Kanisa la Mwenyezi Mungu Tamko La Ishirini Na Nane |
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko La Ishirini Na Nane
Mwenyezi Mungu alisema: Nilipokuja kutoka Zayuni, vitu vyote vilikuwa vimenisubiri, na Niliporudi Zayuni, Nilisalimiwa na wanadamu wote. Nilipokuja na kwenda, hatua Zangu hazikuwahi zuiliwa na vitu vilivyokuwa na uadui Kwangu, na kwa hivyo kazi Yangu iliendelea kwa utaratibu. Leo, Ninapokuja miongoni mwa viumbe vyote, vitu vyote vinanisalimu kwa kimya, kwa uoga mkuu kuwa Nitaondoka tena na Niondoe usaidizi kwao. Vitu vyote vinafuata uongozi Wangu, na vyote vinaangalia upande ulioashiriwa na mkono Wangu.
Maneno ya kinywa Changu yamefanya kamili viumbe vingi na kuwaadibu wana wengi wa uasi Kwa hivyo, wanadamu wote wanaangalia maneno Yangu kwa makini, na kusikiza kwa karibu maneno ya kinywa Changu, na wanaogopa sana kupitwa na fursa hii nzuri. Ni kwa sababu hii ndio kwamba Nimeendelea kuzungumza, ili kazi Yangu iendelezwe kwa haraka, na ili hali ya kufurahisha ije duniani mapema na kuponya maeneo ya ukiwa duniani. Ninapoangalia mawinguni ndipo mara tena Namrejelea mwanadamu; nchi zote zinajaa uhai mara moja, hamna vumbi tena hewani, na wala matope hayafuniki ardhi nzima tena. Macho Yangu yaangaza mbele mara moja, na kuwafanya watu wa nchi zote Kunitazama na kutafuta usalama Kwangu. Miongoni mwa watu wa dunia ya sasa—wakiwemo wote walioko katika nyumba Yangu—Ni nani wanaotafuta kwa kweli hifadhi Kwangu? Ni nani wanaotoa mioyo yao kwa ajili ya gharama ambayo Nimelipa? Ni nani amewahi kuishi katika nyumba Yangu? Ni nani amewahi kujitolea kwa kweli mbele Zangu? Ninapotoa mahitaji Yangu kwa mwanadamu, anafunga “kijighala” chake mara moja. Ninapompatia mwanadamu, mara moja yeye hufungua mdomo wake kuchukua mali Yangu kichinichini, na katika moyo wake, mara nyingi hutetemeka, akiwa na uoga mwingi kuwa Nitalipiza kisasi. Kwa hivyo kinywa cha mwanadamu ni nusu wazi na nusu kimefungwa na hana uwezo wa kuufurahia kwa kweli utajiri Niliompa. Huwa Simlaani mwanadamu kwa urahisi, lakini kila mara hunishika mkono na kuniomba Nirudishe huruma juu yake; na ni wakati tu mwanadamu anaponisihi ndipo Ninapotoa “huruma” juu yake, na Ninampa maneno makali ya kinywa Changu, kiasi kwamba anashikwa na aibu mara moja, na kwa kuwa hana uwezo wa kupata “huruma” Yangu moja kwa moja, badala yake anawafanya wengine wampishie huruma hiyo. Wakati ameelewa maneno Yangu yote kwa undani, kimo cha mwanadamu kiko sawa na matakwa Yangu, na maombi yake yanazaa matunda, na sio bure au batili; Ninabariki maombi ya mwanadamu yaliyo ya kweli, na sio kujifanya.
Nimekuwa Nikifanya matendo na kuzungumza kwa miaka, ila mwanadamu hajawahi sikia maneno Ninayoyazungumza leo, na hajawahi onja adhama Yangu na hukumu Yangu. Hata ingawa watu wa dunia za kale wamesikia kumbukumbu za ukuu Wangu, hakuna ambaye amegundua kwa kweli upana wa mali Yangu. Ingawa watu wa sasa wanasikia maneno kutoka kwa kinywa Changu, wamebaki wapumbavu kuhusu siri zilizoko kinywani Mwangu, na hivyo wanauchukulia mdomo Wangu kama utoaji wa mambo mema ya namna maalum. Watu wote wanatamani kupata kitu kutoka kwenye kinywa Changu. Kama ni siri za taifa, au siri za mbinguni, au mienendo ya ulimwengu wa kiroho, au hatima ya mwanadamu, watu wote wanatamani kupata vitu kama hivyo. Hivyo, kama Ningewakusanya watu pamoja na kuwasimulia “hadithi”, wangeamka mara moja kutoka “vitanda walimolazwa” na kusikiza njia Yangu. Vitu vingi vinakosekana ndani ya mwanadamu: Hahitaju tu “nyongeza ya lishe” bali “usaidizi wa kimawazo” na “usambazaji wa lishe ya kiroho”. Hii ndiyo inayokosekana kwa watu wote: huu ndio “ugonjwa” wa kila mwanadamu. Ninatoa uponyaji kwa ugonjwa wa mwanadamu ili matokeo bora yatimizwe, ili watu wote wawe na afya nzuri, na ili, kupitia uponyaji Wangu warejelee hali ya kawaida. Je, mnalichukia kwa kweli lile joka kuu jekundu? Mnalichukia kwa kweli? Mbona Nimewauliza mara nyingi? Mbona Nimewauliza swali hili, mara tena na tena? Kuna picha gani ya joka kuu jekundu katika mioyo yenu? Picha hiyo kwa kweli imeondolewa? Hammchukulii kwa kweli kama baba yenu? Watu wote wanafaa kuona nia Yangu katika maswali Yangu. Sio kuwafanya watu wawe na hasira, au kuchochea uasi kati ya mwanadamu, au ili mwanadamu agundue njia yake mwenyewe, bali ni kuwawezesha watu wote wajifungue kutoka kwa minyororo ya lile joka kuu jekundu. Ila mtu yeyote asiwe na wasiwasi. Yote yatakamilika na maneno Yangu; hakuna mwanadamu atakayekula, na hakuna mwanadamu anayeweza kufanya kazi ambayo Nitaifanya. Nitaifanya hewa ya nchi yote iwe safi na Nitatoa madoadoa yote ya mapepo duniani. Tayari Nimeanza, na Nitaanza hatua ya kwanza ya kazi Yangu ya kuadibu katika makazi ya joka kuu jekundu. Hivyo inaweza kuonekana kuwa kuadibu Kwangu kumeifikia dunia nzima, na lile joka kuu jekundu na mapepo yote machafu yatashindwa kuepuka kuadibu Kwangu, kwa kuwa Ninaziangalia nchi zote. Kazi Yangu duniani itakapokamilika, hapo ndipo, kipindi cha hukumu Yangu kitakamilika, Nitamuadibu kirasmi lile joka kuu jekundu. Watu Wangu wataona kuadibu Kwangu kwa haki kwa lile joka kuu jekundu, watamwaga sifa mbele kwa sababu ya haki Yangu, na milele watalisifu jina Langu takatifu kwa sababu ya haki Yangu. Hivyo basi, mtatenda wajibu wenu kirasmi, na mtanisifu kirasmi kotekote katika nchi, milele na milele!
Kipindi cha hukumu kitakapofika kilele, Sitaharakisha kumaliza kazi Yangu, bali Nitajumuisha ndani ushahidi wa enzi ya kuadibu na kuruhusu ushahidi huo kuonekana na watu Wangu wote; na katika haya kutazaliwa matunda mengi zaidi. Ushahidi huu ndio njia ambayo kwayo Naliadibu lile joka kuu jekundu, na Nitafanya watu Wangu kuliona kwa macho yao ili wajue zaidi kuhusu tabia Yangu. Wakati watu Wangu wananifurahia ni wakati joka kuu jekundu linaadibiwa. Kuwafanya watu wa joka kubwa jekundu kusimama na kuliasi joka ndiyo nia Yangu, na ndiyo njia ambayo Ninawakamilisha watu Wangu, na ni nafasi nzuri ya watu Wangu wote kukua maishani. Mwezi unaong’aa unapochomoza, usiku mtulivu unaangamizwa mara moja. Ingawa mwezi umepasuka, mwanadamu yumo katika hali ya uchangamfu, na anakaa kwa utulivu chini ya mwangaza wa mwezi, akifurahia eneo la kupendeza chini ya mwangaza. Mwanadamu hawezi elezea hisia zake; ni kama ana matamanio ya kuelekeza mawazo yake kwa wakati wa kale, ni kama anataka kuangalia mbele kwa mambo ya baadaye, ni kama anafurahia yanayojiri. Tabasamu linaonekana usoni mwake, na katika hali ya hewa ya kupendeza kunatokea harufu kavu; wakati upepo mwanana kinapopuliza, mwanadamu anagundua harufu hiyo nzuri na anaonekana kuleweshwa nayo, akishindwa kujisimamisha. Huu ndio wakati haswa ambapo Mimi Mwenyewe Nimekuja miongoni mwa mwanadamu, na mwanadamu anahisi kwa hali ya juu harufu yenye uzuri tele, na kwa hivyo wanadamu wote wanaishi kati ya harufu hii. Niko na amani na mwanadamu, na mwanadamu anaishi kwa amani Nami, na hana uasi tena katika jinsi anavyonichukulia, Sipogoi tena upungufu wa mwanadamu, hakuna tena huzuni katika uso wa mwanadamu. Kifo hakitishii tena wanadamu wote. Leo, Naenda pamoja na mwanadamu katika enzi ya kuadibu, kuenda mbele pamoja na yeye upande kwa upande. Nafanya kazi Yangu, ambayo ni kusema, Naipiga fimbo Yangu chini miongoni mwa mwanadamu na inaanguka juu ya kile kilicho na uasi ndani ya mwanadamu. Katika macho ya mwanadamu, fimbo Yangu huonekana kuwa na nguvu spesheli: inaangukia wale wote ambao ni maadui Wangu na haiwasamehei kwa urahisi: miongoni mwa wale wote wanaonipinga, fimbo hiyo inafanya kazi yake ya kiasili; wale wote walioko mikononi Mwangu wanafanya wajibu wao kulingana na nia Yangu ya asili, na wala hawajawahi enda kinyume na matakwa Yangu au kubadilisha nia yao. Kutokana na hayo, maji yatanguruma, milima itaanguka, mito mikuu itatawanyika, mwanadamu atabadilika, jua litakua na mwangaza mdogo, mwezi utakuwa na giza zaidi, mwanadamu hatakuwa tena na siku za kuishi kwa amani, hakutakuwa tena na wakati wa amani katika nchi, mbingu haitawahi tena kuwa shwari, na kimya na haitawahi tena kuendelea. Vitu vyote vitafanywa vipya na kurudia hali vilivyoonekana mwanzoni. Nyumba zote duniani zitasambaratishwa, na mataifa yote duniani yatagawanywa; siku za marudiano kati ya mke na mume zitapita, mama na mwanawe hawatakutana tena, hakutakuwa tena na kuja pamoja kwa baba na bintiye. Nitayaharibu yote yaliyokuwa duniani. Siwapi watu fursa ya kutoa hisia zao, kwani Mimi sina hisia, na Nimekua katika kuchukia hisia za watu kwa kiasi. Ni kwa sababu ya hisia baina ya watu ndiposa Nimewekwa kando, na hivyo Nimekuwa “mwingine” machoni mwao; ni kwa sababu ya hisia kati ya binadamu ndiposa Nimesahaulika; ni kwa sababu ya hisia za mwanadamu ndipo anapochukua fursa ya kuchukua “dhamira” yake; ni kwa sababu ya hisia za mwanadamu ndiposa kila mara amekuwa mwoga wa kuadibu Kwangu; ni kwa sababu ya hisia za mwanadamu ndiposa ananiita mkosa haki na mdhulumu, na kusema kuwa Sisikizi hisia za mwanadamu Ninapofanya mambo Yangu. Je Nina mrithi duniani? Ni nani kamwe, kama Mimi, amewahi kufanya kazi usiku na mchana, bila kufikiria chakula au usingizi, kwa ajili ya mipangilio yangu yote ya usimamizi? Mwanadamu anawezaje kulinganishwa na Mungu? Anawezaje kuwa sambamba na Mungu? Inawezekanaje, Mungu, anayeumba, Awe sawa na mwanadamu, anayeumbwa? Ninawezaje kuishi na kufanya mambo pamoja na mwanadamu duniani? Nani anahofia moyo Wangu? Ni maombi ya mwanadamu? Wakati mmoja Nilikubali kujumuika na mwanadamu na kutembea pamoja na yeye—na ndio, hadi sasa mwanadamu anaishi chini ya ulinzi Wangu, lakini ni siku gani mwanadamu atajitenga kutoka kwa ulinzi Wangu? Hata ingawa mwanadamu hajawahi jali kuhusu moyo Wangu, nani anaweza kuendelea kuishi katika nchi isiyo na mwangaza? Ni kwa sababu tu ya baraka Zangu ndiposa mwanadamu ameishi mpaka leo.
Aprili 4, 1992
kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili
Kujua zaidi: Kuhusu Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni