Smiley face
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo ushahidi. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo ushahidi. Onyesha machapisho yote

Jumanne, 3 Julai 2018

Ujana Uliotumiwa Bila Majuto

Ujana Uliotumiwa Bila Majuto

Xiaowen, Chongqing
"Upendo ni hisia safi, safi bila ya dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au vikwazo au umbali. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Ukipenda hudanganyi, kunung'unika, kutelekeza, kutarajia kupata malipo" ("Upendo safi bila Dosari" katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya).

Jumatano, 4 Aprili 2018

Kutoka kwa Mateso Kunatoka Harufu Nzuri ya Upendo

Kutoka kwa Mateso Kunatoka Harufu Nzuri ya Upendo

Xiaokai, Mkoa wa Jiangxi
Mimi ni mwanamke wa kawaida wa mashambani, na, kwa sababu ya dhana ya kikabaila ya kuthamini tu watoto wa kiume, sikuweza kuinua kichwa changu mbele ya wengine kwa ajili ya aibu ya kutozaa mtoto wa kiume. Wakati tu nilikuwa nikiteseka zaidi kabisa, nilichaguliwa na Bwana Yesu na, miaka miwili baadaye, nilikubali wokovu wa Mwenyezi Mungu.

Jumanne, 3 Aprili 2018

Nguvu ya Maisha Ambayo Haiwezi Kuzimwa Kamwe

Nguvu ya Maisha Ambayo Haiwezi Kuzimwa Kamwe

Dong Mei, Mkoa wa Henan
Mimi ni mtu wa kawaida. Niliishi maisha ya kawaida. Kama wengi wanaotamani sana mwanga, nilijaribu njia nyingi kutafuta maana ya kweli ya uwepo wa wanadamu, nikijaribu kuyapa maisha yangu umuhimu zaidi. Mwishowe, juhudi zangu zote zilikuwa bure. Lakini baada ya kuwa na bahati ya kutosha kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, mabadiliko ya muujiza yalitokea katika maisha yangu.

Jumatatu, 2 Aprili 2018

Upendo wa Mungu Ulikuwa Nami Katika Gereza la Giza la Ibilisi

Upendo wa Mungu Ulikuwa Nami Katika Gereza la Giza la Ibilisi

Yang Yi, Mkoa wa Jiangsu
Mimi ni Mkristo wa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Nimekuwa mfuasi wa Mwenyezi Mungu kwa zaidi ya miaka kumi. Katika wakati huu, kitu kimoja ambacho sitawahi kusahau ni taabu mbaya sana nilipokamatwa na polisi wa CCP muongo mmoja uliopita.

Jumanne, 23 Januari 2018

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo | Kwa Nini Nimetembea Njia ya Mafarisayo?


Kwa Nini Nimetembea Njia ya Mafarisayo?


Suxing Mkoa wa Shanxi
Mimi ni mtu mwenye kiburi na majivuno, na cheo kimekuwa udhaifu wangu. Kwa miaka mingi, nimefungwa na sifa na cheo na sijaweza kujiweka huru kutoka kwazo. Mara kwa mara nimepandishwa cheo na kubadilishwa na mtu mwingine; nimekuwa na vizuizi vingi katika cheo changu na nimekumbwa na matuta mengi njiani. Baada ya miaka mingi ya kushughulikiwa na kusafishwa, nilihisi kwamba sikuwa nachukulia cheo changu kwa uzito. Sikutaka kuwa kama nilivyokuwa katika nyakati zilizopita nikifikiri kwamba mradi nilikuwa kiongozi ningeweza kukamilishwa na Mungu na kwamba iwapo sikuwa kiongozi, basi sikuwa na matumaini.

Jumatatu, 22 Januari 2018

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo | Sababu ya Kweli ya Kazi Isiyofaa


Sababu ya Kweli ya Kazi Isiyofaa


Xinyi Mji wa Xi’an, Mkoa wa Shaanxi
Katika ziara zangu za karibuni kwa makanisa, mara nyingi niliwasikia viongozi na wafanyakazi wakisema kwamba watu wengine, baada ya kuhudhuria ushirika na mimi, waligeuka hasi, wanyonge na walikosa motisha ya kuendelea kutafuta. Wengine walisema ilikuwa vigumu sana kumwamini Mungu na walimwelewa Mungu visivyo. Wengine walisema kwamba hali zao zilikuwa nzuri kabla ya wao kukutana na mimi, lakini punde tu waliponiona, walihisi shinikizo kubwa mno na wasio na raha.

Ijumaa, 12 Januari 2018

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo | Kukubali Ukweli kwa Hakika Ni Nini?



 Kukubali Ukweli kwa Hakika Ni Nini?



Xiaohe Mji wa Puyang, Mkoa wa Henan
Hapo awali, kila wakati niliposoma maneno yaliyofichuliwa na Mungu kuhusu jinsi watu hawakubali ukweli, sikuamini kwamba maneno hayo yangetumika kwangu. Nilifurahia kula na kunywa neno la Mungu na kuwasiliana kuhusu neno la Mungu, na niliweza kukubali na kukiri kila kitu ambacho Mungu amesema kuwa ukweli—bila kujali jinsi kilivyoumiza moyo wangu au jinsi hakikuambatana na mawazo yangu. Aidha, bila kujali kiwango cha dosari kaka na dada zangu wangeonyesha, ningekikiri na kukikubali. Sikutafuta kujitetea mwenyewe, hivyo nilidhani kwamba nilikuwa mtu ambaye kwa hakika alikubali ukweli.

Jumatano, 27 Desemba 2017

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo | Kanuni Zangu za Maisha Ziliniacha Nikiwa Nimeharibika


Kanuni Zangu za Maisha Ziliniacha Nikiwa Nimeharibika


Changkai Mji wa Benxi, mkoa wa Liaoning


Maneno ya kawaida "Watu wazuri humaliza wakiwa wa mwisho" ni ambayo mimi binafsi ninayafahamu sana. Mimi na mume wangu sote tulikuwa hasa watu wasio na hatia: Wakati wa masuala yaliyohusisha faida au hasara yetu binafsi, hatukuwa aina ya watu wa kubishana na kusumbuana na wengine. Pale ambapo tuliweza kuwa wavumilivu tulikuwa wavumilivu, pale ambapo tungeweza kuwa na fadhila tulifanya tulivyoweza kuwa na fadhila. Kama matokeo yake, mara nyingi tulijipata tukiwa tumedanganywa na kudhulumiwa na wengine. 

Jumapili, 24 Desemba 2017

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo | Ni Nini Husababisha Uongo


Ni Nini Husababisha Uongo


Xiaojing Jijini Heze, Mkoani Shandong

Kila mara nilipoona neno la Mungu likituomba kuwa watu waaminifu na kuzungumza kwa usahihi, niliwaza, “Sina tatizo na kuzungumza kwa usahihi. Si ni kusema tu kitu jinsi kilivyo na kusema mambo jinsi yalivyo? Je, hiyo si rahisi? Kilichokuwa kimenikera zaidi daima katika dunia hii walikuwa watu waliotia chumvi walipozungumza.” Kwa sababu ya hili, nilihisi imani kuu, nikifikiri kwamba sikuwa na shida katika hali hii. Lakini kupitia tu kwa ufunuo wa Mungu ndio niligundua kwamba, bila kuingia katika ukweli au kubadili tabia ya mtu, mtu hawezi kwa vyovyote kuzungumza kwa usahihi.

Alhamisi, 21 Desemba 2017

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo | Matunda Machungu ya Kiburi


Matunda Machungu ya Kiburi

Hu Qing Jijini Suzhou, Mkoani Anhui
Nilipoona maneno ya Mungu yakisema: “Wale miongoni mwenu ambao huhudumu kama viongozi daima hutaka kuwa na ubunifu mkubwa, kuwa wazuri kuliko wengine, kupata hila mpya ili Mungu aweze kuona jinsi kweli mlivyo viongozi wakuu. … Nyinyi daima hutaka kuringa; si huu ni ufunuo kwa usahihi wa asili ya kiburi?” (“Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo), Nilifikiri mwenyewe: Nani ana ujasiri kama huo kujaribu kupata ujanja mpya ya ubunifu?

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo | Kuona Uhalisi Wangu Kwa Dhahiri


Kuona Uhalisi Wangu Kwa Dhahiri


Xiaoxiao Jijini Xuzhou, Mkoani Jiangsu
Kwa sababu ya mahitaji ya kazi ya kanisa, nilihamishwa mpaka mahali pengine ili kutimiza wajibu wangu. Wakati huo, kazi ya injili mahali pale ilikuwa katika hali duni, na hali ya akina kaka na dada kwa kawaida haikuwa nzuri. Lakini kwa kuwa nilikuwa nimeguswa na Roho Mtakatifu, bado nilijitwisha kila kitu nilichoaminiwa nacho kwa matumaini kamili. Baada ya kukubali kuaminiwa, nilihisi uwajibikaji kamili, kupata nuru kamili, na hata nikafikiri kwamba nilikuwa na uamuzi kiasi fulani. Niliamini kuwa nilikuwa na uwezo na ningeweza kutekeleza kazi hii vizuri.

Jumatano, 20 Desemba 2017

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo | Baada ya Kupoteza Hadhi Yangu …


Baada ya Kupoteza Hadhi Yangu …

Huimin Mji wa Jiaozuo, Mkoa wa Henan
Kila wakati nilipoona au kusikia kuhusu mtu aliyekuwa amebadilishwa naye kujisikia mwenye huzuni, dhaifu au mnunaji, na kutotaka kufuata tena, basi niliwaangalia kwa dharau. Nilidhani haikuwa kitu zaidi ya watu tofauti waliokuwa na majukumu tofauti ndani ya kanisa, kwamba hakukuwa na tofauti kati ya juu au chini, kwamba sote tulikuwa uumbaji wa Mungu na hakukuwa na sababu ya kuhuzunikia.

Jumatano, 29 Novemba 2017

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo | Ufahamu wa Kuokolewa


Lin Qing Jijini Qingzhou, Mkoa wa Shandong
Kwa miaka hii mingi ya kumfuata Mungu, nimeacha furaha ya familia yangu na mwili, na nimekuwa na shughuli nyingi siku nzima nikitimiza wajibu wangu kanisani. Kwa hiyo niliamini: Mradi tu nisiache kazi katika kanisa ambayo nimeaminiwa, nisimsaliti Mungu, nisiache kanisa, na kumfuata Mungu hadi mwisho, nitahurumiwa na kuokolewa na Mungu. Niliamini pia kuwa nilikuwa nikitembea katika njia ya wokovu na Mungu, na yote niliyokuwa niyafanye ni kumfuata Yeye mpaka mwisho.

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo | Roho Ya Majivuno Kabla ya Kuanguka


Roho Ya Majivuno Kabla ya Kuanguka


Baixue Mji wa Shenyang
Kwa sababu ya mahitaji ya kazi, nilihamishiwa hadi sehemu nyingine ya kazi. Wakati huo, nilikuwa na shukurani sana kwa Mungu. Nilihisi kwamba nilikuwa ninapungukiwa sana, lakini kwa njia ya ukuzwaji mtakatifu na Mungu, nilipewa nafasi ya kutimiza wajibu wangu katika eneo la kazi la ajabu hivyo. Niliweka nadhiri kwa Mungu moyoni mwangu: Ningefanya lote ninaloweza kumlipa Mungu. Hata hivyo, baada ya kufika, nilitambua utata mwingi katika kazi iliyokuwa ikifanyika. Matokeo yake, nilichukua jukumu mwenyewe la kuanza kukagua kila kitu cha kazi.

Ijumaa, 24 Novemba 2017

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo | Kiini cha Ulipizaji Kisasi wa Mtu Binafsi



Kiini cha Ulipizaji Kisasi wa Mtu Binafsi


Zhou Li Mji wa Xintai, Mkoa wa Shandong
Wakati fulani kitambo, tulihitaji kuzichora wilaya katika eneo letu, na kwa msingi wa kanuni zetu kwa ajili ya uteuzi wa viongozi, kulikuwa na ndugu mmoja wa kiume aliyekuwa mtaradhia mzuri kiasi. Nilitayarisha kumpandisha cheo hadi kuwa kiongozi wa wilaya. Siku moja nilipokuwa nikizungumza na ndugu huyu, alitaja kwamba alihisi kuwa nilikuwa mwenye nguvu sana katika kazi yangu, mkali sana, na kwamba katika mkusanyiko pamoja nami hapakuwa na furaha nyingi ....

Alhamisi, 23 Novemba 2017

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo | Kutambua Kuwa Nimekuwa Nikiitembea Njia ya Mafarisayo


Kutambua Kuwa Nimekuwa Nikiitembea Njia ya Mafarisayo


Wuxin Mji wa Taiyuan, Mkoa wa Shanxi
Kitu ambacho tumezungumzia mara kwa mara katika ushirikiano wa awali ni njia ambazo zilitembewa na Petro na Paulo. Inasemekana kwamba Petro alizingatia kujijua mwenyewe na kumjua Mungu, na alikuwa mtu ambaye Mungu alimpenda, ilhali Paulo alizingatia tu kazi yake, sifa na hadhi yake, na alikuwa mtu ambaye Mungu alimdharau. Daima nimekuwa na hofu ya kuitembea njia ya Paulo, ambayo ndiyo sababu mimi kwa kawaida mara nyingi husoma maneno ya Mungu kuhusu uzoefu wa Petro ili kuona jinsi alivyopata kumjua Mungu.