Smiley face
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mapenzi-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mapenzi-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 19 Aprili 2019

Viumbe Wote Lazima Waje Chini ya Utawala wa Mungu


Wimbo wa Maneno ya Mungu | Viumbe Wote Lazima Waje Chini ya Utawala wa Mungu

I
Mungu aliumba vitu vyote,
na hivyo Yeye hufanya viumbe vyote
kuja chini ya amri Yake, na kutii utawala Wake.
Anaamuru vitu vyote, akividhibiti katika mikono Yake.
Vitu hai, milima, mito na mwanadamu
lazima vyote vije chini ya amri Yake.
Vitu angani na duniani
lazima vyote vije chini ya utawala Wake.

Alhamisi, 18 Aprili 2019

Ni Wakati Tu Ambapo Mungu Anakuwa Mwili Ndipo Mwanadamu Anaweza Kuwa Mwandani Wake


Wimbo wa Maneno ya Mungu | Ni Wakati tu Ambapo Mungu Anakuwa Mwili Ndipo Mwanadamu Anaweza Kuwa Mwandani Wake

I
Ni Wakati tu Mungu anapojinyenyekeza kwa kiwango fulani,
kumaanisha Anakuwa mwili ili kuishi kati ya wanadamu,
ndipo wataweza kuwa wasiri Wake,
ndipo watakuwa marafiki Zake wa karibu.
Mwanadamu anawezaje kupata sifa ya kuwa mwandani wa Mungu
Wakati Mungu ni wa Roho,
‘metukuka na mgumu kumwelewa?

Alhamisi, 21 Februari 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu”


Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu”


Mwenyezi Mungu anasema, “Ikiwa ungependa kutumikia mapenzi ya Mungu, ni lazima kwanza ufahamu ni watu wa aina gani wanapendwa na Mungu, ni watu wa aina gani wanachukiwa na Mungu, ni watu wa aina gani wanafanywa kuwa kamili na Mungu, na ni watu wa aina gani wana sifa zinazostahili kumhudumia Mungu. Hiki ni kiasi kidogo zaidi unachopaswa kujiandaa nacho.

Jumatatu, 18 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Sura ya 20

Kazi ya Roho Mtakatifu hushina mbele, ikiwaleta nyinyi ndani ya eneo mpya kabisa, ambayo ni kwamba hali halisi ya maisha ya ufalme imejitokeza mbele yako. Maneno ambayo yamesemwa na Roho Mtakatifu moja kwa moja yamefichua ukina ulio ndani ya mioyo yenu na kwa hiyo picha moja baada ya nyingine zinaonekana mbele yenu. Wale wote ambao wana njaa na kiu ya haki, ambao wana nia ya kutii kwa hakika watabaki Sayuni na watakaa Yerusalemu Mpya.

Jumatatu, 28 Januari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Sura ya 14

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Sura ya 14


Hapana muda wa kupoteza sasa. Roho Mtakatifu hutumia njia nyingi tofauti za kutuongoza katika maneno ya Mungu na kututayarisha na ukweli wote, kutakaswa, kuwa na undani wa kweli na ushirikiano na Mimi; huruhusiwi nafasi yoyote ya kuchagua. Kazi ya Roho Mtakatifu haina hisia na haijali wewe ni mtu wa aina gani. Mradi tu wewe uko tayari kutafuta na kufuata—si kutoa visingizio, si kubishana juu ya mafanikio yako mwenyewe na hasara lakini kutafuta na njaa na kiu ya haki, basi Nitakupa nuru.

Jumatano, 1 Novemba 2017

Kuwa Mzingatifu wa Mapenzi ya Mungu ili Upate Utimilifu



Mwenyezi Mungu alisema: Kadiri unavyozingatia mapenzi ya Mungu, ndivyo unavyokuwa na mzigo zaidi; kadiri unavyokuwa na mzigo, ndivyo uzoefu wako utakuwa mwingi zaidi. Unapokuwa mzingatifu wa mapenzi ya Mungu, Mungu atakupa mzigo huu, na Mungu atakupa nuru ya mambo ambayo amekuaminia. Baada ya Mungu kukupa mzigo huu, utaangalia ukweli wa kipengele hiki unapokula na kunywa maneno ya Mungu. Kama una mzigo unaohusiana na hali ya maisha ya ndugu, huu ni mzigo ulioaminiwa kwako na Mungu, na sala zako za kila siku daima zitaubeba mzigo huu.