwa nini Ninazungumza maneno haya. Kwa kweli, Sijapendezwa na matendo ya yeyote kati yenu. Kwa maana matumaini ambayo Nimekuwa nayo juu yenu si vile tu mlivyo sasa. Kwa hivyo, Naweza kuelezea hivi: Nyinyi nyote mko hatarini kabisa. Vilio vyenu vya kwanza kwa ajili ya wokovu na matamanio yako ya kwanza ya kufuatilia ukweli na kutafuta nuru vinakaribia mwisho.

Ijumaa, 11 Oktoba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Kazi ya Mungu,neno la Mungu,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Njia ya maisha si kitu ambacho kinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, wala hakipatikani kwa urahisi na wote. Hiyo ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote.

Alhamisi, 10 Oktoba 2019

Neno la Mwenyezi Mungu|Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu



Neno la Mwenyezi Mungu|Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu

Enzi ya zama ishaenda, na enzi mpya imefika. Mwaka baada ya mwaka na siku baada ya siku, Mungu amefanya kazi nyingi. Alikuja duniani, kisha Akaondoka. Mzunguko kama huu umeendelea kwa vizazi vingi. Siku ya leo, Mungu anaendelea kama mbeleni kufanya kazi Anayopaswa kufanya, kazi ambayo bado Hajaikamilisha, kwani hadi leo, bado Hajaingia mapumzikoni. Kutoka wakati wa uumbaji hadi leo, Mungu amefanya kazi nyingi, lakini ulijua kwamba kazi anayoifanya Mungu leo ni nyingi kuliko awali na kipimo ni kikubwa zaidi? Hii ndiyo maana Nasema Mungu amefanya jambo kubwa miongoni mwa wanadamu.

Alhamisi, 3 Oktoba 2019

Matamshi ya Kristo | Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Je, ungependa kumwona Yesu? Je, ungependa kuishi na Yesu? Je, ungependa kuyasikia maneno yaliyonenwa na Yesu? Iwapo ni hivyo, basi utakaribishaje kurudi kwa Yesu? Je, uko tayari kabisa? Utakaribisha kurudi kwa Yesu kwa namna gani? Nafikiri kuwa kila ndugu anayemfuata Yesu angependa kumpa Yesu makaribisho mazuri. Lakini Je, mmewaza iwapo mtamjua Yesu kweli Atakaporejea? Je, mtaelewa kweli kila kitu Atakachosema? Je, mtakubali kweli, bila masharti, kila kazi ambayo Anafanya? Wale wote ambao wamesoma Biblia wanajua kuhusu kurudi kwa Yesu, na wale wote ambao wamesoma Biblia wanangoja kwa makini kuja Kwake. 

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Pili)

kazi ya Mungu,Neno la Mungu,ukweli

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Pili)

Punde tu Shetani anaposhindwa, hivyo ni kusema, punde tu mwanadamu anaposhindwa kabisa, mwanadamu ataelewa kwamba kazi yake yote ni kwa ajili ya wokovu, na kuwa mbinu ya wokovu huu ni kurejesha kutoka kwa mikono ya Shetani. Miaka 6,000 ya kazi ya Mungu ya usimamizi imegawanywa katika awamu tatu: Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Awamu hizi zote tatu za kazi ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, ambayo ni kusema, ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu ambaye ameharibiwa na Shetani kwa kiasi kikubwa. Wakati huo huo, hata hivyo, pia ni ili kwamba Mungu afanye vita na Shetani.

Jumapili, 29 Septemba 2019

Matamshi ya Kristo| Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Pili)

Wakati kazi ya Mungu inafikia hatua fulani, na usimamizi Wake kufikia hatua fulani, wale wanaoutafuta moyo Wake wote huwa na uwezo wa kutimiza matakwa yake. Mungu humwekea mwanadamu matakwa kulingana na viwango Vyake mwenyewe, na kulingana na kile ambacho mwanadamu anaweza kufanikisha. Akiwa anazungumzia usimamizi Wake, Yeye humwonyesha njia mwanadamu , na kumpa mwanadamu namna ya kudumu. Usimamizi wa Mungu na vitendo vya mwanadamu vipo katika hatua sawia kikazi, na yote yanafanyika kwa wakati mmoja. Mazungumzo kuhusu usimamizi wa Mungu yanagusia mabadiliko katika tabia ya mwanadamu, na yanazungumzia kuhusu yale yafaayo kufanywa na mwanadamu, na mabadiliko katika tabia ya mwanadamu, hugusia kazi ya Mungu; hakuna wakati ambao haya mawili yanaweza kutenganishwa.

Jumamosi, 28 Septemba 2019

Matamshi ya Kristo|Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza)

Kazi ya Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu haitengani na mwanadamu, kwa kuwa mwanadamu ni chombo cha kazi hii na kiumbe wa pekee aliyeumbwa na Mungu anayeweza kutoa ushuhuda kwa Mungu. Maisha ya mwanadamu na shughuli zake zote havitengani na Mungu, na vyote vinaongozwa na mkono wa Mungu, na inaweza kusemwa kuwa hakuna mtu anayeweza kuishi bila Mungu. Hakuna anayeweza kupinga hili, kwani ndio ukweli. Kila Akifanyacho Mungu ni kwa faida ya mwanadamu, na kinalenga hila za Shetani. Kila anachokihitaji mwanadamu kinatoka kwa Mungu, na Mungu ndiye chanzo cha maisha ya mwanadamu.

Jumatano, 25 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu | Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Kwanza)

Kupata Mwili,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Mungu alifanyika mwili kwa sababu lengo la kazi Yake si roho ya Shetani, au kitu chochote kisicho cha mwili, ila mwanadamu, ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa na Shetani. Ni kwa sababu hii kabisa kwamba mwili wa mwanadamu umeharibiwa ndio maana Mungu akamfanya mwanadamu mwenye mwili kuwa mlengwa wa kazi Yake; aidha, kwa sababu mwanadamu ni mhusika wa uharibifu, Amemfanya mwanadamu kuwa mlengwa wa kazi Yake katika hatua zote za kazi Yake ya wokovu. Mwanadamu ni kiumbe anayekufa, ni wa mwili na damu, na Mungu ndiye tu Anayeweza kumwokoa mwanadamu. Kwa namna hii, Mungu ni lazima Awe mwili ambao una tabia zinazofanana na mwanadamu ili Aweze kufanya kazi Yake, ili kwamba kazi Yake iweze kupata matokeo mazuri zaidi.

Jumanne, 24 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu | Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Pili)


Kazi ya Mungu Mwenyewe ni maono ambayo mwanadamu lazima afahamu, kwa kuwa kazi ya Mungu haiwezi kutekelezwa na mwanadamu, wala haimilikiwi na mwanadamu. Hatua tatu za kazi ndizo ukamilifu wa usimamizi wa Mungu, na hakuna ono kuu kuliko hili linalopaswa kufahamika kwa mwanadamu. Kama mwanadamu hafahamu maono haya makuu, basi si rahisi kumjua Mungu, na si rahisi kujua mapenzi ya Mungu, na, zaidi ya hayo, njia ambayo mwanadamu anapitia inazidi kuwa ngumu. Bila maono, mwanadamu hangeweza kufika umbali huu.

Jumatatu, 23 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu|Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Kwanza)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu.

Jumamosi, 21 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu | Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea (Sehemu ya Pili)


Petro alifanywa mkamilifu kwa kupitia ushughulishaji na usafishaji. Alisema, “Mimi ni lazima nikidhi mapenzi ya Mungu wakati wote. Kwa yote nifanyayo mimi natafuta tu kukidhi mapenzi ya Mungu, na kama mimi ninaadibiwa, au kuhukumiwa, bado nina furaha kufanya hivyo.” Petro alimpa Mungu kila kitu chake, na kazi yake, maneno, na maisha yote yalikuwa yote kwa ajili ya kumpenda Mungu. Alikuwa mtu ambaye alitafuta utakatifu, na alipopitia zaidi, ndivyo upendo wake wa Mungu ndani ya moyo wake ulikuwa mkubwa zaidi. Paulo, wakati huo huo, alifanya tu kazi ya nje, na ingawa alitia bidii katika kazi yake, juhudi zake zilikuwa kwa ajili ya kufanya kazi yake vizuri na hivyo kupata tuzo.

Jumanne, 17 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu|Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu


Ni lazima myafahamu maono ya kazi ya Mungu na mpate mwelekeo wa kazi Yake. Huku ni kuingia kwa njia nzuri. Punde mnapong’amua ukweli wa maono kwa usahihi, kuingia wako utakuwa salama; bila kujali kazi Yake hubadilika kiasi gani, utaendelea kuwa imara moyoni mwako, utakuwa wazi kuhusu maono, na utakuwa na lengo la kuingia na kazi yako. Kwa njia hiyo, tajriba na ufahamu ulio ndani yako utakua kwa kina na kutakaswa zaidi. Punde unapong’amua ukweli wote, hutapoteza kitu maishani na hutapotea. Kama hutazijua hatua hizi za kazi, utapata hasara kwa kila mojawapo. Huwezi kugeuka baada ya siku chache tu na hutaweza kuipata njia mwafaka hata katika majuma machache.

Jumamosi, 14 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu|Wale Waliofanywa Kuwa Watimilifu Ndio tu Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Kwa kweli, kazi inayofanywa sasa ni kuwafanya watu kumtoroka Shetani, kutoroka babu zao wa kale. Hukumu zote kwa neno zinalenga kufichua tabia potovu ya binadamu na kuwawezesha watu kuelewa kiini cha maisha. Hukumu hizi zote zilizorudiwa zinapenyeza mioyo ya watu. Kila hukumu inaathiri kwa njia ya moja kwa moja hatima yao na inalenga kujeruhi mioyo yao ili waweze kuachilia yale mambo yote husika na hivyo basi kuja kujua maisha, kuujua ulimwengu huu mchafu, na pia kujua hekima ya Mungu na uweza Wake na kujua mwanadamu huyu aliyepotoshwa na Shetani. Kwa kadri aina hii ya kuadibu na kuhukumu inapozidi, ndivyo moyo wa binadamu unavyoweza kujeruhiwa zaidi na ndivyo roho yake inavyoweza kuzinduliwa zaidi.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kuhusu Majina na Utambulisho (Sehemu ya Pili)

Yesu,Mungu Kupata Mwili,kumjua Mungu

Mwanzoni, wakati Yesu alikuwa bado hajafanya rasmi huduma Yake, kama wanafunzi waliomfuata, wakati mwingine pia Yeye alihudhuria mikutano, na kuimba tenzi, Akasifu, na kusoma Agano la Kale kwa hekalu. Baada Yeye kubatizwa na kupanda, Roho alishuka rasmi juu yake na kuanza kufanya kazi, Akifichua utambulisho Wake na huduma Aliyokuwa afanye. Kabla ya haya, hakuna aliyejua utambulisho Wake, na mbali na Maria, hata Yohana hakujua. Yesu alikuwa 29 Alipobatizwa. Baada ya ubatizo wake kukamilika, mbingu zilifunguliwa, na sauti ikasema: “Huyu ni Mwana wangu Mpendwa, ambaye Ninapendezwa naye.” Baada ya Yesu kubatizwa, Roho Mtakatifu alianza kumshuhudia kwa njia hii.

Alhamisi, 12 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu: Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo (Sehemu ya Pili)


Kwanza Mungu alimwumba Adamu na Hawa, na pia Alimwumba nyoka. Miongoni mwa mambo haya yote, nyoka ndiye aliyekuwa mwenye sumu zaidi; mwili wake ulikuwa na sumu, na Shetani aliitumia sumu hiyo ili kufaidika. Ni nyoka aliyemjaribu Hawa hadi akatenda dhambi. Adamu alitenda dhambi baada ya Hawa kutenda, na wawili hawa waliweza kutofautisha kati ya mema na maovu. Kama Yehova Alikuwa Amejua kwamba nyoka angemjaribu Hawa, na kwamba Hawa angemjaribu Adamu, kwa nini Akawaweka wote pale katika bustani? Kama Aliweza kutabiri mambo haya kwa nini Akamwumba nyoka na kumweka ndani ya Bustani ya Edeni? Kwa nini Bustani ya Edeni ilikuwa na tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya? Alinuia wao walile hilo tunda? Wakati Yehova alipokuja, Adamu wala Hawa hawakuthubutu kumkabili Yeye, na ulikuwa tu wakati huu ambapo Yehova alijua kwamba walikuwa wamelila tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya na kujipata katika ujanja wa yule nyoka.

Jumatano, 11 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu | Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo (Sehemu ya Kwanza)


Ukamilifu wa kazi ya miaka 6,000 yote umebadilika kwa utaratibu kuambatana na nyakati. Mabadiliko katika kazi hii yamefanyika kulingana na hali za ulimwengu mzima. Kazi ya usimamizi ya Mungu imebadilika tu kwa utaratibu kulingana na mitindo ya kimaendeleo ya binadamu kwa ujumla; haikuwa imepangwa tayari mwanzoni mwa uumbaji. Kabla ya ulimwengu kuumbwa, au punde tu baada ya kuumbwa kwake, Yehova bado hakuwa amepanga hatua ya kwanza ya kazi, ile ya sheria; hatua ya pili ya kazi, ile ya neema; au hatua ya tatu ya kazi, ile ya kushinda, ambapo Angefanya kazi kwanza miongoni mwa kundi la watu—baadhi ya vizazi vya Moabu, na kutokana na hili Angeweza kuushinda ulimwengu mzima. Hakuyaongea maneno haya baada ya kuumba ulimwengu; Hakuyaongea maneno haya baada ya Moabu, wala hata kabla ya Lutu. Kazi Yake yote ilifanywa bila kupangwa.

Jumanne, 3 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu | Inapofikia Mungu, Ufahamu Wako ni Upi?


Watu wamemwamini Mungu kwa muda mrefu, ilhali wengi wao hawaelewi maana ya neno “Mungu”. Wanafuata tu bila kufahamu vyema. Hawajui sababu ya ni kwa nini binadamu anafaa kumwamini Mungu ama Mungu ni nini hasa. Iwapo watu wanajua tu kumfuata na kuamini Mungu, na hawajui Mungu ni nini, wala hawamwelewi Mungu, si huo ni mzaha mkuu ulimwenguni? Ingawa watu wameshuhudia matukio ya kiajabu ya mbinguni wakati huu na wamepata kusikia kuhusu elimu kuu ambayo mwanadamu hajapata kuwa nayo awali, bado wako gizani kuhusu mambo mengi ya kawaida, na ambao ni ukweli ambao haujafikiriwa.

Jumanne, 27 Agosti 2019

Sauti ya Mungu|Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

Mungu Kupata Mwili,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Wokovu wa Mungu

Kila hatua ya kazi iliyofanywa na Mungu ina umuhimu mkubwa. Yesu alipokuja, Alikuwa mwanaume, na wakati huu Yeye ni mwanamke. Kutokana na hili, unaweza kuona kwamba Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke kwa ajili ya kazi Yake na Kwake hakuna tofauti ya jinsia. Roho Wake anapowasili, Anaweza kuchukua umbo la mwili wowote kwa matakwa Yake na mwili unamwakilisha Yeye. Awe mwanamume au mwanamke, wote wanamwakilisha Mungu ili mradi tu ni Mungu mwenye mwili. Kama Yesu angekuja na Angeonekana kama mwanamke, kwa maneno mengine, iwapo mtoto wa kike, sio wa kiume, angezaliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu, hatua hiyo ya kazi ingeweza kukamilika pia.