Mwenyezi Mungu alisema, Ninaibua maswali machache kwa tafakari yenu: Tangu mara ya mwisho tuliposema kwamba kutakuwa na miaka saba mingine ya majaribu makubwa, iwe ni kwa dhiki au majanga, je, mmegundua kusudi la Mungu kupitia kwa hayo? Ni asili gani ya binadamu mnaweza kuona katika mijibizo na mitazamo ya watu kwa miaka hii saba ya majaribu? Hili litachanganuliwa vipi? Fikirieni hilo. Ninazungumzia asili ya binadamu katika kila ushirika, kufikia chanzo, kuchanganua asili ya binadamu, na kuchanganua kiini. Ni juu yenu basi kuwasiliana ufahamu wenu kuhusu hizi mada.
Mnapaswa kuelewa kusudi la Mungu na ni lazima muijue asili ya binadamu kupitia hii miaka saba ya majaribu. Kwa hakika, kila sentensi ya Mungu ina kusudi Lake, ambamo mmefichwa ukweli. Bila kujali ni suala gani linafanyiwa ushirika, au ni ukweli gani unaoenyeshwa, ndani yake mna njia ambayo watu wanapaswa kupitia, matakwa ya Mungu kwa watu, na kusudi la Mungu kwa wanaomtafuta. Katika haya mazungumzo ya majaribu, dhiki, na hatimaye mateso, matakwa kwa watu na kusudi la Mungu pia vimo ndani. Watu, bila shaka, wanaonyesha hisia kwa mitazamo yao, kwa kuwa watu hawajaundwa kwa mbao; wako hai, na wanaonyesha hisia kwa kila kitu. Je, kuna maana kuchanganua ni hali gani za asili ya binadamu zinawakilishwa katika hisia za watu? Ina maana kushiriki kuihusu? Uchanganuzi utasaidia watu kuliona hilo wazi, kulijua wao wenyewe, na kujua vyema kabisa mioyoni mwao ili kwamba hatimaye wawe na njia mwafaka ya kuchagua. Ikiwa mtu amekanganyikiwa na hajui kusudi la Mungu, haelewi ukweli, na ana ufahamu mdogo kuhusu matakwa ya Mungu kwake na wajibu anaopaswa kutekeleza, au njia gani anapaswa kutembea, pengine mtu wa aina hii hatasimama imara. Kwa hivyo, inapaswa kujulikana ni njia gani inapaswa kutumiwa baadaye wakati wa majaribu mbalimbali.
Kila wakati majaribu ya miaka saba yanapotajwa, kuna watu wengi wanaohisi vibaya sana na kuvunjika moyo kusiko kwa kawida, na kuna watu wengine ambao hulalamika, na kuna mchanganyiko wa hisia. Ni dhahiri kutokana na hizi hisia kwamba watu sasa wanahitaji majaribu haya, wanahitaji aina hii ya dhiki na utakasaji. Watu humwamini Mungu kwa nia ya kutaka kupata baraka siku zijazo. Watu wote wana kusudi na tumaini hili. Hata hivyo, upotovu ndani ya asili ya binadamu ni lazima uondolewe kupit majaribu. Katika hali yoyote usiyoipita, ni katika hizi hali ambamo ni lazima usafishwe—huu ni mpango wa Mungu. Mungu anakutengenezea mazingira, Akikulazimisha usafishwe hapo ili ujue upotovu wako mwenyewe. Hatimaye unafika hatua ambapo unaona heri kufa na kuziacha njama na tamaa zako, na kutii mamlaka na mipango ya Mungu.
Hivyo ikiwa watu hawana miaka kadhaa ya usafishaji, ikiwa hawana kiwango fulani cha mateso, hawataweza kuepuka utumwa wa upotovu wa mwili katika mawazo na mioyo yao. Katika hali zozote zile bado ungali mtumwa wa Shetani, katika hali zozote bado ungali na tamaa zako mwenyewe, matakwa yako mwenyewe—ni katika hali hizi ambamo unapaswa kuteseka. Mafunzo yanaweza kupatikana tu katika mateso, yaani, kuweza kupata ukweli, na kuelewa kusudi la Mungu. Kwa kweli, ukweli mwingi unafahamika katika uzoefu wa majaribu makali. Hakuna asemaye kuwa kusudi la Mungu linajulikana, kwamba uweza na busara Yake vinafahamika, kwamba tabia ya haki ya Mungu inaonekana katika mazingira ya utulivu au katika hali zinazofaa. Hilo haliwezekani!
Mungu ametayarisha mazingira mwafaka ambamo Anawafanya watu kuwa wakamilifu, ila haijulikani kwa yeyote ni kwa nini Mungu anaweza kutaka kuwajaribu watu, kuwatakasa. Nyinyi nyote mnasema, “Mungu anawependaje wanadamu kwamba Anaweza kutayarisha miaka saba ya majaribu kuwatakasa watu na kuwafanya safi! Ni mvumilivu kiasi gani! Ni mwenye kuonyesha huruma kiasi gani!” Haina haja uyaseme haya, kila mmoja anaelewa mafundisho, lakini kwa hakika hakuna yeyote anayeifahamu hali halisi Je, miaka saba ya Mungu ya majaribu, miaka saba ya kazi ni ya nini? Bila shaka, inahitajika ili kwamba kazi Yake ifanyike. Hata bila kukuokoa, bado kuna upendo, sawa? Anapokuokoa, unasema, “Haya ni mapenzi aliyonayo Mungu kwetu, hii ni huruma Yake.” Je, Asingekuwa ametayarisha hii miaka saba ya majaribu, na kukamilisha kazi mara moja, bado kusingekuwepo upendo? Je, ingelikuwa miaka miwili ya majaribu, au mwaka mmoja, au siku ingalifika mara moja, je, hayo yasingekuwa mapenzi na huruma? Si kama unavyodhani: Miaka saba ya majaribu ni utakaso wa Mungu kwetu, ni kiwango Anachotupenda: ni lazima tutii. Unasema haya wakati tu hakuna njia nyingine. Hili linadhihirisha nini? Linadhihirisha uhasi, linadhihirisha lawama, na linadhihirisha kukosa njia mbadala na kukata tamaa. Mungu alisema kwamba kutakuwa na miaka saba mingine. Wacha iwe miaka saba basi. Kisha unakurupuka na kusema maneno mazuri: Mungu, Unatupenda; Mungu, ni kwa ajili ya kututakasa. Bila miaka saba ya majaribu, je, huo usingelikuwa mwisho wetu? Kusingelikuwa na fursa. Watu wengine wanatamani kubarikiwa sasa hivi. Hiyo inaweza kuwa faida halisi! Mtu kama huyo hajali kitu kingine chochote kile. Mtu kama huyu hafai hata kwa senti moja. Kuna kazi ya vitendo katika hii miaka saba. Je, haijasemwa awali kwamba maneno mengine ni njia, lakini vilevile ni ukweli? Hakuna kipengele ambacho ni maneno tu bila matendo. Kila kipengele kina dhima. Aidha, kama aionavyo mwanadamu, takribani kila kipengele kina njia, lakini njia hii si ya kukurairai, si ya kukudanganya. Badala yake ni mazingira ya kweli, hali halisi Hakuna njia mwafaka kuliko hii. Baada ya kusikia maneno haya, watu wengine hufikiri: Ikiwa ni kama usemavyo, hii miaka saba inapoisha, ni nani anaweza kutambua umesalia muda kiasi gani! Kutokana na mijibizo ya watu inaonekana kuwa asili ya binadamu imewekwa kwa namna kwamba baada ya kukumbana na majaribu ya mateso, kupokea uchungu mwilini, anataka kuuepuka na kuukataa. Hakuna hata mtu mmoja hujitokeza na kuchukua hatua ya kudai: Mungu, nipe majaribu fulani ya kuteseka, nipatie dhiki fulani. Mungu, nipatie taabu zaidi. Hili linadhihirisha kuwa kiasilia watu hawapendi ukweli. Iwe ni kusudi la Mungu au la, au inafaidi watu vipi, haijalishi ni nzuri kiasi gani, watu wote hukataa hali yoyote inayoiletea miili yao machungu au ile isiyoafiki matamanio yao. Kuna watu wasemao: “Sipingi. Nilifanya uamuzi zamani kuyatoa maisha yangu yote kwa Mungu. Nina furaha kabisa haijalishi ni miaka mingapi, na nitamtumikia Mungu kwa moyo. Sina lawama. Haijalishi ninakumbana na majaribu gani, haijalishi ninakutana na mateso gani, iwe ni kutelekezwa na familia au maumivu ya ugonjwa, nitafuata hadi mwisho.” Huku kutokuwa na lawama kwako pia ni aina ya hali hasi, kwa sababu kila wakati unapokumbana na kitu chochote, kila wakati unaposemewa maneno, kwa hakika huelewi maana iliyo ndani. Hii “sina mjibizo” unayoisema kwa hivyo si kingine bali ni kutojali, njia wakati ambapo hakuna njia nyingine. Hakuna jingine la kufanya ila hili, kwa hivyo unajilazimisha kufuata hata wakati ambapo hauko radhi. Kwa vyovyote vile hakuna awezaye kufaulu kuepuka miaka saba ya majaribu. Hata hivyo, hii ni tofauti na wewe kutaka kutoroka. Ungetamani kuepuka lakini huwezi. Hili ni jambo la asili ya mwanadamu. Lifikirie. Je, ndivyo ilivyo? Watu wengine wanahisi: Nilipokumbana na tukio kama hili miaka kumi iliyopita, daima nilifuata, na niliteseka sana, kwa hivyo ninaweza kuendelea kuvumilia kwa miaka michache. Kutafuta kwenu kwa kusudi la Mungu kumekanganyikiwa na hamjakutilia maanani. Hivyo, ikiwa kwa ndani hujayatii mapenzi ya Mungu, basi umeyasaliti na kukana mapenzi ya Mungu. Ijapokuwa huna hali hii, na hujafanya jambo hili, hizi dalili, haya mambo yaliyo ndani yako, yanamkana Mungu, kwa sababu unachokifiria na kutarajia kwa ndani sicho Mungu anachokihitaji. Aidha kwa hakika humsifu Mungu kutoka ndani ya moyo wako kwa yote Anayohitaji kutoka kwako na yote Anayofanya, iwe ni njia, au kile ulichoambiwa.
Na kwa kila kitu Mungu ambacho anawataka watu wafanye, chochote Mungu alichowapangia watu kulingana na mahitaji yao, asili ya binadamu ni kukikataa, kukosa kukikubali. Haijalishi unautangaza vipi msimamo wako, au iwe una ufahamu kidogo, kwa vyovyote vile, ufahamu wako wa mafundisho hauwezi kutatua kilicho katika asili yako. Kwa hivyo ninasema kwamba watu wengi wanazungumzia vitu vizuri katika mafundisho, na kusema maneno ya juujuu kuyastahimili. Hatimaye, japo, katika maombi wanasema: Nimepitia kwa ufanisi miaka mingi sana. Miaka saba si miaka mingi na wala si miaka michache. Tazama ninavyozeeka, jinsi afya yangu ilivyoharibika, na kwamba sina familia nzuri. Nimeandamana na Wewe miaka hii yote, nifanya bidii hata bila malipo, nimechoka ijapokuwa sijafanya kazi kwa bidii. Hata kama Utaipunguza hata kwa miaka michache, nifanyie hisani mara hii moja! Unajua udahaifu wa watu… Kwa kuomba maneno haya, ni kama kuna utiifu kidogo. Wanaendelea kusema “Unajua udhaifu wa watu”; kuna maana nyingine ndani ya maneno haya, ambayo ni kusema, Unajua udhaifu wa binadamu, basi ni kwa nini inachukua muda mrefu kiasi hiki? Je, hii si hali iliyo ndani mwa watu? Kwa hivyo, mnahisi mnafahamu vitu vingi, tayari mmevikubali, na kuonekana mmefahamu ukweli, lakini kwa hakika bado mnaukataa ukweli, na kwenda kinyume cha ukweli. Vitu mnavyovifanya haviambatani na ukweli. Japo kijuujuu hamjafanya vitendo viovu, na hamjatamka kitu chochote kibaya, hii imejikita tu kwa kutovunja amri za utawala, kwa kutoikosea tabia ya Mungu. Hujaelewa kusudi Lake na hata hivyo hauko tayari kulipokea. Hukubaliani na Yeye kufanya mambo kwa njia hii. Unafikiri: Iwapo nitaifanya kazi hii, sitapoteza muda na nitaikamilisha kazi hii kwa muda mfupi iwezakanavyo, ili kwamba niwasaidie watu wa Mungu kuepuka mateso zaidi kutoka kwa joka kuu jekundu, kuzuia kupotea kwa watu wengi zaidi, kuepuka mateso yangu. Je, hili si wazo walilonalo watu? Watu mioyoni mwao wanatumaini kufika kwa ufalme wa Mungu, na kuangamia kwa haraka kwa ulimwengu wa Shetani. Ni neema kubwa ikiwa neno moja la Mungu litawabadilisha. Mitazamo ya ndani ya watu, matamanio yao makubwa kwa hakika hayatekelezi kusudi la Mungu, na kimsingi hakuna kiini cha kutii. Hili pia linagusa ule msemo: Asilimia mia moja ya kile kilicho ndani ya asili ya binadamu ni usaliti. Kwa hivyo, kwa kulichanganua hili au lile tukio lenu, kwa kulichanganua hili suala, lile wazo, au ile hisia, iwe unaikabili kwa njia hasi, au unalalamika, ikiwa hujali au umenyamaza bila kusema neno, kuna ukinzani katika haya yote. Haya yote ni usaliti. Je, huu uchanganuzi ni sahihi? Nisingalichanganua hili, kungekuwepo na watu wanaohisi: Ninaweza kudhaniwa kuwa mtu mzuri. Ningekumbana na jambo hili miaka michache iliyopita, bila shaka ningelalamika, ikiwezekana ningerudi nyuma, lakini sasa silalamiki. Hulalamiki, lakini je una uelewa? Je, uelewa wako mdogo unajumuisha uelewa wa kweli? Kuna ukweli ndani yake? Je, uelewa wako unalingana na kusudi la Mungu? Je, umepata kibali cha Mungu? Je, una kiini cha kumtii Mungu? Je, uko radhi na tayari kumtii Mungu? Kama sivyo, basi bila shaka unakinzana na Mungu. Inawezekana kwamba hali yako ya moyo sasa hivi ni nzuri, na hujihisi vibaya, au kwa sababu sasa hivi umewekwa katika kufanya kazi. Ikiwa siku moja utatumwa nyumbani, na utakapokuwa katika giza la hali mbaya ya moyo, hata hivyo, kilicho ndani ya moyo wako kitafichuliwa. Kuna watu wengine wenye kimo kidogo, wenye muda mfupi wa uzoefu ambao wanaweza kugeuka na kukimbia, kurudi ulimwenguni. Kwa hakika, katika uchanganuzi wa mwisho, mjibizo wowote ule ulionao, unakataa mazingira aliyokupangia Mungu. Asili ya watu ya kumsaliti Mungu inafichuliwa kila mahali. Ikiwa hili lisingechanganuliwa, watu wasingejijua kwa kina ipasavyo. Watu wakikumbana na kitu chochote, wote wanamsaliti Mungu na wanakosa kumtii. Mijibizo ya baadhi yenu ni kutotaka, au hisia za malalamiko, uhasi na huzuni, na mnasema: Kwa ndani, binadamu hapendi ukweli, na huku kutopenda si kingine bali ni usaliti. Bado haitoshi kama mnazungumza namna hii tu, na hamjachanganua hadi kwenye kina cha kiini. Mnasema kwamba kutopenda ukweli ni usaliti, lakini kwa kweli, hili si sahili hivyo Mmelichanganua vipi? Hamjielewi nyinyi wenyewe. Unaweza usijue hiyo ni hali gani uliyonayo, na huwezi kutofautisha mazuri na mabaya, ikiwa ni usaliti au la, na hujijui wazi wewe mwenyewe iwe umetii au la. Hamuwezi kuchanganua kabisa asili zenu wenyewe. Kila mara mnapokumbana na jambo fulani mnashindwa kujua namna ya kwenda mbele. Hatimaye, utakapokumbana na jaribu, je, utaweza kulitambua kusudi la Mungu? Utalifafanua hili vipi? Unapaswa kutembea katika njia gani? Ni mantiki gani au ni ukweli gani unapaswa kuwa nao ili kukidhi kusudi la Mungu? Kama kiwango cha chini zaidi, ni lazima uwe na mtazamo chanya. Je, mmeyawazia maswali haya?
Zamani watu wengine walikuwa na mawazo kuhusu anachokifanya Mungu mwenye mwili. Ushirika uliofuata ulisababisha kuwepo na ukweli usiohitaji uthibitisho. Ukweli huu usiohitaji uthibitisho ni: Binadamu wanapaswa kukiri kuwa yote anayofanya Mungu ni sahihi, kuwa yote ni muhimu. Kama binadamu hawataelewa wanapaswa hata hivyo kutii na si kupinga. Kama binadamu wana mawazo ni lazima wataaibika. Je, watu wanakumbuka maneno haya? Kila mara wanapokabiliana na kitu, wanajisemea wao wenyewe: Kwa namna yoyote usiwe na mawazo, kwa namna yoyote usiyahukumu. Kuna maana katika kila kitu anachokifanya Mungu. Ijapokuwa hatuwezi kuelewa kwa sasa, siku moja tutapata aibu. Wanazishikilia tu sheria kama hii. Sheria ya aina hii, hata hivyo, yaweza kusuluhisha matatizo kadhaa ya waumini ambao wamekanganyikiwa. Kwa mtu aliye na uelewa haya maneno yatasaidia kuelewa maana ya vitu vingi, na kutumia hii sheria kila mara hali inaposhuhudiwa yaweza kuweka wazi mambo mengi. Ni nini kinachofanyika kama hakuna umaizi? Mtu anaweza tu kutii sheria, na katika kufanya hivyo anaweza pia kulindwa na kuzuia kukiuka amri za utawala, si kueneza maafa. Sheria hii ina manufaa! Sio ati haina maana! Katika sehemu mbalimbali sheria hii imesomwa kwa moyo. Wengine huiandika madaftarini, au kuiandika kwenye jalada la kitabu, na kuisoma kila wakati wanapofungua kitabu, huku wakiikariri. Wanaikariri wanapoomba. Kufanya hivyo kuna manufaa kadhaa. Watu wengine hawathubutu kufanya mambo kwa kubahatisha, na wana uchaji mdogo mioyoni mwao. Ila kulingana na watu wengi, hawana uelewa wa kweli wa hali chanya, na kuna vitu vingi sana vilivyo hasi. Ijapokuwa inaonekana kuwa mnajihisi vyema kabisa na hamjaacha kufanya kazi, kuna vitu vingi hasi kwa kweli kati yenu, na hakuna vitu chanya. Kuna mijibizo mingi sana kanisani kuhusu mambo kama haya. Je, mmejaribu kujijumuishia nyinyi wenyewe? Kama vitu vya aina hii vingekabiliwa tena, mngemkataa Mungu au kumsaliti Mungu? Kuna baadhi ya watu ambao labda wametambua, "Binadamu hana uwezo wa kuielewa asili yake mwenyewe. Bila shaka sitajaribu kukataa tena, na lazima niwe makini. Lazima niombe kila siku!” Huu sio mpango wa uhakika. Nimegundua kuwa huwa mnapata aibu, na mara nyingi mnasema: "Ah, nitafanya nini kuhusu hii asili ya binadamu? Siwezi kuisuluhisha mimi mwenyewe, na siwezi kuielewa. Kwa kweli sina haki ya kujisimamia mimi mwenyewe. Sijui ninaweza kufanya nini siku moja. Ninaogopa sana. Kumwamini Mungu lazima kufanyike kwa makini mno. Uzembe wowote waweza kusababisha maafa, na hilo laweza kuwa jambo baya mno. Hata sijijui, siwezi kujitegemea..." Ingawa watu wanaosema haya mara kwa mara huwa wanajielewa kwa kiasi fulani, wana uelewa kidogo mno kuhusu ukweli. Wanachanganyikiwa kila mara wanapokumbana na kitu chochote. Wanapatwa na wasiwasi, wanahisi uoga, na hawana njia yoyote ile wanapopatwa na chochote kile. Wakati huu umeshinda miaka saba ya majaribu, na hujasababisha maafa, na hujakiuka amri za utawala, lakini je, waweza kuwa na uhakika kuhusu wakati ujao? Wawezaje kuyashinda haya yote bila kizuizi? Unaona kuwa umeyashinda masaibu kwa urahisi sana, kwa kujificha hapa na pale. Ulijificha kwa mwaka mmoja au nusu mwaka hadi yakaisha. Wanadamu wanaweza kujificha, lakini asili ya binadamu ni kitu ambacho hakiwezi kufichika. Je, hakupaswi kuwa na ukweli uisohitaji thibitisho unaohusiana na hili, pia? Katika kila majaribu ya Mungu kuna nia nzuri. Kwa kila tukio linaloshuhudiwa kuna ukweli ambao mtu anapaswa kuwa nao ili kusimama imara. Jiandaeni na ukweli ili kukabiliana na majaribu tofauti tofauti kwa sasa, na hamtaogopa bila kujali miaka ya majaribu hapo mbeleni. Lazima muwe na ujasiri. Kutii mipango ya Mungu kamwe hakuwezi kuwa na dosari. Njia daima itakuwa na matumaini. Mwawezaje kuwa wakamilifu bila majaribu kadhaa? Bila majaribu, hakuna shahidi. Ni vipi basi mtamridhisha Mungu? Majaribu yatawaletea baraka za Mungu. Ni kwa kumfuata tu Mungu hadi mwisho ndipo mtu aweza kuingia katika ufalme. Kumbuka: nyinyi nyote mna fungu katika dhiki, ufalme, na uvumilivu wa Kristo.
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni