Smiley face

Jumatano, 28 Agosti 2019

Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Manne ya Neno la Mungu Juu ya "Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi" (Sehemu ya Pili)



12. Matokeo ya kutimizwa kutoka kwa kazi ya kushinda kimsingi ni kwa ajili ya mwili wa mwanadamu kuacha kuasi, yaani, ili fikira za mwanadamu zipate ufahamu mpya wa Mungu, moyo wake umtii Mungu kabisa, na aamue kuwa wa Mungu. Jinsi ambavyo mwenendo wa mtu ama mwili wake unavyobadilika haiamui ikiwa ameshindwa. Badala yake, ni wakati ambapo fikira zako, utambuzi wako, na ufahamu wako unabadilika—yaani, ni wakati mielekeo yako yote ya kifikira inabadilika—ndipo huwa umeshindwa na Mungu. Ukiamua kutii na kupata fikira mpya, pale ambapo huingizi mawazo na nia zako katika maneno na kazi ya Mungu, na wakati ubongo wako unaweza kufikiri kwa njia ya kawaida, yaani, unapoweza kujitolea kwa Mungu kwa moyo wako wote—huyu ni mtu aliyeshindwa kabisa.

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

13. Katika ulimwengu wa dini, watu wengi huteseka pakubwa maishani mwao mwote, kwa kuihini miili yao au kuubeba msalaba wao, au hata kuteseka na kustahimili hadi pumzi zao za mwisho! Wengine huwa wanafunga hadi siku ya kifo chao. Katika maisha yao yote wanajinyima chakula kizuri na mavazi mazuri, wakisisitiza mateso tu. Wanaweza kuihini miili yao na kuinyima miili yao. Uwezo wao wa kustahimili mateso unastahili sifa. Ila fikira zao, mawazo yao, mielekeo yao ya kiakili, na kwa hakika asili yao ya kale—hakuna kati yavyo kilichoshughulikiwa hata kidogo. Hawajifahamu. Picha ya Mungu akilini mwao ni ya kijadi na ya kidhahania, Mungu asiye yakini. Uamuzi wao wa kuteseka kwa ajili ya Mungu unaletwa na azma na asili yao chanya. Hata ikiwa wanamwamini Mungu, hawamfahamu Mungu wala kuyafahamu mapenzi Yake. Wanamfanyia Mungu kazi na kumtesekea Mungu kama vipofu. Hawawekei utambuzi thamani yoyote na hawajishughulishi na jinsi ambayo huduma yao inatimiza mapenzi ya Mungu kwa kweli. Aidha hawajui jinsi ya kutimiza ufahamu kuhusu Mungu. Mungu wanayemhudumia si Mungu katika sura Yake ya asili, ila ni Mungu waliyejifikiria, Mungu waliyemsikia, au Mungu wa kihadithi wanayemsoma katika maandiko. Kisha wanatumia mawazo yao dhahiri na mioyo yao ya kiungu kumtesekea Mungu na kuifanya kazi ambayo Mungu anapaswa kufanya. Huduma yao haiko sahihi, kiasi kwamba hakuna anayemhudumia Mungu kwa njia inayotimiza mapenzi Yake. Haijalishi wako radhi kiasi gani kuteseka, mitazamo yao asilia ya huduma na picha ya Mungu akilini mwao havibadiliki kwani hawajapitia hukumu ya Mungu na kuadibu na usafishaji Wake na ukamilifu, na kwa sababu hakuna yeyote aliyewaongoza na ukweli. Japo wanasadiki kwa Yesu Mwokozi, hamna kati yao aliyewahi kumwona Mwokozi. Wamemsikia tu kwa hadithi na uvumi. Hivyo huduma yao ni sawa na kuhudumu mara mojamoja macho yao yakiwa yamefungwa kama kipofu anayemhudumia baba yake. Ni nini kinaweza kupatikana kutokana na huduma kama hiyo? Na ni nani anaweza kuikubali? Huduma yao haibadiliki kamwe toka mwanzo hadi mwisho. Wanapokea mafunzo ya kibinadamu na kukita huduma yao katika uasili wao na kile wanachokipenda wao. Hili laweza kuzalisha faida gani? Hata Petro, aliyemwona Yesu, hakujua jinsi ya kumhudumia Mungu kwa njia inayotimiza mapenzi ya Mungu. Ni katika uzee wake ndipo alipopata ufahamu. Hili linaonyesha nini kuhusu wanadamu vipofu ambao hawajapitia ushughulikiaji na hawana upogoaji na ambao hawajawahi kupata yeyote wa kuwaongoza? Je, huduma yenu kubwa sasa si kama ile ya vipofu? Wale wote ambao hawajapokea hukumu, hawajapokea upogoaji na ushughulikiaji, na hawana mabadiliko—je, wao si waliokosa kushindwa kabisa? Wana manufaa gani watu kama hao? Ikiwa fikira zako, ufahamu wako wa maisha, na ufahamu wako wa Mungu hauonyeshi mabadiliko mapya na hautoi faida hata kidogo, hutatimiza chochote kizuri katika huduma yako. Bila maono na bila ufahamu mpya wa kazi ya Mungu, huwezi kuwa mtu aliyeshindwa. Njia yako ya kumfuata Mungu itakuwa kama ile ya wale wanaoteseka na kufunga—itakuwa ya thamani ndogo! Hii ni kwa sababu kuna ushuhuda kidogo katika yale wayafanyayo ndipo Nasema huduma yao ni bure! Kotekote katika maisha yao, hao watu huteseka, hukaa gerezani kwa muda, na kwa kila wakati, hustahimili, husisitiza mapenzi na ukarimu, na kubeba msalaba wao. Wanatukanwa na kukataliwa na ulimwengu na hupitia kila ugumu. Wanatii hadi mwisho ila bado hawapati ushindi na hawawezi kutoa ushuhuda wa kutwaliwa. Wameteseka si haba, ila kwa ndani hawamfahamu Mungu kabisa. Hakuna fikira zao za zamani, mawazo ya zamani, vitendo vyao, uelewa wa wanadamu, na mawazo ya wanadamu yaliyoshughulikiwa. Kamwe hakuna uelewa mpya ndani yao. Hakuna hata chembe ya ufahamu wao wa Mungu ambao ni wa kweli au ni sahihi. Wamekosa kuyaelewa mapenzi ya Mungu. Je, huku kwaweza kuwa kumhudumia Mungu? Japo ulimfahamu Mungu zamani, tuseme umeudumisha ufahamu huo hadi leo na kuendelea kukita ufahamu wako kuhusu Mungu kwenye fikira na mawazo yako bila kujali Mungu anafanya nini. Yaani, ikiwa huna ufahamu mpya na wa kweli kuhusu Mungu na ukose kutambua sura na tabia ya kweli ya Mungu. Ikiwa ufahamu wako wa Mungu bado unaongozwa na fikira za uhasama na ushirikina na bado una mawazo na fikira za mwanadamu. Ikiwa hii ndiyo hali, basi hujashindwa. Lengo langu la kukwambia maneno haya yote sasa ni kukupa fursa ya kufahamu na kutumia utambuzi huu kukuongoza katika ufahamu sahihi na mpya. Aidha yanalengwa kukuondolea mawazo ya zamani na utambuzi wa zamani ulio nao ili uweze kuwa na ufahamu mpya. Ikiwa unakula na kunywa matamshi Yangu kweli, basi ufahamu wako utabadilika kwa kiwango kikubwa. Bora tu udumishe moyo mtiifu kwa kula na kunywa matamshi ya Mungu, mtazamo wako utabadilika. Bora tu unaweza kukubali kuadibu kwa kila mara, fikira zako za zamani zitabadilika taratibu. Bora tu fikira zako za zamani zimebadilishwa kabisa na kuwa mpya, vitendo vyako vitabadilika ipasavyo. Kwa njia hii, huduma yako itaendelea kuwa yenye malengo zaidi, na itaweza kutimiza mapenzi ya Mungu. Ukibadilisha maisha yako, ufahamu wako wa maisha, na mawazo yako mengi kuhusu Mungu, basi uasili wako utadidimia taratibu. Hili, na hakuna jingine ila hili, ndilo tokeo baada ya Mungu kumshinda mwanadamu; haya ndiyo mabadiliko yatakayoonekana ndani ya mwanadamu. Ikiwa katika kumwamini Mungu, yote ujuayo ni kuutiisha na kuuhini mwili wako na kustahimili na kuteseka, na hujui wazi ikiwa unachokifanya ni sawa au la, bila kujali unamfanyia nani kazi, basi vitendo kama hivi vitaletaje mabadiliko?

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

14. Mnapaswa kufahamu kuwa Ninachokitarajia kutoka kwenu si kwamba miili yenu iwekwe katika kifungo au bongo zenu zitawaliwe na kuzuiwa kufikiria mawazo dhahania. Hili si lengo la kazi wala kazi inayopaswa kufanywa hivi sasa. … Mnatakiwa kufahamu kazi ya Mungu na mjue asili yenu, uwezo wenu, na yale maisha yenu ya zamani. Hususan mnapaswa kujua kuhusu vile vitendo vyenu vyenye makosa vya zamani na mienendo yenu ya kibinadamu. Ili Kubadilika, mnapaswa kuanza kwa kubadilisha fikira zenu. Kwanza, badilisha fikira zenu za zamani kwa fikira mpya, na mruhusu fikira zenu mpya ziongoze maneno na matendo yenu na maisha yenu. Hili ndilo ombi kwa kila mtu sasa hivi. Msitende kama kipofu au kufuata kama kipofu. Ni sharti muwe na msingi na lengo. Msijidanganye. Mnapaswa mjue kabisa imani yenu kwa Mungu ni kwa ajili ya nini, ina faida gani, na kitu gani mnachopaswa kuingia kwacho sasa hivi. Ni muhimu kwamba uyafahamu haya yote.

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

15. Ufahamu wako wa matendo ya Mungu unapobadilika, unapokuwa na ufahamu mpya wa ukweli wa kila anachokisema Mungu, na ufahamu wako wa ndani unapoinuliwa, maisha yako yanabadilika na kuwa bora. Kila kitu kinachofanywa na kusemwa na mwanadamu sasa ni cha utendaji. Haya si mafundisho ya dini, ila kile ambacho watu wanahitaji kwa ajili ya maisha yao na kile wanachopaswa kumiliki. Hili ndilo badiliko linalotokea kwa mwanadamu wakati wa kazi ya kushinda, badiliko ambalo mwanadamu anapaswa kupitia, na ndiyo matokeo baada ya mwanadamu kushindwa. Ukishabadilisha fikira zako, uchukue mwelekeo mpya wa kimawazo, ubadilishe mawazo yako na nia zako na mantiki yako ya zamani, uache mambo yaliyokita mizizi ndani yako, na kupata ufahamu mpya wa imani kwa Mungu, basi, ushuhuda unaotoa utainuliwa na uwepo wako mzima, kwa kweli utakuwa umebadilika. Yote haya ndiyo ya kiutendaji zaidi, halisi zaidi, na vitu vya kimsingi kabisa—vitu vilivyokuwa vigumu kwa mwanadamu kushika hapo zamani na vitu ambavyo wasingeweza kukumbana navyo. Ndiyo kazi ya kweli ya Roho.

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

16. Katika hitimisho la kazi yote ya kushinda, ni muhimu kwamba nyinyi nyote mfahamu kwamba Mungu si Mungu wa Israeli tu, ila ni Mungu wa kila kiumbe. Aliumba wanadamu wote wala si Waisraeli tu. Ukisema kuwa Mungu ni Mungu wa Israeli tu au kwamba haiwezekani Mungu kupata mwili katika taifa lolote lililo nje ya Israeli, basi bado hujafikia ufahamu wowote katika harakati ya kazi ya kushinda na hutambui kamwe kwamba Mungu ni Mungu wako. Kile unachokitambua ni kuwa Mungu alitoka Israeli Akaenda Uchina na Analazimishwa kuwa Mungu wako. Iwapo huu ndio mtazamo wako wa vitu, basi kazi Yangu haijazaa matunda ndani yako na hujaelewa chochote Nilichokisema. Hatimaye, ikiwa utaandika ukoo Wangu, sawa na Mathayo, Nitafutie babu afaaye na Nitafutie mizizi sahihi—ili kwamba Mungu ana koo mbili kwa sababu ya kupata Kwake mwili mara mbili—je, huo hautakuwa mzaha mkubwa zaidi duniani? Wewe “mtu mwenye nia njema” uliyenipatia ukoo, je, huwezi kuwa mtu uliyemgawa Mungu? Je, uko tayari kuubeba mzigo huu wa dhambi? Baada ya hii kazi yote ya kushinda, ikiwa huamini kwamba Mungu ni Mungu wa viumbe wote, ikiwa bado unadhani kwamba Mungu ni Mungu wa Waisraeli tu, je, wewe si mtu anayemkana Mungu waziwazi? Kusudi la kukushinda leo ni kukufanya utambue kuwa Mungu ni Mungu wako, na Mungu wa wengine, na muhimu zaidi ni Mungu wa wote wanaompenda, na Mungu wa viumbe wote. Ni Mungu wa Israeli na Mungu wa Misiri. Ni Mungu wa Waingereza na Mungu wa Wamarekani. Si Mungu wa Adamu na Hawa tu, bali pia Mungu wa kizazi cha Adamu na Hawa. Ni Mungu wa kila Kitu mbinguni na duniani.

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

17. Familia ya Waisraeli na familia zote za Mataifa zimo mikononi mwa Mungu. Hakufanya kazi katika nchi ya Israeli pekee kwa miaka elfu kadhaa na kuzaliwa Uyahudi, ila leo Anashuka Uchina, nchi hii ambapo joka kuu jekundu limejikunja. Ikiwa kuzaliwa Uyahudi kunamfanya Mfalme wa Wayahudi, basi si kushuka kwake miongoni mwenu leo kunamfanya Mungu wenu? Aliwaongoza Waisraeli na alizaliwa Uyahudi na vilevile amezaliwa katika nchi ya Mataifa. Je, kazi Yake yote si ya wanadamu wote Aliowaumba? Je, Anawapenda Waisraeli mara mia moja na kuwachukia Mataifa mara elfu moja? Je, hayo siyo mawazo yenu? Ni ninyi ambao hamtambui Mungu; si kwamba Mungu Hakuwa Mungu wenu. Ni ninyi mnaomkataa Mungu; si kwamba Mungu hapendi kuwa Mungu wenu. Ni nani kati ya walioumbwa hayuko mikononi mwa mwenye Uweza? Kwa kuwashinda leo, je, lengo si kuwafanya mtambue kuwa Mungu ni Mungu wenu? Iwapo bado mnashikilia kuwa Mungu ni Mungu wa Waisraeli tu, na kuendelea kushikilia kuwa nyumba ya Daudi huko Israeli ni asili ya uzao wa Mungu na kuwa hakuna taifa tofauti na Israeli limewezeshwa “kumzaa” Mungu, na hata zaidi kuwa hakuna familia ya Mataifa yenye uwezo wa kupokea kazi ya Yehova—ikiwa bado unafikiria hivi, je, haikufanyi kuwa mshikiliaji wa ukaidi? Usikazie macho Israeli kila wakati. Mungu Yuko hapa miongoni mwenu leo. Vilevile msitazamie mbingu tu. Acheni kutamani Mungu wenu Aliye mbinguni! Mungu ametua miongoni mwenu, basi Anawezaje kuwa mbinguni? Hujaamini katika Mungu kwa muda mrefu, ilhali una mawazo mengi kuhusu Mungu, kiasi kwamba unathubutu kutofikiri hata kwa sekunde moja kuwa Mungu wa Israeli Anaweza kukutunukia na uwepo wake. Wala hamthubutu kufikiri jinsi mnavyoweza kumwona Mungu Akijitokeza binafsi, ikitiliwa maanani jinsi mlivyo wachafu. Aidha hamjawahi kufikiri jinsi Mungu anavyoweza kushuka miongoni mwa Mataifa. Anapaswa kushuka juu ya Mlima Sinai au Mlima wa Mizeituni na kuonekana kwa Waisraeli. Je, si watu wa Mataifa (yaani watu wa nje ya Israeli) ndio walengwa wa chuki Yake? Anawezaje kufanya kazi miongoni mwao? Haya yote ni mawazo yaliyokita mizizi ndani yenu ambayo mmeyakuza kwa miaka mingi. Kusudi la kuwashinda leo ni kuyaharibu haya mawazo yenu. Kwa njia hiyo mmeweza kumwona Mungu akijionyesha Mwenyewe miongoni mwenu—si katika Mlima Sinai au Mlima wa Mizeituni, bali miongoni mwa watu ambao Hajawahi kuwaongoza hapo awali.

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

18. Baada ya Mungu kufanyia hatua mbili za kazi Yake Israeli, Waisraeli na watu wa Mataifa walishikilia wazo hili: Japo ni kweli Mungu aliumba viumbe wote, yuko radhi kuwa Mungu wa Waisraeli tu, si Mungu wa Mataifa. Waisraeli wanaamini yafuatayo: Mungu anaweza tu kuwa Mungu wetu, sio Mungu wenu Mataifa, na kwa sababu humchi Yehova, Yehova—Mungu wetu—Anawachukia. Zaidi, Wayahudi hao huamini hili: Bwana Yesu alichukua sura yetu Wayahudi na ni Mungu aliye na alama ya Wayahudi. Mungu anafanyia kazi miongoni mwetu. Sura ya Mungu na sura zetu zinafanana; sura zetu na sura ya Mungu zinakaribiana. Bwana Yesu ni Mfalme wetu Wayahudi; watu wa Mataifa hawajawezeshwa kupokea wokovu mkubwa kiasi hicho. Bwana Yesu ni sadaka ya dhambi kwetu Wayahudi. Ni kwa misingi ya hatua hizi mbili za kazi ndipo Waisraeli na Wayahudi walijijengea haya mawazo mengi. Wanamdai Mungu kuwa wao tu, bila kukubali kwamba Mungu vilevile ni Mungu wa Mataifa. Kwa njia hii, Mungu alikuwa pengo katika mioyo ya watu wa Mataifa. Hii ni kwa sababu kila mtu aliamini kuwa Mungu hataki kuwa Mungu wa watu wa Mataifa na kuwa Anawapenda tu Waisraeli—Wateule wake—na Anawapenda Wayahudi hasa wafuasi waliomfuata. Je, wajua kuwa kazi aliyoifanya Yehova na Yesu ilikuwa ni kwa ajili ya uzima wa wanadamu wote? Je, sasa unatambua kuwa Mungu ni wa wale wote waliozaliwa nje ya Israeli? Je, Mungu Hayumo miongoni mwenu leo? Hii haiwezi kuwa ndoto, ama vipi? Je, hamkubali uhalisi huu? Mnathubutu kutoamini au kulifikiria. Licha ya jinsi mnavyolitazama, je, Mungu hayumo miongoni mwenu? Je, bado mnaogopa kuyaamini maneno haya? Kuanzia leo, je, wote walioshindwa, na wale wote wanaotaka kuwa wafuasi wa Mungu, si wateule wa Mungu? Je, nyote mlio wafuasi leo, si wateule nje ya Israeli? Je, nafasi yenu si sawa na ya Waisraeli? Je, hili silo mnalopaswa kutambua? Je, hili si lengo la kazi ya kukushinda? Kwa kuwa mwaweza kumwona Mungu, basi Atakuwa Mungu wenu milele, tangu mwanzo hadi siku za baadaye. Hatawaacha, mradi tu nyinyi nyote mko radhi Kumfuata na kuwa viumbe Wake waaminifu na watiifu.

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

19. Kukamilishwa kuna maana gani? kushindwa kuna maana gani? Ni vigezo vipi mtu anapaswa kuwa navyo ili apate kushindwa? Na ni vigezo vipi mtu anapaswa kuwa navyo ili afanywe mkamilifu? Kushinda na kukamilisha yote yanakusudiwa kumfanyia kazi mwanadamu ili aweze kurudi katika asili yake na awe huru na tabia zake potovu za shetani na ushawishi wa Shetani. Huu ushindi huja mapema katika mchakato wa kumfinyanga mwanadamu, ikiwa na maana kwamba ni hatua ya kwanza ya kazi. Kukamilisha ni hatua ya pili, au hitimisho la kazi. Kila mwanadamu ni lazima apitie hali ya kushindwa; la sivyo hataweza kumfahamu Mungu na hawezi kujua kuwa kuna Mungu, yaani, hawezi kumtambua Mungu. Na iwapo mtu hamtambui Mungu, hataweza kufanywa mkamilifu na Mungu kwa sababu hatakuwa na vigezo vya kufanywa mkamilifu. Ikiwa humtambui Mungu, utawezaje kumfahamu? Utawezaje kumtafuta? Aidha, hutaweza kumshuhudia, wala kumtosheleza. Kwa hivyo, kila anayetaka kukamilishwa, hatua ya kwanza lazima iwe kupitia kazi ya kushinda. Hili ndilo sharti la kwanza. Ila, iwe ni kushinda au ukamilifu, kila moja ni lengo la mwanadamu afanyaye kazi na kubadilishwa na kazi hiyo, na kila moja ni kipengele katika kazi ya kusimamia mwanadamu. Hizi hatua mbili ndizo zinahitajika kumgeuza yeyote kuwa mtu mkamilifu; hakuna moja kati yazo inaweza kurukwa. Ni kweli kuwa “kushindwa” hakuonekani kuwa ni jambo zuri, ila ni kweli kuwa mchakato wa kumshinda mtu ni mchakato wa kumbadilisha mwanadamu. Baada ya kushindwa, unaweza kuwa hujapoteza tabia yako mbovu kabisa, ila utakuwa umeijua. Kupitia kazi ya kushinda, utapata kujua uduni wa ubinadamu wako, na vilevile kufahamu utovu wako wa nidhamu. Japo hutaweza kuyaacha haya au kuyabadilisha ndani ya muda mfupi wa kazi ya kushinda, utayajua baadaye. Haya yanaujenga msingi wa ukamilifu wako. Kwa hivyo kushinda na kukamilisha yote yanafanywa kumbadilisha mwanadamu, kumtoa mwanadamu tabia zake mbovu za Kishetani ili ajitolee kikamilifu kwa Mungu. Ni kwamba tu kushindwa ni hatua ya kwanza katika kubadilisha tabia ya mwanadamu na pia hatua ya kwanza ya mwanadamu kujitoa kikamilifu kwa Mungu, hatua iliyo chini ya ukamilifu. Tabia za maisha ya mtu aliyeshindwa hubadilika kiasi kidogo kuliko ya mtu ambaye amepata ukamilifu. Kushindwa na kufanywa mkamilifu ni tofauti kabisa kwa kuwa ni hatua tofauti za kazi na kwa kuwa huhitaji vigezo tofauti kutoka kwa wanadamu, huku ushindi ukiwa na vigezo vya chini na ukamilifu ukiwa na vigezo vya juu. Walio wakamilifu ni wenye haki, watu watakatifu na safi; ni udhihirisho wa kazi ya kusimamia wanadamu, au matokeo ya mwisho. Japo si wanadamu wasio na doa, ni watu wanaotaka kuishi maisha ya thamani. Na walioshindwa je? Hukiri tu kwa vinywa vyao kuwa Mungu Yupo; wanakiri kuwa Mungu amepata mwili, kwamba neno linaonekana katika mwili, na kwamba Mungu amekuja duniani kufanya kazi ya hukumu na kuadibu watu. Aidha wanakiri kuwa hukumu na kuadibu kwa Mungu na mapigo Yake na usafishaji Wake ni faida kwa mwanadamu. Yaani, wameanza kuwa na sifa za ubinadamu, na wana ufahamu mdogo kuhusu maisha ila si bayana. Kwa maneno mengine, wameanza tu kuwa na ubinadamu. Haya ni matokeo ya kushindwa. Watu waingiapo katika njia ya ukamilifu, tabia zao za zamani zaweza kubadilishwa. Aidha, maisha yao huendelea kukua na taratibu hujitosa zaidi katika ukweli. Wanaweza kuchukia dunia na kuwachukia wale ambao hawapendi ukweli. Hususan hujichukia wao wenyewe, na hata zaidi ya hayo, wanajitambua vyema. Wana hiari kuishi katika ukweli na hulenga kutafuta ukweli. Hawako radhi kuishi katika mawazo ya bongo zao, na huchukia kujitukuza, kujisifu, na kujiinua kwa mwanadamu. Wananena kwa adabu ya hali ya juu, wanafanya mambo kwa utambuzi, ni wenye busara na watiifu kwa Mungu. Wakipata kuadibu na hukumu, hawaoni unyonge, bali hutoa shukrani. Hawawezi kuishi bila kuadibu na hukumu ya Mungu; wanaweza kupata ulinzi wake kupitia kuadibu na hukumu Yake. Hawafuati imani ya amani na furaha na ya kutafuta mkate wa kuwashibisha. Wala hawafuati raha za muda za kimwili. Hili ndilo wakamilifu huwa nalo.

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

20. Unasema kwamba unatambua Mungu mwenye mwili na unatambua kuwa Neno laonekana katika mwili, na bado unafanya mambo fulani kinyume, na hutendi jinsi Anataka utende, na humwogopi. Je, huku ni kumtambua Mungu? Unatambua Anachokisema ila unakataa kuyaweka katika vitendo hata yale mambo unayoweza kufanya na huzifuati njia zake. Je, huku ni kumtambua? Unamtambua ila mawazo yako ni kujikinga dhidi Yake, kutomcha kamwe. Ikiwa umeona na kuitambua kazi Yake na unafahamu kuwa Yeye ni Mungu, na bado unaendelea kuwa vuguvugu na bado hujabadilika hata kidogo, basi bado hujapata ushindi.

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

21. Mtu aliyeshindwa hufanya chochote awezacho; anataka kuingia na kuufikia ukweli wa juu hata kama bado hana uwezo. Ni kwamba tu ana mipaka katika yale anayoweza kufanya, yaani, vitendo vyake vimefungiwa na kuwekewa mipaka. Lakini angalau anapaswa kufanya chochote katika uwezo wake. Ukifanya haya mambo, itakuwa ni kwa sababu ya kazi ya kushinda. Hata ukisema, “Kwa sababu Anaweza kunena maneno mengi ambayo mwanadamu hawezi, ikiwa si Mungu, ni nani?” Kuwa na mawazo kama haya hakumaanishi unamtambua Mungu. Ikiwa unamtambua Mungu unapaswa kuthibitisha kwa matendo. Ukiongoza kanisa lakini usiweze kutenda haki, na kutamani pesa na kufuja pesa za kanisa kisiri kwa faida yako—je, huku ni kutambua kuwa kuna Mungu? Mungu ni mwenye Uweza na wa kumcha. Unawezaje kukosa kuogopa kama kweli unatambua kuwa kuna Mungu? Unawezaje kuwa ulifanya kitu cha kuchukiza namna hiyo? Je, huko kunaweza kuitwa kuamini? Je, kweli wamtambua Mungu? Je, unamwamini Mungu? Unayemwamini ni Mungu asiye yakini; ndiyo maana huogopi! Wale wote wanaomtambua Mungu kweli na kumfahamu wanamcha na wanaogopa kufanya chochote kinachompinga na chochote kinachoenda kinyume na dhamiri yao; hususan wanaogopa kufanya chochote kinachoenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Hili tu ndilo laweza kuwa ni kumtambua Mungu. Utafanya nini wazazi wako wakikuzuia kumwamini Mungu? Utampenda vipi Mungu ikiwa mume wako asiye muumini anakutendea mema? Aidha utampendaje Mungu ikiwa ndugu na dada zako wanakuchukia? Ikiwa unamtambua, basi utatenda ipasavyo na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi katika hali hizi zote. Ukikosa kutenda wazi na kusema tu kwamba unatambua uwepo wa Mungu, basi wewe ni msemaji tu. Unasema unamwamini na kumtambua. Je, unamtambua kwa njia gani? Unamwamini kwa njia gani? Je, unamwogopa? Unamcha? Unampenda moyoni mwako? Unapokuwa na huzuni bila yeyote wa kuegemea, unahisi Mungu ni wa kupendwa, halafu baadaye unasahau. Huku si kumpenda au kumwamini Mungu! Je, Mungu anataka mwanadamu apate nini mwishoni? Hali zote Nilizozitaja, kama vile: kufikiri kuwa wewe ni mtu mkubwa, kwamba unaelewa mambo upesi, kuwadhibiti wengine, kuwadharau wengine, kuwahukumu watu kwa misingi ya sura zao, kuwadhulumu watu waaminifu, kutamani pesa za kanisa, na kadhalika—kuondokewa na sehemu ya tabia mbovu za kishetani kama hizo ndiko kunakotakiwa kuonekana ndani yako baada ya wewe kushindwa.

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

22. Kazi ya kushinda inayofanywa kwenu nyie ni ya umuhimu mkubwa sana. Kwa upande mmoja, kusudi la hii kazi ni kukikamilisha kikundi cha watu, yaani, kuwakamilisha na kuwa kundi la washindi, kama kundi la kwanza la watu waliofanywa wakamilifu, yaani matunda ya kwanza. Kwa upande wa pili, ni kuruhusu viumbe wa Mungu kufurahia mapenzi ya Mungu, kupokea wokovu mkubwa wa Mungu, na kupokea wokovu kamili wa Mungu, na kumfanya mwanadamu kufurahia si tu huruma na ukarimu wa upendo, ila muhimu zaidi ni kuadibu na hukumu. Tangu uumbaji wa dunia hadi sasa, Mungu katika kazi Yake Amekuwa na mapenzi, bila chuki yoyote kwa mwanadamu. Hata kuadibu na hukumu uliyoiona ni mapenzi pia, mapenzi ya kweli na ya dhati, mapenzi yanayomwongoza mwanadamu kwenye njia sahihi ya maisha ya mwanadamu. Kwa upande wa tatu, ni kushuhudia mbele ya Shetani. Kwa upande wa nne, ni kuweka msingi wa kueneza kazi ya baadaye ya injili. Kazi yote Aliyoifanya ni kumwongoza mwanadamu kwenye njia sahihi ya maisha ya wanadamu, ili kwamba wawe na maisha ya kawaida ya wanadamu, kwani mwanadamu hajui jinsi ya kuishi. Bila uongozi kama huo, utaishi maisha tupu yasiyo na maana wala thamani, na kamwe hutajua jinsi ya kuwa mwanadamu wa kawaida. Huu ndio umuhimu mkuu wa kumshinda mwanadamu.

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

23. Nyinyi nyote mnaishi mahala pa dhambi na ufisadi; nyinyi nyote ni watu wafisadi na wenye dhambi. Leo hii hamwezi tu kumwona Mungu, ila la muhimu zaidi, mmepokea kuadibu na hukumu, mmepokea wokovu wa kina, yaani, mmepokea upendo mkubwa zaidi wa Mungu. Yote Ayafanyayo ni mapenzi ya dhati kwako; Hana nia mbaya. Anawahukumu kwa sababu ya dhambi zenu, ili kwamba mweze kujichunguza wenyewe na kupokea wokovu mkubwa. Haya yote hufanywa kumfinyanga mwanadamu. Tangu mwanzo hadi mwisho, Mungu amekuwa Akifanya kila Awezalo kumwokoa mwanadamu, na hakika hayuko tayari kuwaangamiza kabisa wanadamu Aliowaumba kwa mikono Yake Mwenyewe. Sasa Amekuja miongoni mwenu kufanya kazi; je, huu si wokovu zaidi? Je, Angalikuchukia, Angaliendelea kufanya kazi ya kiwango hicho cha juu ili kukuongoza wewe Mwenyewe? Ni kwa nini Ateseke hivyo? Mungu hawachukii wala hana nia mbaya juu yenu. Mnapaswa kufahamu kuwa mapenzi ya Mungu ndiyo mapenzi ya kweli zaidi. Anawaokoa kupitia hukumu kwa sababu tu ya uasi wa mwanadamu; la sivyo, hawangepata wokovu. Kwa kuwa hamjui jinsi ya kuishi, na mnaishi katika mahala pa ufisadi na dhambi na ni mapepo wenye ufisadi na uchafu, Hana moyo wa kuwaacha mpotoshwe zaidi; wala Hana moyo wa kutaka kuwaona mkiishi mahala pachafu kama hapa, mkikandamizwa na Shetani apendavyo, Hana moyo wa kuwaacha mtumbukie Kuzimu. Anataka tu kulipata hili kundi lenu na kuwakomboa vilivyo. Hili ndilo kusudi kuu la kufanya kazi ya kushinda miongoni mwenu—ni kwa ajili ya wokovu tu.

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

24. Iwapo huwezi kuona kuwa kila kitu unachofanyiwa ni mapenzi na wokovu, ukidhani kuwa ni mbinu tu, njia ya kumtesa mwanadamu na kitu kisichoaminika, basi ni bora urudi duniani mwako uendelee kupata mateso na ugumu wa maisha! Ikiwa uko tayari kuwa kwenye mkondo huu na kufurahia hukumu hii na wokovu huu wa ajabu, na kufurahia baraka hizi ambazo haziwezi kupatikana kokote katika ulimwengu wa wanadamu, na kufurahia mapenzi yake, basi baki kuwa mnyenyekevu kwenye mkondo huu kukubali kazi ya kushinda ili uweze kufanywa mkamilifu. Japokuwa kwa sasa unapitia mateso na usafishaji kwa sababu ya hukumu, mateso haya ni ya thamani na ya maana. Japo kuadibu na hukumu ni usafishaji na ufichuzi usio na huruma kwa mwanadamu, uliokusudiwa kuadhibu dhambi zake na kuadhibu mwili wake, kazi hii haijanuiwa kukashifu na kuuzima mwili wake. Ufichuzi mkali wa neno ni kwa kusudi la kukuongoza kwenye njia sahihi. Ninyi wenyewe mmeipitia sana kazi hii na, ni wazi, haijawaongoza kwenye njia mbaya. Yote ni kukuwezesha kuishi kulingana na ubinadamu wa kawaida, yote ni kitu ambacho kinaweza kutimizwa na ubinadamu wa kawaida. Kila hatua ya kazi hufanywa kwa misingi ya mahitaji yako, kulingana na udhaifu wako, kulingana na kimo chako halisi, na hamjatwikwa mzigo msioweza kuubeba. Japo huwezi kuliona hili wazi kwa sasa, na unajihisi Ninakuwa mgumu kwako, japo unadhani kuwa Ninakuadibu na kukuhukumu na kukuadibu kila siku kwa kuwa Ninakuchukia, na ingawa unachokipokea ni kuadibu na hukumu, hali halisi ni kuwa yote ni mapenzi kwako, pia ni ulinzi mkubwa kwako. Ikiwa huwezi kung’amua maana ya ndani ya kazi hii, basi huna njia ya kuendelea katika uzoefu wako. Unapaswa kuliwazwa kwa sababu ya huo wokovu. Usikatae kuzirudia busara zako. Baada ya kusafiri umbali huu, unapaswa kuuona wazi umuhimu wa kazi hii ya kushinda. Hupaswi tena kushikilia mtazamo fulani kama huo!

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni