Smiley face

Jumatano, 3 Januari 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII (II) Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote(Sehemu ya Pili )


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote 
(I)

Mwenyezi Mungu alisema, Leo Nitashiriki nawe mada mpya. Mada itakuwa ni nini? Kichwa cha mada kitakuwa "Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote." Je, hii siyo mada kubwa kidogo kuweza kuijadili? Je, inaonekana kama kitu ambacho kidogo hakiwezi kufikika? Mungu kuwa chanzo cha uhai kwa vitu vyote inaweza kuonekana ni mada ambayo watu wanahisi kutohusika nayo, lakini wote wanaomfuata Mungu wanapaswa kuielewa. Hii ni kwa sababu mada hii haihusiani kwa kuchanganulika na kila mtu anayemjua Mungu, kuweza kumridhisha na kumheshimu. Hivyo, mada hii inapaswa kuwasilishwa. Awali, pengine baadhi ya watu walikuwa na ufahamu wa msingi wa mada hii, au pengine baadhi ya watu waliifahamu. Wanaweza wakawa na ufahamu sahili kuhusu au ufahamu wa juu juu wa hii katika akili zao. Wengine wanaweza kuwa na ufahamu kiasi maalumu kuihusu; kutokana na uzoefu wao wa kipekee, mioyoni mwao wana uelewa wa kina juu ya mada hii. Lakini ama maarifa ya mada hii ni ya kina au ya juujuu, kwenu nyinyi ni ya upande mmoja na wala si mahususi vya kutosha. Hivyo, mada hii inapaswa kuwasilishwa, kusudi lake ni kuwapatia uelewa wa kina zaidi na mahususi. Nitatumia njia maalumu kushiriki na nyinyi mada hii, njia ambayo hatujawahi kuitumia hapo awali na njia ambayo kidogo mtaona si ya kawaida, au ambayo haifurahishi kidogo. Hata hivyo, baada ya kuisikia mtaijua, njia yoyote ile itakayotumika. Je, mnapenda kusikiliza hadithi? (Ndiyo.) Ni aina gani ya hadithi mnayopenda kusikiliza? Ngano, hekaya au simulizi za kisayansi? (Hekaya.) (Hadithi kuhusu Mungu na mwanadamu.) Je, kuna hadithi kuhusu Mungu na mwanadamu? (Ndiyo.) Kuna hadithi kuhusu Mungu na mwanadamu ambazo zinatokea kwenu kila siku. Je, Nina haja hata ya kuzitaja? Inaonekana kwamba Nilikuwa sahihi kuchagua njia ya kusimulia hadithi. Nyinyi nyote mnapenda kusikiliza hadithi. Sawa, hebu tuanze. Hamna haja ya kuandika hii kwenye matini zenu. Ninawaomba muwe watulivu, na msihangaike. Unaweza kufumba macho yako ikiwa unahisi kwamba kufumbua macho yako mazingira yanayokuzunguka au watu wanaokuzunguka wanaweza kukupotezea umakini. Nina hadithi ndogo nzuri ya kuwasimulia. Ni hadithi kuhusu mbegu, ardhi, mti, mwanga wa jua, chiriku, na mwanadamu. Hadithi Ninayokwenda kuwasimulia ina wahusika gani wakuu ndani yake? (Mbegu, ardhi, mti, mwanga wa jua, chiriku, na mwanadamu.) Mungu atakuwa ndani yake? (Hapana.) Lakini Nina uhakika kwamba baada ya hadithi kusimuliwa mtajihisi kuburudika na kuridhika. Sawa basi, unaweza kusikiliza kimya kimya.
Hadithi ya 1. Mbegu, Ardhi, Mti, Mwanga wa Jua, Chiriku, na Mwanadamu
Mbegu ndogo ilidondoka ardhini. Baada ya mvua kubwa kunyesha, mbegu ilianza kuchipuka na mizizi yake ikamea taratibu kwenda ardhini. Chipuko lilirefuka kadri muda ulivyozidi kwenda, yakivumilia upepo mkali na mvua kubwa, yakiangalia mabadiliko ya misimu kadri mwezi unavyopevuka na kufifia. Wakati wa kiangazi ardhi ilileta zawadi ya maji ili kwamba chipuko liweze kuhimili joto kali. Na kwa sababu ya ardhi, chipuko halikuhisi joto na hivyo lilihimili joto la kiangazi. Msimu wa baridi ulipokuja, ardhi ililifunika chipuko katika kumbatio la vuguvugu lake na kushikamana kwa nguvu. Na kwa sababu ya vuguvugu la ardhi, chipuko lilihimili baridi kali, likivuka bila kudhurika katika dhoruba ya msimu wa baridi na barafu za msimu. Likivikwa na ardhi, chipuko lilikua kwa ujasiri na lilikuwa na furaha. Lilirefuka na kujivunia malezi yasiyokuwa ya ubinafsi ambayo ardhi iliyatoa. Chipuko lilikua kwa furaha. Liliimba wakati mvua ilipokuwa ikinyesha na kucheza na kuyumba kadri upepo ulivyokuwa ukivuma. Na hivyo, chipuko na ardhi hutegemeana...
Miaka ilipita, na chipuko sasa lilikuwa mnara wa mti. Lilikuza matawi manene juu yake yaliyokuwa na majani yasiyohesabika na kusimama imara juu ya nchi. Mizizi ya mti ilimea aridhini kama ilivyomea hapo kabla, lakini sasa ilizama kabisa ardhini chini kabisa. Kile ambacho mwanzo kilililinda chipuko sasa kilikuwa msingi wa mti mkubwa sana.
Mwale wa mwanga wa jua ulimulika mti na shina likatikisika. Mti ulitoa nje matawi yake kwa upana na kufaidi sana kutoka kwenye mwanga. Ardhi chini ilipumua kwa wizani pamoja na mti, na ardhi ilihisi kufanywa upya. Baada ya hapo tu, upepo mwanana ulivuma katika matawi, na mti ulifurahia sana, ukiwa na nguvu. Na hivyo, mti na mwanga wa jua vinategemeana ...
Watu walikaa katika kivuli tulivu cha mti na wakafurahia hewa changamfu inayonukia vizuri. Hewa ilitakasa mioyo na mapafu yao, na ilitakasa damu ndani yao. Watu hawakuhisi tena kuchoka au kuelemewa. Na hivyo, watu na miti wanategemeana ...
Kundi la chiriku waliimba kwa uchangamfu walivyokuwa wakitua kwenye matawi ya mti. Pengine walikuwa wanamwepuka adui fulani, au walikuwa wanazaliana na kuwalea watoto wao, au pengine walikuwa wanapata pumziko fupi. Na hivyo, ndege na mti wanategemeana ...
Mizizi ya mti, ikiwa imesokotana na kusongamana, ilijikita chini kabisa ardhini. Shina lake liliifunika ardhi dhidi ya upepo na mvua na kuyatoa nje matawi yake makubwa na kuilinda ardhi chini yake, na mti ulifanya hivi kwa sababu ardhi ni mama yake. Yanaishi pamoja, yanategemeana, na kamwe hayatatengana ...
Kwa hiyo, hadithi imefikia mwisho. Mnaweza kufumbua macho yenu sasa. Nimewasimulia hadithi kuhusu mbegu, ardhi, mti, mwanga wa jua, chiriku na mwanadamu. Hadithi ina sehemu chache tu. Iliwapatia hisia gani? Baada ya kuwasimulia kwa namna hii, je, mmeielewa? (Tunaelewa.) Mnaweza kuzungumza kuhusu hisia zenu. Sasa, Mnahisi nini baada ya kusikia hadithi hii? (Inagusa sana na inaonekana ni hadithi inayomhusu Mungu na mwanadamu na kwamba hii ni njia ambayo kwayo Anamlea mwanadamu, Anamlinda mwanadamu ili kwamba baada ya hapo mwanadamu anaweza kukua akiwa imara. Wakati mwanadamu anakuwa mwanadamu kamili anaweza kuelewa upendo wa Mungu na kuurudisha upendo huo Kwake. Mungu na mwanadamu wako karibu sana kiasi kwamba hawawezi kutenganishwa.) Kwanza Nitawaambia kwamba vitu vyote Nilivyovitaja kwenu mnaweza kuviona na kuvishika; haya ni mambo halisi, sio sitiari. Ninawataka sasa mtafakari juu ya yale Niliyoyajadili. Hakuna Nilichokizungumza ambacho kilikuwa cha kina, na kuna sentensi chache ambazo zinatengeneza hoja kuu ya hadithi. (Ama iwe ni mmea au mnyama, ama iwe ni ndege au mwanadamu, chanzo cha uhai wake ni Mungu.) Nini zaidi? (Ingawa matukio katika hadithi hii ni vitu vinavyotokea karibu nasi, hata hivyo mara nyingi huwa tunapuuzia kanuni ya Mungu. Mungu anaisema kiasili kabisa na kiasili kabisa inatokea pembeni mwetu, lakini ndani yake kuna kanuni ya Mungu. Mungu anatawala vitu vyote na ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.) Kuna kitu kingine chochote cha kuongeza? (Hadithi tuliyoisikia inatoa picha nzuri: Mbegu inapata uhai na kadiri inavyokua inapitia misimu minne ya mwaka: majira ya kuchipua, kiangazi, kipupwe na baridi. Ardhi ni kama mama kwa namna ambavyo inalea. Inatoa vuguvugu wakati wa baridi ili kwamba chipuko lihimili baridi. Baada ya chipuko kukua na kuwa mti, mwale wa jua unagusa matawi yake, ukiupatia mti furaha zaidi. Tunaona kwamba miongoni mwa vitu vyote vya uumbaji wa Mungu, ardhi ipo hai na kwamba inategemea mti. Pia tunaona kwamba mwanga wa jua unaupatia mti vuguvugu nyingi sana, na ingawa ndege ni vitu vya kawaida vya kuona, tunaona jinsi gani ndege, mti, na watu wote wanakuja pamoja kwa maafikiano. Tunaposikia hadithi hii, hii ndiyo hisia tuliyonayo mioyoni mwetu kwamba, kimsingi, vitu vyote vya uumbaji wa Mungu ni hai.) Imesemwa vizuri! Je, kuna mtu ana kitu chochote cha kuongeza? (Katika hadithi kadri mbegu inapokua na kuwa mti mrefu kabisa, tunaona mambo ya ajabu ambayo Mungu ameyafanya. Mungu alifanya vitu vyote kuishi na kutegemeana na vyote kuunganika pamoja na kuhudumiana. Tunaiona hekima ya Mungu, maajabu Yake, na tunaona kwamba Yeye ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.)
Mambo yote Niliyoyazungumzia ni mambo ambayo mmeshawahi kuyaona hapo awali, kama vile mbegu, mnajua kuhusiana na hili, sio? Mbegu kukua na kuwa mti unaweza usiwe mchakato unaouangalia katika maelezo ya kina, lakini unajua kwamba ni ukweli, sio? Unajua kuhusu ardhi na mwanga wa jua. Taswira ya chiriku wakitua mtini ni kitu ambacho watu wote wamekwishakiona, sio? (Ndiyo.) Na watu kutuliza joto chini ya kivuli cha mti, wote mmekwishawahi kuona, sio? (Tumeona hilo.) Sasa, mnapata hisia gani mnapoona mifano yote hii katika taswira moja? (Upatanifu.) Je, mifano yote hii iliyopo katika taswira hii inatoka kwa Mungu? (Ndiyo.) Kwa kuwa inatoka kwa Mungu, Mungu anajua thamani na umuhimu wa mifano hii kadhaa inayokaa pamoja ardhini. Mungu alipoviumba vitu vyote, Alikuwa na mpango kwa kila kitu, na kila kitu Alichokiumba huonesha makusudi Yake na Yeye Hujaza uhai ndani yao. Alitengeneza mazingira hai kwa ajili ya binadamu, ambayo yamejadiliwa katika hadithi tuliyoisikia. Imejadili hali ya kutegemeana baina ya mbegu na ardhi; ardhi inastawisha mbegu na mbegu inafungamana na ardhi. Uhusiano kati ya hivi vitu viwili uliamuliwa kabla na Mungu kuanzia mwanzoni kabisa, sio? (Ndiyo.) Mti, mwanga wa jua, chiriku, na mwanadamu katika taswira hii, je, ni mifano ya mazingira hai ambayo Mungu aliyaumba kwa ajili ya mwanadamu? (Ndiyo.) Kwanza, je, mti unaweza kuiacha ardhi? (Hapana.) Je, mti unaweza kuishi bila mwanga wa jua? (Hapana.) Basi kusudi la Mungu la kuumba mti lilikuwa ni nini? Je, tunaweza kusema kuwa ilikuwa tu ni kwa ajili ya ardhi? Je, tunaweza kusema ilikuwa tu ni kwa ajili ya chiriku? Je, tunaweza kusema ilikuwa tu ni kwa ajili ya watu? (Hapana.) Kuna uhusianao gani kati yao? Uhusianao kati yao ni wa kutegemeana ambapo haviwezi kutengana. Yaani, ardhi, mti, mwanga wa jua, chiriku, na watu wanategemeana kwa ajili ya kuishi na wanaleana. Mti unailinda ardhi wakati ardhi inaulea mti; mwanga wa jua unatoa huduma kwa mti, wakati mti unatengeneza hewa nzuri kutoka katika mwanga wa jua, na husaidia kuituliza ardhi kutokana na joto la mwanga wa jua. Nani anayefaidika mwishoni? Mwanadamu ndiye anayefaidika, siyo? Na hii ndiyo kanuni juu ya kwa nini Mungu alifanya mazingira ya kuishi kwa ajili ya binadamu na ambaye ndiye lengo kuu kwa ajili yake. Ingawa hii ni taswira rahisi, tunaweza kuona hekima za Mungu na nia yake. Binadamu hawezi kuishi bila ardhi, au bila miti, au bila chiriku na mwanga wa jua, sio? Ingawa ilikuwa ni hadithi, ni mfano mdogo wa uumbaji wa Mungu wa ulimwengu na fadhili Zake za mazingira ya kuishi kwa mwanadamu.
Mungu aliumba mbingu na nchi na vitu vyote kwa ajili ya mwanadamu na pia akafanya mazingira ya kuishi. Kwanza, hoja kuu tuliyoijadili katika hadithi ni mwingiliano wa mahusiano na hali ya kutegemeana ya vitu vyote. Chini ya kanuni hii, mazingira ya kuishi kwa ajili ya binadamu yamelindwa, yanaendelea kuishi na kudumu; kwa sababu ya uwepo wa mazingira haya hai, mwanadamu anaweza akastawi na kuzaliana. Tuliona mti, ardhi, mwanga wa jua, na chiriku, na watu katika tukio. Mungu alikuwepo pia? Watu wanaweza wakose kuiona, sio? Lakini watu wanaweza kuona kanuni za mahusiano ya kuingiliana kati ya vitu katika tukio; ni kupitia kanuni hizi ndipo watu wanaweza kuona kwamba Mungu yupo na kwamba ni Mtawala. Mungu anatumia kanuni hizi na sheria kulinda uhai na uwepo wa vitu vyote. Ni kwa njia hii ndipo Anavikimu vitu vyote na Anamkimu binadamu. Je, hadithi hii ina uhusiano wowote na dhamira tuliyoijadili? Kwa juujuu inaonekana kama hakuna uhusiano, lakini kwa uhalisia, kanuni ambazo Mungu anazifanya kama Muumbaji na utawala Wake juu ya vitu vyote zinahusiana kwa karibu sana na Yeye kuwa chanzo cha uhai kwa vitu vyote na zimeunganika bila kuachana. Sio? (Ndiyo.) Umejifunza angalau kidogo, sio?
Mungu ni Bwana wa kanuni zinazoudhibiti ulimwengu, Anadhibiti kanuni zinazoongoza kuishi kwa vitu vyote, na pia Anadhibiti ulimwengu na vitu vyote kiasi kwamba vinaweza kuishi pamoja; Anaifanya ili kwamba visikwishe au kutoweka ili kwamba binadamu aendelee kuishi, binadamu anaweza kuishi katika mazingira hayo kupitia uongozi wa Mungu. Kanuni hizi zinazoongoza vitu vyote zipo chini ya utawala wa Mungu, na binadamu hawawezi kuingilia na hawawezi kuzibadilisha; ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anajua kanuni hizi na ni Yeye pekee ndiye anazisimamia. Ni lini miti itachipuka, ni lini mvua itanyesha, ni maji kiasi gani na virutubisho kiasi gani ardhi itaipatia mimea, ni katika msimu gani majani yatapukutika, ni katika msimu gani miti itazaa matunda, ni nishati kiasi gani jua litaipatia miti, miti itatoa nini kutoka katika nishati inayopata kutoka juani—haya ni mambo yote ambayo Mungu alikuwa amekwishayapangilia tayari Alipouumba ulimwengu na ni sheria ambazo haziwezi kuvunjwa na mwanadamu. Vitu vilivyoumbwa na Mungu—ama ni hai au vinaonekana kwa watu si hai—vyote vipo mikononi mwa Mungu na chini ya utawala Wake. Hakuna mtu anayeweza kubadilisha au kuvunja kanuni hii. Hii ni kusema, Mungu alipoviumba vitu vyote Aliweka kanuni ya jinsi vinavyopaswa kuwa. Miti isingeweza kuzamisha mizizi, kuchipua na kukua bila ardhi. Ardhi isingekuwa na miti, ingekauka. Sio? Pia, mti ni makazi ya chiriku, ni sehemu ambapo wanapata kujikinga dhidi ya upepo. Je, ingekuwa sawa ikiwa miti ingekuwa bila mwanga wa jua? (Isingekuwa sawa.) Ikiwa miti ingekuwa na ardhi peke yake hiyo isingefanya kazi. Hii yote ni kwa ajili ya mwanadamu na kuendelea kuishi kwa mwanadamu. Mwanadamu anapokea hewa safi kutoka kwenye miti, na anaishi katika ardhi inayomlinda. Mwanadamu hawezi kuishi bila mwanga wa jua, mwanadamu hawezi kuishi bila viumbe hai mbalimbali. Ingawa uhusiano baina ya vitu hivi ni changamani, mnapaswa kukumbuka kwamba Mungu alitengeneza kanuni ambazo zinaongoza vitu vyote ili kwamba viweze kuishi kwa kuhusiana na kutegemeana; kila kitu alichokiumba kina thamani na umuhimu. Ikiwa Mungu aliumba kitu bila kuwa na umuhimu, Mungu angeacha kipotee. Hii ni njia mojawapo Aliyoitumia katika kuvikimu vitu vyote. “Kukimu” kuna maana gani katika hadithi hii? Je, Mungu kila siku anatoka na kwenda kumwagilia mti maji? Je, mti unahitaji msaada wa Mungu ili uweze kupumua? (Hapana.) “Kukimu” hapa ina maana ya usimamizi wa Mungu wa vitu vyote baada ya uumbaji; Alichokuwa akikihitaji kilikuwa ni sheria ili kufanya vitu kwenda vizuri. Mti ulikuwa wenyewe kwa kupandwa ardhini. Masharti ili uweze kukua yote yalitengenezwa na Mungu. Alitengeneza mwanga wa jua, maji, udongo, hewa, na mazingira, upepo, umande, barafu, na mvua, na misimu minne; haya ndiyo masharti ambayo mti huyahitaji ili uweze kukua, hivi ni vitu ambavyo Mungu aliviandaa. Kwa hiyo, Mungu ni chanzo cha mazingira haya hai? (Ndiyo.) Je, Mungu analazimika kwenda kila siku na kuhesabu kila jani kwa miti? Hakuna haja, sio? Mungu pia hahitaji kuusaidia mti ili uweze kupumua. Mungu pia hahitaji kuuamsha mwanga wa jua kila siku kwa kusema, “Ni muda wa kuiangazia miti sasa.” Hana haja ya kufanya hivyo. Mwanga wa jua humulika wenyewe kama ulivyoamriwa na kanuni: inapohitajika, miti huufyonza huo mwanga na wakati mwanga hauhitajiki, mti huo bado huishi ndani ya kanuni. Pengine hamwezi kuelezea jambo hili kwa uwazi, lakini ni ukweli ambao kila mtu anaweza kuona na kuukubali. Chote unachopaswa kufanya ni kutambua kwamba kanuni kwa ajili ya uwepo wa vitu vyote inatoka kwa Mungu na jua kwamba ukuaji na kuishi kwao kupo chini ya utawala wa Mungu. Unaelewa, sio?
Je, istiari imetumika katika hadithi hii, kama watu wanavyoiita? (Hapana.) Je, ni hadithi iliyopewa sifa za kibinadamu? (Hapana.) Kile Nilichokizungumza ni ukweli. Kila kitu ambacho ni hai, kila kitu ambacho kina uhai kipo chini ya utawala wa Mungu. Kila kitu kilipewa uhai baada ya Mungu kukiumba; ni uhai uliotolewa kutoka kwa Mungu na unafuata sheria na njia Alizozitengeneza kwa ajili yake. Hii haihitaji kubadilishwa na mwanadamu, na haihitaji msaada kutoka kwa mwanadamu; hivi ndivyo Mungu anavyokimu vitu vyote. Unaelewa, sio? Je, unadhani ni lazima watu watambue hili? (Ndiyo.) Hivyo, hadithi hii ina uhusiano wowote na biolojia? Je, ina uhusiano wowote na uwanja wowote wa maarifa au sayansi? (Hapana.) Hatujadili biolojia hapa na hakika hatufanyi utafiti wa kibiolojia. Je, hoja kuu tunayoizungumzia hapa ni ipi? (Kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.) Hii ndiyo hoja muhimu. Mnaona nini miongoni mwa vitu vyote vya uumbaji? Mmeiona miti? Mmeiona ardhi? (Ndiyo.) Mmeuona mwanga wa jua, sio? Mmewaona ndege wakikaa mtini? (Ndiyo.) Je, mwanadamu anafurahia kuishi mazingira kama hayo? (Anafurahia.) Yaani, Mungu anatumia vitu vyote—vitu alivyoviumba—kudumisha makazi ya binadamu kwa ajili ya kuishi na kulinda makazi ya binadamu, na hivi ndivyo Anavyomkimu mwanadamu na anavyokimu vitu vyote.

Mnajisikiaje kuhusu kujadili Kwangu mambo kwa namna hii na kufanya Kwangu mawasiliano kwa namna hii? (Vizuri.) Ni vizuri? Ni vizuri kwa nini? (Ni rahisi kuelewa na kuna mifano ya vitendo ambayo ni halisi.) Hii ni njia ya kweli ya kujadili mambo, sio? Hadithi hii ni ya lazima kuwasaidia watu kutambua kuwa Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote? (Ndiyo.) Kama ni ya lazima, basi tutaendelea na hadithi inayofuata. Maudhui katika hadithi inayofuata ni tofauti kidogo na hoja kuu ni tofauti kidogo pia; mambo yaliyomo katika hadithi hii ni ambayo watu wanaweza kuona miongoni mwa uumbaji wa Mungu. Kwa mara nyingine tena Nitatumia njia ya kusimulia hadithi, ambayo ninyi nyote mnaweza kusikiliza mkiwa kimya na kutafakari juu ya kile Ninachokizungumzia. Baada ya kumaliza kusimulia hadithi, nitawauliza maswali kuona mmeelewa kiasi gani. Wahusika wakuu katika hadithi ni mlima mkubwa, kijito kidogo, upepo mkali, na wimbi kubwa.
Hadithi ya 2. Mlima Mkubwa, Kijito Kidogo, Upepo Mkali, na Wimbi Kubwa
Kulikuwa na kijito kidogo kilichotiririka kwa kuzungukazunguka, hatimaye kikawasili chini ya mlima mkubwa. Mlima ulikuwa unazuia njia ya kijito hiki, hivyo kijito kikauomba mlima kwa sauti yake dhaifu na ndogo, "Tafadhali naomba kupita, umesimama kwenye njia yangu na umenizibia njia yangu kuendelea mbele." Basi mlima ukauliza, "Unakwenda wapi?" Swali ambalo kijito kililijibu, "Ninatafuta makazi yangu." Mlima ukasema, "Sawa, endelea na tiririkia juu yangu!" Lakini kwa sababu kijito kilikuwa dhaifu sana na kichanga sana, hakukuwa na namna kwake kutiririka juu ya mlima mkubwa hivyo, hivyo hakikuwa na uchaguzi bali kuendelea kutiririka chini ya mlima...
Upepo mkali ukavuma, ukiwa umekusanya mchanga na vumbi kuelekea ambapo mlima ulikuwa umesimama. Upepo ukaungurumia mlima, "Hebu nipite!" Mlima ukauliza, "Unakwenda wapi?" Upepo ukavuma kwa kujibu, "Ninataka kwenda upande ule wa mlima." Mlima ukasema, "Sawa, kama unaweza kupenya katikati yangu, basi unaweza kwenda!" Upepo mkali ukavuma huku na kule, lakini haijalishi ulikuwa mkali kiasi gani, haukuweza kupenya katikati ya mlima. Upepo ukachoka na ukaacha ili upumzike. Hivyo katika upande ule wa mlima ni upepo dhaifu tu ndio ulivuma kwa vipindi, ambao uliwafurahisha watu waliopo kule. Hiyo ilikuwa ni salamu ambayo mlima ulikuwa unaitoa kwa watu ...
Ufukweni mwa bahari, mawimbi tulivu ya bahari yalizunguka taratibu kwenye mwamba. Ghafula, wimbi kubwa likaja na likanguruma kuelekea kwenye mlima. “Pisha!” wimbi kubwa lilipiga kelele. Mlima ukauliza, “Unakwenda wapi?” Wimbi kubwa halikusita, na likaendelea kutapakaa huku likijibu, “Ninapanua eneo langu na ninataka kunyoosha mikono yangu kidogo.” Mlima ukasema, “Sawa, kama utaweza kupita juu ya kilele changu, nitakupisha njia.” Wimbi kubwa likarudi nyuma kidogo, na kisha likavurumiza kuelekea mlimani. Lakini haijalishi lilijaribu kwa nguvu kiasi gani, halikuweza kufika juu ya mlima. Halikuwa na jinsi bali kurudi nyuma taratibu kurudi kule lilipotoka ...
Kwa karne nyingi kijito kidogo kilichururika taratibu kuzunguka chini ya mlima. Kwa kufuata njia ambayo mlima uliifanya, kijito kidogo kilifanikiwa kufika nyumbani; kilijiunga na mto, na kutiririka kwenda baharini. Chini ya uangalizi wa mlima, kijito kidogo hakikuweza kupotea. Kijito kidogo na mlima mkubwa walitumainiana, walizuiana, na kutegemeana.
Kwa karne nyingi, upepo mkali haukuacha tabia yake ya kuvuma kwenye mlima. Upepo mkali ulivumisha kimbunga "ulipoutembelea" mlima kama ulivyofanya kabla. Uliutisha mlima, lakini haukuwahi kupenya katikati ya mlima. Upepo mkali na mlima mkubwa walitumainiana, walizuiliana, na walitegemeana.
Kwa karne nyingi, wimbi kubwa wala halikupumzika, na kamwe halikuacha kupanuka. Lingenguruma na kuvurumiza tena na tena kwenda kwenye mlima, lakini mlima haukuwahi kusogea hata inchi moja. Mlima uliilinda bahari, na kwa namna hii viumbe ndani ya bahari viliongezeka na kustawi. Wimbi kubwa na mlima mkubwa walitumainiana, walizuiliana, na walitegemeana.
Hadithi hii imeishia hapo. Kwanza, mnaweza kuniambia nini kuhusu hadithi hii, maudhui makuu yalikuwa ni nini? Kwanza kulikuwa na mlima, halafu nini? (Kijito kidogo, upepo mkali, na wimbi kubwa.) Nini kilikitokea kijito kidogo na mlima mkubwa katika sehemu ya kwanza? Mnakumbuka? (Kijito kidogo kilikuwa kinatiririka chini ya mlima mkubwa.) Kijito kidogo kutiririka chini ya mlima, ndicho kisa kilichotokea kati yao? Kijito kilikwenda wapi? Kwa nini tuzungumze juu ya mlima mkubwa na kijito kidogo? (Kwa sababu mlima ulikilinda kijito, kijito hakikuweza kupotea. Walitegemeana.) Unaweza kusema kuwa mlima ulikilinda au kukizuia kijito kidogo? (Ulikilinda.) Inawezekana kuwa ulikizuia? Mlima na kijito kidogo vilikuwa pamoja; ulikilinda kijito, na pia ulikuwa ni kizuizi. Mlima ulikilinda kijito ili kiweze kutiririka kwenda mtoni, lakini pia ulikizuia kutiririka kutapakaa kila sehemu ambapo kingeweza kufurika na kuwa majanga kwa watu. Hii ndiyo hoja kuu ya sehemu hii? (Ndiyo.) Ulinzi wa mlima kwa kijito na kufanya kwake kazi kama kizuizi kulilinda makazi ya watu. Kisha unapata kijito kidogo kikiunganika na mto chini ya mlima na baadaye kutiririka kwenda baharini; je, huo si umuhimu wa kijito kidogo? Kijito kilipotiririka kwenda kwenye mto halafu kwenda baharini, kilikuwa kinategemea nini? Hakikuwa kinategemea mlima? Kilikuwa kinategemea ulinzi wa mlima na mlima kufanya kazi kama kizuizi; je, hii ndiyo hoja kuu? (Ndiyo.) Je, mnauona umuhimu wa milima kwa maji katika tukio hili? (Ndiyo.) Je, hiyo ni muhimu? (Ndiyo.) Je, Mungu ana makusudi Yake ya kutengeneza milima mirefu na mifupi? Kuna makusudi, sio? Hii ni sehemu ndogo ya hadithi, na kutoka tu katika kijito kidogo na mlima mkubwa tunaweza kuona thamani na umuhimu wa Mungu kuviumba vitu hivi viwili. Tunaweza pia kuona hekima Yake na makusudi katika jinsi ya kutawala vitu hivi viwili. Sivyo?
Sehemu ya pili ya hadithi inashughulika na nini? (Upepo mkali na mlima mkubwa.) Je, upepo ni kitu kizuri? (Ndiyo.) Sio lazima, kwa kuwa wakati mwingine ikiwa upepo ni mkali sana unaweza kuwa janga. Ungejisikiaje kama ungelazimika kukaa nje kwenye upepo mkali? Inategemea ulikuwa mkali kiasi gani, sio? Kama ukiwa ni upepo mwanana kidogo, au kama ukiwa ni upepo wa kiwango cha 3-4 basi bado ungeweza kuvumilika, angalau mtu anaweza kupata shida kuendelea kuacha macho wazi bila kufumba. Lakini ungeweza kuvumilia kama upepo ungevuma kwa nguvu na kuwa kimbunga? Usingeweza kuvumilia. Hivyo, ni kosa watu kusema kwamba siku zote upepo ni mzuri, au kwamba siku zote ni mbaya kwa sababu inategemeana na upepo ni mkali kiasi gani. Hivyo mlima una matumizi gani hapa? Je, kwa kiasi fulani haufanyi kazi kama kichujio cha upepo? Mlima unachukua upepo mkali na kuutuliza na kuwa nini? (Upepo mwanana.) Watu wengi wanaweza kuugusa na kuuhisi katika mazingira ambamo wanaishi—je, wanachohisi ni upepo mkali au upepo mwanana? (Upepo mwanana.) Je, hili sio kusudi mojawapo la Mungu la kuumba milima? Je, hii siyo nia Yake? Ingekuwaje kwa watu kuishi katika mazingira ambamo upepo mkali unavumisha vipande vya mchanga bila kitu chochote kuuzuia au kuuchuja? Inaweza kuwa kwamba na mchanga na mawe kuvumishwa, watu wasingeweza kusihi katika eneo hilo? Baadhi ya watu wanaweza kupigwa kichwani na mawe yanayoruka, au wengine wangeingiliwa na mchanga machoni mwao na hivyo kutoweza kuona. Watu wangemezwa kwenye hewa au upepo ungevuma kwa nguvu sana kiasi kwamba wasingeweza kusimama. Nyumba zingeharibiwa na kila aina ya majanga yangetokea. Je, upepo mkali una thamani? (Ndiyo.) Ni thamani gani hii? Niliposema kuwa ni mbaya, basi watu wangeweza kuhisi kwamba hauna thamani, lakini hiyo ni sahihi? Je, kubadilika kuwa upepo mwanana hakuna thamani? Watu wanahitaji nini zaidi kunapokuwa na unyevunyevu au kusongwa? Wanahitaji upepo mwanana kuwapepea, kuchangamsha na kusafisha vichwa vyao, kuamsha kufikiria kwao, kurekebisha na kuboresha hali zao za akili. Kwa mfano, nyote mmekaa chumbani kukiwa na watu wengi na hewa sio safi, ni kitu gani mtakihitaji zaidi? (Upepo mwanana.) Katika maeneo ambapo hewa imetibuliwa na imejaa uchafu inaweza kushusha uwezo wa kufikiri wa mtu, kupunguza mzunguko wao wa damu, na kuwafanya vichwa vyao visiwe vyepesi. Hata hivyo, hewa itakuwa safi ikiwa itapata nafasi ya kujongea na kuzunguka na watu watajihisi nafuu zaidi. Ingawa kijito kidogo na upepo mkali vingeweza kuwa janga, alimradi mlima upo utavibadilisha na kuwa vitu ambavyo kwa kweli vinawanufaisha watu; hiyo si kweli?
Sehemu ya tatu ya hadithi inazungumzia nini? (Mlima mkubwa na wimbi kubwa.) Mlima mkubwa na wimbi kubwa. Mandhari hapa ni mlima mkubwa uliopo kando ya bahari ambapo tunauona mlima, mawimbi tulivu ya bahari, na pia wimbi kubwa. Mlima ni nini kwa wimbi hapa? (Mlinzi na kinga.) Ni mlinzi na pia ni kinga. Lengo la kulinda ni kuilinda sehemu hii ya bahari isipotee ili kwamba viumbe vinavyoishi ndani yake viweze kuishi na kustawi. Kama kinga, mlima hulinda maji ya bahari—chanzo hiki cha maji—yasifurike na kusababisha janga, ambalo linaweza kudhuru na kuharibu makazi ya watu. Hivyo tunaweza kusema kwamba mlima ni kinga na mlinzi. Hii inaonyesha hali ya kutegemeana kati ya mlima na kijito, mlima na upepo mkali, na mlima na wimbi kubwa, na jinsi vinavyozuiliana na kutegemeana, ambayo nimezungumzia.
Kuna kanuni na sheria inayoongoza vitu hivi ambavyo Mungu aliviumba kuendelea kuishi. Mnaweza kuona kile ambacho Mungu alifanya kutokana na kile kilichotokea kwenye hadithi? Je, Mungu aliumba ulimwengu na kupuuzia kile kilichotokea baada ya hapo? Je, Alitoa kanuni na kuunda namna ambazo wao hufanya kazi na halafu kuwapuuza baada ya hapo? Je, hicho ndicho kilichotokea? (Hapana.) Ni nini hicho sasa? (Mungu Anadhibiti.) Mungu bado Anadhibiti maji, upepo na mawimbi. Haviachi bila udhibiti na haviachi vidhuru au kuharibu makazi ya watu, na kwa sababu hii watu wanaweza kuendelea kuishi na kustawi katika nchi hii. Kitu kinachomaanisha kwamba Mungu alikwishapanga kanuni kwa ajili ya kuishi Alipofanya mbingu. Mungu Alipotengeneza vitu hivi, Alihakikisha kwamba vingewanufaisha binadamu, na pia Alividhibiti ili kwamba visiwe shida au majanga kwa binadamu. Ikiwa havingesimamiwa na Mungu, je, maji yangetiririka kila mahali? Je, upepo usingevuma kila sehemu? Yanafuata sheria? Ikiwa Mungu hakuvisimamia visingeongozwa na kanuni yoyote, na upepo ungevuma na maji yangeinuka na kutiririka kila sehemu. Ikiwa wimbi kubwa lingekuwa refu kuliko mlima, je, sehemu hiyo ya bahari ingekuwa bado ipo? Bahari isingeweza kuwepo. Ikiwa mlima haungekuwa mrefu kama wimbi, eneo la bahari lisingekuwepo na mlima ungepoteza thamani na umuhimu wake.
Je, unaiona hekima ya Mungu katika visa viwili hivi? (Ndiyo.) Mungu aliumba ulimwengu na ni Bwana wake; Yeye ndiye Anausimamia na Anaukimu huku Akiangalia kila neno na tendo. Pia Anatazama kila pembe ya maisha ya mwanadamu. Hivyo Mungu Aliuumba ulimwengu na umuhimu na thamani ya kila kitu na vile vile kazi yake, asili yake, na kanuni zake kwa ajili ya kuendelea kuishi zinaeleweka vizuri Kwake kama kiganja cha mkono wake. Mungu Aliuumba ulimwengu; unadhani Anapaswa kufanya utafiti juu ya kanuni hizi zinazouongoza ulimwengu? Je, Mungu Anahitajika kusoma maarifa au sayansi ya kibinadamu kufanya utafiti na kuyaelewa? (Hapana.) Je, kuna mtu yeyote miongoni mwa binadamu ambaye ana elimu kubwa na hekima ya kutosha kuelewa mambo yote kama Mungu Anavyoelewa? Hakuna. Sio? Je, kuna mamajusi au wanabiolojia ambao wanaelewa kweli jinsi ambavyo vitu vinaishi na kukua? Je, wanaweza kweli kuelewa thamani ya uwepo wa kila kitu? (Hawawezi.) Kwa nini? Vitu vyote viliumbwa na Mungu, na haijalishi ni kwa kiasi kikubwa au kwa kina kiasi gani binadamu anajifunza maarifa haya, au ni kwa muda mrefu kiasi gani wanajitahidi kujifunza, hawataweza kuelewa siri na makusudi ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, hiyo si sahihi? (Ndiyo.)
Januari 18, 2014
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi:  Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu,  Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni