Mwenyezi Mungu alisema, Tamaduni za asili na mitazamo ya kiakili madhubuti vimeweka kivuli katika roho safi na ya kitoto ya mwanadamu, vimeshambulia roho ya mwanadamu bila ubinadamu hata kidogo kana kwamba anaondolewa hisia na hali yoyote ya nafsi. Mbinu za mashetani hawa ni za kikatili kupita kiasi, na ni kana kwamba "elimu" na "malezi" vimekuwa ni njia za kitamaduni ambazo kwazo mfalme wa mashetani anamchinja mwanadamu;
Kanisa la Mwenyezi Mungu lilikuja kuwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu.
NYUMBANI
Usomaji wa Maneno ya Mwenyezi Mungu
Filamu za Injili
Kwaya za Injili
Maisha ya Kanisa—Mfululizo wa Maonyesho Mbalimbali
Video za Nyimbo na Ngoma
Msururu wa MV za Ufalme
Video za Nyimbo za Dini
Filamu za Maisha ya Kanisa
Filamu za Uzoefu wa Mateso
Kufunua Mfululizo wa Video za Ukweli
Sehemu za Filamu
Aina za Dondoo za Video
Jumamosi, 31 Machi 2018
Ijumaa, 30 Machi 2018
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (8)
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (8) |
Mwenyezi Mungu alisema, Nimezungumza mara nyingi sana kwamba kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kwa ajili ya kubadilisha roho ya kila mtu, kubadilisha nafsi ya kila mtu, ili kwamba moyo wake, ambao umeteseka sana na kiwewe, uwe umebadilishwa, hivyo kuokoa nafsi yake, ambayo imeumizwa kwa kina zaidi na Shetani; ni kwa sababu ya kuamsha roho za watu, kuyeyusha mioyo yao baridi, na kuwaruhusu kurudisha nguvu za ujana. Haya ndiyo mapenzi makubwa ya Mungu.
Alhamisi, 29 Machi 2018
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (7)
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (7) |
Imemchukua mwanadamu mpaka siku hii kutambua kwamba kile mtu anachokosa si tu kuruzukiwa maisha ya kiroho na uzoefu wa kumjua Mungu, lakini, muhimu zaidi, mabadiliko katika tabia yake. Kutokana na ujinga kamili wa mwanadamu wa historia na utamaduni wa kale wa wanadamu, hana ujuzi wa kazi ya Mungu hata kidogo. Mwanadamu hutumaini kuwa ndani kabisa ya moyo, mwanadamu anaweza kumpenda Mungu sana, lakini kwa sababu ya upotovu mkubwa mno wa mwili wa mwanadamu, pamoja na kutojali na upumbavu, mwanadamu ameshushwa kuwa asiye na ufahamu wa Mungu hata kidogo.
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (2)
Kazi na kuingia kwenu ni duni kabisa; mwanadamu hafikirii kwamba kazi ni muhimu na hata yeye ni mzembe zaidi na kuingia. Mwanadamu haoni haya kuwa mafunzo mazuri anayopaswa kuingia ndani; kwa hivyo, katika uzoefu wake wa kiroho, kwa kweli yote ambayo mwanadamu huona ni njozi za kiajabu. Si mengi yanatakiwa kutoka kwenu kuhusu uzoefu wenu katika kazi, lakini, kama yule anayetakiwa kukamilishwa na Mungu, mnapaswa kujifunza kumfanyia Mungu kazi ili hivi punde muweze kuupendeza moyo wa Mungu.
Jumatano, 28 Machi 2018
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (1)
Tangu watu waanze kuikanyaga njia sahihi ya maisha, kumekuwa na mambo mengi ambayo bado hayajaeleweka vizuri. Bado wapo kwenye mkanganyiko kabisa kuhusu kazi ya Mungu, na kuhusu kiasi gani cha kazi wanapaswa kufanya. Hii, kwa upande mmoja, ni kwa sababu ya kuwa na uelekeo tofauti wa uzoefu wao na mipaka katika uwezo wao wa kupokea; kwa upande mwingine, ni kwa sababu kazi ya Mungu bado haijawaleta watu katika hatua hii. Kwa hiyo, kila mtu anapata utata kuhusu masuala mengi ya kiroho.
Jumanne, 27 Machi 2018
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (6)
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (6) |
Mwenyezi Mungu alisema, Kazi na kuingia kwa uhalisia ni vya kiutendaji na vinarejelea kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu. Mwanadamu kukosa kabisa uelewa juu ya sura halisi ya Mungu na kazi ya Mungu kumesababisha shida kubwa katika kuingia kwake. Leo hii, watu wengi bado hawajui kazi ambayo Mungu anatimiza katika siku za mwisho, au kwa nini Mungu Anastahimili fedheha kubwa kupita kiasi kuja katika mwili na kusimama na mwanadamu katika makovu na majonzi.
Jumatatu, 26 Machi 2018
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (4)
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (4) |
Ikiwa mwanadamu anaweza kuingia kabisa kulingana na kazi ya Roho Mtakatifu, maisha yake yatachipuka haraka kama mmea wa mwanzi baada ya mvua ya majira ya kuchipua. Kwa kuangalia kimo cha sasa wa watu wengi, hakuna mtu hata mmoja anayetilia mkazo umuhimu wa uzima. Badala yake, watu wanaweka umuhimu katika baadhi ya mambo ya juujuu yasiyokuwa na umuhimu.
Jumapili, 25 Machi 2018
"Vunja Pingu na Ukimbie" (4) - Jifungue Kutoka kwa Utumwa wa Mafarisayo wa Kidini na Kurudi Kwa Mungu
Katika jumuiya ya kidini, wachungaji wanajua Biblia kwa kina na mara nyingi huelezea vifungu kutoka kwa Biblia kwa watu. Kutoka kwa macho yetu, inaonekana kuwa wote wanamjua Mungu, lakini kwa nini kuna watu wengi katika ulimwengu wa kidini ambao huilaumu na kuipinga kazi ya Mungu mwenye mwili ya siku za mwisho? Mwenyezi Mungu anasema, "Wale wanaosoma Biblia kwa makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu.
Jumamosi, 24 Machi 2018
"Vunja Pingu na Ukimbie" (3) - Enda Nje ya Biblia: Hudhuria Karamu ya Ufalme wa Mbinguni Pamoja na Bwana
Watu wengi ambao wana imani katika Bwana huhisi kwamba maneno na kazi ya Mungu vyote viko katika Biblia, kwamba wokovu wa Mungu kama ulivyoelezewa katika Biblia tayari umejaa, kwamba imani katika Mungu lazima iwe kwa msingi wa Biblia na kwamba kama imani yetu kwa Mungu ni kwa msingi wa Biblia, basi kwa hakika tutanyakuliwa kuingia katika ufalme wa mbinguni. Dhana hizi za kidini hutenda kama kamba zisizoonekana ambazo huzifunga kwa uthabiti na kuzisonga fikira zetu kiasi kwamba hatuitafuti kazi ya Roho Mtakatifu na hutufanya tusiweze kuitii kazi ya sasa ya Mungu.
Ijumaa, 23 Machi 2018
"Vunja Pingu na Ukimbie" (2) - Je, Kila Kitu Kilicho Katika Biblia ni Neno la Mungu?
Kama watu wengi wa kidini wenye imani katika Bwana, Mzee Li daima amehisi kwamba "kila kitu kilicho katika Biblia kilitiwa msukumo na Mungu," "Biblia ni neno la Mungu," na "Biblia humwakilisha Mungu." Dhana hizi zilikuwa kwa muda mrefu zimeunda msingi wa imani yake. Zilikuwa zimekita mizizi ndani ya moyo wake na zilikuwa zimekuwa kikwazo kwa kujifunza kwake njia ya kweli na pia utumwa uliomzuia kukubali njia ya kweli.
Alhamisi, 22 Machi 2018
"Vunja Pingu na Ukimbie" (1) - Legeza Pingu na Ujifunze Njia ya Kweli
Mzee wa kanisa Li, kutokana na imani pofu katika maneno ya wachungaji wa kidini, alihisi kwamba kazi na maneno yote ya Mungu yaliandikwa katika Biblia na kwamba chochote nje ya Biblia hakingeweza kuwa kazi na neno la Mungu. Li alifikiri kwamba yote aliyohitaji kufanya ni kushika Biblia na wakati Bwana angekuja tena, angenyakuliwa kuingia katika ufalme wa mbinguni. Kwa hiyo, Li hakuipa fikira kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho.
Jumatano, 21 Machi 2018
Maono ya Kazi ya Mungu (2)
Maono ya Kazi ya Mungu (2) |
Enzi ya Neema ilihubiri injili ya toba, na alimradi mwanadamu aliamini, basi angeokolewa. Leo, badala ya wokovu kuna majadiliano tu ya ushindi na ukamilifu. Haisemwi katu kwamba mtu mmoja akiamini, familia yake yote itabarikiwa, au kwamba wokovu ni ya mara moja na kwa wote. Leo, hakuna mtu anayezungumza maneno haya, na vitu kama vile vimepitwa na wakati. Wakati huo kazi ya Yesu ilikuwa ni ukombozi wa wanadamu wote.
Maono ya Kazi ya Mungu (3)
Maono ya Kazi ya Mungu (3) |
Mara ya kwanza Mungu alipopata mwili ilikuwa kupitia kutungwa mimba kwa Roho Mtakatifu, na ilihusiana na kazi Aliyokusudia kufanya. Jina la Yesu liliashiria mwanzo wa Enzi ya Neema. Wakati Yesu Alianza kufanya huduma Yake, Roho Mtakatifu Alianza kutoa ushuhuda kwa jina la Yesu, na jina la Yehova halikuzungumziwa tena, na badala yake Roho Mtakatifu Alianza kazi mpya hasa kwa jina la Yesu.
Jumanne, 20 Machi 2018
Maono ya Kazi ya Mungu (1)
Maono ya Kazi ya Mungu (1) |
Yohana alimfanyia Yesu kazi kwa miaka saba, na tayari alikuwa ameandaa njia Yesu alipofika. Kabla ya haya, injili ya ufalme wa mbinguni iliyohubiriwa na Yohana ilisikika kotekote katika nchi, hivyo ilienea kutoka upande mmoja hadi upande mwingine wa Uyahudi, na kila mtu alimwita nabii. Wakati huo, Mfalme Herode alitamani kumuua Yohana, lakini hakuthubutu, kwani watu walimheshimu sana Yohana, na Herode aliogopa kwamba kama angemuua Yohana wangemuasi.
Jumatatu, 19 Machi 2018
Ni kwa Nini Ulimwengu wa Kidini Wenye Wayowayo kwa Hasira Unaipinga na Kuishutumu Kazi Mpya ya Mungu Daima?
Ni kwa Nini Ulimwengu wa Kidini Wenye Wayowayo kwa Hasira Unaipinga na Kuishutumu Kazi Mpya ya Mungu Daima? |
Mara mbili ambapo Mungu amepata mwili kutembea duniani na kufanya kazi ya kumwokoa mwanadamu Amekumbana na upinzani mkubwa, shutuma na mateso ya hasira kutoka kwa viongozi katika dunia ya kidini, ukweli ambao umewakanganya na hata kuwashtua watu: Ni kwa nini kila wakati Mungu anapoonyesha hatua ya kazi mpya Yeye daima hukumbana na aina hii ya utendewaji?
Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Wafuasi wengi wa Bwana Yesu Kristo husikia kuhusu Umeme wa Mashariki kutoka kwa wachungaji wao, wazee wa kanisa, au wahubiri, lakini kwa hakika hakuna mtu anayejua Umeme wa Mashariki ulitoka wapi. Linapokuja suala la asili ya Umeme wa Mashariki, kila mtu ana maoni yake mwenyewe: Watu wengine wanaamini kuwa ni dhehebu jipya tu katika Ukristo, wengine huitweza kuwa "uasi" au "dhehebu bovu."
Jumapili, 18 Machi 2018
Kuamini Uvumi ni Kupoteza Wokovu wa Mungu wa Siku za Mwisho
Kuamini Uvumi ni Kupoteza Wokovu wa Mungu wa Siku za Mwisho |
Wakati wowote wanaposikia mtu akizungumza juu ya injili ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, ndugu wengi wa kiume na wa kike kanisani wanashindwa kusikiliza na hawathubutu kukubali kile kinachosemwa kwa kuwa wameshtushwa na uvumi wa mihemko. Wanaweza kusikia mtu akisema: "Wale wanaomwamini Mwenyezi Mungu ni watu muhimu kweli, utadanganywa ukiwasiliana nao.
Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki
Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki |
Kila wakati Umeme wa Mashariki linapotajwa, ndugu wengi katika Bwana huhisi mafadhaiko: Ni kwa nini jumuiya ya kidini kwa ujumla huzidi kuhuzunika na kupotoka, wakati kila dhehebu linazidi kuwa na hadhari na kushikilia ukale katika kushutumu na kufukuza Umeme wa Mashariki, Umeme wa Mashariki halihuzuniki tu na kudhoofika, lakini linaendelea mbele kama mawimbi yasiyoweza kusimamishwa, likienea kote China Bara?
Jumamosi, 17 Machi 2018
Kwa nini Umeme wa Mashariki Hutapakaa Kwenda Mbele na Maendeleo Yasiyozuilika?
Kristo wa siku za mwisho amekuwa akifanya kazi Yake nchini China kwa zaidi ya miaka 20, kazi ambayo imetetemesha makundi mbalimbali ya kidini kwa kina. Swali la kufadhaisha zaidi kwa jumuiya za kidini wakati huu limekuwa: Wachungaji wengi na wazee wa kanisa katika jumuiya ya kidini wamefanya liwezekanalo kuuhukumu na kuushambulia Umeme wa Mashariki kupitia njia mbalimbali kama vile kueneza uvumi kuhusu na kuukashifu Umeme wa Mashariki.
Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo | Kuvunja Pingu
Kuvunja Pingu
Zhenxi Jijini Zhenzhou, Mkoani Hena
Miaka kumi iliyopita, nikiendeshwa na asili yangu ya kiburi, sikuweza kamwe kutii kikamilifu mipangilio ya kanisa. Ningetii ikiwa ilinifaa, lakini iwapo haingenifaa ningechagua iwapo ningetii au la. Hili lilisababisha kukiuka sana mipangilio ya kazi wakati wa kutimiza wajibu wangu. Nilifanya jambo langu mwenyewe na kuichukiza tabia ya Mungu, na hivyo baada ya hapo nilitumwa nyumbani. Baada ya miaka kadhaa ya kujitafakari, nilikuwa kwa kiwango fulani na maarifa ya asili yangu mwenyewe, lakini kuhusu kipengele cha ukweli ambacho ni kiini cha Mungu bado sikuwa na maarifa mengi.
Ijumaa, 16 Machi 2018
Ngoma ya Kikristo | Swahili Worship Song "Ufalme wa Kristo Unapatikana Miongoni mwa Wanadamu"
Ufalme wa Kristo Unapatikana Miongoni mwa Wanadamu |
Ufalme wa Kristo Unapatikana Miongoni mwa Wanadamu
Alhamisi, 15 Machi 2018
"Wakati Wa Mabadiliko"(2) - Njia ya Pekee ya Kuinuliwa Kwenda Katika Ufalme wa Mbinguni
Watu wengine huamini, kwa kuwa Mungu aliweza kuumba mbingu na dunia na vitu vyote kwa neno moja, kuweza kuwafufua wafu kwa neno moja, Mungu pia Ataweza kubadili taswira zetu mara moja, kutufanya watakatifu, kutuinua hewani kukutana na Bwana wakati Atakaporudi katika siku za mwisho. Je, kweli ni ili kuinuliwa kwenda katika ufalme wa mbinguni? Je, kazi ya kurudi kwa Mungu katika siku za mwisho rahisi hivyo jinsi tunavyofikiri? Mungu husema, "Lazima ufahamu wala usirahisishe mambo zaidi. Kazi ya Mungu ni tofauti na kazi nyingine ya kawaida. Uzuri wake hauwezi kutambuliwa na akili za mwanadamu wala hekima yake kupatikana vile.
"Wakati Wa Mabadiliko"(1) - Wanawali Wenye Hekima Hunyakualiwaje?
Watu wengine huongozwa na maneno ya Paulo katika suala la kumngoja Bwana ili kuinuliwa kwenda katika ufalme wa mbinguni: "Kwa ghafla, kufumba na kufumbua, wakati wa tarumbeta ya mwisho: kwa maana tarumbeta italia, na wafu watafufuliwa bila uovu, na tutabadilishwa" (1Kor 15:52). Wanaamini kwamba ingawa bado tunatenda dhambi siku zote bila kujinasua kutoka kwa pingu za asili ya dhambi, Bwana atazibadili taswira zetu mara moja na kutuleta katika ufalme wa mbinguni Atakapokuja.
Jumatano, 14 Machi 2018
Ngoma ya Kikristo | Swahili Worship Song "Ufalme wa Kristo Unapatikana Miongoni mwa Wanadamu"
I
Mwenyezi Mungu mwenye mwili
Anaonekana katika siku za mwisho Mashariki,
kama tu vile jua la haki likichomoza;
mwanadamu ameona mwanga wa kweli ukionekana.
Mungu wa haki na mwenye uadhama, mwenye upendo na huruma
Anajificha kwa unyenyekevu miongoni mwa wanadamu,
Akitoa ukweli, kuzungumza na kufanya kazi.
Swahili Gospel Movie "Vunja Pingu Na Ukimbie" | Bwana ni Mchungaji Wangu
Lee Chungmin alikuwa mzee wa kanisa fulani huko Seoul, Korea ya Kusini. Kwa zaidi ya miaka ishirini, alimtumikia Bwana kwa shauku kubwa, akamakinika kikamilifu juu ya kusoma Biblia. Akifuatia mfano wa viongozi wake wa kidini, alidhani kuwa kumwamini Bwana kulimaanisha kuiamini Biblia, na kwamba kuwa na imani katika Biblia kulikuwa sawa kabisa na kuwa na imani katika Bwana. Aliamini kwamba almuradi angeshika Biblia, angenyakuliwa kuingia katika ufalme wa mbinguni. Dhana hizi zilimbana kama jozi ya pingu, zikimzuia kufuata nyayo za Mungu na kumwamini Mungu. Matokeo yake, Lee Chungmin kamwe hakufikiria kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho …
Jumanne, 13 Machi 2018
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia... (8)
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia... (8) |
Wakati ambapo Mungu anakuja duniani kuchanganyika na wanadamu, kuishi nao, sio tu kwa siku moja au mbili. Labda kwa wakati huu wote watu wamemjua Mungu kwa kiwango fulani, na labda wamepata utambuzi muhimu wa kumhudumia Mungu, na wamepata uzoefu sana katika imani yao katika Mungu. Hata iweje, watu wanaelewa vizuri sana tabia ya Mungu, na maonyesha ya kila aina ya tabia za binadamu yanatofautiana kwa kweli. Jinsi Nionavyo, maonyesho tofautitofauti ya watu yanatosha kwa Mungu kuyatumia kama sampuli, na shughuli zao za fikira zinatosha kwa Yeye kurejelea.
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (7)
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (7) |
Sote tunaweza kuona katika uzoefu wetu wa utendaji kwamba kuna nyakati nyingi ambazo Mungu binafsi ametufungulia njia ili tuwe tunakanyaga njia iliyo imara zaidi, ya kweli zaidi. Hii ni kwa sababu hii ndiyo njia ambayo Mungu alitufungulia tangu mwanzo wa wakati na imepitishwa kwa kizazi chetu baada ya makumi ya maelfu ya miaka. Kwa hiyo tunarithi watangulizi wetu ambao hawakutembea njia hii mpaka mwisho wake; sisi ndio tumechaguliwa na Mungu kutembea sehemu ya mwisho ya njia hii.
Jumatatu, 12 Machi 2018
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia... (6)
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia... (6) |
Ni kwa sababu ya kazi ya Mungu ndio tumeletwa katika siku hii. Kwa hiyo, sisi sote ni wasaliaji katika mpango wa usimamizi wa Mungu, na kwamba tunaweza kubakizwa mpaka siku hii ni kutiwa moyo kwa hali ya juu kutoka kwa Mungu. Kulingana na mpango wa Mungu, nchi ya joka kuu jekundu inapaswa kuangamizwa, lakini Ninadhani kwamba labda Ameanzisha mpango mwingine, au Anataka kutekeleza sehemu nyingine ya kazi Yake. Kwa hiyo mpaka leo Sijaweza kuueleza kwa dhahiri—ni kama kwamba ni kitendawili kisichofumbuliwa.
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (5)
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (5) |
Ilikuwa kwamba hakuna aliyejua Roho Mtakatifu, na hasa hawakujua njia ya Roho Mtakatifu ilikuwa gani. Ndio maana watu kila mara walifanya upumbavu mbele ya Mungu. Inaweza kusemwa kwamba karibu watu wote wanaoamini katika Mungu hawamjui Roho, lakini tu wana aina ya imani iliyochanganyikiwa. Ni wazi kutokana na hili kwamba watu hawamfahamu Mungu, na hata ingawa wanasema wanaamini katika Yeye, kuhusu kiini chake, kulingana na matendo yao wanaamini katika wao wenyewe, sio Mungu.
Jumapili, 11 Machi 2018
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (4)
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (4) |
Kwamba watu wanaweza kugundua kupendeza kwa Mungu, kutafuta njia ya kumpenda Mungu katika enzi hii, na kwamba wako radhi kukubali mafunzo ya ufalme wa leo—hii yote ni neema ya Mungu na hata zaidi, ni Yeye ndiye anawainua wanadamu. Kila Nifikiriapo juu ya hili Mimi huhisi kwa uthabiti kupendeza kwa Mungu. Ni kweli kwamba Mungu anatupenda. La sivyo, nani angeweza kutambua kupendeza Kwake? Ni kutoka tu kwa hili ndio Naona kwamba kazi hii yote inafanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, na watu wanaongozwa na kuelekezwa na Mungu.
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (3)
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (3) |
Katika maisha Yangu, Niko radhi kila mara kujitolea Mwenyewe kwa Mungu kabisa, mwili na fikra. Kwa njia hii, hakuna lawama kwa dhamiri Yangu na Naweza kupata kiasi kidogo cha amani. Mtu anayeandama uzima ni lazima kwanza aukabidhi moyo wake wote kwa Mungu kabisa. Hili ni sharti la mwanzo. Ningependa ndugu na dada Zangu wamwombe Mungu pamoja na Mimi: “Ee Mungu!
Jumamosi, 10 Machi 2018
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (2)
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (2) |
Labda ndugu na dada zetu wana muhtasari kidogo wa utaratibu, hatua, na mbinu za kazi ya Mungu katika China bara, lakini Mimi huhisi kila mara kwamba ni heri kuwa na kumbukumbu au muhtasari kidogo wa ndugu na dada zetu. Ninatumia tu nafasi hii kusema machache ya kile kilicho moyoni Mwangu; Sizungumzi juu ya chochote nje ya kazi hii. Natarajia kwamba ndugu na dada wanaweza kuelewa hali ya moyo Wangu, na pia Naomba kwa unyenyekevu kwamba wote wanaosoma maneno Yangu wafahamu na kusamehe kimo Changu kidogo, kwamba uzoefu Wangu wa maisha kweli si wa kutosha, na kwamba kweli Siwezi kuwa na ujasiri mbele ya Mungu.
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (1)
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (1) |
Katika maisha yake, hakuna mtu anayejua ni aina gani ya vipingamizi ataenda kukutana navyo, wala hajui ni aina gani ya kusafishwa ambayo atapata mara kwa mara. Kwa wengine ni katika kazi yao, kwa wengine ni katika matazamio yao ya siku za baadaye, kwa wengine ni katika familia yao ya asili, na kwa wengine ni katika ndoa yao. Lakini kilicho tofauti nayo ni kwamba leo sisi, kundi hili la watu, tunateseka kwa ajili ya neno la Mungu. Yaani, kama mtu anayemtumikia Mungu, amekutana na vipingamizi katika njia ya kuamini katika Yeye, na hii ni njia ambayo waumini wote hufuata na ni njia iliyo chini ya miguu yetu yote.
Ijumaa, 9 Machi 2018
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kuhusu Desturi ya Sala
Kuhusu Desturi ya Sala |
Nyinyi hamtilii maanani sala katika maisha yenu ya kila siku. Watu daima wamepuuza sala. Katika sala zao hapo awali walikuwa wakifanya tu mambo kwa namna isiyo ya dhati na kufanya mchezo tu, na hakuna mtu aliyeupeana moyo wake kwa ukamilifu mbele ya Mungu na kumwomba Mungu kweli. Watu humwomba Mungu tu wakati kitu kinawatendekea. Katika wakati huu wote, umewahi kweli kumwomba Mungu? Je, umewahi kutoa machozi ya uchungu mbele ya Mungu? Je, umewahi kujijua mwenyewe mbele ya Mungu?
Ukweli Wafichuliwa Kuhusu Kesi ya Zhaoyuan ya Mei 28 – CCP Ilikuwa Mwelekezi wa Siri wa Tendo Zima
Katika mwaka wa 2014, CCP ilibuni bila msingi maalum Tukio la Zhaoyuan lenye sifa mbaya la mnamo 5/28 katika jimbo la Shandong ili kutunga msingi wa maoni ya umma kwa ajili ya ukomeshaji kamili wa makanisa ya nyumba, na ikaeneza uwongo duniani kulaani na kuliharibia jina Kanisa la Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, baadhi ya washiriki wasiokusudiwa ambao hawakujua ukweli walidanganywa na propaganda za CCP.
Alhamisi, 8 Machi 2018
“Utamu katika Shida” - Ukweli wa Sera ya CCP juu ya Dini Iliyofunikwa na Katiba Yake | clip 6/6
Katiba ya serikali ya Kikomunisti ya Kichina hutamka dhahiri juu ya uhuru wa dini na ibada, lakini kwa siri kuna ukandamizaji wa jeuri na mashambulizi kwa dini na ibada. Wafuasi wa Kristo wanasingiziwa kuwa wahalifu wakubwa wa kitaifa na mbinu za mapinduzi zinachukuliwa ili kuwakandamiza, kuwazuilia, kuwatesa na hata kuwaua kwa ukatili. Serikali ya kikomunisti ya Kichina hutumia Katiba ili kupata umaarufu kwa kuudanganya umma lakini ni siri gani hata hivyo ambazo huathiri mambo na ambazo kufichiwa umma? Kwa nini serikali ya Kikomunisti ya Kichina husisitiza kuwachukulia wafuasi wa Kristo kama maadui, kwa nini hawawezi kupatana na wafuasi wa Kristo?
"Utamu katika Shida" (V): Kwa nini Chama cha Kikomunisti cha China Kilibuni Tukio la 5/28 la Zhaoyuan?
Baada ya kesi ya hadharani ya Tukio la Shandong Zhaoyuan, watu wenye utambuzi wote walitambua kuwa kesi hii ilibuniwa kabisa na Chama cha Kikomunisti cha China ili kulisingizia na kuliaibisha Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa makusudi. Ilikuwa kesi ya kuundwa na utumiaji vibaya wa haki. Sababu ya nia mbaya ya Chama cha Kikomunisti cha China kufanya hivi ni nini?
Jumatano, 7 Machi 2018
"Utamu katika Shida" (IV): Kwa nini Chama cha Kikomunisti cha China Huwalazimisha Wakristo Kujiunga na Kanisa la Utatu Binafsi?
Nchini China, makanisa ya nyumbani yameteseka moja kwa moja matokeo ya ukandamizaji na utesaji wenye wayowayo wa serikali kanamungu ya Kikomunisti ya China. Wanawalazimisha kuingia katika Kanisa la Utatu Binafsi ambalo linadhibitiwa na Idara ya Kazi ya Muungano. Chama cha Kikomunisti cha China kinaficha siri gani kwa kufanya hili? Wakristo wanakabili hatari ya kufungwa jela na hata kupoteza maisha yao ili kueneza injili na kuwa na ushuhuda kwa Mungu. Ni kwa nini hasa wanafanya hili?
"Utamu katika Shida" (III): Mjadala Kati ya Njia Mbili za Maisha na Kifo
Chama cha Kikomunisti cha China kinakandamiza kwa hasira na kushambulia imani ya kidini. Wanawafunga jela na kuwatesa kikatili Wakristo bila kujizuilia. Wanawaruhusu watu tu kufuata Chama cha Kikomunisti. Hawawaruhusu watu kumwamini Mungu na kumfuata Mungu wanapotembea njia sahihi ya maisha. Matokeo ya mwisho ya Chama cha Kikomunisti cha China yatakuwa nini? Chini ya ukandamizaji, ukamataji na utesaji wa hasira wa Chama cha Kikomunisti cha China, Wakristo kwa thabiti wanaendelea kumfuata Mungu, wakieneza injili na kuwa na ushuhuda kwa Mungu.
Jumanne, 6 Machi 2018
"Utamu katika Shida" (II): Kwa Nini Chama cha Kikomunisti cha China Kwa Hasira Kinakandamiza na Kutesa Imani ya Kidini?
Chama cha Kikomunisti cha China wakati huu wote kimewakandamiza kwa hasira, kuwashambulia na kupiga marufuku imani za kidini. Wanawachukulia Wakristo kama wahalifu wakuu wa taifa. Hawasiti kutumia njia za mapinduzi kukandamiza, kukamata, kutesa na hata kuwachinja. Sababu zao za kufanya mambo haya ni nini? Wale wanaoamini katika Mungu wanamheshimu Mungu kama mkuu. Wanamcha Mungu na wanalenga kutafuta ukweli na kutembea njia sahihi ya maisha. Kwa nini Chama cha Kikomunisti cha China kiwachukulie Wakristo kama maadui?
Mbinu ya Chama cha Kikomunisti cha China ya Kuwashurutisha Wakristo kwa Kutishia Familia Zao
Ili kuwashurutisha Wakristo kulighilibu kanisa, wamsaliti Mungu na kuharibu nafasi zao za kuokolewa na Mungu, Chama cha Kikomunisti cha China kwa ufidhuli kinawatishia wanafamilia wa Wakristo na kutumia hisia za familia za Wakristo kuwashurutisha kumsaliti Mungu. Je, njama za Chama cha Kikomunisti cha China zinaweza kuendelea? Katika mapambano haya kati ya mema na mabaya, Wakristo watawezaje kumtegemea Mungu ili kushinda majaribu ya Shetani na kusimama imara na kuwa na ushuhuda kwa Mungu?
Jumatatu, 5 Machi 2018
"Ivunje Laana" (6) - Je, Utiifu kwa Wachungaji na Wazee wa Kanisa ni Sawa na Kumtii Mungu?
Waumini wengine huamini kwamba wachungaji na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa kidini wamechaguliwa na kuteuliwa na Bwana, na kwamba wote ni watu wanaomtumikia Bwana. Hivyo wanaamini kwamba kuwatii tu wachungaji na wazee wa kanisa ni kumtii Bwana, na kwamba kuwaasi au kuwahukumu wachungaji na wazee wa kanisa ni kumpinga Bwana. Wao huamini hata kuwa, katika makanisa, wachungaji na wazee wa kanisa peke ndio huelewa Biblia na huweza kuelezea Biblia, na almradi kile kinachohubiriwa au kufanywa na wachungaji na wazee wa kanisa kinakubaliana na Biblia na kina msingi katika Biblia, basi watu wanapaswa kuwatii na kuwafuata.
"Ivunje Laana" (5) - Je, Wachungaji na Wazee wa Kanisa wa Ulimwengu wa Dini Wanateuliwa na Bwana Kweli?
Mungu mwenyewe hutoa ushuhuda kwa kila mtu Anayemteua na kumtumia. Angalau, wote hupokea uthibitisho wa kazi ya Roho Mtakatifu, huonyesha matunda ya kazi ya Roho Mtakatifu, na wanaweza kuwasaidia watu wa Mungu waliochaguliwa kupokea utoaji wa maisha na uchungaji wa kweli. Kwa sababu Mungu ni mwenye haki na mtakatifu, kila mtu Anayemteua na kumtumia lazima alingane na mapenzi ya Mungu. Wachungaji na wazee wa kanisa katika kutoka ulimwengu wa kidini hawana neno la Mungu kama ushuhuda, na pia hawana uthibitisho wa kazi ya Roho Mtakatifu.
Jumapili, 4 Machi 2018
Swahili Gospel Movie | “Ivunje Laana” Movie Clip: Je, Imani katika Biblia ni Sawa na Imani katika Bwana?
Wachungaji wengi sana na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa kidini huamini kwamba Biblia inamwakilisha Bwana, na kwamba kuamini katika Bwana ni kuamini katika Biblia, na kuamini katika Biblia ni kuamini katika Bwana. Wao huamini kwamba mtu akiachana na Biblia basi hawezi kuitwa muumini, na kwamba mtu anaweza kuokolewa na anaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni almradi ashikilie Biblia. Je, Bibilia inaweza kweli kumwakilisha Bwana? Je, uhusiano kati ya Biblia na Bwana ni upi hasa?
"Ivunje Laana" (3) - Je, Neno la Mungu Lipo Isipokuwa Biblia?
Baadhi ya watu wa kidini huamini kuwa maneno na kazi zote za Mungu ziko katika Biblia, na kwamba hakuna maneno na kazi ya Mungu isipokuwa yale yaliyo katika Biblia. Je, aina hii ya mtazamo inaafikiana na ukweli? Biblia inasema, "Na kuna mambo mengi pia aliyoyafanya Yesu, ambayo, kama yakiandikwa kila moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa." (Yohana 21:25)." Mwenyezi Mungu alisema, “Kile Mungu alicho na anacho milele hakiishi wala hakina mipaka. Mungu ni chanzo cha uhai na vitu vyote.
Jumamosi, 3 Machi 2018
"Ivunje Laana" (2) - Bwana Atakaporudi, Ataonekanaje kwa Wanadamu?
Siku za mwisho tayari zimefika, na waumini wengi wanatamani Bwana arudi na kuwachukua kwenda katika ufalme wa mbinguni. Lakini unajua Bwana atakavyoonekana kwetu Atakaporudi? Je, kweli itakuwa kama tunavyofikiria, kwamba Ataonekana wazi, moja kwa moja Akishuka juu ya wingu? Mwenyezi Mungu alisema, "Je, ungependa kumwona Yesu? Je, ungependa kuishi na Yesu? Je, ungependa kusikia maneno yaliyonenwa na Yesu?… Yesu Atarejea kwa namna gani? Mnaamini kuwa Yesu Atarudi juu ya wingu jeupe, lakini Nawauliza: wingu hili jeupe linaashiria nini?
"Ivunje Laana" (1) - Tunawezaje Kukaribisha Kurudi kwa Bwana?
Miezi minne ya damu tayari imeonekana. Hii ina maana kwamba majanga makubwa yatakuja hivi karibuni, kama ilivyotabiriwa katika kitabu cha Yoeli, “Na pia juu ya watumishi wanaume kwa wanawake katika siku zile, nitamimina roho yangu. Na nitaonyesha maajabu mbinguni na duniani, damu, na moto, na miimo ya moshi. Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja kwa siku kuu na ya kutisha ya BWANA” (Yoeli 2:29-31). Kabla ya maafa makubwa kutufika, roho wa Mungu atawastawisha watumishi na wajakazi Wake, na Yeye atafanya kamili kundi la washindi.
Ijumaa, 2 Machi 2018
"Ndoto Yangu ya Ufalme wa Kibinguni" (5) - Ushuhuda wa Kupitia Hukumu Mbele ya Kiti cha Kristo na Kupokea Uzima
Mwenyezi Mungu ameanzisha kazi ya hukumu akianza na nyumba ya Mungu kwa kuonyesha ukweli. Utangulizi wa hukumu kabla ya ufalme mkuu mweupe kuanza. Tunapitia hukumu ya Mungu na kuadibiwa na Mungu vipi? Je, ni aina gani ya utakaso na mabadiliko yanaweza kupatikana baada ya kupitia hukumu na adabu ya Mungu? Ni maarifa gani ya kweli ya Mungu yanaweza kuarifiwa?
"Ndoto Yangu ya Ufalme wa Kibinguni" (4): Ni nini Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu ya Hukumu katika Siku za Mwisho na Kazi ya Bwana Yesu?
Baadhi ya watu huamini kwamba baada ya Bwana Yesu kufufuka na kupaa mbinguni, Roho Mtakatifu alishuka kufanya kazi kwa mtu katika siku ya Pentekoste. Yeye aliishutumu dunia ya dhambi, na ya haki, na ya hukumu. Tunapopokea kazi ya Roho Mtakatifu na kutubu kwa Bwana kwa ajili ya dhambi zetu, tunapitia hukumu ya Bwana. Kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu katika siku ya Pentekoste inapaswa kuwa kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho. Je, tu sahihi katika njia tunayoipokea? Je, kuna tofauti gani kati ya kazi ya Bwana Yesu na kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho?
Alhamisi, 1 Machi 2018
"Ndoto Yangu ya Ufalme wa Kibinguni" (3) - Ufalme wa Mbinguni u Wapi Hasa?
Matamanio yetu makuu sisi tunaoamini katika Bwana ni kukaribisha kurudi kwa Bwana, kuletwa katika ufalme wa mbinguni, na kupokea ahadi na baraka za Mungu. Watu wengi wanaamini kwamba Bwana atakaporudi, tutainuliwa hewani kukutana na Bwana. Lakini katika Biblia, inasemekana kwamba Yerusalemu mpya itashuka kutoka mbinguni. "maskani ya Mungu yako pamoja na wanadamu," "falme za dunia zimekuwa falme za Bwana wetu, na za Kristo wake." Je, ufalme wa mbinguni uko angani au duniani? Bwana atawapelekaje watakatifu katika ufalme wa mbinguni atakaporudi?
"Ndoto Yangu ya Ufalme wa Kibinguni" (2) - Jinsi ya Kufuatilia Ili Kuingia katika Ufalme wa Mbinguni (2)
Waumini wengi wa Bwana wanahisi kwamba almradi tukiyafuata maneno ya Bwana, tukitenda unyenyekevu na uvumilivu, na kufuata mfano wa Paulo kwa kujitolea, kutumia rasilmali na kufanya kazi kwa ajili ya Bwana, tutayaridhisha mapenzi ya Mungu. Na tutaletwa katika ufalme wa mbinguni Bwana atakaporudi. Hata hivyo, je, tumewahi kufikiria iwapo jitihada kama hizi kweli zitastahili sifa za Bwana na ruhusa ya kuingia katika ufalme wa mbinguni? Kama sivyo, tunapaswa kufuatilia kupata sifa ya Bwana na kuletwa katika ufalme wa mbinguni vipi?
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)