Mtu huwa na tatizo lipi anapopenda kupeana visingizio? Ni nini kiini chake? Yeye ni mkaidi. Watu wakaidi hawakubali ukweli kwa urahisi; sio watiifu, na wanaposikia neno moja ambalo haliambatani na dhana, mitazamo, wanayopenda, hisia au mihemko yao wenyewe, basi hawalikubali; husema, “Sijali iwapo liko sahihi au ni mbaya, ni nani aliyelinena, lilinenwa katika muktadha gani, au iwapo linahusiana na majukumu na wajibu wangu; siyajali mambo haya.
Kuziridhisha hisia zangu mwenyewe ni suala muhimu .” Hii sio ukaidi? Ukaidi huwafanya watu kupoteza nini mwishowe? Huifanya vigumu kwao kupata ukweli. Kutokubali ukweli husababishwa na tabia potovu ya mwanadamu, lakini mwishowe, utapata ikiwa vigumu kuupata ukweli. Mambo ambayo watu hulazimika kuishi kwa kudhihirisha na kwa kawaida kufichua kwa asili yao, hali na silika zao—yale ambayo huwa wanafanya, yale ambayo huwa wanafikiri, mtazamo ambao wao huwa nao na hali zao zilivyo, mambo ambayo kwa kawaida yamefunuliwa—yote ni kinyume cha ukweli. Yaani, hawataki kuukubali ukweli, hawatilii maanani usahihi au makosa ya ukweli, na mambo ambayo huwa wanafikiri kuyahusu na kufanya hayana uhusiano wowote na ukweli. Wanataka kufanya mambo kila wakati kulingana na dhana na tamaa zao wenyewe, na kulingana na wanayopenda. Hizi ni silika za mwanadamu na ni maonyesho asilia ya tabia yake potovu. Lakini iwapo wewe si kaidi, iwapo umekomaa kidogo, wewe ni mnyenyekevu kidogo, iwapo huonyeshi uasili wako jambo fulani likitendeka kwako, lakini unatulia na kuomba, na unamruhusu Mungu kukushughulikia na unahusiana na Mungu katika moyo wako, iwapo unaweza kunyamaza mbele za Mungu, iwapo unakubali ukweli—iwapo una aina hii ya hali ya akili katika matendo yako, katika jinsi unavyopatana na watu, katika kutekeleza wajibu wako na kuusikiliza ushirika—iwapo kila wakati una aina hii ya hali ya akili na iwapo moyo wako unakuwa sahihi mbele za Mungu kila wakati, basi haijalishi ni tabia potovu ngapi ulizo nazo na haijalishi jinsi ulivyopotoka sana. Moyo wako uko sahihi, hutaonyesha uasili wako mambo yanapotendeka kwako na hutatenda ukitegemea mapenzi yako mwenyewe. Utayakubali mambo yaliyo sahihi na, mara unapoyakubali, utayasimilisha polepole kwa muda. Wakati huo, huenda ukawa na hisia kubwa zinazogongana, au unaweza kuhisi kutoridhika kidogo. Lakini una aina kama hiyo iliyo sahihi, unayakubali, kisha katika siri unasoma kwa kuomba polepole, kutafakari na kushiriki. Mambo unayozozana nayo au yale ambayo huwa unaona yakiwa magumu kuyakubali yatasimilishwa kidogokidogo, kwa muda fulani, utaelewa na kukubali ukweli ndani yake na utakuwa maisha yako. Utakapokuwa maisha yako, mwishowe utakuwa unaishi katika uhalisi wa kweli. Utaweza kuishi katika uhalisi wa kweli na, wakati huu, utapata tajriba na kuelewa uhalisi wa kweli; hivyo hutaweza kushiriki kuhusu uhalisi wa kweli? Na iwapo wewe ni kaidi? “Ndugu hapo juu hunena vibaya, Mungu hunena vibaya, mtu fulani na fulani hunena vibaya, hivyo sipaswi kusikiliza, na nina kisingizio cha kutosikiza.” Hii sio kuwa mkaidi? Tabia yako ya kuasi hutokea wazi na huwa unapeana visingizio kila wakati. Hujui wanachosema watu wengine wakati huo au ni sura gani ya ukweli wanayozungumza kuhusu, kisha baadaye hautendi ukweli wa utiifu, na husomi au kuingia katika somo la jinsi ya kutii ukweli. Mwishowe, kamwe huwezi ukaupata ukweli, kamwe hauko katika hali ya kawaida, mambo hayo yaliyo ndani yako kwa kawaida ni ya juujuu sana na maisha yako kwa kawaida hayajakomaa kabisa. Hivyo, matokeo ya mwisho ni yapi? (Maisha yetu hayawezi kukomaa.) Na kipengele kikuu ni kipi? Kosa lako la ukaidi kamwe haliwezi kamwe kubadilisha. Unategemea kujizuia kwako mwenyewe, na labda leo uko katika afya nzuri, hali zako ni nzuri sana na, kulingana na wewe, hali zako zote ni za kufaa, na inaonekana kama kwamba wewe sio kaidi. Lakini punde jambo linatendeka kwako linalohusisha ukaidi wako, hutoka tena na hauwezi kubadilishwa. Kutegemea kujizuia kwako mwenyewe—kuuhini mwili wako—ni kuchukua usukani kwa kutegemea nguvu zako mwenyewe, na hivyo hutafaulu; hata hutaweza kulihini kosa kidogo kama hilo. Lakini iwapo utajifunza utiifu na uwe mtulivu mbele za Mungu, basi makosa haya, tabia hizi potovu, zitasuluhishwa kidogo kidogo kutoka kwa mzizi kwenda juu, na hutahitaji tena kufanya mazoezi ya kujizuia mwenyewe. Ni lazima kwanza ujifunze jinsi ya kufanya mazoezi, na jinsi ya kuingia na ufanye mazoezi ya njia ambayo husuluhisha matatizo yanayohusiana na sura hii. Kisha polepole utakuja kuelewa ukweli na polepole kuingia katika uhalisi wa ukweli. Kusuluhisha tabia yako potovu ni sawa na mchwa kuguguna mfupa. Unaanza kwa hali zako na kuzisuluhisha kidogokidogo; mara zinaposuluhishwa, kosa hili lako kwa kweli pia litasuluhishwa kidogokidogo; na mara kosa hili linaposuluhisha, tabia yako potovu kwa kweli, kidogokidogo, itabadilishwa.
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni