Smiley face

Jumatatu, 19 Agosti 2019

Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya "Maono ya Kazi ya Mungu" (Sehemu ya Kwanza)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

1. Yohana alianza kueneza injili ya ufalme wa mbinguni miaka saba kabla ya ubatizo wa Yesu. Kwa watu, kazi aliyoifanya ilionekana kuwa juu zaidi ya kazi ya baadaye ya Yesu, ilhali yeye alikuwa, hata hivyo, nabii tu. Hakufanya kazi au kuzungumza ndani ya hekalu, lakini katika miji na vijiji nje yake. Hii alifanya, bila shaka, miongoni mwa taifa la Wayahudi, hasa wale waliokuwa maskini. Ni mara chache ambapo Yohana alitangamana na watu kutoka ngazi za juu za jamii, na alieneza injili miongoni mwa watu wa kawaida wa Yudea tu ili kuandaa watu wema kwa Bwana Yesu, na kuandaa maeneo yafaayo Kwake kufanya kazi. Kwa sababu ya kuwa na nabii kama Yohana wa kuandaa njia, Bwana Yesu Alikuwa na uwezo wa kuanzisha njia Yake ya msalaba mara moja punde tu Alipowasili. Wakati Mungu Alipogeuka kuwa mwili ili kufanya kazi yake, hakuwa na jukumu la kufanya kazi ya kuwachagua watu, na hakuwa na haja ya kuwatafuta watu binafsi au mahali ambapo Angefanyia kazi. Hakufanya kazi kama hii Alipokuja; mtu afaaye alikuwa tayari Amemwandalia kabla Yeye hajawasili. … Yohana alifanya kazi kwa miaka saba, ambapo ni kusema kwamba alieneza injili kwa miaka saba. Wakati wa kazi yake, Yohana hakufanya miujiza mingi, kwa sababu kazi yake ilikua kuandaa njia, ilikuwa kazi ya maandalizi. Kazi zote zingine, kazi ambazo Yesu Alikuwa afanye, hazikuwa na uhusiano naye; alimwomba mwanadamu tu aungame dhambi zake na atubu, na aliwabatiza watu, ili waweze kuokolewa. Ingawa alifanya kazi mpya, na kufungua njia ambayo kamwe mwanadamu alikuwa bado hajaitembea, bado alimwandalia Yesu njia. Alikuwa nabii tu ambaye alifanya kazi ya maandalizi, na hakuwa na uwezo wa kufanya kazi ya Yesu. Ingawa Yesu hakuwa wa kwanza kuhubiri kuhusu ufalme wa mbinguni, na japokuwa aliendelea na njia ambayo Yohana alianzisha, bado hakukuwa na mwingine ambaye angeweza kufanya kazi yake, na ilikuwa juu zaidi ya kazi ya Yohana. Yesu hangeandaa njia yake mwenyewe; kazi yake ilitekelezwa moja kwa moja kwa niaba ya Mungu. Na hivyo, bila kujali ni miaka mingapi Yohana alifanya kazi, bado alikuwa nabii, na bado yule aliyeandaa njia. Miaka mitatu ya kazi iliyofanywa na Yesu ilizidi miaka saba ya kazi aliyofanya Yohana, kwa kuwa kiini cha kazi yake hakikuwa cha kiwango sawa.

kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili

2. Wakati huo, sehemu ya kazi ya Yesu ilikuwa kwa mujibu wa Agano la Kale, pia na sheria za Musa na maneno ya Bwana wakati wa kipindi cha Enzi ya Sheria. Yote hayo Yesu Alitumia kufanya sehemu ya kazi yake. Alihubiri kwa watu na kuwafundisha kwenye masinagogi, na yeye Alitumia utabiri wa manabii katika Agano la Kale kuwakemea Mafarisayo waliokuwa na uhasama Naye, na Alitumia maneno katika Maandiko kufichua uasi wao na hivyo kuwahukumu. Kwa maana wao walidharau mambo ambayo Yesu Aliyafanya; hasa, nyingi ya kazi ya Yesu haikufuatana na sheria katika Maandiko, na zaidi ya hayo, kile Alichofundisha kilikuwa kikuu kuliko maneno yao wenyewe, na hata kikubwa kuliko kile ambacho kilikuwa kimetabiriwa na manabii katika Maandiko. Kazi ya Yesu ilikuwa kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu na kusulubiwa tu. Kwa hivyo, hakukuwa na haja Kwake kusema maneno zaidi ili kumshinda mtu yeyote. Mengi ya yale Aliyomfundisha mwanadamu yalitolewa kutoka kwa Maandiko, na hata kama kazi yake haikuzidi Maandiko, bado Aliweza kutimiza kazi ya kusulubiwa. Yake haikuwa kazi ya neno, wala kwa ajili ya kumshinda mwanadamu, lakini kwa minajili ya kumkomboa mwanadamu. Yeye Alihusika kama dhabihu ya dhambi tu kwa mwanadamu, na hakuhusika kama chanzo cha Neno kwa mwanadamu. Hakufanya kazi ya watu wa Mataifa mengine, ambayo ilikuwa kazi ya kumshinda mwanadamu, bali Alifanya kazi ya kusulubiwa, kazi ambayo ilifanywa miongoni mwa wale ambao waliamini kulikuwa na Mungu. Japokuwa kazi yake ilifanywa juu ya msingi wa Maandiko, na Alitumia yale yaliyotabiriwa na manabii wa kale kuwahukumu Mafarisayo, hii ilikuwa ya kutosha kukamilisha kazi ya kusulubiwa. Kama kazi ya leo ingekuwa bado inafanyika juu ya misingi ya utabiri wa manabii wa kale katika Maandiko, basi haingewezekana nyinyi kushindwa, kwa kuwa Agano la Kale halina kumbukumbu ya uasi na dhambi zenu nyinyi watu wa China, hakuna historia ya dhambi zenu. Kwa hivyo, kama kazi hii bado ingedumu katika Biblia, hamngeweza kutoa matunda. Biblia inaandika lakini kwa uchache historia ya wana wa Israeli, ambayo haina uwezo wa kusadikisha iwapo nyinyi ni waovu ama wema, ama ya kukuhukumu. Hebu Fikiria kama Ningekuwa wa kuwahukumu nyinyi kadri ya historia ya wana wa Israeli—bado mngenifuata Mimi kama mnavyonifuata hivi leo? Je, mnajua jinsi ambavyo nyinyi m wagumu? Kama hakuna maneno ambayo yalisemwa wakati wa awamu hii, basi itakuwa vigumu kukamilisha kazi ya ushindi. Kwa sababu Mimi sijakuja kugongomewa msumari msalabani, sharti Mimi niseme maneno ambayo ni tofauti na yatokayo kwa Biblia, ilimradi muweze kushindwa.

kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili

3. Yote ambayo hufanywa leo ni kwa msingi wa siku hizi, lakini bado yako juu ya msingi wa kazi ya Bwana katika Enzi ya Sheria, na hayavuki mipaka ya eneo hili. Kuulinda ndimi zenu, na kutozini, kwa mfano—Je, hizi si sheria za Agano la Kale? Leo, kile kinachotakikana kwenu sio chenye upeo wa amri kumi tu, lakini ni amri ambazo zina ukuu kuliko hizo zilizokuwepo hapo awali, ila hii haina maana kuwa kile kilichokuja hapo awali kimeondolewa, kwa kuwa kila awamu ya kazi ya Mungu hufanywa juu ya msingi wa awamu ambayo ilikuja hapo awali. … Kama, leo, mngetakiwa tu kufuata amri na kutii sheria za Agano la Kale, kwa namna sawa na wana wa Israeli, na kama, hata, nyinyi mlitakiwa mkariri sheria ambazo ziliwekwa na Bwana, hakungekuwa na uwezekano kwamba mngeweza kubadilika. Kama mngekuwa tu mnatakiwa kutii zile amri chache zilizo na mipaka ama kukariri sheria zisizohesabika, asili zenu za zamani zingebaki zimekita mizizi, na hakungekuwa na mbinu ya kuzing’oa. Hivyo mngeendelea kuzidi kupotoshwa, na hakuna hata mmoja wenu angeweza kuwa mtiifu. Ambayo ni kusema kwamba amri chache rahisi au sheria zisizohesabika hazina uwezo wa kuwasaidia kujua matendo ya Yehova. Nyinyi si sawa na wana wa Israeli: kwa kufuata sheria na kukariri amri waliweza kushuhudia matendo ya Yehova, na kumpa Yeye pekee ibada yao , lakini hamwezi kufanikisha hili, na amri chache za Agano la Kale haziwezi tu kuwafanya nyinyi kupeana mioyo yenu, au kuwalinda, lakini badala yake itawafanya muwe wazembe, na kuwateremsha mpaka Kuzimu. Kwa sababu kazi Yangu ni kazi ya ushindi, na inalenga uasi wenu na asili yenu ya zamani. Maneno yenye huruma ya Yehova na Yesu yanapungukiwa mno na maneno makali ya hukumu leo. Bila maneno makali kama haya, ingekuwa vigumu kuwashinda ninyi "wataalam," ambao mmekua wasiotii kwa miaka elfu nyingi. Sheria za Agano la Kale zilipoteza nguvu zake kwenu kwa muda mrefu uliopita, na hukumu ya leo ni ya kuogofya mno kuliko sheria za zamani. Ya kuwafaa nyinyi zaidi ni hukumu, na wala si vikwazo duni vya sheria, kwa kuwa ninyi si wanadamu wa mwanzo kabisa, lakini wanadamu ambao wamekuwa fisadi kwa miaka elfu nyingi. Kile ambacho mwanadamu lazima atimize sasa ni kulingana na hali halisi ya mwanadamu leo, kulingana na tabia bora na kimo halisi cha mwanadamu wa siku hizi, na hakihitaji kwamba wewe ufuate mafundisho ya dini. Hii ni kwa minajili ya mabadiliko yaweze kupatikana katika asili zako za zamani, na ili uweze kutupa kando dhana zako.

kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili

4. Wakati huo kazi ya Yesu ilikuwa ni ukombozi wa wanadamu wote. Dhambi za wote ambao walimwamini zilisamehewa; ilimradi wewe ulimwamini, Angeweza kukukomboa wewe; kama wewe ulimwamini Yeye, wewe hukuwa tena mwenye dhambi, wewe ulikuwa umeondolewa dhambi zako. Hii ndiyo ilikuwa maana ya kuokolewa, na kuhesabiwa haki kwa imani. Hata hivyo, kati ya wale walioamini, kulibaki na kitu ambacho kilikuwa na uasi na pingamizi kwa Mungu, na ambacho kilibidi kiondolewe polepole. Wokovu haukuwa na maana kuwa mwanadamu alikuwa amepatwa na Yesu kabisa, lakini ni kuwa mwanadamu hakuwa tena mwenye dhambi, na kuwa alikuwa amesamehewa dhambi zake; mradi tu uliamini, wewe kamwe hungekuwa mwenye dhambi. … Yesu hakuja kumkamilisha na kumpata mwanadamu, lakini kufanya awamu moja ya kazi: kuleta injili ya ufalme wa mbinguni na kukamilisha kazi ya kusulubiwa—na punde tu Yesu Aliposulubishwa, kazi Yake ilifika mwisho kamili. Lakini kwa awamu iliyoko sasa—kazi ya ushindi—maneno mengi zaidi lazima yasemwe, kazi nyingi zaidi lazima ifanywe, na lazima kuwe na hatua nyingi. Hivyo pia ni lazima siri za kazi ya Yesu na Yehova zitafichuliwa, ili wanadamu wote waweze kuwa na ufahamu na uwazi wa imani yao, kwa kuwa hii ni kazi ya siku za mwisho, na siku za mwisho ni mwisho wa kazi ya Mungu, wakati wa kuhitimisha kazi hii. Hii awamu ya kazi itakufafanulia sheria ya Yehova na ukombozi wa Yesu, na ni hasa ili uweze kuelewa kazi nzima ya mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita, na kuelewa kusudi la kazi zote Alizozifanya Yesu na maneno Aliyoyasema, na hata upofu wako wa imani kwenye na katika ibada ya Biblia. Yote haya yatakuwezesha kujua. Wewe utakuja kufahamu kazi anayoifanya Yesu na kazi ya Mungu leo; utaelewa na kushuhudia ukweli wote, uzima, na njia. Katika awamu ya kazi Aliyoifanya Yesu, kwa nini Yesu Aliondoka bila kumaliza kazi ya Mungu? Kwa sababu awamu ya kazi ya Yesu haikuwa kazi ya kumalizia. Wakati Yeye Alisulubishwa msalabani, maneno ambayo Alikuwa Ameyasema pia yalikuwa yamefika mwisho; baada ya kusulubiwa kwake, kazi Yake kwa hivyo ilimalizika. Awamu ya sasa ni tofauti. Ni baada tu ya maneno hayo kusemwa hadi mwisho na kazi nzima ya Mungu iwe imehitimika ndipo kazi yake itakapokuwa imemalizika. Wakati wa awamu ya kazi ya Yesu, kulikuwa na maneno mengi yaliyobakia bila kusemwa, au ambayo hayakuwa yameelezwa kikamilifu kwa ufasaha. Waama, Yesu hakujali Alichosema au kile ambacho hakusema, kwa kuwa huduma yake haikuwa huduma ya maneno; na hivyo baada ya Yeye kusulubishwa msalabani Aliondoka. Awamu hiyo ilikuwa hasa kwa ajili ya kusulubiwa, na ni tofauti na awamu ya sasa. Awamu ya kazi hii ni hasa kwa ajili ya kukamilisha, kufumbua, na kuleta kazi yote kwenye hitimisho. Kama maneno hayasemwi hadi tamati yake kabisa, hakutakuwa na mbinu ya kuhitimisha kazi hii, kwa kuwa awamu hii ya kazi yote inafikishwa mwisho na kukamilika kwa kutumia maneno. Wakati huo, Yesu Alifanya kazi kubwa isiyoeleweka na mwanadamu. Akaondoka kimya kimya, na leo bado kunao wengi wasioelewa maneno Yake, ambao ufahamu wao ni potofu lakini bado unaaminika nao kwamba ni sahihi, ambao hawajui kuwa wao si sahihi. Mwishoni, awamu hii ya sasa itafikisha kazi ya Mungu mwisho ulio kamilifu, na kutoa hitimisho Lake. Wote watakuja kufahamu na kujua mpango wa usimamizi wa Mungu. Dhana zilizo ndani ya mwanadamu, nia yake, fahamu yake potofu, dhana zake kuhusu kazi ya Yehova na Yesu, maoni yake kuhusu watu wa Mataifa mengine na michepuko na makosa yake yote yatarekebishwa. Na mwanadamu ataelewa njia yote ya haki ya uzima, na kazi yote anayofanya Mungu, na ukweli wote. Wakati hayo yatafanyika, awamu hii ya kazi itafikia kikomo.

kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (2)" katika Neno Laonekana katika Mwili

5. Kazi ya Yehova ilikuwa uumbaji wa ulimwengu, ilikuwa mwanzo; awamu hii ya kazi ni mwisho wa kazi, na ni hitimisho. Hapo mwanzo, kazi ya Mungu ilifanyika miongoni mwa wateule wa Israeli, na ilikuwa mapambazuko ya kipindi kipya katika pahali patakatifu zaidi ya popote. Awamu ya mwisho ya kazi inafanywa katika nchi ambayo ni chafu zaidi ya zote, kuhukumu ulimwengu na kuleta enzi kwenye kikomo. Katika awamu ya kwanza kazi ya Mungu ilifanyika katika maeneo yenye kung’aa kuliko maeneo yote, na awamu ya mwisho inafanyika katika maeneo yaliyo katika giza kuliko maeneo yote, na giza hili litaondolewa, na mwanga kufunguliwa, na watu wote kushindwa. Wakati watu wa maeneo haya yaliyo chafu kuliko yote na yaliyo na giza watakuwa wameshindwa na idadi yote ya watu wametambua kuwa Mungu yupo, na ya kuwa ni Mungu wa kweli, na kila mtu Amemwamini kabisa, basi ukweli huu utatumika kutekeleza kazi ya ushindi katika ulimwengu mzima. Awamu hii ya kazi ni ya ishara: Punde tu kazi ya kipindi hiki itakapomalizika, kazi ya miaka 6,000 ya usimamizi itafikia mwisho kabisa. Mara baada ya wale walioko katika maeneo yaliyo na giza kuliko yote watakapokuwa wameshindwa, bila shaka itakuwa hivyo pia kila mahali pengine. Kwa hivyo, kazi ya ushindi tu katika China inabeba ishara ya maana. China inajumuisha nguvu zote za giza, na watu wa China wanawakilisha wale wote ambao ni wa mwili, wa Shetani, na wa mwili na damu. Ni watu wa China ndio wamepotoshwa sana na joka kubwa jekundu, ambao wana upinzani wenye nguvu dhidi ya Mungu, ambao wana ubinadamu ulio mbovu zaidi na ulio mchafu, na kwa hivyo hao ni umbo asili la wanadamu wote wenye matendo maovu. … Kwa nini mimi daima Nimesema yakuwa nyinyi ni kiungo cha mpango wangu wa usimamizi? Ni katika watu wa China ambapo upotovu, uchafu, udhalimu, upinzani, na uasi unadhihirishwa kikamilifu zaidi na kufichuliwa kwa hali zao mbalimbali. Kwa upande mmoja, wao ni wa kimo cha umaskini, na kwa upande mwingine, maisha yao na mawazo yao ni ya nyuma kimaendeleo, na tabia zao, mazingira ya kijamii, familia ya kuzaliwa—yote ni ya umaskini na ya nyuma kimaendeleo kuliko yote. Hadhi yao, pia, ni ya chini. Kazi katika eneo hili ni ya ishara, na baada ya kazi hii ya majaribio hufanywa kwa ukamilifu wake, na kazi yake inayofuata itakwenda vizuri zaidi. Kama awamu hii ya kazi inaweza kukamilika, basi kazi inayofuata itakamilika bila shaka. Mara baada ya awamu ya kazi hii kutimizwa, na mafanikio makubwa kufikiwa kikamilifu, kazi ya ushindi katika ulimwengu mzima itakua imefikia kikomo kamili. Kwa kweli, mara baada ya kazi miongoni mwenu imekuwa ya mafanikio, hii itakuwa sawa na mafanikio katika ulimwengu mzima. Huu ndio umuhimu wa sababu Yangu kuwafanya mfano wa kuigwa na kielelezo. Uasi, upinzani, uchafu, udhalimu—yote haya hupatikana kwa watu hawa, na ndani yao pamewakilishwa uasi wote wa wanadamu. Wao ni wa kushangaza kweli. Hivyo, wanafanywa kuwa mfano wa ushindi, na punde tu watakaposhindwa watakuwa kama ilivyo kawaida kielelezo na mfano wa kuigwa na wengine.

kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (2)" katika Neno Laonekana katika Mwili

6. Hakuna kilichokuwa cha ishara zaidi ya awamu ya kwanza iliyofanyika katika Israeli: Waisraeli walikuwa watakatifu sana na wenye upotovu wa chini zaidi kuliko watu wote, na hivyo pambazuko la kipindi kipya katika nchi hii kilibeba umuhimu mkubwa. Inaweza kusemwa kwamba mababu wa wanadamu walitoka Israeli, na kwamba Israeli, ilikuwa watani wa kazi ya Mungu. Hapo mwanzo, watu hawa walikuwa watakatifu sana, na wote walimwabudu Yehova, na kazi ya Mungu ndani yao iliweza kuzaa mazao makubwa. … Walikuwa wenye upotovu wa chini zaidi ya wanadamu wote, na hapo mwanzo, walikuwa na nia ya kumtazamia Mungu na kumheshimu Yeye. Walitii maneno ya Bwana, na daima walitumika katika hekalu, na walivaa mavazi ya kikuhani au mataji. Walikuwa watu wa kwanza kabisa kuabudu Mungu, na chombo cha kwanza kabisa cha kazi yake. Watu hawa walikuwa kielelezo na mfano wa kuiga kwa wanadamu wote. Walikuwa kielelezo na mfano wa kuiga wa utakatifu na haki. Watu kama Ayubu, Ibrahim, Lutu, au Petro na Timotheo—wote walikuwa Waisraeli, na vielelezo na mifano mitakatifu zaidi ya watu wote. Israeli ilikuwa nchi ya kwanza ya kuabudu Mungu miongoni mwa wanadamu wote, na watu wengi wenye haki walitoka hapa kuliko mahali pengine popote. Mungu Alifanya kazi kati yao ili aweze kusimamia vizuri mwanadamu katika nchi zote na katika siku zijazo. Mafanikio yao na haki ya ibada yao ya Yehova yaliandikwa kwenye kumbukumbu, ili waweze kuhudumu kama vielelezo na mifano kwa watu waliokuwa nje ya Israeli wakati wa Enzi ya Neema; na matendo yao yamezingatia miaka elfu kadhaa ya kazi, mpaka hivi leo.

kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (2)" katika Neno Laonekana katika Mwili

7. Jina la Yesu liliashiria mwanzo wa Enzi ya Neema. Wakati Yesu Alianza kufanya huduma Yake, Roho Mtakatifu Alianza kutoa ushuhuda kwa jina la Yesu, na jina la Yehova halikuzungumziwa tena, na badala yake Roho Mtakatifu Alianza kazi mpya hasa kwa jina la Yesu. Ushuhuda wa wale waliomwamini Yeye ulitolewa kwa ajili ya Yesu Kristo, na kazi waliyoifanya walifanya pia kwa ajili ya Yesu Kristo. Hitimisho Enzi ya Sheria ya Agano la Kale lilimaanisha kuwa kazi iliyofanywa hasa kutumia jina la Yehova ilikuwa imefikia kikomo. Baada ya hii, jina la Mungu halikuwa Yehova tena; badala yake Yeye Aliitwa Yesu, na kutoka hapa Roho Mtakatifu Alianza kazi hasa kwa kutumia jina la Yesu.

kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili

8. Wakati Yesu Atakuja tena, enzi itakuwa tayari imebadilika, je, hivyo bado Ataweza kuitwa Yesu? Je, Mungu Anajulikana tu kwa jina la Yesu? Je, hangeweza kuitwa kwa jina jipya katika enzi mpya? Je, sura ya mtu mmoja na hasa jina moja vinaweza kumwakilisha Mungu katika ukamilifu wake? Katika kila enzi, Mungu Anafanya kazi mpya na huitwa kwa jina jipya; Je, anawezaje kufanya kazi sawa katika enzi tofauti? Itakuwaje Yeye kugandamana na yale ya zamani? Jina la Yesu lilichukuliwa kuwa la kazi ya ukombozi, hivyo bado Yeye Anaweza kuitwa kwa jina moja wakati Atarudi katika siku za mwisho? Je, bado Yeye Atafanya kazi ya ukombozi? Ni kwa nini Yehova na Yesu ni kitu kimoja, ilhali wanaitwa kwa majina tofauti katika enzi hizi tofauti? Je, si kwa sababu enzi za kazi Yao ni tofauti? Jina moja linawezaje kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake? Kwa njia hii, lazima Mungu aitwe kwa jina tofauti katika enzi tofauti, lazima atumie jina kubadilisha enzi na kuwakilisha hiyo enzi, kwa kuwa hakuna jina moja linaweza kumwakilisha Mungu mwenyewe kikamilifu. Na kila jina linaweza tu kuwakilisha kipengele cha wakati cha tabia ya Mungu katika enzi fulani; yote linahitaji kufanya ni kuwakilisha kazi Yake. Kwa hivyo, Mungu Anaweza kuchagua jina lolote ambalo linafaa tabia yake kuwakilisha enzi nzima. Bila kujali iwapo ni enzi ya Yehova, au ni enzi ya Yesu, kila enzi inawakilishwa kwa jina. Baada ya Enzi ya Neema, enzi ya mwisho imewadia na Yesu Amekwisha kuja. Itakuwaje awe bado anaitwa Yesu? Itakuwaje awe bado anachukua umbo la Yesu miongoni mwa watu? Je, umesahau kuwa Yesu Alikuwa tu sura ya Mnazareti? Je, umesahau kuwa Yesu Alikuwa tu mkombozi wa wanadamu? Itakuwaje achukue kazi ya kushinda na kurekebisha mwanadamu katika siku za mwisho?

kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili

9. Kila wakati ambao Mungu Atawasili hapa duniani, Yeye Atabadilisha jina lake, jinsia yake, mfano wake, na kazi yake; Yeye harudii kazi yake, na Yeye daima yu mpya na kamwe si wa zamani. Wakati Alikuja hapo awali, Aliitwa Yesu; Je, anaweza bado kuitwa Yesu anapokuja tena wakati huu? Alipokuja hapo awali, Alikuwa wa kiume, Ataweza kuwa wa kiume tena wakati huu? Kazi Yake Alipokuja wakati wa Enzi ya Neema ilikuwa ya kusulubishwa msalabani; Atakapokuja tena, je, bado Atawakomboa wanadamu kutoka kwenye dhambi? Je, bado Atasulubishwa msalabani? Je, hayo hayatakuwa marudio ya kazi yake? Je, hujui kwamba Mungu daima ni mpya na kamwe si wa zamani?

kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili

10. Kuna wale ambao wanasema kuwa Mungu habadiliki. Hiyo ni sahihi, lakini inaashiria mabadiliko ya tabia ya Mungu na pia kiini chake. Mabadiliko ya jina lake na kazi hayathibitishi ya kuwa kiini chake kimebadilika; kwa maneno mengine, Mungu siku zote Atakuwa Mungu, na hii kamwe haitabadilika. Iwapo utasema kuwa kazi ya Mungu daima inabaki vile vile, basi Angekuwa na uwezo wa kumaliza mpango wake wa usimamizi wa miaka elfu sita? Wewe hujua tu kwamba Mungu habadiliki milele, lakini je, unajua kuwa Mungu ni mpya milele na kamwe si wa zamani? Kama kazi ya Mungu kamwe haikubadilika, basi Angeweza kulea mwanadamu hadi leo? Kama Mungu habadiliki, basi mbona Yeye tayari Amefanya kazi ya nyakati mbili? Kazi yake daima inaendelea mbele, na hivyo pia ndivyo tabia yake inafichuliwa kwa binadamu hatua kwa hatua, na kile ambacho kinafichuliwa ni tabia yake ya asilia. Hapo mwanzo, tabia ya Mungu ilikuwa siri kwa mwanadamu, na kamwe Yeye hadharani hakumfichulia mwanadamu tabia yake, na mwanadamu hakuwa na ufahamu kuhusu Yeye, na hivyo hatua kwa hatua Alitumia kazi Yake kumfichulia mwanadamu tabia Yake, lakini hii haina maana kuwa tabia Yake inabadilika katika kila enzi. Sio kweli kuwa tabia ya Mungu kila wakati inabadilika kwa ajili mapenzi Yake daima hubadilika. Bali, kwa kuwa enzi za kazi Yake ni tofauti, asili ya tabia Yake kwa ujumla hufichuliwa kwa binadamu hatua kwa hatua, ili mwanadamu aweze kumjua Yeye. Lakini hii si kwa njia yoyote ushahidi kuwa Mungu hapo awali hakuwa na tabia fulani na tabia Yake imebadilika hatua kwa hatua kwenye enzi zinazopita—ufahamu kama huo ni wenye kosa. Mungu humfichulia mwanadamu tabia yake fulani ya asili—kile Alicho—kwa mujibu wa enzi zinazopita. Kazi ya enzi moja haiwezi kueleza tabia nzima ya Mungu. Na kwa hivyo, maneno haya "Mungu daima ni mpya na kamwe si wa zamani" yanarejelea kazi yake, na maneno haya "Mungu habadiliki" ni kuhusiana na asili ya kile ambacho Mungu anacho na kile ambacho Yeye ni. Bila kujali, huwezi kubaini kazi ya miaka elfu sita kwa mtazamo mmoja, ama kwa kuielezea tu kwa maneno ambayo hayabadiliki. Huo ni ujinga wa mwanadamu. Mungu si wazi kama mwanadamu anavyofikiria, na kazi yake haitasimama katika enzi moja. Yehova, kwa mfano, haliwezi daima kusimamia jina la Mungu; Mungu pia hufanya kazi yake kwa kutumia Jina la Yesu, ambayo ni ishara ya vile ambavyo kazi ya Mungu daima inaendelea mbele.

kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili

11. Mungu siku zote huwa Mungu, na kamwe hatakuwa Shetani; Shetani daima ni Shetani, na hawezi kuwa Mungu. Hekima ya Mungu, ajabu ya Mungu, haki ya Mungu, na adhama ya Mungu kamwe hayatabadilika. Kiini chake na anachomiliki na kile Anacho na alicho kamwe hakitabadilika. Kazi yake, hata hivyo, daima inaendelea mbele, daima inaenda ndani zaidi, kwa kuwa Mungu daima ni mpya na kamwe si wa zamani. Katika kila enzi Mungu huchukua jina jipya, katika kila enzi anafanya kazi mpya, na kwa kila enzi anaruhusu viumbe kuona mapenzi yake mapya na tabia yake mpya. Ikiwa watu hawaoni dhihirisho la tabia mpya ya Mungu katika enzi mpya, wao si watamsulubisha msalabani milele? Na kwa kufanya hivyo, si watakuwa wamebaini Mungu?

kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili

12. Mungu harudii kazi yake katika kila enzi mpya. Kwa kuwa siku za mwisho zimewadia, Yeye Atafanya kazi ya siku za mwisho, na kufichua tabia yake yote siku za mwisho. Siku za mwisho ni enzi tofauti, enzi ambayo Yesu Alisema lazima mteseke kwa maafa, na ukabiliwe na mitetemeko ya ardhi, njaa, na baa, ambavyo vitaonyesha kuwa hii ni enzi mpya, na sio tena Enzi ya Neema ya zamani. Kama, watu wanavyosema, Mungu daima habadiliki, tabia yake daima ni ya huruma na ya upendo, na Yeye anampenda mwanadamu jinsi Anavyojipenda, na Anampa kila mwanadamu wokovu na kamwe hamchukii mwanadamu, basi Angekuwa na uwezo wa kukamilisha kazi yake? Wakati Yesu Alikuja, Alisulubishwa msalabani, na Yeye Alijitoa kama sadaka kwa sababu ya wote wenye dhambi na kwa kujitoa Yeye mwenyewe madhabahuni. Yeye tayari Alikuwa Amemaliza kazi ya ukombozi na tayari Alikuwa Ametamatisha Enzi ya Neema, na hivyo ni nini kiini cha kurudia kazi ya enzi hiyo katika siku za mwisho? Je, kufanya kitu kimoja haitakuwa kukanusha kazi ya Yesu? Iwapo Mungu hatafanya kazi ya kusulubiwa awamu hii itakapofika, lakini Yeye Asalie mwenye mapenzi na Mungu wa huruma, je, anaweza kufikisha enzi hii mwisho? Je, Mungu mwenye upendo na mwenye huruma, si Angeweza kuhitimisha enzi hii? Katika kazi yake ya kuhitimisha enzi, tabia ya Mungu ni ile ya kuadibu na hukumu, ambayo inafichua yote ambayo si ya haki, na kuhukumu wanadamu hadharani, na kukamilisha wale ambao wanampenda kwa ukweli. Ni tabia tu kama hii ndiyo ambayo inaweza kufikisha enzi hii mwisho.

kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili

13. Siku za mwisho tayari zimewadia. Kila kitu kitabainishwa kulingana na aina, na kitagawanywa katika makundi tofauti kulingana na asili yake. Huu ni wakati ambapo Mungu Atafichua hatima ya wanadamu na kikomo cha safari yao. Kama mwanadamu hatashuhudia kuadibu na hukumu yake, basi hakutakuwepo na mbinu ya kufichua uasi na udhalimu wao mwanadamu. Ni kwa njia ya kuadibu na hukumu ndipo mwisho wa mambo yote yatafunuliwa. Mwanadamu huonyesha tu ukweli ulio ndani yake anapoadibiwa na kuhukumiwa. Mabaya yataekwa na mabaya, mema na mema, na wanadamu watabainishwa kulingana na aina. Kupitia kuadibu na hukumu, mwisho wa mambo yote utafichuliwa, ili mabaya yaadhibiwe na mazuri yatunukiwe zawadi, na watu wote watakuwa wakunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Kazi hii yote inapaswa kutimizwa kupitia kuadibu kwa haki adhibu na hukumu. Kwa sababu upotovu wa mwanadamu umefika upeo wake na uasi wake umekua mbaya mno, ni haki ya tabia ya Mungu tu, ambayo hasa ni ya kuadibu na hukumu, na imefichuliwa kwa kipindi cha siku za mwisho, inayoweza kubadilisha na kukamilisha mwanadamu. Ni tabia hii pekee ambayo itafichua maovu na hivyo kuwaadhibu watu wote dhalimu. Kwa hivyo, tabia kama hii imejazwa umuhimu wa wakati, na ufunuo na maonyesho ya tabia yake ni kwa ajili ya kazi ya kila enzi mpya. Mungu hafichui tabia yake kiholela na bila umuhimu. Kama, wakati wa mwisho wa mwanadamu umefichuliwa katika kipindi cha siku za mwisho, Mungu bado anamfadhili binadamu kwa huruma na upendo usioisha, kama yeye bado ni wa kupenda mwanadamu, na kumkabili hukumu ya haki, bali anamwonyesha stahamala, uvumilivu, na msamaha, kama bado Yeye anamsamehe mwanadamu bila kujali ubaya wa makosa anayofanya, bila hukumu yoyote ya haki, basi kungekuwepo na mwisho wa usimamizi wa Mungu? Ni wakati gani tabia kama hii itaweza kuwaongoza wanadamu katika hatima inayofaa? Chukua, kwa mfano, hakimu ambaye daima ni mwenye upendo, mwenye roho safi na mpole. Anawapenda watu bila kujali dhambi wanazozifanya, na ni mwenye upendo na stahamala kwa watu bila kujali hao ni nani. Kisha ni lini ambapo ataweza kufikia uamuzi wa haki? Katika siku za mwisho, ni hukumu ya haki tu inaweza kubainisha mwanadamu na kuleta mwanadamu katika utawala mpya. Kwa njia hii, enzi nzima inafikishwa mwisho kupitia kwa tabia ya Mungu iliyo ya haki ya hukumu na kuadibu.

kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni