Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Uendelezo wa Sehemu ya Kwanza
Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Hakuna Awezaye Kuzuia Kazi Ambayo Mungu Anaamua Kufanya
Kazi ya Usimamizi wa Mungu na Wokovu wa Wanadamu Yaanza na Ibrahimu Kumtoa Isaka
Mungu Hajali Kama Binadamu Ni Mjinga—Anahitaji Tu Binadamu Awe Mkweli
Binadamu Anapata Baraka za Mungu kwa Sababu ya Uaminifu na Utii Wake
Kuwapata Wale Wanaomjua Mungu na Wanaoweza Kumshuhudia Ndilo Tamanio la Mungu Lisilobadilika
Mwenyezi Mungu anasema, “Mnaona nini katika ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu? Mungu alimpa baraka kuu Ibrahimu kwa sababu tu ya yeye kusikiliza maneno ya Mungu. Ingawaje, juujuu, hali hii yaonekana ya kawaida na suala ambalo bila shaka, ndani yake tunauona moyo wa Mungu: Mungu hasa anathamini utiifu wa binadamu kwake Yeye, na hutunzwa mno na uelewa wa binadamu kuhusu Yeye na uaminifu wake Kwake. Mungu anathamini kiasi kipi uaminifu huu? Huenda msielewe ni kiasi kipi ambacho Yeye Anauthamini, na huenda hata kusiwe na yeyote anayeutambua. Mungu alimpa Ibrahimu mwana, na wakati mwana huyo alipokua, Mungu alimwomba Ibrahimu kumkabidhi mtoto wake Kwake. Ibrahimu alifuata amri ya Mungu kwa umakinifu, alitii neno la Mungu na uaminifu wake ulimpendeza Mungu na ukathaminiwa sana na Mungu. Mungu aliuthamini kiasi kipi? Na kwa nini Akauthamini sana? Kwa wakati ambao hakuna aliyefahamu maneno ya Mungu au kuuelewa moyo Wake, Ibrahimu alifanya kitu kilichotikisa mbingu na kutetemesha ardhi, na kikafanya Mungu kuhisi hali fulani ya kutosheka kwa mara ya kwanza, kikamletea Mungu furaha ya kumpata mtu ambaye aliweza kutii maneno Yake. Uradhi na furaha hii ilitoka kwa kiumbe aliyeumbwa kwa mikono ya Mungu, na ndiyo iliyokuwa “sadaka” ya kwanza ambayo binadamu aliwahi kumpa Mungu na ambayo ilithaminiwa sana na Mungu, tangu binadamu kuumbwa. Mungu alikuwa na wakati mgumu kusubiria sadaka hii, na Aliichukulia kama zawadi ya kwanza muhimu zaidi kutoka kwa binadamu, ambaye Alikuwa amemuumba. Hii ilionyesha Mungu tunda la kwanza la jitihada Zake, na gharama ambayo Alikuwa amelipia na ikamruhusu Yeye kuliona tumaini kwa wanadamu. Baadaye, Mungu alikuwa na hata tamanio kubwa zaidi la kundi la watu kama hao wa kushinda na Yeye kumchukulia Yeye kwa uaminifu, kumtunza Yeye kwa uaminifu. Mungu alitamani hata kwamba Ibrahimu angeendelea kuishi, kwani Alipenda kuwa na moyo kama huo ukiandamana na Yeye na kuwa na Yeye Alipoendelea na usimamizi Wake. Haijalishi ni nini alichotaka Mungu, yalikuwa tu ni matakwa, wazo tu—kwani Ibrahimu alikuwa tu binadamu aliyeweza kumtii Yeye, na wala hakuwa na uelewa au maarifa hata madogo zaidi kuhusu Mungu. Yeye alikuwa mtu aliyepungukiwa pakubwa na viwango vya mahitaji ya Mungu kwa binadamu: kumjua Mungu, kuweza kushuhudia Mungu, na kuwa na akili sawa na Mungu. Na hivyo, hangeweza kutembea na Mungu. Katika sadaka ya Ibrahimu ya Isaka, Mungu aliuona uaminifu na utiifu huu wa Ibrahimu, na Akaona kwamba alikuwa amestahimili jaribio la Mungu kwake yeye. Hata ingawaje Mungu aliukubali uaminifu na utiifu wake, bado hakustahili kuwa mwandani wa Mungu, wa kuwa mtu aliyemjua Mungu, na kumwelewa Mungu, na alifahamishwa kuhusu tabia ya Mungu; alikuwa mbali sana na kuwa na akili sawa na Mungu na vilevile kuweza kufanya mapenzi ya Mungu. Hivyo basi, katika moyo Wake, Mungu alikuwa bado mpweke na mwenye wasiwasi. Kwa kadri Mungu alipokuwa mpweke na mwenye wasiwasi zaidi, ndipo Yeye alipohitaji zaidi kuendelea na usimamizi Wake haraka iwezekanavyo, na kuweza kuchagua na kulipata kundi la watu wa kukamilisha mpango Wake wa usimamizi na kutimiza mapenzi Yake haraka iwezekanavyo. Hili ndilo lilikuwa tamanio lenye hamu kubwa la Mungu, na limebakia vilevile kuanzia mwanzo kabisa hadi leo. Tangu Alipomuumba binadamu hapo mwanzo, Mungu ametamani kuwa na kundi la washindi, kundi ambalo litatembea na Yeye na linaweza kuelewa, kufahamu na kujua tabia Yake. Mapenzi haya ya Mungu hayajawahi kubadilika. Haijalishi ni muda gani bado Atasubiria, haijalishi barabara iliyo mbele ni ngumu kiasi gani, hata malengo Anayoyatamani yawe mbali kiasi kipi, Mungu hajawahi kubadilisha au kukata tamaa katika matarajio Yake kuhusu binadamu. Kwa vile nimeyasema haya, mnatambua chochote kuhusu mapenzi ya Mungu? Pengine kile ulichotambua hakina uzito sana—lakini kitajitokeza kwa utaratibu!”
Yaliyopendekezwa: Neno la Mungu |“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu I” Sehemu ya Pili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni