Smiley face

Jumamosi, 24 Agosti 2019

Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu “Fumbo la Kupata Mwili” (Sehemu ya Pili)

11. Mungu mwenye mwili Anajidhihirisha mwenyewe kwa watu kadhaa wanaomfuata Anapofanya kazi Yeye binafsi, na sio kwa viumbe wote. Alijifanya mwili ili Akamilishe hatua ya kazi Yake, na sio ili amwonyeshe mwanadamu mfano Wake. Hata hivyo, kazi Yake lazima ifanywe na Yeye binafsi, kwa hivyo inalazimu Afanye kazi hiyo katika mwili. Kazi hii inapokamilika, Ataondoka duniani; Hawezi kusalia duniani kwa muda mrefu kwa hofu ya kuzuia kazi inayokuja. Anachokionyesha kwa halaiki ni tabia Yake ya haki na matendo Yake yote, na sio umbo la mwili Wake wakati Amejifanya mwili mara mbili, kwa maana mfano wa Mungu unaweza tu kuonyeshwa kupitia kwa tabia Yake, na si kubadilishwa na mfano wa mwili Wake wa nyama. Mfano wa mwili Wake wa nyama huonyeshwa kwa watu wachache tu, kwa wale wanaomfuata Anapofanya kazi katika mwili. Hiyo ndio maana kazi inayofanywa wakati huu inafanywa kwa siri. Ni kama tu vile Yesu alivyojionyeshwa kwa Wayahudi pekee yao Alipofanya kazi Yake, na hakujionyesha hadharani kwa mataifa mengine. Hivyo, pindi Alipomaliza kazi Yake, Aliondoka miongoni mwa wanadamu na hakukawia; kwa wakati uliofuata Hakujionyesha kwa nafsi Yake kwa mwanadamu, bali kazi iliendeshwa moja kwa moja na Roho Mtakatifu. Mara tu kazi ya Mungu katika mwili inapokamilika, Anaondoka katika dunia ya mwanadamu, na kamwe Hafanyi tena kazi sawa na ile Aliyofanya Akiwa katika mwili. Kazi inayofuata hufanywa na Roho Mtakatifu moja kwa moja. Wakati huu, mwanadamu hawezi kuona mfano Wa Mungu katika mwili; Yeye Hajionyeshi wazi kwa mwanadamu hata kidogo, na daima Anabaki mafichoni. Muda wa kazi ya Mungu mwenye mwili ni mchache, ambayo lazima ifanywe katika Enzi bayana, muda, taifa na kati ya watu bayana. Kazi kama hiyo inawakilisha tu kazi ya wakati wa Mungu katika mwili, na inalenga enzi fulani, ikiwakilisha kazi ya Roho wa Mungu katika enzi moja hasa, na sio ujumla wa kazi Yake. Kwa hivyo, umbo la Mungu mwenye mwili halitaonyeshwa kwa kila mwanadamu. Kinachoonyeshwa kwa halaiki ni uhaki wa Mungu na tabia Yake kwa ukamilifu, na wala sio mfano Wake Alipokuwa mwili mara mbili. Sio sura inayoonyeshwa kwa mwanadamu, wala mifano yote miwili ikijumlishwa. Kwa hivyo, ni muhimu kwamba mwili wa Mungu uondoke duniani baada ya kukamilisha kazi Anayohitajika kufanya, kwa kuwa Anakuja tu kufanya kazi Anayopaswa kufanya, na sio kuwaonyesha wanadamu mfano wa umbo Lake. Ingawa umuhimu wa kuingia katika mwili umeshatimizwa na Mungu mara mbili Akijifanya mwili na nyama, bado hatajionyesha wazi kwa taifa ambalo halijawahi kumwona mbeleni.

kutoka kwa “Fumbo la Kupata Mwili (2)” katika Neno Laonekana Katika Mwili

12. Mnapaswa kujua kwamba kazi ya Mungu katika mwili inafaa kufungua enzi mpya. Kazi hii ni ya muda wa miaka michache tu, na Hawezi kukamilisha kazi yote ya Roho wa Mungu. Hii ni sawia na vile umbo la Yesu kama Myahudi linaweza tu kuwakilisha mfano wa Mungu alivyofanya kazi katika Yudea, na Angefanya tu kazi ya msalabani. Wakati ambao Yesu Alikuwa katika mwili, Hangefanya kazi ya kutamatisha enzi au kumwangamiza mwanadamu. Kwa hivyo, baada ya kusulubiwa na kukamilisha kazi Yake, Alipaa juu na daima Akajificha kutoka kwa mwanadamu. Kutoka wakati huo kuendelea, wale waumini wa mataifa waliweza tu kuiona picha Yake ambayo walibandika kwenye kuta zao, na sio udhihirisho wa Bwana Yesu. Picha hii imechorwa na mwanadamu tu, na si mfano ambao Mungu Mwenyewe Alimwonyesha mwanadamu. Mungu Hatajionyesha kwa halaiki wazi wazi katika mfano ambao Yeye Alikuwa nao mara mbili Akiwa katika mwili. Kazi Anayofanya miongoni mwa wanadamu ni kuwaruhusu kuelewa tabia Yake. Haya yote yanafanyika kwa kumpitisha mwanadamu katika kazi za enzi tofauti, na vile vile tabia ambazo Ameziweka wazi na kazi ambayo Amefanya, na bali si kupitia kwa udhihirisho wa Yesu. Hiyo ni kusema, umbo la Mungu halionyeshwi kwa mwanadamu kupitia katika mfano wa Mungu mwenye mwili, lakini ni kwa kupitia katika kazi iliyotekelezwa na Mungu mwenye mwili wa sura na umbo; na kupitia katika kazi Yake, mfano Wake unaonekana na tabia Yake inajulikana. Huu ndio umuhimu wa kazi Angependa kufanya katika mwili.

kutoka kwa “Fumbo la Kupata Mwili (2)” katika Neno Laonekana Katika Mwili

13. Wakati kazi ya Alipokuwa mwili mara mbili inakamilika, Anaanza kuonyesha tabia Yake ya haki katika mataifa, Akiruhusu halaiki ione mfano wa umbo Lake. Anapenda kudhihirisha tabia Yake, na kupitia katika hili Aweke wazi tamati za aina tofauti ya wanadamu, hapo kuifikisha mwishokabisa enzi nzee. Kazi Yake katika mwili haitendeki katika sehemu pana (kama vile Yesu Alivyofanya kazi katika sehemu ya Yuda peke Yake, na leo hii Ninafanya kazi miongoni mwenu pekee) kwa sababu kazi Yake katika mwili ina mipaka na kingo. Anafanya tu kazi ya muda mchache katika mfano wa kawaida na mwili wa kawaida, badala ya kufanya kazi ya milele kupitia kwa Mungu mwenye mwili, ama kufanya kazi ya kuwaonekania watu wote wa mataifa. Kazi hii katika mwili lazima izuiliwe katika mawanda (kama vile kufanya kazi katika Yuda ama kati Yenu), kisha kupanua kazi iliyofanyika katika mipaka hii. Bila shaka, kazi ya upanuzi huu huendeshwa na Roho Mtakatifu moja kwa moja na haiwezi kuwa kazi ya mwili Wake wa nyama. Kwa maana kazi katika mwili iko na mipaka na haiwezi kuenea katika pembe zote za ulimwengu. Hauwezi kuyatekeleza haya. Kupitia kwa kazi katika mwili, Roho Wake hutekeleza kazi inayofuatia. Kwa hivyo, kazi inayofanywa katika mwili ni ya utayarisho inayotekelezwa ndani ya mipaka; Roho Wake kisha Anaendeleza kazi hii, na kuipanua.

kutoka kwa “Fumbo la Kupata Mwili (2)” katika Neno Laonekana Katika Mwili

14. Mungu huja tu katika dunia hii kufanya kazi ya kuongoza enzi; kufungua enzi mpya na kutamatisha enzi ya zamani. Hajakuja kuishi kulingana na maisha ya mwanadamu wa kawaida kwa kikamilifu, kupitia Mwenyewe raha na machungu ya maisha kama mwanadamu, au kumfanya mtu fulani mkamilifu kwa mkono Wake au kumtazama binafsi mtu Fulani anavyokua. Hii sio kazi Yake; kazi Yake ni kufunua tu enzi mpya na kutamatisha enzi iliyotangulia. Hiyo ina maana, Atafungua enzi mpya, akamilishe iliyotangulia, amshinde shetani kwa kufanya kazi Yake Yeye binafsi. Kila mara Anapotekeleza kazi Yeye Mwenyewe, ni kana kwamba Anakanyaga mguu wake katika uwanja wa vita Katika mwili, kwanza Anaishinda dunia kisha Anatawala juu ya Shetani; Anachukua utukufu wote na kufungua pazia kwa kazi ya enzi yote elfu mbili, na kuwapa binadamu wote duniani njia ya kweli ya kufuata, na maisha ya amani na furaha. Hata hivyo, Mungu Hawezi kuishi na mwanadamu duniani kwa muda mrefu, kwa maana Mungu ni Mungu, ni si kama mwanadamu kamwe. Hawezi kuishi urefu wa maisha ya mwanadamu wa kawaida, hiyo ina maana, Hawezi kuishi duniani kama mwanadamu ambaye si wa kawaida, kwa maana Yuko na sehemu ndogo ya ubinadamu wa kawaida wa wanadamu wa kawaida kumuwezesha kuishi vile. Kwa maneno mengine, Mungu Anawezaje kuanzisha familia na kukuza watoto duniani? Je, si hii itakuwa ni aibu? Yeye anao ubinadamu wa kawaida tu kwa minajili ya kutekeleza kazi Yake kwa njia ya kawaida, na sio kumwezesha Yeye kuanzisha familia kama mwanadamu wa kawaida. Hisia Zake za kawaida, mawazo ya kawaida, na kula kwa kawaida na mavazi ya mwili Wake yanatosha kuthibitisha kuwa Yuko na ubinadamu wa kawaida; Hakuna haja Yake kuanzisha familia ndio athibitishe kwamba Yeye kweli yuko na ubinadamu wa kawaida. Hiyo haina maana hata kidogo! Mungu Anakuja duniani, kumaanisha Neno linageuka kuwa mwili; Kwa urahisi Anamruhusu mwanadamu kulielewa neno Lake na kuliona neno Lake, hiyo ni, kumruhusu mwanadamu kuona kazi inayotekelezwa na mwili. Nia Yake sio kwamba wanadamu wauchukue mwili Wake kwa njia Fulani, bali kwamba mwanadamu awe mtiifu mpaka mwisho, kumaanisha, aweze kutii maneno yote yanayotoka katika kinywa Chake, na kunyenyekea na kukubali kazi yote Anayofanya. Yeye Anafanya kazi katika mwili tu, sio kumfanya mwanadamu kwa kujua aabudu ukuu na utukufu wa mwili Wake. Anamwonyesha tu mwanadamu hekima ya kazi Yake na mamlaka yote Aliyo nayo. Kwa hivyo, ingawa Anao ubinadamu wa kipekee, Hafanyi matangazo yoyote, na Anatilia tu maanani kazi ambayo Anapaswa kufanya. Mnapaswa kujua ni kwa nini Mungu Alijifanya mwili ilhali hajigambi wala kushuhudia juu ya ubinadamu Wake wa kawaida, na badala Yake Anatekeleza tu kazi ambayo Angependa kufanya. Hii ndio sababu mnaona tu uwepo wa uungu katika Mungu mwenye mwili, kwa sababu Hatangazi kuwa Kwake katika mwili ndio mwanadamu aige. Wakati tu mwanadamu anamwongoza mwanadamu ndipo anapozungumzia kuhusu kile alicho kama binadamu, ndivyo apate heshima na utii wao vyema zaidi na hivyo kufanikisha uongozi wa wengine. Kinyume na hilo, Mungu huwashinda watu kupitia katika kazi Yake pekee (hiyo ni, kazi isiyoweza kufanywa na mwanadamu). Hamshawishi mwanadamu au kuwafanya wanadamu wote wamwabudu, bali Anaweka tu katika mwanadamu hisia za uchaji Kwake au kumfanya mwanadamu aweze kujua kuhusu kutowezekana kwa kumchunguza Yeye. Hakuna haja ya Mungu kumpendeza mwanadamu. Kile anachohitaji ni kuwa wewe umheshimu na kumwabudu mara tu unaposhuhudia tabia Yake.

kutoka kwa “Fumbo la Kupata Mwili (2)” katika Neno Laonekana Katika Mwili

15. Kazi ya Mungu mwenye mwili ni tofauti na ile ya wale wanaotumiwa na Roho Mtakatifu. Mungu anapofanya kazi Yake duniani, Yeye anajali kutimilika kwa huduma Yake pekee Yake. Na kwa mambo mengine yasiyohusiana na huduma Yake, Yeye kimatendo hajishughulishi hata kidogo, hata kwa kiwango cha kuzipa mgongo shughuli hizo. Yeye hufanya tu kazi Anayopaswa kufanya, na hajishughulishi na kazi ambayo mwanadamu anapaswa kufanya. Kazi Anayofanya ni ile tu inahusiana na enzi Aliyomo na huduma Anayopaswa kukamilisha, kana kwamba mambo mengine yote si jukumu Lake. Yeye hajijazi na maarifa ya kawaida kuhusu jinsi ya kuishi kama mwanadamu, na Hajifunzi mahusiano ya jamii au mambo yoyote ambayo mwanadamu anaelewa. Hajishughulishi kamwe na mambo ambayo mwanadamu anapaswa kujua na Anafanya tu kitu ambacho ni jukumu Lake. Kwa hivyo, mwanadamu anavyoona, Mungu mwenye mwili ni mwenye upungufu katika mambo mengi mno, hata kwa kiasi kwamba Anavipa mgongo vingi ambavyo mwanadamu anapaswa kuwa navyo, na kwamba hana ufahamu wa mambo kama hayo. Mambo kama ufahamu wa maisha ya kawaida, na vile vile kanuni za tabia na kuhusiana na wengine, huonekana kuwa hazina uhusiano Kwake. Hata hivyo, huwezi kuona kutoka kwa Mungu mwenye mwili tabia zozote zisizo za kawaida. Hiyo ni kusema, ubinadamu Wake unadumisha maisha Yake kama mwanadamu wa kawaida na fikira za kawaida za ubongo Wake, na kumpa uwezo wa kutofautisha kati ya mazuri na mabaya. Hata hivyo, Hajajazwa na kingine chochote, yote ambayo ni ya wanadamu (walioumbwa) pekee. Mungu anapata mwili ili kukamilisha huduma Yake pekee. Kazi Yake inaelekezwa kwa enzi nzima na sio kwa mtu binafsi au mahali fulani. Kazi Yake inaelekezwa kwa ulimwengu mzima. Huu ndio mwelekeo wa kazi Yake na kanuni Anayofuata katika kazi Yake. Hii haiwezi kubadilishwa na yeyote, na mwanadamu hawezi kuhusika kwa sehemu yoyote.

kutoka kwa “Fumbo la Kupata Mwili (3)” katika Neno Laonekana Katika Mwili

16. Mungu anakuja tu duniani kukamilisha kazi Yake, na kwa hivyo Kazi Yake duniani ni ya muda mfupi. Haji duniani na nia ya Roho wa Mungu kukuza mwili Wake kuwa mkuu wa kipekee wa kanisa. Mungu anapokuja duniani, ni Neno ambalo kugeuka kuwa mwili; mwanadamu, hata hivyo, hajui kuhusu kazi Yake na kwa nguvu anaona Yeye kuwa sababu ya mambo. Lakini nyote mnapaswa kufahamu kuwa Mungu ni Neno lililogeuka kuwa mwili, na sio mwili uliokuzwa na Roho wa Mungu ili kusimamia nafasi ya Mungu kwa ufupi. Mungu Mwenyewe hakuzwi, ila ni Neno kugeuka mwili, na leo hii Anatekeleza kazi Yake kirasmi miongoni mwenu.

kutoka kwa “Fumbo la Kupata Mwili (3)” katika Neno Laonekana Katika Mwili

17. Mungu hugeuka mwili ili tu Aiongoze enzi na Aanzishe kazi mpya. Lazima muelewe hoja hii. Hii ni tofauti kabisa na kazi ya mwanadamu, na mawili haya hayawezi kuzungumzwa kwa pamoja. Mwanadamu anahitaji muda mrefu wa kukuzwa na kufanywa mkamilifu kabla mwanadamu aweze kutumiwa kutekeleza kazi, na ubinadamu wa hali ya juu unahitajika. Mwanadamu hapaswi kudumisha hali yake ya ubinadamu wa kawaida tu, bali pia mwanadamu zaidi ya hapo lazima aelewe kanuni nyingi na sheria za tabia kabla ya mengine, na zaidi ya hayo lazima ajifunze zaidi kuhusu hekima na maadili ya mwanadamu. Haya ndiyo mwanadamu lazima kujengwa nayo. Hata hivyo, hivi sivyo ilivo na Mungu mwenye mwili, kwa maana kazi Yake haimwakilishi mwanadamu na wala si ya binadamu; bali ni dhihirisho la moja kwa moja la hali Yake na utekelezi wa moja kwa moja wa kazi Anayopaswa kufanya. (Kwa kawaida, kazi Yake hufanyika wakati inapaswa kufanyika, na sio tu wakati wowote kiholela. Badala Yake, kazi Yake hufanyika wakati ambapo ni wakati wa kukamilisha huduma Yake). Yeye hajihusishi katika maisha ya mwanadamu wala katika kazi ya mwanadamu, hiyo inamaanisha, ubinadamu Wake haujengwi na yoyote kati ya haya (lakini hili haliathiri kazi Yake). Anatimiza huduma Yake tu ikiwa wakati umewadia wa kufanya hivyo; haijalishi hali Aliyomo, Yeye huendelea mbele na kazi Anayopaswa kufanya. Haijalishi mwanadamu anajua nini kumhusu, au maoni ya mwanadamu kumhusu, kazi Yake haiathiriki. Hii ni kama tu vile Yesu Alivyofanya kazi Yake; hakuna Aliyejua Yeye ni nani, lakini Aliendelea tu mbele na kazi Yake. Mambo haya hayakumuathiri katika utendaji wa kazi Yake Aliyopaswa kufanya. Kwa hivyo, Hakukiri au kutangaza kuwa Yeye ni nani, na Yeye Alimfanya mwanadamu Amfuate tu. Kwa kawaida, huu haukuwa tu uvumilivu wa Mungu; ilikuwa ni njia ambayo Yesu Anafanya kazi katika mwili. Angeweza tu kufanya kazi kwa namna hii, kwani mwanadamu hangeweza kumtambua Yesu kwa jicho la kawaida. Na hata kama mwanadamu angeweza, mwanadamu hangeweza kusaidia katika kazi Yake. Zaidi ya hayo, hakugeuka mwili ili mwanadamu apate kujua mwili huu Wake; ilikuwa ni kwa ajili ya kufanya kazi Yake na kukamilisha huduma Yake. Kwa sababu hii, hakutilia maanani hali ya kufanya Ajulikane. Alipokamilisha kazi Aliyopaswa kufanya, utambulisho Wake na hadhi Yake vilijulikana wazi kwa mwanadamu. Mungu mwenye mwili hukaa kimya na hafanyi matangazo yoyote. Yeye hajishughulishi na mwanadamu au vile mwanadamu anaendelea katika kumfuata, na yeye husonga tu mbele katika kutimiza huduma Yake na kufanya kazi Anayopaswa kufanya. Hakuna Anayeweza kusimama mbele ya njia ya kazi Yake. Wakati muda unawadia wa kazi Yake kukamilika, ni muhimu kazi hiyo ikamilike na kufikishwa kikomo. Hakuna anayeweza kusema vinginevyo. Baada tu ya Yeye kuondoka kutoka kwa mwanadamu baada ya kukamilisha kazi Yake ndipo mwanadamu ataelewa kazi Anayofanya, ingawa hataifahamu kikamilifu. Na itachukua muda mrefu ndipo mwanadamu aelewe nia Yake Alipofanya kazi hiyo mara ya kwanza. Kwa maneno mengine, kazi ya enzi ambapo Mungu anageuka mwili imegawanywa katika sehemu mbili. Sehemu moja ni kupitia katika kazi na maneno ya Mungu mwenye mwili Mwenyewe. Pindi tu huduma ya mwili Wake imetimika kikamilifu, sehemu nyingine ya kazi inatakiwa kutekelezwa na Roho Mtakatifu; basi utakuwa wakati wa mwanadamu kutimiza wajibu wake, kwa maana Mungu ameshafungua njia tayari, na lazima itembelewe na mwanadamu mwenyewe. Hiyo ni kusema, Mungu anageuka kuwa mwili ili kutekeleza sehemu moja ya kazi Yake, na inaendelezwa kwa urithi na Roho Mtakatifu na vile vile wale watu wanaotumiwa na Roho Mtakatifu. Kwa hivyo mwanadamu anapaswa kujua kazi ya msingi inayopaswa kutekelezwa na Mungu mwenye mwili katika hatua hii ya kazi. Mwanadamu lazima aelewe hasa umuhimu wa Mungu kugeuka kuwa mwili na kazi Anayopaswa kufanya, badala ya kumuuliza Mungu ni nini kinachotakiwa kwa mwanadamu. Haya ni makosa ya mwanadamu, na vile vile fikira, na zaidi ya hayo, ni kutotii kwake.

kutoka kwa “Fumbo la Kupata Mwili (3)” katika Neno Laonekana Katika Mwili

18. Mungu anakuwa mwili bila nia ya kumfanya mwanadamu apate kuujua mwili Wake, ama kukubali mwanadamu kutofautisha tofauti kati ya mwili wa Mungu mwenye mwili na ule wa mwanadamu; Mungu hapati mwili ili kufunza mwanadamu uwezo wa utambuzi, na zaidi nia ya mwanadamu kumwabudu Mungu mwenye mwili, ambayo kupitia kwayo atapata utukufu mkuu. Hakuna kati ya haya yaliyo mapenzi ya Mungu ya awali ya Mungu kuwa mwili. Mungu hawi mwili ili kulaani mwanadamu, kufichua mwanadamu akipenda, ama kufanya vitu kuwa vigumu kwa mwanadamu. Hakuna kati ya hayo lililo penzi la awali la Mungu. Kila wakati ambapo Mungu anakuwa mwili, ni kazi isiyo na budi. Ni kwa ajili ya kazi Yake kuu na usimamizi Wake mkuu ndio maana Anafanya hivyo, na si kwa sababu ambazo mwanadamu anafikiria. Mungu anakuja tu duniani Anavyohitajika na kazi Yake, na kila wakati ikiwa lazima. Haji duniani Akiwa na nia ya kuzurura, ila kutekeleza kazi ambayo Anapaswa kufanya. Mbona basi Ajipatie kazi hii ngumu na kujiweka katika hatari kubwa kufanya kazi hii? Mungu anakuwa mwili tu inapobidi, na kila wakati ikiwa na umuhimu wa kipekee. Kama ingekuwa tu kwa sababu ya kumfanya mwanadamu amuangalie na kufungua macho yao, basi kwa uhakika kabisa, hangekuja kati ya wanadamu kwa kubembeleza. Anakuja duniani kwa usimamizi Wake na kazi Yake kuu, na kuwa na uwezo wa kutwaa wanadamu zaidi. Anakuja kuwakilisha enzi na kumshinda Shetani, na ni katika mwili ndimo Anakuja kumshinda Shetani. Zaidi, Anakuja kuwaongoza binadamu wote katika maisha yao. Haya yote yanahusu uongozi Wake, na yanahusu kazi ya ulimwengu wote. Mungu angekuwa mwili ili tu kumruhusu mwanadamu kuja kuujua mwili Wake na kuyafungua macho ya mwanadamu, basi mbona Hangesafiri kwa kila taifa? Je hili sio jambo la wepesi zaidi? Lakini hakufanya hivyo, badala yake, Akachagua mahali palipofaa pa kuishi na kuanza kazi Aliyopaswa kufanya. Mwili huu pekee ni wa umuhimu mkuu. Anawakilisha enzi nzima, na Anatekeleza kazi ya enzi nzima; Analeta enzi ya zamani kufika tamati na kuikaribisha mpya. Haya yote ni mambo muhimu yanayohusu usimamizi wa Mungu, na ni umuhimu wa hatua ya kazi iliyotekelezwa na Mungu kuja duniani.

kutoka kwa “Fumbo la Kupata Mwili (3)” katika Neno Laonekana Katika Mwili

19. Kazi ya kila enzi huanzishwa na Mungu Mwenyewe, lakini unapaswa kujua kwamba licha ya kazi yoyote ya Mungu, Yeye haji kuanzisha muungano au kufanya mikutano yoyote halisi au kuanzisha makundi ya aina yoyote kwa ajili yenu. Yeye huja tu kufanya kazi Anayopaswa kufanya. Kazi Yake haizuiliwi na mwanadamu yeyote. Yeye hufanya kazi Yake vile Anavyopenda; haijalishi kile mwanadamu anajua au kufikiri, Yeye hutilia maanani katika kutekeleza kazi Yake. Tangu kuumbwa kwa dunia, kumekuwa na hatua tatu za kazi; kutoka kwa Yehova mpaka kwa Yesu, na kutoka kwa Enzi ya Sheria mpaka kwa Enzi ya Neema, Mungu hajawahi kuitisha mkutano halisi kwa mwanadamu, wala hajawahi kuwakusanya wanadamu wote pamoja kufanya mkutano halisi wa ulimwengu ili kupanua kazi Yake. Yeye hufanya tu kazi ya mwanzo wa enzi nzima wakati muda na wakati na mahali uko sawa, na kupitia kwa hili Anaikaribisha enzi ili kuwaongoza wanadamu katika maisha yao. Mikutano halisi ni mikutano ya wanadamu; kuwakusanya watu pamoja kusherehekea siku kuu katika kazi za mwanadamu. Mungu hasherehekei siku kuu na, zaidi ya hayo, Anachukizwa nazo; Yeye haitishi mikutano halisi na zaidi ya hayo Anachukizwa nayo. Sasa lazima uelewe ni nini hasa kazi ya Mungu mwenye mwili!

kutoka kwa “Fumbo la Kupata Mwili (3)” katika Neno Laonekana Katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni