Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Tatu
Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Namna Ambavyo Mungu Huanzisha Matokeo Ya Binadamu na Kiwango Ambacho Hutumia Kuasisi Matokeo ya Binadamu
Swali la Kiutendaji Huleta Aina Zote za Aibu kwa Watu
Soma Zaidi:
Mwenyezi Mungu anasema, “Kunayo aina nyingine ya mtu aliye na matokeo mabaya zaidi kati ya yote. Hawa ndio Nisiopenda kutaja sana. Hali si mbaya kwa sababu mtu huyu hupokea adhabu ya Mungu, au kwamba mahitaji ya Mungu kwao ni makali na wana matokeo mabaya. Badala yake, hali ni mbaya kwa sababu wanajifanyia wenyewe, kama inavyosemwa mara kwa mara: Wanajichimbia kaburi lao. Mtu kama huyu ni aina gani? Mtu huyu hatembei kwenye njia inayofaa, na matokeo yake yanafichuliwa mapema. Mungu humwona mtu wa aina hii kama lengo Lake kubwa zaidi la chuki Yake. Kama watu wanavyosema hawa ndio wa huzuni kuliko wote. Mtu wa aina hii ni mwenye shauku anapoanza kumfuata Mungu; wanalipia bei nyingi; wanayo maoni mazuri kuhusu mtazamo wa kazi ya Mungu; kufikiria kwao ni kwingi kuhusu mustakabali wao binafsi; wao hasa wanayo imani katika Mungu, wanasadiki kwamba Mungu anaweza kumfanya binadamu kuwa kamili, na kumfanya huyo binadamu kufikia hatima yenye utukufu. Ilhali kwa sababu isiyoeleweka, mtu huyu kisha hukimbia akiwa katika harakati ya kazi ya Mungu. Ni nini maana ya mtu huyu kukimbia? Maana yake ni kwamba wanatoweka bila kwaheri, bila sauti yoyote. Wanaondoka bila kutaja neno lolote. Ingawa mtu wa aina hii anadai kuwa anasadiki Mungu, huwa haweki kamwe mizizi yoyote kwenye njia ya kusadiki Mungu. Hivyo basi, haijalishi ni kwa muda upi wamesadikia, bado wanaweza kumgeuka Mungu. Baadhi ya watu huondoka ili kufanya biashara, baadhi ya watu huondoka ili kuishi maisha yao, baadhi ya watu huondoka ili kutajirika, baadhi ya watu huondoka kuoa au kuolewa, kuwa na watoto…. Miongoni mwa wale wanaondoka, kunao wanaopata shambulizi la nadhari na wanataka kurudi, na wengine wanaoendelea vibaya sana kimaisha, wanaishi maisha tu na kuyasukuma kwa miaka na miaka. Wasukuma maisha hawa wamepitia mateso mengi, na wanasadiki kwamba kuwa ulimwenguni kuna maumivu mno, na hawawezi kutenganishwa na Mungu. Wanataka kurudi nyumba ya Mungu ili kupokea tulizo, amani, furaha, na kuendelea kusadiki katika Mungu ili kukwepa janga, au kuokolewa na kupata hatima nzuri. Hii ni kwa sababu watu hawa wanasadiki kwamba upendo wa Mungu hauna mipaka, kwamba neema ya Mungu haiwezi kuisha na kwamba haiwezi kutumika yote. Wanasadiki kwamba haijalishi ni nini mtu amefanya, Mungu anafaa kumsamehe na kuvumilia maisha yao ya kale. Watu hawa wanasema kwamba wanataka kurudi na kutekeleza wajibu wao. Kuna wale ambao hata wanatoa msaada wa baadhi ya mali yao kwa kanisa, wakitumai kwamba hii ndiyo njia yao ya kurudi katika nyumba ya Mungu. Mwelekeo wa Mungu kwa watu aina hii ni upi? Mungu anafaa kuanzisha vipi matokeo yao? Kuwa huru kuongea. (Ulifikiri kwamba Mungu angewakaribisha watu wa aina hii, lakini baada ya kusikia kwamba sasa hivi, pengine hawatakaribishwa tena.) Na wewe unafikiria vipi? (Mtu wa aina hii huja mbele ya Mungu ili matokeo yao yasije yakawa yale ya kifo. Hawafanyi hivyo kutokana na uaminifu wa kweli. Badala yake, kutokana na maarifa kwamba kazi ya Mungu itakamilika hivi karibuni, wanadanganyika kuwa watapata baraka.) Unasema kwamba mtu huyu kwa kweli hasadiki katika Mungu, na hivyo basi Mungu hawezi kumkubali? Ndivyo ilivyo? (Ndiyo.) (Uelewa wangu ni kwamba mtu wa aina hii ni yule wa kujali maslahi yake kuliko uhaki wa jambo, na kwamba hamsadiki Mungu kwa dhati.) Hajapata kumsadiki Mungu; yeye ni mtu mwenye kuangalia maslahi yake kuliko haki. Yamesemwa vizuri! Watu hawa wanaojali maslahi yao ni wale ambao kila mmoja anawachukia. Wanaenda na mkondo tu, na hawawezi kusumbuliwa ili kufanya kitu isipokuwa kama watafaidi kwa jambo hilo. Bila shaka wanastahili dharau! Je, kati ya ndugu zangu wengine kunaye anayo maoni? (Mungu hatawakubali tena kwa sababu kazi ya Mungu karibu inakamilika na sasa ndipo matokeo ya watu yanaandaliwa. Ni wakati huu ambapo watu hawa wanataka kurudi. Si kwa sababu kwa kweli wanataka kufuata ukweli; wanataka kurudi kwa sababu wanayaona majanga yakishushwa, au wanashawishiwa na mambo ya nje. Kama kweli walikuwa na moyo uliokuwa ukifuatilia ukweli, wasingewahi kukimbia wakiwa katikati ya safari.) Je, yapo maoni mengine? (Hawatakubaliwa. Kwa kweli Mungu aliwapa fursa lakini mwelekeo wao kwake Mungu ulikuwa siku zote kutomsikiliza. Bila kujali nia za mtu huyu ni zipi, na hata kama atatubu, Mungu bado hatamkubali. Hii ni kwa sababu Mungu tayari aliwapa fursa nyingi ajabu ilhali wao walionyesha mtazamo wao: Walitaka kumwacha Mungu. Hivyo basi, watakaporudi sasa, Mungu hatawakaribisha.) (Ninakubali pia kwamba Mungu hatamkaribisha mtu wa aina hii, kwa sababu kama mtu ameona njia ya kweli, akapitia kazi ya Mungu kwa kipindi kirefu kama hicho, na bado anaweza kurudi kwa ulimwengu, kurudi kwa kumbatio la Shetani, basi huu ni usaliti mkuu kwa Mungu. Licha ya hoja kwamba kiini cha Mungu ni rehema, ni upendo, inategemea ni mtu wa aina gani ambaye kiini hicho kinaelekezwa kwake. Kama mtu huyu atakuja mbele ya Mungu akitafuta faraja, kitu cha kuwekea tumaini lake, basi mtu wa aina hii kwa kweli si mtu anayemsadiki Mungu kwa dhati, na rehema za Mungu kwake zinafika hapo.) Kiini halisi cha Mungu ni rehema, kwa hivyo ni kwa nini Hampatii mtu wa aina hii rehema zaidi kidogo tu? Kwa rehema kidogo, hawapati fursa? Awali, mara nyingi ilisemekana: Mungu anamtaka kila mmoja kuokolewa, na hataki mtu yeyote kuangamia. Kama kondoo mmoja miongoni mwa kondoo mia moja atapotea, Mungu atawaacha wale kondoo tisini na tisa kumtafuta yule kondoo aliyepotea. Siku hizi, kuhusiana na mtu wa aina hii, kama ni kwa minajili ya kusadiki kwao kwa Mungu, je, Mungu anafaa kuwakaribisha na kuwapa fursa ya pili? Kwa kweli hilo si swali gumu; ni rahisi mno! Kama kwa kweli mnamtambua Mungu na mnao uelewa halisi wa Mungu, basi hamna ufafanuzi mwingi unaohitajika; hamna kukisia kwingi kunahitajika vilevile, kweli? Majibu yenu yamo katika njia sahihi, lakini bado upo umbali fulani kati yao na mwelekeo wa Mungu.
Sasa hivi tu kulikuwepo na baadhi yenu mliokuwa na hakika kwamba Mungu asingeweza kumkubali mtu wa aina hii. Wengine hawakuwa na hakika sana kuwa Mungu anaweza kuwakubali, na huenda asiwakubali—mwelekeo huu ndio ule wa wastani; na kisha kulikuwa na wale ambao mtazamo wao ulikuwa kwamba wanatumai kwamba Mungu atamkaribisha mtu wa aina hii—huu ndio mwelekeo ule usioeleweka. Wale walio na mwelekeo hakika wanasadiki kuwa Mungu ameshughulika mpaka sasa, na shughuli Yake imekamilika, hivyo basi Mungu hahitaji kuwa mvumilivu na watu hawa, na kwamba Hatawakaribisha tena. Wale watu wa wastani wanasadiki kwamba masuala haya yanafaa kushughulikiwa kulingana na hali inayoyazunguka: Kama moyo wa mtu huyu hauwezi kutenganishwa na wa Mungu, na bado wao ni watu wanaomsadiki Mungu kwa kweli, mtu anayefuatilia ukweli, basi Mungu hafai kukumbuka udhaifu na makosa yao ya awali; Anafaa kuwasamehe, na kuwapa fursa nyingine, kuwaruhusu kurudi katika nyumba ya Mungu, na kukubali wokovu wa Mungu. Hata hivyo, kama mtu huyu atatoroka kwa mara nyingine, hapo ndipo Mungu hatataka mtu huyu na kitendo hiki hakitachukuliwa kuwa cha ukiukaji wa haki. Kunalo kundi jingine ambalo linatumaini kwamba Mungu anaweza kumkaribisha mtu huyu. Kundi hili halina uhakika sana kama Mungu anawakaribisha au la. Kama wanaamini kwamba Mungu anafaa kuwakaribisha, lakini Mungu asiwakaribishe, basi yaonekana kwamba wamepotoka kidogo na mtazamo wa Mungu. Kama watasadiki kwamba Mungu hafai kuwakaribisha, naye Mungu atokee kusema kwamba upendo Wake kwa binadamu hauna kikomo na kwamba Yuko radhi kumpa mtu fursa nyingine, basi huu si mfano wa kutojua kwa binadamu ukimulikwa waziwazi? Kwa vyovyote vile, nyinyi nyote mna mitazamo yenu binafsi. Mitazamo hii ni maarifa katika fikira zenu binafsi; ni onyesho pia ya kina cha uelewa wenu wa kweli na uelewa wenu wa nia za Mungu. Imesemwa vyema, sio? Ni jambo la kupendeza kwamba mnayo maoni katika suala hili! Lakini suala kuhusu kama maoni yenu ni sahihi au si sahihi, kunayo alama ya kiulizo. Je, nyinyi nyote hamna wasiwasi kidogo? “Basi ni gani sahihi? Siwezi kuona vizuri, na sijui hasa kile anachofikiria Mungu. Mungu hakuniambia chochote. Nawezaje kujua anachofikiria Mungu? Mtazamo wa Mungu kwake binadamu ni upendo. Kulingana na mwelekeo wa kale wa Mungu, Anafaa kumkubali mtu huyu. Lakini sina hakika kuhusu mwelekeo wa sasa wa Mungu—ninaweza kusema tu kwamba pengine Atamkaribisha mtu huyu na pengine Hatamkaribisha.” Je, waona vile jambo hili lilivyo la mzaha? Jambo hili limewakoroga. Kama hamna msimamo bora wa suala hili basi ni nini mtakachofanya endapo kanisa lenu litakumbana kwa kweli na mtu wa aina hii? Kama hamtalishughulikia kwa njia bora, basi pengine mtamkosea Mungu. Je, hamuoni kwamba suala hili ni hatari mno?
Kwa nini Ninataka kuulizia maoni yenu kuhusu kile Nilichokuwa Nazungumzia? Nataka kupima mitazamo yenu, kupima ni maarifa kiasi kipi ya Mungu mliyo nayo, ni uelewa kiasi kipi mlio nao katika nia za Mungu na mwelekeo wa Mungu. Jibu ni gani? Jibu limo kwenye mitazamo yenu. Baadhi yenu mnashikilia sana ukale, na baadhi yenu mnatumia kufikiria kwenu katika kukisia. “Kukisia” ni nini? Ni wakati ule ambao hamna wazo lolote namna ambavyo Mungu anafikiria, hivyo basi mnakuja na mawazo yasiyo na msingi kuhusu namna ambavyo Mungu anafaa kufikiria kwa namna hii au namna ile. Hamjui kwa hakika kama kukisia kwenu ni sahihi au si sahihi, na hivyo basi mnatoa mtazamo usioleweka. Mkikumbwa na hoja hii mnaona nini? Wakati wakimfuata Mungu, ni nadra sana kwa watu kutilia maanani makusudi ya Mungu, na wanatilia maanani fikira za Mungu na mwelekeo wa Mungu kwa binadamu kwa nadra sana. Ninyi hamwelewi fikira za Mungu, kwa hivyo mnapoulizwa maswali yanayohusisha nia za Mungu, yanayohusisha tabia ya Mungu, mnaingia katika hali ya kutokuwa na hakika; mnakuwa kwa kweli hamna uhakika, na mnakisia au kubahatisha. Mwelekeo huu ni upi? Unathibitisha hoja hii: Watu wengi wanaomwamini Mungu wanamchukulia kuwa hewa tupu, asiyebainika. Kwa nini Nasema hivyo? Kwa sababu kila wakati mnapokumbwa na suala, hamzijui nia za Mungu. Kwa nini hamzijui? Si kwamba hamzijui tu kwa sasa. Badala yake kuanzia mwanzo hadi mwisho hamjui mwelekeo wa Mungu katika suala hili. Kwenye nyakati zile ambazo huwezi kuona na hujui mwelekeo wa Mungu, umewahi kuutafakaria? Umeutafuta? Umewasiliana ili kuupata? La! Hii inathibitisha hoja: Mungu unayemsadiki na Mungu wa kweli hawajaunganika. Wewe, unayemsadiki Mungu, unafikiria Mungu kuhusu mapenzi yako, unafikiria tu kuhusu mapenzi ya kiongozi wako, na unafikiria tu yale mambo ya juujuu na maana ya kifalsafa ya neno la Mungu, lakini hujaribu kwa kweli kujua na kutafuta mapenzi ya Mungu kamwe. Sivyo ndivyo hali ilivyo? Kiini halisi cha suala hili hakipendezi! Kwa miaka na mikaka Nimeona watu wanaomsadiki Mungu. Kusadiki huku kunachukua mfumo gani? Baadhi ya watu wanasadiki katika Mungu ni kana kwamba Yeye ni hewa tupu. Watu hawa hawana majibu ya maswali kuhusu uwepo wa Mungu kwa sababu hawawezi kuhisi au kuwa na ufahamu uwepo au kutokuwepo kwa Mungu, sikuambii hata kuuona waziwazi au kuuelewa. Kwa nadharia yao, watu hawa wanafikiria kwamba Mungu hayupo. Baadhi wanasadiki katika Mungu ni kana kwamba Yeye ni binadamu. Watu hawa wanasadiki kwamba Mungu hawezi kufanya mambo yale ambayo wao hawawezi kufanya, na kwamba Mungu anafaa kufikiria namna wanavyofikiria. Ufafanuzi wa mtu huyu kuhusu Mungu ni “mtu asiyeonekana na asiyegusika.” Kunalo pia kundi la watu wanaosadiki katika Mungu kana kwamba Yeye ni kikaragosi. Watu hawa wanasadiki kwamba Mungu hana hisia, kwamba Mungu ni sanamu. Wakati wanapokabiliwa na suala, Mungu hana mwelekeo, hana mtazamo, hana mawazo; Anatawaliwa na binadamu. Watu wanasadiki tu wanavyotaka kusadiki. Wakimfanya kuwa mkubwa, Yeye ni mkubwa; wakimfanya kuwa mdogo, Yeye ni mdogo. Wakati wanapotenda dhambi na wanahitaji rehema ya Mungu, wanahitaji uvumilivu wa Mungu, wanahitaji upendo wa Mungu, basi Mungu anafaa kutoa rehema Zake. Watu hao wanafikiria kuhusu Mungu kwenye akili zao binafsi na kumfanya Mungu kutimiza mahitaji yao na kutosheleza matamanio yao yote. Haijalishi ni lini na ni wapi, na haijalishi hata mtu huyu anafanya nini, watakubali mvuto huu katika matendo yao kwa Mungu na kusadiki kwao katika Mungu. Kuna hata wale wanaosadiki katika Mungu kuweza kuwaokoa baada kuikera tabia ya Mungu. Hii ni kwa sababu wanasadiki kuwa upendo wa Mungu hauna mipaka, tabia ya Mungu ni haki, na kwamba bila kujali ni vipi ambavyo watu wanakosea Mungu, Hatakumbuka chochote. Kwa sababu makosa ya binadamu, dhambi za binadamu na kutotii kwa binadamu ni maonyesho ya mara moja ya tabia ya mtu huyo, Mungu atawapatia watu fursa, kuvumilia na kuwa na subira nao. Mungu angali atawapenda kama awali. Kwa hivyo tumaini la wokovu wao lingali kubwa. Kwa hakika, haijalishi ni vipi mtu anavyosadiki Mungu, mradi tu hafuatilii ukweli basi Mungu anashikilia mwelekeo mbaya kwake. Hii ni sababu wakati unamsadiki Mungu, labda unakithamini kile kitabu cha neno la Mungu unakichambua kila siku, unakisoma kila siku, lakini unamweka Mungu halisi pembeni, unamchukulia kama hewa tupu, unamchukulia Yeye kama mtu, na baadhi yenu mnamchukulia kuwa kikaragosi. Kwa nini Nasema hivi? Kwa sababu kutokana na vile Ninavyoona, licha ya kama unakabiliwa na suala au kukumbana na hali, yale mambo yanayopatikana katika nadharia yako, yale mambo ambayo yameimarishwa ndani kwa ndani—hakuna kati ya haya ambayo yana uunganisho wa neno la Mungu au yanafuatilia ukweli. Unajua tu kile wewe mwenyewe unatafuta, maoni yako wewe binafsi, na kisha mawazo yako binafsi, mitazamo yako binafsi inalazimishiwa Mungu. Inakuwa mitazamo ya Mungu, ambayo inatumika kama viwango vya kutii bila kusita. Kwa muda, kuendelea namna hii kunakufanya uwe mbali zaidi na Mungu.”
Sikiliza zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni