Smiley face

Jumatatu, 9 Desemba 2019

Si Rahisi Kuwa Mtu Mwaminifu

Maisha ya kanisa
Imeandikwa na Zixin, Mkoa wa Hubei
Baada ya kuikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, kwa kusoma maneno ya Mungu na kusikiliza mahubiri, nilikuja kuelewa umuhimu wa kufuatilia kuwa mtu mwaminifu katika imani ya mtu, na kwamba ni kwa kuwa mtu mwaminifu tu ndipo mtu anaweza kupata wokovu wa Mungu. Hivyo nikaanza kushiriki kuwa mtu mwaminifu katika maisha halisi. Baada ya kipindi cha muda, nilitambua kuwa nilipata kuingia kiasi katika maisha. Kwa mfano: Wakati nikiomba au kuzungumza na mtu, ningeweza kusema ukweli na kutoka moyoni; pia niliweza kuuchukua utekelezaji wa wajibu wangu kwa uzito kabisa, na nilipofichua upotovu niliweza kuzitoa siri zangu kwa watu wengine. Kwa sababu ya hili, nilifikiri kuwa mtu mwaminifu kulikuwa rahisi sana kutenda, na sio vigumu kamwe kama ilivyodaiwa kuwa na maneno ya Mungu: “Wengi wanaona afadhali washutumiwe hadi kuzimu kuliko kuongea na kutenda kwa uaminifu” (“Maonyo Matatu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Ni baadaye tu nilipoweza kutambua vyema kupitia matukio kadhaa kwamba kwa kweli sio rahisi kwetu, wanadamu wapotovu, kuwa watu waaminifu. Maneno ya Mungu kwa kweli ni ya kweli kikamilifu na hayajatiwa chumvi kabisa.
Nilipokuwa nikitunga hati siku moja, nilitambua kuwa dada mmoja kutoka kanisani alikuwa bora kuniliko kwa kutunga hati. Kisha nikawaza: “Ni lazima nizishughulikie kabisa hati ambazo yeye hutunga, endapo viongozi wataona kwamba yeye ni bora kuniliko na wampandishe cheo, wakiiweka kazi yangu mwenyewe katika hatari.” Baada ya wazo hili kuibuka, nilihisi kulaumiwa na dhamiri yangu. Baada ya kuchunguza na kuchangua hili nilitambua kwamba lilikuwa ni dhihirisho la kujitahidia umaarufu na faida na kuwa na wivu wa talanta ya kweli, hivyo nikamwomba Mungu na kujikana mara moja. Katika mkutano mmoja, kwanza nilikuwa nimetaka kutangaza upotovu wangu wazi, lakini nikawaza: “Nikishirikiana ushirika juu ya nia zangu mwenyewe mbovu, yule dada yangu niliyefanya kazi naye na dada yangu wa familia mwenyeji wangu wangenionaje? Wangesema moyo wangu ni wenye nia mbaya mno na asili yangu ni mbovu mno? Lisahau, bora nisiliseme. Lilikuwa ni wazo tu, na si kama kwa kweli nilikuwa nimefanya hivyo kwa vyovyote vile.” Na hivyo tu, nilitaja tu kikawaida jinsi nilivyokuwa na wasiwasi sana kwamba nafasi yangu ingechukuliwa nilipoona mtu mwingine akitunga hati vizuri—niliuficha upande wangu halisi wa giza. Baada ya hapo hisia ya lawama moyoni mwangu ilikua. Kwa hiyo niliapa mbele ya Mungu kwamba hili lingetokea tu mara moja, na kwamba wakati ujao ningeweka kabisa kuwa mtu mwaminifu katika vitendo.
Siku chache baadaye nilpokuwa nikizungumza na patna wangu na dada yangu wa familia mwenyeji wangu, nikasikia dada wa familia mwenyeji akiongea juu ya jinsi dada wawili ambao waliishi nyumbani kwake walivyokuwa wazuri (niliwajua pia), lakini hakusema hata neno moja kuhusu jinsi nilivyokuwa mzuri. Nilihuzunika sana. Ili kumfanya anistahi na kuniheshimu, niliorodhesha dosari za dada hao wawili moja moja kumwonyesha kuwa hawakuwa wazuri kama mimi. Baada ya kusema hili, nilitambua kwamba kile nilichokuwa nimekisema hakikufaa, na kwamba dhamira yangu na kusudi langu lilikuwa kuwalaumu wengine ili kujipandisha hadhi. Lakini nilikuwa nimeaibika mno kiasi cha kutoweza kuzitoa siri zangu, hivyo nikamwambia dada wa familia mwenyeji: “Niliposikia ukiwasifu dada hao wawili, nilihisi kuwa ulikuwa na sanamu wachache ndani ya moyo wako, kwa hiyo ilinibidi niharibu picha yao ili usiwape heshima kubwa tena.” Mara tu maneno hayo yalipokuwa yametoka kinywani mwangu, yule dada patna wangu akasema: “Hili linategemea kama ulikuwa na nia zozote fiche. Kama ulikuwa nazo, hilo kwa kweli ni jambo bovu. Kama hukuwa nazo, basi inaweza tu kusemwa kuwa ulikuwa ufunuo wa upotovu.” Kumsikia akisema hili, niliogopa mno kwamba wangeweza kukuza fikira mbaya kunihusu, hivyo nikajaribu kujieleza mwenyewe kwa haraka: “Sikuwa na nia zozote fiche. Ni kwamba tu sikuliwasilisha kwa njia sahihi….” Baada ya utoaji hoja huu wa kuhadaa, nikawa na hasira mno na nikahisi hasa kulaumiwa kwa ndani nilipoomba: “Wewe ni mjanja mno. Unanena kwa njia za kuzungukazunguka, kubuni uongo, na kuuficha ukweli, daima ukizificha nia zako mbovu na tamaa zako za kiburi. Si huku ni kumdanganya Mungu?” Hata hivyo, mimi, nikiwa nimeshupazwa sana, bado sikutubu na nilimwomba tu Mungu anisamehe.
Siku iliyofuata, nilishikwa na homa kali ghafla, na kila kiungo mwilini mwangu kiliuma. Mwanzoni nilifikiri nilikuwa nimeshikwa na mafua usiku kucha na kwamba ningepata nafuu kama ningekunywa tu dawa. Lakini nani aliyejua—kunywa dawa haukuwa msaada, na siku mbili baadaye sikuweza hata kutoka kitandani. Aidha, ulimi wangu ulivimba na ukawa mgumu zaidi, na koo yangu pia ilivimba kwa maumivu, ikiniuma sana kiasi kwamba sikuweza hata kuzungumza. Kumeza kulikuwa kugumu kivyake, sembuse kula. Nikiwa nimekabiliwa na ugonjwa huu wa ghafla, nilikua na hofu, na nikamwomba Mungu moyoni mwangu tena na tena. Wakati huo, nilitambua kwamba ugonjwa huu haukutokea kwa ajali, na hivyo nikaja mbele ya Mungu kutafakari mambo yote niliyoyasema na kuyafanya katika kipindi hiki. Nilipokuwa nikitafakari, nilielewa kwamba kulikuwa na matukio kadhaa ambapo nilikuwa nimezungumza kwa kuepaepa na nilikuwa nimezificha nia zangu mwenyewe zenye kustahili dharau. Nilikuwa nimejua vizuri kabisa kwamba nilikuwa nikiongea uongo tu na nilikuwa nimewadanganya dada zangu, na nilikuwa nimehisi hisia ya aibu, na bado sikuwa nimepata ujasiri wa kusema ukweli. Sikutambua kwamba njia zangu za hila tayari zilikuwa zimekuwa asili yangu ya pili, na sikuweza kulidhibiti tena. Kwa ajili ya sifa na hadhi yangu, majivuno na fahari kuu, nilikuwa nimejaribu kumdanganya Mungu na kuwadanganya dada zangu tena na tena bila haya. Sikuwa nimejitolea kutoa siri juu ya upotovu wangu na sikuwa nimetafuta ukweli ili kutatua matatizo yangu; kama ningekuwa nimeendelea hivyo, si ingekuwa ni mimi ambaye ningepitia upotezaji? Mungu huchunguza chokomeani ya moyo wa mwanadamu, na bila kujali nilivyojaribu kujificha, sikuweza kuuficha ubaya wangu unaostahili dharau. Mara nilipokuja kujielewa mwenyewe kiasi, nilipiga magoti mbele ya Mungu na kuomba: “Ee Mungu! Ni sasa tu ninapoona jinsi nilivyo mpotovu. Kudhibitiwa na asili yangu ya udanganyifu, ninaona vigumu sana kusema hata neno moja la kweli. Ee Mungu! Ninaomba kuwa Uniongoze kufichua siri zangu na kuweka wazi makosa yangu, na kuwa mtu mwaminifu mbele Yako.” Chini ya uongozi wa Mungu, hatimaye nilijipa moyo na kuwaambia dada zangu ukweli juu ya jambo lote, tangu mwanzo hadi mwisho. Ni wakati huo tu ndipo moyo wangu ulihisi kuwa na amani kidogo na utulivu.
Ilikuwa tu kwa njia ya uzoefu huu ndipo nilielewa kwa kina maneno ya Mungu kwamba “Wengi wanaona afadhali washutumiwe hadi kuzimu kuliko kuongea na kutenda kwa uaminifu” hasa ni kweli. Baada ya kupotoshwa na Shetani, kusema uongo, kudanganya, na kujihusisha na udanganyifu vikawa asili ya binadamu na vikawa vimekita mizizi katika mioyo ya wanadamu. Aidha, watu kwa kweli huthamini sifa njema, hadhi, na aina zote za faida; wale ambao wamewekewa vizuizi na mambo haya huona ikiwa vigumu sana kuzungumza kwa uaminifu. Hivyo kwa watu, kuwa mtu mwaminifu ni vigumu kuliko kupanda juu mbinguni. Nilikuwa nikidhani kwamba kuwa mtu mwaminifu ilikuwa rahisi. Hiyo ilikuwa ni kwa sababu siri niliyoitoa ilikuwa ni juu ya upotovu usiofungamana tu nilioufichua ambao kila mtu alishirikiana mara kwa mara katika ushirika. Haukuhusu mambo ya kina zaidi katika nafsi yangu, kwa hiyo hakuna yeyote ambaye angeniangalia kwa dharau kwa kuzungumza juu ya mambo hayo. Aina hiyo ya matendo ilikuwa chini ya sharti la mwanzo kwamba vilikuwa vitendo vya juujuu na havingegusa maslahi yangu binafsi. Kama ingeathiri maslahi yangu muhimu, hadhi yangu na ujasiri wangu, basi asili yangu ingejifichua na singeweza tena kudumisha hila yangu. Nikiwa na ukweli mbele yangu, nilianza kufahamu kwa kina kwamba si rahisi kuwa mtu mwaminifu. Hasa kwa mtu kama mimi ambaye hufikiria sifa na hadhi kuwa muhimu sana, nisipoweka kando mambo yote ya ujasiri, kama kuadibu na hukumu ya Mungu haviambatani nami, nitakuwa asiyeweza kabisa kufikia uhalisi wa ukweli wa kuwa mtu mwaminifu katika vitendo. Kuanzia sasa kwendelea, nitafuatilia ukweli kwa makini, kuyakubali maneno yote ya Mungu, na kuelewa asili yangu ya udanganyifu hata kwa kina zaidi. Nitaweka kando ujasiri wangu na hadhi yangu na kwa kweli kuwa mtu mwaminifu; Nitaishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu wa kweli ili kulipa upendo wa Mungu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni