Watu wengi hawawezi kuainisha ni watu gani wana ukweli, watu gani hawana ukweli na watu gani husema mambo yaliyo na ukweli. Unapoulizwa kueleza ni nini maana ya "ukweli," huwezi kueleza kwa wazi. Lakini mara tu mtu anaposema kitu, unasema: “Mtazamo wake ni wa kweli. Maneno ayasemayo yanaonyesha ufahamu wa utendaji uliopatikana kupitia kwa uzoefu.” Unaelewa mara tu unapowasikia wakizungumza. Kwa ninyi hapa mlio wapya, Nikiwauliza ni nini maana ya 'uhalisi,' hamtaweza tu kunijibu, lakini pia hamtaweza kueleza tofauti kati ya mtu anayezungumza uhalisi na mtu anayezungumza mafundisho ya dini.
Hili halisemwi kuwadunisha ninyi, ni tu kwamba hamna uzoefu. Tazama wale wakongwe wa kanisa; ingawa washawishi wengine wa kufanya mengi huenda wakawakanganya na vitu wasivyoweza haswa kutambua sababu sahihi, bado wanajua kwamba wanachosema watu hao si sahihi. Wanaweza kutambua ni watu gani wanazungumza mafundisho ya dini, na watu gani wanazungumza uhalisi. Ninyi, kwa hali yoyote, hata bado hamjababia. Hili halisemwi kuwashushia hadhi, kwa hivyo msione vibaya kwa sababu ya hili. Hii ni njia ya kawaida ya uzoefu ambayo kila mtu ni lazima apitie. Kila mtu ni lazima apitie miaka mingi ya kunyunyiziwa maji, kufanyiwa uchunguji, kusikiliza, kuhisi, kutambua na kupitia kabla ya kufahamu polepole lakini kwa kina uzoefu wa maisha, kabla ya kuvuka lango na kufungua macho yao. Ukizungumza tu mafundisho ya dini na kusikia mafundisho ya dini, ikiwa huwezi kutambua masuala yanayohusu uhalisi na usiwe na utambuzi, basi macho yako hayajafunguliwa; bado tu hayajafunguliwa. Ni nini maana ya "macho yako hayajafunguliwa"? Inamaanisha bado hujavuka lango, na huo ni ukweli. Inamaanisha kwamba hujavuka lango panapohusiana na ukweli. Jitazameni sasa. Labda unaweza kufanya kazi ya uchungaji, kuwasaidia wengine, kutoa msaada na kutumia, au kufanya mambo mengine ya desturi katika familia ya Mungu. Lakini wewe hasa huna uhalisi, wala hutakuwa hasa na utambuzi wowote wa kufikia uhalisi au kufikia nyaraka na mafundisho ya dini. Labda hamjaridhishwa na hili, mpaka siku moja mtu fulani aje anayezungumza mafundisho ya dini, aliye na maneno ya kushawishi, na kisha huenda mtamkweza. Na wakati mtu yule aliye na uhalisi wa kweli ajapo, aliye kimya, asiyetoa sauti, basi huenda mtamdharau. Mara mnapofanya hivi, wakati huo mtajua kimo chenu wenyewe kiko wapi. Ndio, kimo cha mwanadamu, ufahamu wa mtu kuhusu uhalisi na wa mtu mwenyewe, uzoefu wa mtu kuhusu kweli, ufahamu wa mtu kuhusu Mungu—mambo haya yote hutokana na uzoefu, hutokana na kuishi siku baada ya siku, hili ni wazi na dhahiri. Vitu hivi bila shaka havitokani na kusoma wala kutoka kwa mambo mangapi uliyoyasikia. "Nina mambo haya, nimeyasikia na ninayakumbuka. Kiwango changu cha maarifa kiko juu sana, mimi ni mwanafunzi wa chuo, ninafanya kazi fulani, ninachunguza jambo fulani, na mimi huyajua mambo mara tu niyasikiapo." Unaweza kutumia maarifa uliyojifunza kusikia falsafa, siasa au fasihi. Lakini huwezi kuyatumia hapa, hayana maana! Tuna nini hapa, basi? Maarifa uliyojifunza huenda yakakusaidia kujua maneno yaliyoandikwa ya ukweli au kuhusu vile yameelezwa vizuri zaidi kuliko wengine, lakini wewe si bora kuliko wengine inapohusu wewe kuupitia ukweli; huna heri kuhusiano na hilo. Mnalikubali hili, sivyo? Hamchunguzi masuala ya uzoefu wa maisha na mnakosa mambo mengi sana. Lakini kwa ninyi ambao mna maarifa fulani, ambao sasa mko katika nafasi ya heri ya kuwa kiongozi juu ya watu wengine, ambao mko kazini mara kwa mara na ambao hukutana na wakongwe wa kanisa walio katika viwango vya juu, na ambao hufanya kazi fulani maalum, mnaweza kuendelea haraka zaidi. Mnaweza kuendelea haraka sana kuliko vile wale wakongwe wa kanisa wangeweza hapo awali, haraka na ufahamu wenu wa uhalisi, na hali yoyote ya ukweli na kwa kujifahamu wenyewe. Labda hamtatembea katika njia inayopinda au labda ninyi pia mtahitajika kupatwa na vipingamizi fulani. Hali ya kila mtu ni tofauti, hali zao ni tofauti. Watu wengine wanahitajika kupatwa na vipingamizi fulani kabla ya kuweza kupitia mabadiliko makuu. Na kisha kuna watu wengine ambao hawahitaji kupatwa na vipingamizi vikubwa, lakini hugundua njia wanayopaswa kutembea na upotovu wao wenyewe katika mambo yanayotendeka kandokando yao, na wao hupata ujuzi fulani katika watu, mambo na vitu vilivyo kandokando yao—huyu ni mtu anayeendelea upesi sana kwa kulinganisha.
Hivyo mnapaswa kuzingatia nini sasa? Ikiwa mtazingatia tu kuyafanyia kazi na kujishughulisha na mambo ya ukingoni, basi maendeleo yenu yatacheleweshwa. Mnapoamini katika Mungu, maendeleo yenu binafsi maishani ni muhimu zaidi na ni ya maana zaidi. Huenda ukajiandaa tu na mafundisho ya dini, au na uwezo wa kufanya kazi, au huenda ukafanya jambo fulani kwa kutumia mbinu fulani nzuri sana, au kwa hekima; mambo haya yote ni ya kufuata, ingawa bado huwezi kuendelea bila hayo. Suala kuu la imani yako kwa Mungu ni kwamba lazima uujue ukweli kabisa, upitie ukweli na uwe na ufahamu fulani wa ukweli, na uweze kuwa na moyo mtiifu na kutosheleza mapenzi ya Mungu mbele Yake. Iwapo unaamini katika Mungu lakini kadri unavyoamini, ndivyo uhusiano wako na Mungu unaenda mrama, ndivyo unavyosonga mbali zaidi na Mungu na ndivyo unavyokuwa na sehemu nyingi ndani yako zinazopingana na ukweli, basi hilo linathibitisha kwamba imani yako haikuongozi kuendelea, kwamba Roho Mtakatifu hajakushughulikia, na kwamba umepotea na umevuka mipaka. Iwapo unaamini kwa kipindi fulani na kisha unakuwa na ufahamu fulani wa uhalisi, kujifahamu kwa kiasi fulani, na ufikirie umeelewa mambo fulani ya uhalisi, basi hili linathibitisha kwamba unafahamu mambo ya kiroho, macho yako yamefunguka na unatembea katika njia sahihi. Kuna wakongwe wengine sasa ambao wamefuata kwa miaka miwili au mitatu, ambao hata hawajababia, ambao ni waasi na wasiozuiwa na ambao hujitayarisha kupokea baraka, ambao wanajitayarisha kufurahia utajiri wao mzuri baada ya kazi kukamilishwa. Hata bado hawajababia kulingana na uzoefu wa maisha, na hawana uhusiano wenye upatanifu na Mungu hata kidogo. Ni vyema kuwa nao kwa kipindi kifupi, na watatii shingo upande, na hawatathubutu kutoa sauti ikiwa wana dhana. Lakini baada ya muda fulani kupita, mara tu wanapoanza kupinga, wanakuwa vyombo vya kuangamia. Kila mtu yuko juu ya ardhi hatari, na hili ni jambo la kuogofya. Ikiwa unamwamini Mungu na unatembea kwenye njia sahihi, basi imani yako ni muafaka na utapata baraka. Ikiwa utaenda kombo, ukitembea kwenye njia isiyo sahihi au njia isiyonyooka, usipoendelea mbele, usipoendelea mbele kwa uwezo wako wote, basi utaangamia na utapata adhabu.
Watu wana njia mbili za imani katika Mungu: Moja ni kuweza kumwamini Mungu kabisa; na nyengine ni kumuasi Mungu na kumpinga Yeye. Hizi ndizo njia mbili pekee. Haiwezekani kwamba humpingi Mungu lakini pia humtii Yeye; hili haliwezekani. Ikiwa humtii Mungu na huna ufahamu halisi, basi unaweza tu kuwa mkaidi na muasi. Huenda usionyeshe uasi kwa mambo unayosema, na huenda usimpinge Yeye waziwazi kwa silaha zilizochukuliwa, lakini bado moyo wako ni mkaidi. Au iwapo huulizwi kufanya jambo, huenda ukahisi umejawa na upendo kwa Mungu na kuhisi uko karibu sana na Mungu. Lakini mara tu unapoulizwa kufanya jambo, basi ukaidi wako, kiburi chako, kujidai kwako na mambo yako ya Shetani hufichuliwa; mara tu yanapofichuliwa, basi ukaidi wako unakuwa wa kweli. Je, si hivyo? Huenda ukaichukulia imani yako kwa Mungu kama tu "Mimi nimebarikiwa kwa kuamini katika Mungu na baadaye nitakuwa chombo cha baraka Zake. Mimi ni mshirika wa familia ya Mungu na mimi nimeinuliwa na Mungu; mimi ni mtu aliyekwezwa na Mungu. Nimebarikiwa na Mungu ni mwema kwangu." Lakini ikiwa unliona kwa njia hii, kuna maana gani? Kuna maana gani kupiga makelele kwa maneno haya matupu yanayorudiwarudiwa? Jambo kuu sasa ni iwapo unaweza kuokolewa au la, iwapo unatembea kwa njia sahihi ya maisha au la, iwapo Mungu anakusifu katika imani yako au la, iwapo Mungu anakubali kuwa kwako mshirika wa familia ya Mungu au la, na iwapo Mungu anakukubali au la; ni hayo tu ndiyo yanaweza kuchukuliwa kama kuwa makini katika imani yako kwa Mungu. Imani ya kipumbavu, kama vile "Ah, Mungu ni mwema kwangu, Mungu hunifadhili, nimebarikiwa na mimi hufanikiwa kila mahali. Tazama, Mungu ameniinua na kunifanya kuwa kiongozi katika familia Yake. Nimekuwa na bahati sana na nyota yangu imekuwa ikiinuka tangu nilipokuja katika familia ya Mungu." Kuringia tu jambo la aina hii hakuna maana. Ni tupu; lisilo na maana! Ikiwa umepewa nafasi lakini huishikilii upesi, basi ilitolewa bure, na hakutakuwa na maana hata ukipewa nafasi nyingi kiasi gani. Shikilia upesi mambo fulani ya kweli, na halisi. Baadhi ya waumini wakongwe husema: "Ah, nimebarikiwa! Mimi nimebarikiwa na mimi ni mtu aliyebarikiwa zaidi katika dunia yote, katika ulimwengu wote!" Haingekusaidia hata ungekuwa malaika; huwezi tu kusema mambo ya aina hii, ni lazima ushikilie upesi mambo ya kweli. Hasa ninyi ambao mumeamini katika Mungu kwa muda mfupi tu na mmepata uzoefu kidogo kutokana na kufanya mambo, ambao hamkupitia zile hatua za kazi hapa mwanzo, na ambao mlikuja mwisho kabisa—je, uko tayari kuwa na uhakika kabisa ili baadaye uweze kuokolewa? Je, uko tayari? Huko tayari, sivyo? Ikiwa huko tayari kuwa na uhakika kabisa kuhusu jambo hilo, basi uko katika nafasi hatari!
Ikiwa huelewi ni nini maana ya kumhudumia Mungu au nini maana ya kutii Mungu, na unaelewa kidogo sana namna ya kumwabudu Mungu au jinsi watu wanapaswa kuamini katika Mungu; iwapo hujashikilia mambo haya na huyafahamu katika moyo wako, basi utaenda mrama kwa urahisi sana na utamuasi Mungu kwa urahisi sana. Kama wale walioanguka hapa awali waliosema: "Roho Mtakatifu na atufunulie mambo haya!" Ninyi nyote sasa mnaona jambo hili kwa dhahiri. Wakati huo hawakuwa na nia yoyote ya kufanya chochote kibaya na kumuasi Mungu, na walijua kwmba Mungu alikuwa amewainua na kwamba ni lazima wafanye kazi kwa bidii. Ilhali hawakutembea kwenye njia sahihi, wakifikiria tu kwamba Mungu alikuwa amewainua, kwamba walitaka kufanya kazi kwa bidii, na kufanya kazi nzuri ya kuwa wachungaji wa wale waliokuwa chini yao kanisani; walidhani chochote kile ambacho waliokuwa juu yao waliwataka wafanye, wangefanya. Hawakuwa wameshika mambo ya utendaji na hakika walikuwa wanafanya mambo bila kutambua, wakitegemea ushupavu wao wenyewe. Walipokuwa hawatumiwi tena, walikasirika sana na kusema: "Mungu ni mwenye haki. Roho na afichue hili! Imani yangu haiko katika mwanadamu, iko katika Mungu." Hawakupanga awali kusema maneno haya, hivyo yalisemwa bila hiari? Sababu yake ilikuwa gani? Ilikuwa ni kwa sababu mwanadamu hamchi Mungu na hamfahamu Yeye. Unaona kwamba watu wengine husema mambo mengine ambayo ni ya upumbavu na ujinga, na wao husamehewa. Wao husamehewa kwa ajili ya ujinga wao na kile ambacho wajibu wao ulikuwa hakichunguzwi. Mbona hali si hiyo kwa watu wengine? Kwa sababu walisema mambo yaliyokuwa mazito sana: "Wewe ni Mungu, lakini bado sitakutii Wewe." Watu hawa ni wapinga Kristo; wao humuasi Mungu na hawakubali ukweli. Watu wengine ni wapumbavu na wajinga. Ni sawa kuonyesha upumbavu wako na ujinga mara moja au mara mbili; lakini ukikosea amri za Mungu za usimamizi au ukikosea tabia ya Mungu, basi utakuwa matatani. Tazama njia ambayo Petro alitembea. Alipata nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu hapo mwanzo na alizungumza na Yesu, akisema: "Wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu aishiye." Mara tu Roho Mtakatifu alipokuwa amempa nuru, wakati huo alipata ujuzi fulani na moyo wake ulijazwa nuru. Hata kama wakati huo hakuwa na ufahamu wa kina, lakini alitafuta kumfahamu Mungu, na akatembea kwenye njia sahihi ya kumhudumia Mungu. Kumhudumia Mungu ni jambo la hatari zaidi, na pia ni jambo la utukufu zaidi. Kwa sababu wanadamu ni wakaidi na wapotovu, mara tu wanapopotea, wao humalizika. Watu humhudumia Mungu, sio watu wengine; kumhudumia Mungu ni jambo la hatari. Petro alitembea katika njia hiyo na alikuwa na imani hii. Na je, kuhusu Paulo? Hakukubali kwamba Yesu alikuwa Kristo. Alimuwinda bila kukoma na, baada ya kuangushwa chini, bado Paulo hakutambua kwamba Mungu alikuwa Bwana wa vitu vyote, wala vile wanadamu wanapaswa kumtii Yeye. Hakuwa na akili ya kawaida ya kufikiria, lakini kuanzia mwanzo hadi mwisho alihodhi fikira za kiburi: "Ninakupa Wewe kiasi hiki kwa hivyo unapaswa kunipa kiasi hicho; ninatumia rasilimali kiashi hiki, kwa hivyo Wewe unapaswa kunituza kiasi hicho na kunipa kiasi hicho cha mshahara." Kazi yake ilikuwa chini ya utawala wa fikira za aina hii wakati huo wote. Hivyo hakuwahi kuwa na moyo wa kumheshimu Mungu, hakuwahi kuwa na moyo wa kumcha Mungu. Angalia toni ya maneno yake: "Nimepigana vita"—Nimepigana vita Ulivyonifanya nipigane; "Nimemaliza kazi yangu"—Nimekimbia kwenye njia uliyoniambia nikimbie; "Nimeidumisha imani"—je, hukunifanya niidumishe?" Nimeidumisha, kwa hivyo taji ya utukufu haipaswi kuhifadhiwa kwa ajili yangu? Je, hakunena na toni ya aina hii? Bila shaka hangeweza kuzungumza waziwazi namna hii katika waraka. Alizungumza kitasifida na kimafumbo, lakini maneno yake yalianza kutoka kwa dhana hizi. Ni nini kilifanyika mwishowe? Yeye bado aliadhibiwa, au sivyo? Mnatakiwa kuona dhahiri vile wanadamu wanapaswa kuchagua kwenye njia ya kumhudumia Mungu, kwenye njia ya kuamini katika Mungu. Ni njia zipi za kumhudumia Mungu ni za njia za Paulo? Ni njia zipi za kuamini ni za njia ya Paulo? Ni jinsi gani njia ya kumcha Mungu ya kumhudumia Mungu kama ya Petro inaweza kutimizwa? Kuna njia ambayo viumbe wa Mungu wanapaswa kutembea ili kumwabudu Yeye; njia hiyo ni lazima ichaguliwe sawasawa na malengo yenu ni lazima yawe dhahiri. Usiwe mpumbavu, lakini tembea kwa bidii na kusimama juu ya ardhi imara, na maono yaliyo dhahiri kikamilifu. Ni hatari wewe kutembea kwenda mbele katika njia ya kipumbavu na ina hakikisha kwamba siku moja utakosea amri za usimamizi za Mungu au kuanza kunung'unika.
Je, mna hakika kuhusu asili gani au hali gani ndani ya wanadamu huwaongoza kwa urahisi sana katika uangamiaji, bila kujali ikiwa ni kiongozi au mfuasi? Je, unajua kuhusu asili ya kawaida ya wanadamu? Ukawaida wa asili ya wanadamu ni kumsaliti Mungu; kila mtu na watu wote wanaweza kumsaliti Mungu. Je, kutoamini pekee sio kumsaliti Mungu? Je, kumsaliti Mungu ni nini? Ni mambo gani yanamaanisha kumsaliti Mungu? Ni lazima ufahamu kiini cha wanadamu kimeumbwa na nini; ni lazima uelewe hili na kufahamu mzizi wa mambo hayo. Udhaifu wako wa mauti, hasira, njia mbaya, tabia mbaya au adabu mbaya—mambo haya yote ni ya juujuu. Ukiyashika tu mambo haya kwa kukaza na kiini chako kibakie kisichofumbuliwa, basi bado utatembea kwenye njia isiyonyooka na bado utamuasi Mungu. Je, sivyo? Ninyi bado kila mara tu mnababia na kukamata utondoti hafifu. Mwanadamu anaweza kumsaliti Mungu wakati wowote au mahali popote na hili ni tatizo kubwa. Labda wakati huu unaweza kumpenda Mungu kwa kiwango kikubwa, kutumia rasilimali nyingi kwa ajili ya Mungu, kuwa mwaminifu hasa; labda wakati huu unaweza kuwa wa akili hasa na kuwa na dhamiri. Lakini huenda kukaja na wakati na mahali ambapo kitu fulani kitakuongoza kumsaliti Mungu. Tuseme kwamba mtu fulani ni wa akili hasa wakati huu; Roho Mtakatifu anamshughulikia, ana uzoefu fulani wa utendaji, amebeba mzigo, yeye hutekeleza jukumu lake kwa uaminifu na ana imani thabiti sana. Basi tuseme Mungu angefanya jambo fulani la kumsikitisha, jambo alilodhani si sahihi. Dhana zingeinuka ndani yake wakati huo, mara moja angekuwa mbaya, na angepoteza shauku na kuwa ovyoovyo katika kazi yake, na angeachana na maombi, akisema, "Ni nini ambacho ninaombea? Mungu hapaswi kufanya jambo hili! Ninawezaje kuomba?" Nguvu zake zingeisha na shauku yake ya maombi ingeipotea. Hii inaitwa nini? Je, hili sio dhihirisho la usaliti? Katika wakati wowote au mahali popote, mwanadamu anaweza kumwacha Mungu, kumkana Mungu na kumshutumu Mungu—je, haya yote si usaliti? Hili ni jambo la kuogofya. Tazama, unadhani kwamba sasa huna dhana zozote na unaweza kumtii Mungu wakati mwingi, kwamba unaposhughulikiwa na kupogolewa hutamwacha Mungu. Ilhali unaweza bado kumsaliti Mungu wakati wowote au mahali popote. Ni lazima ufahamu vilivyo asili ya mwanadamu. Bila shaka, baadhi ya watu wakati mwingine watakuwa na dhamiri fulani, na hao watakuwa watu ambao asili zao ni nzuri kwa kulinganisha. Wengine watakuwa na ubinadamu wa uovu, na asili zao zitakuwa mbaya. Lakini haijalishi iwapo mtu yeyote anasema ubinadamu wako ni mzuri au mbaya, au iwapo ubora wako ni mzuri au mbaya, asili ya kawaida ni kwamba unaweza kumsaliti Mungu. Asili ya mwanadamu ni kumsaliti Mungu, hivyo watu wangeweza kumsaliti Mungu kama hawangekuwa wamepotoshwa? Bado mnafikiri sasa: "Asili za watu ambao wamepotoshwa na Shetani zitamsaliti Mungu kwa hivyo hakuna ninachoweza kufanya. Nitahitajika tu kubadilika polepole." Je, bado mnawaza kwa njia hii? Basi Niambieni, je, watu wangeweza kumsaliti Mungu ikiwa hawangekuwa wamepotoshwa? Watu wangeweza pia kumsaliti Mungu ikiwa hawangekuwa wamepotoshwa. Wanadamu walipoumbwa walipewa hiari, walikuwa wadhaifu sana, na hawakuwa na moyo ambao ungeweza kumfikia Mungu kwa kweli au uliogeuka kumwelekea Mungu kwa kweli: Mungu ni Muumba wetu na sisi ni viumbe Wake. Wanadamu hakuwa na moyo huu. Wanadamu hawakuwa na ukweli ndani yao wala chochote ambacho kingeweza kuwasaidia kumwabudu Mungu. Mungu aliwapa hiari ili kwamba wanadamu waweze kufikiria, lakini wanadamu hawakujua Mungu ni nani na hawakufahamu jinsi ya kumwabudu Mungu. Hawakuwa na kitu kama hiki ndani yao. Hata kama hungepotoshwa, bado ungeweza tu kumsaliti Mungu. Kwa nini ni hivi? Shetani hukushawishi ili umfuate yeye na kumsaliti Mungu. Wewe uliumbwa na Mungu lakini humfuati Yeye. Badala yake unamfuata Shetani. Je, wewe si msaliti basi? Wasaliti husaliti. Wewe unafahamu kwelikweli kiini hiki, au sivyo? Hivyo wanadamu wanaweza kumsaliti Mungu wakati wowote na katika mahali popote. Ni wakati tu wanadamu watakapoishi kikamilifu ndani ya ufalme wa Mungu na ndani ya nuru ya Mungu, wakati Shetani atakuwa ameangamizwa na hakuna tena ushawishi wowote, hapo tu ndipo wanadamu hawataweza tena kumsaliti Mungu. Wakati bado kuna ushawishi, wanadamu badow wanaweza kumsaliti Mungu; hivyo inasemekana kwamba wanadamu hawana thamani. Bado unafikiria: "Sasa nimepata mambo fulani. Nina mambo fulani ambayo hayamsaliti Mungu, lakini yaliyo na upatanifu na Mungu. Siwezi kufikiriwa kuwa kioo kinachong'aa, lakini angalau kama chupa ya udongo. Siwezi kufikiriwa kuwa dhahabu, lakini labda shaba nyekundu." Unajistahi mwenyewe kwa hali ya juu sana. Je, unajua mwanadamu ni kitu cha aina gani? Mwanadamu anaweza kumsaliti Mungu wakati wowote au mahali popote na hafikii hata thamani ya peni moja. Kama tu alivyosema Mungu: "Rundo la mavi ya mbwa, wakatili na mafidhuli." Watu hufikiria: "Mimi si fidhuli! Mimi si fidhuli kamwe! Kwa nini nisiweze kuelewa jambo hili? Kwa nini sijalipitia? Ikiwa sijapotoshwa, basi siwezi kumsaliti Mungu." Kuna mifano ya hili, na kuna ukweli. Ninachowaambia sasa hakikosi msingi. Mambo haya yote ni kuwaonyesha ninyi, kuwaridhisha ninyi; ni kwa njia hii pekee ndio mnaweza kufikia ufahamu wa upotovu wenu wenyewe na kutatua tatizo la usaliti. Hakutakuwa tena na usaliti wowote ndani ya wanadamu katika ufalme, wanadamu wataishi chini ya utawala wa Mungu na Shetani hatakuwa na utawala juu yao, na wanadamu wataishi huru na hawatahitaji kuwa na wasiwasi, wakidhani, "Je, naweza kumsaliti Mungu?" Hakutakuwa na haja ya kuwa na wasiwasi; haitakuwa na maana! Baadaye, inaweza kutangazwa kwamba humtakuwa na chochote ndani yenu kinachomsaliti Mungu. Lakini sasa, mambo hayajakuwa sawa, kwani kiini cha wanadamu ni kile kinachoweza kumsaliti Mungu wakati wowote na katika mahali popote. Sio kwamba utamsaliti Mungu kwa sababu ya hali fulani mbaya, au kwamba bila hali yoyote mbaya au bila mtu yeyote kukulazimisha basi hutamsaliti Mungu. Unaweza bado kumsaliti Mungu hata iwapo hakuna anayekulazimisha; hili ni tatizo la kiini potovu cha wanadamu, na ni tatizo la asili yao. Ona jinsi unavyopumua tu sasa, jinsi hujafanya chochote, hujasonga, hujafikiria chochote, na ilhali hiyo asili inayomsaliti Mungu iko ndani yako—je, hii ni sahihi? Kwa nini? Kwa sababu wanadamu wana usaliti ndani yao na Mungu hayuko ndani yao. Roho ya wanadamu na nafsi ya wanadamu havina sehemu ya Mungu ndani yao. Hivyo, unaweza kumsaliti Mungu wakati wowote au katika mahali popote. Angalia, malaika ni tofauti. Hawana tabia ya Mungu, wala hawana kiini cha Mungu. Lakini wanaweza kumtii Mungu kikamilifu kwa sababu waliumbwa na Mungu sanasana kumhudumia Yeye na wao hutumwa kila mahali; wao ni mali ya Mungu. Wanadamu, kwa hali yoyote, waliumbwa kuishi duniani na hawakuumbwa na akili ya kumwabudu Mungu. Wanadamu wana uwezo wa kumsaliti Mungu na ni vyombo vinavyoweza kutumiwa au kupiganiwa na mtu yeyote. Wao ni wa thamani duni! Kwamba wanadamu wana asili hii imefichuliwa ili watu waweze kupata ufahamu wa jambo hili na wao wenyewe. Kutokana na hali hii, watu wanaweza kuanza kubadilika, na kuanzia hapa wanaweza kutafuta njia ya utendaji. Kufahamu ni katika mambo gani unaweza kumsaliti Mungu na ni kasoro gani unahitaji kurekebisha ili usimsaliti Mungu, utafikia hatua ambapo hutamsaliti tena Mungu katika hali nyingi na utaepuka kumsaliti Yeye katika nyingi ya hali hizo. Iwapo baadaye utamsaliti Mungu au la haitakuwa juu yako. Safari yako ya maisha itafikia mwisho wake, na itafikia wakati huo ambapo kazi ya Mungu itafanyika, lakini iwapo baadaye utamsaliti Mungu au la hautakuwa wajibu wako. Kwa nini hilo lilisemwa wakati huu tu? Kabla ya wanadamu kupotoshwa na Shetani, alikuja na akawashawishi wanadamu, na hapo basi waliweza kumsaliti Mungu. Baada ya Shetani kuangamizwa, je, wanadamu wakati huo hawatamsaliti Mungu tena? Wakati huo haujafika bado. Kwa hivyo wanadamu bado wana tabia potovu ya kishetani ndani yao, na wanaweza kumsaliti Mungu wakati wowote na mahali popote. Mara tu uzoefu wako wa maisha unapofikia hatua fulani, vitu vingi ndani yako vinavyomsaliti Mungu vitatupiliwa mbali. Wewe wakati huo utakuwa na vitu vingi vizuri, utaweza kutekeleza kujizuia na utaweza kujitawala mwenyewe. Hutakuwa na uwezo wa kumsaliti Mungu tena kwa wingi wa wakati huo, na baada ya Shetani kuangamia utapitia mabadiliko kamili. Hatua hii ya kazi ni kutatua sasa usaliti wa wanadamu na kutatua ukaidi wa wanadamu. Baadaye watu hawatamsaliti Mungu kwani Shetani atakuwa ameangamizwa, na hili haliwahusu wanadamu hata kidogo. Je, unafahamu? Kufahamu asili ya wanadamu ya kusaliti kunaanzia hapa: Ni mambo gani ni ya asili inayomsaliti Mungu, ni mambo gani ni sehemu ya kuonyesha usaliti, jinsi wanadamu wanapaswa kuingia na jinsi wanapaswa kufahamu. Kiini hiki cha wanadamu bado kiko ndani yao, wao bado wanaweza kumsaliti Mungu wakati wowote au mahali popote, na bado wanaweza kufanya mambo ambayo hawafikirii kuwa ni ya kumsaliti Mungu. Wanadamu wanaweza kumsaliti Mungu wakati wowote na mahali popote, hiyo ni kusema kwamba wanadamu hawana hali ya kujitawala, kwani Shetani amewamiliki. Unaweza bado kumsaliti Mungu hata kama hujapotoshwa, achilia mbali wakati huu ambapo umejazwa na tabia potovu ya kishetani. Wewe unaweza hata zaidi kumsaliti Mungu wakati wowote na mahali popote. Sasa unahitajika kutupilia mbali tabia potovu, ili kwamba hayo mambo yaliyo ndani yako yanayomsaliti Mungu yatapungua zaidi na zaidi, na utakuwa na nafasi nyingi zaidi mbele ya Mungu kumruhusu Yeye kukukamilisha na kukukubali. Ikiwa utapata uzoefu mwingi kuhusu wokovu wa Mungu katika mambo yote, utakamilishwa wakati wa hatua hii. Hivyo, ikiwa kitu fulani cha Shetani, au pepo mchafu, atakuja kukudanganya na kukusumbua, unaweza basi kutumia utambuzi wako, au sivyo? Kwa njia hii, tabia yako ya usaliti itapungua, na hiki ni kitu ambacho kitahemshwa ndani yako katika siku za baadaye. Wanadamu walipoumbwa kwa mara ya kwanza, hawakuwa na akili hii, wala hawakufahamu ibada ya Mungu, jinsi ya kumtii Mungu au usaliti wa Mungu ni nini. Shetani alikuja kuwashawishi wanadamu na wakamfuata, walimsaliti Mungu, na wakawa wasaliti kwa Mungu. Hii ni kwa sababu wanadamu hawakuwa na uwezo wa kutambua mema na mabaya, hawakuwa na akili ya kumwabudu Mungu, wala hawakuwa na ufahamu wowote kwamba Mungu alikuwa Muumba au ufahamu wowote wa jinsi wanadamu wanapaswa kumwabudu Mungu. Katika siku za baadaye, Mungu kuwafinyanga wanadamu sasa ni kufanya kweli hizi (ufahamu wa kiini cha Mungu na tabia Yake...) ndani ya wanadamu, ili kwamba waweze kufahamu hali hizi na wawe kiwango fulani cha kujitawala na hali hizi. Yaani, kadiri uzoefu wako unavyokuwa wa kina, ndivyo utakavyomfahamu Mungu na ndivyo utapunguza kuwa na mambo yanayomsaliti Mungu. Kadiri unavyokuwa na mambo yanayopatana na Mungu, ndivyo utakavyoweza kumshinda Shetani, kadiri unavyokuwa na hali ya kujitawala, ndivyo utakavyoweza kuishi kwa kudhihirisha maisha ya kweli. Baadhi ya watu huuliza: "Wanadamu wana kiini cha upotovu ndani yao na wanaweza kumsaliti Mungu wakati wowote na mahali popote; ni vipi ambavyo Mungu anaweza kusema bado Amewafanya wanadamu kuwa wakamilifu?" Kufanywa mkamilifu ni kumfahamu Mungu kupitia kwa uzoefu, na pia ni kufahamu asili yao wenyewe, kujua jinsi ya kumwabudu Mungu na kumtii Mungu, kuweza kutambua kati ya kazi ya Mungu na kazi ya wanadamu, na kutambua tofauti kati ya kazi ya Roho Mtakatifu na kazi ya pepo wachafu kupitia kwa uzoefu. Pia ni kuwa na ufahamu wa jinsi Shetani ibilisi humuasi Mungu, jinsi wanadamu humuasi Mungu, uumbaji ni nini na Muumba ni nani. Ninyi mnafahamu mambo haya, au sivyo? Haya yote ni mambo waliyopewa wanadamu kupitia kwa kazi ya Mungu katika siku za baadaye. Hivyo, wale watakaofanywa wakamilifu mwishowe watabeba uzito zaidi na watakuwa na thamani zaidi kuliko wale wa hapo mwanzo ambao hawakuwa wamepitia upotovu. Kwa sababu kuna mambo mengine ambayo yameongezwa ndani ya wanadamu na mambo mengine ambayoyamehemshwa ndani yao, watu wanaofanywa wakamilifu mwishowe watakuwa na hali ya kujitwala kuliko Adamu na Hawa wa wakati huo, na watafahamu ukweli zaidi wa jinsi ya kumwabudu Mungu na kumtii Yeye; watafahamu zaidi jinsi ya kuwa binadamu. Adamu na Hawa hawakujua mambo haya na nyoka alikuja kuwashawishi na wakala tunda kutoka kwa mti wa kufahamu mema na mabaya. Mwishowe walijua aibu, na wakaendelea kutojua jinsi ya kumwabudu Mungu, na wakawa wapotovu zaidi na zaidi, hadi wakati huu. Hili ni jambo la kina kabisa, na hakuna yeyote katika ubinadamu potovu anayeweza kulifahamu kabisa. Wanadamu bado wanaweza kumsaliti Mungu wakati wowote na mahali popote kwa sababu ya silika za mwili wao. Ilhali, mwishowe, Mungu atawakamilisha wanadamu na kuwaingiza katika hatua inayofuata; hili ni jambo ambalo watu huona ni vigumu kulifahamu.
Kwa nini wanadamu wanahitajika kumfahamu Mungu? Ikiwa wanadamu hawatamfahamu Mungu au hawatafahamu hali hii ya ukweli, basi watatumiwa kwa urahisi sana na kudanganywa na pepo wachafu. Mara tu wanapofahamu ukweli, basi haitakuwa rahisi kwao kudanganywa na kutumiwa na pepo wachafu. Lakini ikiwa, baada ya wewe kupata ufahamu huu, na ukaendelea kufanya jambo unalojua kwamba ni kukosea amri za usimamizi za Mungu au linafanywa kwa kuasi Mungu, basi hutaweza kukombolewa. Wewe uko katika hali gani wakati huu? Maadamu sasa mna tumaini moja, bila kujali iwapo Mungu anakumbuka mambo ya zamani au la, mnapaswa kudumisha fikira hizi: Ni lazima nitafute badiliko katika tabia yangu, nitafute kumfahamu Mungu, kutodanganywa na Shetani tena na kutofanya chochote kinacholeta aibu kwa jina la Mungu. Ni sehemu gani kuu huamua iwapo mtu sasa ana thamani yoyote, iwapo ataokolewa au la na iwapo ana tumaini yoyote au la? Nazo ni, baada ya wewe kusikia mahubiri, iwapo unaweza kupokea ukweli au la, iwapo unaweza kutekeleza ukweli huo au la na iwapo unaweza kubadilika au la. Hizi ni sehemu muhimu. Ikiwa utahisi tu majuto, ikiwa utaenda tu kufanya mambo na kuendelea kufikiria kwa njia hiyo hiyo ya zamani, na ukose kuwa na ufahamu wowote kabisa kuhusu jambo hili lakini badala yake uwe mbaya zaidi na zaidi, basi utakosa tumaini na unapaswa kutangazwa kuwa asiye na thamani. Kadiri unavyomfahamu Mungu, na kadiri unavyojifahamu, basi ndivyo utakavyoweza kujitawala mwenyewe. Kadiri unavyoweza kupenya katika asili yako mwenyewe kwa ufahamu, ndivyo utakavyoweza kujitawala mwenyewe. Baada ya wewe kujumlisha uzoefu wako, hutawahi tena kushindwa katika jambo hili. Kwa kweli kabisa, kila mtu ana madoa fulani juu yake ambayo hayajachunguzwa tu. Kila mtu anayo, wengine wana madogo, wengine wana makubwa; wengine huongea waziwazi, na wengine huficha nia zao na kufanya kazi kwa siri. Kila mtu anayo; Baadhi ya watu hufanya mambo ambayo watu wengine wanajua kuyahusu na baadhi ya watu hufanya mambo ambayo watu wengine hawajui kuyahusu. Kuna mawaa juu ya kila mtu na yote yanafichua tabia fulani za upotovu, kama vile kiburi au majivuno, au wao hufanya dhambi fulani, au makosa fulani au kupotoka katika kazi zao, au wanaonyesha kiasi kidogo cha ukaidi. Haya yote ni mambo ya kusamehewa kwani ni mambo ambayo mtu yeyote aliyepotoka hawezi kuepuka. Ilhali yanapaswa kuepukika mara tu unapofahamu ukweli. Na hakutakuwa tena na haja ya wewe kusumbuliwa mara kwa mara na mambo yaliyofanyika katika siku za zamani. Badala yake, inafaa kuhofiwa kwamba bado hutabadilika hata baada ya kupata kufahamu, eti utajua kwamba si sahihi kufanya kitu na bado uendelee kukifanya, na kwamba utaendelea kufanya kitu fulani hata baada ya kuambiwa kwamba ni kibaya. Watu hawa hawawezi kukombolewa.
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni