Smiley face

Jumatatu, 19 Agosti 2019

Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Nne)


34. Tamaduni za asili na mtazamo wa kiakili vilivyo madhubuti vimeiharibu roho safi na ya kitoto ya mwanadamu kwa muda mrefu, vimeishambulia roho ya mwanadamu bila ubinadamu hata kidogo, kana kwamba imiondolewa hisia na hali yoyote ya nafsi. Mbinu za mashetani hawa ni za kikatili kupita kiasi, na ni kana kwamba "elimu" na "malezi" vimekuwa njia za kitamaduni ambazo kwazo mfalme wa mashetani anamchinja mwanadamu; kwa kutumia "mafundisho yake ya kina" anaifunika kabisa roho yake mbaya, akiwa amevalia mavazi ya kondoo ili mwanadamu amwamini na kisha kumvizia mwanadamu akiwa amelala ili ammeze kabisa. Masikini binadamu—wangewezaje kujua kwamba nchi ambayo kwayo wamelelewa ni nchi ya Shetani, kwamba aliyewalea kimsingi ni adui ambaye anawaumiza. Lakini bado mwanadamu hazinduki kabisa; baada ya kushibisha hasira na kiu chake, anajiandaa kuulipiza "wema" wa "wazazi" wake kwa kumlea. Hivyo ndivyo mwanadamu alivyo. Leo, bado hajui kwamba mfalme ambaye alimlea ni adui yake. Mifupa ya wafu imetapakaa nchini, Shetani anafanya sherehe za wazimu bila kukoma, na anaendelea kuumeza mwili wa mwanadamu huko "kuzimu," akishiriki kaburi pamoja na mifupa ya wanadamu na akijaribu bila mafanikio kumaliza masalio ya mwisho wa mwili wa mwanadamu uliobakia kuwa matambara. Lakini mwanadamu bado ni mjinga, na hajawahi kumchukulia Shetani kama adui yake, lakini badala yake anamtumikia kwa moyo wake wote. Watu kama hao waliokengeuka hawawezi kumjua Mungu. Je, ni rahisi kwa Mungu kuwa mwili na kuja miongoni mwa wanadamu, Akitekeleza kazi Zake zote za wokovu? Mwanadamu, ambaye tayari amejiingiza Kuzimu, anawezaje kukidhi matakwa ya Mungu?

kutoka katika "Kazi na Kuingia (9)" katika Neno Laonekana katika Mwili

35. Mungu amekosa usingizi kwa siku nyingi kwa ajili ya kazi ya binadamu. Kutoka vina vya juu hadi vya chini, Amepanda kwenda katika kuzimu ambapo mwanadamu anaishi ili Awe pamoja na mwanadamu, Hajawahi kulalamikia uchakavu walio nao wanadamu, Hajawahi kumlaumu mwanadamu kwa ukaidi wake, lakini Anavumilia mateso makuu kadri Anavyofanya kazi Yake. Inawezekanaje Mungu awe wa kuzimu? Inawezekanaje Aishi maisha yake kuzimu? Lakini kwa ajili ya binadamu wote, ili binadamu wote waweze kupata pumziko mapema zaidi, Amestahimili fedheha na kupitia udhalimu kuja duniani, na kuingia mwenyewe “jahanamu” na “kuzimu,” katika tundu la duma, kumwokoa mwanadamu. Mwanadamu amefuzu vipi kumpinga Mungu? Ana sababu gani tena ya kulalamika kuhusu Mungu? Anawezaje kuwa na ujasiri wa kumwangalia Mungu tena? Mungu wa mbinguni Amekuja katika nchi hii chafu zaidi ya uovu, na Hajawahi kutangaza manung'uniko Yake, au kulalamika kuhusu mwanadamu, lakini badala yake Anakubali kimyakimya maangamizi[27] na ukandamizaji wa mwanadamu. Hajawahi kamwe kuyazuia matakwa ya mwanadamu yasiyokuwa na msingi, Hajawahi kutaka mambo mengi yanayomzidi mwanadamu, na Hajawahi kumwekea mwanadamu matakwa yasiyokuwa na msingi; Anafanya tu kazi zote ambazo mwanadamu anahitajika kufanya bila malalamiko: kufundisha, kutia nuru, kukaripia, usafishaji wa maneno, kukumbusha, kusihi, kufariji, kuhukumu na kufunua. Ni gani kati ya hatua Zake ambazo sio kwa ajili ya maisha ya mwanadamu? Ingawa Ameondoa matarajio na majaliwa ya mwanadamu, ni hatua zipi zilizochukuliwa na Mungu ambazo hazikuwa kwa ajili ya majaliwa ya mwanadamu? Ni ipi kati ya hatua hizo ambayo haijawahi kuwa kwa ajili ya mwanadamu kuendelea kuishi? Ni ipi kati ya hatua hizo haikuwepo kwa ajili ya kumweka mwanadamu huru dhidi ya mateso na minyanyaso ya nguvu za giza ambazo ni nyeusi kama usiku? Ni ipi kati ya hatua hizo si kwa ajili ya mwanadamu? Ni nani awezaye kuuelewa moyo wa Mungu, ambao ni sawa na mama mwenye upendo? Ni nani awezaye kuuelewa moyo wa Mungu wenye shauku? Moyo wa upendo na matarajio ya shauku ya Mungu vimelipwa kwa mioyo ya baridi, na usugu, na macho yanayoonyesha kutojali, kwa makaripio mara kwa mara na matusi ya mwanadamu, kwa maneno yenye kuumiza na dhihaka na udhalilishaji, vimelipwa kwa dhihaka ya mwanadamu, kwa kukanyagwa na kukataliwa kwake, kwa kutokuwa na ufahamu kwake, na kupiga kite, na farakano, na uepukaji, kwa uongo tu, mashambulizi na uchungu. Maneno ya wema ya Mungu yamekutana na nyuso kali na ufidhuli wa maneno makali. Mungu anaweza tu kustahimili, Akiwa Ameinamisha kichwa, Akiwahudumia watu kama ng'ombe aliye radhi[28]. Ni idadi gani ya miezi na jua, ni mara ngapi Amekabiliana na nyota, ni mara ngapi Ameondoka alfajiri na kurudi jioni, na kujipinduapindua na kugaagaa, Akivumilia maumivu makubwa mara elfu moja kuliko maumivu Aliyoyapata Alipokuwa Anaondoka kutoka kwa Baba Yake, Akivumilia mashambulizi na kuvunja kwa mwanadamu, na kumshughulikia na kumpogoa mwanadamu. Unyenyekevu na kufichika kwa Mungu vimelipwa kwa upendeleo[29] wa mwanadamu, kwa mitazamo na vitendo vya mwanadamu visivyokuwa vya haki, na kutojulikana Kwake, ustahimilivu, na uvumilivu vimelipizwa kwa jicho la tamaa la mwanadamu; mwanadamu hujaribu kumkanyaga Mungu hadi afe, bila majuto, na hujaribu kumkanyagia Mungu ardhini. Mtazamo wa mwanadamu katika vile anavyomtendea Mungu ni wa "ujanja adimu," na Mungu, ambaye Anachokozwa na kutwezwa na mwanadamu, Anakanyagwa na kuwa bapa chini ya miguu ya makumi ya maelfu ya watu wakati mwanadamu mwenyewe anasimama wima, kana kwamba angeweza kuwa mfalme wa kasri, kana kwamba anataka kuchukua mamlaka kamili[30], kuendesha mahakama akiwa nyuma ya jukwaa, kumfanya Mungu kuwa mwongozaji mwangalifu sana mwenye kufuata kanuni akiwa nyuma ya jukwaa, ambaye haruhusiwi kupigana au kusababisha shida; lazima Mungu ni achukue nafasi ya Mtawala wa Mwisho, ni lazima Awe kibaraka[31], bila uhuru wote. Matendo ya mwanadamu hayaongeleki, basi ana sifa gani ya kutaka hiki au kile kuhusu Mungu? Ana sifa gani ya kutoa mapendekezo kwa Mungu? Anafaa kwa kiasi gani kumtaka Mungu amhurumie juu ya udhaifu wake? Anafaa kwa kiasi gani kupokea huruma ya Mungu? Anafaa kwa kiasi gani kupokea ukarimu wa Mungu kila mara? Anafaa kwa kiasi gani kupokea msamaha wa Mungu kila mara? Dhamiri yake iko wapi? Aliuvunja moyo wa Mungu muda mrefu uliopita, aliuacha moyo wa Mungu katika vipande kitambo sana. Mungu alikuja miongoni mwa wanadamu Akiwa na nguvu nyingi na mwenye shauku kubwa, Akitegemea kwamba mwanadamu atakuwa mkarimu Kwake, hata kama ni kwa wema kidogo tu. Bado moyo wa Mungu haujafarijiwa na mwanadamu, yote Aliyoyapokea ni mashambulizi na mateso ya kuongezeka haraka[32]; moyo wa mwanadamu ni wenye tamaa sana, tamaa yake ni kubwa sana, hawezi akatosheka, siku zote yeye ni mtundu na jasiri pasi busara, hawezi kamwe kumpatia Mungu uhuru au haki ya kuzungumza, na anamwacha Mungu bila cha kufanya bali kukubali unyanyasaji, na kumruhusu mwanadamu kumtawala anavyotaka.

kutoka katika "Kazi na Kuingia (9)" katika Neno Laonekana katika Mwili

36. Tangu uumbaji hadi leo, Mungu amestahimili maumivu mengi sana, na kupata mashambulizi mengi sana. Ilhali hata leo, bado mwanadamu hayalegezi matakwa yake kwa Mungu, bado anamchunguza Mungu, bado hana uvumilivu naye, na anachofanya tu ni kumpa ushauri, na kumkosoa, na kumfundisha nidhamu kana kwamba anaogopa sana kuwa Mungu atapotoka njia, kwamba Mungu duniani ni hayawani na Hana busara, au Anafanya fujo, au kwamba Hatafanya kitu chochote cha maana. Mwanadamu siku zote huwa na mtazamo wa aina hii kwa Mungu. Inawezekanaje isimhuzunishe Mungu? Kwa kuwa mwili, Mungu amevumilia maumivu na mateso mengi; ni vibaya kiasi gani, basi, kumfanya Mungu akubali mafundisho ya mwanadamu? Kuwasili Kwake miongoni mwa wanadamu kumemnyang’anya uhuru wote, kana kwamba Alikuwa Amefungwa Kuzimu, na Amekubali uchunguzi wa mwanadamu bila upinzani hata kidogo. Je jambo hili sio la kuaibisha? Katika kuja miongoni mwa familia ya wanadamu wa kawaida, Yesu amepitia uonevu mkubwa mno. Na kinachofedhehesha zaidi ni kwamba Amekuja katika ulimwengu huu wa vumbi na kujinyenyekeza hadi hadhi ya chini kabisa, na Amechukua mwili wa kawaida kabisa. Katika kuwa binadamu mwembamba, je, Mungu Mwenyezi hapati shida? Je, na hii yote si kwa ajili ya binadamu? Kuna wakati wowote ambapo alikuwa Anajifikiria? Baada ya kukataliwa na kuuawa na Wayahudi, na kukejeliwa na kudhihakiwa na watu, Hakuwahi kulalamika Mbinguni au kupinga duniani. Leo, janga hili ambalo limekuwepo kwa muda wa milenia limetokea tena miongoni mwa watu hawa wanaofanana na Wayahudi. Je, hawafanyi dhambi ile ile? Nini kinamfanya mwanadamu kuwa na sifa ya kupokea ahadi za Mungu? Je, hampingi Mungu na kisha kukubali baraka Zake? Kwa nini hapati haki kamwe, au kuutafuta ukweli? Kwa nini havutiwi kamwe na kile ambacho Mungu anafanya? Uadilifu wake uko wapi? Haki yake iko wapi? Je, ana ujasiri wa kumwakilisha Mungu? Ziko wapi hisia zake za haki? Ni kiasi gani cha kile kinachopendwa na mwanadamu ndicho kinachopendwa na Mungu? Mwanadamu hawezi kutambua tofauti muhimu[33], siku zote anachanganya kati ya nyeusi na nyeupe, anakandamiza haki na ukweli, na anashikilia kutokuwa na uadilifu na haki kwa kiwango kikubwa. Anafukuzia mbali mwanga, na anarukaruka gizani. Wale wanaotafuta ukweli na haki wanafukuzia mbali mwanga badala yake, wale wanaomtafuta Mungu wanamkanyaga chini ya miguu yao, na kujikweza. Mwanadamu hana tofauti na gaidi[34]. Mantiki yake ipo wapi? Nani anayeweza kutofautisha kati ya jema na baya? Nani anayeweza kushikilia haki? Nani ambaye yuko tayari kuteseka kwa ajili ya ukweli? Watu ni waovu na wabaya sana! Baada ya kumuangika Mungu msalabani wanapiga makofi na kufurahi, vilio vyao havikomi. Wao ni kama kuku na mbwa, wanashirikiana na kula njama, wameanzisha ufalme wao, udukuzi wao umeathiri kila mahali, wanafumba macho yao na kulia kwa maumivu makali zaidi na zaidi, wote wameungana pamoja, na hali ya kututumka inaenea kote, ni ya harakaharaka na yenye ucheshi, na wale ambao wanajishikamanisha kwa wengine bila kufikiria wanazidi kuibuka, wote wakiwa wameshikilia majina "mashuhuri" ya mababu zao. Hawa mbwa na kuku walimsahau Mungu kitambo sana, na hawajawahi kuzingatia kabisa hali ya moyo wa Mungu. Si ajabu kwamba Mungu anasema kwamba mwanadamu ni kama mbwa au kuku, mbwa anayebweka anayewafanya wengine mia kutoa mlio mkali; kwa nia hii, kwa makelele mengi ameileta kazi ya Mungu katika siku ya leo, bila kujali kazi ya Mungu ni ya namna gani, kama kuna haki, kama Mungu ana nafasi ya kuweka miguu Yake, jinsi kesho ilivyo, kuhusu uduni wake mwenyewe, na hali yake mwenyewe ya kuwa mchafu. Mwanadamu hajawahi kufikiria juu ya mambo kiasi hicho, hajawahi kuhofia kesho, na amekusanya yale yote ambayo ni ya manufaa na ya thamani na kuyakumbatia, na bila kumwachia Mungu chochote isipokuwa mabaki na makombo[35]. Binadamu ni katili kiasi gani! Hawi na hisia hata kidogo kumhusu Mungu, na baada ya kuteketeza kila kitu cha Mungu, anamsahau Mungu kabisa, naye hajali tena kuhusu uwepo Wake. Anamfurahia Mungu, halafu anampinga Mungu, na anamkanyagia chini ya miguu yake, wakati mdomoni mwake anamshukuru na kumsifu Mungu; anamwomba Mungu, na anamtegemea Mungu, wakati huo pia akimdanganya Mungu; "analiinua" jina Mungu, na kuutazama uso wa Mungu, halafu pia bila haya na bila kuwa na aibu anakaa katika kiti cha enzi cha Mungu na kuuhukumu "udhalimu" wa Mungu; kutoka katika kinywa chake yanatoka maneno kwamba anapaswa kumshukuru Mungu, na anayatazama maneno ya Mungu, ilhali katika moyo wake anavurumisha shutuma kwa Mungu; yeye ni "mvumilivu" kwa Mungu halafu anamkandamiza Mungu, na kinywa chake kinasema ni kwa ajili ya Mungu; mikononi mwake ameshikilia vitu vya Mungu, na kinywani mwake anatafuna chakula ambacho Mungu amempa, lakini macho yake yanamtazama Mungu bila hisia kabisa, kana kwamba anatamani kummeza mzima; anautazama ukweli lakini anasisitiza kuwa ni hila ya Shetani; anatazama haki lakini anailazimisha iwe kujikana; anatazama matendo ya mwanadamu lakini anasisitiza kuwa ni kile Mungu alicho; anatazama karama za asili za mwanadamu lakini anasisitiza kuwa ni ukweli; anatazama matendo ya Mungu lakini anasisitiza kuwa ni kiburi na majivuno, matendo ya kiburi na kujidai; mwanadamu anapomwangalia Mungu, anasisitiza kumpachika kuwa kama mwanadamu, na anajitahidi sana kumweka katika kiti cha kiumbe aliyeumbwa anayeshirikiana na Shetani; anajua kweli kabisa kuwa ni matamshi ya Mungu, lakini atasema si kitu chochote zaidi ya maandiko ya mwanadamu; anajua vizuri kabisa kwamba Roho anatambulika katika mwili, Mungu anakuwa mwili, lakini anasema tu kuwa mwili huu ni uzao[36] wa Shetani; anajua kikamilifu kuwa Mungu ni mnyenyekevu na amejificha, lakini anasema tu kwamba Shetani ameaibishwa, na Mungu ameshinda. Ni mambo yasiyofaa! Mwanadamu hata hafai kuwa mbwa mlinzi! Hawezi kutofautisha kati ya nyeusi na nyeupe, na hata anachanganya kwa makusudi nyeusi kuwa nyeupe. Je, nguvu na husuru za mwanadamu vinaweza kustahimili siku ya ukombozi wa Mungu? Baada ya kumpinga Mungu kwa kukusudia, mwanadamu hajali, au anakaribia kumuua, asimpatie Mungu nafasi ya kujionyesha. Haki iko wapi? Upendo uko wapi? Anakaa kando ya Mungu, na kumshurutisha Mungu apige magoti ili Aombe msamaha, kutii mipango yake yote, kuridhia hila zake zote, na anamfanya Mungu kufuata nyayo Zake zote katika yote Afanyayo, la sivyo anaghadhibishwa[37] na kupandwa na hasira. Inawezekanaje Mungu asijawe na maumivu katika ushawishi huo wa giza, ambao unachanganya nyeusi kuwa nyeupe? Angewezaje kukosa kuwa na wasiwasi? Kwa nini inasemwa kwamba Mungu alipoanza kazi yake ya hivi karibuni kabisa, ilikuwa kama alfajiri ya mwanzo mpya? Matendo ya mwanadamu ni "yenye utajiri," ni "chemchemi isiyokoma ya maji ya uzima" bila kukoma "yanajaza tena" shamba la moyo wa mwanadamu, wakati "chemchemi isiyokoma ya maji ya uzima" ya mwanadamu inashindana dhidi ya Mungu bila haya[38]; wawili hawa hawapatani, na anawapa watu vitu kwa niaba ya Mungu bila kuacha chochote, wakati mwanadamu anashirikiana naye bila kujali hatari iliyopo. Na kwa athari gani? Anamtupilia mbali Mungu upande mmoja, na kumweka mbali, mahali ambapo watu hawatamzingatia, wakiogopa sana kwamba Atawavutia, na anaogopa sana kwamba chemchemi isiyokoma ya maji ya uzima ya Mungu itamteka mwanadamu, na kumpata mwanadamu. Hivyo, baada ya kupitia uzoefu wa miaka mingi wa masuala ya kidunia, anakula njama dhidi ya Mungu, na hata anamfanya Mungu kuwa mlengwa wa adhabu yake. Ni kana kwamba Mungu amekuwa kama gogo machoni pake, na anatamani kumnyakua Mungu na kumweka motoni ili Atakaswe na kusafishwa. Mwanadamu anapoona mahangaiko ya Mungu, anapiga kifua chake na kucheka, anacheza kwa furaha, na kusema kwamba Mungu pia Ametumbukizwa katika usafishaji, na anasema kwamba atausafisha uchafu wa Mungu, kana kwamba hii ni ya kiurazini na ina maana, kana kwamba hizi tu ndizo njia za haki na zenye mantiki za Mbinguni. Tabia hii ya fujo ya mwanadamu inaonekana kuwa ni ya makusudi na ya kutofahamu. Mwanadamu anaufichua uso wake mbaya na roho yake mbaya, vilevile sura ya kusikitisha ya ombaomba; baada ya kufanya ghasia sana, anavaa sura ya kuhurumisha na kuomba msamaha kutoka Mbinguni, akifanana na udongo uliokandwa wa kisikitisha. Mwanadamu siku zote hutenda kwa namna asivyotarajiwa, siku zote "humwendesha duma ili kuwatisha wengine[b]", anajiunga katika raha apatapo nafasi, haujali moyo wa Mungu hata kidogo, wala halinganishi hadhi yake mwenyewe. Kimyakimya anampinga Mungu tu, kana kwamba Mungu amemkosea, na Hapaswi kumtendea hivyo, na kana kwamba Mbingu haina macho na inafanya mambo kuwa magumu kwake kwa makusudi. Hivyo mwanadamu anapanga njama za siri siku zote, na halegezi matakwa yake kwa Mungu hata kidogo, akitazama kwa macho ya kupora, akitazama kwa hasira kila kitu Anachokifanya Mungu, hafikirii kamwe kwamba yeye ni adui ya Mungu, na ana matumaini kwamba siku itakuja ambapo Mungu atautawanya umande, na kuviweka vitu wazi, na kumwokoa kutoka katika "kinywa cha duma" na kulipiza kisasi kwa niaba yake. Hata leo, watu bado hawafikiri kwamba wanatekeleza jukumu la kumpinga Mungu, jukumu ambalo limetekelezwa na wengi kwa enzi nyingi sana; wangewezaje kujua kwamba, katika yote wanayofanya, wamepotoka toka kitambo, kwamba yote waliyoyaelewa yalimezwa na bahari kitambo.


Ni nani ambaye amewahi kuukubali ukweli? Ni nani ambaye amewahi kumkaribisha Mungu kwa mikono yote? Nani ambaye amewahi kuutamani uwepo wa Mungu? Tabia ya mwanadamu imeoza toka kitambo, na unajisi wake umelifanya hekalu la Mungu lisitambulike toka zamani. Mwanadamu, wakati ule ule, bado anaendelea kufanya kazi yake mwenyewe, akimdharau Mungu siku zote. Ni kana kwamba upinzani wake kwa Mungu umeandikwa kwenye jiwe, na haubadiliki, na kwa hiyo, ni bora alaaniwe kuliko kuendelea kuteseka kutendewa vibaya na maneno na matendo yake. Watu kama hawa wangewezaje kumjua Mungu? Wangewezaje kupata pumziko kwa Mungu? Na wangewezaje kufaa kuja mbele za Mungu?

kutoka katika "Kazi na Kuingia (9)" katika Neno Laonekana katika Mwili

37. Nimetumia siku nyingi nikiwa na mwanadamu, Nimeishi duniani pamoja na mwanadamu, na Sijawahi kutaka vitu zaidi kutoka kwa mwanadamu; Ninamwongoza tu mwanadamu kusonga mbele zaidi, ninamwongoza tu mwanadamu, na kwa ajili ya hatima ya binadamu, bila kuchoka Nafanya kazi ya kupangilia. Nani ambaye amewahi kuelewa mapenzi ya Baba wa mbinguni? Nani amewahi kupita kati ya mbingu na dunia? Sitamani kuishi tena na mwanadamu katika "uzee" wake tena, kwani mwanadamu ni wa mtindo wa zamani sana, haelewi chochote, kitu pekee anachojua ni kula kwa kuvimbiwa kwenye sherehe Niliyoiandaa, akijitenga na yote—hafikirii suala jingine lolote lile. Binadamu anateseka sana, makelele, huzuni, na hatari miongoni mwa wanadamu ni kubwa sana, na hivyo Sitamani kushiriki naye matunda ya thamani ya kupata ushindi niliyoyapata wakati wa siku za mwisho. Acha mwanadamu afurahie baraka tele ambazo ametengeneza yeye mwenyewe, maana mwanadamu hanikaribishi–kwa nini Nimlazimishe binadamu kulazimisha tabasamu? Kila kona ya dunia imeondolewa joto, hakuna hata chembe ya chemchemi katika ardhi yote ya nchi, maana, kama vile kiumbe aishiye majini, hana joto hata kidogo, yeye ni kama maiti, na hata damu inayopita katika mishipa yake ni kama barafu iliyoganda inayofanya moyo kuwa baridi. Wema uko wapi? Mwanadamu alimsulubisha Mungu msalabani bila sababu yoyote, na baadaye hakuhisi wasiwasi wowote. Hakuna hata mmoja aliyekuwa na majuto, na madikteta hawa katili bado wanapanga "kumkamata Akiwa hai[39]" Mwana wa Adamu kwa mara nyingine na kumleta mbele ya kikosi cha wanajeshi, ili kukomesha chuki iliyo ndani ya mioyo yao. Kuna faida gani Kwangu kubaki katika nchi hii ya hatari? Nikibaki, kitu pekee Nitakachomletea mwanadamu ni mgogoro na fujo, na hakutakuwa na mwisho wa shida, maana Sijawahi kumpa mwanadamu amani, ni vita tu. Siku za mwisho za binadamu lazima zijae vita, na hatima ya mwanadamu lazima ipinduliwe katikati ya vurugu na mgogoro. Siko tayari "kushiriki" katika "furaha" ya vita, singeweza kuandamana naumwagaji damu na mwanadamu kujitoa mhanga, maana mwanadamu kunikataa kumenipelekea "hali ya kukata tamaa," na Sina ujasiri wa kuangalia vita vya mwanadamu—hebu mwanadamu apigane kuuridhisha moyo wake, Natamani kupumzika, Nataka kulala, acha mapepo wawe washirika wa binadamu wakati wa siku zake za mwisho! Nani ajuaye mapenzi Yangu? Kwa sababu sijakaribishwa na mwanadamu, na hajawahi kunisubiri, Ninaweza tu kumuaga, nami Ninamkabidhi hatima yake, Namwachia mwanadamu utajiri Wangu wote, Nayapanda maisha Yangu ndani ya mwanadamu, Napanda mbegu ya maisha Yangu ndani ya shamba la moyo wa mwanadamu, Namwachia kumbukumbu za milele, Namwachia upendo Wangu wote kwa binadamu, Nampa mwanadamu yote ambayo anafurahia Kwangu, kama zawadi ya upendo ambayo kwayo tunaitamani kwa kila mmoja. Ningependa tupendane milele, kwamba jana yetu iwe kitu kizuri sana tunachopeana mmoja kwa mwingine, maana Nimejitoa kikamilifu kwa binadamu–ni malalamiko gani ambayo mwanadamu anaweza kuwa nayo? Tayari Nimeyaacha maisha Yangu yote kwa mwanadamu, na bila neno lolote, Nimefanya bidii kulima ardhi nzuri ya upendo kwa ajili ya binadamu; Sijawahi kutaka matakwa yoyote linganifu kutoka kwa mwanadamu, nami Nijitiisha tu katika mipangilio ya mwanadamu na kutengeneza kesho nzuri zaidi ya binadamu.

kutoka katika "Kazi na Kuingia (10)" katika Neno Laonekana katika Mwili

38. Mungu kupata mwili imesababisha mawimbi mazito katika vikundi na madhehebu yote, "imeparaganya" mpangilio wao wa awali, na imetikisa mioyo ya wale wanaotamani sana kuonekana kwa Mungu. Ni nani asiyeabudu? Nani hatamani kumwona Mungu? Mungu amekuwa miongoni mwa wanadamu kwa miaka mingi, lakini mwanadamu kamwe hajawahi kutambua. Leo, Mungu mwenyewe Amejitokeza, na Ameonyesha kwa watu—inawezekanaje hii isiufurahishe moyo wa mwanadamu? Mungu aliwahi kushiriki furaha na huzuni pamoja na mwanadamu, na leo Ameunganika tena na mwanadamu, na Anashiriki visa vya muda uliopita Akiwa pamoja naye. Baada ya kutoka Uyahudi, watu hawakuweza Kumwona tena. Wanatamani kukutana na Mungu tena, bila kujua kwamba leo wamekutana naye tena, na kuungana naye tena. Inawezekanaje hii isiamshe mawazo ya jana? Siku kama ya leo miaka elfu mbili iliyopita, Simoni wa Yona, uzao wa Wayahudi, alimtazama Yesu Mwokozi, alikula meza moja naye, na baada ya kumfuata kwa miaka mingi alihisi kumpenda sana: Alimpenda sana kutoka moyoni mwake, alimpenda sana Bwana Yesu. Wayahudi hawakujua jinsi mtoto huyu mwenye nywele za dhahabu, Aliyezaliwa katika hori la ng'ombe lililo baridi, Alikuwa sura ya kwanza ya Mungu kupata mwili. Wote walidhani kwamba Alikuwa mmoja wao, hakuna aliyemfikiria kuwa tofauti—watu wangewezaje kumtambua Yesu huyu wa kawaida? Wayahudi walidhani kwamba alikuwa ni mtoto wa Kiyahudi wa wakati huo. Hakuna aliyemtazama kama Mungu mwenye upendo, na watu walitoa masharti Kwake tu bila kufikiri, wakiomba Awape neema nyingi, na amani, na furaha. Walijua tu kwamba, kama milionea, Alikuwa na kila kitu ambacho mtu angetamani kuwa nacho. Lakini watu hawakumchukulia kama mtu ambaye Alikuwa mpendwa; watu wa wakati huo hawakumpenda, na walimpinga tu, na walitoa masharti yasiyokuwa na mantiki kutoka Kwake, na Hakuwahi kupinga, Aliendelea kutoa neema kwa mwanadamu, hata ingawa mwanadamu hakumjua. Hakufanya chochote isipokuwa kwa kimya kumpatia mwanadamu wema, upendo, na huruma, na hata zaidi, Alimpatia mwanadamu njia mpya ya kutenda, Akimwondoa mwanadamu kutoka katika vifungo vya sheria. Mwanadamu hakumpenda, alimhusudu tu na kutambua talanta Zake za kipekee. Wanadamu vipofu wangejuaje jinsi ambavyo Yesu Mwokozi Alipitia mateso makubwa Alipokuja miongoni mwa wanadamu? Hakuna aliyejali dhiki Zake, hakuna mtu aliyejua upendo Wake kwa Mungu Baba, na hakuna ambaye angeweza kujua kuhusu upweke Wake; hata ingawa Maria alikuwa mama Yake wa kumzaa, angewezaje kujua mawazo yaliyokuwa moyoni mwa Bwana Yesu mwenye huruma? Nani alijua mateso yasiyoelezeka Aliyoyapitia Mwana wa Adamu? Baada ya kutoa masharti Kwake, watu wa kipindi hicho walimsahau bila huruma, na kumtupa nje. Basi Alizungukazunguka mitaani, siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka, Akienda bila mwelekeo kwa miaka mingi hadi Alipofikisha miaka thelathini na mitatu, miaka ambayo ilikuwa mirefu na mifupi. Watu walipomhitaji, walimwalika nyumbani mwao wakiwa na nyuso za tabasamu, wakijaribu kutoa masharti Kwake—na baada Yake kuwasaidia, walimsukuma nje ya mlango mara moja. Watu walikula Alichokitoa mdomoni Mwake, walikunywa damu Yake, walifurahia neema Alizowapatia, lakini bado walimpinga, maana hawakuwahi kujua nani aliyewapa uhai wao. Hatimaye, walimsulubisha msalabani, lakini bado Hakutoa sauti. Hata leo, bado Anabakia kimya. Watu wanakula mwili Wake, wanakula chakula Anachowatengenezea, wanapita njia ambayo Ameifungua kwa ajili yao, na wanakunywa damu Yake, lakini bado wanakusudia kumkataa, kimsingi wanamchukulia Mungu ambaye Amewapa maisha yao kama adui, na badala yake wanawachukulia wale ambao ni watumwa kama wao jinsi walivyo kama Baba wa mbinguni. Katika hili, je, hawampingi kwa makusudi? Yesu aliwezaje kufa msalabani? Je, mnajua? Je, Hakusalitiwa na Yuda, ambaye alikuwa karibu kabisa naye, na alikuwa amemla, akamnywa, na akamfurahia? Je, sababu ya usaliti wa Yuda haikuwa kwa sababu Yesu alikuwa tu mwalimu mdogo wa kawaida? Ikiwa watu walikuwa wameona kweli kwamba Yesu hakuwa wa kawaida, na Ambaye Alitoka mbinguni, wangewezaje kumsulubisha msalabani Akiwa hai kwa masaa ishirini na manne, hadi Alipoishiwa na pumzi katika mwili wake? Nani awezaye kumjua Mungu? Watu wanamfurahia Mungu tu kwa tamaa isiyotosheka, lakini hawajawahi kumjua. Walipewa inchi na wamechukua maili, na wanamfanya Yesu kutii kabisa amri zao, maelekezo yao. Nani ambaye amewahi kuonyesha huruma kwa Mwana wa Adamu huyu, Ambaye hana mahali pa kuweka kichwa Chake? Nani ambaye amewahi kufikiria kuungana naye ili kukamilisha agizo la Mungu Baba? Ni nani ambaye amewahi kumuwaza? Ni nani mbaye amewahi kuyajali matatizo Yake? Bila upendo hata kidogo, mwanadamu anamvuta nyuma na mbele; mwanadamu hajui nuru na uhai wake vinatoka wapi, na anapanga kwa siri tu jinsi ya kumsulubisha tena Yesu wa miaka elfu mbili iliyopita, ambaye amepitia uzoefu wa maumivu miongoni mwa wanadamu. Je, Yesu anawatia anachochea chuki ya namna hiyo? Je, yote Aliyoyafanya yamesahaulika kitambo? Chuki ambayo ilichanganyika kwa maelfu ya miaka itaibuka tena. Nyinyi tabaka la Wayahudi! Yesu amewahi kuwa adui kwenu lini, hadi mmchukie kiasi hicho? Amefanya mengi sana, na kuzungumza mengi sana—je, hakuna chochote chenye manufaa kwenu? Ameyatoa maisha Yake kwenu bila kutazamia kulipwa chochote, Amejitoa mzima kwenu—kweli bado mnataka kumla Akiwa mzima? Amejitoa kwenu kikamilifu bila kuacha kitu chochote, bila kufurahia utukufu wa kidunia, wema miongoni mwa wanadamu, na upendo miongoni mwa wanadamu, au baraka zote miongoni mwa wanadamu. Watu ni wachoyo sana Kwake, Hajawahi kufurahia utajiri wote duniani, Anautoa moyo Wake wote, wa upendo na dhati, kwa mwanadamu, Amejitoa Yeye mzima kwa mwanadamu—na nani ambaye amemfanyia wema? Ni nani aliyewahi kumpatia faraja? Mwanadamu amemjazia mashinikizo yote, balaa yote amempatia Yeye, Amejitwika shida zote mbaya kati ya wanadamu, anamtupia lawama kwa uonevu wote, na Ameikubali kimyakimya. Je, Amewahi kumpinga mtu yeyote? Je, Amewahi kuomba fidia hata ndogo kutoka kwa mtu yeyote yule? Nani amewahi kuonyesha huruma yoyote Kwake? Kama watu wa kawaida, ni nani miongoni mwenu ambaye hakuwa na kipindi cha utotoni chenye mapenzi ya dhati? Ni nani ambaye hakuwa na ujana wa kupendeza? Ni nani ambaye hana joto la wapendwa? Ni nani ambaye hana upendo wa jamaa na marafiki? Ni nani ambaye haheshimiwi na wengine? Ni nani ambaye hana familia yenye upendo? Ni nani ambaye hana faraja ya wandani wake? Je, Amewahi kufurahia yote kati ya haya? Ni nani ambaye amewahi kumtendea wema hata kidogo? Ni nani ambaye amewahi kumpa faraja hata kidogo? Ni nani ambaye amewahi kumwonyesha angalau maadili kidogo ya kibinadamu? Ni nani ambaye amewahi kuwa mvumilivu Kwake? Ni nani ambaye amewahi kuwa pamoja naye katika nyakati za shida? Ni nani ambaye amewahi kupitia maisha ya shida pamoja naye? Mwanadamu hajawahi kulegeza matakwa yake Kwake; anatoa masharti Kwake tu bila hata haya, kana kwamba kwa kuwa Amekuja katika ulimwengu wa mwanadamu, Anapaswa kuwa ng'ombe au farasi wake, mtumwa wake, na Anapaswa kumpa mwanadamu kila kitu Chake; Asipofanya hivyo, mwanadamu hatawahi kumsamehe, hatawahi kumtendea vyema, hatawahi kumwita Mungu, na hatawahi kumheshimu. Mwanadamu ni katili sana katika mtazamo wake kwa Mungu, kana kwamba ana nia ya kumtesa Mungu hadi kifo, ni baada ya hapo tu ndipo atapunguza masharti yake kwa Mungu; kama sivyo, mwanadamu hatapunguza kiwango cha matakwa yake kwa Mungu. Inawezekanaje mwanadamu kama huyu asidharauliwe na Mungu? Je, hili si janga la siku hizi? Dhamiri ya mwanadamu haionekani. Anasema tu ataulipiza upendo wa Mungu, lakini anamchanachana Mungu na kumtesa hadi kifo. Je, hii sio "mbinu ya siri" kwa imani yake kwa Mungu, iliyorithishwa kutoka kwa mababu zake? Hakuna mahali popote ambapo "Wayahudi" hawapatikani, na leo bado wanafanya kazi ile ile, bado wanafanya kazi ile ile ya kumpinga Mungu, na bado wanaamini kwamba wanamheshimu Mungu. Inawezekanaje macho ya mwanadamu yamjue Mungu? Inawezekanaje mwanadamu, anayeishi katika mwili, kumchukulia Mungu kama Mungu mwenye mwili ambaye Amekuja kutokana na Roho? Ni nani miongoni mwa wanadamu anaweza kumjua? Ukweli uko wapi miongoni mwa wanadamu? Haki ya kweli iko wapi? Ni nani anayeweza kuijua tabia ya Mungu? Ni nani anayeweza kushindana na Mungu mbinguni? Haishangazi kwamba, Alipokuja miongoni mwa wanadamu, hakuna aliyemjua Mungu, na amekataliwa. Mwanadamu anawezaje kuvumilia kuwepo kwa Mungu? Anawezaje kuruhusu mwanga kuliondosha giza la ulimwengu? Je, hii yote si kujitoa kwa heshima kwa mwanadamu? Je, huku sio kuingia adilifu kwa mwanadamu? Na kazi ya Mungu haijajikita katika kuingia kwa mwanadamu? Ningependa muunganishe kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu, na kuimarisha uhusiano mzuri kati ya mwanadamu na Mungu, na kutekeleza jukumu ambalo linapaswa kutekelezwa na mwanadamu kadri ya uwezo wake. Kwa njia hii, kazi ya Mungu hatimaye itafikia mwisho, ikimalizika na utukufu Wake!

kutoka katika "Kazi na Kuingia (10)" katika Neno Laonekana katika Mwili

Tanbihi:

27. "Maangamizi" inatumiwa kuweka wazi kutotii kwa wanadamu.

28. "Yamekutana nyuso kali na ufidhuli wa maneno makali. Mungu anaweza tu kustahimili, Akiwa Ameinamisha kichwa, Akiwahudumia watu kama ng'ombe aliye radhi" ni kwa asili sentensi moja, lakini hapa imegawanywa mara mbili ili kuyafanya mambo wazi zaidi. Sentensi ya kwanza inahusu matendo ya mwanadamu, huku ya pili inaonyesha mateso aliyoyapitia Mungu, na kwamba Mungu ni mnyenyekevu na Aliyefichika.

29. "Upendeleo" unahusu tabia ya watu ya ukaidi.

30. "Chukua mamlaka kamili" inahusu tabia ya watu ya ukaidi. Wanajitukuza, huwafunga wengine, wakiwafanya wawafuate na kuteseka kwa ajili yao. Wao ni majeshi ambayo ni yenye uadui kwa Mungu.

31. "Kibaraka" inatumiwa kuwadhihaki wale ambao hawamjui Mungu.

32. "Kuongezeka kwa haraka" inatumiwa kuonyesha tabia duni ya watu.

33. "Hawezi kutambua tofauti muhimu" inaonyesha wakati ambapo watu wanageuza mapenzi ya Mungu kuwa kitu cha kishetani, ikitaja kwa upana tabia ambayo kwayo watu humkataa Mungu.

34. "Gaidi" inatumiwa kuonyesha kwamba watu ni wapumbavu na hawana ufahamu.

35. "Mabaki na makombo" inatumiwa kuonyesha tabia ambazo kwazo watu humdhulumu Mungu.

36. "Uzao" inatumiwa kwa dhihaka.

37. "Anaghadhibishwa" inahusu uso mbaya wa mwanadamu aliye na hasira na aliyeudhika.

38. "Bila haya" inahusu wakati ambapo watu hawajali, na hawana uchaji kuhusiana na Mungu hata kidogo.

39. "Kamata Akiwa hai" inahusu tabia ya vurugu na yenye kustahili dharau ya mwanadamu. Mwanadamu ni mkatili na hayuko tayari kumsamehe Mungu hata kidogo, na hufanya madai ya upuuzi Kwake.

b. Hii ni istiara ya Kichina.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni