Mwenyezi Mungu anasema, Ni kitu gani ambacho mwanadamu amepokea tangu alipomwamini Mungu mara ya kwanza? Umejua kitu gani kumhusu Mungu? Umebadilika kiasi gani kwa sababu ya imani yako kwa Mungu? Sasa mnajua nyote ya kwamba imani ya mwanadamu katika Mungu si kwa ajili ya wokovu wa roho na ustawi wa mwili tu, wala si kuimarisha maisha yake kwa njia ya upendo wa Mungu, na kadhalika. Kama ilivyo sasa, kama unampenda Mungu kwa ajili ya ustawi wa mwili au furaha ya muda, basi hata kama, mwishoni, upendo wako kwa Mungu utafikia kilele chake na wewe hutaulizia kitu chochote, upendo huu unaoutafuta ni upendo mchafu na haumpendezi Mungu.
Wale wanaotumia upendo kwa Mungu kusitawisha maisha yao yasiyopendeza na kujaza utupu katika mioyo yao ni wale ambao wanataka kuishi katika raha, si wale ambao kweli wanatafuta kumpenda Mungu. Upendo wa aina hii ni kinyume na matakwa ya mtu, harakati ya ridhaa ya hisia, na Mungu hahitaji upendo wa aina hii. Upendo wako, basi, ni upendo wa aina gani? Ni kwa ajili gani unampenda Mungu? Je, ni kiasi gani cha upendo wa kweli, ulicho nacho kwa Mungu sasa? Upendo wa watu wengi kati yenu ni kama uliotajwa hapo awali. Upendo wa aina hii unaweza tu kudumisha hali kama ilivyo; hauwezi kufikia uthabiti wa milele, wala kuchukua mizizi katika mtu. Aina hii ya upendo ni ule wa ua ambalo halizai matunda baada ya kuchanuka na hatimaye kunyauka. Kwa maneno mengine, baada ya wewe kumpenda Mungu mara moja kwa jinsi hii na hakuna mtu wa kukuongoza kwa njia ya mbele, basi utaanguka. Kama unaweza tu kumpenda Mungu katika nyakati za kumpenda Mungu na kutofanya mabadiliko katika tabia ya maisha yako baadaye, basi utaendelea kufunikwa na ushawishi wa giza, bila uwezo wa kutoroka, na bila uwezo wa kujinasua kwa minyororo ya kutumiwa na kupumbazwa na Shetani. Hakuna mtu kama huyu anayeweza kukubaliwa na Mungu; mwishowe, roho zao, nafsi na mwili bado ni mali ya Shetani. Hili ni bila ya shaka. Wale wote ambao hawawezi kukubaliwa kikamilifu na Mungu watarudi mahali pao pa awali, yaani, kwa Shetani, na watakwenda chini kwa ziwa liwakalo moto wa jahanamu kukubali hatua ya pili ya adhabu kutoka kwa Mungu. Wale wanaokubaliwa na Mungu ni wale ambao wanamkataa shetani na kutoroka kutoka kwa miliki ya Shetani. Watu kama wale watahesabiwa rasmi miongoni mwa watu wa ufalme. Hivi ndivyo watu wa ufalme huja kuwa. Je, uko tayari kuwa mtu wa aina hii? Je, uko tayari kukubaliwa na Mungu? Je, uko tayari kutoroka kutoka miliki ya Shetani na kurudi kwa Mungu? Je, sasa wewe ni mali ya Shetani au umehesabiwa miongoni mwa watu wa ufalme? Mambo hayo lazima yote yawe wazi na hayahitaji maelezo zaidi.
Katika nyakati zilizopita, watu wengi walifuatilia kwa jitihada na fikira za mwanadamu na kwa ajili ya matumaini ya mwanadamu. Mambo haya hayatajadiliwa sasa. La muhimu ni kupata njia ya kutenda ambayo itawezesha kila mmoja wenu kudumisha hali ya kawaida mbele ya Mungu na hatimaye kuvunja pingu za ushawishi wa Shetani, ili mpate kuwa wakubalika wa Mungu, na kuishi kwa kudhihirisha duniani matakwa ya Mungu kwenu. Ni haya tu yanayoweza kutimiza mapenzi ya Mungu. Wengi wanaamini katika Mungu, ila hawajui ni kitu gani Anachotamani Mungu wala ni nini anachotamani Shetani. Wao wanaamini kipumbavu na kuwafuata watu wengine kama vipofu, na kwa hivyo hawajakuwa kamwe na maisha ya kawaida ya Kikristo; hawana uhusiano wa kawaida wa binafsi na watu wengine, sembuse uhusiano wa kawaida ambao mwanadamu anao na Mungu. Kutoka kwa hili inaweza kuonekana kwamba matatizo na makosa ya mtu, na mambo mengine ambayo yanaweza kuzuia mapenzi ya Mungu ni mengi. Hili linatosha kuthibitisha kwamba mwanadamu hajajiandaa kikamilifu kufuata njia iliyo sahihi wala kuwa na uzoefu wa maisha halisi. Kujiandaa kufuata njia iliyo sahihi ni nini? Kujiandaa kufuata njia iliyo sahihi ina maana kwamba unaweza kunyamazisha moyo wako mbele za Mungu wakati wote na wasiliana kwa karibu na Mungu, hatua kwa hatua ukipata kujua ni nini kinachokosa ndani ya mwanadamu na polepole kupata kumfahamu Mungu zaidi. Kwa njia hii, utakuwa kila siku utapata maono mapya na kupata nuru kiroho; hamu yako inakua, na wewe kutafuta kuingia katika ukweli. Kila siku kuna mwanga mpya na ufahamu mpya. Kupitia njia hii, wewe hatua kwa hatua unavunja ushawishi wa Shetani na kuwa huru, na maisha yako yanakua kwa kiasi kikubwa. Mtu kama huyu ameweka mikakati ya kufuata mwenendo sawa. Tathmini uzoefu wako mwenyewe halisi na kuchunguza njia uliyoichukua katika imani yako kwa Mungu dhidi ya yaliyotajwa hapo juu. Wewe ni yule ambaye amepangwa kufuata mwenendo sawa? Ni katika masuala gani ambapo umejiweka huru kutokana na pingu za shetani na kutokana na ushawishi wa Shetani? Kama bado hujajiandaa kufuata njia iliyo sahihi, uhusiano wako na Shetani bado haujaisha. Kwa jinsi hiyo, ukimbiziaji huu wa upendo kwa Mungu inaweza kusababisha upendo ambao ni sahihi, wa kujitolea, na safi? Unasema kwamba upendo wako kwa Mungu ni wa dhati na imara, bali hujajinasua kutoka kwa pingu za Shetani. Je, wewe si unajaribu kumpumbaza Mungu? Ukitaka kuufikia upendo safi kwa Mungu, kuwa wa Mungu kikamilifu, na kuwa mhesabiwa miongoni mwa watu wa ufalme, basi lazima kwanza ujiandae kufuata njia iliyo sahihi.
Kujua zaidi: Dhana na Fikira Hazitawahi Kukusaidia Kumjua Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni