Smiley face
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo neno-la-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo neno-la-Mungu. Onyesha machapisho yote

Jumanne, 15 Oktoba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Kunayo mambo mengi ambayo Ninatumai mtaweza kufikia. Hata hivyo, matendo yenu na maisha yenu yote hayawezi kutimiza kwa ujumla mahitaji Yangu, kwa hiyo lazima Nilenge suala moja kwa moja na kuwafafanulia moyo na akili Zangu. Tukichukulia kwamba uwezo wenu wa utambuzi na ufahamu wenu vyote ni duni sana, karibu mmekosa kabisa kujua tabia na dutu Yangu, na hivyo ni suala la dharura kwangu Mimi kuwafahamisha kuhusu haya. Haijalishi hapo awali ulielewa kiwango kipi au kama uko radhi kuelewa masuala haya, lazima bado Niyaelezee kwenu kwa undani.

Jumapili, 13 Oktoba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Wewe U Mwaminifu kwa Nani?

kazi ya Mungu,Sauti ya Mungu,kumjua Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Wewe U Mwaminifu kwa Nani?

Kila siku mnayoiishi sasa ni ya maana sana na muhimu sana kwa hatima yenu na majaliwa yenu, kwa hivyo mnapaswa kufurahia kila mlicho nacho na kila dakika inayopita. Mnapaswa kutumia muda wenu vizuri ili muweze kujinufaisha, ili msije kuishi maisha haya bure. Pengine mnajihisi kukanganyikiwa mnaojiuliza ni kwa nini Ninazungumza maneno haya. Kwa kweli, Sijapendezwa na matendo ya yeyote kati yenu. Kwa maana matumaini ambayo Nimekuwa nayo juu yenu si vile tu mlivyo sasa. Kwa hivyo, Naweza kuelezea hivi: Nyinyi nyote mko hatarini kabisa. Vilio vyenu vya kwanza kwa ajili ya wokovu na matamanio yako ya kwanza ya kufuatilia ukweli na kutafuta nuru vinakaribia mwisho.

Jumamosi, 12 Oktoba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako

Kazi ya Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako

Nimefanya kazi nyingi miongoni mwenu na, ni wazi kwamba, Nimezungumza vizuri pia. Hata hivyo, Nahisi kwamba maneno na kazi Yangu havijatimiza lengo la kazi Yangu ya siku za mwisho. Maana, katika siku za mwisho, kazi Yangu si kwa ajili ya mtu au watu fulani bali ni kwa manufaa ya kufafanua tabia Yangu asilia. Hata hivyo, kutokana na sababu nyingi—pengine ukosefu wa muda au shughuli nyingi za kazi—tabia Yangu haijamwezesha binadamu kunijua hata kidogo.

Ijumaa, 11 Oktoba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Kazi ya Mungu,neno la Mungu,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Njia ya maisha si kitu ambacho kinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, wala hakipatikani kwa urahisi na wote. Hiyo ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote.

Jumatano, 9 Oktoba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi.

Jumatatu, 7 Oktoba 2019

Neno la Mwenyezi Mungu|Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?

Kazi ya Mungu,Neno la Mungu,Mwenyezi Mungu

Neno la Mwenyezi Mungu|Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?

Huenda ikawa safari yako ya imani katika Mungu imekuwa ndefu zaidi ya mwaka mmoja au miwili, na labda kwa maisha yako umestahimili ugumu mwingi miaka hii yote; au labda haujapitia ugumu na badala yake umepokea neema nyingi. Kuna uwezekano pia kuwa hujapitia ugumu wala kupokea neema, na badala yake umeishi maisha ya kawaida tu. Hiyo haijalishi, kwani wewe bado u mfuasi wa Mungu, kwa hivyo tushikiriane kuhusu mada ya kumfuata Mungu. Lakini, lazima Niwakumbushe wote wanaoyasoma maneno haya kwamba neno la Mungu huelekezwa kwa wale wanaomtambua na wale wanaomfuata Mungu, na sio kwa watu wote wa ulimwengu, wakiwemo wale wasiomtambua Mungu.

Jumapili, 6 Oktoba 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo


Neno la Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

Nimefanya kazi kubwa miongoni mwa binadamu, na maneno ambayo Nimeeleza wakati huu yamekuwa mengi. Maneno haya ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, na yalikuwa yanaeleza ili binadamu aweze kulingana na Mimi. Ilhali Nimewapokea watu wachache tu duniani ambao wanalingana na Mimi, na hivyo Nimesema kwamba binadamu hathamini maneno Yangu, kwa kuwa binadamu halingani na Mimi. Kwa njia hii, kazi ambayo Naifanya sio tu kwa ajili ya mwanadamu aweze kuniabudu; muhimu zaidi, ni kwa ajili ya mwanadamu aweze kulingana na Mimi.

Jumamosi, 5 Oktoba 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa

Kazi ya Mungu,Sauti ya Mungu,Umeme wa Mashariki

Neno la Mwenyezi Mungu | Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa

    Nimewatafuta wengi duniani wawe wafuasi Wangu. Kati yao ni wale wanaohudumu kama makuhani, wanaoongoza, wanaojumuisha wana, wanaojumuisha watu, na wale wanaotoa huduma. Ninawagawa katika makundi haya tofauti kwa msingi wa uaminifu wanaonionyesha. Wakati wanadamu wote wameainishwa kulingana na aina, yaani, asili ya kila aina ya mwanadamu inapowekwa wazi, basi Nitamhesabu kila mwanadamu miongoni mwa aina yake kamili na kuweka kila aina katika nafasi yake kamili ili Nikamilishe lengo Langu la ukombozi wa mwanadamu.

Ijumaa, 4 Oktoba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu


Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu

Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na wote hutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu. Kabla ya nyinyi kumwona Yesu, yaani, kabla ya nyinyi kumwona Mungu Aliye kwenye mwili, mnaweza kuwa na mawazo mengi, kwa mfano, kuhusu sura ya Yesu, njia Yake ya kuzungumza, njia Yake ya maisha, na kadhalika. Hata hivyo, wakati mmemwona hasa, mawazo yenu yatabadilika haraka. Ni kwa nini? Je, mnataka kujua? Hata ingawa fikira za mwanadamu hakika haziwezi kupuuzwa, haikubaliki hata zaidi kwa mwanadamu kubadilisha kiini cha Kristo.

Alhamisi, 3 Oktoba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Pili)

kazi ya Mungu,Neno la Mungu,ukweli

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Pili)

Punde tu Shetani anaposhindwa, hivyo ni kusema, punde tu mwanadamu anaposhindwa kabisa, mwanadamu ataelewa kwamba kazi yake yote ni kwa ajili ya wokovu, na kuwa mbinu ya wokovu huu ni kurejesha kutoka kwa mikono ya Shetani. Miaka 6,000 ya kazi ya Mungu ya usimamizi imegawanywa katika awamu tatu: Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Awamu hizi zote tatu za kazi ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, ambayo ni kusema, ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu ambaye ameharibiwa na Shetani kwa kiasi kikubwa. Wakati huo huo, hata hivyo, pia ni ili kwamba Mungu afanye vita na Shetani.

Jumatatu, 30 Septemba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni

Kupata Mwili,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni

    Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu. Kwa hivyo, chemichemi Yake ni ile ya Mungu Mwenyewe; Dutu hii haitapinga kazi Yake Mwenyewe, na Yeye hangeweza kufanya kitu chochote kinachoharibu kazi Yake Mwenyewe, wala milele Yeye kutamka maneno yoyote ambayo yanakwenda kinyume na mapenzi Yake Mwenyewe.

Jumamosi, 28 Septemba 2019

Matamshi ya Kristo|Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza)

Kazi ya Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu haitengani na mwanadamu, kwa kuwa mwanadamu ni chombo cha kazi hii na kiumbe wa pekee aliyeumbwa na Mungu anayeweza kutoa ushuhuda kwa Mungu. Maisha ya mwanadamu na shughuli zake zote havitengani na Mungu, na vyote vinaongozwa na mkono wa Mungu, na inaweza kusemwa kuwa hakuna mtu anayeweza kuishi bila Mungu. Hakuna anayeweza kupinga hili, kwani ndio ukweli. Kila Akifanyacho Mungu ni kwa faida ya mwanadamu, na kinalenga hila za Shetani. Kila anachokihitaji mwanadamu kinatoka kwa Mungu, na Mungu ndiye chanzo cha maisha ya mwanadamu.

Ijumaa, 27 Septemba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Kupata Mwili,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Mungu mwenye mwili wa kwanza Aliishi duniani kwa miaka thelathini na tatu na nusu, lakini Alitekeleza huduma Yake kwa miaka mitatu na nusu pekee ya hiyo miaka yote. Kipindi Alichofanya kazi na kabla Aanze kazi Yake, Alikuwa na ubinadamu wa kawaida. Aliishi na ubinadamu Wake wa kawaida kwa miaka thelathini na tatu na nusu. Katika miaka yote mitatu na nusu ya mwisho Alijifichua kuwa Mungu mwenye mwili. Kabla Aanze kutekeleza kazi ya huduma Yake, Alikuwa na ubinadamu wa kawaida, bila kuonyesha ishara ya uungu Wake, na ni baada tu ya kuanza rasmi kutekeleza huduma Yake ndipo uungu Wake uliwekwa wazi.

Alhamisi, 26 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu | Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Pili)

Kazi Yake katika mwili ni ya umuhimu mkubwa, ambao umezungumzwa kuhusiana na kazi, na Yule ambaye hatimaye anahitimisha kazi ni Mungu mwenye mwili, na sio Roho. Baadhi ya watu wanaamini kwamba Mungu wakati fulani anaweza kuja duniani na kumtokea mwanadamu, ambapo atawahukumu wanadamu wote, akimjaribu mmoja baada ya mwingine bila mtu yeyote kupitwa. Wale wanaofikiri kwa namna hii hawafahamu hatua hii ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Mungu hamhukumu mwanadamu mmoja baada ya mwingine, na hamjaribu mwanadamu mmoja baada ya mwingine; kufanya hivyo sio kazi ya hukumu.

Jumatatu, 23 Septemba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Pili)


Kazi ya mwanadamu ina mipaka na kadiri inavyoweza kufika. Mtu mmoja anaweza kufanya kazi ya wakati fulani na hawezi kufanya kazi ya enzi nzima—vinginevyo anaweza kuwaongoza watu katika kanuni. Kazi ya mwanadamu inaweza kufaa tu katika kipindi au awamu fulani. Hii ni kwa sababu uzoefu wa mwanadamu una mipaka. Mtu hawezi kulinganisha kazi ya mwanadamu na kazi ya Mungu. Namna mwanadamu anavyofanya mambo na maarifa yake ya ukweli yote yanatumika tu katika mawanda fulani. Huwezi kusema kwamba njia ambayo mwanadamu anaiendea ni matakwa ya Roho Mtakatifu kabisa, kwa sababu mwanadamu anaweza kupewa nuru na Roho Mtakatifu tu na hawezi kujazwa kikamilifu na Roho Mtakatifu.

Jumamosi, 21 Septemba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza)

Kupata Mwili,Yesu Kristo,Kanisa la Mwenyezi Mungu

Ni kiasi gani cha kazi ya mwanadamu ni kazi ya Roho Mtakatifu na uzoefu wa mwanadamu ni kiasi gani? Hata sasa, tunaweza kusema kuwa watu bado hawayaelewi maswali haya, ambayo yote ni kwa sababu watu hawaelewi kanuni za utendaji kazi wa Roho Mtakatifu. Kazi ya mwanadamu Ninayoizungumzia, kimsingi, ni kwa kurejelea kazi za wale ambao wana kazi ya Roho Mtakatifu au wale ambao wanatumiwa na Roho Mtakatifu. Sizungumzii kazi ambayo inatokana na matakwa ya mwanadamu bali kazi ya mitume, watendaji kazi au kaka na dada wa kawaida waliopo katika mawanda ya kazi ya Roho Mtakatifu. Hapa, kazi ya mwanadamu hairejelei kazi ya Mungu mwenye mwili bali mawanda na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu kwa watu.

Alhamisi, 19 Septemba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Hatua moja ya kazi ya enzi mbili za awali ilifanyika Israeli; nyingine ilifanyika Uyahudi. Kuzungumza kwa jumla, hakuna hatua ya kazi hii iliyotoka Israeli; zilikuwa ni hatua za kazi zilizofanywa miongoni mwa wateule wa mwanzo. Hivyo, kwa mtazamo wa Wanaisraeli, Yehova Mungu ni Mungu wa Wanaisraeli pekee. Kwa sababu ya kazi ya Yesu huko Uyahudi, na kwa sababu ya kukamilisha Kwake kwa kazi ya kusulubiwa, kwa mtazamo wa Wayahudi, Yesu ni Mkombozi wa watu wa Kiyahudi. Yeye ni Mfalme wa Wayahudi pekee, sio wa watu wengine wowote; Yeye si Bwana anayewakomboa Waingereza, wala Bwana anayewakomboa Wamarekani, lakini Yeye ni Bwana anayewakomboa Wanaisraeli, na katika Israeli ni Wayahudi ndio Anaowakomboa. Kwa kweli, Mungu ni Bwana wa mambo yote.

Alhamisi, 12 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu: Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo (Sehemu ya Pili)


Kwanza Mungu alimwumba Adamu na Hawa, na pia Alimwumba nyoka. Miongoni mwa mambo haya yote, nyoka ndiye aliyekuwa mwenye sumu zaidi; mwili wake ulikuwa na sumu, na Shetani aliitumia sumu hiyo ili kufaidika. Ni nyoka aliyemjaribu Hawa hadi akatenda dhambi. Adamu alitenda dhambi baada ya Hawa kutenda, na wawili hawa waliweza kutofautisha kati ya mema na maovu. Kama Yehova Alikuwa Amejua kwamba nyoka angemjaribu Hawa, na kwamba Hawa angemjaribu Adamu, kwa nini Akawaweka wote pale katika bustani? Kama Aliweza kutabiri mambo haya kwa nini Akamwumba nyoka na kumweka ndani ya Bustani ya Edeni? Kwa nini Bustani ya Edeni ilikuwa na tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya? Alinuia wao walile hilo tunda? Wakati Yehova alipokuja, Adamu wala Hawa hawakuthubutu kumkabili Yeye, na ulikuwa tu wakati huu ambapo Yehova alijua kwamba walikuwa wamelila tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya na kujipata katika ujanja wa yule nyoka.

Jumatano, 11 Septemba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Majina na Utambulisho (Sehemu ya Kwanza)

Yesu Kristo,Kupata Mwili,Kanisa la Mwenyezi Mungu

Iwapo unataka kufaa kwa ajili ya matumizi na Mungu, lazima uijue kazi ya Mungu; lazima uijue kazi Aliyofanya awali (katika Agano Jipya na la Kale), na, zaidi ya hayo, lazima uijue kazi Yake ya leo. Ndiyo kusema, ni lazima uzitambue hatua tatu za kazi ya Mungu ya zaidi ya miaka 6,000. Ukiulizwa ueneze injili, basi hutaweza kufanya hivyo bila kuijua kazi ya Mungu. Watu watakuuliza yote kuhusu Biblia, na Agano la Kale, na nini Yesu alisema na kufanya wakati huo. Watasema, "Mungu wenu hajawaeleza haya yote? Kama Yeye (Mungu) hawezi kuwaeleza ni nini hasa yanayoendelea kwa Biblia, basi Yeye si Mungu; kama Anaweza, basi tumeamini." Mwanzoni, Yesu alizungumzia sana Agano la Kale na wanafunzi Wake. 

Jumapili, 8 Septemba 2019

Sauti ya Mungu | Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sauti ya Mungu | Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia

Watu wote wanahitaji kuelewa kusudio la kazi Yangu ulimwenguni, yaani, lengo la mwisho la kazi Yangu na ni kiwango kipi ambacho lazima Nitimize katika kazi hii kabla inaweza kukamilika. Kama, baada ya kutembea na Mimi hadi leo, watu hawaelewi kazi Yangu inahusu nini, basi hawajakuwa wakitembea na Mimi bure? Watu wanaonifuata Mimi wanafaa kujua mapenzi Yangu. Nimekuwa nikifanya kazi ulimwenguni kwa maelfu ya miaka, na hadi leo ningali nafanya kazi Yangu vivyo hivyo sasa. Ingawa kunavyo vipengele vingi hasa vilivyojumuishwa katika kazi Yangu, kusudio la kazi hii linabakia lilelile.