Smiley face

Jumatatu, 20 Novemba 2017

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II(Sehemu ya Pili)



Kwenye kipindi sawa na kile cha Ibrahimu, Mungu pia aliliangamiza jiji. Jiji hili liliitwa Sodoma. Bila shaka, watu wengi wanaijua hadithi ya Sodoma, lakini hakuna yeyote aliyejua fikira za Mungu zilikuwa usuli wa kuangamiza Kwake jiji hili.
Na hivyo leo, kupitia mazungumzo yake Mungu na Ibrahimu hapa chini, tutajifunza fikira Zake wakati huo, huku pia tukijifunza kuhusu tabia Yake. Kinachofuata, hebu tusome vifungu vya maandiko.
B. Mungu Lazima Aangamize Sodoma.
(Mwa 18:26) Kisha BWANA akasema, Nikipata katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, basi Nitapaacha mahali pote kwa ajili yao.
(Mwa 18:29) Na akazungumza tena naye, akasema, Huenda wakapatikana humo arobaini. Akasema, Sitafanya hivyo.
(Mwa 18:30) Akamwambia, labda watapatikana huko thelathini. Naye akasema, Sitafanya hivyo.
(Mwa 18:31) Kisha akasema, huenda wakaonekana huko ishirini. Naye akasema, Sitauharibu.
(Mwa 18:32) Naye akasema, huenda wakaonekana huko kumi. Naye akasema, Sitauharibu.
Hizi ni dondoo chache Nilizochagua kutoka kwenye Biblia. Dondoo hizi si kamilifu, za matoleo ya awali. Kama mngependa kuziona hizo, mnaweza kuzitafuta kwenye Biblia nyinyi wenyewe; ili kuokoa muda, Nimeiacha sehemu ya maudhui asilia. Hapa Nimechagua tu vifungu na sentensi mbalimbali kuu, huku nikiziacha sentensi mbalimbali ambazo hazina umuhimu katika ushirika wetu wa leo. Katika vifungu na maudhui yote tunayotumia katika ushirika, zingatio letu haliyaendei maelezo ya hadithi na mwenendo wa binadamu katika hadithi hizi; badala yake, tunazungumzia tu fikira za Mungu na mawazo Yake wakati huo. Katika fikira na mawazo ya Mungu, tutaiona tabia ya Mungu, na kutoka katika kila kitu alichofanya Mungu, tutaweza kumuona Mungu Mwenyewe wa kweli—na katika haya tutaweza kutimiza malengo yetu.

Mungu Anawajali tu Wale Wanaoweza Kutii Maneno Yake Na Kufuata Amri Zake

Vifungu hivi vilivyotajwa hapo juu vinayo maneno msingi mbalimbali: nambari. Kwanza, Yehova alisema kwamba kama Angewapata wenye haki hamsini ndani ya Jiji, basi Angepanusurisha mahali hapo, hii ni kusema, Asingeangamiza jiji hilo. Hivyo walikuwepo, kwa hakika, watakatifu hamsini ndani ya Sodoma? Hawakuwemo. Muda mfupi baadaye, Ibrahimu alimwambia nini Mungu? Alisema, labda kutakuwemo arubaini waliopatikana humo? Naye Mungu akasema, Sitafanya hivyo. Kisha, Ibrahimu akasema huenda wakawepo thelathini watakaopatikana hapo? Naye Mungu akasema, Sitafanya hivyo. Na labda ishirini? Sitafanya hivyo. Kumi? Sitafanya hivyo. Kulikuwemo, kwa hakika, wenye haki kumi ndani ya jiji? Hapakuwa kumi—lakini kulikuwemo na mmoja. Na huyu mmoja alikuwa nani? Alikuwa Loti. Wakati huo, kulikuwepo tu na mwenye haki mmoja kwenye eneo la Sodoma, lakini Mungu alikuwa mmakinifu sana au mkali kuhusiana na nambari hii? La, hakuwa hivyo! Na wakati binadamu aliendelea kuulizia, “Na je wale arubaini?”“Na je wale thelathini?” mpaka pale alipofika katika sehemu ile ya “Na je wale kumi?” Mungu alisema, “Hata kama wangalikuwemo kumi, Singeangamiza jiji hilo; Ningelinusurisha, na kuwasamehe wale watu wengine mbali na wale kumi.” Idadi ya watu kumi ingekuwa ya kuhurumiwa vya kutosha, lakini ilitokea kwamba, kwa hakika, hakukuwemo na hata ile idadi inayohitajika ya watu wenye haki kule Sodoma. Unaona, basi, kwamba katika macho ya Mungu dhambi na maovu ya watu wa jiji ilikuwa kwa kiasi kwamba Mungu hakuwa na chaguo lolote ila kuwaangamiza. Mungu alimaanisha nini Aliposema kwamba Asingeliharibu jiji kama kungekuwemo na wenye haki hamsini? Nambari hizi hazikuwa muhimu kwa Mungu. Kile kilichokuwa muhimu kilikuwa kama jiji lilikuwa na wenye haki Aliotaka au la. Kama jiji lisingekuwa na mwenye haki yeyote isipokuwa mmoja, Mungu asingewaruhusu madhara kuwepo kutokana na Yeye kuangamiza jiji hilo. Kile ambacho haya yote yanamaanisha ni kwamba, haijalishi kama Mungu angeliangamiza jiji au la, na haijalishi idadi ya wenye haki waliokuwa ndani ya jiji hilo, kwake Mungu jiji hili lenye dhambi lilikuwa limelaaniwa na lilikuwa limejaa maovu, na hivyo lilifaa kuangamizwa, na kutoweka kwenye macho ya Mungu huku nao wenye haki wakisali. Haikulijalisha enzi husika, haikujalisha awamu ya maendeleo ya mwanadamu, mwelekeo wa Mungu haubadiliki: Anachukia maovu, na Anawajali wenye haki mbele ya macho Yake. Mwelekeo huu wazi wa Mungu ndiyo pia ufunuo wa kweli wa kiini cha Mungu. Kwa sababu hakukuwepo na mwenye haki yeyote isipokuwa mmoja ndani ya jiji, Mungu hakusita tena. Matokeo yake ni kwamba Sodoma ingeangamizwa bila kusita. Unaona nini katika haya? Katika enzi hiyo, Mungu asingeangamiza jiji kama wamo wenye haki hamsini ndani yake, wala kama kulikuwemo kumi, kumaanisha kwamba Mungu angeamua kusamehe na kumvumilia mwanadamu, au angefanya kazi ya kuongoza, kwa sababu ya watu wachache ambao waliweza kumstahi na kumwabudu Yeye. Mungu hutilia maanani haki ya binadamu, Hutilia maanani sana kwa wale wanaoweza kumwabudu Yeye, na Anatilia maanani sana wale wanaoweza kufanya matendo mema mbele yake.
Kutoka nyakati za mapema sana hadi leo, umewahi kusoma ndani ya Biblia kuhusu Mungu kuuwasilisha ukweli, au kuzungumzia kuhusu njia ya Mungu, kwa mtu yeyote? La, hujawahi. Maneno ya Mungu kwa binadamu tunayoyasoma yaliwaambia watu tu cha kufanya. Baadhi walienda na wakayafanya, baadhi hawakuyafanya; baadhi walisadiki, na baadhi hawakusadiki. Hivyo ndivyo ilivyokuwa tu. Hivyo, wenye haki wa enzi hiyo—wale waliokuwa wenye haki mbele ya macho ya Mungu—walikuwa wale tu ambao wangeweza kuyasikia maneno ya Mungu na kufuata amri za Mungu. Walikuwa watumishi waliotekeleza maneno ya Mungu miongoni mwa binadamu. Je, watu kama hao wangeweza kuitwa wale wanaomjua Mungu? Wangeweza kuitwa watu waliofanywa kuwa watimilifu na Mungu? La, wasingeweza kuitwa hivyo. Na hivyo, licha ya idadi yao, kwenye macho ya Mungu hawa wenye haki walistahili kuitwa wandani wa Mungu? Wangeweza kuitwa mashahidi wa Mungu? Bila shaka la! Hawakustahili kamwe kuitwa wandani na mashahidi wa Mungu. Na hivyo Mungu aliwaita watu kama hawa vipi? Kwenye Biblia, hadi kufikia kwenye vifungu vya maandiko ambavyo tumetoka kusoma hivi punde, kulikuwa na matukio mengi ya Mungu kuwaita “Mtumishi wangu.” Hivi ni kusema, kwa wakati huo kwenye macho ya Mungu watu hawa wenye haki walikuwa watumishi wa Mungu, walikuwa watu waliomhudumia Yeye duniani. Naye Mungu alifikiria vipi kuhusu jina hilo? Kwa nini Akawaita hivyo? Je, Mungu anavyo viwango ambavyo Anatumia katika Kuwaita watu ndani ya moyo Wake? Bila shaka anavyo. Mungu anavyo viwango, haijalishi kama Anawaita watu wenye haki, watimilifu, wanyofu, au watumishi. Anapomwita mtu mtumishi Wake, Anayo imani thabiti kwamba mtu huyu anaweza kuwapokea wajumbe Wake, na anaweza kufuata amri Zake, na anaweza kutekeleza kile ambacho ameamrishwa kufanya na wale wajumbe. Na mtu huyu anatekeleza nini? Kile ambacho Mungu anamwamuru binadamu kufanya na kutekeleza duniani. Wakati huo, kile ambacho Mungu alimwomba binadamu kufanya na kutekeleza duniani kingeweza kuitwa njia ya Mungu? La, kisingeweza. Kwani wakati huo, Mungu alimwomba tu binadamu kufanya mambo machache rahisi; Alitamka amri chache rahisi, Akimwambia binadamu kufanya hiki au kile, na si zaidi ya hayo. Mungu alikuwa akifanya kazi kulingana na mpango Wake. Kwa sababu, wakati huo, masharti mengi hayakuwepo, muda ulikuwa haujatimia, na ilikuwa vigumu kwake mwanadamu kuvumilia njia ya Mungu, hivyo basi njia ya Mungu ilikuwa bado haijaanza kuwasilishwa mbele kutoka kwenye moyo wa Mungu. Katika haya, tunaona kwamba haijalishi kama kulikuwa thelathini au ishirini ya wale wenye haki aliozungumzia Mungu, mbele ya macho Yake wote walikuwa watumishi Wake. Wakati wajumbe wa Mungu walipowajia watumishi hawa, wangeweza kuwapokea, na kufuata amri zao, na kutenda kulingana na maneno yao. Haya ndiyo hasa yaliyofaa kufanywa, na kutimizwa, na watumishi mbele ya macho ya Mungu. Mungu ni mwenye busara katika majina Yake kwa watu. Hakuwaita watumishi Wake kwa sababu walikuwa vile mlivyo sasa—kwa sababu walikuwa wamesikia mahubiri mengi, walijua kile ambacho Mungu alifaa kufanya, walielewa mengi kuhusu mapenzi ya Mungu na walifahamu mpango Wake wa usimamizi—lakini kwa sababu ubinadamu wao ulikuwa wenye uaminifu na waliweza kutii maneno ya Mungu; wakati Mungu alipowaamuru, waliweza kuweka pembeni kile walichokuwa wakifanya na kutekeleza kile ambacho Mungu aliwaamuru kufanya. Na hivyo, kwake Mungu safu ile nyingine ya maana kwenye cheo cha[b] mtumishi ni kwamba walishirikiana na kazi Yake duniani na ingawaje hawakuwa wajumbe wa Mungu, hao ndio waliokuwa watekelezaji na wafuatiliaji wa maneno ya Mungu duniani. Unaona, basi, watumishi hawa au wenye haki hawa walikuwa na umuhimu mkubwa katika moyo wa Mungu. Kazi ile ambayo Mungu alifaa kuishughulikia duniani isingeweza kufanyika bila ya watu wa kushirikiana na Yeye, na wajibu uliotekelezwa na watumishi wa Mungu usingeweza kufanywa na wajumbe wa Mungu. Kila kazi ambayo Mungu alitoa amri kwa watumishi hawa ilikuwa yenye umuhimu mkubwa Kwake, na hivyo basi Asingeweza kuwapoteza. Bila ya ushirikiano wa watumishi hawa na Mungu, kazi Yake miongoni mwa wanadamu ingefikia kikomo, na matokeo yake ni kwamba mpango wa usimamizi wa Mungu na matumaini ya Mungu vyote visingewezekana.

Mungu ni Mwenye Wingi wa Rehema Kwa Wale Anaowajali, na Mwenye Hasira Kali kwa Wale Anaochukia na Kukataa

Kwenye simulizi za Biblia, kulikuwepo na watumishi kumi wa Mungu kule Sodoma? La, hakukuwepo! Kulikuwepo na jiji lililostahili kusamehewa na Mungu? Mtu mmoja tu kwenye jiji hilo—Loti—ndiye aliye wapokea wajumbe wa Mungu. Matokeo ya haya ni kwamba kulikuwa na mtumishi mmoja tu wa Mungu kwenye jiji, na hivyo basi Mungu hakuwa na chaguo ila kumwokoa Loti na kuliangamiza jiji la Sodoma. Mabadilishano haya kati ya Ibrahimu na Mungu yanaweza kuonekana kuwa rahisi tu, lakini yanaonyesha kitu fulani kikuu: Kuna kanuni za vitendo vya Mungu, na kabla ya kufanya uamuzi Atachukua muda mrefu akiangalia na kutafakari; kabla ya wakati kuwa sawa, bila shaka Hatafanya au kukimbilia hitimisho zozote. Mabadilishano kati ya Ibrahimu na Mungu yanatuonyesha kwamba uamuzi wa Mungu wa kuangamiza Sodoma haukuwa mbaya hata kidogo, kwani Mungu alijua tayari kwamba kwenye jiji hakukuwa na watu arubaini wenye haki, na wala thelathini wenye haki, wala ishirini. Hawakuwa hata kumi. Mtu mwenye haki pekee kwenye jiji alikuwa Loti. Yote yaliyofanyika ndani ya Sodoma na hali zake ziliangaliwa na Mungu, na zilizoeleka kwa Mungu kama sehemu ya nyuma ya mkono Wake. Hivyo, uamuzi Wake usingekosa kuwa sahihi. Kinyume na haya, tukilinganisha uweza wa Mungu, binadamu hajali katu, ni mjinga na asiyejua neno, asiyeona-mbele katu. Haya ndiyo tunayoona katika mabadilishano kati ya Ibrahimu na Mungu. Mungu amekuwa akiwasilisha mbele tabia Yake kuanzia mwanzo hadi leo. Hapa, vilevile, kuna pia tabia ya Mungu tunayofaa kuona. Nambari ni rahisi, na hazionyeshi chochote, lakini hapa kuna maonyesho muhimu sana ya tabia ya Mungu. Mungu asingeangamiza jiji kwa sababu ya watu hamsini wenye haki. Je, haya ni kutokana na rehema ya Mungu? Ni kwa sababu ya upendo na uvumilivu Wake? Je umeuona upande huu wa tabia ya Mungu? Hata kama kungekuwa na wenye haki kumi pekee, Mungu asingeangamiza jiji hili kwa sababu ya watu hawa kumi wenye haki. Je, haya yanaonyesha uvumilivu na upendo wa Mungu au la? Kwa sababu ya rehema, uvumilivu, na kujali kwa Mungu kwa wale watu wenye haki, Asingeliangamiza jiji hili. Huu ndio uvumilivu wa Mungu. Na hatimaye, ni matokeo gani tunayoyaona? Wakati Ibrahimu aliposema, “huenda wakaonekana huko kumi,” Mungu akasema, “Sitauharibu .” Baada ya hapo, Ibrahimu hakusema tena—kwani ndani ya Sodoma hakukuwa na wenye haki kumi aliowarejelea, na hakuwa na chochote ziada cha kusema, na kwa wakati huo alielewa ni kwa nini Mungu alikuwa ameamua kuangamiza Sodoma. Katika haya, ni tabia gani ya Mungu unayoiona? Ni aina gani ya utatuzi ambayo Mungu alifanya? Yaani, kama jiji hili lisingekuwa na wenye haki kumi, Mungu asingeruhusu uwepo wake, na bila shaka Angeliangamiza. Je hii si hasira ya Mungu? Je, hasira hii inawakilisha tabia ya Mungu? Je, hii tabia ni ufunuo wa kiini cha haki cha Mungu? Je, huu ni ufunuo wa kiini cha haki ya Mungu, ambacho binadamu hafai kukosea? Baada ya kuthibitisha kwamba hakukuwa na wenye haki kumi kule Sodoma, Mungu alikuwa na hakika ya kuliangamiza jiji, na angewaadhibu vikali watu walio ndani ya hilo jiji, kwani walimpinga Mungu, na kwa sababu walikuwa wachafu na waliopotoka.
Kwa nini tumechambua vifungu hivi kwa njia hii? Kwa sababu sentensi hizi chache rahisi zinatupa maonyesho kamili ya tabia ya Mungu ya wingi wa rehema na hasira kali. Wakati sawa na kuthamini sana wale wenye haki na kuwa na rehema juu yao, kuwavumilia, na kuwajali, ndani ya moyo wa Mungu kulikuwa na chukizo kuu kwa wale waliokuwa ndani ya Sodoma ambao walikuwa wamepotoshwa. Je, hii ilikuwa, au haikuwa rehema nyingi na hasira kali? Ni kwa mbinu zipi Mungu aliliangamiza jiji? Kwa moto. Na kwa nini Aliliangamiza kwa kutumia moto? Unapoona kitu kikiungua kwa moto, au wakati uko karibu kuchoma kitu, ni nini hisia zako juu ya kitu hicho? Kwa nini unataka kukichoma? Unahisi kwamba hukihitaji tena, kwamba hutaki tena kukiangalia? Unataka kukiacha? Matumizi ya moto na Mungu yanamaanisha uwachaji, na chuki, na kwamba hakutaka tena kuiona Sodoma. Hii ilikuwa ni hisia iliyomfanya Mungu kuteketeza Sodoma kwa moto. Matumizi ya moto yanawakilisha namna ambavyo Mungu alikuwa amekasirika. Rehema na uvumilivu wa Mungu kwa kweli vipo, lakini utakatifu na uhaki wa Mungu Anapoachilia hasira Yake pia inaonyesha binadamu upande wa Mungu usiyovumilia kosa lolote. Wakati binadamu anaweza kabisa kutii amri za Mungu na kutenda kulingana na mahitaji ya Mungu, Mungu anakuwa mwingi katika huruma Yake kwa binadamu; wakati binadamu amejawa na upotoshaji, chuki na uadui kwake Yeye, Mungu anakuwa mwenye ghadhabu nyingi. Na anakuwa na ghadhabu nyingi hadi kiwango kipi? Hadi kiwango kipi ndipo anapokuwa na ghadhabu nyingi? Hasira yake itaendelea kuwepo mpaka pale ambapo Mungu hataona tena upinzani wa binadamu na matendo maovu, mpaka vyote hivi havipo tena mbele ya macho Yake. Hapo tu ndipo ghadhabu ya Mungu itakapotoweka. Kwa maneno mengine, haijalishi mtu husika ni yupi, kama moyo wake umekuwa mbali na Mungu, na yeye amemgeukia Mungu, asirudi tena, basi haijalishi ni vipi, kwa mionekano yote au kuhusiana na matamanio yake ya kibinafsi, atapenda kuabudu na kufuata na kutii Mungu katika mwili wake au katika kufikiria kwake pindi tu moyo wake utakapokuwa mbali na ule wa Mungu, hasira ya Mungu itaachiliwa bila kikomo. Itakuwa kwamba wakati Mungu anapoiachilia kabisa ghadhabu Yake, akiwa amempa binadamu fursa za kutosha, pindi inapoachiliwa hakutakuwepo na njia yoyote ya kuirudisha, na hatawahi tena kuwa mwenye huruma na mvumilivu kwa mtu kama huyo. Huu ni upande mmoja wa tabia ya Mungu isiyovumilia kosa. Hapa, yaonekana kawaida kwa watu kwamba Mungu angeliangamiza jiji, kwani ndani ya macho ya Mungu, jiji lililojaa dhambi lisingeweza kuwepo na kuendelea kubakia pale, na ilikuwa jambo ya kueleweka kwamba jiji hilo liangamizwe na Mungu. Lakini katika kile kilichofanyika kabla ya na kufuatia uangamizi Wake wa Sodoma, tunaiona tabia nzima ya Mungu. Yeye ni mvumilivu na mwenye huruma kwa viumbe walio na upole, na wenye wema; kwa vitu viovu, na vyenye dhambi, na vilivyojaa maovu, Yeye anayo hasira kali , kiasi cha kwamba Hawachi kuendeleza hasira Yake. Hivi ndivyo vipengele viwili vikuu na vinavyojitokeza zaidi kuhusu tabia ya Mungu, na, zaidi, vimefichuliwa na Mungu kutoka mwanzo hadi mwisho: wingi wa huruma na ghadhabu nyingi. Wengi wenu hapa mmepitia huruma ya Mungu, lakini wachache sana wameweza kutambua hasira ya Mungu. Huruma na upole wa upendo wa Mungu unaweza kuonekana kwa kila mmoja; yaani, Mungu Amekuwa mwingi wa huruma kwa kila mmoja. Ilhali ni nadra sana—au, inaweza kusemekana, kwamba—Mungu amekuwa na ghadhabu nyingi kwa watu binafsi au sehemu yoyote ya watu miongoni mwenu hapa leo. Tulia! Hivi karibuni au baadaye, hasira ya Mungu itaonekana na kupitiwa na kila mmoja, lakini kwa sasa bado muda haujawadia. Na kwa nini hivi? Kwa sababu wakati Mungu anakuwa na ghadhabu kila mara kwa mtu, yaani, wakati Anapoiachilia hasira Yake kuu kwao, inamaanisha kwamba Amekuwa akichukia na Akikataa kwa muda mrefu mtu huyu, kwamba Anadharau uwepo wake na kwamba Hawezi kuvumilia uwepo wake; pindi tu ghadhabu Yake inapomjia, watatoweka. Leo, kazi ya Mungu bado haijafikia hapo. Hakuna yeyote kati yenu ambaye ataweza kuivumilia pindi tu Mungu anapoghadhabika kupindukia. Unaona, kisha, kwamba kwa wakati huu Mungu anayo huruma nyingi tu kwa watu wote, na ungali hujaona ghadhabu yake nyingi. Kama wapo wale wanaobakia wakiwa hawajashawishika, mnaweza kuuliza kuwa hasira ya Mungu ije kwenu e, ili mweze kuipitia na kujua kama ghadhabu ya Mungu na tabia Yake isiyokosewa kwa binadamu ipo kwa kweli au la. Mtathubutu kufanya hivyo?

Watu Wa Siku Za Mwisho Wanaiona tu Hasira Ya Mungu Katika Maneno Yake, na Hawaipitii kwa Kweli Hasira Ya Mungu

Je, pande mbili za tabia ya Mungu zinazoonekana kwenye vifungu hivi vya maandiko zinastahili ushirika? Baada ya kuisikia hadithi hii, je, unao uelewa mpya kuhusu Mungu? Ni uelewa aina gani? Inaweza kusemekana kwamba kuanzia wakati wa uumbaji mpaka leo, hakuna kikundi ambacho kimefurahia neema au huruma nyingi za Mungu pamoja na upole wa upendo kama kikundi hiki cha mwisho. Ingawaje, kwenye awamu ya mwisho, Mungu amefanya kazi Yake ya hukumu na kuadibu, na Amefanya kazi Yake kwa adhama na hasira, wakati mwingi Mungu anatumia tu maneno kukamilisha kazi Yake; Anatumia maneno ili kufunza, kunyunyiza na kutosheleza, na kulisha. Hasira ya Mungu, wakati haya yakiendelea, siku zote imefichwa, na mbali na kuipitia tabia ya Mungu yenye hasira kwa maneno Yake, watu wachache sana wamepitia ghadhabu Yake ana kwa ana. Hivi ni kusema, kwamba wakati wa kazi ya hukumu na kuadibu kwa Mungu, ingawaje hasira iliyofichuliwa katika maneno ya Mungu inawaruhusu watu kupitia adhama na kutovumilia kosa kwa Mungu, hasira hii haizidi maneno Yake. Kwa maneno mengine, Mungu hutumia maneno ili kukemea binadamu, kumfichua binadamu, kuhukumu binadamu, kumwadhibu binadamu na hata kumshutumu binadamu—lakini Mungu angali hajawa mwenye wingi wa ghadhabu kwa binadamu, na hata hajaachilia hasira Yake kwa binadamu nje ya maneno yake. Hivyo, rehema na upole wa upendo wa Mungu uliopitiwa na binadamu kwenye enzi hii ni ufunuo wa tabia ya kweli ya Mungu, huku hasira ya Mungu iliyoipitiwa na binadamu ikiwa tu ni athari ya sauti na hisia za matamko Yake. Watu wengi wanachukulia athari hii kimakosa na kuiona kuwa njia ya kweli ya kupitia na maarifa ya kweli ya hasira ya Mungu. Hivyo basi, watu wengi wanasadiki kwamba wameiona huruma ya Mungu na upole wa upendo ndani ya maneno Yake, kwamba wameweza pia kushuhudia kutovumilia Kwake kwa kosa la binadamu, na wengi wao wamekuja hata kutambua huruma na uvumilivu wa Mungu kwake binadamu. Haijalishi tabia ya binadamu ni mbaya kiasi kipi, au upotovu wa tabia yake, Mungu siku zote anavumiliwa. Katika kuvumiliwa, nia Yake ni kusubiria maneno Aliyokuwa Ametamka, jitihada Alizofanya na gharama Aliyolipia ili kutimiza athari iliyo ndani ya wale Anaotaka kupata. Kusubiria matokeo kama haya yanachukua muda, na yanahitaji uumbaji wa mazingira tofauti ya binadamu, kwa njia sawa ambayo watu hawawi watu wazima pindi tu wanapozaliwa; huchukua miaka kumi na minane au kumi na tisa na baadhi ya watu hata huhitaji miaka ishirini au thelathini kabla hawajakomaa na kuwa mtu mzima halisi. Mungu husubiria kukamilika kwa mchakato huu, Yeye husubiria kuwadia kwa muda huo, na Yeye husubiria kufika kwa matokeo haya. Na kwa muda wote Anaousubiria, Mungu huwa mwenye wingi wa huruma. Kwenye kipindi cha kazi ya Mungu, hata hivyo, kiwango kidogo sana cha watu kinaangamizwa, na baadhi wanaadhibiwa kwa sababu ya upinzani wao mkuu kwa Mungu. Mifano kama hiyo ni ithibati kubwa zaidi ya tabia ya Mungu ambayo haivumilii kosa la binadamu, na inathibitisha kabisa uwepo wa kweli wa uvumilivu na ustahimilivu wa Mungu kwa wale wateule. Bila shaka, katika mifano hii halisi, ufunuo wa sehemu ya tabia ya Mungu kwa watu hawa hauathiri jumla ya mpango wa usimamizi wa Mungu. Kwa hakika, kwenye awamu hii ya mwisho ya kazi ya Mungu, Mungu amevumilia kwenye kipindi hiki chote ambacho Amekuwa akisubiria na Amebadilisha uvumilivu Wake na maisha Yake kwa wokovu wa wale wanaomfuata Yeye. Unayaona haya yote? Mungu haharibu mpango Wake bila sababu. Anaweza kuiachilia hasira Yake na Anaweza pia kuwa mwenye huruma; huu ndio ufunuo wa sehemu mbili kuu za tabia ya Mungu. Je, hii iko au haiko wazi kabisa? Kwa maneno mengine, tunapokuja kwa Mungu, sahihi na isiyokuwa sahihi, yenye haki na dhalimu, nzuri na mbaya—hivi vyote vimeonyeshwa waziwazi kwa binadamu. Kile Atakachofanya, kile Anachopenda, kile Anachochukia—yote haya yanaweza kuonyeshwa moja kwa moja katika tabia Yake. Mambo kama hayo yanaweza pia kuwa ya waziwazi sana na ya kuonekana katika kazi ya Mungu na hayako juujuu au kwa jumla; badala yake, yanaruhusu watu wote kutazama tabia ya Mungu na kile Anacho na alicho hasa kwa njia thabiti, ya kweli na ya kimatendo. Huyu ndiye Mungu Mwenyewe wa kweli.

Tabia ya Mungu Haijawahi Kufichwa Kutoka Kwa Binadamu—Moyo wa Binadamu Umepotoka kwa Mungu

Kama Sikushiriki kuhusu mambo haya, hakuna yeyote kati yenu ambaye angeweza kutazama tabia ya kweli ya Mungu katika hadithi za Biblia. Hii ni ukweli. Hiyo ni kwa sababu, ingawaje hadithi hizi za kibiblia zilirekodi baadhi ya mambo ambayo Mungu alifanya, Mungu aliongea mambo machache na hakuitambulisha tabia Yake kwa njia ya moja kwa moja au kuwasilisha mbele waziwazi mapenzi Yake kwa binadamu. Vizazi vya baadaye vimechukulia rekodi hizi kama tu hadithi, na hivyo yaonekana kwa watu kwamba Mungu anajificha kutoka kwa binadamu na kwamba si mwili wa Mungu ambao umefichwa kutoka kwa binadamu, lakini tabia na mapenzi Yake. Baada ya ushirika wangu leo, bado unahisi kwamba Mungu amefichwa kabisa kutoka kwa binadamu? Bado unasadiki kwamba tabia ya Mungu imefichwa kutoka kwa binadamu?
Tangu wakati wa uumbaji, tabia ya Mungu imeenda sako kwa bako na kazi Yake. Haijawahi kufichwa kutoka kwa binadamu, lakini imewekwa kadamnasi na kwa dhahiri kabisa kwa binadamu. Ilhali, kwa kadri muda unavyopita, moyo wa binadamu umekua hata mbali zaidi na Mungu, na kwa kuwa upotovu wa mwanadamu umekuwa wa kina zaidi, binadamu na Mungu wamekuwa mbali na mbali zaidi kati yao. Kwa utaratibu lakini kwa uhakika, binadamu ametoweka kutoka kwa macho ya Mungu. Binadamu ameshindwa kuweza “kuona” Mungu, jambo ambalo limemwacha yeye bila “habari” zozote kuhusu Mungu; hivyo, hajui kama Mungu yupo, na hata anaenda mbali mno kiasi cha kukataa kabisa kuwepo kwa Mungu. Kwa hivyo, kutofahamu kwa binadamu kuhusu tabia ya Mungu na kile Anacho na alicho si kwa sababu Mungu amefichwa kutoka kwa binadamu, lakini kwa sababu moyo wake umemgeukia Mungu. Ingawaje binadamu anamsadiki Mungu, moyo wa binadamu haupo na Mungu, na hajui chochote kuhusu namna ya kumpenda Mungu, wala hataki kumpenda Mungu, kwani moyo wake haujawahi kusonga karibu na Mungu na siku zote anamuepuka Mungu. Kutokana na haya, moyo wa binadamu umekuwa mbali sana na Mungu. Kwa hivyo moyo wake uko wapi? Kwa hakika, moyo wa binadamu haujaenda popote: Badala ya kuupatia moyo huo Mungu, au kuufichua kwa Mungu ili Aweze kuuona, amejiekea yeye mwenyewe. Hiyo ni licha ya ukweli kwamba baadhi mara nyingi wanamwomba Mungu na kusema, “Ee Bwana, utazame moyo wangu—unajua yote ninayofikiria,” na baadhi hata huapa kumruhusu Mungu kuwafikiria, kwamba waweze kuadhibiwa kama watavunja kiapo chao. Ingawaje binadamu anamruhusu Mungu kuangalia ndani ya moyo wake, hii haimanishi kwamba anaweza kutii mipango na mipangilio ya Mungu, wala kwamba ameacha hatima na matarajio yake na mambo yake yote katika udhibiti wa Mungu. Hivyo, licha ya viapo unavyotoa kwa Mungu au mwelekeo kwake Yeye, kwa macho ya Mungu moyo wako ungali umefungwa kwake Yeye, kwani unamruhusu Mungu tu kuangalia kwenye moyo wako lakini humruhusu Yeye kuudhibiti. Kwa maneno mengine, hujampa Mungu moyo wako kamwe, na unazungumza tu maneno yanayosikika kuwa matamu ili Mungu asikie; nia zako mbalimbali za kijanja, huku, unajificha kutoka kwa Mungu, unajificha usionekane na Mungu, pamoja na maajabu, njama, na mipango yako, na unashikilia matarajio na hatima yako mikononi mwako, ukiwa na hofu kubwa kwamba huenda yakachukuliwa na Mungu. Hivyo, Mungu hatazamii uaminifu wa binadamu kwake Yeye. Ingawaje Mungu anaangalia kina cha moyo wa binadamu, na Anaweza kuona kile ambacho binadamu anafikiria na anataka kufanya moyoni mwake, na Anaweza kuona ni mambo yapi yamewekwa ndani ya moyo wake, moyo wa binadamu haumilikiwi na Mungu, hajautoa ili udhibitiwe na Mungu. Hivi ni kusema, Mungu anayo haki ya kuangalia, lakini Hana haki ya kuudhibiti moyo huo. Kwenye nadharia za kibinafsi za binadamu, binadamu hataki wala hanuii kujiacha kwenye huruma za Mwenyezi Mungu. Binadamu hajajifungia tu kutoka kwa Mungu, bali kunao hata watu wanaofikiria njia za kusetiri mioyo yao, kwa kutumia mazungumzo matamu na sifa za kinafiki ili kuunda hali ya uongo na kupata uaminifu wa Mungu, na kuficha uso wao wa kweli dhidi ya kuonekana na Mungu. Nia yao ya kutomruhusu Mungu kuona ni kutoruhusu Mungu kuelewa namna walivyo kwa kweli. Hawataki kuitoa mioyo yao kwa Mungu lakini wanajihifadhia wao wenyewe. Maandishi madogo ya haya ni kwamba kile ambacho binadamu anafanya na kile ambacho anataka kimepangiliwa chote, kikapigiwa hesabu, na kuamuliwa na binadamu mwenyewe; haihitaji kushiriki au kuingilia kati kwa Mungu, na isitoshe hahitaji mipango na mipangilio ya Mungu. Hivyo, iwapo ni kuhusiana na amri za Mungu, agizo Lake, au mahitaji ambayo Mungu anamwekea binadamu, uamuzi wa binadamu unatokana na nia na maslahi yake mwenyewe, katika mazingira na hali yake mwenyewe ya wakati huo. Siku zote binadamu anatumia maarifa na maono ambayo amezoeana nayo, na akili zake binafsi ili kuamua na kuchagua njia anayofaa kutembelea na haruhusu uingiliaji kati au udhibiti wa Mungu. Huu ndio moyo wa binadamu ambao Mungu anaona.
Juni 13, 2014
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili 
Kujua zaidi:  Kuhusu Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni