Smiley face

Jumapili, 28 Aprili 2019

Wimbo wa Kuabudu |Maneno Ya Mungu Ni Ukweli Usiobadilika Milele



Wimbo wa Kuabudu |Maneno Ya Mungu Ni Ukweli Usiobadilika Milele        

     I
Maneno ya Mungu ni ukweli, usiobadilika milele.
Mungu ndiye mpaji wa uzima,
na kiongozi pekee wa mwanadamu.
Thamani na maana ya maneno Yake
yanaamuliwa na kiini chao,
sio kama mwanadamu anayakubali au kuyatambua.
Hata kama hakuna mwanadamu ulimwenguni
anayapokea maneno Yake,
thamani yao na usaidizi kwa mwanadamu hayapimiki.
Maneno ya Mungu ni ukweli, usiobadilika milele.
Mungu ndiye mpaji wa uzima,
na kiongozi pekee wa mwanadamu.

     II
Kwa wale wanaoasi, kupinga na kutoheshimu maneno Yake,
Jibu pekee la Mungu kwao ni hili:
Acha muda na ukweli uwe shahidi Wake,
uonyeshe maneno Yake ni ukweli, njia na uzima;
uonyeshe kuwa yote Aliyosema ni kweli,
ni kile ambacho mwanadamu anafaa kuwa nacho na kufuata.
Maneno ya Mungu ni ukweli, usiobadilika milele.
Mungu ndiye mpaji wa uzima,
na kiongozi pekee wa mwanadamu.

     III
Kwa wale wote wanaomfuata
Mungu atawaruhusu kuona ukweli huu:
Wale ambao hawakubali maneno Yake
au kuyatekeleza katika matendo yao,
na wale ambao hawawezi kugundua kusudi
ama wanaokosa kupata wokovu katika maneno Yake,
Hawa wote ni wale watu ambao maneno ya Mungu yamewalaani.
Wamepoteza wokovu wa Mungu.
Kutoka kwao, adhabu Yake haitapotea mbali
Maneno ya Mungu ni ukweli, usiobadilika milele.
Mungu ndiye mpaji wa uzima,
na kiongozi pekee wa mwanadamu.
Maneno ya Mungu ni ukweli, usiobadilika milele.
Mungu ndiye mpaji wa uzima,
na kiongozi pekee wa mwanadamu.

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

    Sikiliza zaidi:Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni