Maisha yote ya mwanadamu yamekuwa chini ya himaya ya Shetani, na hakuna mtu yeyote anayeweza kujitoa kutoka katika ushawishi wa Shetani yeye mwenyewe. Wote wanaishi katika dunia chafu, kwa upotovu na utupu, bila maana yoyote au thamani; wanaishi maisha ya kutojali kwa ajili ya mwili, tamaa, na kwa ajili ya Shetani. Hakuna maana yoyote kwa kuwepo kwao. Mwanadamu hana uwezo wa kupata ukweli utakaomweka huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Ingawa mwanadamu anaamini katika Mungu na anasoma Biblia haelewi jinsi ya kujitoa kutoka kwa ushawishi wa Shetani.
Kutoka kitambo, watu wachache sana wametambua siri hii, wachache sana wameiguza. Hivyo, hata kama mwanadamu anamchukia Shetani, na anachukia mwili, hajui jinsi ya kujitoa kutoka kwa ushawishi mkuu wa Shetani. Je, leo bado hamjamilikiwa na Shetani? Hamjuti juu ya matendo yenu ya uasi, zaidi ya hayo, hamhisi kama wachafu na waasi. Baada ya kumpinga Mungu, bado mna amani ya moyo na mnahisi utulivu mwingi. Je, utulivu wako si kwa sababu wewe ni mpotovu? Je, hii amani ya mawazo haitokani na kuasi kwako? Mwanadamu anaishi katika jehanamu ya binadamu, anaishi katika ushawishi wa giza la Shetani; mkabala katika ardhi, mapepo yanaishi na mwanadamu, yakienea katika mwili wa mwanadamu. Duniani, hauishi katika Paradiso ya kupendeza. Mahali ambapo ulipo ni ulimwengu wa Shetani, jehanamu ya binadamu, dunia ya chini. Mwanadamu asipotakaswa, basi yeye ni wa uchafu; asipolindwa na kutunzwa na Mungu, basi yeye bado ni mfungwa wa Shetani; asipohukumiwa na kuadibiwa, basi hatakuwa na njia ya kuepuka ukandamizaji na ushawishi mbaya wa Shetani. Tabia potovu unayoonyesha, na tabia ya uasi unayoishi kwa kudhihirisha inatosha kuonyesha kwamba bado unaishi katika himaya ya Shetani. Kama akili na mawazo yako hayajatakaswa, na tabia yako haijahukumiwa na kuadibiwa, basi nafsi yako yote bado inadhibitiwa na himaya ya Shetani, akili yako bado inadhibitiwa na Shetani, mawazo yako yanatawaliwa na Shetani, na nafsi yako yote inadhibitiwa na mikono ya Shetani. Je, unajua uko umbali gani, sasa, na kiwango alichokuwa Petro? Je, wewe ni wa kiwango hicho? Ni kiasi gani unajua kuhusu adabu na hukumu ya wakati wa leo? Unacho kiasi gani cha yale Petro alipata kujua? Iwapo, leo, huna uwezo wa kutambua, je utaweza kupata maarifa haya baadaye? Mtu mzembe na mwoga kama wewe hawezi kujua kuhusu adabu na hukumu ya Mungu. Ukifuata amani ya kimwili, na raha za kimwili, basi hutakuwa na njia yoyote ya kutakaswa, na mwishowe utarudi kwa Shetani, kwa sababu hali unayoishi kwa kudhihirisha ni ya Shetani, na ya mwili. Vitu vilivyo sasa, watu wengi hawayafuati maisha, kwa hivyo inamaanisha kuwa hawajali kuhusu kutakaswa, ama kuingia katika uzoefu wa ndani ya maisha. Je, watawezaje kufanywa kuwa wakamilifu? Wale wasiofuata maisha hawana fursa ya kufanywa wakamilifu, na wale wasiofuata maarifa ya Mungu, na hawafuati mabadiliko katika tabia zao, hawataweza kuepuka ushawishi wa giza wa Shetani. Kwa kuashiria maarifa yao kuhusu Mungu na kuingia kwao katika mabadiliko ya tabia zao, hawana umakini kuzihusu, kama wale wanaoamini katika dini pekee, na wale wanaofuata tu sherehe katika kuabudu kwao. Je, hiyo si kupoteza wakati? Kama, kwa imani yake kwa Mungu, mwanadamu hayuko makini katika mambo ya maisha, hafuati kuingia katika ukweli, hazingatii mabadiliko katika tabia yake, ama kufuata maarifa ya kazi ya Mungu, basi hawezi kufanywa mkamilifu. Kama unatamani kufanywa mkamilifu, lazima uelewe umuhimu wa kazi ya Mungu. Hasa, lazima uelewe umuhimu wa adabu na hukumu Yake, na kwa nini haya yanafanywa juu ya mwanadamu. Je, unaweza kukubali? Wakati wa adabu ya aina hii, unaweza kupata uzoefu na maarifa kama Petro? Ukifuata maarifa ya Mungu na ya kazi ya Roho Mtakatifu, na kuzingatia mabadiliko katika tabia yako, basi una fursa ya kufanywa mkamilifu. Kwa wale ambao wanatakiwa kufanywa wakamilifu, hatua hii ya kazi ya kushinda ni ya lazima; Ni baada ya kushindwa tu ndipo mwanadamu anaweza kuiona kazi ya kufanywa mkamilifu. Hakuna maana kubwa ya kufanya kazi ya kushindwa, ambayo itakufanya usiwe mwenye kufaa kufanya kazi yoyote ya Mungu. Hutakuwa na uwezo wowote wa kufanya kazi yako ya kueneza injili, kwa sababu hufuati maisha, na hujibadilishi na kujifanya mpya, na hivyo basi huna uzoefu kamili wa maisha. Katika kazi hii ya hatua kwa hatua, uliwahi kuwa na nafasi ya mtendaji-huduma, na foili[b], lakini kwa hakika usipofuata kuwa kama Petro, na ufuasi wako sio kama wenye njia ambayo Petro alifanywa mkamilifu, basi, kiasili hutapata mabadiliko katika tabia yako. Kama wewe ni mtu anayefuata kuwa mkamilifu, basi utakuwa na ushuhuda, na utasema: "Katika hii kazi ya hatua kwa hatua ya Mungu, nimekubali kazi ya Mungu ya adabu na hukumu, na hata kama nimepitia mateso mengi, nimepata kujua jinsi Mungu hufanya mwanadamu kuwa mkamilifu, nimepata kazi iliyofanywa na Mungu, nimekuwa na maarifa ya haki ya Mungu, na adabu Yake imeniokoa. Tabia Yake ya haki imekuja juu yangu, na ikaniletea baraka na neema, na hukumu Yake na adabu imenilinda na kunitakasa. Kama singeadibiwa na kuhukumiwa na Mungu, na kama maneno makali ya Mungu hayangekuja juu yangu, singalimjua Mungu, ama kuokolewa. Leo, naona, kama kiumbe, kwamba mtu hafurahii tu vitu vilivyoumbwa na Muumba, lakini pia, la maana sana ni kwamba viumbe vyote watafurahia haki ya tabia ya Mungu, na kufurahia hukumu Yake ya haki, kwa sababu tabia ya Mungu ina umuhimu katika furaha ya Mwanadamu. Kama kiumbe ambaye amepotoshwa na Shetani, kila mmoja anafaa kufurahia tabia ya haki ya Mungu. Katika tabia Yake ya haki, kuna adabu na hukumu, na pia, kuna upendo mkuu. Ingawa sina uwezo wa kupata kwa kikamilifu upendo wote wa Mungu leo, nimekuwa na bahati nzuri ya kuuona, na katika haya, nimebarikiwa." Hii ndio njia ambayo wale waliofanywa wakamilifu hutembea na maarifa wanayoongelea. Watu hao wanafanana na Petro; wanao uzoefu sawa na wa Petro. Watu kama hao pia ndio wale ambao wamepokea maisha, na walio na ukweli. Mwanadamu akipitia haya mpaka mwisho, wakati wa hukumu ya Mungu kwa hakika ataweza kikamilifu kujitoa katika ushawishi wa Shetani, na atakuwa wa Mungu.
Baada ya kushindwa, watu hawana ushuhuda wa kusikia. Kwa hakika wameaibisha tu Shetani, lakini hawajaishi kwa kudhihirisha ukweli wa neno la Mungu. Haujapata wokovu wa pili; umepata tu sadaka ya dhambi, ilhali haujafanywa mkamilifu—hii ni hasara kubwa ilioje. Lazima muelewe yale mnafaa kuingia ndani yake, na yale mnafaa kuishi kwa kudhihirisha, na lazima muingie ndani mwao. Kama mwishowe, hautafaulu kufanywa mkamilifu, basi hautakuwa binadamu wa kweli, na utajawa na majuto. Adamu na Hawa waliumbwa na Mungu hapo mwanzo wakiwa watu watakatifu, ni kama kusema, katika bustani ya Edeni, walikuwa watakatifu, wasiokuwa na uchafu. Walikuwa watiifu kwa Yehova, na hawakujua chochote kuhusu kuasi Yehova. Hii ni kwa sababu hawakuwa na kusumbuliwa na ushawishi wa Shetani, hawakuwa na sumu ya Shetani, na walikuwa watu wasafi kati ya binadamu wote. Waliishi katika bustani ya Edeni, bila kutiwa najisi na uchafu wowote, bila kuingiliwa na mwili, na heshima kwa Yehova. Baadaye, walipojaribiwa na Shetani, wakawa na sumu ya nyoka, na tamaa ya kuasi Yehova, na wakaishi chini ya ushawishi wa Shetani. Hapo mwanzo, walikuwa watakatifu na wenye kuheshimu sana Yehova; hivyo tu ndivyo walikuwa binadamu. Baadaye, baada ya kujaribiwa na Shetani, wakala tunda la maarifa ya kujua mazuri na mabaya, na wakaishi chini ya ushawishi wa Shetani. Waliendelea kupotoshwa na Shetani, na wakapoteza sura asili ya mwanadamu. Hapo mwanzo, mwanadamu alikuwa na pumzi ya Yehova, na hakuwa muasi hata kidogo, na hakuwa na uovu wowote katika moyo wake. Wakati huo, mwanadamu alikuwa binadamu wa kweli. Baada ya kupotoshwa na Shetani, mwanadamu akawa mnyama: Fikra zake zikajawa na uovu na uchafu, bila mazuri ama utakatifu. Je, huyu si Shetani? Umepata kujua mengi kuhusu kazi ya Mungu, ilhali haujabadilika wala kutakaswa. Bado unaishi katika himaya ya Shetani, na bado hujajitoa na kunyenyekea kwa Mungu. Huyu ni mtu ambaye ameshindwa lakini hajafanywa mkamilifu. Na mbona inasemekana kuwa mtu kama huyu hajafanywa mkamilifu? Kwa sababu mtu huyu hafuati maisha ama maarifa ya kazi ya Mungu, na hutamani tu raha za kimwili na starehe ya muda mfupi. Na kwa hivyo hakuna mabadiliko katika tabia zao, na hawajapata sura asili ya mwanadamu ilivyoumbwa na Mungu. Watu hao ni maiti zinazotembea, ni waliokufa na hawana roho! Wale wasiofuata maarifa ya mambo katika Roho, wasiofuata utakatifu, na wasiofuata kuishi kulingana na maisha ya ukweli, wanaotosheka na kushindwa kwa upande wa kanusho, na hawawezi kuishi kulingana na kuonyesha ukweli, na kuwa watu watakatifu—ni watu ambao hawajaokolewa. Kwani, kama hana ukweli, mwanadamu hataweza kusimama imara katika majaribu ya Mungu; wale watakaoweza kusimama imara katika majaribu ya Mungu pekee ndio wale ambao wameokolewa. Ninalotaka Mimi ni watu kama Petro, watu wanaofuata kufanywa wakamilifu. Ukweli wa leo unatolewa kwa wale ambao wanautamani na kuutafuta. Wokovu huu unapewa wale ambao wanatamani kuokolewa na Mungu, na haujakusudiwa kuwafaidi tu, lakini ili pia ili upatwe na Mungu. Mnampata Mungu ili Mungu pia awapate. Leo nimenena hayo maneno kwako, na mmeyasikia, na mnafaa kutenda kulingana na maneno haya. Mwishowe, mkiweka maneno haya katika matendo ndipo nitakapowapata nyinyi kupitia katika maneno haya; na pia, mtakuwa mmepata maneno haya, kumaanisha, mtakuwa mmepata wokovu mkuu. Punde mtakapofanywa wasafi, mtakuwa wanadamu wa halisi. Kama huwezi kuishi kulingana na ukweli, ama kuishi kulingana na aliyefanywa mkamilifu, basi inaweza kusemwa kuwa wewe si binadamu, ila wewe ni mfu anayetembea, mnyama, kwa sababu huna ukweli, ni kusema huna pumzi ya Yehova, na basi wewe ni mtu aliyekufa ambaye hana roho! Ingawa unaweza kuwa na ushuhuda baada ya kushindwa, unachopata ni wokovu kidogo, na hujakuwa kiumbe chenye roho. Ingawa umepata adabu na hukumu, tabia yako haijafanywa upya ama kubadilishwa kama matokeo; umebaki tu ulivyokuwa, bado wewe ni wa Shetani, na wewe si mtu aliyetakaswa Wale tu waliofanywa wakamilifu ndio wenye thamani, na watu tu kama hao ndio wamepata maisha ya kweli. Siku moja, mtu atakuambia, "Umeishuhudia kazi ya Mungu, basi zungumzia kidogo jinsi kazi Yake ilivyo. Daudi aliishuhudia kazi ya Mungu, na kuona kazi ya Yehova, Musa pia alishuhudia matendo ya Yehova, na wawili hao waliweza kuelezea juu ya matendo ya Yehova, na wangeweza kuongelea maajabu ya Yehova. Mmeona kazi iliyofanywa na Mungu mwenye mwili; unaweza kuongea kuhusu hekima Yake? Unaweza kuongelea maajabu ya kazi Yake? Ni nini Mungu alihitaji kutoka kwenu, na mliyaona vipi? Mmeiona kazi ya Mungu katika siku za mwisho; maono yenu makuu ni yapi? Mnaweza kuzungumza kuhusu haya? Mnaweza kuongea juu ya tabia ya haki ya Mungu?" Utajibu nini utakapokabiliana na maswali hayo? Kama unaweza kusema, "Mungu ni mwenye haki sana, Anaadibu na kutuhukumu, na kutuonyesha kwa wazi. Tabia ya Mungu kwa hakika haistahimili makosa ya mwanadamu. Baada ya kuiona kazi ya Mungu, nimejua unyama wetu, na kwa hakika nimeona tabia ya haki ya Mungu," halafu yule mtu mwingine ataendelea kukuuliza, "Ni nini kingine unachojua kumhusu Mungu? Mtu anaingiaje katika uzima? Je, una matarajio yoyote ya kibinafsi?" Utajibu, "Baada ya kupotoshwa na Shetani, viumbe wa Mungu walikuwa wanyama, na hawakuwa na tofauti na punda. Leo, ninaishi katika mikono ya Mungu, kwa hivyo lazima nikidhi matakwa na matamanio ya Muumba, na kutii kile Anachofunza. Sina chaguo lingine." Kama unaongea kwa ujumla kama huo pekee, mtu yule hataelewa kile unachokisema. Wakikuuliza ni maarifa gani unayo juu ya kazi ya Mungu, wanazungumzia kazi uliyofanya na mambo uliyopitia binafsi. Wanataka kujua juu ya ufahamu ulionao juu ya adabu na hukumu ya Mungu baada ya kuipitia, na kwa hiyo wanaongelea kuhusu matukio yako ya binafsi, na kuuliza uongelee ufahamu wako juu ya ukweli. Kama huwezi kuongelea mambo haya, hii inadhihirisha kwamba hujui lolote kuhusu kazi ya leo. Wewe huzungumza kuhusu maneno ya kupotosha, au yale yanayojulikana na kila mtu; hujapitia matukio yoyote halisi, wala huna dutu katika maarifa yako, na huna ushuhuda wa ukweli, na hivyo wengine hawatashawishiwa na mambo yako. Usiwe mfuasi tu wa kutazama Mungu, na usifuate mambo yaliyo na shaka. Kwa kutokuwa moto ama baridi utajitoa na kuchelewesha maisha yako. Lazima ujitoe kutoka kwa utazamaji na kutofanya chochote na uwe wa kufuata vitu vyema na kuushinda udhaifu wako, ili uweze kupata ukweli na kuishi kwa kudhihirisha maisha ya ukweli. Hakuna kitu cha kuogopesha kuhusu udhaifu wako, na kasoro zako sio shida yako kubwa. Shida yako kubwa, na kasoro yako kubwa, ni kutokuwa baridi ama moto na kutokuwa na hamu ya kuutafuta ukweli. Shida kubwa na nyinyi wote ni hali ya uwoga ambapo mnaridhika na hali ilivyo, na kungoja mkitazama tu. Hiki ndicho kizuizi chenu kikuu, na adui mkubwa kwa harakati yenu ya kutafuta ukweli. Kama unatii tu kwa sababu maneno Ninayosema ni makubwa, basi huna maarifa kwa kweli, wala huuthamini ukweli. Kutii kama kwako hakuhesabiki kama ushuhuda, na Siukubali utiifu wa aina hii. Mtu anaweza kukuuliza, "Mungu wako anatoka wapi hasa? Huyu Mungu wako ana kiini gani hasa?” Utajibu, “Dutu yake ni adabu na hukumu." "Je, Mungu si wa huruma na upendo kwa mwanadamu? Je, unajua hivyo?" Utasema, "Huyo ni Mungu wa wengine. Ni Mungu ambaye watu wa dini wanaamini, si Mungu wetu." Wakati watu kama wewe wanaeneza injili, ukweli unapotoshwa na wewe, basi una maana gani? Watu wengine watawezaje kuupata ukweli kutoka kwako? Huna ukweli, na huwezi kuongea chochote cha ukweli, ama, zaidi ya hayo, huwezi kuishi kwa kudhihirisha ukweli. Ni nini kinakuhitimisha kuishi mbele ya Mungu? Ukieneza injili kwa wengine, na ukiongea juu ya ukweli, na kuwa na ushuhuda kuhusu Mungu, kama hutaweza kuwatwaa kuja kwa Mungu, watayakataa maneno yako. Je, hutakuwa mpotezaji wa nafasi? Umeona mengi kuhusu kazi ya Mungu, ilhali ukiongelea ukweli, haueleweki. Je, wewe si bure tu? Wewe una maana gani? Mngewezaje kuwa mmeshuhudia kazi nyingi ya Mungu vile, ilhali hamna ufahamu kuhusu Mungu? Wakiuliza ni maarifa gani hasa uliyonayo ya Mungu, huna la kusema, au unajibu na kitu kisichoambatana na swali—ukisema kuwa Mungu ni mkuu, kuwa baraka ambayo umepokea ni uadhimisho wa Mungu, na kwamba hakuna bahati kuu kushinda kumwona Mungu kibinafsi. Kuna thamani gani ndani ya kusema hivyo? Ni maneno matupu yasiyo na maana! Kwa kuwa umeshuhudia kazi nyingi ya Mungu, je, unajua kuwa uadhimisho wa Mungu ni ukweli? Lazima ujue kazi ya Mungu, na hapo tu ndipo utakuwa na ushuhuda wa kweli kwa Mungu. Watu ambao hawajaupata ukweli watawezaje kumshuhudia Mungu?
Ikiwa kazi nyingi, na maneno mengi, hayajakuwa na mabadiliko kwako, basi wakati utakapofika wa kueneza kazi ya Mungu hutaweza kufanya kazi yako, na utaaibika na kufedheheshwa. Wakati huo utajisikia kuwa una deni kubwa kwa Mungu, kwamba maarifa yako juu ya Mungu ni juujuu. Usipofuata maarifa ya Mungu leo, Akiwa bado Anafanya kazi, basi baadaye itakuwa umechelewa. Mwishowe hutakuwa na maarifa yoyote ya kuongelea—utawachwa tupu, bila chochote. Ni nini, basi, utakachotumia kupeana uwajibikaji wako kwa Mungu? Je, una uchungu kuangalia Mungu? Unafaa kujitahidi katika shughuli yako sasa, ili mwishowe uweze, kama, Petro, kujua jinsi adabu na hukumu ya Mungu ina manufaa kwa binadamu, na bila adabu na hukumu Yake mwanadamu hawezi kuokolewa, na atazidi kuzama kwenye ardhi chafu, ndani zaidi kwenye tope. Wanadamu wamepotoshwa na Shetani, wamefitini wenyewe kwa wenyewe, wamekuliana njama wenyewe kwa wenyewe, wamepoteza heshima yao kwa Mungu, na uasi wao ni mkubwa sana, dhana zao ni nyingi, na wote ni wa Shetani. Bila adabu na hukumu ya Mungu, tabia potovu ya mwanadamu haiwezi kutakaswa na hangeweza kuokolewa. Kinachoelezwa na Mungu anayefanya kazi katika mwili hasa ndicho kile kinachoelezwa na Roho, na kazi afanyayo inafanyika kulingana na ile ifanywayo na Roho. Leo, kama huna maarifa yoyote juu ya hii kazi, basi wewe ni mpumbavu sana, na umepoteza mengi! Kama hujapata wokovu wa Mungu, basi imani yako ni ya kidini, na wewe ni Mkristo wa dini. Kwa sababu umeshikilia mafundisho yaliyokufa, umepoteza kazi mpya ya Roho Mtakatifu; wengine, wanaofuata upendo wa Mungu, wanaweza kupata ukweli na uhai, ambapo imani yako haiwezi kupata idhini ya Mungu. Badala yake, umekuwa mtenda maovu, mtu afanyaye vitendo vyenye kuharibu na vya chuki, umekuwa kilele cha utani wa Shetani, na mfungwa wa Shetani. Mungu si wa kuaminiwa na mwanadamu, lakini wa kupendwa na yeye, na kufuatwa na kuabudiwa na yeye. Usipomfuata leo, basi siku itakuja ambapo utasema, “Kama ningalimfuata Mungu, na kumkidhi vizuri. Kama ningalibadilisha tabia ya maisha yangu. Najuta kutojiwasilisha kwa Mungu kwa wakati ufaao, na kutotafuta maarifa ya neno la Mungu. Mungu alisema mengi wakati ule; nilikosa vipi kufuata? Nilikuwa mjinga!” Utajichukia mpaka kiwango fulani. Leo, huamini maneno ninayosema, na huyatilii maanani; wakati utakapofika kwa hii kazi kuenezwa, na unaona ukamilifu wake, utajuta, na wakati huo utakuwa bubu. Kuna baraka, ilhali hujui kuzifurahia, na kuna ukweli, ilhali hujui kuufuata. Je, hujiletei dharau? Leo ingawa hatua inayofuata kwa kazi ya Mungu haijaanza, hakuna kitu cha kipekee juu ya mahitaji yanayohitajika kwako na unachoulizwa kuishi kwa kudhihirisha. Kuna kazi nyingi, na ukweli mwingi; Je, hazina maana kujulikana na wewe? Je, adabu na hukumu ya Mungu haitoshi kuamsha roho yako? Je, adabu na hukumu ya Mungu haitoshi kukufanya ujichukie? Umetosheka kuishi katika ushawishi wa Shetani, kwa amani na furaha, na raha kidogo ya kimwili? Je, wewe si mtu wa chini zaidi kati ya watu wote? Hakuna aliye mpumbavu kuliko wale ambao wameona wokovu lakini hawaufuati ili kuupata: Ni watu ambao wanalafua mwili na kufurahia Shetani. Unatumai kwamba imani yako kwa Mungu haitakuwa na changamoto ama dhiki, ama mateso yoyote. Unafuata vile vitu ambavyo havina maana, na huambatanishi faida yoyote kwa maisha, badala yake kuweka mawazo ya fujo kabla ya ukweli. Huna maana! Unaishi kama nguruwe—kuna tofauti gani kati yako, nguruwe na mbwa? Je, hao wasiofuata ukweli na badala yake wanafuata mapenzi ya kimwili, si wote ni wanyama? Hao waliokufa na bila roho si wafu wanaotembea? Maneno mangapi yamenenwa kati yenu? Je, kazi kidogo imefanywa kati yenu? Ni kiasi gani nimetoa kati yenu? Na mbona hujapata chochote? Una nini cha kulalamikia? Je, si ni kweli kuwa hujapata chochote kwa sababu unapenda mwili sana? Na ni kwa sababu mawazo yako ni ya fujo sana? Je, si kwa sababu wewe ni mpumbavu sana? Kama huna uwezo wa kupata baraka hizi, unaweza kumlaumu Mungu kwa kutokukuokoa? Unachofuata ni cha kukuwezesha kupata amani baada ya kumwamini Mungu—watoto wako wawe huru kutokana na magonjwa, ili mme wako apate kazi nzuri, ili mwana wako apate mke mwema, binti wako apate mme anayeheshimika, ili ndume na farasi wako walime shamba vizuri, kwa mwaka wa hali ya anga nzuri kwa mimea yako. Hili ndilo unalolitafuta. Harakati yako ni kuishi kwa starehe, ili ajali isipate familia yako, ili upepo ukupite, ili uso wako usiguswe na changarawe, ili mazao ya familia yako yasipate mafuriko, ili usiguswe na majanga yoyote, kuishi katika mikono ya Mungu, kuishi kwenye kiota chenye joto. Mwoga kama wewe, anafuata mwili kila wakati—je, una moyo, una roho? Si wewe ni mnyama? Nakupa njia ya ukweli bila kukuuliza chochote, ilhali hauifuati. Je, wewe ni wale wamwaminio Mungu? Nahifadhi uhai wa ukweli wa binadamu juu yako, ila hauufuati. Je, una tofauti kati ya nguruwe na mbwa? Nguruwe hawafuati maisha ya binadamu, hawafuati kutakaswa, na hawaelewi maana ya maisha. Kila siku wanapokula na kushiba, wanalala. Nimekupa njia ya ukweli, ila hujaipata: Wewe u mkono mtupu. Je, unakubali kuendelea na maisha haya, maisha ya nguruwe? Umuhimu wa watu hao kuwa hai ni nini? Maisha yako ni ya kudharauliwa na kutoheshimika, unaishi huku ukiwa na uchafu na uzinzi, na hufuati lengo lolote; je, si maisha yako ni ya kutoheshimika kwa yote? Je, una ujasiri wa kumtazamia Mungu? Ukiendelea kuwa na uzoefu wa haya, je, si utakosa kupata chochote? Umepewa njia ya ukweli, lakini kama utaipata ama hapana inategemea na kutafuta kwako. Watu husema Mungu ni Mungu wa haki, na kwamba mradi tu mwanadamu atamfuata mpaka mwisho, basi Hatakuwa na upendeleo kwa mwanadamu, kwani Yeye ni mwenye haki. Je, mwanadamu akimfuata mpaka mwisho kabisa, Mungu anaweza kumtupa mwanadamu nje? Sina upendeleo kwa mwanadamu yeyote, na Huwahukumu wanadamu wote kwa tabia Yangu ya haki, ilhali kuna mahitaji yanayofaa Ninayohitaji kutoka kwa mwanadamu, na Ninahitaji yakamilishwe na wanadamu wote, bila kujali ni nani. Sijali kiwango cha kufuzu kwako au kuheshimiwa kwako; najali tu kama utatembea kwa njia Yangu, na kama unapenda na una kiu ya ukweli. Kama huna ukweli, na unaleta aibu katika jina Langu, na matendo yako ni kinyume cha njia Yangu, kufuata tu bila kujali, basi wakati huo nitakupiga na kukuadhibu kwa uovu wako, na utakuwa na nini la kusema? Utaweza kusema Mungu si mwenye haki? Leo kama umezingatia maneno ambayo nimenena, basi wewe ni mtu ambaye Namkubali. Unasema umeumia ukifuata Mungu, kwamba umemfuata kwa marefu na mapana, na umeshiriki na yeye katika wakati mzuri na mbaya, lakini hujaishi kulingana na maneno yaliyosemwa na Mungu; unataka tu kukimbilia Mungu kila siku, na hujafikiria kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana. Unasema kwamba, kwa vyovyote, unaamini Mungu ni mwenye haki: Umeteseka kwa ajili Yake, ukashughulika kwa ajili Yake, kujitoa kikamilifu Kwake, na umefanya bidii ingawa hujapata kutambuliwa; Yeye atakukumbuka. Ni ukweli kwamba Mungu ni mwenye haki, na haki hii haijatiwa doa na uchafu wowote: Haina mapenzi ya binadamu, na haijatiwa doa na mwili, ama kitendo chochote cha binadamu. Wale wote ambao ni waasi na wako kwa upinzani, na hawazingatii njia Zake wataadhibiwa; hakuna atakayesamehewa, na hakuna atakayeepuka! Watu wengine husema, "Leo nakimbia juu yako; mwisho ukifika, utanipa baraka kidogo?" Sasa Nakuuliza, "Umezingatia maneno Yangu?" Haki unayoongelea inategemea matendo. Unafikiria kwamba Mimi ni mwenye haki, na asiye na mapendeleo kwa binadamu wote, na kwamba wale wanifuatao hadi mwisho wataokolewa na kupata baraka Yangu. Kuna maana ya ndani kwa maneno Yangu kwamba "wale wote wanifuatao hadi mwisho wataokolewa": Wale wanifuatao mpaka mwisho ndio Nitakaowapata, ni wale, baada ya kushindwa Nami, watautafuta ukweli na kufanywa wakamilifu. Ni hali gani umepata? Umepata kunifuata hadi mwisho, lakini nini kingine? Je, umezingatia maneno Yangu? Umekamilisha moja kati ya tano ya mahitaji Yangu, ilhali huna mpango wa kumaliza manne yaliyobaki. Umepata ile njia rahisi, na ukafuata ukifikiria umebahatika. Kwa mtu kama wewe, haki Yangu ni adabu na hukumu, ni adhabu ya haki, na ni adhabu ya haki kwa watenda maovu wote; wale wote wasiotembea kwa njia Yangu wataadhibiwa, hata kama watafuata mpaka mwisho. Hii ndio haki ya Mungu. Wakati tabia hii ya haki inapodhihirishwa katika adhabu ya mwanadamu, mwanadamu atakosa la kusema, na kujuta kwamba, alipokuwa akimfuata Mungu hakutembea katika njia Yake. Wakati uo huo aliumia kidogo tu akimfuata Mungu, lakini hakutembea katika njia ya Mungu. Kuna udhuru gani? Hakuna namna ila kuadibiwa! Ila kwa akili yake anafikiria, "Nimefuata hadi mwisho, hata Ukiniadibu haitakuwa adabu kali, na baada ya kuadibu kwa kuchosha, bado Utanihitaji. Najua Wewe ni mwenye haki, na Hutanifanyia hivyo milele. Mimi si kama wale watakaofagiliwa nje; wale watakaofagiliwa watapokea adabu kuu, na adabu Yangu itakuwa kidogo." Adabu ya Mungu ya tabia ya haki si unavyosema. Sio kwamba wale ambao wanatubu dhambi zao kila wakati wataadibiwa kwa huruma. Haki ni utakatifu, na ni tabia ambayo haipendi makosa ya mwanadamu, na yale yote ambayo ni machafu na hayajabadilika ndiyo shabaha ya chukizo kwa Mungu. Haki ya Mungu si sheria, lakini amri ya utawala: Ni amri ya utawala katika ufalme, na hii amri ya utawala ni adhabu ya haki kwa yeyote asiye na ukweli na hajabadilika, na hakuna kiwango cha wokovu. Mwanadamu akiwekwa kulingana na aina, wazuri watazawadiwa na wabaya kuadhibiwa. Ndio wakati hatima ya mwanadamu itawekwa wazi, na ndio ni wakati ambao kazi ya wokovu itafika mwisho, kazi ya kuokoa binadamu haitafanyika tena, na adabu italetwa kwa wale waliotenda maovu. Watu wengine husema, "Mungu hukumbuka kila mmoja ambaye huwa kando Yake kila wakati. Mimi ni mmoja wa wale ndugu, na Mungu hawezi kusahau hata mmoja wetu. Tumehakikishiwa kufanywa wakamilifu na Mungu. Hatawakumbuka wote walio chini yetu, wale kati yao watakaofanywa wakamilifu wana uhakika kuwa watakuwa duni kutuliko sisi, tunaokutana na Mungu kila wakati; kati yetu hakuna ambaye amesahaulika na Mungu, wote tumeshakubaliwa na Mungu, na tunalo hakikisho la kufanywa wakamilifu na Mungu." Nyote mna mawazo ya aina hii; je, hii ni haki? Je, umeweka ukweli katika vitendo au la? Kwa hakika unaeneza uvumi kama huu—huna aibu!
Leo, watu wengine wanatafuta kutumiwa na Mungu, lakini baada ya kushindwa hawawezi kutumika moja kwa moja. Kwa maneno yaliyonenwa leo, kama, wakati Mungu anapotumia watu, bado huwezi kuyakamilisha, basi hujafanywa mkamilifu. Kwa maneno mengine, kufika kwa mwisho wa wakati ambao mwanadamu anafanywa mkamilifu kutabaini iwapo mwanadamu atatupwa ama atatumiwa na Mungu. Wale walioshindwa ni mifano wa kutojihusisha na uhasi tu; ni sampuli na mifano, lakini si chochote ila ni ujazio wa wimbo. Ni wakati wanadamu wanapokuwa na uhai tu, tabia yake imebadilika, na amepata mabadiliko ndani na nje, ndipo atapokuwa amefanywa mkamilifu. Leo, ni nini utakacho, kushindwa ama kufanywa mkamilifu? Ni nini unachotamani kupata? Ni masharti mangapi ya kufanywa mkamilifu ambayo umeyatimiza? Ni yapi ambayo hujatimiza? Utajihami vipi, na utaweka mikakati ipi ili kuondoa upungufu wako? Utaingia vipi katika njia ya kufanywa mkamilifu? Utajiwasilisha vipi kikamilifu? Unataka kufanywa mkamilifu, je, unafuata utakatifu? Je, unafuata adabu na hukumu ili ulindwe na Mungu? Unatafuta kutakaswa, kwa hivyo una nia ya kukubali adabu na hukumu? Unataka kujua Mungu, lakini je, una maarifa ya adabu na hukumu Yake? Leo, kazi nyingi Anayofanya kwenu ni adabu na hukumu; ufahamu wako wa kazi hii ni upi, ambayo imetekelezwa juu yako? Je, adabu na hukumu ambayo umepitia imekutakasa? Imekubadilisha? Imekuwa na mabadiliko yoyote kwako? Umechoka na hii kazi ya leo—laana, hukumu na ufichuzi—ama unaona yakiwa ya manufaa kwako? Unapenda Mungu, lakini ni juu ya nini ndiyo unampenda? Je, unampenda Mungu kwa sababu umepokea neema kidogo, ama unapenda Mungu baada ya kupata amani na furaha? Ama unampenda Mungu baada ya kutakaswa na adabu na hukumu yake? Ni nini hasa kinachokufanya umpende Mungu? Ni masharti yapi ndiyo Petro alikamilisha ili afanywe mkamilifu? Baada ya kufanywa mkamilifu, ni njia gani muhimu ndiyo ilitumiwa kudhihirisha? Je, alimpenda Bwana Yesu kwa sababu alitamani kuwa na Yeye, ama kwa sababu hangemuona, ama ni kwa sababu alikuwa ameshutumiwa? Ama alimpenda Bwana Yesu zaidi kwa sababu alikubali mateso ya shida, na alikuwa amejua uchafu wake na kuasi, na alikuwa amepata kujua utakatifu wa Bwana? Je, mapenzi yake kwa Mungu yalikuwa safi kwa sababu ya adabu na hukumu ya Mungu, ama kwa sababu ya kitu kingine? Ni nini hasa? Unampenda Mungu kwa sababu ya neema ya Mungu, na kwa sababu leo amekupa baraka kidogo. Je, huu ni upendo wa ukweli? Unapaswa kumpenda Mungu vipi? Je, unapaswa kukubali adabu na hukumu Yake, na, baada ya kuona tabia Yake ya haki, uweze kumpenda kwa kweli, hivi kwamba umeshawishika kabisa, na kuwa na maarifa Yake? Kama Petro, unaweza kusema kwamba huwezi kumpenda Mungu vya kutosha? Je, unachofuata kishindwe baada ya adabu na hukumu, ama kutakaswa, kimelindwa na kushughulikiwa baada ya adabu na hukumu? Ni gani kati ya haya unayofuata? Je, maisha yako yana maana ama hayana maana wala dhamani? Unataka mwili ama ukweli? Unataka hukumu, ama faraja? Baada ya kupitia na kuiona kazi nyingi ya Mungu, na baada ya kuuona utakatifu na haki ya Mungu, unafaa kumfuata vipi? Unapaswa kutembea vipi katika njia hii? Utahitajika kuweka mapenzi ya Mungu katika matendo kivipi? Je, adabu na hukumu ya Mungu zimekuwa na athari yoyote kwako? Kama una maarifa ya adabu na hukumu ya Mungu itategemea jinsi unavyoishi kwa kudhihirisha, na kiwango gani unapenda Mungu! Kinywa chako kinasema unampenda Mungu, ilhali unachoishi kwa kudhihirisha ni tabia nzee, zilizo potovu; humchi Mungu, na zaidi ya yote huna dhamiri. Je, watu wa aina hii wanampenda Mungu? Je, watu wa aina hii ni waaminifu kwa Mungu? Je, wao ni wale wanaokubali adabu na hukumu ya Mungu? Unasema unampenda na kumwamini Mungu, ilhali huachi hisia zako. Katika kazi yako, kuingia kwako, maneno uzungumzayo, na katika maisha yako, hakuna udhihirisho wa mapenzi yako kwa Mungu, na hakuna heshima kwa Mungu. Je, huyu ni mtu ambaye amepata adabu na hukumu? Mtu kama huyu anaweza kuwa Petro? Wale walio kama Petro wana maarifa, lakini je, wanaishi kulingana nayo? Leo, ni hali gani inahitaji mwanadamu aishi kwa kudhihirisha maisha ya ukweli? Maombi ya Petro hayakuwa maneno matupu yaliyotoka mdomoni mwake? Hayakuwa maneno kutoka moyoni mwake? Petro aliomba tu, na hakuweka ukweli katika matendo? Kufuata kwako ni kwa niaba ya nani? Utajilinda aje na kutakaswa wakati wa adabu na hukumu ya Mungu? Je, adabu na hukumu ya Mungu haina faida yoyote kwa mwanadamu? Je, hukumu yote ni adhabu? Je, amani na furaha, baraka ya vitu vya dunia na faraja, ni muhimu kwa maisha ya mwanadamu? Mwanadamu akiishi katika mazingira mazuri ya raha, bila maisha ya hukumu, anaweza kutakaswa? Iwapo mwanadamu anataka kubadilika na kutakaswa, anafaa kukubali vipi kufanywa mkamilifu? Ni njia gani unayopaswa kuchagua leo?
Tanbihi:
b. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni