Smiley face

Jumapili, 19 Mei 2019

"Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)" Sehemu ya Kwanza




"Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)" Sehemu ya Kwanza


         Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii: Jinsi Mungu Anavyotawala na Kuongoza Ulimwengu wa Kiroho 1. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Wasioamini 2. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Mbalimbali Wenye Imani

Mwenyezi Mungu anasema:

Leo, tunafanya ushirika juu ya mada maalum. Kwa kila mmoja wenu, kuna vitu viwili vikuu tu ambavyo mnapaswa kujua, kuvipitia na kuvielewa—na vitu hivi viwili ni vipi? Cha kwanza ni kuingia binafsi kwa watu katika maisha, na cha pili kinahusu kumjua Mungu. Leo Nawapa uchaguzi: Chagua kimoja. Mngependa kusikia kuhusu mada inayouhusu uzoefu wa maisha ya kibinafsi ya watu, au mngependa kusikia inayohusu kumjua Mungu Mwenyewe? Na kwa nini Ninawapa uchaguzi huu? Kwa sababu leo Ninafikiria kufanya ushirika nanyi juu ya mambo mapya kuhusu kumjua Mungu. Lakini, hata hivyo, kwanza nitawaacha mchague kimoja kati ya vitu viwili ambavyo Nimezungumzia hivi punde. (Ninachagua kuhusu kumjua Mungu.) (Tunafikiri kwamba kufanyia ushirika maarifa ya Mungu ni bora pia.) Mnadhani mambo ambayo tumekuwa tukiyafanyia ushirika hivi karibuni kuhusu kumjua Mungu yanawezekana? Ni haki kusema kuwa ni nje ya uwezo wa watu wengi. Mwaweza kukosa kusadiki maneno haya. Kwa nini Ninasema hili? Kwa sababu mlipokuwa mkisikiliza Niliyokuwa nikisema awali, haijalishi Niliyasema vipi, au ni kwa maneno gani, moja kwa moja na kinadharia mlikuwa mnatambua Nilichokuwa nikisema, lakini tatizo lenu kubwa ni kwamba, hamkuelewa ni kwa nini Niliyasema mambo haya, ni kwa nini nilizizungumzia hizi mada. Hiki ndicho kiini cha hili suala.

Tazama Video: Matamshi ya Mungu | "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I)" Sehemu ya Pili
        Yaliyopendekezwa: Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni