Smiley face

Jumatatu, 26 Agosti 2019

Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Manne ya Neno la Mungu Juu ya “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi” (Sehemu ya Kwanza)



1. Wanadamu kwa kupotoshwa sana na Shetani, hawajui kuwa kuna Mungu na wameacha kumwabudu Mungu. Adamu na Hawa walipoumbwa mwanzoni, utukufu wa Yehova na Ushuhuda wa Yehova daima vilikuwepo. Lakini baada ya kupotoshwa, mwanadamu alipoteza utukufu na ushuhuda kwa sababu kila mtu alimwasi Mungu na kuacha kumtukuza kabisa. Kazi ya sasa ya kushinda ni kuupata ushuhuda na utukufu wote, na kuwafanya wanadamu wote wamwabudu Mungu, ili kuwepo na ushuhuda miongoni mwa viumbe wote. Hili ndilo linapaswa kufanywa katika hatua hii ya kazi. Wanadamu watashindwa vipi hasa? Watapata kushindwa kwa kutumia hii kazi ya maneno kumshawishi mwanadamu kwa dhati; kwa kutumia toba, hukumu, kuadibu, na laana isiyo na huruma dhibiti kabisa; na kwa kuweka wazi uasi wa mwanadamu na kwa kuhukumu upinzani wake ili ajue udhalimu wa mwanadamu na uchafu wake, mambo ambayo yatatumiwa kuangazia tabia ya haki ya Mungu. Kwa kiwango kikubwa, ni matumizi ya maneno haya yatakayomshinda mwanadamu na kumshawishi kabisa. Maneno ndiyo njia ya kuwashinda wanadamu na wote wanaokubali ushindi lazima wakubali mapigo na hukumu ya maneno. Mchakato wa sasa wa kunena ni mchakato wa kushinda. Ni kwa njia gani watu wanapaswa hasa kushirikiana? Ni kwa kula na kunywa haya maneno ipasavyo na kuyafahamu. Watu hawawezi kujipatia ushindi wao wenyewe. Ni lazima, kwa kula na kunywa haya matamshi, wapate kufahamu uovu na uchafu wao, uasi na udhalimu wao, na waanguke chini mbele ya Mungu. Ikiwa waweza kufahamu mapenzi ya Mungu kisha uyatie katika vitendo, na zaidi, uwe na maono, na ikiwa waweza kuyatii maneno haya kabisa na usitende kulingana na mapenzi yako, basi utakuwa umeshindwa. Na itakuwa ni haya maneno yamekuwezesha kushindwa. Ni kwa nini wanadamu walipoteza ushuhuda? Ni kwa sababu hakuna aliye na imani kwa Mungu au anamshikilia Mungu rohoni mwake. Kuwashinda wanadamu kunamaanisha watu wairudie hii imani. Watu daima wanauegemea ulimwengu, wakiwa na matumaini mengi sana, wakitaka kujua mengi sana kwa ajili ya maisha yao ya usoni, na wakiwa na mahitaji mengi ya kupita kiasi. Wanaifikiria na kuipangia miili yao kila mara wala hawatamani kutafuta njia ya kumwamini Mungu. Roho zao zimetekwa na Shetani, wameacha kumheshimu Mungu, na wanatoa mioyo yao kwa Shetani. Ila mwanadamu aliumbwa na Mungu. Hivyo, mwanadamu amepoteza ushuhuda, kumaanisha amepoteza utukufu wa Mungu. Kusudi la kumshinda mwanadamu ni kuurejesha utukufu wa mwanadamu wa kumheshimu Mungu.

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

2. Kazi ya sasa ya kushinda ni kazi inayokusudiwa kuweka wazi hatima ya mwanadamu itakuwaje. Ni kwa nini Ninasema kuwa kuadibu na hukumu ni hukumu mbele ya kiti cha enzi kikubwa cheupe cha siku za mwisho? Hulioni hili? Ni kwa nini kazi ya kushinda ni hatua ya mwisho? Je, si kudhihirisha kwa usahihi hatima ya kila tabaka la wanadamu? Si kumruhusu kila mtu, katika harakati ya kazi ya kushinda ya kuadibu na hukumu, kuonyesha tabia zake halisi na kisha kuwekwa katika aina yake baadaye? Badala ya kusema kuwa huku ni kuwashinda wanadamu, inaweza bora kusema kuwa huku ni kuonyesha hatima ya kila aina ya mwanadamu. Yaani, huku ni kuhukumu dhambi zao halafu kuonyesha matabaka mbalimbali ya wanadamu, na kwa njia hiyo kubaini kama ni waovu au ni wenye haki. Baada ya kazi ya kushinda, kazi ya kutuza mazuri na kuadhibu maovu inafuata: watu wanaotii kabisa, yaani walioshindwa kabisa, watawekwa katika hatua nyingine ya kusambaza kazi ulimwenguni kote; wasioshindwa watawekwa gizani na watapatwa na majanga. Hivyo mwanadamu ataainishwa kulingana na aina yake, watenda maovu watawekwa pamoja na maovu, wasiuone mwangaza tena, na wenye haki watawekwa pamoja na mazuri, ili kupokea mwangaza na kuishi milele katika mwangaza. Mwisho wa vitu vyote u karibu, mwisho wa mwanadamu umebainishwa wazi machoni mwake, na vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina yake. Ni vipi basi wanadamu wataepuka kuathiriwa na kuanisha huku? Kufichua mwisho kwa kila jamii ya mwanadamu kutafanywa hatima ya kila kitu ikikaribia, na kutafanywa wakati wa kazi ya kushinda ulimwengu mzima (ikiwemo kazi yote ya kushinda kuanzia kazi ya sasa). Huku kufichua mwisho wa wanadamu kunafanywa mbele ya kiti cha hukumu, katika harakati ya kuadibu, na harakati ya kazi ya kushinda ya siku za mwisho.

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

3. Hatima ya mwanadamu si kitu kilichoamuliwa kabla tangu uumbaji wa dunia. Hii ni kwa sababu mwanzoni kulikuwa na jamii moja tu, ambayo kwa pamoja iliitwa “wanadamu,” na kwa sababu mwanadamu alikuwa bado hajapotoshwa na Shetani, na wanadamu wote waliishi katika mwangaza wa Mungu, bila giza kuwaandama. Lakini baada ya mwanadamu kupotoshwa na Shetani, kila jamii na aina ya watu walitapakaa ulimwenguni kote—kila jamii na aina ya watu waliotokana na ukoo mmoja ujulikanao kwa pamoja kama “wanadamu” uliojumuisha mwanamke na mwanamume. Wote walipotoshwa na mababu zao kutoka kwa nia za mababu zao wa kale sana—wanadamu waliojumuisha mwanamke na mwanamume (yaani, Adamu na Hawa wa asili, mababu zao wa kale sana). Wakati huo, watu wa pekee duniani walioongozwa na Yehova walikuwa Waisraeli. Watu wa aina mbalimbali walioibuka kutoka Israeli nzima (yaani kutoka ukoo wa asili) wakati ule walipoteza uongozi wa Mungu. Watu hawa wa mwanzo, wasiofahamu kabisa masuala ya ulimwengu wa wanadamu, walienda na mababu zao kuishi katika maeneo waliyodai kumiliki, mpaka wa leo. Hivyo hawatambui walipotoka vipi kutoka kwa Yehova na jinsi wamepotoshwa mpaka leo na aina yote ya pepo wachafu na roho waovu. Waliopotoshwa zaidi na kutiwa sumu mpaka leo hii, yaani ambao hatimaye hawawezi kukombolewa, hawatakuwa na budi ila tu kufuata mababu zao—pepo wachafu waliowapotosha. Wale wanaoweza kukombolewa hatimaye watakwenda hatima inayostahili wanadamu, yaani sehemu iliyotengwa kwa ajili ya waliokombolewa na walioshindwa. Kila kitu kitafanywa ili kukomboa wanaoweza kukombolewa, ila wale wasiosikia, watu wasioweza kutibika, chaguo lao pekee litakuwa kuwafuata mababu zao katika kuzimu ya kuadibu. Usidhani kuwa hatima yako iliamuliwa kabla tangu mwanzo na imefichuliwa tu sasa. Ikiwa unadhani hivyo, basi, umesahau kuwa katika uumbaji wa mwanzo wa wanadamu, hakukuumbwa jamii tofauti ya Shetani? Je, umesahau kuwa ni aina moja tu ya mwanadamu, yaani Adamu na Hawa, ndiyo iliumbwa (ikiwa na maana kwamba ni mwanamume na mwanamke tu ndio waliumbwa)? Ungalikuwa uzao wa Shetani kutoka mwanzo, je, hilo halingemaanisha kuwa Yehova alipomuumba mwanadamu Alijumuisha jamii ya Shetani? Je, Angefanya jambo kama hilo? Alimuumba mwanadamu kwa ajili ya ushuhuda Wake; Alimuumba mwanadamu kwa ajili ya utukufu Wake. Angeumbaje kwa makusudi jamii ya vizazi vya Shetani ili kumuasi kwa makusudi? Je, Yehova angeweza kufanya hili? Ikiwa hivyo, ni nani angeweza kusema kuwa Yeye ni Mungu Mwenye haki? Nikisema sasa kuwa baadhi yenu mwishowe mtaenda na Shetani, haimaanishi kuwa ulikuwa na Shetani toka mwanzo; ila, inamaanisha umejishusha chini sana hivi kwamba japo Mungu amejaribu kukukomboa, bado umekosa kuupata ukombozi huo. Hakuna budi ila kukuweka katika jamii moja na Shetani. Hii ni kwa sababu huwezi kukombolewa, si kwa sababu Mungu si mwenye haki kwako, yaani, si kwa sababu Mungu kimakusudi alipangia majaliwa yako kama mfano halisi wa Shetani na baadaye kukuweka katika jamii moja na Shetani na kutaka uteseke kwa makusudi. Huo si ukweli wa ndani wa kazi ya kushinda. Ikiwa unaamini hilo, basi ufahamu wako unaegemea upande mmoja sana!

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

4. Hatua ya mwisho ya kushinda ni ya kukomboa watu na vilevile kufichua mwisho wa kila mtu. Inaweka wazi upotevu wa watu kupitia hukumu na kwa njia hiyo kuwafanya watubu, waamke, na kufuatilia uzima na njia ya haki ya maisha ya mwanadamu. Ni ya kuamsha mioyo ya waliolala na wapumbavu na kuonyesha, kwa njia ya hukumu, uasi wao wa ndani. Hata hivyo, ikiwa watu bado hawawezi kutubu, bado hawawezi kufuata njia ya haki ya maisha ya mwanadamu na hawawezi kuutupa upotovu huu, basi watakuwa vyombo visivyoweza kukombolewa vya kumezwa na Shetani. Hii ndiyo maana ya kushinda—kuwakomboa watu na vilevile kuwaonyesha mwisho wao. Mwisho mzuri, mwisho mbaya—yote yanafichuliwa na kazi ya kushinda. Kama watu watakombolewa au kulaaniwa yote yanafichuliwa wakati wa kazi ya kushinda.

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

5. Siku za mwisho ni wakati ambao vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina zake kupitia kushinda. Kushinda ni kazi ya siku za mwisho; kwa maneno mengine, kuhukumu dhambi za kila mtu ni kazi ya siku za mwisho. La sivyo, watu wangeainishwa vipi? Kazi ya kuainisha inayofanywa miongoni mwenu ni mwanzo wa kazi ya aina hiyo ulimwenguni kote. Baada ya hii, watu wa kila mataifa vilevile watapitia kazi ya kushinda. Hii inamaanisha kuwa watu wote wataainishwa kimakundi na kufika mbele ya kiti cha hukumu kuhukumiwa. Hakuna mtu na hakuna kitu kitakachoepuka kupitia huku kuadibu na hukumu, na hakuna mtu au kitu kinaweza kukwepa uainishaji huu; kila mtu atawekwa katika jamii. Hii ni kwa sababu mwisho u karibu kwa vitu vyote na mbingu zote na dunia zimefikia hatima yake. Mwanadamu anawezaje kukwepa hatima ya maisha yake?

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

6. Sasa hivi Ninatumia kazi ya hawa watu walio Uchina kufichua tabia zao zote za uasi na kuufunua ubaya wao wote. Huu ndio usuli wa kusema kila Ninachotaka kusema. Baadaye Nitafanya hatua nyingine ya kazi ya kuushinda ulimwengu wote. Nitatumia hukumu Yangu kwenu kuhukumu udhalimu wa kila mtu duniani kote kwa sababu ninyi watu ndio wawakilishi wa waasi miongoni mwa wanadamu. Wasiojikakamua watakuwa foili[a] na vyombo vya kuhudumu tu, ila watakaojikakamua watatumika vizuri. Ni kwa nini Ninasema watakuwa foili[a]? Ni kwa sababu maneno na kazi Yangu ya sasa vinalenga usuli wenu na kwa sababu mmekuwa wawakilishi na vielelezo vya uasi miongoni mwa wanadamu. Baadaye Nitapeleka maneno haya yanayowashinda kwa nchi za kigeni na kuyatumia kuwashinda watu wa huko, ila hutakuwa umeyafaidi. Je, hilo halitakufanya foili[a]? Tabia potovu za wanadamu wote, matendo ya uasi wa mwanadamu, maumbile na sura mbaya za mwanadamu, zimeratibiwa zote katika maneno yanayotumiwa kuwashinda nyinyi. Baadaye Nitayatumia maneno haya kuwashinda watu wa kila taifa na kila dhehebu kwa sababu nyinyi ni mfano, kigezo. Hata hivyo, Sikupanga kuwaacha kwa makusudi; ukikosa kufanya vizuri katika utafutaji wako na kwa hivyo unathibitisha kuwa asiyeponyeka, hautakuwa tu chombo cha huduma na foili[a]?

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

7. Leo hii ni imani inayokuruhusu kushindwa, na kushindwa ndiko kunakufanya uamini kila tendo la Yehova. Ni kwa sababu tu ya imani unapokea kuadibu na hukumu ya aina hii. Kupitia kuadibu na hukumu hizi, umeshindwa na kukamilishwa. Bila aina hii ya kuadibu na hukumu upokeayo leo hii, imani yako ingekuwa bure. Kwa sababu humtambui Mungu, haijalishi unamwamini kiasi gani, imani yako bado itakuwa maonyesho matupu yasiyokuwa na misingi katika uhalisi. Ni baada tu ya kupokea aina hii ya kazi ya kushinda inayokufanya mtiifu kabisa ndipo imani yako inakuwa kweli na inayotegemewa na roho yako kumrudia Mungu. Japo umehukumiwa na kulaaniwa sana kwa sababu ya hili neno “imani,” una imani ya kweli, na unapokea kitu cha kweli zaidi, halisi zaidi, na chenye thamani zaidi. Hii ni kwa sababu ni katika harakati ya hukumu tu ndipo unaona hatima ya viumbe wa Mungu; ni katika hukumu hii ndio unapata kuona kuwa Muumba anapaswa kupendwa; ni katika kazi kama hiyo ya kushinda ndio unapata kuona mkono wa Mungu; ni katika kushinda huku unapata kutambua kwa ukamilifu maisha ya mwanadamu; ni katika kushinda huku unapata kujua njia ya haki ya maisha ya mwanadamu na kufahamu maana ya kweli ya “mwanadamu”; ni kupitia tu huku kushinda ndiko unaweza kuona tabia ya haki ya mwenye Uweza na uso Wake mzuri na mtukufu. Ni katika kazi hii ya kushinda ndiko unaweza kujifunza kuhusu asili ya mwanadamu na kufahamu “historia isiyokufa” ya mwanadamu; ni katika kushinda huku ndiko unapata kufahamu mababu za wanadamu na asili ya upotovu wa mwanadamu; ni katika kushinda huku ndio unapokea furaha na starehe pamoja na kuadibu, nidhamu, na maneno ya kuonya kutoka kwa Muumba kwa wanadamu ambao Aliwaumba; katika kazi hii ya kushinda, ndipo unapokea baraka na majanga ambayo mwanadamu anapaswa kupokea…. Je, haya yote si kwa ajili ya hiyo imani yako ndogo? Je, baada ya kuvipata vitu hivi vyote imani yako haijakua? Hujapata kiwango kikubwa ajabu?

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

8. Labda utasema kuwa usingekuwa na imani, basi usingepata aina hii ya kuadibu au aina hii ya hukumu. Ila unapaswa kufahamu kuwa bila imani, usingeweza tu kupokea aina hii ya kuadibu na ulinzi kutoka kwa mwenye Uweza, bali pia daima ungepoteza fursa ya kumwona Muumba. Usingejua asili ya wanadamu na kufahamu umuhimu wa maisha ya mwanadamu. Japo mwili wako utakufa na roho yako kuondoka, bado hutayafahamu matendo yote ya Muumba. Aidha hutafahamu kuwa Muumba alifanya kazi kubwa kiasi hicho duniani baada ya kuwaumba wanadamu. Kama mmojawapo wa hawa wanadamu Aliowaumba, je, uko tayari kutumbukia gizani kiasi hiki bila fahamu na kukumbana na adhabu ya milele? Ukijitenga na kuadibu na hukumu ya sasa, utapatana na kitu gani? Je, unafikiri ukishajitenga na hukumu ya sasa, utaweza kuepukana na haya maisha magumu? Je, si kweli kwamba ukiondoka “mahala hapa,” utakachokipata ni mateso machungu au majeraha kutoka kwa ibilisi? Je, waweza kukumbana na mchana na usiku zisizostahimilika? Je, unafikiri kwamba kwa kuepuka hukumu leo, unaweza kukwepa milele yale mateso ya siku zijazo? Ni kitu gani kitakukumba? Inaweza kuwa paradiso ya duniani unayoitarajia? Unafikiri unaweza kuepuka kuadibu kwa milele kwa baadaye kwa kuukimbia uhalisi kama ufanyavyo? Baada ya leo, je, utawahi kuweza kuipata fursa na baraka kama hii tena? Je, utapata fursa na baraka utakapokuwa umekumbwa na misukosuko? Je, utapata fursa na baraka wanadamu wote waingiapo katika pumziko? Maisha yako ya furaha ya sasa na hiyo familia yako ndogo yenye amani—vyaweza kuwa kibadala cha hatima yako? Iwapo una imani ya kweli, na iwapo unafaidi pakubwa kwa sababu ya imani yako, basi hayo yote ndiyo—wewe kiumbe—unapaswa kufaidi na vilevile kile ambacho ulipaswa kuwa nacho. Aina hii ya kushinda ndiyo ya faida zaidi kwa imani na maisha yako.

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

9. Leo, unapaswa kuelewa namna ya kushindwa, na jinsi watu wanavyofanya baada ya kushindwa. Unaweza kusema umeshashindwa, lakini unaweza kutii hata kufa? Unapaswa uwe na uwezo wa kufuata hadi mwisho kabisa bila kujali kama kuna matumaini yoyote, na hupaswi kupoteza imani kwa Mungu bila kujali mazingira. Mwishowe, unapaswa kutimiza hali mbili za ushuhuda: ushuhuda wa Ayubu—utii hata kifo—na ushuhuda wa Petro—upendo mkuu wa Mungu. Kwa upande mmoja, unapaswa kuwa kama Ayubu: Hakuwa na mali hata kidogo, na alisumbuliwa na maumivu ya mwili, lakini hakulikana jina la Yehova. Huu ulikuwa ushuhuda wa Ayubu. Petro aliweza kumpenda Mungu hadi kifo. Alipokufa—alipoangikwa msalabani—bado alimpenda Mungu; hakufikiria juu ya matarajio yake mwenyewe au kufuatilia mambo yaliyo makuu au fikra za anasa, na alitafuta tu kumpenda Mungu, na kutii mipango yote ya Mungu. Hicho ndicho kiwango unachopaswa kutimiza kabla hujahesabiwa kuwa kuwa na ushuhuda, kabla hujawa mtu ambaye amefanywa mkamilifu baada ya kushindwa. Leo, ikiwa watu wangekuwa wanajua kabisa hulka na hadhi yao, je, bado wangetafuta matarajio yao na matumaini yao? Unachopaswa kujua ni hiki: Bila kujali kama Mungu atanifanya mkamilifu, ni lazima nimfuate Mungu; kila kitu anachofanya sasa ni chema, na kwa ajili yetu, na ili tabia yetu iweze kubadilika na tuweze kuepukana na ushawishi wa Shetani, kuturuhusu kuishi katika nchi ya uchafu na hata hivyo kuepukana na uchafu, kuondoa uchafu na ushawishi wa Shetani, kutuwezesha kuacha nyuma ushawishi wa Shetani.

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

10. Kwa kweli, ukamilifu hutokea wakati mmoja na ushindi: Unaposhindwa, matokeo ya kwanza ya kufanywa mkamilifu pia yanatimizwa. Panapokuwa na tofauti kati ya kushindwa na kufanywa mkamilifu, ni kulingana na kiwango cha mabadiliko kwa watu. Kushindwa ni hatua ya kwanza ya kufanywa mkamilifu, na haimaanishi kwamba wamefanywa wakamilifu kabisa, wala kuthibitisha kwamba wamepatwa na Mungu kabisa. Baada ya watu kushindwa, kunakuwa na mabadiliko fulani katika tabia yao, lakini mabadiliko hayo ni pungufu sana yakilinganishwa na mabadiliko ya watu ambao wamepatwa kabisa na Mungu. Leo, kile kinachofanywa ni kazi ya mwanzo ya kuwafanya watu kuwa wakamilifu—kuwashinda—na kama huwezi kutimiza kushindwa, basi hutaweza kuwa na uwezo wa kufanywa mkamilifu na kupatwa kabisa na Mungu. Utapata tu maneno machache ya kuadibu na hukumu, lakini hayatakuwa na uwezo wa kuubadilisha kabisa moyo wako. Hivyo utakuwa mmoja wa wale ambao wameondolewa; haitakuwa tofauti na kutazama tu karamu ya gharama mezani lakini huli. Je, hilo si la huzuni? Na hivyo, ni lazima utafute mabadiliko: Kama ni kushindwa au kufanywa mkamilifu, yote yanahusiana na kama kuna mabadiliko ndani yako, na kama wewe ni mtii au la, na hili linaamua kama unaweza kupatwa na Mungu au la. Jua kwamba “kushindwa” na “kufanywa mkamilifu” yamejikita katika kiwango cha mabadiliko na utii, vilevile katika jinsi upendo wako kwa Mungu ulivyo. Kinachotakiwa leo ni kwamba uweze kufanywa mkamilifu kabisa, lakini mwanzoni ni lazima ushindwe—ni lazima uwe na ufahamu wa kutosha juu ya kuadibu na hukumu ya Mungu, lazima uwe na imani ya kufuata, na kuwa mtu ambaye anatafuta mabadiliko na matokeo kuweko. Wakati huo tu ndipo utakuwa mtu ambaye anatafuta kufanywa mkamilifu. Unapaswa kuelewa kwamba wakati wa kufanywa kuwa mkamilifu, mtashindwa, na wakati wa kushindwa mtafanywa kuwa wakamilifu. Leo, unaweza kutafuta kufanywa kuwa mkamilifu au kutafuta mabadiliko katika ubinadamu wako wa nje na maendeleo katika ubora wa tabia yako, lakini muhimu kabisa ni kwamba unaweza kuelewa kwamba kila kitu ambacho Mungu anafanya leo kina maana na ni cha manufaa: Kinakuwezesha wewe ambaye unaishi katika nchi ya uchafu kuepuka uchafu na kuuondoa wote, kinakuwezesha kushinda ushawishi wa Shetani na kuacha nyuma ushawishi wa giza wa Shetani—na kwa kulenga vitu hivi, unakuwa umelindwa katika nchi hii ya uchafu. Mwishowe, utaambiwa utoe ushuhuda gani? Unaishi katika nchi ya uchafu lakini unaweza kuwa mtakatifu, na hutakuwa tena mchafu na mwenye najisi, unamilikiwa na Shetani, lakini unaachana na ushawishi wa Shetani, na huimilikiwi au kunyanyaswa na Shetani, na unaishi mikononi mwa Mwenyezi. Huu ndio ushuhuda, na thibitisho la ushindi katika vita na Shetani. Unaweza kumwacha Shetani, unachoishi kwa kudhihirisha hakifichui Shetani, lakini ni kile ambacho Mungu alitaka mwanadamu afikie Alipomuumba mwanadamu: ubinadamu wa kawaida, urazini wa kawaida, umaizi wa kawaida, azimio la kawaida la kumpenda Mungu, na utii kwa Mungu. Huo ndio ushuhuda ambao kiumbe wa Mungu huwa nao.

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

11. Kazi ya siku za mwisho inavunja kanuni zote, bila kujali kama umelaaniwa au kuadhibiwa, maadamu tu uisaidie kazi Yangu, na una manufaa kwa kazi ya ushindi ya leo, na bila kujali kama wewe ni uzao wa Moabu au kizazi cha joka kuu jekundu, maadamu tu unatekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu katika hatua hii ya kazi, na kufanya kadri unavyoweza, basi matokeo yanayotarajiwa yatatimizwa. Wewe ni kizazi cha joka kuu jekundu, na ni uzao wa Moabu; kwa ujumla, wale wote walio wa mwili na damu ni viumbe wa Mungu, na waliumbwa na Muumba. Wewe ni kiumbe wa Mungu, hupaswi kuwa na chaguo lolote, na huu ndio wajibu wako. Bila shaka, leo kazi ya Muumba imeelekezwa kwa ulimwengu mzima. Bila kujali wewe ni uzao wa nani, zaidi ya yote, nyinyi ni mojawapo wa viumbe wa Mungu, ninyi—uzao wa Moabu—ni sehemu ya viumbe wa Mungu, ni vile tu nyinyi mna thamani ya chini. Kwa kuwa, leo, kazi ya Mungu inatekelezwa miongoni mwa viumbe wote, na imelenga ulimwengu mzima, Muumba yuko huru kuchagua watu, masuala, au vitu vyovyote ili viweze kufanya kazi Yake. Hajali wewe ni uzao wa nani; maadamu tu wewe ni mmoja wa viumbe wake, na maadamu una manufaa katika kazi Yake—kazi ya ushindi na ushuhuda—Ataifanya kazi Yake ndani yako bila haya yoyote. Hili linaharibu kabisa dhana za watu za kitamaduni, ambayo ni kwamba Mungu hatawahi kamwe kufanya kazi miongoni mwa Mataifa, hususan wale ambao wamelaaniwa na ambao ni duni; kwa maana wale ambao wamelaaniwa, uzao wao wa baadaye nao utaendelea kulaaniwa milele, hawatakuwa na nafasi ya wokovu; Mungu hatawahi kamwe kushuka na kufanya kazi katika nchi ya Mataifa, na Hatakanyaga mguu Wake katika nchi yenye uchafu, maana Yeye ni mtakatifu. Jua kwamba Mungu ni Mungu wa viumbe vyote, ni mtawala wa mbingu na nchi na vitu vyote, na si Mungu wa watu wa Israeli pekee. Hivyo, kazi hii katika nchi ya Uchina ni ya umuhimu mkubwa, na unadhani haitaenea miongoni mwa mataifa yote? Ushuhuda mkubwa wa siku za usoni hautakomea Uchina tu; ikiwa Mungu angewashinda nyinyi tu, je, mapepo wangeshawishika? Hawaelewi maana ya kushindwa, au nguvu kubwa ya Mungu, na ni pale tu ambapo wateuliwa wa Mungu katika nchi yote watakapoona matokeo ya mwisho ya kazi hii ndipo viumbe wote watakuwa wameshindwa. Hakuna ambao wapo nyuma sana au waovu sana kuliko uzao wa Moabu. Iwapo tu watu hawa wataweza kushindwa—wale ambao ni waovu sana, ambao hawakumtambua Mungu au kuamini kwamba kuna Mungu wameshindwa, na kumtambua Mungu katika vinywa vyao, wakimtukuza, na wanaweza kumpenda—ndipo huu utakuwa ushuhuda wa ushindi. Ingawa wewe si Petro, mnaishi kwa kudhihirisha mfano wa Petro, mnaweza kuwa na ushuhuda wa Petro, na ushuhuda wa Ayubu, na huu ni ushuhuda mkubwa sana.

kutoka kwa “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni