Smiley face
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo neno. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo neno. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 30 Novemba 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Tamko la Sabini na Saba

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Tamko la Sabini na Saba

    Kutokuwa na hakika ya maneno Yangu ni sawa na kushikilia mtazamo wa kukanusha kuelekea matendo Yangu. Yaani, maneno Yangu yamebubujika kutoka ndani ya Mwanangu, lakini hamyatilii maanani. Ninyi hamko makini! Maneno mengi yamebubujika kutoka ndani ya Mwanangu, lakini ninyi ni wenye mashaka, hamyajui sana. Ninyi ni vipofu! Hamwelewi madhumuni ya kila kitu ambacho Nimefanya. Je, maneno Ninayoyaeleza kupitia kwa Mwanangu si maneno Yangu?