Mungu Anajibidiisha kumfanya binadamu kuwa kamili. Haijalishi ni mtazamo gani anaoongelea Yeye, yote ni kwa minajili ya kuwafanya watu hawa kuwa watimilifu. Maneno yaliyotamkwa kutoka kwenye mtazamo wa Roho ni magumu kwa binadamu kuelewa, na binadamu hawezi kupata njia ya kufanyia mazoezi, kwani binadamu ana uwezo finyu wa kupokea. Kazi ya Mungu hutimiza athari tofauti, na kila hatua ya kazi hiyo ina kusudio Lake. Aidha, lazima Aongee kutoka mitazamo tofauti ili kumfanya binadamu kuwa mtimilifu. Kama Angetoa sauti Yake kutoka kwenye mtazamo wa Roho pekee, awamu hii ya kazi ya Mungu isingeweza kukamilishwa. Kutokana na mkazo wa sauti Yake, unaweza kuona Anayo bidii ya kufanya kundi hili la watu kamilifu. Kama mmoja anayependa kufanywa kuwa mtimilifu na Mungu, ni hatua gani ya kwanza ambayo lazima uchukue? Lazima kwanza ujue kazi ya Mungu. Huku mbinu mpya zikitumika na enzi ikiwa imebadilika kutoka moja hadi nyingine, mbinu ambazo Mungu hufanyia kazi pia zimebadilika, sawa tu na njia ambazo Mungu huongelea. Sasa, si mbinu tu za kazi Yake zilizobadilika, lakini pia enzi yenyewe. Awali ilikuwa ni Enzi ya Ufalme, awamu ya kazi ambamo ulistahili kumpenda Mungu. Sasa, ni Enzi ya Ufalme wa Milenia—Enzi ya Neno—yaani, enzi ambamo Mungu hutumia njia nyingi za kuongea ili kumfanya binadamu kuwa mtimilifu na Huongea kutoka kwa mitazamo tofauti ili kumruzuku binadamu. Punde tu nyakati zilipopita hadi katika Enzi ya Ufalme wa Milenia, Mungu alianza kutumia neno ili kumfanya binadamu kuwa mtimilifu, kumwezesha binadamu kuingia katika uhalisia wa maisha na kumwongoza binadamu hadi kwenye njia sahihi. Binadamu amepitia hatua nyingi sana za kazi Yake na ameona kwamba kazi ya Mungu haibakii vilevile. Badala yake, inabadilika kila mara na kuwa yenye kina. Baada ya muda mrefu sana wa uzoefu, kazi imegeuka na kubadilika tena na tena, lakini kwa mabadiliko yoyote yale, haijawahi kutoka kwa lengo la Mungu la kumfinyanga binadamu. Hata kupitia mabadiliko elfu kumi, kusudio lake asilia halibadiliki kamwe, na haliondoki kamwe kutoka kwenye ukweli au uzima. Mabadiliko kwenye mbinu ambazo kazi inafanywa ni mabadiliko tu katika mpangilio wa kazi na mtazamo wa kuongea, na wala si badiliko kwenye lengo kuu la kazi Yake. Mabadiliko katika mkazo wa sauti na mbinu za kufanya kazi yanafanywa ili kutimiza athari fulani. Mabadiliko katika mkazo wa sauti hayamaanishi mabadiliko katika kusudio au kanuni ya kazi. Kiini halisi cha binadamu kusadiki Mungu ni kutafuta uzima. Kama unasadiki Mungu lakini hutafuti uzima au ukweli au maarifa ya Mungu, basi hakuna kusadiki Mungu kokote! Je, ni jambo la kihalisia kwamba ungali unatafuta kuingia kwenye ufalme kuwa mfalme? Mafanikio tu ya upendo wa kweli kwa Mungu kupitia kwa utafutaji wa uzima ndilo jambo la kihalisia; ufuatiliaji na utendaji wa ukweli vyote ni vya kihalisia. Pitia maneno ya Mungu wakati ukisoma maneno Yake; kwa njia hii utaweza kung’amua maarifa ya Mungu kupitia kwa uzoefu halisi. Huu ni ufuatiliaji wa kweli.
Kanisa la Mwenyezi Mungu lilikuja kuwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu.
NYUMBANI
Usomaji wa Maneno ya Mwenyezi Mungu
Filamu za Injili
Kwaya za Injili
Maisha ya Kanisa—Mfululizo wa Maonyesho Mbalimbali
Video za Nyimbo na Ngoma
Msururu wa MV za Ufalme
Video za Nyimbo za Dini
Filamu za Maisha ya Kanisa
Filamu za Uzoefu wa Mateso
Kufunua Mfululizo wa Video za Ukweli
Sehemu za Filamu
Aina za Dondoo za Video
Jumanne, 6 Agosti 2019
Matamshi ya Kristo | Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno
Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno ili kukaribisha enzi mpya, ili kubadilisha mbinu za kazi Yake, na kuweza kufanya kazi katika enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo Mungu hufanyia kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili kuweza kuzungumza kutoka mitazamo tofauti, kumwezesha binadamu kumwona Mungu kwa kweli, ambaye ni Neno linaloonekana katika mwili, na hekima Yake na maajabu. Kazi kama hiyo inafanywa ili kwa njia bora zaidi kutimiza shabaha za kumshinda binadamu, kumfanya binadamu kuwa mtimilifu, na kumwondoa binadamu. Hii ndiyo maana ya kweli ya kutumia neno ili kufanya kazi katika Enzi ya Neno. Kupitia kwenye neno, binadamu anajua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, kiini cha binadamu, na kile ambacho binadamu anastahili kuingia ndani yake.
Kupitia neno, kazi yote ambayo Mungu hupenda kufanya katika Enzi ya Neno inatimizwa. Kupitia neno, binadamu anafichuliwa, anaondolewa, na kujaribiwa. Binadamu ameliona neno, amelisikia neno, na akapata habari ya uwepo wa neno. Kutokana na haya, binadamu anaamini katika uwepo wa Mungu; binadamu anaamini katika uwezo na hekima za Mungu, pamoja na moyo wa upendo wa Mungu kwa binadamu na tamanio Lake la kumwokoa binadamu. Ingawa neno “neno” ni rahisi na kawaida, neno kutoka kwenye kinywa cha Mungu kupata mwili hutikisa dunia nzima; neno Lake hubadilisha moyo wa binadamu, fikira na tabia zee za binadamu, na sura nzee ya ulimwengu mzima. Kupitia enzi nyingi, Mungu pekee wa leo ndiye anayefanya kazi katika njia kama hiyo, na ni Yeye tu Anayeongea na kumwokoa binadamu hivyo. Baadaye, binadamu huishi katika mwongozo wa neno, akichungwa na kujazwa na neno; wanaishi katika ulimwengu wa neno, wanaishi katika laana na baraka za neno la Mungu, na hata zaidi kuishi chini ya na hukumu na kuadibu kwa neno. Maneno haya na kazi hii vyote ni kwa minajili ya wokovu wa binadamu, kutimiza mapenzi ya Mungu, kubadilisha sura asilia wa ulimwengu wa uumbaji wa kale. Mungu aliuumba ulimwengu kwa neno, huwaongoza wanadamu kote ulimwenguni kwa neno, hushinda na kuwaokoa binadamu kwa neno. Hatimaye, Yeye atatumia neno ili kuutamatisha ulimwengu mzima wa kale. Ni hapo tu ndipo mpango wa usimamizi unapokuwa mkamilifu kabisa. Katika Enzi nzima ya Ufalme, Mungu hutumia neno kufanya kazi Yake na kutimiza matokeo ya kazi Yake; Hafanyi maajabu au kutenda miujiza; Anafanya tu kazi Yake kupitia kwa neno. Kwa sababu ya neno, binadamu anastawishwa na kuruzukiwa; kwa sababu ya neno, binadamu hupokea maarifa na kupata uzoefu wa kweli. Binadamu katika Enzi ya Neno amepokea kwa kweli baraka za kipekee. Binadamu huwa hapati maumivu ya mwili na hufurahia tu mjazo mengi ya neno la Mungu; hawahitaji tena kutafuta au kushika safari, na kwa utulivu huona kuonekana kwa Mungu, wanamsikiliza Yeye akiongea binafsi, wanapokea ujazo Wake, na kumwona Yeye binafsi akifanya kazi Yake. Binadamu katika enzi zilizopita hakuweza kufurahia mambo kama haya, na hizi ndizo baraka ambazo wasingewahi kupokea.
Katika Enzi ya Ufalme wa Milenia, iwapo umeingia katika enzi hii mpya inaamuliwa na kama umeingia kwenye uhalisia wa maneno ya Mungu na kama maneno Yake yanakuwa uhalisia katika maisha yako. Neno la Mungu linajuzwa kwa wote, ili hatimaye, binadamu wote waweze kuishi katika ulimwengu wa neno na neno la Mungu litawapa nuru na kuangaza kila mtu kotekote. Kama katika kipindi hiki cha muda, una haraka na uzembe katika kusoma neno la Mungu, na huna kivutio katika neno Lake, yaonyesha kwamba kuna jambo baya na hali yako. Kama huwezi kuingia katika Enzi ya Neno, basi Roho Mtakatifu Hafanyi kazi ndani yako; kama umeingia katika enzi hii, Atafanya kazi Yake. Ni nini unachoweza kufanya kwa sasa, mwanzo wa Enzi hii ya Neno, ili kupata kazi ya Roho Mtakatifu? Katika enzi hii, Mungu atafanya jambo la uhalisia miongoni mwenu ili kwamba kila binadamu aweze kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu, aweze kutia ukweli katika matendo, na kumpenda Mungu kwa dhati; kwamba binadamu wote waweze kutumia neno la Mungu kama msingi na uhalisia wao na kuwa na mioyo ya kumcha Mungu; na kwamba, kupitia kwa kutenda neno la Mungu, binadamu basi anaweza kutawala pamoja na Mungu. Hii ndiyo kazi ambayo Mungu atatimiza. Unaweza kuendelea na maisha bila ya kusoma neno la Mungu? Kuna wengi sasa wanaohisi kwamba hawawezi kukaa hata siku moja au mbili bila ya kusoma neno la Mungu. Lazima wasome neno Lake kila siku, na kama muda hauruhusu, kusikiliza neno Lake kunatosha. Hii ndiyo hisia ambayo Roho Mtakatifu anampa binadamu na namna ambavyo Anaanza kumbadilisha binadamu. Yaani, Hutawala binadamu kupitia kwa maneno ili binadamu aweze kuingia katika uhalisia wa neno la Mungu. Kama unahisi giza na kiu baada ya kula na kunywa neno la Mungu, na unapata kwamba hali hiyo haikubaliki, hii inamaanisha kwamba umeguswa na Roho Mtakatifu, na Hajakugeukia. Basi wewe ndiye mmoja aliye katika mkondo huu. Hata hivyo, kama huna utambuzi au huhisi kiu baada ya siku moja au mbili za kukosa kula na kunywa neno la Mungu, na huhisi kwamba umeguswa, hii inaonyesha kwamba Roho Mtakatifu amekugeukia. Hii inamaanisha, basi, kuwa hali iliyo ndani yako si sahihi; bado hujaingia katika Enzi ya Neno, na wewe ni mmoja aliyebaki nyuma. Mungu hutumia neno ili kumtawala binadamu; unahisi vyema kama utakula na kunywa neno la Mungu, na kama huhisi hivyo, hutakuwa na njia yoyote ya kufuata. Neno la Mungu linakuwa chakula cha binadamu na nguvu zinazomwendesha. Biblia inasema kwamba “Mwanadamu hatadumu kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu.” Hii ndiyo kazi ambayo Mungu ataikamilisha leo. Atafanikisha ukweli huu ndani yenu. Ikoje kwamba binadamu katika siku za kale angekaa siku nyingi bila ya kusoma neno la Mungu lakini angeendelea kula na kufanya kazi? Na kwa nini hali sivyo hivi sasa? Katika enzi hii, Mungu hutumia kimsingi neno ili kutawala yote. Kupitia kwa neno la Mungu, binadamu anahukumiwa na kufanywa mtimilifu, kisha hatimaye kupelekwa katika ufalme. Ni neno la Mungu tu linaloweza kuruzuku maisha ya binadamu, na ni neno la Mungu tu ndilo linaloweza kumpa binadamu nuru na njia ya kutenda, hasa katika Enzi ya Ufalme. Mradi tu kila siku unakula na kunywa neno Lake na huachi uhalisia wa neno la Mungu, Mungu ataweza kukufanya mtimilifu.
Mtu hawezi kuwa na haraka kutimiza ufanisi wakati anapotafuta uzima; ukuzi katika maisha haufanyiki tu kwa siku moja au mbili. Kazi ya Mungu ni kawaida na ya matendo, na lazima ipitie mchakato unaohitajika. Ilimchukua Yesu aliyekuwa mwili mchakato wa miaka 33.5 ili kukamilisha kazi Yake ya kusulubishwa, bila kutaja maisha ya binadamu! Si kazi rahisi pia kumuumba binadamu wa kawaida anayemdhihirisha Mungu. Hali hasa iko hivi kwa watu wa taifa la joka kuu jekundu. Ni wa kundi la watu fukara na wanahitaji kipindi kirefu cha neno na kazi ya Mungu. Hivyo basi usiwe na haraka kuyaona matokeo. Lazima ushughulike katika kula na kunywa neno la Mungu, na kutia jitihada katika maneno ya Mungu. Baada ya kuyasoma maneno Yake, lazima uweze kuyatia katika matendo kwa uhalisia, na katika maneno ya Mungu, uweze kupata maarifa, maono, utambuzi, na hekima. Kupitia haya, utabadilika bila kutambua. Kama unaweza kuchukua kama kanuni zako kula na kunywa na neno la Mungu, kulisoma neno Lake, kulijua kwa undani, kulipitia, na kulitia katika matendo, basi utakua bila kutambua. Baadhi husema kwamba hawawezi kulitia neno la Mungu katika matendo hata baada ya kulisoma! Haraka yako ni ya nini? Unapofikia kimo fulani, utaweza kulitia katika matendo neno Lake. Je, mtoto wa umri wa miaka minne au mitano anaweza kusemaje kwamba hawezi kuwapa msaada au kuwaheshimu wazazi wake? Unafaa kujua sasa kimo chako ni kipi, tia katika matendo kile unachoweza, na usiwe kwamba wewe ndiwe unayekatiza usimamizi wa Mungu. Wewe kula na kunywa tu na maneno ya Mungu na tukisonga mbele, chukulia suala hilo kama kanuni yako. Usiwe na wasiwasi bado kuhusu kama Mungu anaweza kukufanya kuwa kamili. Usiingilie jambo hilo kwa sasa. Wewe kula na kunywa tu na maneno ya Mungu punde unapokutana nayo, na unahakikishiwa kwamba Mungu ataweza kukufanya kuwa kamili. Hata hivyo, kuna kanuni ambayo kwayo lazima ukule na kunywa neno Lake. Usifanye hivyo bila mpango. Badala yake, tafuta maneno unayofaa kujua, yaani, yale yanayohusiana na maono. Mwelekeo mwingine ambao lazima utafute ni ule wa matendo halisi, yaani, mwelekeo ule unaohusu kile unachofaa kuingia kwacho. Mwelekeo mmoja ni kuhusu maarifa, na mwingine unahusiana na kuingia. Punde utakapopata mielekeo hii yote, yaani, utakapong'amua kile unachofaa kujua na kutenda, basi utajua namna ya kula na kunywa neno la Mungu.
Tukisonga mbele, kuzungumzia neno la Mungu ni kanuni ambayo unaongelea. Mnapokuja pamoja, mnafaa kushiriki kuhusu neno la Mungu na kulitumia kama mada yenu; zungumzieni kuhusu kile mnachojua kuhusu neno la Mungu, namna mnavyoitia katika vitendo neno Lake, na namna ambavyo Roho Mtakatifu anafanya kazi. Ukishiriki kuhusu neno la Mungu, Roho Mtakatifu atakuangaza. Binadamu pia lazima ashirikiane kama huu utakuwa ndio ulimwengu wa neno la Mungu. Kama hutaingia ndani ya hili, Mungu hawezi kufanya kazi Yake. Kama hutazungumzia neno Lake, Hawezi kukuangaza. Unapopata nafasi, zungumzia neno la Mungu. Usizungumze tu bila mpango! Acha maisha yako yakajazwe na neno la Mungu; kisha utakuwa muumini mwenye kumcha Mungu. Hata kama ushirika wako ni hafifu, hiyo ni sawa. Bila ya hali hiyo ya juujuu, hakuwezi kuwa na kina. Kunao mchakato ambao lazima upitiwe. Kupitia kwa mazoezi yako, unapata utambuzi wa kuangaziwa na Roho Mtakatifu, na namna unavyoweza kula na kunywa neno la Mungu kwa njia bora. Baada ya kipindi cha uchunguzi kama huo, utaingia katika uhalisia wa neno la Mungu. Ni kama tu utakuwa na uamuzi wa kushirikiana ndipo utakapopokea kazi ya Roho Mtakatifu.
Kunayo mielekeo miwili ya kanuni za kula na kunywa neno la Mungu: Mmoja unahusiana na maarifa, na mwingine ni kuingia. Ni maneno yapi unayofaa kujua? Unafaa kujua maneno yanayohusiana na maono (hivyo ni kusema, ni enzi gani Mungu amekwisha ingia ndani yake, ni nini ambacho Mungu Angependa wewe kutimiza sasa, kupata mwili ni nini, na kadhalika. Haya yote yana uhusiano na maono). Ni njia gani ambamo binadamu anafaa kuingia? Hii inarejelea maneno ya Mungu ambayo binadamu anafaa kufanyia mazoezi na kuingia ndani. Hii ndiyo mielekeo miwili ya kula na kunywa neno la Mungu. Kuanzia sasa, kula na unywe neno la Mungu kwa njia hii. Kama unao uelewa kamili wa maneno yanayohusu maono, basi hakuna haja ya kusoma zaidi. Kilicho na umuhimu mkubwa ni kula na kunywa zaidi ya maneno kuhusu kuingia, kama vile kuelekeza moyo wako kwa Mungu, namna ya kutuliza moyo wako mbele ya Mungu, na namna ya kunyima mwili. Haya ndiyo unayofaa kufanyia mazoezi. Bila ya kujua namna ya kula na kunywa neno la Mungu, ushirika wa kweli hauwezekani. Punde utakapojua namna ya kula na kunywa neno Lake, na umeng'amua kilicho muhimu, ushirika utakuwa huru. Masuala yawayo yote yaulizwapo, unaweza kushiriki kuyahusu na kung'amua uhalisia. Kushiriki kuhusu neno la Mungu bila ya uhalisia kunamaanisha huwezi kung'amua kilicho muhimu, na hii inamaanisha kwamba hujui kula na kunywa neno Lake. Wengine huhisi uchovu wakati wanaposoma neno la Mungu. Hali kama hiyo si kawaida. Kwa hakika, kilicho kawaida ni kutochoka wakati unasoma neno la Mungu, siku zote kuwa na kiu ya neno la Mungu, na kila wakati kufikiria kuwa neno la Mungu ni zuri. Hivi ndivyo mtu ambaye kweli ameingia anakula na kunywa neno la Mungu. Unapohisi kwamba neno la Mungu ni la kimatendo kweli na ndilo hasa lile binadamu anafaa kuingia ndani; unapohisi kwamba neno Lake ni lenye manufaa na faida kubwa kwa binadamu, na huo ndio ujazo wa uzima wa binadamu, unapokea hisia hii kutoka kwa Roho Mtakatifu, kupitia kwa wewe kuguswa na Roho Mtakatifu. Hii inathibitisha kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yako na kwamba Mungu hajakugeukia. Kuona kwamba Mungu siku zote anaongea, baadhi huwa na uchovu wa maneno Yake na kufikiria kwamba hakuna tofauti yoyote kama watasoma maneno Yake au hawatasoma. Hiyo si hali ya kawaida. Mioyo yao haina kiu ya kuingia katika uhalisi, na binadamu kama hao hawana kiu ya kufanywa watimilifu wala kutilia umuhimu kwa kufanywa watimilifu. Kila unapopata huna kiu ya neno la Mungu, yaonyesha kwamba hali yako si ya kawaida. Siku za kale, kama Mungu alikugeukia au la iliamuliwa na kama wewe ulikuwa na amani ndani yako na ulipitia furaha. Sasa kilicho muhimu ni kama una kiu ya neno la Mungu, kama neno Lake ndio uhalisi wako, kama wewe ni mwaminifu, kama unaweza kufanya kile unachoweza kwa ajili ya Mungu. Kwa maneno mengine, binadamu huhukumiwa na uhalisia wa neno la Mungu. Mungu huelekeza neno Lake kwa watu wote. Kama uko radhi kulisoma, Atakupa nuru, lakini kama huko radhi, Hatakupa nuru. Mungu hupa nuru wale walio na njaa na kiu ya haki, na wale wanaomtafuta Yeye. Baadhi husema kwamba Mungu hakuwapa nuru hata baada ya wao kusoma neno Lake. Maneno haya yalisomwa vipi? Ukisoma neno Lake kama kutazama maua mgongoni mwa farasi na hukutilia umuhimu katika uhalisia, Mungu angekupa nuru vipi? Ni vipi ambavyo mtu asiyethamini neno la Mungu atakavyofanywa kuwa mtimilifu na Yeye? Kama huthamini neno la Mungu, basi hutakuwa na ukweli wala uhalisia. Kama utathamini neno Lake, basi utaweza kutia katika matendo ukweli; ni hapo tu ndipo utakapokuwa na uhalisia. Hivyo basi lazima ule na kunywa neno la Mungu licha ya hali yoyote ile, kama una shughuli au la, kama hali ni mbaya au la, na kama unajaribiwa au la. Kwa jumla, neno la Mungu ndilo msingi wa uwepo wa mwanadamu. Hakuna yule anayeweza kugeukia neno Lake na lazima ale neno Lake kana kwamba ndilo milo ile mitatu ya siku. Linaweza kuwa suala rahisi hivyo kufanywa kuwa mtimilifu na kupatwa na Mungu? Iwapo unaelewa au hauelewi kwa sasa au kama una utambuzi wa kazi ya Mungu, lazima ule na kunywa zaidi ya neno la Mungu. Huku ndiko kuingia katika njia makini ya utendaji. Baada ya kulisoma neno la Mungu, harakisha kukitia katika matendo kile unachoweza kuingia ndani, na utenge kwa wakati huu kile huwezi kuingia ndani. Huenda kukawa na mambo mengi katika neno la Mungu ambayo huwezi kuyaelewa mwanzoni, lakini baada ya miezi miwili au mitatu, pengine hata mwaka mmoja, utaweza. Kwa nini hali iko hivi? Hii ni kwa sababu Mungu hawezi kumfanya binadamu kuwa kamili kwa siku moja au mbili. Wakati mwingi, unapolisoma neno Lake, pengine huwezi kuelewa kwa wakati huo. Wakati huo, yaweza kuonekana kama maandishi tu; ni kupitia tu kipindi cha uzoefu ndipo unapoweza kuelewa. Mungu ameongea mengi, hivyo basi unafaa kufanya yale mengi zaidi unayoweza ili kula na kunywa neno Lake. Bila ya kutambua, utakuja kuelewa, naye Roho Mtakatifu atakupa nuru. Wakati Roho Mtakatifu humpa nuru binadamu, mara nyingi ni bila ya ufahamu wa binadamu. Hukupa nuru na kukuongoza unapokuwa na kiu na unapotafuta. Kanuni ambayo Roho Mtakatifu hufanya kazi imekita mizizi katika neno la Mungu ambalo unakula na kunywa. Wale wote ambao hawatilii umuhimu katika neno la Mungu na siku zote wana mwelekeo mwingine katika neno Lake, mwelekeo ule wa uzembe na kusadiki kwamba hakuna tofauti yoyote kama watalisoma neno Lake, ndio wale wasiokuwa na uhalisia. Si kazi ya Roho Mtakatifu wala nuru kutoka Kwake vinavyoweza kuonekana ndani yao. Watu kama hao wanasairi tu, na ni wanafiki wasiokuwa na kufuzu kwa ukweli, kama Bw. Nanguo wa hadithi ya mafumbo.[a]
Bila ya neno la Mungu kama uhalisi wako, huna kimo halisi. Wakati ukiwadia wa kujaribiwa, bila shaka utaanguka, na hapo ndipo kimo chako cha kweli kitakapoonyeshwa. Lakini kwa wakati huo, wale wanaotafuta mara kwa mara kuingia katika uhalisia wataelewa kusudio la kazi ya Mungu. Mtu anayemiliki dhamiri na ana kiu ya Mungu anafaa kuchukua hatua ya kimatendo ili kumlipia Mungu kwa upendo Wake. Wale wasiokuwa na uhalisia hawawezi kusimama imara wanapokumbwa hata na masuala madogo. Kunayo tofauti kati ya wale walio na kimo halisi na wale wasiokuwa nacho. Ni kwa nini wote wanakula na kunywa neno la Mungu, lakini baadhi yao wanaweza kusimama imara katika jaribio huku nao wengine wanalitoroka? Utofauti ulio wazi ni kwamba wanakikosa kimo halisi; hawana neno la Mungu kama uhalisia wao, na neno Lake halijakita mizizi ndani yao. Punde tu wanapojaribiwa, hakuna njia kwao. Kwa nini, hivyo basi, wengine hawawezi kusimama imara kwa hili? Hii ni kwa sababu wanayo maono makubwa, au neno la Mungu limekuwa uzoefu wao ndani yao, na kile ambacho wameona katika uhalisia kimekuwa msingi wa uwepo wao. Kwa hivyo basi wanaweza kusimama imara kupitia kwa majaribio. Hiki ni kimo halisi, na haya ni maisha pia. Baadhi wanaweza pia kusoma neno la Mungu lakini hawawezi katu kulitia katika matendo au wao hawana ari kulihusu. Wale wasio na ari hawaweki umuhimu wowote katika kulitia neno hilo katika matendo. Wale wasiokuwa na neno la Mungu kama uhalisia wao ndio wale wasiokuwa na kimo halisi. Watu kama hao hawawezi kusimama imara katika majaribio.
Wakati Mungu anapoongea, unafaa kupokea mara moja maneno Yake na kuyala. Haijalishi ni kiwango kipi unachokielewa, shikilia mtazamo kwamba uzingatie tu kulila, kulijua, na kulitia katika matendo neno Lake. Hili ni jambo unalofaa kufanya. Usiwe na wasiwasi kuhusu ni kiwango kipi cha ukubwa ambacho kimo chako kinaweza kuwa; zingatia tu katika kula neno Lake. Hivi ndivyo binadamu anavyofaa kushirikiana. Maisha yako ya kiroho kimsingi ni kuingia katika uhalisia pale ambapo unakula na kunywa neno la Mungu na kulitia katika matendo. Hufai kuzingatia jambo lolote jingine. Viongozi wa kanisa wanafaa kuwaongoza ndugu wote katika namna ya kula na kunywa neno la Mungu. Huu ndio wajibu wa viongozi wote wa kanisa. Wawe wachanga au wazee, wote wanafaa kuchukulia kula na kunywa maneno ya Mungu kwa umuhimu na kuyatia maneno Yake katika mioyo yao. Ukiingia katika uhalisia huu, utakuwa umeingia katika Enzi ya Ufalme. Siku hizi, wengi huhisi kwamba hawawezi kuishi bila kula na kunywa neno la Mungu, na haijalishi ni wakati gani, wanahisi kwamba neno Lake ni geni Kisha ndipo binadamu anapoanza kuwa katika njia sahihi. Mungu hutumia neno Lake katika kufanya kazi na kumruzuku binadamu. Wakati wote wanapotamani na kuwa na kiu ya neno la Mungu, wataingia katika ulimwengu wa neno Lake.
Mungu ameongea pakubwa. Unayo maarifa kiasi kipi kuyahusu? Umeingia hadi kiwango kipi? Kama kiongozi wa kanisa bado hajawaongoza ndugu katika uhalisia wa neno la Mungu, basi wamekuwa wazembe katika wajibu wao na kushindwa kukamilisha majukumu yao! Haijalishi ni kina kipi cha kula na kunywa kwako kwa neno, au ni kiasi kipi unachoweza kupokea, lazima ujue namna ya kula na kunywa neno Lake; lazima uchukulie neno Lake kwa umuhimu na uelewe umuhimu na haja ya kushiriki kama huko. Mungu ameongea sana. Kama hutakula na kunywa neno Lake, wala hulitafuti ama kulitia neno Lake katika matendo, huwezi kuchukuliwa kama unayemsadiki Mungu. Kwa sababu unamsadiki Mungu, lazima ule na kunywa neno Lake, upitie neno Lake, na uishi kwa kudhihirisha neno Lake. Hivi tu ndivyo unavyomsadiki Mungu! Kama unasema umemsadiki Mungu ilhali huwezi kuongea maneno Yake yoyote au kuyatia katika matendo, huchukuliwi kuwa unamsadiki Mungu. Hivi ni “kuutafuta mkate ili kuikabili njaa.” Tukizungumzia tu ushuhuda mdogo mdogo, masuala ya kipuzi na masuala ya juujuu, na kutokuwa na hata kiwango kidogo cha uhalisia hakumaanishi kusadiki Mungu. Hivyo basi, bado hujang'amua njia sahihi ya kumsadiki Mungu. Kwa nini ule na kunywa zaidi ya maneno ya Mungu? Je, inadhaniwa kuwa imani usipokula na kunywa maneno Yake na kutafuta tu kupaa mbinguni? Ni nini hatua ya kwanza kwake yule anayesadiki neno Lake Mungu? Ni katika njia gani Mungu humfanya binadamu kuwa mtimilifu? Unaweza kufanywa kuwa mtimilifu bila ya kula na kunywa neno la Mungu? Unaweza kuchukuliwa kuwa mtu wa ufalme bila ya neno la Mungu kuwa uhalisia wako? Ni nini hasa kusadiki Mungu? Wanaomwamini Mungu wanafaa kumiliki tabia nzuri kwa nje, angalau, na kilicho na umuhimu mkubwa zaidi ni kuwa na neno la Mungu. Haijalishi ni nini, huwezi kuligeukia neno la Mungu. Maarifa yako katika Mungu na kukamilishwa kwa mapenzi Yake vyote vinatimizwa kupitia kwa neno Lake. Mataifa yote, imani, madhehebu, na sekta zote zitaweza kushindwa kupitia kwa neno kwenye siku za usoni. Mungu ataongea moja kwa moja, na watu wote watashikilia neno la Mungu katika mikono yao; kupitia haya watu watafanywa kuwa watimilifu. Neno la Mungu limeenea kotekote: Watu huongelea neno la Mungu na kutenda kulingana na neno la Mungu, huku likiwa limehifadhiwa ndani bado huwa ni neno la Mungu. Kwa ndani na hata kwa nje, wanarowekwa katika neno la Mungu, na hivyo basi wanafanywa kuwa watimilifu. Wale wanaokamilisha mapenzi ya Mungu na wanaweza kumshuhudia Yeye ndio wale walio na neno la Mungu kama uhalisi.
Kuingia katika Enzi ya Neno, yaani, Enzi ya Ufalme wa Milenia, ndiyo kazi ambayo inakamilishwa sasa. Kuanzia sasa, fanya mazoezi ya kushiriki kuhusu neno la Mungu. Ni kupitia tu kula na kunywa neno Lake na kulipitia ndipo unapoweza kuonyesha neno la Mungu. Ni kupitia tu maneno yako ya uzoefu ndipo wengine wanapoweza kushawishika na wewe. Kama huna neno la Mungu, hakuna atakayeshawishika! Wale wote wanaotumiwa na Mungu wanaweza kuongea neno la Mungu. Kama huwezi, hii yaonyesha kwamba Roho Mtakatifu bado hajakufanyia kazi na ungali bado hujafanywa kuwa mtimilifu. Huu ndio umuhimu wa neno la Mungu. Je, unao moyo ulio na kiu ya neno la Mungu? Wale walio na kiu ya neno la Mungu huwa na kiu ya ukweli, na binadamu kama hao tu ndio wanaobarikiwa na Mungu. Katika siku za usoni, kunayo maneno mengi zaidi ambayo Mungu atatamka kwenye madhehebu na dini zote. Kwanza anaongea na kutoa sauti Yake miongoni mwenu na kuwafanya kuwa kamili kabla ya kusonga mbele na kuongea na kutoa sauti Yake kwa Mataifa na kuwashinda. Kupitia kwa neno, wote wataweza kushawishika kwa uaminifu na kwa kikamilifu. Kupitia neno la Mungu na ufunuo Wake, tabia iliyopotoka ya binadamu imepungua. Wote wanao wajihi wa binadamu, na tabia asi ya binadamu imelegea vilevile. Neno linafanya kazi kwa binadamu kupitia kwa mamlaka na linamshinda binadamu ndani ya nuru ya Mungu. Kazi ambayo Mungu atafanya katika enzi ya sasa, pamoja na jambo kuu katika kazi Yake vyote vinaweza kupatikana ndani ya neno Lake. Kama hulisomi neno Lake, hutaelewa chochote. Kupitia kula na kunywa kwako mwenyewe kwa neno Lake, kuwa na ushirika na ndugu, na kile utakachopitia kwa uhalisi, maarifa yako ya neno la Mungu yatakuwa pana. Na hapo tu ndipo unapoweza kuishi kwa kulidhihirisha kwa kweli katika uhalisia.
Marejeleo:
a. Maandishi asilia yameacha "wa hadithi ya mafumbo."
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni