Smiley face

Jumanne, 14 Novemba 2017

Sura ya 16. Imani Tatu katika Mungu wa Vitendo


Mwenyezi Mungu alisema, Ndani ya familia ya Mungu, kuna imani kadhaa tofauti katika Mungu; imani hizi tofauti lazima zitambulishwe ili kuona wewe ni wa gani.Na imani ya aina ya kwanza, ambayo pia ni aina bora zaidi, mtu huyo ana uwezo wa kuyaamini maneno ya Mungu katika vitu vyote; ana uwezo wa kukubali ufichuzi wote wa Mungu, ushugulikiaji, na upogoaji; yeye ni mwagalifu kwa mapenzi ya Mungu, hupenda, ni mwaminifu kwa, na humwabudu Mungu, na ako tayari kutenda ukweli.  Imani kama hiyo huzaa maisha, na inawezesha mtu kupata mabadiliko katika tabia na kupatwa na Mungu.
Na imani ya aina ya pili, mtu huyo anamwamini Mungu kwa kiasi, lakini pia ni mwenye tuhumu kwa kiasi. Wakati kazi ya Mungu hairidhiani na yeye, angefanya ulinganishi katika moyo wake, akiwa na shaka kama Mungu Anapaswa kuwa akifanya vitu kama hivyo. Mara kwa mara anamtuhumu Mungu, kwa hivyo ana uwezo tu wa kumtii Mungu kwa kiasi, na hana uwezo wa kumtii Mungu katika vitu vingine; anaweza kulitii lile ambalo analiamini ni sawa, lakini ana mawazo yake mwenyewe anapokabiliwa na vitu ambavyo anahisi si sawa, na migongano katika moyo wake, na anakataa kuyatekeleza. Hili pia ni aina ya imani. Kimo cha watu siku hizi ni hasa kama hiki, wao wana uwezo tu wa kutii kile wanachohisi kuwa sawa, wao hawana uwezo wa kutii kile wanachohisi si sawa, na hawatatekeleza kile ambacho hawako tayari kufanya. Kadhalika, wakati mwingine hali ikiwa, wana shauku na Mungu, wakihisi kwamba wanapaswa kuwa waangalifu kwa mzigo wa Mungu, hivyo wanatimiza wajibu wao; au wakati mwingine wanashughulishwa na ushirika, wanapata Mungu kuwa wa kupendeka kabisa, na sasa tu ndio wenye imani katika Mungu kwa kiasi fulani. Hasa, imani yao katika Mungu ni tu kufuata umati; hawana upendo kwa Mungu, wala si waangalifu kwa Mungu, wakati bila shaka hawamtii na hawamwabudu Mungu kwa kweli. Kwa watu walio na imani kama hii katika Mungu, wako tu na kiasi cha wastani cha upendo, uangalifu, na utiifu kwa Mungu, kwa muda fulani, na inafanyika tu wakati Roho Mtakatifu hasa Anasonga, wakati Roho Mtakatifu anafanya kazi Yake. Wakati wako katika hali mbaya, au wakati wanachanganywa na wengine, wakati wao ni dhaifu na wamekata tamaa, vitu hivi vimeenda, vimetokomea, wakati wao wenyewe hawana habari jinsi hilo limekuja kupita. Hawana uwezo tena wa kumpenda Mungu hata wakitaka, hawana motisha ya kutenda maneno ya Mungu tena, na kisha wanaona kazi ya Mungu kama ya desturi sana, ya kawaida sana; hata kama wao hawana tuhuma tena, wao hawana ari yoyote tena. Kimo cha watu wengi zaidi kiko katika hatua hii, na hii ndiyo aina ya pili ya imani.
Na aina ya tatu ya imani, mtu hana uelewa wa Mungu mwenye mwili, kwake Yeye hujitokeza tu kama mtu wa kawaida, na hakuna tofauti kubwa inaweza kutambulishwa. Kwa hivyo, anamchukulia Mungu mwenye mwili kama tu mtu wa kawaida lakini mwenye cheo cha heshima, ana uwezo wa kufuatana na Mungu na kusema kitu kizuri, na pia ana uwezo wa kuandamana katika imani, lakini imani hii si imani halisi. Ana uwezo wa kufuatana na mambo ya upuuzi mara moja moja, lakini hakuna upendo kwa Mungu katika mtu wa aina hii—upendo si kujali kuhusu mwili lakini utiifu wa kweli katika kazi ya mtu na katika kutimiza wajibu wa mtu, kuwa mwangalifu kwa Mungu na kumcha Mungu. Upendo kwa Mungu ni kitu ambacho mtu aliye na uzoefu mkubwa tu anaweza kutangaza, si kitu ambacho mtu anaweza kusema kwa kupitia tu, kuona kwamba mtu ametekwa na hisia kali hivyo kusema kwamba huyu na huyu humpenda Mungu sana. Ama kusema kwamba watu kutoka dhehebu fulani humpenda Mungu kwa kweli. Huu ni upuuzi. Mtu kama huyu hawezi kukubali na kutii kwa urahisi kunapokuja kwa mambo ya upuuzi, na anapokabiliwa na mambo ya muhimu yanayohusiana na ukweli, hawezi kutii tu, na pia ana mawazo yake mwenyewe, hata anakuwa na tuhuma kuhusu Mungu. Watu kama hawa pia wako katika walio wengi. Wao ni wenye tuhuma kila wakati kuhusu Mungu: Je, huyu ni Mungu? Je, ni kwa nini Yeye hafanani na Mungu? Baadhi ya mambo Alivyosema labda yameelekezwa na Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu alimwelekeleza kusema mambo fulani, na kufanya vitu fulani. …Imani ya watu kama hawa ni ya kusikitisha zaidi.
Kiwango cha imani ya mtu katika Mungu, utiifu kwa Mungu, upendo, uangalifu, na uchaji kwa Mungu, kinatambulishwa hasa na yafuatayo:
Kwanza, kina msingi katika ikiwa mtu huyo hupenda ukweli. Kama unapenda ukweli basi unaweza kuendelea kuufuatilia zaidi, kisha unaweza kulenga kuwa na uelewa wa ukweli, wa maneno ya Mungu, wa kazi ya Mungu, wa umuhimu wa kupata mwili kwa Mungu, wa tabia ya Mungu, na uelewa wa Mungu una msingi hasa katika hiki kitu kimoja. Kadiri Unavyoweza kuelewa Mungu zaidi ndivyo unavyoweza kumtambua zaidi; kadiri unavyoweza kumwelewa Mungu zaidi ndivyo unavyoweza kumfuata bila kuyumbayumba. Hiyo ni, uelewa wa Mungu una msingi katika kufuatilia ukweli.
Pili, kina msingi katika uelewa wa mtu huyo wa Mungu mwenye mwili, hiyo ni muhimu. Bila uelewa wa Mungu wa vitendo, mazungumzo ya kumtii Mungu, kumpenda Mungu, kushuhudia Mungu, na kumhudumia Mungu yote ni maneno matupu. Vitu kama hivi haviwezi tu kufikiwa.
Tatu, kina msingi katika ubinadamu wa mtu huyo, lakini hili si halisi. Kwa sababu, baadhi ya watu wana ubinadamu mzuri, wao ni watu wazuri, lakini wao hawapendi ukweli. Kama wao hawana uelewa kabisa wa Mungu mwenye mwili, basi imani yao haiwezi kusiama, na wakati mwingine nia zao nzuri bila kujua husababisha madakizo. Je, unaweza kusema kwamba wao ni watu ambao wanamwamini Mungu kwa kweli? Wao ni wenye shauku, ni wa asili nzuri, na hufanya mambo fulani mazuri, lakini haya ni tabia nzuri tu ya nje, haya ni sura ya juu juu, haya hayaonyeshi kwamba imani yao ni halisi. Ukisema kwamba kwa kweli unamwamini Mungu, kweli unampenda Mungu, lazima uwe na uwezo wa kusema kwa nini unampenda Mungu, upendo wako kwa Mungu una msingi kwa nini, kwa nini unamwamini Yeye, kama wewe unaufuata umati tu ama unamwamini Yeye kwa sababu unaweza kumwona kwa kweli kama Mungu, imani na upendo wako kwa Mungu yana msingi katika ukweli upi: Haya lazima yategemezwe kwa misingi. Baadhi ya watu hupenda kusema kwamba wanamwamini Mungu kwa kweli na wanampenda Mungu, lakini wakati mtu anatamani kuwasiliana nao ukweli kwa uzito, hawana kitu cha kusema. Nimesikia watu wengi wakisema: “Mimi husikiza chochote ambacho Mungu husema, naamini yote ambayo Mungu husema, kwa njia yoyote ambayo Yeye huyasema. Sina mawazo yangu mwenyewe bila kujali kile Mungu husema, sina mawazo yangu mwenyewe bila kujali kile Mungu hufanya.” Je, wewe kweli ni mtu anayempenda Mungu kwa sababu tu umesema mambo kama haya? Lazima uwe na uzoefu halisi, lazima uwe na uwezo wa kuongea kuhusu uelewa halisi wa Mungu mwenye mwili. Pia, ni nini kiini cha Mungu, ni vitu vipi ambavyo watu huona vigumu kumtii Mungu katika, ni vitu vipi ambavyo watu wanaweza kumtii Mungu katika, wanamtii Mungu kwa kiasi gani, ni vitu vipi ambavyo huna uwezo wa kumtii Mungu katika, unatatua vipi mawazo yako kuhusu Mungu, unapanua vipi uelewa wako wa Mungu polepole? Kama unakosa uzoefu kama huo, basi huna mapenzi ya kweli kwa Mungu. Baadhi ya watu wana furaha hasa wanapoona kufika kwa Mungu, wanampokea kwa ukarimu, na kisha wanalia Mungu Anapoondoka. Watu wengine hufikiri kwamba hili ni onyesho la upendo wake kwa Mungu, lakini hili kweli linaweza kuonyesha kwamba anampenda Mungu? Hili linaweza kuonyesha tu kwamba anao moyo wenye ari, lakini mtu hawezi kusema kwamba matendo na maonyesho yake ni upendo kwa Mungu, kwamba ni imani ya kweli. Baadhi ya watu hutoa pesa kiasi, lakini hilo ni upendo kwa Mungu? Ama unaenda haraka kumwaga gilasi ya maji wakati unaambiwa, lakini hilo ni utiifu wa kweli? Kadhalika, watu wengine husema: “Nilimwamini Mungu baada ya mimi kusoma maneno ya Mungu, niliamini katika kupata mwili kwa Mungu, sina shaka baada ya mimi kumwona Mungu katika mwili wa kawaida.” Je, hili linaweza kuitwa imani ya kweli? Je, umekuwa na ushughulikaji na Mungu? Je, umejihusisha na Yeye? Je, unajua tabia Yake? Je, unajua ni nini Yeye hupenda? Je, unajua vitu unafanya ambavyo vinaikosea tabia Yake? Je, unajua upotovu ndani yako ambao Yeye huchukia? Je, unajua watu ambao Ameleta tabia Yake yenye haki kwao? Je, unajua ni watu wagani Yeye huchukia? Je, unajua ni masuala yapi unayo ambayo Yeye huchukia zaidi? Kama hujui vitu vyovyote kama hivi, linaonyesha kwamba kwa kweli huna uelewa wa Mungu. Huwezi kusema kwamba unamwamini Mungu kwa kweli, huwezi kusema kwamba unamtii Mungu kabisa, na bila shaka huwezi kusema kwamba unafanya vitu kulingana na mapenzi ya Mungu, kwamba unampenda Mungu, unamtii Mungu, ama unamwelewa Mungu. Unaweza kusema tu, kuhusu jambo hili, unayaelewa mapenzi Yake, unajua ni nini Yeye hupenda, kwamba unatenda kulingana na mapenzi ya Mungu katika jambo hili, kwamba unatenda kulingana na ukweli, kwamba unamtii katika jambo hili. Je, wewe ni mtu mtiifu kwa Mungu kwa sababu umemtii katika jambo hili tu? Huwezi kusema hilo, na kusema kwamba mtu humpenda Mungu kwa kuweka msingi tu kwa kitu cha juujuu, hilo ni kosa kubwa. Ukweli kwamba ulitenda kitu kizuri, ama kwamba umemjali Mungu hasa, huonyesha tu kwamba wewe ni mtu mwema, lakini hauonyeshi kwamba wewe ni mwangalifu kwa mapenzi ya Mungu. Bila shaka, upendo wa Mungu na kuwa mwangalifu kwa mapenzi ya Mungu yamejengwa juu ya msingi wa ubinadamu, na hakuwezi kuwa na upendo wa Mungu bila ubinadamu, kwa hivyo kila mmoja wenu lazima ajichunguze na aangalie mahali alipo. Baadhi ya watu hufikiri kwamba wao wako karibu hapo, lakini hili si lenye uhalisi; ilhali baadhi ya watu huenda kwa kiwangi kilichokithiri na hufikiri kwamba hakuna kitu kizuri kuwahusu, kwamba hawawezi kuachwa, na huu ni mtazamo hasi. Baadhi ya watu hufikiri kwamba hakuna mazuri ndani yao, na baadhi ya watu hujifafanua kama mtu anayempenda Mungu. Wao wako katika upande wa kushoto kabisa au katika upande wa kulia kabisa; huu ndio uhalisi wa watu hawa, ambao unaonyesha kwamba wao bado hawako katika njia sawa. Wao wanapaswa kuendelea kujitahidi kuwa dhahiri kuhusu ukweli, na kuingia katika uhalisi, ili kufuata mapenzi ya Mungu.
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni