Kutotikisika kwa Uadilifu wa Ayubu Kunaleta Aibu Kwake Shetani na Kusababisha Shetani Kutoroka kwa Wasiwasi
Mwenyezi Mungu alisema: Na ni nini ambacho Mungu alifanya wakati Ayubu alipopitia mateso haya? Mungu aliangalia, na kutazama, na Akasubiri matokeo. Wakati Mungu Alipokuwa akiangalia na kutazama, Alihisi vipi? Alihisi kuwa mwenye huzuni, bila shaka. Lakini, kutokana na huzuni Yake, Aliweza kujuta ruhusa Yake kwa Shetani ya kumjaribu Ayubu? Jibu ni, La, Asingefanya hivyo. Kwani Yeye alisadiki kwa dhati kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu, kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mungu alikuwa amempa Shetani tu fursa ya kuthibitisha uhaki wa Ayubu mbele ya Mungu, na kufichua maovu yake Shetani na hali ya kudharauliwa kwake binafsi.
Ilikuwa, zaidi ya hapo, fursa ya Ayubu kutolea ushuhuda utakatifu wake na kumcha Mungu kwake na kujiepusha na maovu mbele ya watu wa ulimwengu, Shetani, na hata wale wanaomfuata Mungu. Je, matokeo ya mwisho yalithibitisha kwamba ukadiriaji wa Mungu kuhusu Ayubu ulikuwa sahihi na bila makosa? Je, Ayubu alimshinda kweli Shetani? Hapa tunasoma kuyahusu maneno yale halisi yaliyozungumzwa na Ayubu, maneno ambayo ni thibitisho kwamba alikuwa amemshinda Shetani. Alisema: “Nilitoka tumboni mwa mama yangu nikiwa uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile.”Huu ndio mwelekeo wa utiifu ambao Ayubu anao kwa Mungu. Kisha, akasema: “BWANA alinipa, na BWANA amechukua; jina la BWANA libarikiwe..” Maneno haya yaliyozungumzwa na Ayubu yanathibitisha kwamba Mungu anaangalia kina cha moyo wa binadamu, kwamba Anaweza kuangalia kwenye akili ya binadamu, na yanathibitisha kwamba kuidhinisha kwake kwa Ayubu hakuna kosa, kwamba binadamu huyu aliyeidhinishwa na Mungu alikuwa mwenye haki. “…BWANA alinipa, na BWANA amechukua; jina la BWANA libarikiwe.”Maneno haya ni ushuhuda wa Ayubu kwa Mungu. Yalikuwa maneno haya ya kawaida yaliyomfanya Shetani kuogopa, yaliyoleta aibu kwake na kumsababisha kutoroka kwa wasiwasi, na, vilevile, yaliyomfunga pingu Shetani na kumuacha bila rasilimali zozote. Hivyo, pia, ndivyo maneno haya yalivyomfanya Shetani kuhisi matendo ya kustaajabisha na yenye nguvu ya Yehova Mungu, na kumruhusu kuelewa haiba kubwa na isiyo ya kawaida ya yule ambaye moyo wake ulitawaliwa na njia ya Mungu. Zaidi, yalionyesha Shetani nguvu za kipekee zilizoonyeshwa na mtu mdogo asiyekuwa na umuhimu wowote katika kutii njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu Shetani hivyo basi alishindwa kwenye shindano la kwanza. Licha ya utambuzi wake “uliopatikana kwa hali ngumu,” Shetani hakuwa na nia ya kumwachilia Ayubu, wala hakukuwa na badiliko lolote katika asili yake ya unafiki. Shetani alijaribu kuendelea kumshambulia Ayubu, na kwa mara nyingine tena akamjia Mungu …
Kisha, hebu tuyasome maandiko kuhusu mara ya pili ambapo Ayubu alijaribiwa.
3. Shetani Amjaribu Ayubu Mara Nyingine Tena (Majipu Mabaya Yaupiga Mwili wa Ayubu)
a. Maneno Yaliyotamkwa na Mungu
(Ayubu 2:3) BWANA akamwuliza Shetani, je, umemwangalia mtumishi wangu Ayubu, kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu; naye hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ujapokuwa ulinichochea dhidi yake, ili nimwangamize pasipo sababu.
(Ayubu 2:6) BWANA akamwambia Shetani, Tazama, yeye yumo mkononi mwako; lakini uutunze uhai wake.
b. Maneno Yaliyotamkwa na Shetani
(Ayubu 2:4-5) Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake. Lakini sasa nyosha mkono wako, uuguse mfupa wake na nyama yake, naye atakukufuru mbele ya uso wako.
c. Namna Ayubu Anavyoshughulikia Majaribio
(Ayubu 2:9-10) Kisha mkewe akamwambia, Je, Wewe bado unashikamana na utimilifu wako? mkufuru Mungu, ufe. Lakini yeye akamwambia, Wewe unazungumza kama mmoja wa wanawake wapumbavu wanavyozungumza. Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika yote haya Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.
(Ayubu 3:3) ) Itokomee mbali ile siku niliyozaliwa, na ule usiku uliosema, Mtoto mume ameingia katika mimba.
Upendo wa Ayubu ya Njia ya Mungu Inazidi Yoyote Ile Nyingine
Maandiko yanarekodi maneno haya yaliyozungumzwa kati ya Mungu na Shetani: “BWANA akamwuliza Shetani, je, umemwangalia mtumishi wangu Ayubu, kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu; naye hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ujapokuwa ulinichochea dhidi yake, ili nimwangamize pasipo sababu” (Ayubu 2:3). Katika maneno haya Mungu Anarudia swali moja kwa Shetani. Ni swali linalotuonyesha ukadiriaji wa uthibitisho wa Yehova Mungu kuhusu kile kilichoonyeshwa na kuishi na kudhihirishwa na Ayubu kwenye jaribio lake la kwanza, na ule ambao si tofauti na ukadiriaji wa Mungu wa Ayubu kabla ya kupitia jaribio lile la Shetani. Hivi ni kusema, kabla jaribio halijamfika, katika macho ya Mungu Ayubu alikuwa mtimilifu, na hivyo basi Mungu Alimlinda yeye na familia yake, na Akambariki, alistahili kubarikiwa kwa macho ya Mungu. Baada ya jaribio, Ayubu hakutenda dhambi kwa midomo yake kwa sababu alikuwa amepoteza mali yake na watoto wake, lakini aliendelea kulisifu jina la Yehova. Mwenendo wake halisi ulimfanya Mungu kumpongeza, na kumpa alama zote. Kwani machoni mwa Ayubu, watoto wake au rasilimali zake hazikutosha kumfanya yeye kumkataa Mungu. Nafasi ya Mungu katika moyo wake, kwa maneno mengine, isingeweza kusawazishwa na watoto wake au kipande chochote cha mali yake. Kwenye jaribio la kwanza la Ayubu, alimwonyesha Mungu kwamba upendo wake kwake na upendo wake wa njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu ulizidi kila kitu kingine. Ni kwa sababu tu jaribio hili lilimpa Ayubu uzoefu wa kupokea tuzo kutoka kwa Yehova Mungu na kufanya mali yake na watoto wake kuchukuliwa na Yeye.
Kwa Ayubu, hali hii aliyoipitia ilikuwa ya kweli na ambayo ilisafisha nafsi yake ikawa safi, ulikuwa ni ubatizo wa maisha uliotimiza uwepo wake, na, isitoshe, ilikuwa ni karamu ya kutosha iliyojaribu utiifu wake kwa, na yeye kumcha Mungu. Jaribio hili lilibadilisha hadhi ya Ayubu kutoka ule wa bwana tajiri hadi kwa mtu ambaye hakuwa na chochote, na pia likamruhusu kupitia dhuluma za shetani kwa mwanadamu. Ufukara wake haukumfanya kuchukia Shetani; badala yake, kwenye vitendo vibovu vya Shetani aliuona ubaya na hali ya kudharau ya Shetani pamoja na uadui wa Shetani na uasi wake kwa Mungu, na hali hii ilimhimiza vizuri zaidi kushikilia daima njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Aliapa kwamba asingewahi kumwacha Mungu na kugeuka njia ya Mungu kwa sababu ya mambo ya nje kama vile mali, watoto au urithi, wala hangewahi kuwa mtumwa wa Shetani, mali, au mtu yeyote; mbali na Yehova Mungu, hakuna mtu ambaye angekuwa Bwana wake, au Mungu wake. Hayo ndiyo yaliyokuwa maazimio ya Ayubu. Kwa upande mwingine wa jaribio, Ayubu alikuwa pia amepata jambo jingine: Alikuwa amepata utajiri mkubwa katikati ya majaribio hayo aliyoyapitia kutoka kwa Mungu.
Wakati wa maisha yake katika miongo kadhaa iliyopita, Ayubu aliyaona matendo ya Yehova na kupata baraka za Yehova Mungu kwake yeye. Zilikuwa ni baraka zilizomwacha akihisi wasiwasi mkubwa na mwenye wingi wa shukrani, kwani aliamini kwamba alikuwa hajamfanyia chochote Mungu, ilhali alikuwa amepata baraka nyingi na akawa anafurahia neema nyingi. Kwa sababu hii, ndani ya moyo wake mara nyingi aliomba, akitumai angeweza kumlipa Mungu, akitumai kwamba angekuwa na fursa ya Kuwa na ushuhuda wa matendo na ukubwa wa Mungu , na kutumai kwamba Mungu angeweza kuujaribu utiifu wake, na, zaidi, kwamba imani yake ingetakaswa, mpaka pale ambapo utiifu wake na imani yake vyote vingepata idhini ya Mungu. Na wakati Ayubu alipojaribiwa, alisadiki kwamba Mungu alikuwa amesikia maombi yake. Ayubu alifurahia sana fursa hii zaidi ya kitu kingine chochote, na hivyo basi hakuthubutu kuchukulia jambo hili vivi hivi, kwani tamanio kubwa zaidi la maisha yake lingetimia. Kufika kwa fursa hii kulimaanisha kwamba utiifu wake na kumcha Mungu vyote vingeweza kutiwa kwenye majaribu, na kutakaswa. Zaidi, ilimaanisha kwamba Ayubu alikuwa na fursa ya kupata idhini ya Mungu, hivyo kumleta karibu zaidi na Mungu. Wakati wa jaribio, imani kama hiyo na kufuatilia huko kulimruhusu yeye kuwa mtimilifu zaidi, na kupata uelewa mkubwa zaidi wa mapenzi ya Mungu. Ayubu alikuwa mwenye shukrani zaidi kwa baraka na neema za Mungu, katika moyo wake alimwaga sifa kubwa zaidi kwa matendo ya Mungu, na alizidi kumcha Mungu na kumstahi, na kutamani hata zaidi upendo, ukubwa, na utakatifu wa Mungu. Wakati huu, ingawaje Ayubu alikuwa bado yuleyule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu kwenye macho ya Mungu, kuhusiana na yale aliyopitia, imani na maarifa ya Ayubu vyote vilikuwa vimeimarika pakubwa: Imani yake ilikuwa imeongezeka, utiifu wake ulikuwa umeimarika pakubwa, na hali yake ya kumcha Mungu ilikuwa ya kina zaidi. Ingawaje jaribio hili lilibadilisha roho na maisha ya Ayubu, mabadiliko kama hayo hayakumtosheleza Ayubu, wala hayakufanya maendeleo yake ya kwenda mbele kwenda polepole. Wakati huo, akiwa anapiga hesabu kile alichokuwa amepata kutoka kwenye jaribio hilo, na akitilia maanani upungufu wake binafsi, aliomba kimyakimya, akisubiri jaribio linalofuata ambalo lingemsibu yeye, kwa sababu alitamani sana, imani, utiifu, na kumcha Mungu kwake kuweze kuimarishwa kwenye jaribio linalofuata la Mungu.
Mungu Anaziangalia fikira za ndani zaidi za binadamu na yale yote ambayo binadamu anasema na kufanya. Fikira za Ayubu zilifikia masikio ya Yehova Mungu, na Mungu alisikiliza maombi yake na kwa njia hii jaribio la Mungu kwa Ayubu lililofuata liliwasili kama lilivyotarajiwa.
Katikati ya mateso makuu, Ayubu Anatambua kwa kweli utunzaji wa Mungu kwa mwanadamu
Kufuatia maswali ya Yehova Mungu kwa Shetani, Shetani alifurahi kisirisiri. Kwa sababu Shetani alijua kwamba angeweza kwa mara nyingine kuruhusiwa kumshambulia mtu aliyekuwa mtimilifu katika macho ya Mungu—jambo ambalo kwa Shetani lilikuwa fursa ya nadra. Shetani alitaka kutumia fursa hii kudhalilisha kabisa kujitolea kwa Ayubu kumfanya kupoteza imani yake kwa Mungu na hivyo basi kutomcha Mungu tena au kubariki jina la Yehova. Hali hii ingempa Shetani fursa: Haijalishi ni wapi au ni muda gani, angeweza kumfanya Ayubu kuwa kikaragosi cha kufuata amri zake. Shetani alificha njama zake za maovu bila kuacha alama, lakini hakuweza kudhibiti asili yake ya maovu. Ukweli huu unaashiriwa kupitia kwa majibu yake kwa maneno ya Yehova Mungu, kama yalivyorekodiwa kwenye maandiko. “Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake. Lakini sasa nyosha mkono wako, uuguse mfupa wake na nyama yake, naye atakukufuru mbele ya uso wako” (Ayubu 2:4-5). Haiwezekani kutopata maarifa makuu na hali ya kuonea kijicho ya Shetani kutokana na mabadilishano haya kati ya Mungu na Shetani. Baada ya kusikia uongo huu wa Shetani, wale wote wanaoupenda ukweli na kuchukia uovu bila shaka watakuwa na chuki kubwa zaidi kwa utwezo na kutokuwa na aibu kwa Shetani, watahisi wakiwa wametishika na kusinyika kutokana na uongo wa Shetani, na, wakati huohuo, watatoa maombi yao ya kina na heri zao za dhati kwa Ayubu, wakiomba kwamba binadamu huyu mwenye unyofu ataweza kutimiza utimilifu wake, wakitamani kwamba binadamu huyu anayemcha Mungu na kujiepusha na maovu aweze kushinda milele majaribio ya Shetani, na kuishi kwa mwangaza, na kuishi katikati ya mwongozo na baraka za Mungu, hivyo, pia ndivyo watakavyotaka matendo ya haki ya Ayubu yaweze milele kuenea na kuhimiza wale wanaofuatilia njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na Shetani. Ingawaje nia ya kijicho ya Shetani inaweza kuonekana kupitia kwa tangazo hili, Mungu alikubali kwa urahisi “ombi” la Shetani — lakini alikuwa pia na sharti moja: “yeye yumo mkononi mwako; lakini uutunze uhai wake” (Ayubu 2:6). Kwa sababu, wakati huu, Shetani aliomba kunyosha mbele mkono wake ili kudhuru mwili na mifupa ya Ayubu, Mungu Alisema, “lakini okoa maisha yake.” Maana ya maneno haya ni kwamba alimpa Shetani mwili wa Ayubu, lakini Akabakiza maisha yake. Shetani asingeweza kuyachukua maisha ya Ayubu, lakini isipokuwa haya angeweza kutumia njia au mbinu zozote dhidi ya Ayubu.
Baada ya kupata ruhusa kutoka kwa Mungu, Shetani alimkimbilia Ayubu na kunyosha mbele mkono wake ili kuathiri ngozi yake na akamsababishia majipu mabaya yaliyoupiga mwili wake wote, naye Ayubu akahisi maumivu kwenye ngozi yake. Ayubu aliyasifu maajabu na utakatifu wa Yehova Mungu, jambo ambalo lilimfanya Shetani hata kuwa wazi zaidi katika ufidhuli wake. Kwa sababu alikuwa amehisi furaha ya kumwumiza binadamu, Shetani aliunyosha mkono wake na akakwaruza nyama ya Ayubu, na kusababisha majipu yake mabaya kutunga usaha.. Mara moja Ayubu alihisi maumivu na mateso kwenye mwili wake ambayo hayakuwa na kifani, na asingeweza kujisaidia kwa vyovyote vile isipokuwa kujikanda yeye mwenyewe kutoka kwenye kichwa hadi miguu akitumia mikono yake, ni kana kwamba kufanya hivi kungetuliza balaa ile iliyofanyikia roho yake kutokana na maumivu haya ya nyama za mwili wake. Alitambua kwamba Mungu Alikuwa kando yake akimwangalia, na akajaribu kwa njia bora zaidi kujituliza. Kwa mara nyingine alipiga magoti kwenye ardhi, na kusema: Unaangalia ndani ya binadamu, unauona umaskini wake; kwa nini unyonge wake unakuhusu wewe? Jina la Yehova Mungu lisifiwe. Shetani aliyaona yale maumivu yasiyovumilika ya Ayubu, lakini hakumwona Ayubu akiliacha neno la Yehova Mungu. Hivyo aliunyoosha haraka haraka mkono wake mbele ili kudhuru mifupa ya Ayubu, akiwa na tamaa ya kudhuru kila kiungo cha mwili wake. Mara, Ayubu akahisi mateso asiyoyatarajia; ni kana kwamba mwili wake ulikuwa umepasuliwa katikati kutoka kwenye mifupa, na kana kwamba mifupa yake ilikuwa ikipasuliwa kipande hadi kipande. Mateso haya ya kuumiza yalimfanya akafikiria afadhali basi afe. …uwezo wake wa kuvumilia ulikuwa umefikia kilele. … Alitaka kulia kwa sauti, alitaka kuirarua ngozi kwenye mwili wake ili kupunguza maumivu—lakini alishikilia mayowe yake, na hakuirarua ngozi yake kutoka kwenye mwili wake, kwani hakutaka Shetani auone udhaifu wake. Na hivyo alipiga magoti chini kwa mara nyingine, lakini wakati huu hakuhisi uwepo wa Yehova Mungu. Alijua kwamba mara nyingi alikuwa mbele yake, na nyuma yake, na upande wake. Lakini kwenye maumivu haya, Mungu alikuwa hajawahi kuyatazama; Aliufunika uso wake na Akawa Amefichwa, kwa maana uumbaji wake wa binadamu haukuwa wa kumletea mateso binadamu. Wakati huu, Ayubu alikuwa akilia, na akijaribu kwa njia bora zaidi kuvumilia maumivu yake ya kimwili, lakini asingeweza kujizuia tena dhidi ya kutoa shukrani kwa Mungu: Binadamu aanguka kwa mpigo wa kwanza, yeye ni myonge na asiye na nguvu, yeye ni mchanga na asiyejua—kwa nini ukataka kumtunza na kuwa mzuri kwake yeye? Unanipiga, ilhali inakuumiza kufanya hivyo. Ni nini cha binadamu kinastahili utunzaji na kujali Kwako? Maombi ya Ayubu yalifikia masikio ya Mungu, na ya Mungu Alikuwa kimya, Akitazama tu bila kutoa sauti. … Akiwa amejaribu kila ujanja kwenye kitabu bila mafanikio, Shetani aliondoka kimyakimya, lakini haya hayakufikisha hadi tamati majaribio ya Ayubu kutoka kwa Mungu. Kwa sababu nguvu za Mungu zilizokuwa zimefichuliwa ndani ya Ayubu zilikuwa hazijajulikana kwa umma, hadithi ya Ayubu haikuishia pale ambapo Shetani alijiondoa. Huku wahusika wengine wakiingia katika tukio hilo, matukio mengine ya ajabu zaidi yalikuwa yaje.
Maonyesho Mengine ya Kumcha Mungu na Kujiepusha na Maovu kwa Ayubu ni Kutukuza Kwake kwa Jina la Mungu Katika Mambo Yote
Ayubu alikuwa ameteseka kutokana na maudhi ya Shetani, lakini bado hakuliacha jina la Yehova Mungu. Mke wake ndiye aliyekuwa wa kwanza kujiondoa na kuendeleza wajibu wa Shetani unaoweza kuonekana kwa kumshambulia Ayubu. Maandishi asilia yanafafanua hali hii hivyo basi: “Kisha mkewe akamwambia, Je, Wewe bado unashikamana na utimilifu wako? mkufuru Mungu, ufe.” (Ayubu2:9). Haya yalikuwa maneno yaliyozungumzwa na Shetani akisingizia kuwa binadamu. Yalikuwa ni shambulizi, na shtaka, pamoja na kichocheo, jaribio, na matusi. Baada ya kushindwa kushambulia mwili wa Ayubu, Shetani sasa alishambulia moja kwa moja uadilifu wa Ayubu, akitaka kutumia jambo hili kumfanya Ayubu kutupilia mbali uadilifu wake, kumwacha Mungu, na kusita kuishi. Hivyo, pia, ndivyo Shetani alivyotaka kutumia maneno kama hayo kumjaribu Ayubu: Kama Ayubu angeacha jina la Yehova, asingelazimika kuvumilia mateso kama hayo, angejiondolea mateso ya mwili. Akiwa amekabiliwa na ushauri wa mke wake, Ayubu alimkosoa kwa kusema, “Lakini yeye akamwambia, Wewe unazungumza kama mmoja wa wanawake wapumbavu wanavyozungumza. Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya?” (Ayubu 2:10). Ayubu alikuwa amejua kwa muda mrefu maneno haya, lakini wakati huu ukweli wa maarifa ya Ayubu kuhusu maneno haya ulikuwa umethibitishwa.
Wakati mke wake alimshauri kulaani Mungu na kufa, maana yake ilikuwa: Mungu wako anakushughulikia hivi, kwa hivyo kwa nini usimlaani yeye? Kama ungali hai unafanya nini? Mungu wako hakufanyii haki, na ilhali ungali unabariki jina la Yehova. Angekuleteaje janga hili huku unabariki jina Lake? Harakisha na uliache jina la Mungu, na usimfuate yeye tena. Kwa njia hii matatizo yako yataisha. Kwa wakati huu, ushuhuda ulitolewa ambao Mungu alitaka kuuona kwa Ayubu. Hakuna mtu yeyote wa kawaida ambaye angeweza kuwa na ushuhuda huu, wala hatuusomi katika mojawapo ya hadithi za Biblia—lakini Mungu Alikuwa ameuona mapema kabla hata Ayubu kuongea maneno haya. Mungu Alitaka tu kutumia fursa hii kumruhusu Ayubu kuthibitisha kwa wote kwamba Mungu alikuwa sahihi. Akiwa amekabiliwa na ushauri wa mke wake, Ayubu hakutupilia tu mbali uadilifu wake au kumuacha Mungu, bali pia alimwambia mke wake: “Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya?” Je, maneno haya yanao uzito mkuu? Hapa, kunayo ukweli mmoja tu unaoweza kuthibitisha uzito wa maneno haya. Uzito wa maneno haya ni kwamba yameidhinishwa na Mungu ndani ya moyo Wake, ndiyo yale yaliyotamaniwa na Mungu, ndiyo yale Mungu Alitaka kusikia, na ndiyo matokeo ambayo Mungu Alitamani kuona; maneno haya ndiyo pia kiini cha ushuhuda wa Ayubu. Katika haya, utimilifu, unyofu, kumcha Mungu, kujiepusha na maovu kwa Ayubu kulithibitishwa. Thamani ya Ayubu ilikuwa namna ambavyo, alipojaribiwa, na hata wakati mwili wake mzima ulikuwa umefunikwa na majipu mabaya, alipovumilia mateso ya kiwango cha juu zaidi, na wakati mke na watu wake wa ukoo walipomshauri, bado aliyatamka maneno hayo. Ili niweze kuiweka kwa njia nyingine, ndani ya moyo wake alisadiki kwamba, haijalishi ni kiasi kipi cha majaribio, au ni vipi ambavyo masaibu au mateso yalivyokuwa, hata kama kifo kingemjia, hangemuacha Mungu au kugeuka na kuacha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Unaona, basi, kwamba Mungu Alishikilia sehemu muhimu sana ndani ya moyo wake, na kwamba kulikuwa tu na Mungu moyoni mwake. Ni kwa sababu ya haya ndipo tunasoma ufafanuzi kama huo kuhusu yeye katika maandiko kama: Katika yote haya Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake. Hakutenda dhambi kwa kutumia mdomo wake tu, lakini ndani ya moyo wake hakulalamika katu kuhusu Mungu. Hakusema maneno mabaya kuhusu Mungu, wala hakutenda dhambi dhidi ya Mungu. Kinywa chake hakikubariki tu jina la Mungu, lakini ndani ya moyo wake alibariki pia jina la Mungu; mdomo na moyo wake ulikuwa kitu kimoja. Huyu ndiye aliyekuwa Ayubu wa kweli aliyeonekana na Mungu, na hii ndiyo iliyokuwa sababu ya kweli kwa nini Mungu alimthamini sana Ayubu.
Kutoelewa Kwingi Kwa Watu Kuhusu Ayubu
Ugumu aliopitia Ayubu haukuwa kazi ya malaika waliotumwa na Mungu, wala haukusababishwa na mkono wa Mungu mwenyewe. Badala yake, ulisababishwa na Shetani mwenyewe, adui wa Mungu. Hivyo basi, kiwango cha ugumu alioupitia Ayubu kilikuwa kikubwa. Ilhali kwa wakati huo Ayubu alionyesha, kwa moyo mkunjufu, maarifa yake ya kila siku kumhusu Mungu ndani ya moyo wake, kanuni za vitendo vyake vya kila siku, na mwelekeo wake kwa Mungu—na huu ndio ukweli. Kama Ayubu hangekuwa amejaribiwa, kama Mungu Asingekuwa Amemletea Ayubu majaribio, wakati Ayubu aliposema, “BWANA alinipa, na BWANA amechukua; jina la BWANA libarikiwe,” ungesema kwamba Ayubu alikuwa mnafiki; Mungu alikuwa amempa rasilimali nyingi, hivyo bila shaka alilibariki jina la Yehova. Kama, kabla ya kupitia majaribio, Ayubu angekuwa amesema, “Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya?” Ungesema kwamba Ayubu alikuwa akipiga chuku, na kwamba hangeliacha jina la Mungu kwa sababu mara nyingi alibarikiwa kwa mkono wa Mungu. Kama Mungu Angekuwa Amemletea janga, basi kwa kweli angeliacha jina la Mungu. Lakini wakati Ayubu alipojipata katika hali hizi ambazo hakuna yeyote angetaka kujipata ndani au kutaka kuona, au kutaka zimpate, ambazo watu wangeogopa kupata, hali ambazo hata Mungu mwenyewe Hakuweza kuvumilia kuzitazama, bado Ayubu aliweza kushikilia uadilifu wake: “BWANA alinipa, na BWANA amechukua; jina la BWANA libarikiwe” na “Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya??” Kama wangekumbwa na mwenendo wa Ayubu wakati huu, wale wanaopenda kuzungumzia maneno ya kuonyesha umuhimu na kuvutia, na wale wanaopenda kuongea barua na mafundisho ya dini, wanaachwa wanyamavu. Wale wanaotukuza jina la Mungu kwa matamshi pekee, ilhali hawajawahi kukubali majaribio ya Mungu, wanashutumiwa na uadilifu ambao Ayubu alishikilia kwa dhati, na wale ambao hawajawahi kusadiki kwamba binadamu anaweza kushikilia kwa dhati njia ya Mungu wanahukumiwa na ushuhuda wa Ayubu. Wakiwa wamekabiliwa na mwenendo wa Ayubu wakati wa majaribio haya na maneno aliyoyaongea, baadhi ya watu watahisi wakiwa wamechanganyikiwa, baadhi watamwonea wivu, baadhi wahisi shaka, baadhi wataonekana hata wasio na haja ya kufuatilia mambo haya, huku wakiukataa ushuhuda wa Ayubu kwa sababu hawayaoni tu mateso yaliyompata Ayubu wakati wa majaribio, na kusoma maneno yaliyozungumzwa na Ayubu, lakini pia ule “unyonge” wa binadamu uliofichuliwa na Ayubu wakati majaribio yalipomsibu. “Unyonge” huu wanaoamini kuwa ile hali ya kudaiwa ya kutokuwa mtimilifu katika utimilifu wa Ayubu, doa katika binadamu ambaye katika macho ya Mungu alikuwa mtimilifu. Hivi ni kusema kwamba, inasadikiwa kwamba wale walio watimilifu hawana doa wala toa, hawana dosari wala hila, kwamba hawana unyonge wowote, hawana habari yoyote kuhusu maumivu, kwamba hawahisi katu wakiwa wamehuzunika au wamekataliwa, na hawana chuki au tabia yoyote ya nje isiyofaa; kutokana na haya, watu wengi hawasadiki kwamba Ayubu alikuwa kwa kweli mtimilifu. Watu hawaidhinishi mambo mengi kuhusu tabia yake wakati wa majaribio yake. Kwa mfano, wakati Ayubu alipopoteza mali yake na watoto wake, hakuweza, kama vile watu wanavyofikiria, kuanza kulia. “Utovu wake wa adabu” unawafanya watu kufikiria alikuwa jiwe, kwani hakuwa na machozi wala upendo kwa familia yake. Hii ndiyo picha mbaya ya kwanza ambayo Ayubu anawaonyesha watu. Wanafikiri tabia yake baada ya hapo kuwa ya kushangaza zaidi: “Kulirarua joho lake” ni kauli iliyotafsiriwa na watu kuonyesha utovu wake wa heshima kwa Mungu, na “kunyoa kichwa chake” kunasadikiwa visivyo kumaanisha kukufuru kwa Ayubu na upinzani wake kwa Mungu. Mbali na maneno ya Ayubu kwamba “BWANA alinipa, na BWANA amechukua; jina la BWANA libarikiwe,” watu hawatambui uhaki wowote ndani ya Ayubu uliosifiwa na Mungu, na hivyo ukadiriaji kuhusu Ayubu kwa wengi wao si chochote zaidi ya kutofahamu, kutoelewa, shaka, lawama, na idhinisho kwa nadharia tu. Hakuna kati yao anayeweza kuelewa na kushukuru kwa kweli maneno ya Yehova Mungu kwamba Ayubu alikuwa binadamu mtimilifu na mnyofu, yule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu.
Kutokana na picha yao kuhusu Ayubu hapo juu, watu wana shaka zaidi kuhusiana na uhaki wake, kwani vitendo na mwenendo wa Ayubu uliorekodiwa kwenye maandiko haukuwa wenye mguso wa kina kama vile watu wangefikiria. Hakutekeleza tendo lolote kubwa tu, lakini pia alikichukua kigae ili ajikwaruze akiwa ameketi kwenye jivu. Kitendo hiki kinawashangaza pia watu na kuwafanya kutilia shaka—na hata kukataa—uhaki wa Ayubu, kwani wakati akijikwaruza Ayubu hakumwomba Mungu, au kutoa ahadi kwa Mungu; wala, zaidi ya hayo, hakuonekana akilia machozi ya maumivu. Wakati huu, watu wanauona tu unyonge wa Ayubu na wala sio chochote kingine, na hivyo hata wanapomsikia Ayubu akisema “Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? hawaguswi kamwe, au vinginevyo hawaonekani kuamua chochote, na bado hawawezi kutambua uhaki wa Ayubu kutoka kwa maneno haya. Picha ya kimsingi ambayo Ayubu anapatia watu wakati wa mateso ya majaribio yake ni kwamba alikuwa si mnyenyekevu wala mwenye kiburi. Watu hawaioni hadithi inayotokana na tabia yake iliyojitokeza katika kina cha moyo wake, wala hawaioni ile hali yake ya kumcha Mungu ndani ya moyo wake au kutii kwa kanuni ya njia ya kujiepusha na maovu. Utulivu wake unawafanya watu kufikiria kuwa utimilifu na unyofu wake vyote vilikuwa ni maneno matupu tu, kwamba kumcha kwake Mungu kulikuwa tu uvumi; ule “unyonge” alioufichua kwa nje, wakati huo, unawaachia picha ya kina, ukiwapatia “mtazamo mpya” kuhusu, na hata “uelewa mpya” kuhusu binadamu yule ambaye Mungu anafafanua kuwa mtimilifu na mnyofu. “Mtazamo mpya” na “uelewa mpya” kama huo vyote vinathibitishwa wakati Ayubu alipokifungua kichwa chake na kulaani siku aliyozaliwa.
Ingawaje kiwango cha mateso aliyoyapitia hakifikiriki wala kufahamika kwa binadamu yeyote, hakuzungumza maneno yoyote ya uvumi, lakini alipunguza tu maumivu ya mwili wake kwa njia zake mwenyewe. Kama ilivyorekodiwa kwenye maandiko, alisema: “Itokomee mbali ile siku niliyozaliwa, na ule usiku uliosema, Mtoto mume ameingia katika mimba.” (Ayubu3:3). Pengine, hakuna yeyote aliyewahi kutilia maanani maneno haya na kuona kwamba ni muhimu, na pengine kunao watu ambao wameyatilia maanani. Kwa maoni yako, yanamaanisha kwamba Ayubu alimpinga Mungu? Je, ni malalamiko dhidi ya Mungu? Najua kwamba wengi wenu mnayo mawazo fulani kuhusu maneno haya yaliyozungumzwa na Ayubu na mnasadiki kwamba kama Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu, hakufaa kuonyesha unyonge wowote au huzuni yoyote, na badala yake alifaa kukabiliana vilivyo na shambulizi lolote kutoka kwa Shetani kwa njia nzuri, na hata kutabasamu wakati alikumbwa na majaribio ya Shetani. Hakufaa kuwa na mwitikio hata mdogo kuhusiana na mateso aliyoyapata kwenye mwili wake kutokana na Shetani, wala hakufaa kuonyesha hisia zozote ndani ya moyo wake. Alifaa hata kuuliza kwamba Mungu Ayafanye majaribio haya kuwa mabaya zaidi. Haya ndiyo yanayofaa kuonyeshwa na kumilikiwa na mtu ambaye hatikisiki na ambaye anamcha Mungu kwa kweli na kujiepusha na maovu. Katikati ya mateso haya makuu, Ayubu hakufanya chochote ila kulaani siku aliyozaliwa. Hakulalamika kuhusu Mungu, hakuwa na nia yoyote ya kumpinga Mungu. Hali hii ni rahisi zaidi ikisemwa kuliko kutendwa, kwani tangu enzi za zamani hadi wa leo, hakuna yeyote ambaye amewahi kupitia majaribio kama hayo au kuteseka kama vile Ayubu alivyoteseka. Na kwa nini hakuna yeyote ambaye amepitia aina hiyo ya majaribio ya Ayubu? Kwa sababu, kama vile Mungu Anavyoona, hakuna yeyote anayeweza kuvumilia wajibu au agizo kama hilo, hakuna anayeweza kufanya kama Ayubu alivyofanya, na, zaidi, hakuna yule ambaye bado, mbali na kuilaani siku ya kuzaliwa kwake, anaweza kutoliacha jina la Mungu na kuendelea kubariki jina la Yehova Mungu, kama vile Ayubu alivyofanya wakati mateso kama hayo yalimpata. Je, mtu yeyote angeweza kufanya hivi? Tunaposema haya kumhusu Ayubu, tunapongeza tabia yake? Alikuwa binadamu mwenye haki, na aliyeweza kuwa na ushuhuda kama huo kwa Mungu, aliyeweza kumfanya Shetani kutoroka kwa haraka sana, ili asiwahi kuja mbele ya Mungu tena na kumshtaki yeye—kwa hivyo nini mbaya na kumpongeza? Inaweza kuwa kwamba kunavyo viwango vya juu zaidi kuliko Mungu? Inaweza kuwa kwamba ungechukua hatua hata bora zaidi kuliko Ayubu wakati majaribio yatakapokusibu? Ayubu alisifiwa na Mungu—ni upinzani upi unaoweza kuwa nao?
Ayubu Anailaani Siku Ya Kuzaliwa Kwake Kwa Sababu Hataki Mungu Kupata Maumivu Kwa Sababu Yake Yeye
Mara nyingi mimi husema kwamba Mungu huangalia ndani ya mioyo ya watu, na watu huangalia namna watu walivyo kwa nje. Kwa sababu Mungu anaangalia ndani ya mioyo ya watu, Anaelewa kiini chao, huku nao watu wanafafanua kiini cha watu wengine kutokana na wanavyoonekana kwa nje. Wakati Ayubu alipoufunua mdomo wake na kulaani siku ya kuzaliwa kwake, kitendo hiki kilishangaza wahusika wote wa kiroho, wakiwemo wale marafiki watatu wa Ayubu. Binadamu alitoka kwa Mungu, na anafaa kuwa mwenye shukrani kwa maisha na mwili, pamoja na siku yake ya kuzaliwa, aliopewa na Mwenyezi Mungu, na wala hafai kuilaani. Hali hii inaeleweka na kufahamika na watu wengi. Kwa yeyote yule anayemfuata Mungu, uelewa huu ni takatifu na wenye dhabiti, ni ukweli usioweza kubadilika. Ayubu, kwa mkono mwingine, alizivunja sheria: Aliilaani siku ya kuzaliwa kwake. Hiki ni kitendo ambacho watu wengi huchukulia kuwa ni kuvuka hadi kwenye eneo haramu. Yeye hastahili tu uelewa na huruma ya watu, lakini pia hastahili msamaha wa Mungu. Wakati huohuo, hata watu wengi zaidi wanatilia shaka uhaki wa Ayubu, kwani inaonekana kana kwamba kibali cha Mungu kwake yeye kilimfanya Ayubu kujifikiria yeye mwenyewe, kilimfanya kuwa jasiri sana na asiyejali kiasi cha kwamba hakuweza tu kutoshukuru Mungu kwa kumbariki yeye na kumtunza yeye wakati wa maisha yake, lakini pia aliilaani siku ya kuzaliwa kwake na kuomba ingeangamizwa. Hii ni nini, kama si kumpinga Mungu? Mambo ya juujuu kama hayo yanawapa watu ithibati ya kushutumu kitendo hiki cha Ayubu, lakini ni nani anayejua kile Ayubu alichokuwa akifikiria kwa kweli wakati huo? Na ni nani anayeweza kujua sababu ya Ayubu kufanya hivyo? Mungu pekee na Ayubu mwenyewe ndio wanaojua hadithi ya ndani na sababu husika hapa.
Wakati Shetani alipounyosha mbele mkono wake ili kudhuru mifupa ya Ayubu, Ayubu aliangukia mashiko yake, bila ya mbinu za kutoroka au nguvu za kumpinga. Mwili na nafsi yake iliteseka na kupata maumivu makali, na maumivu haya yalimfanya kufahamu kwa kina kuhusu kutokuwa na umuhimu, unyonge, na hali ya kutokuwa na mamlaka iliyokuwemo ndani ya mwili. Wakati huohuo, alipata uelewa mkubwa wa kwa nini Mungu Anatilia maanani kujali na kumtunza mwanadamu. Akiwa ameangukia mashiko ya shetani, Ayubu alitambua kwamba binadamu, aliye katika mwili na damu, kwa hakika hana nguvu kamwe. Wakati aliposujudu na kumwomba Mungu, alihisi ni kana kwamba Mungu Alikuwa akiufunika uso Wake, na kujificha, kwani Mungu Alikuwa Amemweka kabisa katika mikono ya Shetani. Wakati huohuo, Mungu Alimlilia yeye, na, zaidi, Alimsikitikia yeye; Mungu Aliumizwa na maumivu yake na Aliumia kwa maumivu yake. … Ayubu alihisi maumivu ya Mungu, pamoja na namna ambavyo haikuweza kuvumilika kwa Mungu. … Ayubu hakutaka kuleta huzuni wowote zaidi kwa Mungu, wala hakutaka Mungu kulia kwa ajili yake yeye, isitoshe hakutaka kumwona Mungu akiwa katika maumivu kwa sababu yake yeye. Wakati huu, Ayubu alitaka tu kujiondoa mwenyewe kwenye mwili wake, kuacha kuvumilia tena maumivu yaliyoletewa kwake kupitia kwa mwili wake, kwani kufanya hivi kungekomesha Mungu kuteseka kwa maumivu yake—lakini hakuweza kufanya hivyo, na alifaa kuvumilia tu maumivu ya mwili, na pia mateso ya kutotaka kumfanya Mungu kuwa na wasiwasi. Maumivu haya mawili—moja kutoka kwa mwili, na mengine kutoka kwa roho—yalileta maumivu makali ya moyoni, yakusokotesha tumbo kwake Ayubu, na kumfanya yeye kuhisi namna ambavyo mipaka ya binadamu aliye na mwili na damu inavyoweza kumfanya mtu kuhisi akiwa amedhalilishwa na asiye na njia ya kusaidika. Katika hali hizi, tamanio lake la Mungu lilizidi kukua, na chuki yake kwa Shetani ikazidi kuwa nyingi. Wakati huu, Ayubu angependelea kutowahi kuzaliwa kwenye ulimwengu huu wa binadamu, afadhali asingekuwepo badala ya kumuona Mungu Akilia au Akihisi maumivu kwa sababu yake. Alianza kuchukia kwa kina mwili wake, kuwa mgonjwa na mchovu ndani yake mwenyewe, siku yake ya kuzaliwa, na hata ya hayo yote ambayo yalikuwa yameunganishwa kwake. Hakutaka kuwepo na kutajwa kokote zaidi kuhusu siku yake ya kuzaliwa au chochote kilichohusu siku hiyo, na hivyo aliufunua mdomo wake na kuilaani siku yake ya kuzaliwa: “Itokomee mbali ile siku niliyozaliwa, na ule usiku uliosema, Mtoto mume ameingia katika mimba. Siku hiyo na iwe giza; acha Mungu asiiangalie kutoka juu, wala mwanga usiiangazie.” (Ayubu3:3-4). Maneno ya Ayubu yanaonyesha kuchukia kwake kwa nafsi yake mwenyewe, “Itokomee mbali ile siku niliyozaliwa, na ule usiku uliosema, Mtoto mume ameingia katika mimba,” pamoja na yeye kujilaumu mwenyewe na kuwa katika hali ya kuhisi kwamba yuko katika hatia kwa kumsababishia Mungu maumivu, “Siku hiyo na iwe giza; acha Mungu asiiangalie kutoka juu, wala mwanga usiiangazie.” Vifungu hivi viwili ni maonyesho ya namna Ayubu alivyohisi wakati huo, na vinaonyesha kikamilifu utimilifu wake na unyofu wake kwa wote. Wakati huohuo, kama vile tu Ayubu alivyokuwa ametaka, imani na utiifu wake kwa Mungu, pamoja na kumcha Mungu kwake, vyote viliinuliwa. Bila shaka, kuinuliwa huku kwa hakika ni athari ambayo Mungu Alikuwa Ametarajia.
Ayubu Amshinda Shetani na Kuwa Binadamu Wa Kweli Machoni mwa Mungu
Wakati Ayubu alipopitia majaribio yake kwa mara ya kwanza, alinyang’anywa mali yake yote na watoto wake wote, lakini hakujisujudia na kusema chochote ambacho kilikuwa dhambi dhidi ya Mungu kutokana na hayo. Alikuwa ameshinda majaribio ya Shetani, na alikuwa ameshinda rasilimali zake zote za dunia na watoto wake, na majaribio ya kupoteza mali yake ya dunia, hivi ni kusema kwamba aliweza kutii Mungu kuchukua na kutwaa kutoka kwake na akatoa shukrani na sifa kwa Mungu kwa sababu ya hayo. Hivyo ndivyo ulivyokuwa mwenendo wa Ayubu wakati wa jaribio la kwanza la Shetani, na huo ndio uliokuwa ushuhuda wa Ayubu wakati wa jaribio la kwanza la Mungu. Kwenye jaribio la pili, Shetani aliunyosha mbele mkono wake ili kumdhuru Ayubu, na ingawaje Ayubu alipitia maumivu yaliyokuwa makubwa zaidi kuliko yale aliyokuwa amepitia awali, bado ushuhuda wake ulikuwa wa kutosha wa kuacha watu wakiwa wameshangazwa. Alitumia ujasiri wake, imani yake, na utiifu kwa Mungu, pamoja na kumcha Mungu kwake, kwa mara nyingine tena kumshinda Shetani, na mwenendo wake na ushuhuda wake viliweza kwa mara nyingine tena kuidhinishwa na kupata kibali cha Mungu. Wakati wa majaribio haya, Ayubu alitumia mwenendo wake halisi kumtangazia Shetani kwamba maumivu ya mwili wake yasingebadilisha imani yake na utiifu wake kwa Mungu au kuchukua ule upendo wake kwa Mungu na kumcha Mungu; asingemuacha Mungu au kutupilia mbali utimilifu wake binafsi na unyofu kwa sababu alikuwa amekabiliwa na kifo. Bidii ya Ayubu ilimfanya Shetani mwoga, imani yake ilimuacha Shetani akiwa na dukuduku na kutetemeka, nguvu za vita vya maisha yake na kifo chake na Shetani viliweza kuzua chuki na dharau nyingi kwa Shetani, utimilifu na unyofu wake ulimuacha Shetani akiwa hana chochote zaidi cha kumfanya kiasi cha kwamba Shetani aliyaacha mashambulizi yake kwake na kukata tamaa na mashtaka yake dhidi ya Ayubu mbele ya Yehova Mungu. Hii ilimaanisha kwamba Ayubu alikuwa ameushinda ulimwengu, alikuwa ameushinda mwili wake, alikuwa amemshinda Shetani, na alikuwa ameshinda kifo; alikuwa kwa kweli na hakika binadamu aliyemilikiwa na Mungu. Wakati wa majaribio haya mawili, Ayubu alisimama imara katika ushuhuda wake, na kwa hakika aliishi kwa kudhihirisha utimilifu wake na unyofu, na akapanua upana wa kanuni zake za kuishi za kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Baada ya kupitia majaribio haya mawili, ndani ya Ayubu kulizaliwa uzoefu mwingi, na uzoefu huu ulimfanya yeye kuwa mwenye kimo na uzoefu zaidi, ilimfanya kuwa mwenye nguvu zaidi, na imani kubwa zaidi, na ilimfanya yeye kuwa na ujasiri zaidi kuhusu haki na ustahili wa uadilifu ambao yeye alishikilia kwa dhati. Majaribio ya Yehova Mungu kwa Ayubu yalimpa uelewa wa kina na hisia za wasiwasi wa Mungu kwa binadamu, na kumruhusu yeye kuhisi thamani ya upendo wa Mungu, ambapo vyote vinaelekezwa katika utiliaji maanani kwa na kuhusu upendo wa Mungu na vyote viliweza kuongezwa katika kumcha Mungu. Majaribio ya Yehova Mungu kumwondoa tu Ayubu kutoka Kwake, lakini pia yaliuleta moyo wake karibu na Mungu. Wakati maumivu yale ya mwili yaliyovumiliwa na Ayubu yalifikia kilele, wasiwasi aliouhisi kutoka kwa Yehova Mungu haukumpa chaguo lolote ila kuilaani siku yake ya kuzaliwa. Mwenendo kama huo haukuwa umepangiliwa mapema lakini ulikuwa ni ufunuo wa kiasili wa kutilia maanani na kumpenda Mungu kutoka ndani ya moyo wake, ulikuwa ni ufunuo wa kiasili uliotoka kwenye kutilia maanani na kumpenda Mungu kwake. Hivi ni kusema, kwa sababu alijichukia, na hakuwa na radhi na hakuweza kuvumilia kuona Mungu Akiteswa, hivyo kutilia maanani na upendo wake vilifika hali ya kutojijali. Wakati huu, Ayubu aliimarisha kuabudu kwake kwa muda mrefu na kutamani kwake kwa Mungu na upendo kwa Mungu hadi katika kiwango cha utiliaji maanani na upendo. Wakati huohuo, aliweza kupandisha imani na utiifu wake kwa Mungu na kumcha Mungu kwake hadi katika kiwango cha kutilia maanani na upendo. Hakujiruhusu kufanya chochote ambacho kingesababisha madhara kwa Mungu, hakujiruhusu mwenendo ambao ungemuumiza Mungu, na hakujiruhusu kuleta masikitiko, huzuni au hata kutokuwa na furaha kokote kwake Mungu kwa sababu zake mwenyewe.. Katika Macho ya Mungu, ingawaje Ayubu alikuwa bado Ayubu wa hapo awali, imani, utiifu na kumcha Mungu kwake kulikuwa kumemletea Mungu utoshelezi kamilifu. Wakati huu, Mungu alitarajia Ayubu kuweza kutimiza, alikuwa amegeuka kuwa mtu aliyestahili kuitwa “mtimilifu na mnyofu” mbele ya macho ya Mungu. Vitendo vyake vya haki vilimruhusu yeye kumshinda Shetani na kuwa makini katika ushuhuda wake kwa Mungu. Hivyo, pia, matendo yake ya haki yalimfanya kuwa mtimilifu, na kuruhusu thamani ya maisha yake kuimarishwa, kuzidishwa zaidi kuliko awali, na kumfanya yeye kuwa mtu wa kwanza kutoweza kushambuliwa au kujaribiwa zaidi na Shetani. Kwa sababu Ayubu alikuwa mwenye haki, alishtakiwa na kujaribiwa na Shetani; kwa sababu Ayubu alikuwa mwenye haki, alikabidhiwa Shetani; na kwa sababu Ayubu alikuwa mwenye haki, alishinda na kumlemea Shetani, na kuweza kusimama imara katika ushuhuda wake. Kuendelea mbele, Ayubu akawa binadamu wa kwanza ambaye hangewahi tena kukabidhiwa Shetani, kwa kweli alikuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na akaishi kwenye nuru, katika baraka za Mungu bila ya kupelelezwa au kuangamizwa na shetani. … Alikuwa amekuwa binadamu wa kweli katika macho ya Mungu, alikuwa ameachiliwa huru. …
Juni 13, 2014
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi: Kuhusu Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni